Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   
 


Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Tisa - Wanaume Na Wanawake Wanojihifadhi Tupu
 
Wanawake Ndoa Urafiki Katika Uislamu Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Tisa - Wanaume Na Wanawake Wanojihifadhi Tupu Zao

Anasema Allaah سبحانه وتعالى:
((إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِينَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِينَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ وَالصَّائِمِينَ وَالصَّائِمَاتِ وَالْحَافِظِينَ فُرُوجَهُمْ وَالْحَافِظَاتِ ….))

((Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na watiifu wanaume na watiifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wasemao kweli wanawake, na wanaosubiri wanaume na wanaosubiri wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanyenyekevu wanawake, na watoao sadaka wanaume na watoao sadaka wanawake, na wanaofunga wanaume na wanaofunga wanawake, na wanaojihifadhi tupu zao wanaume na wanawake…)) [Al-Ahzaab:35]



Maana ya kujihifadhi tupu zao:

Kwamba wanahifadhi tupu zao kutokana na mambo ya haram yote ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ameharamisha kama zinaa, liwaat (wanaume kwa wanaume) na pia wafanyao uchafu baina ya wanawake kwa wanawake. Hawamkaribii yeyote isipokuwa wale waliohalalishwa nao na wale iliyomiliki mikono yao ya kuume kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ ﴿29﴾ إِلَّا عَلَى أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ ﴿30﴾ فَمَنِ ابْتَغَى وَرَاء ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْعَادُونَ ﴿31﴾

29. Na ambao wanahifadhi tupu zao

30. Isipokuwa kwa wake zao, au iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi

31. Lakini wanaotaka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka. [Al-Ma'aarij 29-31]

Sifa hii vile vile ni miongoni mwa sifa Alizozitaja Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kuwa pindi Muislamu akizimiliki, atalipwa Pepo ya Firdaws kama ilivyo katika Suratul-Mu-uminuun:

﴿ بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ﴾
قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ ﴿1﴾ الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ ﴿2﴾ وَالَّذِينَ هُمْ عَنِ اللَّغْوِ مُعْرِضُونَ ﴿3﴾ وَالَّذِينَ هُمْ لِلزَّكَاةِ فَاعِلُونَ ﴿4﴾ وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ ﴿5﴾ إِلَّا عَلَى أَزْوَاجِهِمْ أوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ ﴿6﴾ فَمَنِ ابْتَغَى وَرَاء ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْعَادُونَ ﴿7﴾ وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ ﴿8﴾ وَالَّذِينَ هُمْ عَلَى صَلَوَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ ﴿9﴾ أُوْلَئِكَ هُمُ الْوَارِثُونَ ﴿10﴾ الَّذِينَ يَرِثُونَ الْفِرْدَوْسَ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿11


KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI

WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

1. HAKIKA wamefanikiwa Waumini
2. Ambao ni wanyenyekevu katika Swalah zao
3. Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi,
4. Na ambao wanatoa Zaka
5. Na ambao wanazilinda tupu zao,
6. Isipokuwa kwa wake zao au kwa iliyowamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa
7. Lakini anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka.
8. Na ambao wanazitimiza amana zao na ahadi zao
9. Na ambao Swalah zao wanazihifadhi
10. Hao ndio warithi,
11. Ambao watairithi Pepo ya Firdausi, wadumu humo

Na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) pia ametubashiria Pepo kwa wenye kuhifadhi tupu zao:

((مَنْ يَكْفُل لِي مَا بَيْن لَحْيَيْهِ وَمَا بَيْن رِجْلَيْهِ أَكْفُل لَهُ الْجَنَّة)) البخاري

((Atakayenipa dhamana (ya kuhifadhi) baina ya ndevu (ulimi) zake na miguu yake (tupu) basi atadhaminiwa pepo)) [Al-Bukhaariy]
Muislamu anaweza kujihifadhi na hayo kwa kufuata amri nyingine ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ya kuinamisha macho yake:

قُل لِّلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا مِنْ أَبْصَارِهِمْ وَيَحْفَظُوا فُرُوجَهُمْ ذَلِكَ أَزْكَى لَهُمْ إِنَّ اللَّهَ خَبِيرٌ بِمَا يَصْنَعُونَ ﴿30﴾ وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَى جُيُوبِهِنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاء بُعُولَتِهِنَّ أَوْ أَبْنَائِهِنَّ أَوْ أَبْنَاء بُعُولَتِهِنَّ أَوْ إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي إِخْوَانِهِنَّ أَوْ بَنِي أَخَوَاتِهِنَّ أَوْ نِسَائِهِنَّ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُنَّ أَوِ التَّابِعِينَ غَيْرِ أُوْلِي الْإِرْبَةِ مِنَ الرِّجَالِ أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَى عَوْرَاتِ النِّسَاء وَلَا يَضْرِبْنَ بِأَرْجُلِهِنَّ لِيُعْلَمَ مَا يُخْفِينَ مِن زِينَتِهِنَّ وَتُوبُوا إِلَى اللَّهِ جَمِيعًا أَيُّهَا الْمُؤْمِنُونَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿31


30. Waambie Waumini wanaume

 wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Allah Anazo khabari za wanayoyafanya.

31. Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unaodhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafuasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyokhusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajulikane mapambo waliyoyaficha. Na tubuni nyote kwa Allah enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa.

Tuelezee kidogo kuhusu kutodhihirisha wanawake uzuri wao, yaani kutimiza hijaab. Sio maana kwamba wanawake tu ndio wenye kuingia katika maasi ya zinaa, bali ni kwa sababu mwanamke akiongoka na akihifadhi stara yake, basi jamii yake yote pia itaongoka na itahifadhi stara yake. Hata hivyo, ni muhimu kuwataja wanawake kwa sababu mwanamke akipoteza stara yake, ni rahisi kwa vijana pia kupotea. Kwani anapojiweka wazi mwanamke na kudhihirisha mapambo yake, humvutia mwanamume haraka akataka kumtongoza na kumkaribia kwa kila aina ya njia hadi waingie katika zinaa, hivyo basi ni rahisi kwa jamii nzima kupoteza stara yao.

Na wanawake wasiotimiza hijaab, wao wameharamishwa na Pepo bali hata harufu ya Pepo hawataisikia:

عن أبي هريرة رضي الله عنه :قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( صنفان من أهل النارلم أَرَهُمَا : قوم معهم سِياطٌ كأذناب البقر يضربون بها الناس , ونساء كاسيات عاريات , مُمِيلاتٌ مائلات , رؤوسهن كأسنمة البُخْتِ المائلة , لا يدخلن الجنة , ولا يجدن ريحها , وإن ريحها ليوجد من مسيرة كذا وكذا (( مسلم

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allahu 'anhu): Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Aina mbili za watu wa motoni siwaoni; Watu ambao wana fimbo (mijeledi) kama za mkia wa ng'ombe dume ambazo wanawapigia watu, na wanawake ambao wamevaa lakini wako uchi, wanawashawishi wanaume wawatongoze, na wanaelekea kwao (kwa kuwa warahisi). Vichwa vyao kama nundu za ngamia zinazoyumba. Hawataingia Peponi wala hawatasikia harufu yake ingawa harufu yake inaweza kunuswa kutoka masafa kadhaa na kadhaa)) [Muslim]
Hadiyth hiyo ya Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inatudhihirikia uhakika wake kwani tunawaona dada zetu wengi wakidhani kuwa wamevaa mavazi ya hijaab na hali hawakutimiza hijab ya sheria inavyopasa. Utamuona mwanamke amejifunika kichwa tu lakini mwili wake wote haukusitirika kutokana na mavazi aliyovaa. Hivyo hudhani kuwa hijaab hasa ina maana ya kujifunika nywele pekee.

Basi hebu tutaje hapa hijaab ya Kiislamu inayotakikana kisheria:

1. Nguo iwe ndefu ya kukufunika mwili mzima mpaka miguu, na kama ni fupi kidogo basi uvae soksi. Ukivaa nguo ambayo itaonyesha sehemu yoyote ya mwili isipokuwa uso na viganja, basi utakuwa hukuvaa hijaab sawa sawa
2. Nguo hiyo iwe pana na sio yenye kuonyesha umbo lako, yaani isiwe yenye kukubana popote mwilini khaswa kuanzia kifuani hadi magotini.
3. Nguo iwe nzito na si nyepesi yenye kuonyesha mwili wako, yaani kitambaa cha nguo kisiwe chepesi.
4. Kutokuvaa nguo zinazofanana na nguo za kiume.
5. Kutokuvaa nguo zenye urembo sana za kuvutia
6. Kutotia manukato.

Dada zetu wa Kiislamu watakapotimiza haya watakuwa wamekamilisha hijaab zao na watakuwa katika stara pamoja na kusitiri jamii na ndipo watakapokuwa wamejitahidi kujihifadhi waweze kuingia katika sifa hiyo ya kuhifadhi tupu zao Insha Allah.

KISA CHA KWELI CHA ZAHRAH NA SAFARI YAKE YA KUVAA HIJAAB

"Safari yangu ya hijaab au labda niseme 'hijaab inayopasa kisheria' ni ndefu na ya pole pole na sio ya tamthilia.

Nilikuwa na umri wa miaka 14 nikienda shule pamoja na kaka yangu na dada zangu. Baba yangu alikuwa akitupeleka na kuturudisha shuleni. Kwa vile baba yangu alikuwa ana kazi nyingi sana na wakati wake ulikuwa wa dhiki, aliamua kutuwekea teksi kwa muda wa wiki mbili. Dereva wa teksi alikuwa mtu mwema na mchangamfu. Alikuwa akitutolea visa na vichekesho wakati tunaelekea shuleni na kurudi. Tukaanza kumpenda na kumheshimu kama vile ni mjomba wetu. Hakuwa anajua Kiingereza, lakini siku moja alitupa tafsiyr ya Qur-aan ya Marmaduke Pickthall.

Siku moja wakati anaturudisha nyumbani, mara ghafla akasema kuwa: "Wasichana wa Kiislamu ni lazima wavae hijaab". Maneno yake yakawa yananigonga masikioni siku nzima! Sikupata kuvaa hijaab kabla, na karibu nisba ya 99% ya wasichana darasani mwangu hawakuwa wanavaa hijaab, wala sikupenda fikra hiyo ya kuvaa hijaab mwenyewe. Lakini sikuweza kupinga aliyoyasema dereva huyo ingawa sikuwa na pendekezo nalo jambo hili, na sikuweza kukanusha kwamba wanawake wa Kiislamu wanapaswa kuvaa hijaab.

Nikaanza kuvaa kitambaa cha kichwa siku ya pili na nakiri kwamba nilianza kuvaa kwa sababu ya heshima niliyo kuwa nayo ya dereva huyo bila ya kufikiri kwamba ni makosa kwani nilitakiwa nimkumbuke Mola wangu kwanza. Na sikuwa na sababu ya kunizua kuvaa hijaab. Wazazi wangu walifurahia uamuzi wangu.

Siku za mwanzo, nilianza kuvaa kitambaa cha kichwa kwa kujifunika nusu na huku baadhi ya nywele zikionekana! Nilitambua kuwa hivyo sivyo ilivyopasa kuvaliwa. Baada ya hapo nikatamuba unafiki wangu nikaanza kuivaa vizuri na kufunika nywele zote. Haikuwa wepesi ingawa nilikuwa naishi katika nchi ya Kiislamu na marafiki zangu walikuwa wakiniuliza: "Kwa nini unafanya hivyo? Unaonakana kama mzee". Kwao wao jambo hilo lilikuwa ni kama tendo wa watu wazima tu. Na sisi tulio vijana tukiwa bado shuleni tunatakiwa tuwe na furaha. Lakini Alhamdulillah sikuwasikiliza maneno yao kwani hijaab ilinifanya nionekane mtu makini na heshima zaidi. Nikaamua kuivaa moja kwa moja. Nikaanza kuvaa nguzo zilizofunika mikono yote, na zilizokuwa pana kila mahali nilikokwenda hadi ilipofika mwezi wa Septemba nikajifunza kwamba jilbaab ni lazima nikaanza kuvaa jilbaab.

Nikitazama nyuma nawaza kwamba hijaab imenisaidia sana kuniunda kama mwanamke hasa wa Kiislam. Nilipoanza kuivaa hata sikuwa nadumisha Swalah zangu tano. Lakini Alhamdulillah hatua baada ya hatua hijaab yangu imenisaidia kufunga milango yote ya shari na mambo yasiyopasa ya Kiislamu yaliyonizunguka katika mazingira yangu. Nimeunda picha fulani katika macho yangu na ya wengine, hivyo ikanibidi niishi katika kigezo hicho cha picha hiyo. Picha ya Staha.


 Posted By Posted juu ya Monday, December 03 @ 22:46:55 PST na MediaSwahiliTeam
 

Comments 💬 التعليقات
 

For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا

Kuhusiana Viungo

· zaidi Wanawake Ndoa Urafiki Katika Uislamu
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu Wanawake Ndoa Urafiki Katika Uislamu:
EDA - Hikma Yake, Hukmu Zake, Yanayopasa Na Yasiyopasa


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora
Vizuri Sana
Mema
Kawaidar
Mbaya


Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa Rafiki





Mada zinazohusiana

Wanawake Ndoa Urafiki Katika Uislamu

 

Ẹsin Islam الدين الإسلامي Religion of Islam Addinin Musulunci Agama Islam Religión del Islam 伊斯兰教 Dini ya Kiislamu Религия Ислам Religião do Islã イスラム教 Esin Islam 이슬람의 종교 Portal African Muslim Website - Arabic English African Islamic Website For World News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Articles, Radio, Audio, Video, Quran, Hadith, TV Channels, Fatwas, Muslim News, Newspapers, Magazines Headlines, Forums, College, Schools, Universities, Mosques, Quranic, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Ramadan, Vidoes, Books, Fasting, PDFs On EsinIslam.Com And IslamAfrica.Com