Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   
 


Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Nane - Wanaume Na Wanawake Wanaofunga
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Nane - Wanaume Na Wanawake Wanaofunga

((إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِينَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِينَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ وَالصَّائِمِينَ وَالصَّائِمَاتِ....))
Anasema Allaah سبحانه وتعالى:

((Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na watiifu wanaume na watiifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wasemao kweli wanawake, na wanaosubiri wanaume na wanaosubiri wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanyenyekevu wanawake, na watoao sadaka wanaume na watoao sadaka wanawake, na wanaofunga wanaume na wanaofunga wanawake…)) [Al-Ahzaab:35]

Nini maana ya Swawm?



Kilugha:

Kufunga na kujizuilia, huenda ikawa ni chakula, kinywaji au kitu chochote kingine hata kusema kama Alivyosema Allaah (Subhaana wa Ta’ala):
((إِنِّي نَذَرْتُ لِلرَّحْمَنِ صَوْمًا فَلَنْ أُكَلِّمَ الْيَوْمَ إِنسِيًّا))

))Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Allah ya kufunga kwa hivyo leo sitasema na mtu )) [Maryam:26]

Maana ya Swawm kisheria:

Ni kufunga, yaani kuacha kula na kunywa pamoja na matamanio ya mwili na tumbo kuanzia kupambazuka kwa Alfajiri hadi linapozama jua yaani wakati wa Magharibi pamoja na niya ya kumuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)

Ibaada hii ya Swawm ilikwishawatangulia walio kabla yetu kama ni sheria ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala)

((يَا أَيهَا الذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ لَعَلكُمْ تَتقُونَ))

((Enyi mlioamini! Mmeandikiwa Swawm, kama walivyoandikiwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu)) [Al-Baqarah:183]
Fadhila za Swawm:

Swawm ni ibada tukufu kabisa ambayo inamkaribisha mja kwa Mola wake; na fadhila zake ni nyingi sana. Muumini hulipwa thawabu zisizo na idadi, na pia hufutiwa madhambi yake, vile vile huepushwa na kuwekwa mbali na moto. Na mwenye kufunga anastahiki kuingia katika mlango wa Pepo uliowekwa hasa kwa ajili ya wanaofunga, na pia hufurahi mja kuonana na Mola wake.

Tutazitaja hapa fadhila chache tu miongoni mwa nyingi za mwenye kufunga kama zilivyokuja katika Hadiyth:

قال صلى الله عليه وسلم : )) كل عمل ابن آدم له الحسنة بعشر أمثالها إلى سبعمائة ضعف . يقول الله عز وجل : إلا الصيام فإنه لي وأنا أجزي به ، ترك شهوته وطعامه وشرابه من أجلي، للصائم فرحتان ؛ فرحة عند فطره ، وفرحة عند لقاء ربه، و لخلوف فم الصائم أطيب عند الله من ريح المسك)) أخرجه البخاري ومسلم

((Amesema Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kila amali njema ya mwanaadamu inalipwa mara kumi na inaongezewa thawabu kutoka kumi hadi mia saba, na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema isipokuwa Swawm, kwani hiyo ni kwa ajili Yangu na Mimi Ndiye Nitakayemlipa. Ameacha matamanio yake na chakula chake na maji yake kwa ajili Yangu. Kwa aliyefunga atapata furaha mbili; furaha anapofuturu na furaha atakapoonana na Mola wake, harufu inayotoka kinywani mwa aliyefunga ni nzuri mbele ya Allaah kuliko harufu ya misk)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

قال صلى الله عليه وسلم : (( من صام رمضان إيماناً و احتساباً غفر له ما تقدم من ذنبه)) أخرجه البخاري ومسلم

Amesema Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ((Atakayefunga Ramadhaan kwa iymaan na kutegemea malipo ataghufuriwa madhambi yake yaliotangulia)) [Al Bukhaariy na Muslim].

عن أبي سعيد الخدري قال: قال رسول الله: ((ما من عبد يصوم يوما في سبيل اللّه، إلاّ باعد اللّه بذلك اليوم وجهه عن النّار سبعين خريفا)) متفق عليه .

Kutoka kwa Abiy Sa'iydil-Khudriy (Radhiya Allahu ‘anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hapana mja afungaye siku kwa ajili ya Allah, isipokuwa Allah Atauweka mbali uso wake kutokana na moto siku hiyo, kwa umbali wa miaka sabini)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Swawm imegawanyika katika sehemu mbili:

Ya kwanza : Swawm ya wajib – nayo ni Swawm ya mwezi wa Ramadhaan, Swawm ya kafara (fidia/malipo) na Swawm ya kuondosha nadhiri.
Ya pili: Swawm za Sunnah kama Swawm siku ya ‘Arafah, Swawm ya ‘Ashuraa, Jumatatu na Alkhamiys, Ayaamul-Biydhw (siku tatu katika mwezi yaani tarehe 13, 14 na 15), na pia Swawm nyinginezo kama katika mwezi wa Muharram n.k.

Muislamu anapofunga aina zozote hizo za Swawm basi hupata thawabu na fadhila hizo na nyinginezo.

Aina za watu wanaofunga Swawm:

Aina ya kwanza ya wanaofunga:

Wanaofunga Swawm ya kawaida, nao ni wale wanaofunga na kujizuia na kula, kunywa na matamanio ya mwili, lakini hawazuii ndimi zao kutokana na maneno mabaya na hawafungi macho yao na masikio yao kutazama na kusikia yale yaliyoharamishwa, na hawazuii mikono yao na miguu yao kutokana na maudhi ya wenzi wao. Wanapoteza muda wao katika upuuzi na kusubiri tu ufike wakati wa kufungua Swawm.
Aina ya pili ya wanaofunga:

Swawm ya hasa, nao ni wale ambao juu ya kujizuia kula, kunywa, matamanio ya mwili, kusema maneno ya ovyo, huwa wanafunga viungo vyao vyote vya mwili kutokana na yale yaliyoharamisha na hushughulisha ndimi zao katika kumkumbuka Mola wao usiku na mchana kwa kusoma Qur-aan na Adhkaar mbalimbali. Pia huwa kutwa kucha wakirukuu na kusujudu. Hujaa khofu katika nyoyo zao ya Mola wao. Nao pia kufanya mema mengi kama kulisha masikini, kutoa sadaka na mengineyo. Aina hii ya wenye kufunga hutamani mwaka mzima uwe Ramadhaan.

Swahaabiyaah aliyekuwa akipenda kufunga sana:

Hafswah bint ‘Umar ibnul-Khatwaab (Radhiya Allahu ‘anhumaa)

Ni mtoto wa ‘Umar ibnul-Khatwaab Khaliyfah wa pili wa Waislamu. Aliolewa na Khunis ibn Hudhaafa bin Qays As-Sahaamiy ambaye alikuwa katika kabila ya Quraysh. Mumewe alihama mara mbili; kwenda Abyssinia na kwenda Madiynah. Alipigana vita vya Badr kisha Uhud akariki akimuacha Hafswah (Radhiya Allahu ‘anhaa) akiwa na miaka kumi na nane.

‘Umar (Radhiya Allahu ‘anhu) alihuzunika kwa msiba ya binti yake ambaye alikuwa mjane. Kila alipokwenda nyumbani kwake akimtazama hali yake huwa anahuzunika.

Baada ya muda akaamua kumtafutia mume binti yake akaanza kwa Abu Bakar (Radhiya Allahu ‘anhu) ambaye ni rafiki mpenzi wa Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Alipomuomba amuoe, Abu Bakar hakumjibu kitu. ‘Umar akarudi akiwa amevunjika moyo na wala hakuamini kuwa Abu Bakar angemvunja hivyo.

Kisha akaenda kwa ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhiya Allahu ‘anhu) ambaye mkewe ni Ruqayyah mtoto wa Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Alipomuomba, alimjibu kuwa: “Sipendi kuoa kwa hivi sasa”.

“Umar akazidi kusikitika huku akiwa amekasirika na marafiki hawa wawili. Akaenda kwa Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumlalamikia kuhusu Abu Bakar na ‘Uthmaan, Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamuambia: ((Hafswah (Radhiya Allahu ‘anhaa) ataolewa na mtu aliye bora kuliko ‘Uthmaan na ‘Uthmaan ataoa aliye bora kuliko Hafswah)) [Al-Bukhaariy]

‘Umar Alifurahi akawa anamuambia kila aliyemuona. Abu Bakar alipomuona, alitambua furaha yake akampa hongera kisha akamuomba msamaha na kumuambia: “Usikasirike na mimi kwani Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimtaja Hafswah (Radhiya Allahu ‘anhaa) kabla na sikuweza kutaja siri yake. Ingelikuwa hakumtaja ningelimuoa”.

Watu wote Madiynah walifurahiwa na ndoa ya Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Hafswah bint ‘Umar (Radhiya Allahu ‘anhuma) hivyo akaungana na mama waumini wengine kwa furaha.

Hafswah (Radhiya Allahu ‘anhaa alikuwa rafiki mkubwa wa bibi ‘Aishah (Radhiya Allahu ‘anhaa) hivyo walipatana sana. Imesemekana kwamba Mtume alimpa talaka Hafswah (Radhiya Allahu ‘anhaa) mara moja kutokana na makosa aliyoyafanya ya kutoa siri, lakini alimrudia kutokana na amri kutoka kwa Jibryil (‘alayhis-salaam) alipomuambia: “Mrudie Hafswah (Radhiya Allahu ‘anhaa) kwani yeye anafunga (Swawm) na kuswali usiku kucha”.

Hafswah (Radhiya Allahu ‘anhaa) alitambua makosa yake akajirudi na kuwa mke mtiifu na mwema.

Alipofariki Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Abu Bakar alipokuwa Khaliyfah, Hafswah (Radhiya Allahu ‘anhaa) alichaguliwa kuwa msimamizi wa nuskha ya kwanza ya Qur-aan. Aliendelea kumuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kwa kufunga (Swawm) na kutunza Qur-aan. Kabla ya kuuawa baba yake, Hafswah (Radhiya Allahu ‘anhaa) aliachiwa kuwa msimamizi wa mirathi yake.

Hafswah (Radhiya Allahu ‘anhaa) alifariki katika uongozi wa Mu’aawiyah ibn Abu Sufyaan. Alimuamrisha kaka yake ‘Abdullah bin 'Umar (Radhiya Allahu 'anhuma) yale aliyoamrishwa na baba yake. Allaah Subhana wa Ta’ala Awe Radhi naye.


 Posted By Posted juu ya Monday, December 03 @ 22:53:51 PST na MediaSwahiliTeam
 

Comments 💬 التعليقات
 

For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا

Kuhusiana Viungo

· zaidi Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis:
Jinsi Ya Kumfurahisha Mkeo


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora
Vizuri Sana
Mema
Kawaidar
Mbaya


Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa Rafiki





Mada zinazohusiana

Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

 

Ẹsin Islam الدين الإسلامي Religion of Islam Addinin Musulunci Agama Islam Religión del Islam 伊斯兰教 Dini ya Kiislamu Религия Ислам Religião do Islã イスラム教 Esin Islam 이슬람의 종교 Portal African Muslim Website - Arabic English African Islamic Website For World News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Articles, Radio, Audio, Video, Quran, Hadith, TV Channels, Fatwas, Muslim News, Newspapers, Magazines Headlines, Forums, College, Schools, Universities, Mosques, Quranic, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Ramadan, Vidoes, Books, Fasting, PDFs On EsinIslam.Com And IslamAfrica.Com