Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   
 


Facebook Au Fitnabook
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis Ilyaasa bint Mawlaana

Facebook Au Fitnabook

Kwanza kabisa, ijulikane wazi kwamba kusudio la makala hii si kutoa fatwa wala hukumu. Lengo ni kuweka wazi manufaa na madhara ya Facebook ili mtu binafsi atoe hukumu yake mwenyewe.
Je, ni Facebook au Fitnabook? Hili ni suali ambalo watu wengi wameanza kujiuliza baada ya kujionea vitimbi na kashfa kadhaa katika huu mtandao ambao unazidi kujipatia umaarufu kila pembe ya dunia. Naam, kuna vitimbi kadhaa vinafanyika kwa jina la Facebook. Na ndio kuna vijana wengi ambao wametumbikia katika janga la fitna katika Facebook lakini nini suluhisho la hili?
Kabla hatujatazama hebu kwanza tuangalie manufaa na madhara ya Facebook.

Manufaa
Kama ilivyo kawaida ya vitu vingi, Facebook ina faida yake. Lakini je, hizo faida ni nyingi kuliko madhara? Katika sehemu hii tutaja manufaa ambayo yako wazi kutokana na utumiaji wa Facebook. Manufaa hayo ni kama yafuatayo:
1. Kufanya da’wah ( kuwalingania watu kwenye Uislam)
Madaa’iyah kadhaa pamoja na baadhi ya Mashaykh hutumia Facebook kwa kazi za da’wah. Huwekwa na kutumwa vitu mbalimbali vya kufikisha mafunzo mbalimbali ya Dini kama: video za mawaidha, makala za Kislamu na njia mbalimbali za kunufaisha wasomaji.

2. Kuwasiliana na jamaa na marafiki wa mbali
Mara nyingi watu hutumia Facebook kwa kuwasiliana na jamaa zao ambao wanaishi nje ya nchi kwa hoja ya kwamba ni njia rahisi na ya nyepesi ukilinganisha na njia nyinginezo.

3. Kutangaza shughuli na harakati za Kiislam
Ijtimai na mikusanyiko mingi ya Kiislamu na mambo yanayowahusu Waislamu mara nyingi huwa yanatangaziwa kwa kutumia Facebook. Njia hii pia inaruhusu waandaaji kujua watu wangapi watahudhuria au kupatikana katika shughuli au harakati zao.

Madhara
Ijapokuwa kuna manufaa kadhaa juu ya utumiaji wa Facebook, kuna balaa na fitnah nyingi hupatikana humo, kadhalika watu wengi wanaitumia kwa njia mbaya. Katika madhara ya Facebook ni haya:

1. Kupoteza muda kwa mambo ya upuuzi
Watu wengi hasa vijana hupoteza masaa juu ya Facebook wakati wangeliutumia muda ule kwa kufanya kitu cha muhimu.

2. Mchanganyiko wa wanaume na wanawake
Ada kuu iliyoshamiri na kuenea kati ya watumiaji ya Facebook ni kutazama na kuongea na watu wasio Mahram zao.

3. Kutokewepo kwa hayaa na heshima
Uislamu umekuja kulinda heshima ya binaadam lakini cha ajabu vijana wengi wa Kiislamu hutokwa na hayaa na huvuruga heshima zao kupitia Facebook. Wasichana wangapi wameweka picha zao bila ya hijaab kwenye Facebook kwa kutaka kujionyesha? Wanawake wangapi wameharibu heshima zao na za familia zao kwa kutuma maasi yao kwenye Facebook?

4. Kukashifiwa Mtume na Uislam
Kubwa zaidi na baya zaidi na la hatari zaidi, ni hili lililotokea majuzi la kukashiwa kwa Mtume kwenye Facebook, jambo ambalo limewasikitisha wengi wetu na tuna kila haki ya kuhuzunika juu ya hilo. Picha mbalimbali za kashfa na za kumlinganisha Mtume wetu mtukufu Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mambo maovu na machafu, zimewekwa huko kwa kuchorwa vikatuni vinavyodaiwa kuwa ni yeye. Na yamejitokeza makundi tofauti yaliyoungana huko kwenye Facebook ili kuukashifu Uislamu na Waislamu na kumdhalilisha Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Haya yote ni matunda ya hiyo Facebook.

Suluhisho
Baada ya kujionea na kutafakari juu ya madhara na manufaa yaliyomo kwenye Facebook, lilobakia ni kujiamulia mwenyewe. Ikiwa utaona kwamba Facebook madhara yake ni makubwa kuliko faida, basi ni juu yako kujihadhari juu ya kuitumia na bora zaidi kujiepusha nayo.
Ikiwa utaona kwamba manufaa yamezidi basi ni pia juu yako kujichunga na madhara yaliyomo huko. Inawezekana kitu ukakiona kina manufaa kadhaa lakini madhara yake ni mengi zaidi. Allaah Anasema kuhusu ulevi na kamari
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَآ أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا
“Wanakuuliza kuhusu ulevi na kamari, sema ndani yake yamo madhara mengi na manufaa kwa watu, lakini madhara ni makubwa kuliko manufaa.” [Al-Baqarah 2: 219]
Isitoshe, pahala ambapo anatukanwa Allaah au Mtume Wake, au Qur-aan au Sunnah au jambo lolote la Dini, basi sehemu hiyo inapaswa kuhamwa au kutengwa hadi itakapojirudi au kuomba radhi na kubadili mwelekeo wako. Na ikiwa Facebook imeomba radhi kwa matendo yake ya kumtusi na kumdhalilisha Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), hapo tena Muislamu ana khiyari ya kutumia ukumbi huo kwa manufaa yaliyotajwa au kuuacha na kuutenga kwa madhara yaliyoelezwa. Na bia shaka madhara na uadui waliouonyesha kwa Uislamu na Waislamu, unamtosha Muislamu kuwa mbali na ukumbi kama huo au mwengine wowote unaofanana na huo.
Kadhalika hivi sasa Waislamu wamefungua kumbi kama hizo za kuweka mambo yanayowahusu Waislamu na yasiyokuwa na fitnah ndani yake wala utata.
Kwahiyo, tujihadhari, hasa katika mambo ambayo yana utata ili tuweze kulinda Dini yetu na heshima yetu.

 Posted By Posted juu ya Monday, December 03 @ 23:09:49 PST na MediaSwahiliTeam
 

Comments 💬 التعليقات
 

For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا

Kuhusiana Viungo

· zaidi Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis:
Jinsi Ya Kumfurahisha Mkeo


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora
Vizuri Sana
Mema
Kawaidar
Mbaya


Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa Rafiki





Mada zinazohusiana

Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

 

Ẹsin Islam الدين الإسلامي Religion of Islam Addinin Musulunci Agama Islam Religión del Islam 伊斯兰教 Dini ya Kiislamu Религия Ислам Religião do Islã イスラム教 Esin Islam 이슬람의 종교 Portal African Muslim Website - Arabic English African Islamic Website For World News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Articles, Radio, Audio, Video, Quran, Hadith, TV Channels, Fatwas, Muslim News, Newspapers, Magazines Headlines, Forums, College, Schools, Universities, Mosques, Quranic, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Ramadan, Vidoes, Books, Fasting, PDFs On EsinIslam.Com And IslamAfrica.Com