1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ
Swahili
Alif Lam Raa. Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha.
|
Ayah 12:2 الأية
إِنَّا أَنزَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ
Swahili
Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'ani kwa Kiarabu ili mpate kuzingatia.
|
Ayah 12:3 الأية
نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ بِمَا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ هَٰذَا
الْقُرْآنَ وَإِن كُنتَ مِن قَبْلِهِ لَمِنَ الْغَافِلِينَ
Swahili
Sisi tunasimulia simulizi nzuri kwa kukufunulia Qur'ani hii. Na ijapo kuwa kabla
ya haya ulikuwa miongoni mwa wasio jua.
|
Ayah 12:4 الأية
إِذْ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ إِنِّي رَأَيْتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوْكَبًا
وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ رَأَيْتُهُمْ لِي سَاجِدِينَ
Swahili
Yusuf alipo mwambia baba yake: Ewe babaangu! Hakika mimi nimeota nyota kumi na
moja, na jua, na mwezi. Nimeota zikinisujudia.
|
Ayah 12:5 الأية
قَالَ يَا بُنَيَّ لَا تَقْصُصْ رُؤْيَاكَ عَلَىٰ إِخْوَتِكَ فَيَكِيدُوا لَكَ
كَيْدًا ۖ إِنَّ الشَّيْطَانَ لِلْإِنسَانِ عَدُوٌّ مُّبِينٌ
Swahili
(Baba) akasema: Ewe mwanangu! Usiwasimulie nduguzo ndoto yako, wasije
wakakufanyia vitimbi. Hakika Shet'ani ni adui aliye dhaahiri kwa mwanaadamu.
|
Ayah 12:6 الأية
وَكَذَٰلِكَ يَجْتَبِيكَ رَبُّكَ وَيُعَلِّمُكَ مِن تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ
وَيُتِمُّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَعَلَىٰ آلِ يَعْقُوبَ كَمَا أَتَمَّهَا عَلَىٰ
أَبَوَيْكَ مِن قَبْلُ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ
Swahili
Na kadhaalika Mola wako Mlezi atakuteuwa na atakufundisha tafsiri ya mambo. Na
atatimiza neema zake juu yako na juu ya ukoo wa Yaa'qub, kama alivyo watimizia
hapo zamani baba zako Ibrahim na Is-haq. Hakika Mola wako Mlezi ni Mjuzi Mwenye
hikima.
|
Ayah 12:7 الأية
لَّقَدْ كَانَ فِي يُوسُفَ وَإِخْوَتِهِ آيَاتٌ لِّلسَّائِلِينَ
Swahili
Kwa yakini katika Yusuf na nduguze ziko ishara kwa wanao uliza.
|
Ayah 12:8 الأية
إِذْ قَالُوا لَيُوسُفُ وَأَخُوهُ أَحَبُّ إِلَىٰ أَبِينَا مِنَّا وَنَحْنُ
عُصْبَةٌ إِنَّ أَبَانَا لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ
Swahili
Pale walipo sema: Hakika Yusuf na nduguye wanapendwa zaidi na baba yetu kuliko
sisi, hali sisi ni kikundi chenye nguvu. Hakika baba yetu yumo katika upotofu wa
dhaahiri.
|
Ayah 12:9 الأية
اقْتُلُوا يُوسُفَ أَوِ اطْرَحُوهُ أَرْضًا يَخْلُ لَكُمْ وَجْهُ أَبِيكُمْ
وَتَكُونُوا مِن بَعْدِهِ قَوْمًا صَالِحِينَ
Swahili
Muuweni Yusuf, au mtupeni nchi mbali ili uso wa baba yenu ukuelekeeni nyinyi. Na
baada ya haya mtakuwa watu wema.
|
Ayah 12:10 الأية
قَالَ قَائِلٌ مِّنْهُمْ لَا تَقْتُلُوا يُوسُفَ وَأَلْقُوهُ فِي غَيَابَتِ
الْجُبِّ يَلْتَقِطْهُ بَعْضُ السَّيَّارَةِ إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ
Swahili
Akasema msemaji kati yao: Msimuuwe Yusuf. Lakini mtumbukizeni ndani ya kisima.
Wasafiri watakuja mwokota; kama nyinyi mna sharti ya kufanya jambo.
|
Ayah 12:11 الأية
قَالُوا يَا أَبَانَا مَا لَكَ لَا تَأْمَنَّا عَلَىٰ يُوسُفَ وَإِنَّا لَهُ
لَنَاصِحُونَ
Swahili
Wakasema: Ewe baba yetu! Una nini hata hutuamini kwa Yusuf? Na hakika sisi ni
wenye kumtakia kheri!
|
Ayah 12:12 الأية
أَرْسِلْهُ مَعَنَا غَدًا يَرْتَعْ وَيَلْعَبْ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ
Swahili
Mpeleke kesho pamoja nasi, ale kwa furaha na acheze; na bila ya shaka sisi
tutamhifadhi.
|
Ayah 12:13 الأية
قَالَ إِنِّي لَيَحْزُنُنِي أَن تَذْهَبُوا بِهِ وَأَخَافُ أَن يَأْكُلَهُ
الذِّئْبُ وَأَنتُمْ عَنْهُ غَافِلُونَ
Swahili
Akasem: Kwa hakika inanihuzunisha kwamba nyinyi mwende naye, na ninaogopa asije
mbwa mwitu akamla nanyi mmeghafilika naye.
|
Ayah 12:14 الأية
قَالُوا لَئِنْ أَكَلَهُ الذِّئْبُ وَنَحْنُ عُصْبَةٌ إِنَّا إِذًا لَّخَاسِرُونَ
Swahili
Wakasema: Ikiwa mbwa mwitu atamla na hali sisi ni kundi lenye nguvu kabisa, basi
bila ya shaka sisi tutakuwa khasarani.
|
Ayah 12:15 الأية
فَلَمَّا ذَهَبُوا بِهِ وَأَجْمَعُوا أَن يَجْعَلُوهُ فِي غَيَابَتِ الْجُبِّ ۚ
وَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِ لَتُنَبِّئَنَّهُم بِأَمْرِهِمْ هَٰذَا وَهُمْ لَا
يَشْعُرُونَ
Swahili
Basi walipo mchukua na wakakubaliana wamtumbukize ndani ya kisima, tulimfunulia
Yusuf: Hapana shaka yoyote utakuja waambia kwa jambo lao hili, na wala wao
hawatambui.
|
Ayah 12:16 الأية
وَجَاءُوا أَبَاهُمْ عِشَاءً يَبْكُونَ
Swahili
Wakaja kwa baba yao usiku wakilia.
|
Ayah 12:17 الأية
قَالُوا يَا أَبَانَا إِنَّا ذَهَبْنَا نَسْتَبِقُ وَتَرَكْنَا يُوسُفَ عِندَ
مَتَاعِنَا فَأَكَلَهُ الذِّئْبُ ۖ وَمَا أَنتَ بِمُؤْمِنٍ لَّنَا وَلَوْ كُنَّا
صَادِقِينَ
Swahili
Wakasema: Ewe baba yetu! Hakika tulikwenda kushindana na tukamwacha Yusuf penye
vitu vyetu. Basi mbwa mwitu akamla. Lakini wewe hutuamini ijapo kuwa tunasema
kweli.
|
Ayah 12:18 الأية
وَجَاءُوا عَلَىٰ قَمِيصِهِ بِدَمٍ كَذِبٍ ۚ قَالَ بَلْ سَوَّلَتْ لَكُمْ
أَنفُسُكُمْ أَمْرًا ۖ فَصَبْرٌ جَمِيلٌ ۖ وَاللهُ الْمُسْتَعَانُ عَلَىٰ مَا
تَصِفُونَ
Swahili
Wakaja na kanzu yake ina damu ya uwongo. Akasema: Bali nafsi zenu
zimekushawishini kutenda kitendo. Lakini subira ni njema; na Mwenyezi Mungu
ndiye wa kuombwa msaada kwa haya mnayo yaeleza.
|
Ayah 12:19 الأية
وَجَاءَتْ سَيَّارَةٌ فَأَرْسَلُوا وَارِدَهُمْ فَأَدْلَىٰ دَلْوَهُ ۖ قَالَ يَا
بُشْرَىٰ هَٰذَا غُلَامٌ ۚ وَأَسَرُّوهُ بِضَاعَةً ۚ وَاللهُ عَلِيمٌ بِمَا
يَعْمَلُونَ
Swahili
Ukafika msafara, wakamtuma mchota maji wao, naye akatumbukiza ndoo yake.
Alisema: Kheri Inshallah! Huyu hapa mvulana! Wakamficha ili kumfanya ni bidhaa.
Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa wanayo yatenda.
|
Ayah 12:20 الأية
وَشَرَوْهُ بِثَمَنٍ بَخْسٍ دَرَاهِمَ مَعْدُودَةٍ وَكَانُوا فِيهِ مِنَ
الزَّاهِدِينَ
Swahili
Na wakamuuza kwa thamani duni, kwa akali ya pesa. Wala hawakuwa na haja naye.
|
Ayah 12:21 الأية
وَقَالَ الَّذِي اشْتَرَاهُ مِن مِّصْرَ لِامْرَأَتِهِ أَكْرِمِي مَثْوَاهُ عَسَىٰ
أَن يَنفَعَنَا أَوْ نَتَّخِذَهُ وَلَدًا ۚ وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي
الْأَرْضِ وَلِنُعَلِّمَهُ مِن تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ ۚ وَاللهُ غَالِبٌ عَلَىٰ
أَمْرِهِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ
Swahili
Na yule aliye mnunua huko Misri alimwambia mkewe: Mtengenezee makaazi ya hishima
huyu; huenda akatufaa au tukamfanya mwenetu. Na kama hivyo tulimweka Yusuf
katika nchi ili tumfundishe kufasiri mambo. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye
kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.
|
Ayah 12:22 الأية
وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي
الْمُحْسِنِينَ
Swahili
Na alipo fikilia utu uzima tulimpa hukumu na ilimu. Na kama hivi tunawalipa
wanao tenda mema.
|
Ayah 12:23 الأية
وَرَاوَدَتْهُ الَّتِي هُوَ فِي بَيْتِهَا عَن نَّفْسِهِ وَغَلَّقَتِ الْأَبْوَابَ
وَقَالَتْ هَيْتَ لَكَ ۚ قَالَ مَعَاذَ اللهِ ۖ إِنَّهُ رَبِّي أَحْسَنَ
مَثْوَايَ ۖ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ
Swahili
Na yule bibi wa nyumba aliyo kuwamo Yusuf alimtamani kinyume cha nafsi yake, na
akafunga milango. Akamwambia: Njoo! Yusuf akasema: Audhubillahi! Najikinga na
Mwenyezi Mungu. Huyu bwana wangu kaniweka maskani nzuri, na hakika wenye
kudhulumu hawatengenekewi.
|
Ayah 12:24 الأية
وَلَقَدْ هَمَّتْ بِهِ ۖ وَهَمَّ بِهَا لَوْلَا أَن رَّأَىٰ بُرْهَانَ رَبِّهِ ۚ
كَذَٰلِكَ لِنَصْرِفَ عَنْهُ السُّوءَ وَالْفَحْشَاءَ ۚ إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا
الْمُخْلَصِينَ
Swahili
Na hakika yule mwanamke alimtamani, na Yusuf angeli mtamani lau kuwa hakuona
ishara ya Mola wake Mlezi. Hayo hivyo ni kwa ajili tumuepushe na uovu na uchafu.
Hakika yeye alikuwa katika waja wetu walio safishwa.
|
Ayah 12:25 الأية
وَاسْتَبَقَا الْبَابَ وَقَدَّتْ قَمِيصَهُ مِن دُبُرٍ وَأَلْفَيَا سَيِّدَهَا
لَدَى الْبَابِ ۚ قَالَتْ مَا جَزَاءُ مَنْ أَرَادَ بِأَهْلِكَ سُوءًا إِلَّا أَن
يُسْجَنَ أَوْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Swahili
Na wote wawili wakakimbilia mlangoni, na mwanamke akairarua kanzu yake Yusuf kwa
nyuma. Na wakamkuta bwana wake mlangoni. Mwanamke akasema: Hapana malipo ya
mwenye kutaka kumfanyia maovu mkeo isipo kuwa kufungwa au kupewa adhabu chungu.
|
Ayah 12:26 الأية
قَالَ هِيَ رَاوَدَتْنِي عَن نَّفْسِي ۚ وَشَهِدَ شَاهِدٌ مِّنْ أَهْلِهَا إِن
كَانَ قَمِيصُهُ قُدَّ مِن قُبُلٍ فَصَدَقَتْ وَهُوَ مِنَ الْكَاذِبِينَ
Swahili
Yusuf akasema: Yeye ndiye aliye nitaka bila ya mimi kumtaka. Na shahidi aliye
kuwa katika jamaa za mwanamke alisema: Ikiwa kanzu yake imechanwa mbele basi
mwanamke amesema kweli, naye Yusuf ni katika waongo.
|
Ayah 12:27 الأية
وَإِن كَانَ قَمِيصُهُ قُدَّ مِن دُبُرٍ فَكَذَبَتْ وَهُوَ مِنَ الصَّادِقِينَ
Swahili
Na ikiwa kanzu yake imechanwa nyuma, basi mwanamke amesema uwongo, naye Yusuf ni
katika wakweli.
|
Ayah 12:28 الأية
فَلَمَّا رَأَىٰ قَمِيصَهُ قُدَّ مِن دُبُرٍ قَالَ إِنَّهُ مِن كَيْدِكُنَّ ۖ إِنَّ
كَيْدَكُنَّ عَظِيمٌ
Swahili
Basi yule bwana alipoona kanzu yake imechanwa kwa nyuma, alisema: Hakika haya ni
katika vitimbi vyenu wanawake. Bila ya shaka vitimbi vyenu ni vikuu.
|
Ayah 12:29 الأية
يُوسُفُ أَعْرِضْ عَنْ هَٰذَا ۚ وَاسْتَغْفِرِي لِذَنبِكِ ۖ إِنَّكِ كُنتِ مِنَ
الْخَاطِئِينَ
Swahili
Yusuf! Wachilia mbali haya. Na wewe, mwanamke, omba msamaha kwa dhambi zako. Kwa
hakika wewe ni katika walio fanya makosa.
|
Ayah 12:30 الأية
وَقَالَ نِسْوَةٌ فِي الْمَدِينَةِ امْرَأَتُ الْعَزِيزِ تُرَاوِدُ فَتَاهَا عَن
نَّفْسِهِ ۖ قَدْ شَغَفَهَا حُبًّا ۖ إِنَّا لَنَرَاهَا فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ
Swahili
Na wanawake wa mjini wakawa wanasema: Mke wa Mheshimiwa anamtamani mtumishi wake
! Hakika amesalitika kwa mapenzi. Sisi hakika tunamwona yumo katika upotovu ulio
dhaahiri.
|
Ayah 12:31 الأية
فَلَمَّا سَمِعَتْ بِمَكْرِهِنَّ أَرْسَلَتْ إِلَيْهِنَّ وَأَعْتَدَتْ لَهُنَّ
مُتَّكَأً وَآتَتْ كُلَّ وَاحِدَةٍ مِّنْهُنَّ سِكِّينًا وَقَالَتِ اخْرُجْ
عَلَيْهِنَّ ۖ فَلَمَّا رَأَيْنَهُ أَكْبَرْنَهُ وَقَطَّعْنَ أَيْدِيَهُنَّ
وَقُلْنَ حَاشَ لِلَّهِ مَا هَٰذَا بَشَرًا إِنْ هَٰذَا إِلَّا مَلَكٌ كَرِيمٌ
Swahili
Alipo sikia yule bibi masengenyo yao aliwaita, na akawawekea matakia ya
kuegemea, na akampa kila mmoja wao kisu. Akamwambia Yusuf: Tokeza mbele yao.
Basi walipo mwona waliona ni kitu kikubwa kabisa, na wakajikata mikono yao.
Wakasema: Hasha Lillahi! Huyu si mwanaadamu. Hakuwa huyu ila ni Malaika mtukufu.
|
Ayah 12:32 الأية
قَالَتْ فَذَٰلِكُنَّ الَّذِي لُمْتُنَّنِي فِيهِ ۖ وَلَقَدْ رَاوَدتُّهُ عَن
نَّفْسِهِ فَاسْتَعْصَمَ ۖ وَلَئِن لَّمْ يَفْعَلْ مَا آمُرُهُ لَيُسْجَنَنَّ
وَلَيَكُونًا مِّنَ الصَّاغِرِينَ
Swahili
Yule bibi aksema: Huyu basi ndiye huyo mliye nilaumia! Na kweli mimi nilimtaka
naye akakataa. Na akitofanya ninayo muamrisha basi hapana shaka atafungwa
gerezani, na atakuwa miongoni mwa walio chini kabisa.
|
Ayah 12:33 الأية
قَالَ رَبِّ السِّجْنُ أَحَبُّ إِلَيَّ مِمَّا يَدْعُونَنِي إِلَيْهِ ۖ وَإِلَّا
تَصْرِفْ عَنِّي كَيْدَهُنَّ أَصْبُ إِلَيْهِنَّ وَأَكُن مِّنَ الْجَاهِلِينَ
Swahili
Yusuf akasema: Ee Mola Mlezi wangu! Nastahabu kifungo kuliko haya anayo niitia.
Na usipo niondoshea vitimbi vya wanawake mimi nitamili kwao, na nitakuwa katika
wajinga.
|
Ayah 12:34 الأية
فَاسْتَجَابَ لَهُ رَبُّهُ فَصَرَفَ عَنْهُ كَيْدَهُنَّ ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ
الْعَلِيمُ
Swahili
Basi Mola wake Mlezi akamwitikia, na akamwondoshea vitimbi vyao. Hakika Yeye ni
Msikizi Mjuzi.
|
Ayah 12:35 الأية
ثُمَّ بَدَا لَهُم مِّن بَعْدِ مَا رَأَوُا الْآيَاتِ لَيَسْجُنُنَّهُ حَتَّىٰ
حِينٍ
Swahili
Basi ikawadhihirikia baada ya kuona Ishara kuwa wamfunge kwa muda.
|
Ayah 12:36 الأية
وَدَخَلَ مَعَهُ السِّجْنَ فَتَيَانِ ۖ قَالَ أَحَدُهُمَا إِنِّي أَرَانِي أَعْصِرُ
خَمْرًا ۖ وَقَالَ الْآخَرُ إِنِّي أَرَانِي أَحْمِلُ فَوْقَ رَأْسِي خُبْزًا
تَأْكُلُ الطَّيْرُ مِنْهُ ۖ نَبِّئْنَا بِتَأْوِيلِهِ ۖ إِنَّا نَرَاكَ مِنَ
الْمُحْسِنِينَ
Swahili
Wakaingia gerezani pamoja naye vijana wawili. Mmoja wao akasema: Hakika mimi
nimeota nakamua mvinyo. Na mwingine akasema: Mimi nimeota nimebeba mikate juu ya
kichwa changu, na ndege wanaila. Hebu tuambie tafsiri yake, kwani sisi tunakuona
wewe ni katika watu wema.
|
Ayah 12:37 الأية
قَالَ لَا يَأْتِيكُمَا طَعَامٌ تُرْزَقَانِهِ إِلَّا نَبَّأْتُكُمَا بِتَأْوِيلِهِ
قَبْلَ أَن يَأْتِيَكُمَا ۚ ذَٰلِكُمَا مِمَّا عَلَّمَنِي رَبِّي ۚ إِنِّي تَرَكْتُ
مِلَّةَ قَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ بِاللهِ وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ
Swahili
Akasema: Hakitakufikilieni chakula mtakacho pewa ila nitakwambieni hakika yake
kabla hakijakufikieni. Haya ni katika yale aliyo nifundisha Mola wangu Mlezi.
Hakika mimi nimeacha mila ya watu wasio muamini Mwenyezi Mungu, na wakawa
hawaiamini Akhera.
|
Ayah 12:38 الأية
وَاتَّبَعْتُ مِلَّةَ آبَائِي إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۚ مَا كَانَ
لَنَا أَن نُّشْرِكَ بِاللهِ مِن شَيْءٍ ۚ ذَٰلِكَ مِن فَضْلِ اللهِ عَلَيْنَا
وَعَلَى النَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ
Swahili
Na nimefuata mila ya baba zangu, Ibrahim, na Is-haq, na Yaa'qub. Hatuna haki ya
kumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote. Hiyo ni katika fadhila ya Mwenyezi
Mungu juu yetu na juu ya watu; lakini watu wengi hawashukuru.
|
Ayah 12:39 الأية
يَا صَاحِبَيِ السِّجْنِ أَأَرْبَابٌ مُّتَفَرِّقُونَ خَيْرٌ أَمِ اللهُ
الْوَاحِدُ الْقَهَّارُ
Swahili
Enyi wafungwa wenzangu wawili! Je, mabwana wengi wanao farikiana wao kwa wao ni
bora au Mwenyezi Mungu Mmoja Mwenye nguvu?
|
Ayah 12:40 الأية
مَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِهِ إِلَّا أَسْمَاءً سَمَّيْتُمُوهَا أَنتُمْ وَآبَاؤُكُم
مَّا أَنزَلَ اللهُ بِهَا مِن سُلْطَانٍ ۚ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ ۚ
أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ
وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ
Swahili
Hamuabudu badala yake ila majina tu mliyo yapanga nyinyi na baba zenu. Mwenyezi
Mungu hakuyateremshia hayo uthibitisho wowote. Hapana hukumu ila ya Mwenyezi
Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini
Iliyo Nyooka. Lakini watu wengi hawajui.
|
Ayah 12:41 الأية
يَا صَاحِبَيِ السِّجْنِ أَمَّا أَحَدُكُمَا فَيَسْقِي رَبَّهُ خَمْرًا ۖ وَأَمَّا
الْآخَرُ فَيُصْلَبُ فَتَأْكُلُ الطَّيْرُ مِن رَّأْسِهِ ۚ قُضِيَ الْأَمْرُ
الَّذِي فِيهِ تَسْتَفْتِيَانِ
Swahili
Enyi wafungwa wenzangu wawili! Ama mmoja wenu atamnywesha bwana wake mvinyo. Na
ama mwengine atasulubiwa, na ndege watamla kichwa chake. Imekwisha katwa hukumu
ya hilo jambo mlilo kuwa mkiuliza.
|
Ayah 12:42 الأية
وَقَالَ لِلَّذِي ظَنَّ أَنَّهُ نَاجٍ مِّنْهُمَا اذْكُرْنِي عِندَ رَبِّكَ
فَأَنسَاهُ الشَّيْطَانُ ذِكْرَ رَبِّهِ فَلَبِثَ فِي السِّجْنِ بِضْعَ سِنِينَ
Swahili
Na akamwambia yule aliye jua kuwa atavuka katika wale wawili: Nikumbuke kwa
bwana wako. Lakini Shet'ani alimsahaulisha kumtaja kwa bwana wake. Basi Yusuf
akakaa gerezani miaka kadhaa.
|
Ayah 12:43 الأية
وَقَالَ الْمَلِكُ إِنِّي أَرَىٰ سَبْعَ بَقَرَاتٍ سِمَانٍ يَأْكُلُهُنَّ سَبْعٌ
عِجَافٌ وَسَبْعَ سُنبُلَاتٍ خُضْرٍ وَأُخَرَ يَابِسَاتٍ ۖ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ
أَفْتُونِي فِي رُؤْيَايَ إِن كُنتُمْ لِلرُّؤْيَا تَعْبُرُونَ
Swahili
Na siku moja mfalme alisema: Hakika mimi nimeota ng'ombe saba wanene wanaliwa na
ng'ombe saba walio konda. Na mashuke saba mabichi na mengine makavu. Enyi
waheshimiwa! Nambieni maana ya ndoto zangu, ikiwa nyinyi mnaweza kuagua ndoto.
|
Ayah 12:44 الأية
قَالُوا أَضْغَاثُ أَحْلَامٍ ۖ وَمَا نَحْنُ بِتَأْوِيلِ الْأَحْلَامِ بِعَالِمِينَ
Swahili
Wakasema: Hizi ni ndoto zilizo paraganyika, wala sisi sio wenye kujua tafsiri ya
ndoto hizi.
|
Ayah 12:45 الأية
وَقَالَ الَّذِي نَجَا مِنْهُمَا وَادَّكَرَ بَعْدَ أُمَّةٍ أَنَا أُنَبِّئُكُم
بِتَأْوِيلِهِ فَأَرْسِلُونِ
Swahili
Hapo akasema yule aliye okoka katika wale wawili akakumbuka baada ya muda: Mimi
nitakwambieni tafsiri yake. Basi nitumeni.
|
Ayah 12:46 الأية
يُوسُفُ أَيُّهَا الصِّدِّيقُ أَفْتِنَا فِي سَبْعِ بَقَرَاتٍ سِمَانٍ
يَأْكُلُهُنَّ سَبْعٌ عِجَافٌ وَسَبْعِ سُنبُلَاتٍ خُضْرٍ وَأُخَرَ يَابِسَاتٍ
لَّعَلِّي أَرْجِعُ إِلَى النَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَعْلَمُونَ
Swahili
Yusuf! Ewe mkweli! Tueleze nini maana ya ng'ombe saba wanene kuliwa na ng'ombe
saba walio konda. Na mashuke saba mabichi na mengine makavu, ili nirejee kwa
watu wapate kujua.
|
Ayah 12:47 الأية
قَالَ تَزْرَعُونَ سَبْعَ سِنِينَ دَأَبًا فَمَا حَصَدتُّمْ فَذَرُوهُ فِي
سُنبُلِهِ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّا تَأْكُلُونَ
Swahili
Akasema: Mtalima miaka saba kwa juhudi. Mtacho vuna kiwacheni katika mashuke
yake, isipo kuwa kidogo mtacho kula.
|
Ayah 12:48 الأية
ثُمَّ يَأْتِي مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ سَبْعٌ شِدَادٌ يَأْكُلْنَ مَا قَدَّمْتُمْ
لَهُنَّ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّا تُحْصِنُونَ
Swahili
Kisha itakuja baadaye miaka saba ya shida itakayo kula kile mlicho iwekea isipo
kuwa kidogo mtacho kihifadhi.
|
Ayah 12:49 الأية
ثُمَّ يَأْتِي مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ عَامٌ فِيهِ يُغَاثُ النَّاسُ وَفِيهِ
يَعْصِرُونَ
Swahili
Kisha baada ya haya utakuja mwaka ambao katika mwaka huo watu watasaidiwa, na
watakamua.
|
Ayah 12:50 الأية
وَقَالَ الْمَلِكُ ائْتُونِي بِهِ ۖ فَلَمَّا جَاءَهُ الرَّسُولُ قَالَ ارْجِعْ
إِلَىٰ رَبِّكَ فَاسْأَلْهُ مَا بَالُ النِّسْوَةِ اللَّاتِي قَطَّعْنَ
أَيْدِيَهُنَّ ۚ إِنَّ رَبِّي بِكَيْدِهِنَّ عَلِيمٌ
Swahili
Na mfalme akasema: Mleteni kwangu! Basi mjumbe alipo mjia Yusuf alisema: Rejea
kwa bwana wako ukamuulize khabari ya wale wanawake walio jikata mikono yao.
Hakika Mola wangu Mlezi anazijua vyema hila zao.
|
Ayah 12:51 الأية
قَالَ مَا خَطْبُكُنَّ إِذْ رَاوَدتُّنَّ يُوسُفَ عَن نَّفْسِهِ ۚ قُلْنَ حَاشَ
لِلَّهِ مَا عَلِمْنَا عَلَيْهِ مِن سُوءٍ ۚ قَالَتِ امْرَأَتُ الْعَزِيزِ الْآنَ
حَصْحَصَ الْحَقُّ أَنَا رَاوَدتُّهُ عَن نَّفْسِهِ وَإِنَّهُ لَمِنَ الصَّادِقِينَ
Swahili
Mfalme alisema: Mlikuwa mna nini mlipo mtaka Yusuf kinyume na nafsi yake?
Wakasema: Hasha Lillahi! Sisi hatukujua ubaya wowote kwake. Mke wa Mheshimiwa
akasema: Sasa haki imedhihiri. Mimi ndiye niliye mtaka kinyume na nafsi yake, na
hakika yeye ni katika wakweli.
|
Ayah 12:52 الأية
ذَٰلِكَ لِيَعْلَمَ أَنِّي لَمْ أَخُنْهُ بِالْغَيْبِ وَأَنَّ اللهَ لَا يَهْدِي
كَيْدَ الْخَائِنِينَ
Swahili
Hayo ni apate kujua ya kwamba mimi sikumfanyia khiyana nyuma yake; na ya kwamba
Mwenyezi Mungu haziongoi hila za makhaini.
|
Ayah 12:53 الأية
وَمَا أُبَرِّئُ نَفْسِي ۚ إِنَّ النَّفْسَ لَأَمَّارَةٌ بِالسُّوءِ إِلَّا مَا
رَحِمَ رَبِّي ۚ إِنَّ رَبِّي غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Swahili
NAMI sijitoi lawamani. Kwa hakika nafsi ni mno kuamrisha maovu, isipo kuwa ile
ambayo Mola wangu Mlezi aliyo irehemu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Msamehevu na
Mwenye kurehemu.
|
Ayah 12:54 الأية
وَقَالَ الْمَلِكُ ائْتُونِي بِهِ أَسْتَخْلِصْهُ لِنَفْسِي ۖ فَلَمَّا كَلَّمَهُ
قَالَ إِنَّكَ الْيَوْمَ لَدَيْنَا مَكِينٌ أَمِينٌ
Swahili
Basi mfalme akasema: Mleteni kwangu, awe wangu mwenyewe khasa. Basi alipo
msemeza alinena: Hakika wewe leo umekwisha tamakani kwetu na umeaminika.
|
Ayah 12:55 الأية
قَالَ اجْعَلْنِي عَلَىٰ خَزَائِنِ الْأَرْضِ ۖ إِنِّي حَفِيظٌ عَلِيمٌ
Swahili
Yusuf akasema: Nifanye mshika khazina za nchi. Kwani hakika mimi ni mlinzi
mjuzi.
|
Ayah 12:56 الأية
وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي الْأَرْضِ يَتَبَوَّأُ مِنْهَا حَيْثُ يَشَاءُ
ۚ نُصِيبُ بِرَحْمَتِنَا مَن نَّشَاءُ ۖ وَلَا نُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ
Swahili
Basi namna hivi tukampa Yusuf cheo katika nchi; anakaa humo popote anapo penda.
Tunamfikishia rehema zetu tumtakaye, wala hatupuuzi malipo ya wafanyao mema.
|
Ayah 12:57 الأية
وَلَأَجْرُ الْآخِرَةِ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ
Swahili
Na hakika malipo ya Akhera ni bora zaidi, kwa walio amini na wakawa wachamngu.
|
Ayah 12:58 الأية
وَجَاءَ إِخْوَةُ يُوسُفَ فَدَخَلُوا عَلَيْهِ فَعَرَفَهُمْ وَهُمْ لَهُ مُنكِرُونَ
Swahili
Wakaja ndugu zake Yusuf, na wakaingia kwake. Yeye akawajua na wao hawakumjua.
|
Ayah 12:59 الأية
وَلَمَّا جَهَّزَهُم بِجَهَازِهِمْ قَالَ ائْتُونِي بِأَخٍ لَّكُم مِّنْ أَبِيكُمْ
ۚ أَلَا تَرَوْنَ أَنِّي أُوفِي الْكَيْلَ وَأَنَا خَيْرُ الْمُنزِلِينَ
Swahili
Na alipo watengenezea tayari haja yao alisema: Nileteeni ndugu yenu kwa baba.
Je! Hamwoni ya kwamba mimi ninatimiza kipimo, nami ni mbora wa kukirimu?
|
Ayah 12:60 الأية
فَإِن لَّمْ تَأْتُونِي بِهِ فَلَا كَيْلَ لَكُمْ عِندِي وَلَا تَقْرَبُونِ
Swahili
Na msipo niletea basi hampati kipimo chochote kwangu, wala msinikurubie.
|
Ayah 12:61 الأية
قَالُوا سَنُرَاوِدُ عَنْهُ أَبَاهُ وَإِنَّا لَفَاعِلُونَ
Swahili
Wakasema: Sisi tutamrairai baba yake; na bila ya shaka tutafanya hayo.
|
Ayah 12:62 الأية
وَقَالَ لِفِتْيَانِهِ اجْعَلُوا بِضَاعَتَهُمْ فِي رِحَالِهِمْ لَعَلَّهُمْ
يَعْرِفُونَهَا إِذَا انقَلَبُوا إِلَىٰ أَهْلِهِمْ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ
Swahili
Na Yusuf akawaambia watumishi wake: Tieni bidhaa zao katika mizigo yao, ili
wazione watakapo rudi kwa watu wao wapate kurejea tena.
|
Ayah 12:63 الأية
فَلَمَّا رَجَعُوا إِلَىٰ أَبِيهِمْ قَالُوا يَا أَبَانَا مُنِعَ مِنَّا الْكَيْلُ
فَأَرْسِلْ مَعَنَا أَخَانَا نَكْتَلْ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ
Swahili
Basi walipo rejea kwa baba yao, walisema: Ewe baba yetu! Tumenyimwa chakula
zaidi, basi mpeleke nasi ndugu yetu ili tupate kupimiwa; na yakini sisi
tutamlinda.
|
Ayah 12:64 الأية
قَالَ هَلْ آمَنُكُمْ عَلَيْهِ إِلَّا كَمَا أَمِنتُكُمْ عَلَىٰ أَخِيهِ مِن قَبْلُ
ۖ فَاللهُ خَيْرٌ حَافِظًا ۖ وَهُوَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ
Swahili
Je, nikuaminini kwa huyu ila kama nilivyo kuaminini kwa nduguye zamani? Lakini
Mwenyezi Mungu ndiye Mbora wa kulinda, naye ndiye Mbora wa kurehemu kuliko wenye
kurehemu wote.
|
Ayah 12:65 الأية
وَلَمَّا فَتَحُوا مَتَاعَهُمْ وَجَدُوا بِضَاعَتَهُمْ رُدَّتْ إِلَيْهِمْ ۖ
قَالُوا يَا أَبَانَا مَا نَبْغِي ۖ هَٰذِهِ بِضَاعَتُنَا رُدَّتْ إِلَيْنَا ۖ
وَنَمِيرُ أَهْلَنَا وَنَحْفَظُ أَخَانَا وَنَزْدَادُ كَيْلَ بَعِيرٍ ۖ ذَٰلِكَ
كَيْلٌ يَسِيرٌ
Swahili
Na walipo fungua mizigo yao wakakuta bidhaa zao wamerudishiwa. Wakasema: Ewe
baba yetu! Tutake nini zaidi? Hizi bidhaa zetu tumerudishiwa. Wacha tuwaletee
watu wetu chakula, na tutamlinda ndugu yetu, na tutaongeza shehena ya ngamia. Na
hicho ni kipimo kidogo.
|
Ayah 12:66 الأية
قَالَ لَنْ أُرْسِلَهُ مَعَكُمْ حَتَّىٰ تُؤْتُونِ مَوْثِقًا مِّنَ اللهِ
لَتَأْتُنَّنِي بِهِ إِلَّا أَن يُحَاطَ بِكُمْ ۖ فَلَمَّا آتَوْهُ مَوْثِقَهُمْ
قَالَ اللهُ عَلَىٰ مَا نَقُولُ وَكِيلٌ
Swahili
Akasema: Sitampeleka nanyi mpaka mnipe ahadi kwa Mwenyezi Mungu kwamba lazima
mtamrejeza kwangu, ila ikiwa mmezungukwa. Basi walipo mpa ahadi yao alisema:
Mwenyezi Mungu ndiye Mtegemewa kwa tuyasemayo.
|
Ayah 12:67 الأية
وَقَالَ يَا بَنِيَّ لَا تَدْخُلُوا مِن بَابٍ وَاحِدٍ وَادْخُلُوا مِنْ أَبْوَابٍ
مُّتَفَرِّقَةٍ ۖ وَمَا أُغْنِي عَنكُم مِّنَ اللهِ مِن شَيْءٍ ۖ إِنِ الْحُكْمُ
إِلَّا لِلَّهِ ۖ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ ۖ وَعَلَيْهِ فَلْيَتَوَكَّلِ
الْمُتَوَكِّلُونَ
Swahili
Na akasema: Enyi wanangu! Msiingie mlango mmoja, bali ingieni kwa milango mbali
mbali. Wala mimi sikufaeni kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Hukumu haiko ila kwa
Mwenyezi Mungu tu. Juu yake Yeye mimi nimetegemea, na juu yake Yeye wategemee
wanao tegemea.
|
Ayah 12:68 الأية
وَلَمَّا دَخَلُوا مِنْ حَيْثُ أَمَرَهُمْ أَبُوهُم مَّا كَانَ يُغْنِي عَنْهُم
مِّنَ اللهِ مِن شَيْءٍ إِلَّا حَاجَةً فِي نَفْسِ يَعْقُوبَ قَضَاهَا ۚ
وَإِنَّهُ لَذُو عِلْمٍ لِّمَا عَلَّمْنَاهُ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا
يَعْلَمُونَ
Swahili
Na walipo ingia kama alivyo waamrisha baba yao, haikuwafaa kitu kwa Mwenyezi
Mungu, isipo kuwa ni haja tu iliyo kuwa katika nafsi ya Yaa'qub aliitimiza. Na
hakika yeye alikuwa na ilimu kwa sababu tulimfundisha; lakini watu wengi
hawajui.
|
Ayah 12:69 الأية
وَلَمَّا دَخَلُوا عَلَىٰ يُوسُفَ آوَىٰ إِلَيْهِ أَخَاهُ ۖ قَالَ إِنِّي أَنَا
أَخُوكَ فَلَا تَبْتَئِسْ بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Swahili
Na walipo ingia kwa Yusuf alimchukua nduguye akasema: Mimi hakika ni nduguyo.
Basi usihuzunike kwa waliyo kuwa wakiyafanya .
|
Ayah 12:70 الأية
فَلَمَّا جَهَّزَهُم بِجَهَازِهِمْ جَعَلَ السِّقَايَةَ فِي رَحْلِ أَخِيهِ ثُمَّ
أَذَّنَ مُؤَذِّنٌ أَيَّتُهَا الْعِيرُ إِنَّكُمْ لَسَارِقُونَ
Swahili
Na alipo kwisha watengenezea mahitaji yao akakitia kikopo cha kunywea maji
katika mzigo wa nduguye huyo, kisha mnadi akanadi: Enyi wasafiri! Hapana shaka
nyinyi ni wezi!
|
Ayah 12:71 الأية
قَالُوا وَأَقْبَلُوا عَلَيْهِم مَّاذَا تَفْقِدُونَ
Swahili
Wakasema nao wamewakabili: Kwani mmepoteza nini?
|
Ayah 12:72 الأية
قَالُوا نَفْقِدُ صُوَاعَ الْمَلِكِ وَلِمَن جَاءَ بِهِ حِمْلُ بَعِيرٍ وَأَنَا
بِهِ زَعِيمٌ
Swahili
Wakasema: Tumepoteza kopo la mfalme. Na ataye lileta atapewa shehena nzima ya
ngamia. Nami ni dhaamini wa hayo.
|
Ayah 12:73 الأية
قَالُوا تَاللهِ لَقَدْ عَلِمْتُم مَّا جِئْنَا لِنُفْسِدَ فِي الْأَرْضِ وَمَا
كُنَّا سَارِقِينَ
Swahili
Wakasema: Wallahi! Mnajua vyema kwamba sisi hatukuja kufanya uharibifu katika
nchi hii, wala sisi si wezi.
|
Ayah 12:74 الأية
قَالُوا فَمَا جَزَاؤُهُ إِن كُنتُمْ كَاذِبِينَ
Swahili
Wakasema: Basi malipo yake yatakuwa nini ikiwa nyinyi ni waongo?
|
Ayah 12:75 الأية
قَالُوا جَزَاؤُهُ مَن وُجِدَ فِي رَحْلِهِ فَهُوَ جَزَاؤُهُ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي
الظَّالِمِينَ
Swahili
Wakasema: Malipo yake ni yule ambaye ataonekana nalo yeye huyo ndiye malipo
yake. Hivi ndivyo tunavyo walipa madhaalimu.
|
Ayah 12:76 الأية
فَبَدَأَ بِأَوْعِيَتِهِمْ قَبْلَ وِعَاءِ أَخِيهِ ثُمَّ اسْتَخْرَجَهَا مِن
وِعَاءِ أَخِيهِ ۚ كَذَٰلِكَ كِدْنَا لِيُوسُفَ ۖ مَا كَانَ لِيَأْخُذَ أَخَاهُ فِي
دِينِ الْمَلِكِ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللهُ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَاتٍ مَّن نَّشَاءُ ۗ
وَفَوْقَ كُلِّ ذِي عِلْمٍ عَلِيمٌ
Swahili
Basi akaanza kwenye mizigo yao kabla ya mzigo wa nduguye. Kisha akakitoa katika
mzigo wa nduguye. Hivi ndivyo tulivyo mpangia Yusuf. Hakuweza kumzuia nduguye
kwa sharia ya mfalme isipo kuwa alivyo taka Mwenyezi Mungu. Tunawatukuza kwenye
vyeo tuwatakao; na juu ya kila ajuaye yupo ajuaye zaidi.
|
Ayah 12:77 الأية
قَالُوا إِن يَسْرِقْ فَقَدْ سَرَقَ أَخٌ لَّهُ مِن قَبْلُ ۚ فَأَسَرَّهَا يُوسُفُ
فِي نَفْسِهِ وَلَمْ يُبْدِهَا لَهُمْ ۚ قَالَ أَنتُمْ شَرٌّ مَّكَانًا ۖ وَاللهُ
أَعْلَمُ بِمَا تَصِفُونَ
Swahili
Wakasema: Ikiwa huyu ameiba, basi nduguye vile vile aliiba zamani. Lakini Yusuf
aliyaweka siri moyoni mwake wala hakuwaonyesha. Akawaambia: Nyinyi mko katika
hali mbaya zaidi, na Mwenyezi Mungu anajua zaidi hayo mnayo singizia.
|
Ayah 12:78 الأية
قَالُوا يَا أَيُّهَا الْعَزِيزُ إِنَّ لَهُ أَبًا شَيْخًا كَبِيرًا فَخُذْ
أَحَدَنَا مَكَانَهُ ۖ إِنَّا نَرَاكَ مِنَ الْمُحْسِنِينَ
Swahili
Wakasema: Ewe Mheshimiwa! Huyu anaye baba mzee sana. Kwa hivyo mchukue mmoja
wetu badala yake. Hakika sisi tunakuona wewe ni katika watu wema.
|
Ayah 12:79 الأية
قَالَ مَعَاذَ اللهِ أَن نَّأْخُذَ إِلَّا مَن وَجَدْنَا مَتَاعَنَا عِندَهُ
إِنَّا إِذًا لَّظَالِمُونَ
Swahili
Akasema: Mwenyezi Mungu apishe mbali kumshika yeyote yule isipo kuwa tuliye
mkuta naye kitu chetu. Hivyo basi tutakuwa wenye kudhulumu.
|
Ayah 12:80 الأية
فَلَمَّا اسْتَيْأَسُوا مِنْهُ خَلَصُوا نَجِيًّا ۖ قَالَ كَبِيرُهُمْ أَلَمْ
تَعْلَمُوا أَنَّ أَبَاكُمْ قَدْ أَخَذَ عَلَيْكُم مَّوْثِقًا مِّنَ اللهِ وَمِن
قَبْلُ مَا فَرَّطتُمْ فِي يُوسُفَ ۖ فَلَنْ أَبْرَحَ الْأَرْضَ حَتَّىٰ يَأْذَنَ
لِي أَبِي أَوْ يَحْكُمَ اللهُ لِي ۖ وَهُوَ خَيْرُ الْحَاكِمِينَ
Swahili
Walipo kata tamaa naye wakenda kando kunong'ona. Mkubwa wao akasema: Je! Hamjui
ya kwamba baba yenu amechukua ahadi kwenu kutokana na Mwenyezi Mungu, na kabla
ya hapo mlimkosa katika agano lenu juu ya Yusuf? Basi mimi sitotoka nchi hii
mpaka baba yangu anipe ruhusa au Mwenyezi Mungu anihukumie. Na Yeye ndiye Mbora
wa mahakimu.
|
Ayah 12:81 الأية
ارْجِعُوا إِلَىٰ أَبِيكُمْ فَقُولُوا يَا أَبَانَا إِنَّ ابْنَكَ سَرَقَ وَمَا
شَهِدْنَا إِلَّا بِمَا عَلِمْنَا وَمَا كُنَّا لِلْغَيْبِ حَافِظِينَ
Swahili
Rudini kwa baba yenu, na mwambieni: Ee baba yetu! Mwanao ameiba. Na sisi hatutoi
ushahidi ila kwa tunayo yajua. Wala sisi hatukuwa wenye kuhifadhi mambo ya
ghaibu.
|
Ayah 12:82 الأية
وَاسْأَلِ الْقَرْيَةَ الَّتِي كُنَّا فِيهَا وَالْعِيرَ الَّتِي أَقْبَلْنَا
فِيهَا ۖ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ
Swahili
Na waulize watu wa mji tulio kuwako, na msafara tulio kuja nao. Na hakika sisi
tunasema kweli.
|
Ayah 12:83 الأية
قَالَ بَلْ سَوَّلَتْ لَكُمْ أَنفُسُكُمْ أَمْرًا ۖ فَصَبْرٌ جَمِيلٌ ۖ عَسَى
اللهُ أَن يَأْتِيَنِي بِهِمْ جَمِيعًا ۚ إِنَّهُ هُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ
Swahili
Akasema: Bali nafsi zenu zimekushawishini kwenye jambo fulani. Subira ni njema!
Asaa Mwenyezi Mungu akaniletea wote pamoja. Hakika Yeye ni Mjuzi Mwenye hikima.
|
Ayah 12:84 الأية
وَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَا أَسَفَىٰ عَلَىٰ يُوسُفَ وَابْيَضَّتْ عَيْنَاهُ
مِنَ الْحُزْنِ فَهُوَ كَظِيمٌ
Swahili
Naye akajitenga nao, na akasema: Ah! Masikini Yusuf! Na macho yake yakawa meupe
kwa huzuni aliyo kuwa akiizuia.
|
Ayah 12:85 الأية
قَالُوا تَاللهِ تَفْتَأُ تَذْكُرُ يُوسُفَ حَتَّىٰ تَكُونَ حَرَضًا أَوْ تَكُونَ
مِنَ الْهَالِكِينَ
Swahili
Wakasema: Wallahi! Huachi kumkumbuka Yusuf mpaka uwe mgonjwa au uwe katika walio
hiliki.
|
Ayah 12:86 الأية
قَالَ إِنَّمَا أَشْكُو بَثِّي وَحُزْنِي إِلَى اللهِ وَأَعْلَمُ مِنَ اللهِ
مَا لَا تَعْلَمُونَ
Swahili
Akasema: Hakika mimi namshitakia Mwenyezi Mungu sikitiko langu na huzuni yangu.
Na ninajua kwa Mwenyezi Mungu msiyo yajua nyinyi.
|
Ayah 12:87 الأية
يَا بَنِيَّ اذْهَبُوا فَتَحَسَّسُوا مِن يُوسُفَ وَأَخِيهِ وَلَا تَيْأَسُوا مِن
رَّوْحِ اللهِ ۖ إِنَّهُ لَا يَيْأَسُ مِن رَّوْحِ اللهِ إِلَّا الْقَوْمُ
الْكَافِرُونَ
Swahili
Enyi wanangu! Nendeni mkamtafute Yusuf na nduguye, wala msikate tamaa na faraji
ya Mwenyezi Mungu. Hakika hawakati tamaa na faraji ya Mwenyezi Mungu isipo kuwa
watu makafiri.
|
Ayah 12:88 الأية
فَلَمَّا دَخَلُوا عَلَيْهِ قَالُوا يَا أَيُّهَا الْعَزِيزُ مَسَّنَا وَأَهْلَنَا
الضُّرُّ وَجِئْنَا بِبِضَاعَةٍ مُّزْجَاةٍ فَأَوْفِ لَنَا الْكَيْلَ وَتَصَدَّقْ
عَلَيْنَا ۖ إِنَّ اللهَ يَجْزِي الْمُتَصَدِّقِينَ
Swahili
Basi walipo ingia kwa Yusuf walisema: Ewe Mheshimiwa! Imetupata shida, sisi na
watu wetu. Na tumeleta mali kidogo. Basi tupimie kipimo na fanya kama unatupa
sadaka. Hakika Mwenyezi Mungu huwalipa watoao sadaka.
|
Ayah 12:89 الأية
قَالَ هَلْ عَلِمْتُم مَّا فَعَلْتُم بِيُوسُفَ وَأَخِيهِ إِذْ أَنتُمْ جَاهِلُونَ
Swahili
Akasema: Je! Mmejua mliyo mfanyia Yusuf na nduguye mlipo kuwa wajinga?
|
Ayah 12:90 الأية
قَالُوا أَإِنَّكَ لَأَنتَ يُوسُفُ ۖ قَالَ أَنَا يُوسُفُ وَهَٰذَا أَخِي ۖ قَدْ
مَنَّ اللهُ عَلَيْنَا ۖ إِنَّهُ مَن يَتَّقِ وَيَصْبِرْ فَإِنَّ اللهَ لَا
يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ
Swahili
Wakasema: Kumbe wewe ndiye Yusuf? Akasema: Mimi ndiye Yusuf, na huyu ni ndugu
yangu. Mwenyezi Mungu ametufanyia hisani. Hakika anaye mcha Mungu na akasubiri,
basi Mwenyezi Mungu haachi ukapotea ujira wa wafanyao mema.
|
Ayah 12:91 الأية
قَالُوا تَاللهِ لَقَدْ آثَرَكَ اللهُ عَلَيْنَا وَإِن كُنَّا لَخَاطِئِينَ
Swahili
Wakasema: Wallahi! Mwenyezi Mungu amekufadhilisha wewe kuliko sisi, na hakika
sisi tulikuwa wenye kukosa.
|
Ayah 12:92 الأية
قَالَ لَا تَثْرِيبَ عَلَيْكُمُ الْيَوْمَ ۖ يَغْفِرُ اللهُ لَكُمْ ۖ وَهُوَ
أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ
Swahili
Akasema: Leo hapana lawama juu yenu. Mwenyezi Mungu atakusameheni, naye ni
Mwingi wa kurehemu kuliko wote wanao rehemu.
|
Ayah 12:93 الأية
اذْهَبُوا بِقَمِيصِي هَٰذَا فَأَلْقُوهُ عَلَىٰ وَجْهِ أَبِي يَأْتِ بَصِيرًا
وَأْتُونِي بِأَهْلِكُمْ أَجْمَعِينَ
Swahili
Nendeni na kanzu yangu hii na mumwekee usoni baba yangu, atakuwa mwenye kuona.
Na mje nao watu wenu wote wa nyumbani.
|
Ayah 12:94 الأية
وَلَمَّا فَصَلَتِ الْعِيرُ قَالَ أَبُوهُمْ إِنِّي لَأَجِدُ رِيحَ يُوسُفَ ۖ
لَوْلَا أَن تُفَنِّدُونِ
Swahili
Na ulipo ondoka tu msafara baba yao alisema: Hakika mimi nasikia harufu ya
Yusuf, lau kuwa hamtanituhumu.
|
Ayah 12:95 الأية
قَالُوا تَاللهِ إِنَّكَ لَفِي ضَلَالِكَ الْقَدِيمِ
Swahili
Wakasema: Wallahi! Hakika bado ungali katika upotovu wako wa zamani.
|
Ayah 12:96 الأية
فَلَمَّا أَن جَاءَ الْبَشِيرُ أَلْقَاهُ عَلَىٰ وَجْهِهِ فَارْتَدَّ بَصِيرًا ۖ
قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ إِنِّي أَعْلَمُ مِنَ اللهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ
Swahili
Basi alipo fika mbashiri na akaiweka kanzu usoni pake alirejea kuona. Akasema:
Je! Sikukwambieni kuwa mimi najua ya Mwenyezi Mungu msiyo yajua nyinyi?
|
Ayah 12:97 الأية
قَالُوا يَا أَبَانَا اسْتَغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا إِنَّا كُنَّا خَاطِئِينَ
Swahili
Wakasema: Ee baba yetu! Tuombee msamaha kwa dhambi zetu. Hapana shaka sisi
tulikuwa na makosa.
|
Ayah 12:98 الأية
قَالَ سَوْفَ أَسْتَغْفِرُ لَكُمْ رَبِّي ۖ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ
Swahili
Akasema: Nitakuja kuombeeni msamaha kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ndiye
Mwenye maghfira na Mwenye kusamehe.
|
Ayah 12:99 الأية
فَلَمَّا دَخَلُوا عَلَىٰ يُوسُفَ آوَىٰ إِلَيْهِ أَبَوَيْهِ وَقَالَ ادْخُلُوا
مِصْرَ إِن شَاءَ اللهُ آمِنِينَ
Swahili
Na walipo ingia kwa Yusuf aliwakumbatia wazazi wake na akasema: Ingieni Misri,
Inshallah, mmo katika amani.
|
Ayah 12:100 الأية
وَرَفَعَ أَبَوَيْهِ عَلَى الْعَرْشِ وَخَرُّوا لَهُ سُجَّدًا ۖ وَقَالَ يَا أَبَتِ
هَٰذَا تَأْوِيلُ رُؤْيَايَ مِن قَبْلُ قَدْ جَعَلَهَا رَبِّي حَقًّا ۖ وَقَدْ
أَحْسَنَ بِي إِذْ أَخْرَجَنِي مِنَ السِّجْنِ وَجَاءَ بِكُم مِّنَ الْبَدْوِ مِن
بَعْدِ أَن نَّزَغَ الشَّيْطَانُ بَيْنِي وَبَيْنَ إِخْوَتِي ۚ إِنَّ رَبِّي
لَطِيفٌ لِّمَا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ هُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ
Swahili
Na akawapandisha wazazi wake kwenye kiti cha enzi. Na wote wakaporomoka
kumsujudia. Na akasema: Ewe baba yangu! Hii ndiyo tafsiri ya ile ndoto yangu ya
zamani. Na Mwenyezi Mungu ameijaalia iwe kweli. Na Mwenyezi Mungu amenifanyia
wema kunitoa gerezani, na kukuleteni kutoka jangwani baada ya Shet'ani kuchochea
baina yangu na ndugu zangu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mpole kwa alitakalo. Bila
ya shaka Yeye ni Mjuzi Mwenye hikima.
|
Ayah 12:101 الأية
رَبِّ قَدْ آتَيْتَنِي مِنَ الْمُلْكِ وَعَلَّمْتَنِي مِن تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ
ۚ فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَنتَ وَلِيِّي فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖ
تَوَفَّنِي مُسْلِمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ
Swahili
Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika umenipa utawala, na umenifunza tafsiri ya mambo.
Ewe Muumba wa mbingu na ardhi! Wewe ndiye Mlinzi wangu katika dunia na Akhera.
Nifishe hali ya kuwa ni Muislamu na nichanganyishe na watendao mema.
|
Ayah 12:102 الأية
ذَٰلِكَ مِنْ أَنبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهِ إِلَيْكَ ۖ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ
أَجْمَعُوا أَمْرَهُمْ وَهُمْ يَمْكُرُونَ
Swahili
Hizi ni katika khabari za ghaibu tulizo kufunulia. Na hukuwa pamoja nao walipo
azimia shauri yao, walipo fanya njama zao wakizua vitimbi.
|
Ayah 12:103 الأية
وَمَا أَكْثَرُ النَّاسِ وَلَوْ حَرَصْتَ بِمُؤْمِنِينَ
Swahili
Na wengi wa watu si wenye kuamini hata ukijitahidi vipi..
|
Ayah 12:104 الأية
وَمَا تَسْأَلُهُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۚ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ
لِّلْعَالَمِينَ
Swahili
Wala wewe huwaombi ujira kwa haya. Hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu
wote.
|
Ayah 12:105 الأية
وَكَأَيِّن مِّنْ آيَةٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ يَمُرُّونَ عَلَيْهَا وَهُمْ
عَنْهَا مُعْرِضُونَ
Swahili
Na ishara ngapi katika mbingu na ardhi wanazo zipitia, na hali ya kuwa
wanazipuuza.
|
Ayah 12:106 الأية
وَمَا يُؤْمِنُ أَكْثَرُهُم بِاللهِ إِلَّا وَهُم مُّشْرِكُونَ
Swahili
Na wengi katika wao hawamuamini Mwenyezi Mungu pasina kuwa ni washirikina.
|
Ayah 12:107 الأية
أَفَأَمِنُوا أَن تَأْتِيَهُمْ غَاشِيَةٌ مِّنْ عَذَابِ اللهِ أَوْ تَأْتِيَهُمُ
السَّاعَةُ بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ
Swahili
Je! Wanaaminisha kuwa haitowajia adhabu ya Mwenyezi Mungu ya kuwagubika, au
haitawafikia Saa ya Kiyama kwa ghafla, na hali hawatambui?
|
Ayah 12:108 الأية
قُلْ هَٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ
اتَّبَعَنِي ۖ وَسُبْحَانَ اللهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ
Swahili
Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na
wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina.
|
Ayah 12:109 الأية
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِي إِلَيْهِم مِّنْ أَهْلِ
الْقُرَىٰ ۗ أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ
الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۗ وَلَدَارُ الْآخِرَةِ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ اتَّقَوْا ۗ
أَفَلَا تَعْقِلُونَ
Swahili
Na hatukuwatuma Mitume kabla yako isipo kuwa wanaume tulio wafunulia wahyi
miongoni mwa watu wa mijini. Je! Hawatembei katika ardhi wakaona jinsi ulivyo
kuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Na hakika nyumba ya Akhera ni bora kwa
wamchao Mungu. Basi hamfahamu?
|
Ayah 12:110 الأية
حَتَّىٰ إِذَا اسْتَيْأَسَ الرُّسُلُ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ قَدْ كُذِبُوا جَاءَهُمْ
نَصْرُنَا فَنُجِّيَ مَن نَّشَاءُ ۖ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُنَا عَنِ الْقَوْمِ
الْمُجْرِمِينَ
Swahili
Hata Mitume walipo kata tamaa na wakaona kuwa wamekadhibishwa, hapo ikawajia
nusura yetu, wakaokolewa tuwatakao. Na adhabu yetu haitowawacha kaumu ya
wakosefu.
|
Ayah 12:111 الأية
لَقَدْ كَانَ فِي قَصَصِهِمْ عِبْرَةٌ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ۗ مَا كَانَ حَدِيثًا
يُفْتَرَىٰ وَلَٰكِن تَصْدِيقَ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ كُلِّ شَيْءٍ
وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ
Swahili
Kwa hakika katika hadithi zao limo zingatio kwa wenye akili. Si maneno yaliyo
zuliwa, bali ni ya kusadikisha yaliyo kabla yake, na ufafanuzi wa kila kitu, na
ni uwongofu na rehema kwa kaumu yenye kuamini.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|