1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
الر ۚ كِتَابٌ أُحْكِمَتْ آيَاتُهُ ثُمَّ فُصِّلَتْ مِن لَّدُنْ حَكِيمٍ خَبِيرٍ
Alif-lam-ra kitabun ohkimatayatuhu thumma fussilat min ladun hakeeminkhabeer
Swahili
Alif Lam Ra. Hiki ni Kitabu ambacho Aya zake zimewekwa wazi, kisha
zikapambanuliwa, kilicho toka kwa Mwenye Hikima na Mwenye Khabari,
|
Ayah 11:2 الأية
أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللهَ ۚ إِنَّنِي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ
Alla taAAbudoo illa Allahainnanee lakum minhu natheerun wabasheer
Swahili
Ili msimuabudu isipo kuwa Allah, Mwenyezi Mungu. Hakika mimi kwenu ni mwonyaji
na mbashiri nitokae kwake.
|
Ayah 11:3 الأية
وَأَنِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُمَتِّعْكُم مَّتَاعًا
حَسَنًا إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى وَيُؤْتِ كُلَّ ذِي فَضْلٍ فَضْلَهُ ۖ وَإِن
تَوَلَّوْا فَإِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ كَبِيرٍ
Waani istaghfiroo rabbakum thumma toobooilayhi yumattiAAkum mataAAan hasanan
ilaajalin musamman wayu/ti kulla thee fadlin fadlahuwa-in tawallaw fa-inee
akhafu AAalaykum AAathabayawmin kabeer
Swahili
Na ili mumwombe msamaha Mola wenu Mlezi, kisha mtubie kwake. Atakustarehesheni
starehe nzuri mpaka muda maalumu. Na atampa kila mwenye fadhila, fadhila yake.
Na ikiwa mtakengeuka basi mimi nakukhofieni adhabu ya hiyo Siku Kubwa.
|
Ayah 11:4 الأية
إِلَى اللهِ مَرْجِعُكُمْ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ
Ila Allahi marjiAAukum wahuwaAAala kulli shay-in qadeer
Swahili
Marejeo yenu ni kwa Mwenyezi Mungu tu. Naye ni Muweza wa kila kitu.
|
Ayah 11:5 الأية
أَلَا إِنَّهُمْ يَثْنُونَ صُدُورَهُمْ لِيَسْتَخْفُوا مِنْهُ ۚ أَلَا حِينَ
يَسْتَغْشُونَ ثِيَابَهُمْ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ۚ إِنَّهُ
عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ
Ala innahum yathnoona sudoorahumliyastakhfoo minhu ala heena yastaghshoona
thiyabahumyaAAlamu ma yusirroona wama yuAAlinoona innahuAAaleemun bithati
assudoor
Swahili
Hebu angalia! Ati wanafunika vilivyomo vifuani mwao ili wamfiche Mwenyezi Mungu!
Jueni kuwa wanapo jigubika nguo zao Yeye anajua wanayo yaficha na wanayo
yatangaza. Hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.
|
Ayah 11:6 الأية
وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ إِلَّا عَلَى اللهِ رِزْقُهَا وَيَعْلَمُ
مُسْتَقَرَّهَا وَمُسْتَوْدَعَهَا ۚ كُلٌّ فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ
Wama min dabbatin fee al-ardiilla AAala Allahi rizquha wayaAAlamumustaqarraha
wamustawdaAAaha kullun fee kitabinmubeen
Swahili
NA HAKUNA mnyama yoyote katika ardhi ila riziki yake iko kwa Mwenyezi Mungu.
Naye anajua makao yake na mapitio yake. Yote yamo katika Kitabu chenye
kubainisha.
|
Ayah 11:7 الأية
وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ وَكَانَ
عَرْشُهُ عَلَى الْمَاءِ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا ۗ وَلَئِن
قُلْتَ إِنَّكُم مَّبْعُوثُونَ مِن بَعْدِ الْمَوْتِ لَيَقُولَنَّ الَّذِينَ
كَفَرُوا إِنْ هَٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ
Wahuwa allathee khalaqa assamawatiwal-arda fee sittati ayyamin wakanaAAarshuhu
AAala alma-i liyabluwakum ayyukum ahsanuAAamalan wala-in qulta innakum
mabAAoothoona min baAAdi almawtilayaqoolanna allatheena kafaroo in hatha
illasihrun mubeen
Swahili
Na Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Na Kiti chake cha
Enzi kilikuwa juu ya maji, ili akufanyieni mtihani ajuulikane ni nani miongoni
mwenu mzuri zaidi wa vitendo. Na wewe ukisema: Nyinyi hakika mtafufuliwa baada
ya kufa; wale walio kufuru husema: Hayakuwa haya ila ni uchawi uliyo wazi.
|
Ayah 11:8 الأية
وَلَئِنْ أَخَّرْنَا عَنْهُمُ الْعَذَابَ إِلَىٰ أُمَّةٍ مَّعْدُودَةٍ
لَّيَقُولُنَّ مَا يَحْبِسُهُ ۗ أَلَا يَوْمَ يَأْتِيهِمْ لَيْسَ مَصْرُوفًا
عَنْهُمْ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ
Wala-in akhkharna AAanhumu alAAathabaila ommatin maAAdoodatin layaqoolunna ma
yahbisuhuala yawma ya/teehim laysa masroofan AAanhum wahaqabihim ma kanoo bihi
yastahzi-oon
Swahili
Na tukiwacheleweshea adhabu mpaka muda ulio kwisha hisabiwa wao husema: Nini
kinacho izuia hiyo adhabu? Jueni! Siku itakapo wajia basi haitoondolewa hiyo
kwao. Na yatawazunguka yale waliyo kuwa wakiyafanyia mzaha.
|
Ayah 11:9 الأية
وَلَئِنْ أَذَقْنَا الْإِنسَانَ مِنَّا رَحْمَةً ثُمَّ نَزَعْنَاهَا مِنْهُ إِنَّهُ
لَيَئُوسٌ كَفُورٌ
Wala-in athaqna al-insanaminna rahmatan thumma nazaAAnahaminhu innahu layaoosun
kafoor
Swahili
Na tukimwonjesha mtu rehema inayo toka kwetu, kisha tukamwondolea, hukata tamaa
akakufuru.
|
Ayah 11:10 الأية
وَلَئِنْ أَذَقْنَاهُ نَعْمَاءَ بَعْدَ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُ لَيَقُولَنَّ ذَهَبَ
السَّيِّئَاتُ عَنِّي ۚ إِنَّهُ لَفَرِحٌ فَخُورٌ
Wala-in athaqnahu naAAmaabaAAda darraa massat-hu layaqoolanna thahabaassayyi-atu
AAannee innahu lafarihunfakhoor
Swahili
Na tukimwonjesha neema baada ya madhara yaliyo mpata husema: Taabu zimekwisha
niondokea. Hakika yeye hujitapa na kutafakhari.
|
Ayah 11:11 الأية
إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أُولَٰئِكَ لَهُم مَّغْفِرَةٌ
وَأَجْرٌ كَبِيرٌ
Illa allatheena sabaroowaAAamiloo assalihati ola-ika lahummaghfiratun waajrun
kabeer
Swahili
Ila wale walio subiri wakatenda mema. Hao watapata msamaha na ujira mkubwa.
|
Ayah 11:12 الأية
فَلَعَلَّكَ تَارِكٌ بَعْضَ مَا يُوحَىٰ إِلَيْكَ وَضَائِقٌ بِهِ صَدْرُكَ أَن
يَقُولُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ كَنزٌ أَوْ جَاءَ مَعَهُ مَلَكٌ ۚ إِنَّمَا
أَنتَ نَذِيرٌ ۚ وَاللهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ
FalaAAallaka tarikun baAAda mayooha ilayka wada-iqun bihi sadruka anyaqooloo
lawla onzila AAalayhi kanzun aw jaamaAAahu malakun innama anta natheerun
wallahuAAala kulli shay-in wakeel
Swahili
Basi labda utaacha baadhi ya yale yaliyo funuliwa kwako, na kifua kitaona dhiki
kwa hayo, kwa sababu wanasema: Mbona hakuteremshiwa khazina, au wakaja naye
Malaika? Wewe ni mwonyaji tu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa kila kitu.
|
Ayah 11:13 الأية
أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ فَأْتُوا بِعَشْرِ سُوَرٍ مِّثْلِهِ
مُفْتَرَيَاتٍ وَادْعُوا مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللهِ إِن كُنتُمْ
صَادِقِينَ
Am yaqooloona iftarahu qul fa/toobiAAashri suwarin mithlihi muftarayatin
wadAAoomani istataAAtum min dooni Allahi in kuntum sadiqeen
Swahili
Au wanasema: Ameizua? Sema: Basi leteni Sura kumi zilizo zuliwa mfano wa hii, na
waiteni muwawezao badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli.
|
Ayah 11:14 الأية
فَإِلَّمْ يَسْتَجِيبُوا لَكُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّمَا أُنزِلَ بِعِلْمِ اللهِ
وَأَن لَّا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَهَلْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ
Fa-illam yastajeeboo lakum faAAlamooannama onzila biAAilmi Allahi waan la
ilahailla huwa fahal antum muslimoon
Swahili
Na wasipo kuitikieni, basi jueni ya kwamba (hii Qur'ani) imeteremshwa kwa ujuzi
wa Mwenyezi Mungu, na kwamba hapana mungu ila Yeye. Basi je! Nyinyi ni Waislamu?
|
Ayah 11:15 الأية
مَن كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ
أَعْمَالَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لَا يُبْخَسُونَ
Man kana yureedu alhayataaddunya wazeenataha nuwaffi ilayhim aAAmalahumfeeha
wahum feeha la yubkhasoon
Swahili
Wanao taka maisha ya dunia na pumbao lake tutawalipa humo vitendo vyao kaamili.
Na wao humo hawatopunjwa.
|
Ayah 11:16 الأية
أُولَٰئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ إِلَّا النَّارُ ۖ وَحَبِطَ مَا
صَنَعُوا فِيهَا وَبَاطِلٌ مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Ola-ika allatheena laysa lahumfee al-akhirati illa annaru wahabitama sanaAAoo
feeha wabatilun makanoo yaAAmaloon
Swahili
Hao ndio ambao hawatakuwa na kitu Akhera ila Moto, na yataharibika waliyo
yafanya, na yatapotea bure waliyo kuwa wakiyatenda.
|
Ayah 11:17 الأية
أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّهِ وَيَتْلُوهُ شَاهِدٌ مِّنْهُ وَمِن
قَبْلِهِ كِتَابُ مُوسَىٰ إِمَامًا وَرَحْمَةً ۚ أُولَٰئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۚ
وَمَن يَكْفُرْ بِهِ مِنَ الْأَحْزَابِ فَالنَّارُ مَوْعِدُهُ ۚ فَلَا تَكُ فِي
مِرْيَةٍ مِّنْهُ ۚ إِنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ
لَا يُؤْمِنُونَ
Afaman kana AAala bayyinatinmin rabbihi wayatloohu shahidun minhu wamin qablihi
kitabumoosa imaman warahmatan ola-ikayu/minoona bihi waman yakfur bihi mina
al-ahzabi fannarumawAAiduhu fala taku fee miryatin minhu innahu alhaqqumin
rabbika walakinna akthara annasi layu/minoon
Swahili
Basi je, mtu aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola wake Mlezi, inayo fuatwa na
shahidi anaye toka kwake, na kabla yake kilikuwa Kitabu cha Musa kilicho kuwa
mwongozi na rehema - hao wanamuamini, na anaye mkataa katika makundi, basi Moto
ndio pahala pa miadi yao. Basi usiwe na shaka juu ya hayo. Hii ni Haki itokayo
kwa Mola wako Mlezi; lakini watu wengi hawaamini.
|
Ayah 11:18 الأية
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللهِ كَذِبًا ۚ أُولَٰئِكَ يُعْرَضُونَ
عَلَىٰ رَبِّهِمْ وَيَقُولُ الْأَشْهَادُ هَٰؤُلَاءِ الَّذِينَ كَذَبُوا عَلَىٰ
رَبِّهِمْ ۚ أَلَا لَعْنَةُ اللهِ عَلَى الظَّالِمِينَ
Waman athlamu mimmani iftaraAAala Allahi kathiban ola-ika yuAAradoonaAAala
rabbihim wayaqoolu al-ashhadu haola-iallatheena kathaboo AAala rabbihim
alalaAAnatu Allahi AAala aththalimeen
Swahili
Na nani aliye dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo?
Hao watahudhurishwa mbele ya Mola wao Mlezi, na mashahidi watasema: Hawa ndio
walio mtungia uwongo Mola wao Mlezi. Laana ya Mwenyezi Mungu iwapate walio
dhulumu,
|
Ayah 11:19 الأية
الَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا وَهُم
بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ
Allatheena yasuddoona AAansabeeli Allahi wayabghoonaha AAiwajan wahum
bil-akhiratihum kafiroon
Swahili
Ambao wanazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu, na wanaitakia ipotoke, na wanaikataa
Akhera.
|
Ayah 11:20 الأية
أُولَٰئِكَ لَمْ يَكُونُوا مُعْجِزِينَ فِي الْأَرْضِ وَمَا كَانَ لَهُم مِّن دُونِ
اللهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ۘ يُضَاعَفُ لَهُمُ الْعَذَابُ ۚ مَا كَانُوا
يَسْتَطِيعُونَ السَّمْعَ وَمَا كَانُوا يُبْصِرُونَ
Ola-ika lam yakoonoo muAAjizeena feeal-ardi wama kana lahum min dooni Allahimin
awliyaa yudaAAafu lahumu alAAathabu makanoo yastateeAAoona assamAAa wama
kanooyubsiroon
Swahili
Hao hawawezi kushinda katika ardhi, wala hawana walinzi isipo kuwa Mwenyezi
Mungu. Watazidishiwa adhabu. Hawakuwa wakiweza kusikia wala hawakuwa wakiona.
|
Ayah 11:21 الأية
أُولَٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا
يَفْتَرُونَ
Ola-ika allatheena khasirooanfusahum wadalla AAanhum ma kanoo yaftaroon
Swahili
Hao ndio walio zikhasiri nafsi zao, na yakawapotea waliyo kuwa wakiyazua.
|
Ayah 11:22 الأية
لَا جَرَمَ أَنَّهُمْ فِي الْآخِرَةِ هُمُ الْأَخْسَرُونَ
La jarama annahum fee al-akhiratihumu al-akhsaroon
Swahili
Bila ya shaka hakika wao ndio wenye kukhasiri huko Akhera.
|
Ayah 11:23 الأية
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَأَخْبَتُوا إِلَىٰ رَبِّهِمْ
أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ
Inna allatheena amanoowaAAamiloo asalihati waakhbatoo ilarabbihim ola-ika
as-habu aljannati hum feehakhalidoon
Swahili
Hakika wale walio amini,na wakatenda mema, na wakanyenyekea kwa Mola wao Mlezi,
hao ndio watu wa Peponi, na humo watadumu.
|
Ayah 11:24 الأية
مَثَلُ الْفَرِيقَيْنِ كَالْأَعْمَىٰ وَالْأَصَمِّ وَالْبَصِيرِ وَالسَّمِيعِ ۚ
هَلْ يَسْتَوِيَانِ مَثَلًا ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Mathalu alfareeqayni kalaAAmawal-asammi walbaseeri wassameeAAihal yastawiyani
mathalan afala tathakkaroon
Swahili
Mfano wa makundi mawili ni kama kipofu kiziwi, na mwenye kuona na anasikia. Je,
wawili hawa wanakuwa sawa kwa kufananishwa? Basi, je, hamfikiri?
|
Ayah 11:25 الأية
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ إِنِّي لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ
Walaqad arsalna noohan ilaqawmihi innee lakum natheerun mubeen
Swahili
Na Sisi tulimtuma Nuhu kwa watu wake, akawaambia: Hakika mimi ni mwonyaji kwenu
ninaye bainisha,
|
Ayah 11:26 الأية
أَن لَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللهَ ۖ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ
أَلِيمٍ
An la taAAbudoo illa Allahainnee akhafu AAalaykum AAathaba yawmin aleem
Swahili
Ya kwamba msimuabudu isipo kuwa Mwenyezi Mungu tu. Hakika mimi ninakukhofieni
adhabu ya Siku Chungu.
|
Ayah 11:27 الأية
فَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ مَا نَرَاكَ إِلَّا بَشَرًا
مِّثْلَنَا وَمَا نَرَاكَ اتَّبَعَكَ إِلَّا الَّذِينَ هُمْ أَرَاذِلُنَا بَادِيَ
الرَّأْيِ وَمَا نَرَىٰ لَكُمْ عَلَيْنَا مِن فَضْلٍ بَلْ نَظُنُّكُمْ كَاذِبِينَ
Faqala almalao allatheenakafaroo min qawmihi ma naraka illa basharanmithlana
wama naraka ittabaAAaka illaallatheena hum arathiluna badiya arra/yiwama nara
lakum AAalayna min fadlinbal nathunnukum kathibeen
Swahili
Na wakasema wakuu walio kufuru katika kaumu yake: Hatukuoni wewe ila ni mtu tu
kama sisi, wala hatukuoni wamekufuata ila wale walio kuwa kwetu watu duni, wasio
kuwa na akili. Wala hatukuoneni kuwa mna ubora wowote kutushinda sisi. Bali tuna
hakika nyinyi ni waongo.
|
Ayah 11:28 الأية
قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَآتَانِي
رَحْمَةً مِّنْ عِندِهِ فَعُمِّيَتْ عَلَيْكُمْ أَنُلْزِمُكُمُوهَا وَأَنتُمْ لَهَا
كَارِهُونَ
Qala ya qawmi araaytum inkuntu AAala bayyinatin min rabbee waataneerahmatan min
AAindihi faAAummiyat AAalaykum anulzimukumoohawaantum laha karihoon
Swahili
Akasema: Enyi watu wangu! Hebu fikirini! Ikiwa mimi ninayo hoja wazi iliyo toka
kwa Mola wangu Mlezi, na amenipa rehema kutoka kwake, nayo ikakufichikieni; je,
tukulazimisheni kuikubali hali nyinyi mnaichukia?
|
Ayah 11:29 الأية
وَيَا قَوْمِ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مَالًا ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى
اللهِ ۚ وَمَا أَنَا بِطَارِدِ الَّذِينَ آمَنُوا ۚ إِنَّهُم مُّلَاقُو رَبِّهِمْ
وَلَٰكِنِّي أَرَاكُمْ قَوْمًا تَجْهَلُونَ
Waya qawmi la as-alukumAAalayhi malan in ajriya illa AAala Allahiwama ana
bitaridi allatheena amanooinnahum mulaqoo rabbihim walakinnee arakumqawman
tajhaloon
Swahili
Na enyi watu wangu! Mimi sikuombeni mali kwa ajili ya haya. Mimi sina ujira ila
kwa Mwenyezi Mungu; na mimi sitawafukuza walio amini. Hakika wao watakutana na
Mola wao Mlezi, lakini mimi nakuoneni mnafanya ujinga.
|
Ayah 11:30 الأية
وَيَا قَوْمِ مَن يَنصُرُنِي مِنَ اللهِ إِن طَرَدتُّهُمْ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Waya qawmi man yansurunee minaAllahi in taradtuhum afala tathakkaroon
Swahili
Na enyi watu wangu! Ni nani atakaye nisaidia kwa Mwenyezi Mungu nikiwafukuza
hawa? Basi je, hamfikiri?
|
Ayah 11:31 الأية
وَلَا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا
أَقُولُ إِنِّي مَلَكٌ وَلَا أَقُولُ لِلَّذِينَ تَزْدَرِي أَعْيُنُكُمْ لَن
يُؤْتِيَهُمُ اللهُ خَيْرًا ۖ اللهُ أَعْلَمُ بِمَا فِي أَنفُسِهِمْ ۖ إِنِّي
إِذًا لَّمِنَ الظَّالِمِينَ
Wala aqoolu lakum AAindee khaza-inuAllahi wala aAAlamu alghayba wala aqooluinnee
malakun wala aqoolu lillatheena tazdareeaAAyunukum lan yu/tiyahumu Allahu
khayran AllahuaAAlamu bima fee anfusihim innee ithan lamina aththalimeen
Swahili
Wala sikwambiini kuwa nina khazina za Mwenyezi Mungu; wala kuwa mimi najua mambo
ya ghaibu; wala sisemi: Mimi ni Malaika. Wala siwasemi wale ambao yanawadharau
macho yenu kuwa Mwenyezi Mungu hatawapa kheri - Mwenyezi Mungu anajua yaliomo
katika nafsi zao - hapo bila ya shaka ninge kuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.
|
Ayah 11:32 الأية
قَالُوا يَا نُوحُ قَدْ جَادَلْتَنَا فَأَكْثَرْتَ جِدَالَنَا فَأْتِنَا بِمَا
تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ
Qaloo ya noohu qad jadaltanafaaktharta jidalana fa/tina bimataAAiduna in kunta
mina assadiqeen
Swahili
Wakasema: Ewe Nuhu! Umejadiliana, na umekithirisha kutujadili. Basi tuletee hayo
unayo tuahidi, ukiwa miongoni mwa wasemao kweli.
|
Ayah 11:33 الأية
قَالَ إِنَّمَا يَأْتِيكُم بِهِ اللهُ إِن شَاءَ وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ
Qala innama ya/teekum bihi Allahuin shaa wama antum bimuAAjizeen
Swahili
Akasema: Mwenyezi Mungu atakuleteeni akipenda. Wala nyinyi si wenye kumshinda.
|
Ayah 11:34 الأية
وَلَا يَنفَعُكُمْ نُصْحِي إِنْ أَرَدتُّ أَنْ أَنصَحَ لَكُمْ إِن كَانَ اللهُ
يُرِيدُ أَن يُغْوِيَكُمْ ۚ هُوَ رَبُّكُمْ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ
Wala yanfaAAukum nushee inaradtu an ansaha lakum in kana Allahuyureedu an
yughwiyakum huwa rabbukum wa-ilayhi turjaAAoon
Swahili
Wala nasaha yangu haikufaini kitu nikitaka kukunasihini, ikiwa Mwenyezi Mungu
anataka kukuachieni mpotee. Yeye ndiye Mola wenu Mlezi; na kwake mtarejeshwa.
|
Ayah 11:35 الأية
أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ إِنِ افْتَرَيْتُهُ فَعَلَيَّ إِجْرَامِي
وَأَنَا بَرِيءٌ مِّمَّا تُجْرِمُونَ
Am yaqooloona iftarahu qul iniiftaraytuhu faAAalayya ijramee waana baree-on
mimmatujrimoon
Swahili
Au ndio wanasema: Ameizua? Sema: Ikiwa nimeizua, basi kosa hilo ni juu yangu, na
mimi sikhusiki na makosa myatendayo.
|
Ayah 11:36 الأية
وَأُوحِيَ إِلَىٰ نُوحٍ أَنَّهُ لَن يُؤْمِنَ مِن قَوْمِكَ إِلَّا مَن قَدْ آمَنَ
فَلَا تَبْتَئِسْ بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ
Waoohiya ila noohinannahu lan yu/mina min qawmika illa man qad amanafala
tabta-is bima kanoo yafAAaloon
Swahili
Na akafunuliwa Nuhu akaambiwa: Hataamini yeyote katika watu wako ila wale walio
kwisha amini. Basi usisikitike kwa waliyo kuwa wakiyatenda.
|
Ayah 11:37 الأية
وَاصْنَعِ الْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا وَوَحْيِنَا وَلَا تُخَاطِبْنِي فِي الَّذِينَ
ظَلَمُوا ۚ إِنَّهُم مُّغْرَقُونَ
WasnaAAi alfulka bi-aAAyuninawawahyina wala tukhatibnee fee allatheenathalamoo
innahum mughraqoon
Swahili
Na unda jahazi mbele ya macho yetu na kwa mujibu wa ufunuo wetu. Wala
usinisemeze kuwatetea walio dhulumu. Kwani hao bila ya shaka watazamishwa.
|
Ayah 11:38 الأية
وَيَصْنَعُ الْفُلْكَ وَكُلَّمَا مَرَّ عَلَيْهِ مَلَأٌ مِّن قَوْمِهِ سَخِرُوا
مِنْهُ ۚ قَالَ إِن تَسْخَرُوا مِنَّا فَإِنَّا نَسْخَرُ مِنكُمْ كَمَا تَسْخَرُونَ
WayasnaAAu alfulka wakullamamarra AAalayhi malaon min qawmihi sakhiroo minhu
qala intaskharoo minna fa-inna naskharu minkum kamataskharoon
Swahili
Na akawa anaunda jahazi, na kila wakipita wakuu wa kaumu yake wakimkejeli. Yeye
akasema: Ikiwa nyinyi mnatukejeli na sisi tunakukejelini kama mnavyo tukejeli.
|
Ayah 11:39 الأية
فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَيَحِلُّ عَلَيْهِ عَذَابٌ
مُّقِيمٌ
Fasawfa taAAlamoona man ya/teehi AAathabunyukhzeehi wayahillu AAalayhi AAathabun
muqeem
Swahili
Nanyi mtakuja jua ni nani itakaye mfikia adhabu ya kumhizi, na itakaye mteremkia
adhabu ya kudumu.
|
Ayah 11:40 الأية
حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَمْرُنَا وَفَارَ التَّنُّورُ قُلْنَا احْمِلْ فِيهَا مِن
كُلٍّ زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ وَأَهْلَكَ إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيْهِ الْقَوْلُ
وَمَنْ آمَنَ ۚ وَمَا آمَنَ مَعَهُ إِلَّا قَلِيلٌ
Hatta itha jaaamruna wafara attannooru qulna ihmilfeeha min kullin zawjayni
ithnayni waahlaka illaman sabaqa AAalayhi alqawlu waman amana wama amanamaAAahu
illa qaleel
Swahili
Hata ilipo kuja amri yetu, na tanuri ikafoka maji, tulisema: Pakia humo wawili
wawili, dume na jike, kutoka kila aina, na ahali zako, isipo kuwa wale ambao
imekwisha wapitia hukumu; na watu walio amini. Na hawakuamini pamoja naye ila
wachache tu.
|
Ayah 11:41 الأية
وَقَالَ ارْكَبُوا فِيهَا بِسْمِ اللهِ مَجْرَاهَا وَمُرْسَاهَا ۚ إِنَّ رَبِّي
لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ
Waqala irkaboo feeha bismi Allahimajraha wamursaha inna rabbeelaghafoorun raheem
Swahili
Na akasema: Pandeni humo kwa Bismillahi, Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, kwenda
kwake na kusimama kwake. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kusamehe Mwenye
kurehemu.
|
Ayah 11:42 الأية
وَهِيَ تَجْرِي بِهِمْ فِي مَوْجٍ كَالْجِبَالِ وَنَادَىٰ نُوحٌ ابْنَهُ وَكَانَ
فِي مَعْزِلٍ يَا بُنَيَّ ارْكَب مَّعَنَا وَلَا تَكُن مَّعَ الْكَافِرِينَ
Wahiya tajree bihim fee mawjin kaljibaliwanada noohunu ibnahu wakana
feemaAAzilin ya bunayya irkab maAAana walatakun maAAa alkafireen
Swahili
Ikawa inakwenda nao katika mawimbi kama milima. Na Nuhu akamwita mwanawe naye
alikuwa mbali: Ewe mwanangu! Panda pamoja nasi, wala usiwe pamoja na makafiri.
|
Ayah 11:43 الأية
قَالَ سَآوِي إِلَىٰ جَبَلٍ يَعْصِمُنِي مِنَ الْمَاءِ ۚ قَالَ لَا عَاصِمَ
الْيَوْمَ مِنْ أَمْرِ اللهِ إِلَّا مَن رَّحِمَ ۚ وَحَالَ بَيْنَهُمَا الْمَوْجُ
فَكَانَ مِنَ الْمُغْرَقِينَ
Qala saawee ila jabalinyaAAsimunee mina alma-i qala la AAasimaalyawma min amri
Allahi illa man rahima wahalabaynahuma almawju fakana mina almughraqeen
Swahili
Akasema: Nitakimbilia mlimani unilinde na maji. (Nuhu) akasema: Leo hapana wa
kulindwa na amri ya Mwenyezi Mungu ila aliye mrehemu mwenyewe. Na wimbi
likawatenganisha, akawa katika walio zama.
|
Ayah 11:44 الأية
وَقِيلَ يَا أَرْضُ ابْلَعِي مَاءَكِ وَيَا سَمَاءُ أَقْلِعِي وَغِيضَ الْمَاءُ
وَقُضِيَ الْأَمْرُ وَاسْتَوَتْ عَلَى الْجُودِيِّ ۖ وَقِيلَ بُعْدًا لِّلْقَوْمِ
الظَّالِمِينَ
Waqeela ya ardu iblaAAee maakiwaya samao aqliAAee wagheeda almaowaqudiya al-amru
wastawat AAala aljoodiyyiwaqeela buAAdan lilqawmi aththalimeen
Swahili
Na ikasemwa: Ewe ardhi! Meza maji yako. Na Ewe mbingu! Jizuie. Basi maji
yakadidimia chini, na amri ikapitishwa, na (jahazi) likasimama juu ya (mlima) wa
Al Juudiy. Na ikasemwa: Wapotelee mbali watu walio dhulumu!
|
Ayah 11:45 الأية
وَنَادَىٰ نُوحٌ رَّبَّهُ فَقَالَ رَبِّ إِنَّ ابْنِي مِنْ أَهْلِي وَإِنَّ
وَعْدَكَ الْحَقُّ وَأَنتَ أَحْكَمُ الْحَاكِمِينَ
Wanada noohun rabbahufaqala rabbi inna ibnee min ahlee wa-inna waAAdaka
alhaqquwaanta ahkamu alhakimeen
Swahili
Na Nuhu alimwomba Mola wake Mlezi: Ee Mola Mlezi wangu! Hakika mwanangu ni
katika ahali zangu, na hakika ahadi yako ni haki. Na Wewe ni Mwenye haki kuliko
mahakimu wote.
|
Ayah 11:46 الأية
قَالَ يَا نُوحُ إِنَّهُ لَيْسَ مِنْ أَهْلِكَ ۖ إِنَّهُ عَمَلٌ غَيْرُ صَالِحٍ ۖ
فَلَا تَسْأَلْنِ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۖ إِنِّي أَعِظُكَ أَن تَكُونَ مِنَ
الْجَاهِلِينَ
Qala ya noohu innahulaysa min ahlika innahu AAamalun ghayru salihin falatas-alni
ma laysa laka bihi AAilmun innee aAAithukaan takoona mina aljahileen
Swahili
Akasema: Ewe Nuhu! Huyu si katika ahali zako. Mwendo wake si mwema. Basi
usiniombe jambo usio na ujuzi nalo. Mimi nakuwaidhi usije ukawa miongoni mwa
wajinga.
|
Ayah 11:47 الأية
قَالَ رَبِّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ أَنْ أَسْأَلَكَ مَا لَيْسَ لِي بِهِ عِلْمٌ ۖ
وَإِلَّا تَغْفِرْ لِي وَتَرْحَمْنِي أَكُن مِّنَ الْخَاسِرِينَ
Qala rabbi innee aAAoothu bikaan as-alaka ma laysa lee bihi AAilmun
wa-illataghfir lee watarhamnee akun mina alkhasireen
Swahili
Nuhu akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Mimi najikinga kwako nisikuombe nisio na
ujuzi nalo. Na kama hunisamehe na ukanirehemu, nitakuwa katika walio khasiri.
|
Ayah 11:48 الأية
قِيلَ يَا نُوحُ اهْبِطْ بِسَلَامٍ مِّنَّا وَبَرَكَاتٍ عَلَيْكَ وَعَلَىٰ أُمَمٍ
مِّمَّن مَّعَكَ ۚ وَأُمَمٌ سَنُمَتِّعُهُمْ ثُمَّ يَمَسُّهُم مِّنَّا عَذَابٌ
أَلِيمٌ
Qeela ya noohu ihbitbisalamin minna wabarakatin AAalayka waAAalaomamin mimman
maAAaka waomamun sanumattiAAuhum thumma yamassuhumminna AAathabun aleem
Swahili
Ikasemwa: Ewe Nuhu! Shuka kwa salama itokayo kwetu, na baraka nyingi juu yako na
juu ya watu walio pamoja nawe. Na zitakuwapo kaumu tutakazo zistarehesha, na
kisha zitashikwa na adhabu chungu itokayo kwetu.
|
Ayah 11:49 الأية
تِلْكَ مِنْ أَنبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهَا إِلَيْكَ ۖ مَا كُنتَ تَعْلَمُهَا أَنتَ
وَلَا قَوْمُكَ مِن قَبْلِ هَٰذَا ۖ فَاصْبِرْ ۖ إِنَّ الْعَاقِبَةَ لِلْمُتَّقِينَ
Tilka min anba-i alghaybi nooheehailayka ma kunta taAAlamuha anta wala
qawmukamin qabli hatha fasbir inna alAAaqibatalilmuttaqeen
Swahili
Hizi ni katika khabari za ghaibu tunazo kufunulia. Hukuwa ukizijua wewe, wala
watu wako, kabla ya hii. Basi subiri! Hakika Mwisho ni wa wachamngu.
|
Ayah 11:50 الأية
وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللهَ مَا لَكُم
مِّنْ إِلَٰهٍ غَيْرُهُ ۖ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا مُفْتَرُونَ
Wa-ila AAadin akhahumhoodan qala ya qawmi oAAbudoo Allaha malakum min ilahin
ghayruhu in antum illa muftaroon
Swahili
Na kwa kina A'adi tulimtuma ndugu yao Hud. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni
Mwenyezi Mungu! Nyinyi hamna mungu isipo kuwa Yeye. Nyinyi si chochote ila ni
wazushi tu.
|
Ayah 11:51 الأية
يَا قَوْمِ لَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى
الَّذِي فَطَرَنِي ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ
Ya qawmi la as-alukum AAalayhiajran in ajriya illa AAala allathee fataraneeafala
taAAqiloon
Swahili
Enyi watu wangu! Sikuombeni ujira kwa ajili ya haya. Haukuwa ujira wangu ila kwa
Yule aliye niumba. Basi hamtumii akili?
|
Ayah 11:52 الأية
وَيَا قَوْمِ اسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ يُرْسِلِ السَّمَاءَ
عَلَيْكُم مِّدْرَارًا وَيَزِدْكُمْ قُوَّةً إِلَىٰ قُوَّتِكُمْ وَلَا تَتَوَلَّوْا
مُجْرِمِينَ
Waya qawmi istaghfiroo rabbakumthumma tooboo ilayhi yursili assamaa
AAalaykummidraran wayazidkum quwwatan ila quwwatikum walatatawallaw mujrimeen
Swahili
Na enyi watu wangu! Muombeni msamaha Mola wenu Mlezi, kisha mtubie kwake.
Atakuleteeni mbingu zenye kunyesha mvua ya kumiminika, na atakuzidishieni nguvu
juu ya nguvu zenu. Wala msigeuke mkawa wakosefu.
|
Ayah 11:53 الأية
قَالُوا يَا هُودُ مَا جِئْتَنَا بِبَيِّنَةٍ وَمَا نَحْنُ بِتَارِكِي آلِهَتِنَا
عَن قَوْلِكَ وَمَا نَحْنُ لَكَ بِمُؤْمِنِينَ
Qaloo ya hoodu maji/tana bibayyinatin wama nahnu bitarikeealihatina AAan qawlika
wama nahnulaka bimu/mineen
Swahili
Wakasema: Ewe Hud! Hujatuletea dalili wazi. Wala sisi hatuiachi miungu yetu kwa
kufuata kauli yako. Na wala sisi hatukuamini wewe.
|
Ayah 11:54 الأية
إِن نَّقُولُ إِلَّا اعْتَرَاكَ بَعْضُ آلِهَتِنَا بِسُوءٍ ۗ قَالَ إِنِّي أُشْهِدُ
اللهَ وَاشْهَدُوا أَنِّي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ
In naqoolu illa iAAtaraka baAAdualihatina bisoo-in qala innee oshhidu
Allahawashhadoo annee baree-on mimma tushrikoon
Swahili
Sisi tunasema: Baadhi katika miungu yetu imekusibu kwa baa. Akasema: Hakika mimi
namshuhudisha Mwenyezi Mungu, na nyinyi shuhudieni, ya kwamba mimi najitenga
mbali na hao mnao wafanya washirika,
|
Ayah 11:55 الأية
مِن دُونِهِ ۖ فَكِيدُونِي جَمِيعًا ثُمَّ لَا تُنظِرُونِ
Min doonihi fakeedoonee jameeAAan thumma latunthiroon
Swahili
Mkamwacha Yeye. Basi nyote nyinyi nipangieni vitimbi, na kisha msinipe muhula!
|
Ayah 11:56 الأية
إِنِّي تَوَكَّلْتُ عَلَى اللهِ رَبِّي وَرَبِّكُم ۚ مَّا مِن دَابَّةٍ إِلَّا
هُوَ آخِذٌ بِنَاصِيَتِهَا ۚ إِنَّ رَبِّي عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ
Innee tawakkaltu AAala Allahirabbee warabbikum ma min dabbatin illa huwa
akhithunbinasiyatiha inna rabbee AAala siratinmustaqeem
Swahili
Hakika mimi nimemtegemea Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wangu na Mola Mlezi wenu.
Hapana kiumbe yeyote ila Yeye anamwendesha atakavyo. Hakika Mola wangu Mlezi
yuko juu ya Njia Iliyo Nyooka.
|
Ayah 11:57 الأية
فَإِن تَوَلَّوْا فَقَدْ أَبْلَغْتُكُم مَّا أُرْسِلْتُ بِهِ إِلَيْكُمْ ۚ
وَيَسْتَخْلِفُ رَبِّي قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّونَهُ شَيْئًا ۚ إِنَّ
رَبِّي عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ حَفِيظٌ
Fa-in tawallaw faqad ablaghtukum maorsiltu bihi ilaykum wayastakhlifu rabbee
qawman ghayrakum walatadurroonahu shay-an inna rabbee AAala kullishay-in hafeeth
Swahili
Na ikiwa watarudi nyuma, basi mimi nimekwisha kufikishieni niliyo tumwa kwenu.
Na Mola wangu Mlezi atawaleta watu wengine badala yenu, wala nyinyi hamumdhuru
kitu Yeye. Hakika Mola wangu Mlezi ni Mwenye kuhifadhi kila kitu.
|
Ayah 11:58 الأية
وَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا هُودًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ بِرَحْمَةٍ
مِّنَّا وَنَجَّيْنَاهُم مِّنْ عَذَابٍ غَلِيظٍ
Walamma jaa amrunanajjayna hoodan wallatheena amanoomaAAahu birahmatin minna
wanajjaynahum minAAathabin ghaleeth
Swahili
Ilipo fika amri yetu, tulimwokoa Hud na walio amini pamoja naye, kwa rehema
itokayo kwetu. Na tukawaokoa na adhabu ngumu.
|
Ayah 11:59 الأية
وَتِلْكَ عَادٌ ۖ جَحَدُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ وَعَصَوْا رُسُلَهُ وَاتَّبَعُوا
أَمْرَ كُلِّ جَبَّارٍ عَنِيدٍ
Watilka AAadun jahadoo bi-ayatirabbihim waAAasaw rusulahu wattabaAAoo amra
kullijabbarin AAaneed
Swahili
Na hao ndio kina A'adi. Walizikanusha Ishara za Mola wao Mlezi, na wakawaasi
Mitume wake, na wakafuata amri ya kila jabari mwenye inda.
|
Ayah 11:60 الأية
وَأُتْبِعُوا فِي هَٰذِهِ الدُّنْيَا لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ أَلَا إِنَّ
عَادًا كَفَرُوا رَبَّهُمْ ۗ أَلَا بُعْدًا لِّعَادٍ قَوْمِ هُودٍ
WaotbiAAoo fee hathihi addunyalaAAnatan wayawma alqiyamati ala inna
AAadankafaroo rabbahum ala buAAdan liAAadin qawmi hood
Swahili
Na wakafuatishiwa laana katika dunia hii na Siku ya Kiyama. Basi tambueni
mtanabahi! Hakika kina A'adi walimkufuru Mola wao Mlezi. Na tambueni mtanabahi
kuwa hakika waliangamizwa kina A'adi, kaumu ya Hud.
|
Ayah 11:61 الأية
وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللهَ مَا
لَكُم مِّنْ إِلَٰهٍ غَيْرُهُ ۖ هُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ الْأَرْضِ وَاسْتَعْمَرَكُمْ
فِيهَا فَاسْتَغْفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّي قَرِيبٌ مُّجِيبٌ
Wa-ila thamooda akhahum salihanqala ya qawmi oAAbudoo Allaha malakum min ilahin
ghayruhu huwa anshaakum mina al-ardiwastaAAmarakum feeha fastaghfiroohu
thummatooboo ilayhi inna rabbee qareebun mujeeb
Swahili
Na kina Thamud tuliwapelekea ndugu yao Saleh. Akasema: Enyi watu wangu!
Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Yeye ndiye aliye kuumbeni
katika ardhi, na akakuwekeni humo. Basi mwombeni msamaha, kisha mtubu kwake.
Hakika Mola wangu Mlezi yupo karibu, anaitikia maombi.
|
Ayah 11:62 الأية
قَالُوا يَا صَالِحُ قَدْ كُنتَ فِينَا مَرْجُوًّا قَبْلَ هَٰذَا ۖ أَتَنْهَانَا
أَن نَّعْبُدَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا وَإِنَّنَا لَفِي شَكٍّ مِّمَّا تَدْعُونَا
إِلَيْهِ مُرِيبٍ
Qaloo ya salihuqad kunta feena marjuwwan qabla hatha atanhanaan naAAbuda ma
yaAAbudu abaonawa-innana lafee shakkin mimma tadAAoonailayhi mureeb
Swahili
Wakasema: Ewe Saleh! Hakika kabla ya haya ulikuwa unatarajiwa kheri kwetu. Je,
unatukataza tusiwaabudu waliyo kuwa wakiwaabudu baba zetu? Na hakika sisi tuna
shaka na wasiwasi kwa hayo unayo tuitia.
|
Ayah 11:63 الأية
قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَآتَانِي
مِنْهُ رَحْمَةً فَمَن يَنصُرُنِي مِنَ اللهِ إِنْ عَصَيْتُهُ ۖ فَمَا
تَزِيدُونَنِي غَيْرَ تَخْسِيرٍ
Qala ya qawmi araaytum inkuntu AAala bayyinatin min rabbee waataneeminhu
rahmatan faman yansurunee mina Allahiin AAasaytuhu fama tazeedoonanee ghayra
takhseer
Swahili
Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje ikiwa ninazo dalili zilizo wazi kutokana na
Mola wangu Mlezi, naye akawa kanipa rehema kutoka kwake - je, ni nani atakaye
ninusuru kwa Mwenyezi Mungu nikimuasi? Basi nyinyi hamtanizidishia ila khasara
tu.
|
Ayah 11:64 الأية
وَيَا قَوْمِ هَٰذِهِ نَاقَةُ اللهِ لَكُمْ آيَةً فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ
اللهِ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ قَرِيبٌ
Waya qawmi hathihi naqatuAllahi lakum ayatan fatharooha ta/kulfee ardi Allahi
wala tamassoohabisoo-in faya/khuthakum AAathabun qareeb
Swahili
Enyi watu wangu! Huyu ngamia wa Mwenyezi Mungu ni Ishara kwenu. Basi mwacheni
ale katika ardhi ya Mwenyezi Mungu; wala msimguse kwa ubaya, isije
ikakuangamizeni adhabu iliyo karibu.
|
Ayah 11:65 الأية
فَعَقَرُوهَا فَقَالَ تَمَتَّعُوا فِي دَارِكُمْ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ ۖ ذَٰلِكَ
وَعْدٌ غَيْرُ مَكْذُوبٍ
FaAAaqarooha faqalatamattaAAoo fee darikum thalathata ayyamin thalikawaAAdun
ghayru makthoob
Swahili
Wakamchinja. Basi (Saleh) akasema: Stareheni katika mji wenu muda wa siku tatu.
Hiyo ni ahadi isiyo kuwa ya uwongo.
|
Ayah 11:66 الأية
فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا صَالِحًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ
بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَمِنْ خِزْيِ يَوْمِئِذٍ ۗ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ الْقَوِيُّ
الْعَزِيزُ
Falamma jaa amrunanajjayna salihan wallatheena amanoomaAAahu birahmatin minna
wamin khizyi yawmi-ithininna rabbaka huwa alqawiyyu alAAazeez
Swahili
Basi ilipo kuja amri yetu tulimwokoa Saleh na wale walio amini pamoja naye kwa
rehema yetu kutokana na hizaya ya siku ile. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye
nguvu Mwenye kushinda.
|
Ayah 11:67 الأية
وَأَخَذَ الَّذِينَ ظَلَمُوا الصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دِيَارِهِمْ جَاثِمِينَ
Waakhatha allatheena thalamooassayhatu faasbahoo fee diyarihimjathimeen
Swahili
Na ukelele uliwaangamiza wale walio dhulumu, wakapambazukiwa nao ni maiti
majumbani mwao.
|
Ayah 11:68 الأية
كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۗ أَلَا إِنَّ ثَمُودَ كَفَرُوا رَبَّهُمْ ۗ أَلَا
بُعْدًا لِّثَمُودَ
Kaan lam yaghnaw feeha alainna thamooda kafaroo rabbahum ala buAAdan lithamood
Swahili
Kama kwamba hawakuwako huko. Hebu zingatieni! Hakika kina Thamud walimkufuru
Mola wao Mlezi. Hebu zingatieni! Thamud wamepotelea mbali!
|
Ayah 11:69 الأية
وَلَقَدْ جَاءَتْ رُسُلُنَا إِبْرَاهِيمَ بِالْبُشْرَىٰ قَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ
سَلَامٌ ۖ فَمَا لَبِثَ أَن جَاءَ بِعِجْلٍ حَنِيذٍ
Walaqad jaat rusuluna ibraheemabilbushra qaloo salaman qalasalamun fama labitha
an jaa biAAijlin haneeth
Swahili
Na wajumbe wetu walimjia Ibrahim kwa bishara njema, wakasema: Salama! Naye
akasema: Salama! Hakukaa ila mara akaleta ndama wa kuchoma.
|
Ayah 11:70 الأية
فَلَمَّا رَأَىٰ أَيْدِيَهُمْ لَا تَصِلُ إِلَيْهِ نَكِرَهُمْ وَأَوْجَسَ مِنْهُمْ
خِيفَةً ۚ قَالُوا لَا تَخَفْ إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمِ لُوطٍ
Falamma raa aydiyahum latasilu ilayhi nakirahum waawjasa minhum kheefatan
qaloola takhaf inna orsilna ila qawmi loot
Swahili
Basi alipoona mikono yao haimfikilii aliwatilia shaka, na akawaogopa. Wakasema:
Usiogope! Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya Lut'.
|
Ayah 11:71 الأية
وَامْرَأَتُهُ قَائِمَةٌ فَضَحِكَتْ فَبَشَّرْنَاهَا بِإِسْحَاقَ وَمِن وَرَاءِ
إِسْحَاقَ يَعْقُوبَ
Wamraatuhu qa-imatun fadahikatfabashsharnaha bi-ishaqa wamin wara-iishaqa
yaAAqoob
Swahili
Na mkewe alikuwa kasimama wima, akacheka. Basi tukambashiria (kuzaliwa) Is-haq,
na baada ya Is-haq Yaaqub.
|
Ayah 11:72 الأية
قَالَتْ يَا وَيْلَتَىٰ أَأَلِدُ وَأَنَا عَجُوزٌ وَهَٰذَا بَعْلِي شَيْخًا ۖ إِنَّ
هَٰذَا لَشَيْءٌ عَجِيبٌ
Qalat ya waylata aaliduwaana AAajoozun wahatha baAAlee shaykhan inna
hathalashay-on AAajeeb
Swahili
Akasema: Je, hivyo mimi nizae, na hali yangu ni kikongwe na huyu mume wangu ni
kizee? Hakika haya ni mambo ya ajabu!
|
Ayah 11:73 الأية
قَالُوا أَتَعْجَبِينَ مِنْ أَمْرِ اللهِ ۖ رَحْمَتُ اللهِ وَبَرَكَاتُهُ
عَلَيْكُمْ أَهْلَ الْبَيْتِ ۚ إِنَّهُ حَمِيدٌ مَّجِيدٌ
Qaloo ataAAjabeena min amri Allahirahmatu Allahi wabarakatuhu AAalaykum
ahlaalbayti innahu hameedun majeed
Swahili
Wakasema: Je, unastaajabia amri ya Mwenyezi Mungu? Rehema ya Mwenyezi Mungu na
baraka zake ziko juu yenu, enyi watu wa nyumba hii! Hakika Yeye ndiye Msifiwa wa
kutukuzwa.
|
Ayah 11:74 الأية
فَلَمَّا ذَهَبَ عَنْ إِبْرَاهِيمَ الرَّوْعُ وَجَاءَتْهُ الْبُشْرَىٰ يُجَادِلُنَا
فِي قَوْمِ لُوطٍ
Falamma thahaba AAan ibraheemaarrawAAu wajaat-hu albushra yujadilunafee qawmi
loot
Swahili
Basi khofu ilipo mwondoka Ibrahim, na ikawa ile bishara imemfikia, alianza
kujadiliana nasi juu ya kaumu ya Lut'.
|
Ayah 11:75 الأية
إِنَّ إِبْرَاهِيمَ لَحَلِيمٌ أَوَّاهٌ مُّنِيبٌ
Inna ibraheema lahaleemun awwahunmuneeb
Swahili
Hakika Ibrahim alikuwa mpole, ana huruma, na mwepesi wa kurejea kwa Mwenyezi
Mungu.
|
Ayah 11:76 الأية
يَا إِبْرَاهِيمُ أَعْرِضْ عَنْ هَٰذَا ۖ إِنَّهُ قَدْ جَاءَ أَمْرُ رَبِّكَ ۖ
وَإِنَّهُمْ آتِيهِمْ عَذَابٌ غَيْرُ مَرْدُودٍ
Ya ibraheemu aAAridAAan hatha innahu qad jaa amru rabbika wa-innahum
ateehimAAathabun ghayru mardood
Swahili
(Akaambiwa): Ewe Ibrahim! Wachilia mbali haya! Kwa hakika amri ya Mola wako
Mlezi imekwisha kuja, na hakika hao itawafikia adhabu isiyo rudi nyuma.
|
Ayah 11:77 الأية
وَلَمَّا جَاءَتْ رُسُلُنَا لُوطًا سِيءَ بِهِمْ وَضَاقَ بِهِمْ ذَرْعًا وَقَالَ
هَٰذَا يَوْمٌ عَصِيبٌ
Walamma jaat rusulunalootan see-a bihim wadaqa bihim tharAAan waqalahatha yawmun
AAaseeb
Swahili
Na wajumbe wetu walipo kuja kwa Lut' aliwahuzunukia na akawaonea dhiki. Akasema:
Hii leo ni siku ngumu!
|
Ayah 11:78 الأية
وَجَاءَهُ قَوْمُهُ يُهْرَعُونَ إِلَيْهِ وَمِن قَبْلُ كَانُوا يَعْمَلُونَ
السَّيِّئَاتِ ۚ قَالَ يَا قَوْمِ هَٰؤُلَاءِ بَنَاتِي هُنَّ أَطْهَرُ لَكُمْ ۖ
فَاتَّقُوا اللهَ وَلَا تُخْزُونِ فِي ضَيْفِي ۖ أَلَيْسَ مِنكُمْ رَجُلٌ
رَّشِيدٌ
Wajaahu qawmuhu yuhraAAoona ilayhiwamin qablu kanoo yaAAmaloona assayyi-ati
qalaya qawmi haola-i banatee hunna atharulakum fattaqoo Allaha wala tukhzooni
fee dayfeealaysa minkum rajulun rasheed
Swahili
Wakamjia kaumu yake mbio mbio. Na kabla ya haya walikuwa wakitenda maovu. Yeye
akasema: Enyi watu wangu! Hawa binti zangu, ndio wametakasika zaidi kwenu. Basi
mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi mbele ya wageni wangu. Hivyo, hamna hata
mtu mmoja miongoni mwenu aliye ongoka?
|
Ayah 11:79 الأية
قَالُوا لَقَدْ عَلِمْتَ مَا لَنَا فِي بَنَاتِكَ مِنْ حَقٍّ وَإِنَّكَ لَتَعْلَمُ
مَا نُرِيدُ
Qaloo laqad AAalimta ma lanafee banatika min haqqin wa-innaka lataAAlamu
manureed
Swahili
Wakasema: Bila shaka umekwisha jua hatuna haki juu ya binti zako, na unayajua
tunayo yataka.
|
Ayah 11:80 الأية
قَالَ لَوْ أَنَّ لِي بِكُمْ قُوَّةً أَوْ آوِي إِلَىٰ رُكْنٍ شَدِيدٍ
Qala law anna lee bikum quwwatan aw aweeila ruknin shadeed
Swahili
Akasema: Laiti ningeli kuwa na nguvu kwenu, au nategemea kwenye nguzo yenye
nguvu!
|
Ayah 11:81 الأية
قَالُوا يَا لُوطُ إِنَّا رُسُلُ رَبِّكَ لَن يَصِلُوا إِلَيْكَ ۖ فَأَسْرِ
بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِّنَ اللَّيْلِ وَلَا يَلْتَفِتْ مِنكُمْ أَحَدٌ إِلَّا
امْرَأَتَكَ ۖ إِنَّهُ مُصِيبُهَا مَا أَصَابَهُمْ ۚ إِنَّ مَوْعِدَهُمُ الصُّبْحُ
ۚ أَلَيْسَ الصُّبْحُ بِقَرِيبٍ
Qaloo ya lootu innarusulu rabbika lan yasiloo ilayka faasri bi-ahlika
biqitAAinmina allayli wala yaltafit minkum ahadun illaimraataka innahu museebuha
ma asabahuminna mawAAidahumu assubhu alaysa assubhubiqareeb
Swahili
(Wajumbe) wakasema: Ewe Lut'! Sisi ni wajumbe wa Mola wako Mlezi. Hawa
hawatakufikia. Na wewe ondoka pamoja na ahali zako usiku ungalipo. Wala yeyote
miongoni mwenu asitazame nyuma, isipo kuwa mkeo, kwani yeye utamfika msiba
utakao wafika hao. Hakika miadi yao ni asubuhi. Je, asubuhi si karibu?
|
Ayah 11:82 الأية
فَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا جَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهَا
حِجَارَةً مِّن سِجِّيلٍ مَّنضُودٍ
Falamma jaa amrunajaAAalna AAaliyaha safilahawaamtarna AAalayha hijaratanmin
sijjeelin mandood
Swahili
Basi ilipo fika amri yetu tuliigeuza nchi juu chini, na tukawateremshia mvua ya
changarawe za udongo mgumu ulio kamatana wa Motoni,
|
Ayah 11:83 الأية
مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ ۖ وَمَا هِيَ مِنَ الظَّالِمِينَ بِبَعِيدٍ
Musawwamatan AAinda rabbika wama hiyamina aththalimeena bibaAAeed
Swahili
Zilizo tiwa alama kwa Mola wako Mlezi. Na haya hayako mbali na wenye kudhulumu
wengineo.
|
Ayah 11:84 الأية
وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللهَ مَا
لَكُم مِّنْ إِلَٰهٍ غَيْرُهُ ۖ وَلَا تَنقُصُوا الْمِكْيَالَ وَالْمِيزَانَ ۚ
إِنِّي أَرَاكُم بِخَيْرٍ وَإِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ مُّحِيطٍ
Wa-ila madyana akhahumshuAAayban qala ya qawmi oAAbudoo Allaha malakum min
ilahin ghayruhu wala tanqusooalmikyala walmeezana innee arakumbikhayrin wa-innee
akhafu AAalaykum AAathaba yawminmuheet
Swahili
Na kwa watu wa Madyana tuliwatumia ndugu yao Shua'ib. Akasema: Enyi watu wangu!
Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye, wala msipunguze vipimo na
mizani. Mimi nakuoneni mmo katika hali njema, nami nakukhofieni adhabu ya Siku
kubwa hiyo itakayo kuzungukeni.
|
Ayah 11:85 الأية
وَيَا قَوْمِ أَوْفُوا الْمِكْيَالَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ ۖ وَلَا تَبْخَسُوا
النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ
Waya qawmi awfoo almikyala walmeezanabilqisti wala tabkhasoo annasaashyaahum
wala taAAthaw fee al-ardimufsideen
Swahili
Na enyi watu wangu! Timizeni vipimo na mizani kwa uadilifu wala msiwakhini watu
vitu vyao; wala msieneze uovu katika nchi mkafanya uharibifu.
|
Ayah 11:86 الأية
بَقِيَّتُ اللهِ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ۚ وَمَا أَنَا عَلَيْكُم
بِحَفِيظٍ
Baqiyyatu Allahi khayrun lakum inkuntum mu/mineena wama ana AAalaykum bihafeeth
Swahili
Alivyo kubakishieni Mwenyezi Mungu ndiyo bora kwa ajili yenu, ikiwa nyinyi ni
Waumini. Wala mimi siye mlinzi wenu.
|
Ayah 11:87 الأية
قَالُوا يَا شُعَيْبُ أَصَلَاتُكَ تَأْمُرُكَ أَن نَّتْرُكَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا
أَوْ أَن نَّفْعَلَ فِي أَمْوَالِنَا مَا نَشَاءُ ۖ إِنَّكَ لَأَنتَ الْحَلِيمُ
الرَّشِيدُ
Qaloo ya shuAAaybu asalatukata/muruka an natruka ma yaAAbudu abaonaaw an
nafAAala fee amwalina ma nashaoinnaka laanta alhaleemu arrasheed
Swahili
Wakasema: Ewe Shua'ibu! Ni sala zako ndizo zinazo kuamrisha tuyaache waliyo kuwa
wakiyaabudu baba zetu, au tuache kufanya tupendavyo katika mali zetu? Ama hakika
wewe ni mstahamilivu kweli na mwongofu!
|
Ayah 11:88 الأية
قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي
وَرَزَقَنِي مِنْهُ رِزْقًا حَسَنًا ۚ وَمَا أُرِيدُ أَنْ أُخَالِفَكُمْ إِلَىٰ مَا
أَنْهَاكُمْ عَنْهُ ۚ إِنْ أُرِيدُ إِلَّا الْإِصْلَاحَ مَا اسْتَطَعْتُ ۚ وَمَا
تَوْفِيقِي إِلَّا بِاللهِ ۚ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ
Qala ya qawmi araaytum inkuntu AAala bayyinatin min rabbee warazaqanee minhu
rizqanhasanan wama oreedu an okhalifakum ilama anhakum AAanhu in oreedu illa
al-islahama istataAAtu wama tawfeeqee illa billahiAAalayhi tawakkaltu wa-ilayhi
oneeb
Swahili
Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje ikiwa ninayo dalili wazi inayo tokana na Mola
wangu Mlezi, na ikawa Yeye ameniruzuku riziki njema kutoka kwake? Wala mimi
sipendi kukukhalifuni nikafanya yale ninayo kukatazeni. Sitaki ila kutengeneza
kiasi ninavyo weza. Na sipati kuwezeshwa haya ila na Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye
ninategemea, na kwake Yeye naelekea.
|
Ayah 11:89 الأية
وَيَا قَوْمِ لَا يَجْرِمَنَّكُمْ شِقَاقِي أَن يُصِيبَكُم مِّثْلُ مَا أَصَابَ
قَوْمَ نُوحٍ أَوْ قَوْمَ هُودٍ أَوْ قَوْمَ صَالِحٍ ۚ وَمَا قَوْمُ لُوطٍ مِّنكُم
بِبَعِيدٍ
Waya qawmi la yajrimannakumshiqaqee an yuseebakum mithlu ma asabaqawma noohin aw
qawma hoodin aw qawma salihinwama qawmu lootin minkum bibaAAeed
Swahili
Na enyi watu wangu! Kukhalifiana nami kusikupelekeeni hata mkasibiwa kama
walivyo sibiwa watu wa Nuhu, au watu wa Hud, au watu wa Saleh. Na watu wa Lut'
si mbali nanyi.
|
Ayah 11:90 الأية
وَاسْتَغْفِرُوا رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوا إِلَيْهِ ۚ إِنَّ رَبِّي رَحِيمٌ وَدُودٌ
Wastaghfiroo rabbakum thumma toobooilayhi inna rabbee raheemun wadood
Swahili
Na ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi, tena tubuni kwake. Hakika Mola wangu
Mlezi ni Mwenye kurehemu na Mwenye upendo.
|
Ayah 11:91 الأية
قَالُوا يَا شُعَيْبُ مَا نَفْقَهُ كَثِيرًا مِّمَّا تَقُولُ وَإِنَّا لَنَرَاكَ
فِينَا ضَعِيفًا ۖ وَلَوْلَا رَهْطُكَ لَرَجَمْنَاكَ ۖ وَمَا أَنتَ عَلَيْنَا
بِعَزِيزٍ
Qaloo ya shuAAaybu manafqahu katheeran mimma taqoolu wa-inna lanarakafeena
daAAeefan walawla rahtukalarajamnaka wama anta AAalayna biAAazeez
Swahili
Wakasema: Ewe Shua'ibu! Mengi katika hayo unayo yasema hatuyafahamu. Na sisi
tunakuona huna nguvu kwetu. Lau kuwa si jamaa zako tunge kupiga mawe, wala wewe
si mtukufu kwetu.
|
Ayah 11:92 الأية
قَالَ يَا قَوْمِ أَرَهْطِي أَعَزُّ عَلَيْكُم مِّنَ اللهِ وَاتَّخَذْتُمُوهُ
وَرَاءَكُمْ ظِهْرِيًّا ۖ إِنَّ رَبِّي بِمَا تَعْمَلُونَ مُحِيطٌ
Qala ya qawmi arahteeaAAazzu AAalaykum mina Allahi wattakhathtumoohuwaraakum
thihriyyan inna rabbee bimataAAmaloona muheet
Swahili
Akasema: Enyi watu wangu! Kwani jamaa zangu ni watukufu zaidi kwenu kuliko
Mwenyezi Mungu? Na Yeye mmemueka nyuma ya migongo yenu! Hakika Mola wangu Mlezi
ni Mwenye kuyazunguka yote mnayo yatenda.
|
Ayah 11:93 الأية
وَيَا قَوْمِ اعْمَلُوا عَلَىٰ مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ ۖ سَوْفَ تَعْلَمُونَ
مَن يَأْتِيهِ عَذَابٌ يُخْزِيهِ وَمَنْ هُوَ كَاذِبٌ ۖ وَارْتَقِبُوا إِنِّي
مَعَكُمْ رَقِيبٌ
Waya qawmi iAAmaloo AAala makanatikuminnee AAamilun sawfa taAAlamoona man
ya/teehi AAathabunyukhzeehi waman huwa kathibun wartaqiboo innemaAAakum raqeeb
Swahili
Na enyi watu wangu! Fanyeni mwezayo, na mimi pia ninafanya. Karibuni mtajua ni
nani itakaye mfikia adhabu ya kumhizi, na nani aliye mwongo. Na ngojeni, mimi
pia ninangoja pamoja nanyi.
|
Ayah 11:94 الأية
وَلَمَّا جَاءَ أَمْرُنَا نَجَّيْنَا شُعَيْبًا وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَهُ
بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَأَخَذَتِ الَّذِينَ ظَلَمُوا الصَّيْحَةُ فَأَصْبَحُوا فِي
دِيَارِهِمْ جَاثِمِينَ
Walamma jaa amrunanajjayna shuAAayban wallatheena amanoomaAAahu birahmatin minna
waakhathati allatheenathalamoo assayhatu faasbahoofee diyarihim jathimeen
Swahili
Na ilipo fika amri yetu, tulimwokoa Shua'ibu na wale walio amini pamoja naye kwa
rehema yetu. Na ukelele uliwanyakua walio dhulumu, na wakapambaukiwa majumbani
mwao wamekufa kifudifudi!
|
Ayah 11:95 الأية
كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۗ أَلَا بُعْدًا لِّمَدْيَنَ كَمَا بَعِدَتْ ثَمُودُ
Kaan lam yaghnaw feeha alabuAAdan limadyana kama baAAidat thamood
Swahili
Kama kwamba hawakuwamo humo. Zingatia walivyo angamia watu wa Madyana, kama
walivyo angamia watu wa Thamud!
|
Ayah 11:96 الأية
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍ مُّبِينٍ
Walaqad arsalna moosa bi-ayatinawasultanin mubeen
Swahili
Na hakika tulimtuma Musa pamoja na Ishara zetu na uthibitisho ulio wazi
|
Ayah 11:97 الأية
إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَاتَّبَعُوا أَمْرَ فِرْعَوْنَ ۖ وَمَا أَمْرُ
فِرْعَوْنَ بِرَشِيدٍ
Ila firAAawna wamala-ihi fattabaAAooamra firAAawna wama amru firAAawna birasheed
Swahili
Kwa Firauni na waheshimiwa wake. Lakini wao walifuata amri ya Firauni, na amri
ya Firauni haikuwa yenye uwongofu.
|
Ayah 11:98 الأية
يَقْدُمُ قَوْمَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَأَوْرَدَهُمُ النَّارَ ۖ وَبِئْسَ
الْوِرْدُ الْمَوْرُودُ
Yaqdumu qawmahu yawma alqiyamatifaawradahumu annara wabi/sa alwirdu almawrood
Swahili
Siku ya Kiyama atawatangulia watu wake na atawaingiza Motoni. Na muingio muovu
ulioje huo!
|
Ayah 11:99 الأية
وَأُتْبِعُوا فِي هَٰذِهِ لَعْنَةً وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ بِئْسَ الرِّفْدُ
الْمَرْفُودُ
WaotbiAAoo fee hathihi laAAnatanwayawma alqiyamati bi/sa arrifdu almarfood
Swahili
Nao wamefuatishiwa laana hapa duniani na Siku ya Kiyama. Ni mabaya yalioje
watakayo pewa!
|
Ayah 11:100 الأية
ذَٰلِكَ مِنْ أَنبَاءِ الْقُرَىٰ نَقُصُّهُ عَلَيْكَ ۖ مِنْهَا قَائِمٌ وَحَصِيدٌ
Thalika min anba-i alquranaqussuhu AAalayka minha qa-imun wahaseed
Swahili
Hizi ni katika khabari za miji, tunakusimulia. Mingine ipo bado na mingine
imefyekwa.
|
Ayah 11:101 الأية
وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَٰكِن ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ۖ فَمَا أَغْنَتْ عَنْهُمْ
آلِهَتُهُمُ الَّتِي يَدْعُونَ مِن دُونِ اللهِ مِن شَيْءٍ لَّمَّا جَاءَ أَمْرُ
رَبِّكَ ۖ وَمَا زَادُوهُمْ غَيْرَ تَتْبِيبٍ
Wama thalamnahumwalakin thalamoo anfusahum famaaghnat AAanhum alihatuhumu
allatee yadAAoona min dooni Allahimin shay-in lamma jaa amru rabbika wama
zadoohumghayra tatbeeb
Swahili
Na Sisi hatukuwadhulumu, lakini wao wenyewe wamejidhulumu. Na miungu yao waliyo
kuwa wakiiomba badala ya Mwenyezi Mungu haikuwafaa kitu ilipo kuja amri ya Mola
wako Mlezi. Na hiyo miungu haikuwazidishia ila maangamizo tu.
|
Ayah 11:102 الأية
وَكَذَٰلِكَ أَخْذُ رَبِّكَ إِذَا أَخَذَ الْقُرَىٰ وَهِيَ ظَالِمَةٌ ۚ إِنَّ
أَخْذَهُ أَلِيمٌ شَدِيدٌ
Wakathalika akhthu rabbika ithaakhatha alqura wahiya thalimatuninna akhthahu
aleemun shadeed
Swahili
Na ndio kama hivyo ndivyo inavyo kuwa Mola wako Mlezi anapo ikamata miji inapo
kuwa imedhulumu. Hakika mkamato wake ni mchungu na mkali.
|
Ayah 11:103 الأية
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّمَنْ خَافَ عَذَابَ الْآخِرَةِ ۚ ذَٰلِكَ يَوْمٌ
مَّجْمُوعٌ لَّهُ النَّاسُ وَذَٰلِكَ يَوْمٌ مَّشْهُودٌ
Inna fee thalika laayatanliman khafa AAathaba al-akhirati thalikayawmun
majmooAAun lahu annasu wathalikayawmun mashhoodun
Swahili
Hakika katika haya ipo ishara kwa yule anaye ogopa adhabu ya Akhera. Hiyo ndiyo
Siku itakayo kusanyiwa watu, na hiyo ndiyo Siku itakayo shuhudiwa.
|
Ayah 11:104 الأية
وَمَا نُؤَخِّرُهُ إِلَّا لِأَجَلٍ مَّعْدُودٍ
Wama nu-akhkhiruhu illali-ajalin maAAdood
Swahili
Na Sisi hatuiakhirishi ila kwa muda unao hisabiwa.
|
Ayah 11:105 الأية
يَوْمَ يَأْتِ لَا تَكَلَّمُ نَفْسٌ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ فَمِنْهُمْ شَقِيٌّ
وَسَعِيدٌ
Yawma ya/ti la takallamu nafsun illabi-ithnihi faminhum shaqiyyun wasaAAeed
Swahili
Siku hiyo itakapo fika, hatosema hata mtu mmoja ila kwa idhini yake Mwenyezi
Mungu. Kati yao watakuwamo waliomo mashakani na wenye furaha.
|
Ayah 11:106 الأية
فَأَمَّا الَّذِينَ شَقُوا فَفِي النَّارِ لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَشَهِيقٌ
Faamma allatheena shaqoofafee annari lahum feeha zafeerun washaheeq
Swahili
Ama wale wa mashakani hao watakuwamo Motoni wakiyayayatika na kukoroma.
|
Ayah 11:107 الأية
خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ
ۚ إِنَّ رَبَّكَ فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ
Khalideena feeha ma damatiassamawatu wal-ardu illama shaa rabbuka inna rabbaka
faAAAAalun limayureed
Swahili
Watadumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipo kuwa apendavyo Mola wako
Mlezi. Hakika Mola wako Mlezi hutenda apendavyo.
|
Ayah 11:108 الأية
وَأَمَّا الَّذِينَ سُعِدُوا فَفِي الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ
السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ ۖ عَطَاءً غَيْرَ مَجْذُوذٍ
Waamma allatheena suAAidoofafee aljannati khalideena feeha ma damatiassamawatu
wal-ardu illama shaa rabbuka AAataan ghayra majthooth
Swahili
Na ama wale walio bahatika, wao watakuwamo Peponi wakidumu humo muda wa kudumu
mbingu na ardhi, isipo kuwa apendavyo Mola wako Mlezi. Hicho ni kipawa kisio na
ukomo.
|
Ayah 11:109 الأية
فَلَا تَكُ فِي مِرْيَةٍ مِّمَّا يَعْبُدُ هَٰؤُلَاءِ ۚ مَا يَعْبُدُونَ إِلَّا
كَمَا يَعْبُدُ آبَاؤُهُم مِّن قَبْلُ ۚ وَإِنَّا لَمُوَفُّوهُمْ نَصِيبَهُمْ
غَيْرَ مَنقُوصٍ
Fala taku fee miryatin mimmayaAAbudu haola-i ma yaAAbudoona illakama yaAAbudu
abaohum min qablu wa-innalamuwaffoohum naseebahum ghayra manqoos
Swahili
Basi usiwe na shaka juu ya wanayo yaabudu hao. Hawaabudu ila kama walivyo abudu
baba zao zamani. Na hakika Sisi tutawatimilizia fungu lao bila ya kupunguzwa.
|
Ayah 11:110 الأية
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَاخْتُلِفَ فِيهِ ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ
سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ
مُرِيبٍ
Walaqad atayna moosaalkitaba fakhtulifa feehi walawla kalimatunsabaqat min
rabbika laqudiya baynahum wa-innahum lafeeshakkin minhu mureeb
Swahili
Na kwa yakini tulimpa Musa Kitabu; zikazuka khitilafu ndani yake. Na lau kuwa si
neno lilio kwisha tangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi, bila ya shaka ingeli
hukumiwa baina yao. Na hakika wao wamo katika shaka juu yake inayo wahangaisha.
|
Ayah 11:111 الأية
وَإِنَّ كُلًّا لَّمَّا لَيُوَفِّيَنَّهُمْ رَبُّكَ أَعْمَالَهُمْ ۚ إِنَّهُ بِمَا
يَعْمَلُونَ خَبِيرٌ
Wa-inna kullan lammalayuwaffiyannahum rabbuka aAAmalahum innahu bimayaAAmaloona
khabeer
Swahili
Na hakika Mola wako Mlezi atawatimilizia malipo ya vitendo vyao. Hakika Yeye
anayo khabari ya wayatendayo.
|
Ayah 11:112 الأية
فَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ وَمَن تَابَ مَعَكَ وَلَا تَطْغَوْا ۚ إِنَّهُ بِمَا
تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ
Fastaqim kama omirta waman tabamaAAaka wala tatghaw innahu bima
taAAmaloonabaseer
Swahili
Basi, simama sawa sawa kama ulivyo amrishwa, wewe na wale wanao elekea kwa
Mwenyezi Mungu pamoja nawe; wala msikiuke mipaka. Hakika Yeye anayaona yote
myatendayo.
|
Ayah 11:113 الأية
وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم
مِّن دُونِ اللهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ
Wala tarkanoo ila allatheenathalamoo fatamassakumu annaru wamalakum min dooni
Allahi min awliyaa thumma latunsaroon
Swahili
Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna
walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.
|
Ayah 11:114 الأية
وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ
الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ
Waaqimi assalata tarafayiannahari wazulafan mina allayli inna
alhasanatiyuthhibna assayyi-ati thalika thikraliththakireen
Swahili
Na shika Sala katika ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zilizo karibu na
mchana. Hakika mema huondoa maovu. Huu ni ukumbusho kwa wanao kumbuka.
|
Ayah 11:115 الأية
وَاصْبِرْ فَإِنَّ اللهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ
Wasbir fa-inna Allahala yudeeAAu ajra almuhsineen
Swahili
Na subiri, kwani Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wanao fanya wema.
|
Ayah 11:116 الأية
فَلَوْلَا كَانَ مِنَ الْقُرُونِ مِن قَبْلِكُمْ أُولُو بَقِيَّةٍ يَنْهَوْنَ عَنِ
الْفَسَادِ فِي الْأَرْضِ إِلَّا قَلِيلًا مِّمَّنْ أَنجَيْنَا مِنْهُمْ ۗ
وَاتَّبَعَ الَّذِينَ ظَلَمُوا مَا أُتْرِفُوا فِيهِ وَكَانُوا مُجْرِمِينَ
Falawla kana mina alquroonimin qablikum oloo baqiyyatin yanhawna AAani alfasadi
feeal-ardi illa qaleelan mimman anjayna minhumwattabaAAa allatheena thalamoo
maotrifoo feehi wakanoo mujrimeen
Swahili
Basi mbona hawakuwamo katika watu wa kabla yenu wenye vyeo na wasaa wanao kataza
uharibifu katika nchi, isipo kuwa wachache tu, ambao ndio tulio waokoa? Na walio
dhulumu walifuata starehe zao, na wakawa ni wakosefu.
|
Ayah 11:117 الأية
وَمَا كَانَ رَبُّكَ لِيُهْلِكَ الْقُرَىٰ بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا مُصْلِحُونَ
Wama kana rabbuka liyuhlikaalqura bithulmin waahluha muslihoon
Swahili
Wala hakuwa Mola wako Mlezi wa kuihiliki miji kwa dhulma tu na hali watu wake ni
watenda mema.
|
|