1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
أَتَىٰ أَمْرُ اللهِ فَلَا تَسْتَعْجِلُوهُ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا
يُشْرِكُونَ
Ata amru Allahi falatastaAAjiloohu subhanahu wataAAala AAammayushrikoon
Swahili
Amri ya Mwenyezi Mungu itafika tu. Basi msiihimize. Ametakasika na Ametukuka na
wanayo mshirikisha nayo.
|
Ayah 16:2 الأية
يُنَزِّلُ الْمَلَائِكَةَ بِالرُّوحِ مِنْ أَمْرِهِ عَلَىٰ مَن يَشَاءُ مِنْ
عِبَادِهِ أَنْ أَنذِرُوا أَنَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا أَنَا فَاتَّقُونِ
Yunazzilu almala-ikata birroohimin amrihi AAala man yashao min AAibadihi
ananthiroo annahu la ilaha illa anafattaqoon
Swahili
Huwateremsha Malaika na Roho kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake ili
nyinyi muonye kwamba hapana mungu ila Mimi, basi nicheni Mimi.
|
Ayah 16:3 الأية
خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۚ تَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ
Khalaqa assamawati wal-ardabilhaqqi taAAala AAammayushrikoon
Swahili
Ameziumba mbingu na ardhi kwa Haki. Ametukuka na wanayo shirikisha.
|
Ayah 16:4 الأية
خَلَقَ الْإِنسَانَ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ
Khalaqa al-insana min nutfatinfa-itha huwa khaseemun mubeen
Swahili
Amemuumba mtu kwa tone la manii. Naye mara amekuwa mshindani dhaahiri.
|
Ayah 16:5 الأية
وَالْأَنْعَامَ خَلَقَهَا ۗ لَكُمْ فِيهَا دِفْءٌ وَمَنَافِعُ وَمِنْهَا
تَأْكُلُونَ
Wal-anAAama khalaqahalakum feeha dif-on wamanafiAAu waminhata-kuloon
Swahili
Na nyama hoa amekuumbieni. Katika hao mna vifaa vya kutia joto, na manufaa
mengineyo, na baadhi yao mnawala.
|
Ayah 16:6 الأية
وَلَكُمْ فِيهَا جَمَالٌ حِينَ تُرِيحُونَ وَحِينَ تَسْرَحُونَ
Walakum feeha jamalun heenatureehoona waheena tasrahoon
Swahili
Na wanakupeni furaha pale mnapo warudisha jioni na mnapo wapeleka malishoni
asubuhi.
|
Ayah 16:7 الأية
وَتَحْمِلُ أَثْقَالَكُمْ إِلَىٰ بَلَدٍ لَّمْ تَكُونُوا بَالِغِيهِ إِلَّا بِشِقِّ
الْأَنفُسِ ۚ إِنَّ رَبَّكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ
Watahmilu athqalakum ilabaladin lam takoonoo baligheehi illa bishiqqial-anfusi
inna rabbakum laraoofun raheem
Swahili
Na hubeba mizigo yenu kupeleka kwenye miji msiyo weza kuifikia ila kwa mashaka
ya nafsi. Hakika Mola wenu Mlezi ni Mpole na Mwenye kurehemu.
|
Ayah 16:8 الأية
وَالْخَيْلَ وَالْبِغَالَ وَالْحَمِيرَ لِتَرْكَبُوهَا وَزِينَةً ۚ وَيَخْلُقُ مَا
لَا تَعْلَمُونَ
Walkhayla walbighalawalhameera litarkabooha wazeenatanwayakhluqu ma la
taAAlamoon
Swahili
Na farasi, na nyumbu, na punda ili muwapande, na kuwa ni pambo. Na ataumba
msivyo vijua.
|
Ayah 16:9 الأية
وَعَلَى اللهِ قَصْدُ السَّبِيلِ وَمِنْهَا جَائِرٌ ۚ وَلَوْ شَاءَ لَهَدَاكُمْ
أَجْمَعِينَ
WaAAala Allahi qasdu assabeeliwaminha ja-irun walaw shaa lahadakumajmaAAeen
Swahili
Na ni juu ya Mwenyezi Mungu kuelekeza Njia. Na zipo njia za upotovu. Na angeli
penda angeli kuongoeni nyote.
|
Ayah 16:10 الأية
هُوَ الَّذِي أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً ۖ لَّكُم مِّنْهُ شَرَابٌ وَمِنْهُ
شَجَرٌ فِيهِ تُسِيمُونَ
Huwa allathee anzala mina assama-imaan lakum minhu sharabun waminhu shajarun
feehituseemoon
Swahili
Yeye ndiye anaye kuteremshieni maji kutoka mbinguni. Katika hayo nyinyi mnapata
ya kunywa, na miti ya kulishia.
|
Ayah 16:11 الأية
يُنبِتُ لَكُم بِهِ الزَّرْعَ وَالزَّيْتُونَ وَالنَّخِيلَ وَالْأَعْنَابَ وَمِن
كُلِّ الثَّمَرَاتِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ
Yunbitu lakum bihi azzarAAa wazzaytoonawannakheela wal-aAAnaba wamin kulli
aththamaratiinna fee thalika laayatan liqawmin yatafakkaroon
Swahili
Kwa hayo Yeye anaizalisha kwa ajili yenu mimea, na mizaituni, na mitende, na
mizabibu, na kila namna ya matunda. Hakika katika haya zipo ishara kwa watu
wanao fikiri.
|
Ayah 16:12 الأية
وَسَخَّرَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ وَالنُّجُومُ
مُسَخَّرَاتٌ بِأَمْرِهِ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ
Wasakhkhara lakumu allayla wannaharawashshamsa walqamara
wannujoomumusakhkharatun bi-amrihi inna fee thalika laayatinliqawmin yaAAqiloon
Swahili
Na amefanya ukutumikieni usiku na mchana, na jua na mwezi, na nyota
zikutumikieni kwa amri yake. Hakika katika hayo zipo ishara kwa watu wenye
akili.
|
Ayah 16:13 الأية
وَمَا ذَرَأَ لَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُخْتَلِفًا أَلْوَانُهُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ
لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَذَّكَّرُونَ
Wama tharaa lakum fee al-ardimukhtalifan alwanuhu inna fee thalika
laayatanliqawmin yaththakkaroon
Swahili
Na hivi alivyo vieneza katika ardhi vya rangi mbali mbali. Hakika katika hayo
ipo ishara kwa watu wanao waidhika.
|
Ayah 16:14 الأية
وَهُوَ الَّذِي سَخَّرَ الْبَحْرَ لِتَأْكُلُوا مِنْهُ لَحْمًا طَرِيًّا
وَتَسْتَخْرِجُوا مِنْهُ حِلْيَةً تَلْبَسُونَهَا وَتَرَى الْفُلْكَ مَوَاخِرَ
فِيهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ
Wahuwa allathee sakhkhara albahralita/kuloo minhu lahman tariyyan
watastakhrijoominhu hilyatan talbasoonaha watara alfulkamawakhira feehi
walitabtaghoo min fadlihiwalaAAallakum tashkuroon
Swahili
Yeye ndiye aliye ifanya bahari ikutumikieni, ili kutokana na humo mpate kula
nyama laini, na mtoe humo mapambo mnayo yavaa. Na unaona marikebu zikikata maji
humo, ili mtafute fadhila yake, na mpate kushukuru.
|
Ayah 16:15 الأية
وَأَلْقَىٰ فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِكُمْ وَأَنْهَارًا وَسُبُلًا
لَّعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ
Waalqa fee al-ardi rawasiyaan tameeda bikum waanharan wasubulan laAAallakum
tahtadoon
Swahili
Na kaweka katika ardhi milima ili ardhi isiyumbe yumbe nanyi. Na mito, na njia
ili mpate kuongoka.
|
Ayah 16:16 الأية
وَعَلَامَاتٍ ۚ وَبِالنَّجْمِ هُمْ يَهْتَدُونَ
WaAAalamatin wabinnajmihum yahtadoon
Swahili
Na alama nyengine. Na kwa nyota wao wanajiongoza.
|
Ayah 16:17 الأية
أَفَمَن يَخْلُقُ كَمَن لَّا يَخْلُقُ ۗ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Afaman yakhluqu kaman la yakhluquafala tathakkaroon
Swahili
Ati anaye umba ni kama asiye umba? Basi hebu, hamkumbuki?
|
Ayah 16:18 الأية
وَإِن تَعُدُّوا نِعْمَةَ اللهِ لَا تُحْصُوهَا ۗ إِنَّ اللهَ لَغَفُورٌ
رَّحِيمٌ
Wa-in taAAuddoo niAAmata Allahi latuhsooha inna Allaha laghafoorun raheem
Swahili
Na mkizihisabu neema za Mwenyezi Mungu, hamwezi kuzidhibiti. Hakika Mwenyezi
Mungu ni Mwenye maghfira, Mwenye kurehemu.
|
Ayah 16:19 الأية
وَاللهُ يَعْلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعْلِنُونَ
Wallahu yaAAlamu matusirroona wama tuAAlinoon
Swahili
Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayo yaficha na mnayo yatangaza.
|
Ayah 16:20 الأية
وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللهِ لَا يَخْلُقُونَ شَيْئًا وَهُمْ
يُخْلَقُونَ
Wallatheena yadAAoona mindooni Allahi la yakhluqoona shay-an wahumyukhlaqoon
Swahili
Na wale wanao waomba wasio kuwa Mwenyezi Mungu hawaumbi kitu, bali wao
wameumbwa.
|
Ayah 16:21 الأية
أَمْوَاتٌ غَيْرُ أَحْيَاءٍ ۖ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ
Amwatun ghayru ahya-inwama yashAAuroona ayyana yubAAathoon
Swahili
Ni wafu si wahai, na wala hawajui watafufuliwa lini.
|
Ayah 16:22 الأية
إِلَٰهُكُمْ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ ۚ فَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ
قُلُوبُهُم مُّنكِرَةٌ وَهُم مُّسْتَكْبِرُونَ
Ilahukum ilahun wahidunfallatheena la yu/minoona bil-akhiratiquloobuhum
munkiratun wahum mustakbiroon
Swahili
Mungu wenu ni Mungu Mmoja. Lakini wasio iamini Akhera nyoyo zao zinakataa, nao
wanajivuna.
|
Ayah 16:23 الأية
لَا جَرَمَ أَنَّ اللهَ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ۚ إِنَّهُ لَا
يُحِبُّ الْمُسْتَكْبِرِينَ
La jarama anna Allaha yaAAlamuma yusirroona wama yuAAlinoona innahu la
yuhibbualmustakbireen
Swahili
Hapana shaka kuwa hakika Mwenyezi Mungu anayajua wanayo yaficha na wanayo
yatangaza. Kwa hakika Yeye hawapendi wanao jivuna.
|
Ayah 16:24 الأية
وَإِذَا قِيلَ لَهُم مَّاذَا أَنزَلَ رَبُّكُمْ ۙ قَالُوا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ
Wa-itha qeela lahum mathaanzala rabbukum qaloo asateeru al-awwaleen
Swahili
Na wanapo ambiwa: Kateremsha nini Mola wenu Mlezi? Husema: Hadithi za kubuni za
watu wa kale!
|
Ayah 16:25 الأية
لِيَحْمِلُوا أَوْزَارَهُمْ كَامِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۙ وَمِنْ أَوْزَارِ
الَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ
Liyahmiloo awzarahum kamilatanyawma alqiyamati wamin awzari allatheena
yudilloonahumbighayri AAilmin ala saa ma yaziroon
Swahili
Ili wabebe mizigo yao kwa ukamilifu Siku ya Kiyama, na sehemu ya mizigo ya wale
wanao wapoteza bila ya kujua. Angalia, ni maovu mno hayo wanayo yabeba!
|
Ayah 16:26 الأية
قَدْ مَكَرَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَأَتَى اللهُ بُنْيَانَهُم مِّنَ
الْقَوَاعِدِ فَخَرَّ عَلَيْهِمُ السَّقْفُ مِن فَوْقِهِمْ وَأَتَاهُمُ الْعَذَابُ
مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ
Qad makara allatheena min qablihimfaata Allahu bunyanahum mina
alqawaAAidifakharra AAalayhimu assaqfu min fawqihim waatahumualAAathabu min
haythu la yashAAuroon
Swahili
Walipanga vitimbi walio kuwa kabla yao, Mwenyezi Mungu akayasukua majengo yao
kwenye misingi, dari zikawaporomokea juu yao, na adhabu ikawajia kutoka wasipo
kujua.
|
Ayah 16:27 الأية
ثُمَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يُخْزِيهِمْ وَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ
كُنتُمْ تُشَاقُّونَ فِيهِمْ ۚ قَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ إِنَّ الْخِزْيَ
الْيَوْمَ وَالسُّوءَ عَلَى الْكَافِرِينَ
Thumma yawma alqiyamati yukhzeehimwayaqoolu ayna shuraka-iya allatheena kuntum
tushaqqoonafeehim qala allatheena ootoo alAAilma inna alkhizyaalyawma wassoo-a
AAala alkafireen
Swahili
Kisha Siku ya Kiyama atawahizi na atasema: Wako wapi hao washirika wangu ambao
kwao mkiwakutisha (Manabii) mashaka? Watasema walio pewa ilimu: Hakika leo ndiyo
hizaya na adhabu itawashukia makafiri,
|
Ayah 16:28 الأية
الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ ۖ فَأَلْقَوُا
السَّلَمَ مَا كُنَّا نَعْمَلُ مِن سُوءٍ ۚ بَلَىٰ إِنَّ اللهَ عَلِيمٌ بِمَا
كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Allatheena tatawaffahumu almala-ikatuthalimee anfusihim faalqawoo assalamama
kunna naAAmalu min soo-in bala inna AllahaAAaleemun bima kuntum taAAmaloon
Swahili
Ambao Malaika waliwafisha nao wamejidhulumu nafsi zao! Basi watasalimu amri,
waseme: Hatukuwa tukifanya uovu wowote. (Wataambiwa): Kwani! Hakika Mwenyezi
Mungu anajua sana mliyo kuwa mkiyatenda.
|
Ayah 16:29 الأية
فَادْخُلُوا أَبْوَابَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۖ فَلَبِئْسَ مَثْوَى
الْمُتَكَبِّرِينَ
Fadkhuloo abwaba jahannama khalideenafeeha falabi/sa mathwa almutakabbireen
Swahili
Basi ingieni milango ya Jahannamu, humo mdumu. Ni maovu mno makaazi ya wafanyao
kiburi!
|
Ayah 16:30 الأية
وَقِيلَ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا مَاذَا أَنزَلَ رَبُّكُمْ ۚ قَالُوا خَيْرًا ۗ
لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا فِي هَٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةٌ ۚ وَلَدَارُ الْآخِرَةِ
خَيْرٌ ۚ وَلَنِعْمَ دَارُ الْمُتَّقِينَ
Waqeela lillatheena ittaqaw mathaanzala rabbukum qaloo khayran lillatheena
ahsanoofee hathihi addunya hasanatun waladarual-akhirati khayrun walaniAAma daru
almuttaqeen
Swahili
Na wataambiwa walio mcha Mungu: Mola wenu Mlezi kateremsha nini? Watasema:
Kheri. Walio fanya wema katika dunia hii watapata wema. Na nyumba ya Akhera ni
bora zaidi, na njema mno nyumba ya wachamngu.
|
Ayah 16:31 الأية
جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ لَهُمْ
فِيهَا مَا يَشَاءُونَ ۚ كَذَٰلِكَ يَجْزِي اللهُ الْمُتَّقِينَ
Jannatu AAadnin yadkhuloonahatajree min tahtiha al-anharu lahum feehama
yashaoona kathalika yajzee Allahualmuttaqeen
Swahili
Bustani za milele wataziingia; iwe inapita kati yake mito. Humo watapata
watakacho. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu awalipavyo wenye kumcha.
|
Ayah 16:32 الأية
الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ طَيِّبِينَ ۙ يَقُولُونَ سَلَامٌ
عَلَيْكُمُ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Allatheena tatawaffahumu almala-ikatutayyibeena yaqooloona salamun AAalaykumu
odkhulooaljannata bima kuntum taAAmaloon
Swahili
Wale ambao Malaika huwafisha katika hali njema, wanawaambia: Amani iwe juu yenu!
Ingieni Peponi kwa sababu ya yale mliyo kuwa mkiyatenda.
|
Ayah 16:33 الأية
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا أَن تَأْتِيَهُمُ الْمَلَائِكَةُ أَوْ يَأْتِيَ أَمْرُ
رَبِّكَ ۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ وَمَا ظَلَمَهُمُ اللهُ
وَلَٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ
Hal yanthuroona illa anta/tiyahumu almala-ikatu aw ya/tiya amru rabbika
kathalikafaAAala allatheena min qablihim wama thalamahumuAllahu walakin kanoo
anfusahum yathlimoon
Swahili
Wanangojea jengine hawa ila Malaika wawafikie, au iwafikie amri ya Mola wako
Mlezi? Kama hivyo walitenda walio kuwa kabla yao. Na Mwenyezi Mungu
hakuwadhulumu, lakini walijidhulumu wenyewe.
|
Ayah 16:34 الأية
فَأَصَابَهُمْ سَيِّئَاتُ مَا عَمِلُوا وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ
يَسْتَهْزِئُونَ
Faasabahum sayyi-atu maAAamiloo wahaqa bihim ma kanoo bihiyastahzi-oon
Swahili
Basi ukawafikia uovu wa waliyo yatenda, na waliyo kuwa wakiyakejeli
yakawazunguka.
|
Ayah 16:35 الأية
وَقَالَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا لَوْ شَاءَ اللهُ مَا عَبَدْنَا مِن دُونِهِ مِن
شَيْءٍ نَّحْنُ وَلَا آبَاؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن دُونِهِ مِن شَيْءٍ ۚ
كَذَٰلِكَ فَعَلَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ فَهَلْ عَلَى الرُّسُلِ إِلَّا
الْبَلَاغُ الْمُبِينُ
Waqala allatheena ashrakoo lawshaa Allahu ma AAabadna min doonihimin shay-in
nahnu wala abaonawala harramna min doonihi min shay-in kathalikafaAAala
allatheena min qablihim fahal AAala arrusuliilla albalaghu almubeen
Swahili
Na washirikina wanasema: Mwenyezi Mungu angeli taka tusingeli abudu chochote
badala yake, sisi wala baba zetu, wala tusingeli harimisha chochote bila ya
Yeye. Kama hivyo walifanya walio kuwa kabla yao. Basi lipo lolote juu ya Mitume
isipo kuwa kubalighisha kwa uwazi?
|
Ayah 16:36 الأية
وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللهَ
وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ فَمِنْهُم مَّنْ هَدَى اللهُ وَمِنْهُم مَّنْ
حَقَّتْ عَلَيْهِ الضَّلَالَةُ ۚ فَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ
عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ
Walaqad baAAathna fee kulli ommatinrasoolan ani oAAbudoo Allaha wajtaniboo
attaghootafaminhum man hada Allahu waminhum man haqqatAAalayhi addalalatu
faseeroo fee al-ardifanthuroo kayfa kana AAaqibatualmukaththibeen
Swahili
Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu,
na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo alio waongoa Mwenyezi Mungu. Na kati
yao wapo ambao ulio wathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie
ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha.
|
Ayah 16:37 الأية
إِن تَحْرِصْ عَلَىٰ هُدَاهُمْ فَإِنَّ اللهَ لَا يَهْدِي مَن يُضِلُّ ۖ وَمَا
لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ
In tahris AAala hudahumfa-inna Allaha la yahdee man yudillu wamalahum min
nasireen
Swahili
Hata ukiwa na pupa ya kutaka kuwaongoa, lakini Mwenyezi Mungu hamwongoi yule
anaye shikilia kupotea. Wala hawatapata wa kuwanusuru.
|
Ayah 16:38 الأية
وَأَقْسَمُوا بِاللهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ ۙ لَا يَبْعَثُ اللهُ مَن يَمُوتُ ۚ
بَلَىٰ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ
Waaqsamoo billahi jahda aymanihimla yabAAathu Allahu man yamootu bala
waAAdanAAalayhi haqqan walakinna akthara annasila yaAAlamoon
Swahili
Na wanaapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa viapo vyao kwamba Mwenyezi Mungu
hatomfufua aliye kufa. Kwani! Ni ahadi iliyo juu yake kikweli; lakini watu wengi
hawajui.
|
Ayah 16:39 الأية
لِيُبَيِّنَ لَهُمُ الَّذِي يَخْتَلِفُونَ فِيهِ وَلِيَعْلَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا
أَنَّهُمْ كَانُوا كَاذِبِينَ
Liyubayyina lahumu allatheeyakhtalifoona feehi waliyaAAlama allatheena
kafarooannahum kanoo kathibeen
Swahili
Ili kuwabainishia yale waliyo khitalifiana, na ili wajue walio kufuru kwamba wao
walikuwa ni waongo.
|
Ayah 16:40 الأية
إِنَّمَا قَوْلُنَا لِشَيْءٍ إِذَا أَرَدْنَاهُ أَن نَّقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ
Innama qawluna lishay-inithaaradnahu an naqoola lahu kun fayakoon
Swahili
Kauli yetu kwa kitu tunacho kitaka kiwe, ni kukiambia: Kuwa! Basi kinakuwa.
|
Ayah 16:41 الأية
وَالَّذِينَ هَاجَرُوا فِي اللهِ مِن بَعْدِ مَا ظُلِمُوا لَنُبَوِّئَنَّهُمْ فِي
الدُّنْيَا حَسَنَةً ۖ وَلَأَجْرُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ
Wallatheena hajaroofee Allahi min baAAdi ma thulimoolanubawwi-annahum fee
addunya hasanatanwalaajru al-akhirati akbaru law kanoo yaAAlamoon
Swahili
Na wale walio hama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu baada ya kudhulumiwa, bila ya
shaka tutawaweka duniani kwa wema; na ujira wa Akhera ni mkubwa zaidi; laiti
kuwa wanajua!
|
Ayah 16:42 الأية
الَّذِينَ صَبَرُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ
Allatheena sabaroo waAAalarabbihim yatawakkaloon
Swahili
Wale wanao subiri na wakamtegemea Mola wao Mlezi.
|
Ayah 16:43 الأية
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِي إِلَيْهِمْ ۚ فَاسْأَلُوا
أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ
Wama arsalna min qablika illarijalan noohee ilayhim fas-aloo ahla aththikriin
kuntum la taAAlamoon
Swahili
Nasi hatukuwatuma kabla yako ila watu wanaume tulio wapa Wahyi (Ufunuo). Basi
waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui
|
Ayah 16:44 الأية
بِالْبَيِّنَاتِ وَالزُّبُرِ ۗ وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ
لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ
Bilbayyinati wazzuburiwaanzalna ilayka aththikra litubayyina linnasima nuzzila
ilayhim walaAAallahum yatafakkaroon
Swahili
Kwa Ishara wazi na Vitabu. Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie
watu yaliyo teremshwa kwao, wapate kufikiri.
|
Ayah 16:45 الأية
أَفَأَمِنَ الَّذِينَ مَكَرُوا السَّيِّئَاتِ أَن يَخْسِفَ اللهُ بِهِمُ
الْأَرْضَ أَوْ يَأْتِيَهُمُ الْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ
Afaamina allatheena makaroo assayyi-atian yakhsifa Allahu bihimu al-arda aw
ya/tiyahumualAAathabu min haythu la yashAAuroon
Swahili
Je! Wameaminisha wanao fanya vitimbi vya uovu kwamba Mwenyezi Mungu
hatawadidimiza katika ardhi, na haitawafika adhabu kutoka wasipo pajua?
|
Ayah 16:46 الأية
أَوْ يَأْخُذَهُمْ فِي تَقَلُّبِهِمْ فَمَا هُم بِمُعْجِزِينَ
Aw ya/khuthahum fee taqallubihim famahum bimuAAjizeen
Swahili
Au hatawashika katika nyendo zao, na wala hawataponyoka?
|
Ayah 16:47 الأية
أَوْ يَأْخُذَهُمْ عَلَىٰ تَخَوُّفٍ فَإِنَّ رَبَّكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ
Aw ya/khuthahum AAalatakhawwufin fa-inna rabbakum laraoofun raheem
Swahili
Au hatawashika kwa kitisho na kuwapunguza kidogo kidogo? Hakika Mola wenu Mlezi
ni Mwenye huruma, Mwenye kurehemu.
|
Ayah 16:48 الأية
أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَىٰ مَا خَلَقَ اللهُ مِن شَيْءٍ يَتَفَيَّأُ ظِلَالُهُ عَنِ
الْيَمِينِ وَالشَّمَائِلِ سُجَّدًا لِّلَّهِ وَهُمْ دَاخِرُونَ
Awa lam yaraw ila ma khalaqaAllahu min shay-in yatafayyao thilaluhuAAani
alyameeni washshama-ili sujjadan lillahiwahum dakhiroon
Swahili
Je! Hawavioni vitu alivyo viumba Mwenyezi Mungu - vivuli vyao vinaelekea
kushotoni na kuliani, kumsujudia Mwenyezi Mungu na vikinyenyekea?
|
Ayah 16:49 الأية
وَلِلَّهِ يَسْجُدُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مِن دَابَّةٍ
وَالْمَلَائِكَةُ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ
Walillahi yasjudu ma fee assamawatiwama fee al-ardi min dabbatin
walmala-ikatuwahum la yastakbiroon
Swahili
Na vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi, tangu wanyama mpaka Malaika,
vinamsujuidia Mwenyezi Mungu, na wala havitakabari.
|
Ayah 16:50 الأية
يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ ۩
Yakhafoona rabbahum min fawqihimwayafAAaloona ma yu/maroon
Swahili
Vinamkhofu Mola wao Mlezi aliye juu yao, na vinafanya vinavyo amrishwa.
|
Ayah 16:51 الأية
وَقَالَ اللهُ لَا تَتَّخِذُوا إِلَٰهَيْنِ اثْنَيْنِ ۖ إِنَّمَا هُوَ إِلَٰهٌ
وَاحِدٌ ۖ فَإِيَّايَ فَارْهَبُونِ
Waqala Allahu latattakhithoo ilahayni ithnayni innama huwailahun wahidun
fa-iyyaya farhaboon
Swahili
Na Mwenyezi Mungu amesema: Msiwe na miungu wawili! Hakika Yeye ni Mungu Mmoja.
Basi niogopeni Mimi tu!
|
Ayah 16:52 الأية
وَلَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَهُ الدِّينُ وَاصِبًا ۚ أَفَغَيْرَ
اللهِ تَتَّقُونَ
Walahu ma fee assamawatiwal-ardi walahu addeenu wasibanafaghayra Allahi
tattaqoon
Swahili
Na ni vyake Yeye viliomo katika mbingu na ardhi. Na Dini ni yake Yeye daima. Je!
Mtamcha mwengine asiye kuwa Mwenyezi Mungu?
|
Ayah 16:53 الأية
وَمَا بِكُم مِّن نِّعْمَةٍ فَمِنَ اللهِ ۖ ثُمَّ إِذَا مَسَّكُمُ الضُّرُّ
فَإِلَيْهِ تَجْأَرُونَ
Wama bikum min niAAmatin famina Allahithumma itha massakumu addurru
fa-ilayhitaj-aroon
Swahili
Na neema yoyote mliyo nayo inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Kisha yakikuguseni
madhara mnamyayatikia Yeye.
|
Ayah 16:54 الأية
ثُمَّ إِذَا كَشَفَ الضُّرَّ عَنكُمْ إِذَا فَرِيقٌ مِّنكُم بِرَبِّهِمْ
يُشْرِكُونَ
Thumma itha kashafa addurraAAankum itha fareequn minkum birabbihim yushrikoon
Swahili
Na anapo kuondosheeni madhara mara kundi moja miongoni mwenu linamshirikisha
Mola wao Mlezi,
|
Ayah 16:55 الأية
لِيَكْفُرُوا بِمَا آتَيْنَاهُمْ ۚ فَتَمَتَّعُوا ۖ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ
Liyakfuroo bima ataynahumfatamattaAAoo fasawfa taAAlamoon
Swahili
Wakizikataa neema tulizo wapa. Basi stareheni. Mtakuja jua!
|
Ayah 16:56 الأية
وَيَجْعَلُونَ لِمَا لَا يَعْلَمُونَ نَصِيبًا مِّمَّا رَزَقْنَاهُمْ ۗ تَاللهِ
لَتُسْأَلُنَّ عَمَّا كُنتُمْ تَفْتَرُونَ
WayajAAaloona lima layaAAlamoona naseeban mimma razaqnahum tallahilatus-alunna
AAamma kuntum taftaroon
Swahili
Na hao ambao hata hawawajui wanawawekea sehemu ya tunavyo waruzuku. Wallahi!
Bila ya shaka mtasailiwa kwa hayo mliyo kuwa mnayazua!
|
Ayah 16:57 الأية
وَيَجْعَلُونَ لِلَّهِ الْبَنَاتِ سُبْحَانَهُ ۙ وَلَهُم مَّا يَشْتَهُونَ
WayajAAaloona lillahi albanatisubhanahu walahum ma yashtahoon
Swahili
Na wanamfanyia Mwenyezi Mungu ati ana mabinti, Subhanahu, Aliye takasika! Na wao
wenyewe, ati ndio wawe na hayo wanayo yatamani!
|
Ayah 16:58 الأية
وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِالْأُنثَىٰ ظَلَّ وَجْهُهُ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ
Wa-itha bushshira ahaduhum bilonthathalla wajhuhu muswaddan wahuwa katheem
Swahili
Na mmoja wao akibashiriwa kwa msichana, uso wake unasawijika, naye kajaa chuki.
|
Ayah 16:59 الأية
يَتَوَارَىٰ مِنَ الْقَوْمِ مِن سُوءِ مَا بُشِّرَ بِهِ ۚ أَيُمْسِكُهُ عَلَىٰ
هُونٍ أَمْ يَدُسُّهُ فِي التُّرَابِ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ
Yatawara mina alqawmi minsoo-i ma bushshira bihi ayumsikuhu AAala hoonin
amyadussuhu fee atturabi ala saa mayahkumoon
Swahili
Anajificha asionekane na watu kwa ubaya wa aliyo bashiriwa! Je, akae naye juu ya
fedheha hiyo au amfukie udongoni? Tazama uovu wa wanavyo hukumu!
|
Ayah 16:60 الأية
لِلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ مَثَلُ السَّوْءِ ۖ وَلِلَّهِ الْمَثَلُ
الْأَعْلَىٰ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ
Lillatheena la yu/minoona bil-akhiratimathalu assaw-i walillahi almathalu
al-aAAlawahuwa alAAazeezu alhakeem
Swahili
Hali ya wasio iamini Akhera ni ovu; na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye sifa tukufu.
Naye ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
|
Ayah 16:61 الأية
وَلَوْ يُؤَاخِذُ اللهُ النَّاسَ بِظُلْمِهِم مَّا تَرَكَ عَلَيْهَا مِن دَابَّةٍ
وَلَٰكِن يُؤَخِّرُهُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۖ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ لَا
يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ
Walaw yu-akhithu Allahuannasa bithulmihim ma tarakaAAalayha min dabbatin walakin
yu-akhkhiruhumila ajalin musamman fa-itha jaa ajaluhum layasta/khiroona saAAatan
wala yastaqdimoon
Swahili
Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli wachukulia watu kwa mujibu wa dhulma zao, basi
asingeli mwacha hapa hata mnyama mmoja. Lakini anawaakhirisha mpaka muda ulio
wekwa. Na unapo fika muda wao hawatakawilia hata saa moja wala hawatatangulia.
|
Ayah 16:62 الأية
وَيَجْعَلُونَ لِلَّهِ مَا يَكْرَهُونَ وَتَصِفُ أَلْسِنَتُهُمُ الْكَذِبَ أَنَّ
لَهُمُ الْحُسْنَىٰ ۖ لَا جَرَمَ أَنَّ لَهُمُ النَّارَ وَأَنَّهُم مُّفْرَطُونَ
WayajAAaloona lillahi mayakrahoona watasifu alsinatuhumu alkathiba annalahumu
alhusna la jarama anna lahumu annarawaannahum mufratoon
Swahili
Na wanampa Mwenyezi Mungu wanavyo vichukia wao, na ndimi zao zinasema uwongo
kwamba wao watapata mema. Hapana shaka hakika wamewekewa Moto, nao wataachwa
humo.
|
Ayah 16:63 الأية
تَاللهِ لَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ أُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَزَيَّنَ لَهُمُ
الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ فَهُوَ وَلِيُّهُمُ الْيَوْمَ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Tallahi laqad arsalnaila omamin min qablika fazayyana lahumu
ashshaytanuaAAmalahum fahuwa waliyyuhumu alyawma walahum AAathabunaleem
Swahili
Wallahi! Sisi tulituma Mitume kwa umati zilizo kuwa kabla yako, lakini Shetani
aliwapambia vitendo vyao. Kwa hivyo leo yeye ndiye rafiki yao; nao watapata
adhabu chungu.
|
Ayah 16:64 الأية
وَمَا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ إِلَّا لِتُبَيِّنَ لَهُمُ الَّذِي
اخْتَلَفُوا فِيهِ ۙ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ
Wama anzalna AAalayka alkitabailla litubayyina lahumu allathee ikhtalafoo
feehiwahudan warahmatan liqawmin yu/minoon
Swahili
Na hatukukuteremshia Kitabu isipo kuwa uwabainishie yale ambayo
wanakhitalifiana, na kiwe Uwongofu na Rehema kwa watu wanao amini.
|
Ayah 16:65 الأية
وَاللهُ أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ
مَوْتِهَا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ
Wallahu anzala mina assama-imaan faahya bihi al-arda baAAdamawtiha inna fee
thalika laayatan liqawminyasmaAAoon
Swahili
Na Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni na kwa hayo akaihuisha ardhi
baada ya kufa kwake. Kwa hakika katika hayo imo Ishara kwa watu wanao sikia.
|
Ayah 16:66 الأية
وَإِنَّ لَكُمْ فِي الْأَنْعَامِ لَعِبْرَةً ۖ نُّسْقِيكُم مِّمَّا فِي بُطُونِهِ
مِن بَيْنِ فَرْثٍ وَدَمٍ لَّبَنًا خَالِصًا سَائِغًا لِّلشَّارِبِينَ
Wa-inna lakum fee al-anAAamilaAAibratan nusqeekum mimma fee butoonihi min
baynifarthin wadamin labanan khalisan sa-ighan lishsharibeen
Swahili
Na hakika katika nyama hoa nyinyi mna mazingatio. Tunakunywesheni katika vile
viliomo matumboni mwao, vikatoka baina ya mavi na damu, maziwa safi mazuri kwa
wanywao.
|
Ayah 16:67 الأية
وَمِن ثَمَرَاتِ النَّخِيلِ وَالْأَعْنَابِ تَتَّخِذُونَ مِنْهُ سَكَرًا وَرِزْقًا
حَسَنًا ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ
Wamin thamarati annakheeli wal-aAAnabitattakhithoona minhu sakaran warizqan
hasanan innafee thalika laayatan liqawmin yaAAqiloon
Swahili
Na kutokana na matunda ya mitende na mizabibu mnatengeneza ulevi na riziki
nzuri. Hakika katika hayo ipo Ishara kwa wanao tumia akili.
|
Ayah 16:68 الأية
وَأَوْحَىٰ رَبُّكَ إِلَى النَّحْلِ أَنِ اتَّخِذِي مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا
وَمِنَ الشَّجَرِ وَمِمَّا يَعْرِشُونَ
Waawha rabbuka ila annahliani ittakhithee mina aljibali buyootan wamina
ashshajariwamimma yaAArishoon
Swahili
Na Mola wako Mlezi amemfunulia nyuki: Jitengenezee majumba yako katika milima,na
katika miti, na katika wanayo jenga watu.
|
Ayah 16:69 الأية
ثُمَّ كُلِي مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ فَاسْلُكِي سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلًا ۚ يَخْرُجُ
مِن بُطُونِهَا شَرَابٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَانُهُ فِيهِ شِفَاءٌ لِّلنَّاسِ ۗ إِنَّ
فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ
Thumma kulee min kulli aththamaratifaslukee subula rabbiki thululan yakhruju min
butoonihasharabun mukhtalifun alwanuhu feehi shifaonlinnasi inna fee thalika
laayatanliqawmin yatafakkaroon
Swahili
Kisha kula katika kila matunda, na upite katika njia za Mola wako Mlezi zilizo
fanywa nyepesi kuzipita. Na kutoka matumbo yao kinatoka kinywaji chenye rangi
mbali mbali; ndani yake kina matibabu kwa wanaadamu. Hakika katika haya ipo
Ishara kwa watu wanao fikiri.
|
Ayah 16:70 الأية
وَاللهُ خَلَقَكُمْ ثُمَّ يَتَوَفَّاكُمْ ۚ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰ
أَرْذَلِ الْعُمُرِ لِكَيْ لَا يَعْلَمَ بَعْدَ عِلْمٍ شَيْئًا ۚ إِنَّ اللهَ
عَلِيمٌ قَدِيرٌ
Wallahu khalaqakum thummayatawaffakum waminkum man yuraddu ila arthalialAAumuri
likay la yaAAlama baAAda AAilmin shay-an innaAllaha AAaleemun qadeer
Swahili
Na Mwenyezi Mungu amekuumbeni; kisha anakufisheni. Na miongoni mwenu wapo wanao
rudishwa kwenye umri mbaya kabisa, hata akawa asijue kitu baada ya ujuzi alio
kuwa nao. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi na Mweza.
|
Ayah 16:71 الأية
وَاللهُ فَضَّلَ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ فِي الرِّزْقِ ۚ فَمَا الَّذِينَ
فُضِّلُوا بِرَادِّي رِزْقِهِمْ عَلَىٰ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَهُمْ فِيهِ
سَوَاءٌ ۚ أَفَبِنِعْمَةِ اللهِ يَجْحَدُونَ
Wallahu faddala baAAdakumAAala baAAdin fee arrizqi fama allatheenafuddiloo
biraddee rizqihim AAala mamalakat aymanuhum fahum feehi sawaon
afabiniAAmatiAllahi yajhadoon
Swahili
Na Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yenu kuliko wengine katika riziki. Na
wale walio fadhilishwa hawarudishi riziki zao kwa wale ilio wamiliki mikono yao
ya kulia ili wawe sawa katika riziki hiyo. Basi je, wanazikataa neema za
Mwenyezi Mungu?
|
Ayah 16:72 الأية
وَاللهُ جَعَلَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنْ
أَزْوَاجِكُم بَنِينَ وَحَفَدَةً وَرَزَقَكُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ ۚ
أَفَبِالْبَاطِلِ يُؤْمِنُونَ وَبِنِعْمَتِ اللهِ هُمْ يَكْفُرُونَ
Wallahu jaAAala lakum minanfusikum azwajan wajaAAala lakum min azwajikumbaneena
wahafadatan warazaqakum mina attayyibatiafabilbatili yu/minoona wabiniAAmati
Allahihum yakfuroon
Swahili
Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake katika jinsi yenu, na akakujaalieni kutoka
kwa wake zenu wana na wajukuu, na akakuruzukuni vitu vizuri vizuri. Basi je,
wanaamini upotovu na wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu?
|
Ayah 16:73 الأية
وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَهُمْ رِزْقًا مِّنَ
السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ شَيْئًا وَلَا يَسْتَطِيعُونَ
WayaAAbudoona min dooni Allahi mala yamliku lahum rizqan mina assamawatiwal-ardi
shay-an wala yastateeAAoon
Swahili
Na badala ya Mwenyezi Mungu wanawaabudu wasio wamilikia riziki kutoka mbinguni
wala kwenye ardhi, wala hawawezi kitu.
|
Ayah 16:74 الأية
فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّهِ الْأَمْثَالَ ۚ إِنَّ اللهَ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا
تَعْلَمُونَ
Fala tadriboo lillahial-amthala inna Allaha yaAAlamu waantum lataAAlamoon
Swahili
Basi msimpigie Mwenyezi Mungu mifano. Hakika Mwenyezi Mungu anajua, na nyinyi
hamjui.
|
Ayah 16:75 الأية
ضَرَبَ اللهُ مَثَلًا عَبْدًا مَّمْلُوكًا لَّا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَيْءٍ وَمَن
رَّزَقْنَاهُ مِنَّا رِزْقًا حَسَنًا فَهُوَ يُنفِقُ مِنْهُ سِرًّا وَجَهْرًا ۖ
هَلْ يَسْتَوُونَ ۚ الْحَمْدُ لِلَّهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
Daraba Allahu mathalan AAabdanmamlookan la yaqdiru AAala shay-in waman
razaqnahuminna rizqan hasanan fahuwa yunfiqu minhu sirranwajahran hal yastawoona
alhamdu lillahi balaktharuhum la yaAAlamoon
Swahili
Mwenyezi Mungu anapiga mfano wa mtumwa aliye milikiwa, asiye weza kitu, na
mwingine tuliye mruzuku riziki njema inayo toka kwetu, naye akawa anatoa katika
riziki hiyo kwa siri na dhaahiri. Je, hao watakuwa sawa? Alhamdu Lillahi!
Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wengi wao hawajui.
|
Ayah 16:76 الأية
وَضَرَبَ اللهُ مَثَلًا رَّجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا أَبْكَمُ لَا يَقْدِرُ عَلَىٰ
شَيْءٍ وَهُوَ كَلٌّ عَلَىٰ مَوْلَاهُ أَيْنَمَا يُوَجِّههُّ لَا يَأْتِ بِخَيْرٍ ۖ
هَلْ يَسْتَوِي هُوَ وَمَن يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ ۙ وَهُوَ عَلَىٰ صِرَاطٍ
مُّسْتَقِيمٍ
Wadaraba Allahu mathalanrajulayni ahaduhuma abkamu la yaqdiru AAalashay-in
wahuwa kallun AAala mawlahu aynamayuwajjihhu la ya/ti bikhayrin hal yastawee
huwa wamanya/muru bilAAadli wahuwa AAala siratinmustaqeem
Swahili
Na Mwenyezi Mungu anapiga mfano wa watu wawili. Mmoja wao ni bubu, hawezi
chochote, naye ni mzigo kwa bwana wake. Popote anapo muelekeza haleti kheri. Je!
Huyo anaweza kuwa sawa na yule anaye amrisha uadilifu, naye yuko juu ya Njia
Iliyo Nyooka?
|
Ayah 16:77 الأية
وَلِلَّهِ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَمَا أَمْرُ السَّاعَةِ إِلَّا
كَلَمْحِ الْبَصَرِ أَوْ هُوَ أَقْرَبُ ۚ إِنَّ اللهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ
قَدِيرٌ
Walillahi ghaybu assamawatiwal-ardi wama amru assaAAatiilla kalamhi albasari aw
huwa aqrabu innaAllaha AAala kulli shay-in qadeer
Swahili
Na siri zote za katika mbingu na ardhi ziko kwa Mwenyezi Mungu. Wala halikuwa
jambo la Saa (ya Kiyama) ila kama kupepesa kwa jicho, au akali ya hivyo. Hakika
Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.
|
Ayah 16:78 الأية
وَاللهُ أَخْرَجَكُم مِّن بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ لَا تَعْلَمُونَ شَيْئًا
وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ ۙ لَعَلَّكُمْ
تَشْكُرُونَ
Wallahu akhrajakum min butooniommahatikum la taAAlamoona shay-an wajaAAala
lakumuassamAAa wal-absara wal-af-idatalaAAallakum tashkuroon
Swahili
Na Mwenyezi Mungu amekutoeni matumboni mwa mama zenu, hali ya kuwa hamjui kitu,
na amekujaalieni masikio na macho na nyoyo ili mpate kushukuru.
|
Ayah 16:79 الأية
أَلَمْ يَرَوْا إِلَى الطَّيْرِ مُسَخَّرَاتٍ فِي جَوِّ السَّمَاءِ مَا
يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا اللهُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ
Alam yaraw ila attayrimusakhkharatin fee jawwi assama-i mayumsikuhunna illa
Allahu inna fee thalika laayatinliqawmin yu/minoon
Swahili
Je! Hawawaoni ndege walivyo wat'iifu katika anga la mbingu? Hapana mwenye
kuwashika isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Hakika katika haya zipo ishara kwa watu
wanao amini.
|
Ayah 16:80 الأية
وَاللهُ جَعَلَ لَكُم مِّن بُيُوتِكُمْ سَكَنًا وَجَعَلَ لَكُم مِّن جُلُودِ
الْأَنْعَامِ بُيُوتًا تَسْتَخِفُّونَهَا يَوْمَ ظَعْنِكُمْ وَيَوْمَ إِقَامَتِكُمْ
ۙ وَمِنْ أَصْوَافِهَا وَأَوْبَارِهَا وَأَشْعَارِهَا أَثَاثًا وَمَتَاعًا إِلَىٰ
حِينٍ
Wallahu jaAAala lakum minbuyootikum sakanan wajaAAala lakum min juloodi
al-anAAamibuyootan tastakhiffoonaha yawma thaAAnikumwayawma iqamatikum wamin
aswafihawaawbariha waashAAariha athathanwamataAAan ila heen
Swahili
Na Mwenyezi Mungu amekujaalieni majumba yenu yawe ni maskani yenu, na
amekujaalieni kutokana na ngozi za wanyama nyumba mnazo ziona nyepesi wakati wa
safari zenu na wakati wa kutua kwenu. Na kutokana na sufi zao na manyoya yao na
nywele zao mnafanya matandiko na mapambo ya kutumia kwa muda.
|
Ayah 16:81 الأية
وَاللهُ جَعَلَ لَكُم مِّمَّا خَلَقَ ظِلَالًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ الْجِبَالِ
أَكْنَانًا وَجَعَلَ لَكُمْ سَرَابِيلَ تَقِيكُمُ الْحَرَّ وَسَرَابِيلَ تَقِيكُم
بَأْسَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُتِمُّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تُسْلِمُونَ
Wallahu jaAAala lakum mimmakhalaqa thilalan wajaAAala lakum mina aljibaliaknanan
wajaAAala lakum sarabeela taqeekumu alharrawasarabeela taqeekum ba/sakum
kathalika yutimmuniAAmatahu AAalaykum laAAallakum tuslimoon
Swahili
Na Mwenyezi Mungu amekufanyieni vivuli katika vitu alivyo viumba, na
amekufanyieni maskani milimani, na amekufanyieni nguo za kukingeni na joto, na
nguo za kukingeni katika vita vyenu. Ndio hivyo anakutimizieni neema zake ili
mpate kut'ii.
|
Ayah 16:82 الأية
فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ الْمُبِينُ
Fa-in tawallaw fa-innama AAalaykaalbalaghu almubeen
Swahili
Basi wakikengeuka lilio juu yako wewe ni kufikisha ujumbe wazi wazi.
|
Ayah 16:83 الأية
يَعْرِفُونَ نِعْمَتَ اللهِ ثُمَّ يُنكِرُونَهَا وَأَكْثَرُهُمُ الْكَافِرُونَ
YaAArifoona niAAmata Allahi thummayunkiroonaha waaktharuhumu alkafiroon
Swahili
Wanazijua neema za Mwenyezi Mungu, kisha wanazikanusha; na wengi wao ni
makafiri.
|
Ayah 16:84 الأية
وَيَوْمَ نَبْعَثُ مِن كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا ثُمَّ لَا يُؤْذَنُ لِلَّذِينَ
كَفَرُوا وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ
Wayawma nabAAathu min kulli ommatinshaheedan thumma la yu/thanu
lillatheenakafaroo wala hum yustaAAtaboon
Swahili
Na siku tutakapo wainua kutokana na kila umma shahidi, kisha hawataruhusiwa
walio kufuru wala hawataachiliwa kutaka radhi.
|
Ayah 16:85 الأية
وَإِذَا رَأَى الَّذِينَ ظَلَمُوا الْعَذَابَ فَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُمْ وَلَا هُمْ
يُنظَرُونَ
Wa-itha raa allatheena thalamooalAAathaba fala yukhaffafu AAanhum wala
humyuntharoon
Swahili
Na walio dhulumu watakapo iona adhabu hawatapunguziwa hiyo adhabu, wala
hawatapewa muhula.
|
Ayah 16:86 الأية
وَإِذَا رَأَى الَّذِينَ أَشْرَكُوا شُرَكَاءَهُمْ قَالُوا رَبَّنَا هَٰؤُلَاءِ
شُرَكَاؤُنَا الَّذِينَ كُنَّا نَدْعُو مِن دُونِكَ ۖ فَأَلْقَوْا إِلَيْهِمُ
الْقَوْلَ إِنَّكُمْ لَكَاذِبُونَ
Wa-itha raa allatheenaashrakoo shurakaahum qaloo rabbana haola-ishurakaona
allatheena kunna nadAAoomin doonika faalqaw ilayhimu alqawla innakum lakathiboon
Swahili
Na walio shirikisha watakapo waona hao walio washirikisha na Mwenyezi Mungu,
watasema: Mola wetu Mlezi! Hawa ndio washirikishwa wetu ambao tulikuwa
tukiwaabudu badala yako. Ndipo wale watakapo watupia kauli: Hakika nyinyi ni
waongo!
|
Ayah 16:87 الأية
وَأَلْقَوْا إِلَى اللهِ يَوْمَئِذٍ السَّلَمَ ۖ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا
يَفْتَرُونَ
Waalqaw ila Allahi yawma-ithinassalama wadalla AAanhum ma kanooyaftaroon
Swahili
Na siku hiyo watasalimu amri mbele ya Mwenyezi Mungu, na yatapotea waliyo kuwa
wakiyazua.
|
Ayah 16:88 الأية
الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللهِ زِدْنَاهُمْ عَذَابًا فَوْقَ
الْعَذَابِ بِمَا كَانُوا يُفْسِدُونَ
Allatheena kafaroo wasaddooAAan sabeeli Allahi zidnahum AAathaban
fawqaalAAathabi bima kanoo yufsidoon
Swahili
Wale walio kufuru na kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu tutawazidishia adhabu juu
ya adhabu, kwa walivyo kuwa wakifisidi.
|
Ayah 16:89 الأية
وَيَوْمَ نَبْعَثُ فِي كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا عَلَيْهِم مِّنْ أَنفُسِهِمْ ۖ
وَجِئْنَا بِكَ شَهِيدًا عَلَىٰ هَٰؤُلَاءِ ۚ وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ
تِبْيَانًا لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ
Wayawma nabAAathu fee kulli ommatinshaheedan AAalayhim min anfusihim waji/na
bika shaheedanAAala haola-i wanazzalna AAalaykaalkitaba tibyanan likulli shay-in
wahudan warahmatanwabushra lilmuslimeen
Swahili
Na (waonye) siku tutakapo wainua mashahidi katika kila umma wakiwashuhudia kwa
yanayo tokana na wao, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hao. Na
tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na
rehema, na bishara kwa Waislamu.
|
Ayah 16:90 الأية
إِنَّ اللهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ
وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ
تَذَكَّرُونَ
Inna Allaha ya/muru bilAAadliwal-ihsani wa-eeta-i theealqurba wayanha AAani
alfahsha-i walmunkariwalbaghyi yaAAithukum laAAallakum tathakkaroon
Swahili
Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa;
na anakataza uchafu, na uovu, na dhulma. Anakuwaidhini ili mpate kukumbuka.
|
Ayah 16:91 الأية
وَأَوْفُوا بِعَهْدِ اللهِ إِذَا عَاهَدتُّمْ وَلَا تَنقُضُوا الْأَيْمَانَ
بَعْدَ تَوْكِيدِهَا وَقَدْ جَعَلْتُمُ اللهَ عَلَيْكُمْ كَفِيلًا ۚ إِنَّ
اللهَ يَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ
Waawfoo biAAahdi Allahi ithaAAahadtum wala tanqudoo al-aymanabaAAda tawkeediha
waqad jaAAaltumu Allaha AAalaykumkafeelan inna Allaha yaAAlamu ma tafAAaloon
Swahili
Na timizeni ahadi ya Mwenyezi Mungu mnapo ahidi, wala msivunje viapo baada ya
kuvithibitisha, ilihali mmekwisha mfanya Mwenyezi Mungu ndiye mdhamini wenu.
Hakika Mwenyezi Mungu anayajua myatendayo.
|
Ayah 16:92 الأية
وَلَا تَكُونُوا كَالَّتِي نَقَضَتْ غَزْلَهَا مِن بَعْدِ قُوَّةٍ أَنكَاثًا
تَتَّخِذُونَ أَيْمَانَكُمْ دَخَلًا بَيْنَكُمْ أَن تَكُونَ أُمَّةٌ هِيَ أَرْبَىٰ
مِنْ أُمَّةٍ ۚ إِنَّمَا يَبْلُوكُمُ اللهُ بِهِ ۚ وَلَيُبَيِّنَنَّ لَكُمْ
يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ
Wala takoonoo kallatee naqadatghazlaha min baAAdi quwwatin ankathan
tattakhithoonaaymanakum dakhalan baynakum an takoona ommatun hiya arbamin
ommatin innama yablookumu Allahu bihiwalayubayyinanna lakum yawma alqiyamati ma
kuntumfeehi takhtalifoon
Swahili
Wala msiwe kama mwanamke anaye uzongoa uzi wake baada ya kwisha usokota ukawa
mgumu. Mnavifanya viapo vyenu kuwa ni njia ya kudanganyana baina yenu kwa kuwa
ati taifa moja lina nguvu zaidi kuliko jengine? Hakika Mwenyezi Mungu
anakujaribuni kwa njia hiyo. Na bila ya shaka atakubainishieni Siku ya Kiyama
mliyo kuwa mkikhitalifiana.
|
Ayah 16:93 الأية
وَلَوْ شَاءَ اللهُ لَجَعَلَكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَٰكِن يُضِلُّ مَن يَشَاءُ
وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَلَتُسْأَلُنَّ عَمَّا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Walaw shaa Allahu lajaAAalakumommatan wahidatan walakin yudillu man
yashaowayahdee man yashao walatus-alunna AAamma kuntumtaAAmaloon
Swahili
Na Mwenyezi Mungu angeli taka, kwa yakini angeli kufanyeni umma mmoja. Lakini
anamwachia kupotea anaye mtaka, na anamwongoa amtakaye. Na hakika mtaulizwa kwa
yale mliyo kuwa mkiyafanya.
|
Ayah 16:94 الأية
وَلَا تَتَّخِذُوا أَيْمَانَكُمْ دَخَلًا بَيْنَكُمْ فَتَزِلَّ قَدَمٌ بَعْدَ
ثُبُوتِهَا وَتَذُوقُوا السُّوءَ بِمَا صَدَدتُّمْ عَن سَبِيلِ اللهِ ۖ وَلَكُمْ
عَذَابٌ عَظِيمٌ
Wala tattakhithoo aymanakumdakhalan baynakum fatazilla qadamun baAAda thubootiha
watathooqooassoo-a bima sadadtum AAan sabeeli Allahiwalakum AAathabun AAatheem
Swahili
Wala msifanye viapo vyenu ni njia ya kudanganyana baina yenu. Usije mguu
ukateleza badala ya kuthibiti, na mkaonja maovu kwa sababu ya kule kuzuilia Njia
ya Mwenyezi Mungu, na mkapata adhabu kubwa.
|
Ayah 16:95 الأية
وَلَا تَشْتَرُوا بِعَهْدِ اللهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۚ إِنَّمَا عِندَ اللهِ هُوَ
خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ
Wala tashtaroo biAAahdi Allahithamanan qaleelan innama AAinda Allahi huwa
khayrunlakum in kuntum taAAlamoon
Swahili
Wala msinunue ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa thamani ndogo. Hakika kilichoko kwa
Mwenyezi Mungu ndicho bora kwenu, ikiwa mnajua.
|
Ayah 16:96 الأية
مَا عِندَكُمْ يَنفَدُ ۖ وَمَا عِندَ اللهِ بَاقٍ ۗ وَلَنَجْزِيَنَّ الَّذِينَ
صَبَرُوا أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Ma AAindakum yanfadu wamaAAinda Allahi baqin walanajziyanna allatheenasabaroo
ajrahum bi-ahsani ma kanooyaAAmaloon
Swahili
Mlivyo navyo vitakwisha na vilivyoko kwa Mwenyezi Mungu ndivyo vitakavyo bakia.
Na kwa yakini Sisi tutawapa walio subiri ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa
wakiyatenda.
|
Ayah 16:97 الأية
مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ
حَيَاةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا
يَعْمَلُونَ
Man AAamila salihan min thakarinaw ontha wahuwa mu/minun falanuhyiyannahu
hayatantayyibatan walanajziyannahum ajrahum bi-ahsani makanoo yaAAmaloon
Swahili
Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha
maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda.
|
Ayah 16:98 الأية
فَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ فَاسْتَعِذْ بِاللهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ
Fa-itha qara/ta alqur-ana fastaAAithbillahi mina ashshaytani arrajeem
Swahili
Na ukisoma Qur'ani mwombe Mwenyezi Mungu akulinde na Shetani maluuni.
|
Ayah 16:99 الأية
إِنَّهُ لَيْسَ لَهُ سُلْطَانٌ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ
يَتَوَكَّلُونَ
Innahu laysa lahu sultanun AAalaallatheena amanoo waAAala rabbihimyatawakkaloon
Swahili
Hakika yeye hana madaraka juu ya walio amini na wakamtegemea Mola wao Mlezi.
|
Ayah 16:100 الأية
إِنَّمَا سُلْطَانُهُ عَلَى الَّذِينَ يَتَوَلَّوْنَهُ وَالَّذِينَ هُم بِهِ
مُشْرِكُونَ
Innama sultanuhu AAalaallatheena yatawallawnahu wallatheena humbihi mushrikoon
Swahili
Hakika madaraka yake ni juu ya wanao mfanya rafiki yao, na wale wanao fanya
ushirika naye.
|
Ayah 16:101 الأية
وَإِذَا بَدَّلْنَا آيَةً مَّكَانَ آيَةٍ ۙ وَاللهُ أَعْلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ
قَالُوا إِنَّمَا أَنتَ مُفْتَرٍ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
Wa-itha baddalna ayatanmakana ayatin wallahu aAAlamu bimayunazzilu qaloo innama
anta muftarin bal aktharuhumla yaAAlamoon
Swahili
Na tunapo badilisha Ishara pahala pa Ishara nyengine, na Mwenyezi Mungu anajua
anayo teremsha, wao husema: Wewe ni mzushi. Bali wengi wao hawajui kitu.
|
Ayah 16:102 الأية
قُلْ نَزَّلَهُ رُوحُ الْقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ لِيُثَبِّتَ الَّذِينَ
آمَنُوا وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ
Qul nazzalahu roohu alqudusi minrabbika bilhaqqi liyuthabbita allatheena
amanoowahudan wabushra lilmuslimeen
Swahili
Sema: Ameiteremsha hii Roho takatifu kutokana na Mola wako Mlezi kwa haki, ili
awathibitishe wale walio amini, na kuwa ni uwongofu, na ni bishara kwa Waislamu.
|
Ayah 16:103 الأية
وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّهُمْ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُ بَشَرٌ ۗ لِّسَانُ
الَّذِي يُلْحِدُونَ إِلَيْهِ أَعْجَمِيٌّ وَهَٰذَا لِسَانٌ عَرَبِيٌّ مُّبِينٌ
Walaqad naAAlamu annahum yaqooloona innamayuAAallimuhu basharun lisanu allathee
yulhidoonailayhi aAAjamiyyun wahatha lisanun AAarabiyyunmubeen
Swahili
Na Sisi hakika tunajua kwamba wanasema: Yuko mtu anaye mfundisha. Lugha ya huyo
wanaye muelekezea ni ya kigeni, na hii ni lugha ya Kiarabu mbayana.
|
Ayah 16:104 الأية
إِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِ اللهِ لَا يَهْدِيهِمُ اللهُ
وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Inna allatheena la yu/minoonabi-ayati Allahi la yahdeehimu Allahuwalahum
AAathabun aleem
Swahili
Hakika wasio ziamini Ishara za Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu hawaongoi, nao
watapata adhabu chungu.
|
Ayah 16:105 الأية
إِنَّمَا يَفْتَرِي الْكَذِبَ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِ اللهِ ۖ
وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْكَاذِبُونَ
Innama yaftaree alkathibaallatheena la yu/minoona bi-ayati Allahiwaola-ika humu
alkathiboon
Swahili
Wanao zua uwongo ni wale tu wasio ziamini Ishara za Mwenyezi Mungu. Na hao ndio
waongo.
|
Ayah 16:106 الأية
مَن كَفَرَ بِاللهِ مِن بَعْدِ إِيمَانِهِ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ
مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ وَلَٰكِن مَّن شَرَحَ بِالْكُفْرِ صَدْرًا فَعَلَيْهِمْ
غَضَبٌ مِّنَ اللهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ
Man kafara billahi minbaAAdi eemanihi illa man okriha waqalbuhu
mutma-innunbil-eemani walakin man sharaha bilkufrisadran faAAalayhim ghadabun
mina Allahiwalahum AAathabun AAatheem
Swahili
Anaye mkataa Mwenyezi Mungu baada ya kuamini kwake - isipo kuwa aliye lazimishwa
na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya Imani, lakini aliye kifungulia kifua
chake kukataa - basi hao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ipo juu yao, na wao watapata
adhabu kubwa.
|
Ayah 16:107 الأية
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اسْتَحَبُّوا الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَأَنَّ
اللهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ
Thalika bi-annahumu istahabbooalhayata addunya AAala al-akhiratiwaanna Allaha la
yahdee alqawma alkafireen
Swahili
Hayo ni kwa sababu wameyapenda zaidi maisha ya duniani kuliko ya Akhera, na kwa
sababu Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri.
|
Ayah 16:108 الأية
أُولَٰئِكَ الَّذِينَ طَبَعَ اللهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَسَمْعِهِمْ
وَأَبْصَارِهِمْ ۖ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ
Ola-ika allatheena tabaAAaAllahu AAala quloobihim wasamAAihim
waabsarihimwaola-ika humu alghafiloon
Swahili
Hao ndio Mwenyezi Mungu ameziziba nyoyo zao na masikio yao na macho yao. Na hao
ndio walio ghafilika.
|
Ayah 16:109 الأية
لَا جَرَمَ أَنَّهُمْ فِي الْآخِرَةِ هُمُ الْخَاسِرُونَ
La jarama annahum fee al-akhiratihumu alkhasiroon
Swahili
Hapana shaka ya kwamba hao ndio wenye kukhasiri Akhera.
|
Ayah 16:110 الأية
ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ هَاجَرُوا مِن بَعْدِ مَا فُتِنُوا ثُمَّ جَاهَدُوا
وَصَبَرُوا إِنَّ رَبَّكَ مِن بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ
Thumma inna rabbaka lillatheena hajaroomin baAAdi ma futinoo thumma jahadoo
wasabarooinna rabbaka min baAAdiha laghafoorun raheem
Swahili
Kisha hakika Mola wako Mlezi, kwa wale walio hama makwao baada ya kuteswa, kisha
wakapigania Dini na wakasubiri, bila ya shaka Mola wako Mlezi baada ya hayo ni
Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
|
Ayah 16:111 الأية
يَوْمَ تَأْتِي كُلُّ نَفْسٍ تُجَادِلُ عَن نَّفْسِهَا وَتُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ
مَّا عَمِلَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ
Yawma ta/tee kullu nafsin tujadiluAAan nafsiha watuwaffa kullu nafsin maAAamilat
wahum la yuthlamoon
Swahili
Siku ambayo kila nafsi itakuja jitetea, na kila nafsi italipwa sawa sawa na
a'mali ilizo zifanya, nao hawatadhulumiwa.
|
Ayah 16:112 الأية
وَضَرَبَ اللهُ مَثَلًا قَرْيَةً كَانَتْ آمِنَةً مُّطْمَئِنَّةً يَأْتِيهَا
رِزْقُهَا رَغَدًا مِّن كُلِّ مَكَانٍ فَكَفَرَتْ بِأَنْعُمِ اللهِ فَأَذَاقَهَا
اللهُ لِبَاسَ الْجُوعِ وَالْخَوْفِ بِمَا كَانُوا يَصْنَعُونَ
Wadaraba Allahu mathalanqaryatan kanat aminatan mutma-innatanya/teeha rizquha
raghadan min kulli makaninfakafarat bi-anAAumi Allahi faathaqaha Allahulibasa
aljooAAi walkhawfi bima kanooyasnaAAoon
Swahili
Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mji ulio kuwa na amani na utulivu, riziki
yake ikiufikia kwa nafasi kutoka kila mahali. Lakini ukazikufuru neema za
Mwenyezi Mungu; kwa hivyo Mwenyezi Mungu akauvika vazi la njaa na khofu kwa
sababu ya yale waliyo kuwa wakiyafanya.
|
Ayah 16:113 الأية
وَلَقَدْ جَاءَهُمْ رَسُولٌ مِّنْهُمْ فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمُ الْعَذَابُ وَهُمْ
ظَالِمُونَ
Walaqad jaahum rasoolun minhum fakaththaboohufaakhathahumu alAAathabu wahum
thalimoon
Swahili
Na alikwisha wajia Mjumbe wa miongoni mwao wenyewe. Lakini wakamkanusha; basi
iliwafika adhabu hali ya kuwa wamedhulumu.
|
Ayah 16:114 الأية
فَكُلُوا مِمَّا رَزَقَكُمُ اللهُ حَلَالًا طَيِّبًا وَاشْكُرُوا نِعْمَتَ
اللهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ
Fakuloo mimma razaqakumu Allahuhalalan tayyiban washkuroo niAAmataAllahi in
kuntum iyyahu taAAbudoon
Swahili
Basi kuleni katika vile alivyo kupeni Mwenyezi Mungu, vilivyo halali na vizuri.
Na shukuruni neema za Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye.
|
Ayah 16:115 الأية
إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةَ وَالدَّمَ وَلَحْمَ الْخِنزِيرِ وَمَا
أُهِلَّ لِغَيْرِ اللهِ بِهِ ۖ فَمَنِ اضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ
اللهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Innama harrama AAalaykumualmaytata waddama walahma alkhinzeeri wamaohilla
lighayri Allahi bihi famani idturra ghayra baghinwala AAadin fa-inna Allaha
ghafoorun raheem
Swahili
Amekuharimishieni nyamafu tu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliye
chinjwa kwa ajili isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu. Lakini anaye lazimishwa bila ya
kuasi, wala kuruka mipaka, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na
Mwenye kurehemu.
|
Ayah 16:116 الأية
وَلَا تَقُولُوا لِمَا تَصِفُ أَلْسِنَتُكُمُ الْكَذِبَ هَٰذَا حَلَالٌ وَهَٰذَا
حَرَامٌ لِّتَفْتَرُوا عَلَى اللهِ الْكَذِبَ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ
عَلَى اللهِ الْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ
Wala taqooloo lima tasifualsinatukumu alkathiba hatha halalunwahatha haramun
litaftaroo AAala Allahialkathiba inna allatheena yaftaroona AAalaAllahi
alkathiba la yuflihoon
Swahili
Wala msiseme uwongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu: Hichi halali, na hichi haramu
- mkimzulia uwongo Mwenyezi Mungu. Hakika wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu
hawatafanikiwa.
|
Ayah 16:117 الأية
مَتَاعٌ قَلِيلٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
MataAAun qaleelun walahum AAathabunaleem
Swahili
Ni starehe ndogo, nao watapata adhabu chungu.
|
|