1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَىٰ بِعَبْدِهِ لَيْلًا مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى
الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا ۚ
إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
Subhana allathee asrabiAAabdihi laylan mina almasjidi alharami ilaalmasjidi
al-aqsa allathee barakna hawlahulinuriyahu min ayatina innahu huwa
assameeAAualbaseer
Swahili
SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu
mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, ili tumuonyeshe
baadhi ya Ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.
|
Ayah 17:2 الأية
وَآتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَجَعَلْنَاهُ هُدًى لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ أَلَّا
تَتَّخِذُوا مِن دُونِي وَكِيلًا
Waatayna moosa alkitabawajaAAalnahu hudan libanee isra-eela allatattakhithoo min
doonee wakeela
Swahili
Na tukampa Musa Kitabu, na tukakifanya uwongofu kwa Wana wa Israili.
(Tukawambia): Msiwe na mtegemewa ila Mimi!
|
Ayah 17:3 الأية
ذُرِّيَّةَ مَنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَبْدًا شَكُورًا
Thurriyyata man hamalnamaAAa noohin innahu kana AAabdan shakoora
Swahili
Enyi kizazi tuliyo wachukua pamoja na Nuhu! Hakika yeye alikuwa mja mwenye
shukrani.
|
Ayah 17:4 الأية
وَقَضَيْنَا إِلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ فِي الْكِتَابِ لَتُفْسِدُنَّ فِي الْأَرْضِ
مَرَّتَيْنِ وَلَتَعْلُنَّ عُلُوًّا كَبِيرًا
Waqadayna ila banee isra-eelafee alkitabi latufsidunna fee al-ardi
marratayniwalataAAlunna AAuluwwan kabeera
Swahili
Na tukawahukumia Wana wa Israili katika Kitabu kwamba: Hakika nyinyi mtafanya
fisadi katika nchi mara mbili, na kwa yakini mtapanda kiburi, kiburi kikubwa.
|
Ayah 17:5 الأية
فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ أُولَاهُمَا بَعَثْنَا عَلَيْكُمْ عِبَادًا لَّنَا أُولِي
بَأْسٍ شَدِيدٍ فَجَاسُوا خِلَالَ الدِّيَارِ ۚ وَكَانَ وَعْدًا مَّفْعُولًا
Fa-itha jaa waAAdu oolahumabaAAathna AAalaykum AAibadan lana oleeba/sin
shadeedin fajasoo khilala addiyariwakana waAAdan mafAAoola
Swahili
Basi itapo fika ahadi ya kwanza yake tutakupelekeeni waja wetu wa kali kwa vita.
Watakuingilieni ndani ya majumba. Na hii ilikuwa ahadi iliyo timizwa.
|
Ayah 17:6 الأية
ثُمَّ رَدَدْنَا لَكُمُ الْكَرَّةَ عَلَيْهِمْ وَأَمْدَدْنَاكُم بِأَمْوَالٍ
وَبَنِينَ وَجَعَلْنَاكُمْ أَكْثَرَ نَفِيرًا
Thumma radadna lakumu alkarrataAAalayhim waamdadnakum bi-amwalin
wabaneenawajaAAalnakum akthara nafeera
Swahili
Kisha tukakurudishieni nguvu zenu dhidi yao, na tukakusaidieni kwa mali na wana,
na tukakujaalieni mkawa wengi zaidi.
|
Ayah 17:7 الأية
إِنْ أَحْسَنتُمْ أَحْسَنتُمْ لِأَنفُسِكُمْ ۖ وَإِنْ أَسَأْتُمْ فَلَهَا ۚ فَإِذَا
جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ لِيَسُوءُوا وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُوا الْمَسْجِدَ كَمَا
دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا مَا عَلَوْا تَتْبِيرًا
In ahsantum ahsantumli-anfusikum wa-in asa/tum falaha fa-itha jaawaAAdu
al-akhirati liyasoo-oo wujoohakum waliyadkhulooalmasjida kama dakhaloohu awwala
marratin waliyutabbiroo maAAalaw tatbeera
Swahili
Basi mkifanya wema, mnajifanyia wema nafsi zenu. Na mkifanya ubaya, mnajifanyia
wenyewe. Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu, na waingie
Msikitini kama walivyo ingia mara ya kwanza, na waharibu kila walicho kiteka kwa
uharibifu mkubwa.
|
Ayah 17:8 الأية
عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يَرْحَمَكُمْ ۚ وَإِنْ عُدتُّمْ عُدْنَا ۘ وَجَعَلْنَا
جَهَنَّمَ لِلْكَافِرِينَ حَصِيرًا
AAasa rabbukum an yarhamakumwa-in AAudtum AAudna wajaAAalna jahannama
lilkafireenahaseera
Swahili
Huenda Mola wenu Mlezi akakurehemuni. Na mkirudia na Sisi tutarudia. Na
tumeifanya Jahannamu kuwa ni gereza kwa ajili ya makafiri.
|
Ayah 17:9 الأية
إِنَّ هَٰذَا الْقُرْآنَ يَهْدِي لِلَّتِي هِيَ أَقْوَمُ وَيُبَشِّرُ
الْمُؤْمِنِينَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا كَبِيرًا
Inna hatha alqur-ana yahdeelillatee hiya aqwamu wayubashshiru almu/mineena
allatheenayaAAmaloona assalihati anna lahum ajrankabeera
Swahili
Hakika hii Qur'ani inaongoa kwenye ya yaliyo nyooka kabisa, na inawabashiria
Waumini ambao wanatenda mema ya kwamba watapata malipo makubwa.
|
Ayah 17:10 الأية
وَأَنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ أَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابًا
أَلِيمًا
Waanna allatheena layu/minoona bil-akhirati aAAtadna lahum AAathabanaleema
Swahili
Na yakwamba wale wasio iamini Akhera tumewaandalia adhabu chungu.
|
Ayah 17:11 الأية
وَيَدْعُ الْإِنسَانُ بِالشَّرِّ دُعَاءَهُ بِالْخَيْرِ ۖ وَكَانَ الْإِنسَانُ
عَجُولًا
WayadAAu al-insanu bishsharriduAAaahu bilkhayri wakana al-insanuAAajoola
Swahili
Na mwanaadamu huomba shari kama vile aombavyo kheri, kwani mwanaadamu ni mwenye
pupa.
|
Ayah 17:12 الأية
وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ آيَتَيْنِ ۖ فَمَحَوْنَا آيَةَ اللَّيْلِ
وَجَعَلْنَا آيَةَ النَّهَارِ مُبْصِرَةً لِّتَبْتَغُوا فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ
وَلِتَعْلَمُوا عَدَدَ السِّنِينَ وَالْحِسَابَ ۚ وَكُلَّ شَيْءٍ فَصَّلْنَاهُ
تَفْصِيلًا
WajaAAalna allayla wannaharaayatayni famahawna ayata allayliwajaAAalna ayata
annahari mubsiratanlitabtaghoo fadlan min rabbikum walitaAAlamoo AAadada
assineenawalhisaba wakulla shay-in fassalnahutafseela
Swahili
Na tumefanya usiku na mchana kuwa ishara mbili. Tena tukaifuta ishara ya usiku,
na tukaifanya ishara ya mchana ni yenye mwangaza ili mtafute fadhila itokayo kwa
Mola wenu Mlezi, na mpate kujua idadi ya miaka na hisabu. Na kila kitu
tumekifafanua waziwazi.
|
Ayah 17:13 الأية
وَكُلَّ إِنسَانٍ أَلْزَمْنَاهُ طَائِرَهُ فِي عُنُقِهِ ۖ وَنُخْرِجُ لَهُ يَوْمَ
الْقِيَامَةِ كِتَابًا يَلْقَاهُ مَنشُورًا
Wakulla insanin alzamnahu ta-irahufee AAunuqihi wanukhriju lahu yawma alqiyamati
kitabanyalqahu manshoora
Swahili
Na kila mtu tumemfungia a'mali yake shingoni mwake. Na Siku ya Kiyama tutamtolea
kitabu atakacho kikuta kiwazi kimekunjuliwa.
|
Ayah 17:14 الأية
اقْرَأْ كِتَابَكَ كَفَىٰ بِنَفْسِكَ الْيَوْمَ عَلَيْكَ حَسِيبًا
Iqra/ kitabaka kafa binafsikaalyawma AAalayka haseeba
Swahili
Ataambiwa: Soma kitabu chako! Nafsi yako inakutosha leo kukuhisabu.
|
Ayah 17:15 الأية
مَّنِ اهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِي لِنَفْسِهِ ۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ
عَلَيْهَا ۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۗ وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ
حَتَّىٰ نَبْعَثَ رَسُولًا
Mani ihtada fa-innama yahtadeelinafsihi waman dalla fa-innama yadilluAAalayha
wala taziru waziratun wizra okhrawama kunna muAAaththibeena hattanabAAatha
rasoola
Swahili
Anaye ongoka basi anaongoka kwa ajili ya nafsi yake. Na anaye potea basi
anapotea kwa khasara yake mwenyewe. Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine. Wala
Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume.
|
Ayah 17:16 الأية
وَإِذَا أَرَدْنَا أَن نُّهْلِكَ قَرْيَةً أَمَرْنَا مُتْرَفِيهَا فَفَسَقُوا
فِيهَا فَحَقَّ عَلَيْهَا الْقَوْلُ فَدَمَّرْنَاهَا تَدْمِيرًا
Wa-itha aradna an nuhlikaqaryatan amarna mutrafeeha fafasaqoo feehafahaqqa
AAalayha alqawlu fadammarnahatadmeera
Swahili
Na pindi tukitaka kuuteketeza mji huwaamrisha wale wenye starehe na taanusi,
lakini wao huendelea kutenda maovu humo. Basi hapo kauli huthibiti juu ya mji
huo, nasi tukauangamiza kwa maangamizo makubwa.
|
Ayah 17:17 الأية
وَكَمْ أَهْلَكْنَا مِنَ الْقُرُونِ مِن بَعْدِ نُوحٍ ۗ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ
بِذُنُوبِ عِبَادِهِ خَبِيرًا بَصِيرًا
Wakam ahlakna mina alqurooni minbaAAdi noohin wakafa birabbika
bithunoobiAAibadihi khabeeran baseera
Swahili
Na kaumu ngapi tumeziangamiza baada ya Nuhu! Na Mola wako Mlezi anatosha kabisa
kuwa ni Mwenye kuzijua na kuziona dhambi za waja wake.
|
Ayah 17:18 الأية
مَّن كَانَ يُرِيدُ الْعَاجِلَةَ عَجَّلْنَا لَهُ فِيهَا مَا نَشَاءُ لِمَن
نُّرِيدُ ثُمَّ جَعَلْنَا لَهُ جَهَنَّمَ يَصْلَاهَا مَذْمُومًا مَّدْحُورًا
Man kana yureedu alAAajilataAAajjalna lahu feeha ma nashao limannureedu thumma
jaAAalna lahu jahannama yaslahamathmooman madhoora
Swahili
Anaye taka yapitayo upesi upesi, tutafanya haraka kumletea hapa hapa tunayo
yataka kwa tumtakaye. Kisha tumemwekea Jahannamu; ataingia humo hali ya kuwa ni
mwenye kulaumiwa na kufurushwa.
|
Ayah 17:19 الأية
وَمَنْ أَرَادَ الْآخِرَةَ وَسَعَىٰ لَهَا سَعْيَهَا وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَٰئِكَ
كَانَ سَعْيُهُم مَّشْكُورًا
Waman arada al-akhirata wasaAAalaha saAAyaha wahuwa mu/minun faola-ika
kanasaAAyuhum mashkoora
Swahili
Na anaye itaka Akhera, na akazifanyia juhudi a'mali zake, naye ni Muumini, basi
hao juhudi yao itakuwa ni ya kushukuriwa.
|
Ayah 17:20 الأية
كُلًّا نُّمِدُّ هَٰؤُلَاءِ وَهَٰؤُلَاءِ مِنْ عَطَاءِ رَبِّكَ ۚ وَمَا كَانَ
عَطَاءُ رَبِّكَ مَحْظُورًا
Kullan numiddu haola-i wahaola-imin AAata-i rabbika wama kana AAataorabbika
mahthoora
Swahili
Wote hao tunawakunjulia - hawa na hao - katika neema za Mola wako Mlezi. Wala
neema za Mola wako Mlezi hazizuiliki.
|
Ayah 17:21 الأية
انظُرْ كَيْفَ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ وَلَلْآخِرَةُ أَكْبَرُ
دَرَجَاتٍ وَأَكْبَرُ تَفْضِيلًا
Onthur kayfa faddalnabaAAdahum AAala baAAdin walal-akhiratuakbaru darajatin
waakbaru tafdeela
Swahili
Angalia vipi tulivyo wafadhili baadhi yao kuliko wenginewe. Na hakika Akhera ni
yenye daraja kubwa zaidi na fadhila kubwa zaidi.
|
Ayah 17:22 الأية
لَّا تَجْعَلْ مَعَ اللهِ إِلَٰهًا آخَرَ فَتَقْعُدَ مَذْمُومًا مَّخْذُولًا
La tajAAal maAAa Allahi ilahanakhara fataqAAuda mathmooman makhthoola
Swahili
Usimfanye mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, usije ukawa wa kulaumiwa
uliye tupika.
|
Ayah 17:23 الأية
وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا
ۚ إِمَّا يَبْلُغَنَّ عِندَكَ الْكِبَرَ أَحَدُهُمَا أَوْ كِلَاهُمَا فَلَا تَقُل
لَّهُمَا أُفٍّ وَلَا تَنْهَرْهُمَا وَقُل لَّهُمَا قَوْلًا كَرِيمًا
Waqada rabbuka alla taAAbudooilla iyyahu wabilwalidayni ihsananimma yablughanna
AAindaka alkibara ahaduhumaaw kilahuma fala taqul lahuma offinwala tanharhuma
waqul lahuma qawlan kareema
Swahili
Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi
wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote
wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa
hishima.
|
Ayah 17:24 الأية
وَاخْفِضْ لَهُمَا جَنَاحَ الذُّلِّ مِنَ الرَّحْمَةِ وَقُل رَّبِّ ارْحَمْهُمَا
كَمَا رَبَّيَانِي صَغِيرًا
Wakhfid lahuma janahaaththulli mina arrahmati waqulrabbi irhamhuma kama
rabbayanee sagheera
Swahili
Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu
Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni.
|
Ayah 17:25 الأية
رَّبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَا فِي نُفُوسِكُمْ ۚ إِن تَكُونُوا صَالِحِينَ فَإِنَّهُ
كَانَ لِلْأَوَّابِينَ غَفُورًا
Rabbukum aAAlamu bima fee nufoosikumin takoonoo saliheena fa-innahu kana
lil-awwabeenaghafoora
Swahili
Mola wenu anajua kabisa yaliyo nyoyoni mwenu. Ikiwa nyinyi mtakuwa wema, basi
hakika Yeye ni Mwenye kuwaghufiria wanao tubia kwake.
|
Ayah 17:26 الأية
وَآتِ ذَا الْقُرْبَىٰ حَقَّهُ وَالْمِسْكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَلَا تُبَذِّرْ
تَبْذِيرًا
Waati tha alqurba haqqahuwalmiskeena wabna assabeeli walatubaththir tabtheera
Swahili
Na mpe aliye jamaa yako haki yake, na masikini, na msafiri; wala usitumie ovyo
kwa fujo.
|
Ayah 17:27 الأية
إِنَّ الْمُبَذِّرِينَ كَانُوا إِخْوَانَ الشَّيَاطِينِ ۖ وَكَانَ الشَّيْطَانُ
لِرَبِّهِ كَفُورًا
Inna almubaththireena kanooikhwana ashshayateeni wakana ashshaytanulirabbihi
kafoora
Swahili
Hakika wabadhirifu ni ndugu wa Mashet'ani. Na Shet'ani ni mwenye kumkufuru Mola
wake Mlezi.
|
Ayah 17:28 الأية
وَإِمَّا تُعْرِضَنَّ عَنْهُمُ ابْتِغَاءَ رَحْمَةٍ مِّن رَّبِّكَ تَرْجُوهَا فَقُل
لَّهُمْ قَوْلًا مَّيْسُورًا
Wa-imma tuAAridanna AAanhumuibtighaa rahmatin min rabbika tarjooha faqullahum
qawlan maysoora
Swahili
Na ikiwa unajikurupusha nao, nawe unatafuta rehema ya Mola wako Mlezi unayo
itaraji, basi sema nao maneno laini.
|
Ayah 17:29 الأية
وَلَا تَجْعَلْ يَدَكَ مَغْلُولَةً إِلَىٰ عُنُقِكَ وَلَا تَبْسُطْهَا كُلَّ
الْبَسْطِ فَتَقْعُدَ مَلُومًا مَّحْسُورًا
Wala tajAAal yadaka maghloolatan ilaAAunuqika wala tabsutha kulla
albastifataqAAuda malooman mahsoora
Swahili
Wala usiufanye mkono wako kama ulio fungwa shingoni mwako, wala usiukunjue wote
kabisa, utabaki ukilaumiwa muflisi.
|
Ayah 17:30 الأية
إِنَّ رَبَّكَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّهُ كَانَ
بِعِبَادِهِ خَبِيرًا بَصِيرًا
Inna rabbaka yabsutu arrizqaliman yashao wayaqdiru innahu kana
biAAibadihikhabeeran baseera
Swahili
Hakika Mola wako Mlezi humkunjulia riziki amtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika
Yeye kwa waja wake ni Mwenye kuwajua na kuwaona.
|
Ayah 17:31 الأية
وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُمْ خَشْيَةَ إِمْلَاقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُهُمْ
وَإِيَّاكُمْ ۚ إِنَّ قَتْلَهُمْ كَانَ خِطْئًا كَبِيرًا
Wala taqtuloo awladakumkhashyata imlaqin nahnu narzuquhum wa-iyyakuminna
qatlahum kana khit-an kabeera
Swahili
Wala msiwauwe wana wenu kwa kuogopa umasikini. Sisi tunawaruzuku wao na nyinyi.
Hakika kuwaua hao ni khatia kubwa.
|
Ayah 17:32 الأية
وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَا ۖ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا
Wala taqraboo azzinainnahu kana fahishatan wasaa sabeela
Swahili
Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya.
|
Ayah 17:33 الأية
وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۗ وَمَن
قُتِلَ مَظْلُومًا فَقَدْ جَعَلْنَا لِوَلِيِّهِ سُلْطَانًا فَلَا يُسْرِف فِّي
الْقَتْلِ ۖ إِنَّهُ كَانَ مَنصُورًا
Wala taqtuloo annafsa allateeharrama Allahu illa bilhaqqiwaman qutila mathlooman
faqad jaAAalnaliwaliyyihi sultanan fala yusrif fee alqatli innahukana mansoora
Swahili
Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipo kuwa kwa haki. Na aliye
uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka
katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa.
|
Ayah 17:34 الأية
وَلَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ حَتَّىٰ
يَبْلُغَ أَشُدَّهُ ۚ وَأَوْفُوا بِالْعَهْدِ ۖ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْئُولًا
Wala taqraboo mala alyateemiilla billatee hiya ahsanu hattayablugha ashuddahu
waawfoo bilAAahdi inna alAAahda kanamas-oola
Swahili
Wala msiyakaribie mali ya yatima, isipo kuwa kwa njia iliyo bora, mpaka afike
utuuzimani. Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itasailiwa.
|
Ayah 17:35 الأية
وَأَوْفُوا الْكَيْلَ إِذَا كِلْتُمْ وَزِنُوا بِالْقِسْطَاسِ الْمُسْتَقِيمِ ۚ
ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا
Waawfoo alkayla itha kiltum wazinoobilqistasi almustaqeemi thalika khayrun
waahsanuta/weela
Swahili
Na timizeni kipimo mpimapo. Na pimeni kwa mizani zilizo sawa. Hayo ni wema kwenu
na khatimaye ndio bora.
|
Ayah 17:36 الأية
وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ
وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا
Wala taqfu ma laysa laka bihiAAilmun inna assamAAa walbasara walfu-adakullu
ola-ika kana AAanhu mas-oola
Swahili
Wala usiyafuate usiyo na ujuzi nayo. Hakika masikio, na macho, na moyo - hivyo
vyote vitasailiwa.
|
Ayah 17:37 الأية
وَلَا تَمْشِ فِي الْأَرْضِ مَرَحًا ۖ إِنَّكَ لَن تَخْرِقَ الْأَرْضَ وَلَن
تَبْلُغَ الْجِبَالَ طُولًا
Wala tamshi fee al-ardi marahaninnaka lan takhriqa al-arda walan tablugha
aljibalatoola
Swahili
Wala usitembee katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala
kufikia urefu wa milima.
|
Ayah 17:38 الأية
كُلُّ ذَٰلِكَ كَانَ سَيِّئُهُ عِندَ رَبِّكَ مَكْرُوهًا
Kullu thalika kana sayyi-ohuAAinda rabbika makrooha
Swahili
Haya yote ubaya wake ni wenye kuchukiza kwa Mola wako Mlezi.
|
Ayah 17:39 الأية
ذَٰلِكَ مِمَّا أَوْحَىٰ إِلَيْكَ رَبُّكَ مِنَ الْحِكْمَةِ ۗ وَلَا تَجْعَلْ مَعَ
اللهِ إِلَٰهًا آخَرَ فَتُلْقَىٰ فِي جَهَنَّمَ مَلُومًا مَّدْحُورًا
Thalika mimma awhailayka rabbuka mina alhikmati wala tajAAal maAAaAllahi ilahan
akhara fatulqa feejahannama malooman madhoora
Swahili
Haya ni katika hikima alizo kufunulia Mola wako Mlezi. Wala usimweke pamoja na
Mwenyezi Mungu mungu mwengine, usije ukatupwa katika Jahannamu ukilaumiwa na
kufurushwa.
|
Ayah 17:40 الأية
أَفَأَصْفَاكُمْ رَبُّكُم بِالْبَنِينَ وَاتَّخَذَ مِنَ الْمَلَائِكَةِ إِنَاثًا ۚ
إِنَّكُمْ لَتَقُولُونَ قَوْلًا عَظِيمًا
Afaasfakum rabbukum bilbaneenawattakhatha mina almala-ikati inathaninnakum
lataqooloona qawlan AAatheema
Swahili
Je! Mola wenu Mlezi amekuteulieni wavulana, na Yeye akawafanya Malaika ni banati
zake? Kwa hakika nyinyi mnasema usemi mkubwa.
|
Ayah 17:41 الأية
وَلَقَدْ صَرَّفْنَا فِي هَٰذَا الْقُرْآنِ لِيَذَّكَّرُوا وَمَا يَزِيدُهُمْ
إِلَّا نُفُورًا
Walaqad sarrafna fee hathaalqur-ani liyaththakkaroo wama yazeeduhumilla nufoora
Swahili
Na tumekwisha bainisha katika Qur'ani hii ili wapate kukumbuka. Lakini
haikuwazidisha ila kuwa mbali nayo.
|
Ayah 17:42 الأية
قُل لَّوْ كَانَ مَعَهُ آلِهَةٌ كَمَا يَقُولُونَ إِذًا لَّابْتَغَوْا إِلَىٰ ذِي
الْعَرْشِ سَبِيلًا
Qul law kana maAAahu alihatunkama yaqooloona ithan labtaghaw ila theealAAarshi
sabeela
Swahili
Sema: Lau kuwa wangeli kuwa pamoja naye miungu mingine kama wasemavyo, basi
wangeli tafuta njia ya kumfikia Mwenye Kiti cha Enzi.
|
Ayah 17:43 الأية
سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يَقُولُونَ عُلُوًّا كَبِيرًا
Subhanahu wataAAalaAAamma yaqooloona AAuluwwan kabeera
Swahili
Subhanahu Wa Taa'la, Ametakasika na Ametukuka juu kabisa na hayo wanayo yasema.
|
Ayah 17:44 الأية
تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ ۚ وَإِن مِّن
شَيْءٍ إِلَّا يُسَبِّحُ بِحَمْدِهِ وَلَٰكِن لَّا تَفْقَهُونَ تَسْبِيحَهُمْ ۗ
إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا
Tusabbihu lahu assamawatuassabAAu wal-ardu waman feehinna wa-in minshay-in illa
yusabbihu bihamdihi walakinla tafqahoona tasbeehahum innahu kana
haleemanghafoora
Swahili
Zinamtakasa zote mbingu saba na ardhi na vyote viliomo ndani yake. Na hapana
kitu ila kinamtakasa kwa sifa zake. Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake.
Hakika Yeye ni Mpole na Mwenye maghfira.
|
Ayah 17:45 الأية
وَإِذَا قَرَأْتَ الْقُرْآنَ جَعَلْنَا بَيْنَكَ وَبَيْنَ الَّذِينَ لَا
يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ حِجَابًا مَّسْتُورًا
Wa-itha qara/ta alqur-anajaAAalna baynaka wabayna allatheena layu/minoona
bil-akhirati hijabanmastoora
Swahili
Na unapo soma Qur'ani tunaweka baina yako na wale wasio iamini Akhera pazia
linalo wafunika.
|
Ayah 17:46 الأية
وَجَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ
وَقْرًا ۚ وَإِذَا ذَكَرْتَ رَبَّكَ فِي الْقُرْآنِ وَحْدَهُ وَلَّوْا عَلَىٰ
أَدْبَارِهِمْ نُفُورًا
WajaAAalna AAala quloobihimakinnatan an yafqahoohu wafee athanihim waqran
wa-ithathakarta rabbaka fee alqur-ani wahdahuwallaw AAala adbarihim nufoora
Swahili
Na tunaweka vifuniko juu ya nyoyo zao wasije wakaifahamu, na tunaweka kwenye
masikio yao uziwi. Na unapo mtaja katika Qur'ani Mola wako Mlezi peke yake, basi
wao hugeuka nyuma wakenda zao.
|
Ayah 17:47 الأية
نَّحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَسْتَمِعُونَ بِهِ إِذْ يَسْتَمِعُونَ إِلَيْكَ وَإِذْ
هُمْ نَجْوَىٰ إِذْ يَقُولُ الظَّالِمُونَ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا رَجُلًا
مَّسْحُورًا
Nahnu aAAlamu bimayastamiAAoona bihi ith yastamiAAoona ilayka wa-ithhum najwa
ith yaqoolu aththalimoonain tattabiAAoona illa rajulan mashoora
Swahili
Sisi tunajua vyema kabisa sababu wanayo sikilizia wanapo kusikiliza, na wanapo
nong'ona. Wanapo sema hao madhaalimu: Nyinyi hamumfuati isipo kuwa mtu aliye
rogwa.
|
Ayah 17:48 الأية
انظُرْ كَيْفَ ضَرَبُوا لَكَ الْأَمْثَالَ فَضَلُّوا فَلَا يَسْتَطِيعُونَ سَبِيلًا
Onthur kayfa daraboolaka al-amthala fadalloo fala yastateeAAoonasabeela
Swahili
Tazama vipi wanavyo kupigia mifano. Basi wamepotea. Kwa hivyo hawawezi kuipata
njia.
|
Ayah 17:49 الأية
وَقَالُوا أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا وَرُفَاتًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ خَلْقًا
جَدِيدًا
Waqaloo a-itha kunnaAAithaman warufatan a-innalamabAAoothoona khalqan jadeeda
Swahili
Na walisema: Je! Tutapo kuwa mifupa na mapande yaliyo vurugika, tutafufuliwa kwa
umbo jipya?
|
Ayah 17:50 الأية
قُلْ كُونُوا حِجَارَةً أَوْ حَدِيدًا
Qul koonoo hijaratan aw hadeeda
Swahili
Sema: Kuweni hata mawe na chuma.
|
Ayah 17:51 الأية
أَوْ خَلْقًا مِّمَّا يَكْبُرُ فِي صُدُورِكُمْ ۚ فَسَيَقُولُونَ مَن يُعِيدُنَا ۖ
قُلِ الَّذِي فَطَرَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ ۚ فَسَيُنْغِضُونَ إِلَيْكَ رُءُوسَهُمْ
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هُوَ ۖ قُلْ عَسَىٰ أَن يَكُونَ قَرِيبًا
Aw khalqan mimma yakburu fee sudoorikumfasayaqooloona man yuAAeeduna quli
allathee fatarakumawwala marratin fasayunghidoona ilayka ruoosahumwayaqooloona
mata huwa qul AAasa an yakoona qareeba
Swahili
Au umbo lolote mnalo liona kubwa katika vifua vyenu. Watasema: Nani atakaye
turudisha tena? Sema: Yule yule aliye kuumbeni mara ya kwanza! Watakutikisia
vichwa vyao, na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!
|
Ayah 17:52 الأية
يَوْمَ يَدْعُوكُمْ فَتَسْتَجِيبُونَ بِحَمْدِهِ وَتَظُنُّونَ إِن لَّبِثْتُمْ
إِلَّا قَلِيلًا
Yawma yadAAookum fatastajeeboona bihamdihiwatathunnoona in labithtum illa
qaleela
Swahili
Siku atakapo kuiteni, na nyinyi mkamuitikia kwa kumshukuru, na mkadhani kuwa
hamkukaa ila muda mdogo tu.
|
Ayah 17:53 الأية
وَقُل لِّعِبَادِي يَقُولُوا الَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ۚ إِنَّ الشَّيْطَانَ يَنزَغُ
بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّ الشَّيْطَانَ كَانَ لِلْإِنسَانِ عَدُوًّا مُّبِينًا
Waqul liAAibadee yaqooloo allateehiya ahsanu inna ashshaytana yanzaghubaynahum
inna ashshaytana kana lil-insaniAAaduwwan mubeena
Swahili
Waambie waja wangu waseme maneno mazuri, maana Shet'ani huchochea ugomvi baina
yao. Hakika Shet'ani ni adui aliye dhaahiri kwa mwanaadamu.
|
Ayah 17:54 الأية
رَّبُّكُمْ أَعْلَمُ بِكُمْ ۖ إِن يَشَأْ يَرْحَمْكُمْ أَوْ إِن يَشَأْ
يُعَذِّبْكُمْ ۚ وَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ وَكِيلًا
Rabbukum aAAlamu bikum in yasha/ yarhamkumaw in yasha/ yuAAaththibkum wama
arsalnakaAAalayhim wakeela
Swahili
Mola wenu Mlezi anakujueni vilivyo. Akipenda atakurehemuni, na akipenda
atakuadhibuni. Na hatukukutuma ili uwe mlinzi juu yao.
|
Ayah 17:55 الأية
وَرَبُّكَ أَعْلَمُ بِمَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَلَقَدْ فَضَّلْنَا
بَعْضَ النَّبِيِّينَ عَلَىٰ بَعْضٍ ۖ وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا
Warabbuka aAAlamu biman fee assamawatiwal-ardi walaqad faddalna
baAAdaannabiyyeena AAala baAAdin waataynadawooda zaboora
Swahili
Na Mola wako Mlezi anawajua vilivyo waliomo mbinguni na katika ardhi. Na hakika
tumewafadhilisha baadhi ya Manabii kuliko wengine; na Daudi tulimpa Zaburi.
|
Ayah 17:56 الأية
قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُم مِّن دُونِهِ فَلَا يَمْلِكُونَ كَشْفَ الضُّرِّ
عَنكُمْ وَلَا تَحْوِيلًا
Quli odAAu allatheena zaAAamtum mindoonihi fala yamlikoona kashfa addurriAAankum
wala tahweela
Swahili
Sema: Waombeni hao mnao wadaia badala yake Yeye. Hawawezi kukuondoleeni madhara,
wala kuyaweka pengine.
|
Ayah 17:57 الأية
أُولَٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ
أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ ۚ إِنَّ عَذَابَ
رَبِّكَ كَانَ مَحْذُورًا
Ola-ika allatheena yadAAoonayabtaghoona ila rabbihimu alwaseelata ayyuhum
aqrabuwayarjoona rahmatahu wayakhafoona AAathabahuinna AAathaba rabbika kana
mahthoora
Swahili
Hao wanao waomba, wao wenyewe wanatafuta njia ya kwendea kwa Mola wao Mlezi -
hata miongoni mwao walio karibu mno - na wanataraji rehema zake na wanaikhofu
adhabu yake. Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi yafaa kutahadhari nayo.
|
Ayah 17:58 الأية
وَإِن مِّن قَرْيَةٍ إِلَّا نَحْنُ مُهْلِكُوهَا قَبْلَ يَوْمِ الْقِيَامَةِ أَوْ
مُعَذِّبُوهَا عَذَابًا شَدِيدًا ۚ كَانَ ذَٰلِكَ فِي الْكِتَابِ مَسْطُورًا
Wa-in min qaryatin illa nahnumuhlikooha qabla yawmi alqiyamati aw
muAAaththiboohaAAathaban shadeedan kana thalika fee alkitabimastoora
Swahili
Na hapana mji wowote ila Sisi tutauteketeza kabla ya Siku ya Kiyama, au tutaupa
adhabu kali. Haya yamekwisha andikwa katika Kitabu.
|
Ayah 17:59 الأية
وَمَا مَنَعَنَا أَن نُّرْسِلَ بِالْآيَاتِ إِلَّا أَن كَذَّبَ بِهَا الْأَوَّلُونَ
ۚ وَآتَيْنَا ثَمُودَ النَّاقَةَ مُبْصِرَةً فَظَلَمُوا بِهَا ۚ وَمَا نُرْسِلُ
بِالْآيَاتِ إِلَّا تَخْوِيفًا
Wama manaAAana an nursila bil-ayatiilla an kaththaba biha al-awwaloona
waataynathamooda annaqata mubsiratan fathalamoobiha wama nursilu bil-ayatiilla
takhweefa
Swahili
Na hapana kinacho tuzuia kupeleka miujiza ila ni kuwa watu wa zamani
waliikanusha. Na tuliwapa Wathamudi ngamia jike kuwa ni Ishara iliyo dhaahiri,
lakini walidhulumu kwaye. Nasi hatupeleki Ishara ila kwa ajili ya kuhadharisha.
|
Ayah 17:60 الأية
وَإِذْ قُلْنَا لَكَ إِنَّ رَبَّكَ أَحَاطَ بِالنَّاسِ ۚ وَمَا جَعَلْنَا
الرُّؤْيَا الَّتِي أَرَيْنَاكَ إِلَّا فِتْنَةً لِّلنَّاسِ وَالشَّجَرَةَ
الْمَلْعُونَةَ فِي الْقُرْآنِ ۚ وَنُخَوِّفُهُمْ فَمَا يَزِيدُهُمْ إِلَّا
طُغْيَانًا كَبِيرًا
Wa-ith qulna laka inna rabbakaahata binnasi wama jaAAalnaarru/ya allatee
araynaka illafitnatan linnasi washshajarataalmalAAoonata fee alqur-ani
wanukhawwifuhum famayazeeduhum illa tughyanan kabeera
Swahili
Na tulipo kwambia: Hakika Mola wako Mlezi amekwisha wazunguka hao watu. Na
hatukuifanya ndoto tulio kuonyesha ila ni kuwajaribu watu, na mti ulio laaniwa
katika Qur'ani. Na tunawahadharisha, lakini haiwazidishii ila uasi mkubwa.
|
Ayah 17:61 الأية
وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ
قَالَ أَأَسْجُدُ لِمَنْ خَلَقْتَ طِينًا
Wa-ith qulna lilmala-ikatiosjudoo li-adama fasajadoo illa ibleesa qalaaasjudu
liman khalaqta teena
Swahili
Na pale tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam. Wakamsujudia isipo kuwa Iblisi.
Akasema: Je! Nimsujudie uliye muumba kwa udongo?
|
Ayah 17:62 الأية
قَالَ أَرَأَيْتَكَ هَٰذَا الَّذِي كَرَّمْتَ عَلَيَّ لَئِنْ أَخَّرْتَنِ إِلَىٰ
يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَأَحْتَنِكَنَّ ذُرِّيَّتَهُ إِلَّا قَلِيلًا
Qala araaytaka hatha allatheekarramta AAalayya la-in akhkhartani ila yawmi
alqiyamatilaahtanikanna thurriyyatahu illa qaleela
Swahili
Akasema: Hebu nambie khabari ya huyu uliye mtukuza juu yangu. Ukiniakhirisha
mpaka Siku ya Kiyama, hapana shaka nitawaangamiza dhuriya zake wasipo kuwa
wachache tu.
|
Ayah 17:63 الأية
قَالَ اذْهَبْ فَمَن تَبِعَكَ مِنْهُمْ فَإِنَّ جَهَنَّمَ جَزَاؤُكُمْ جَزَاءً
مَّوْفُورًا
Qala ithhab faman tabiAAakaminhum fa-inna jahannama jazaokum jazaan mawfoora
Swahili
Akasema Mwenyezi Mungu: Ondokelea mbali! Atakaye kufuata katika wao, basi
Jahannamu itakuwa ndiyo malipo yenu, malipo ya kutimia.
|
Ayah 17:64 الأية
وَاسْتَفْزِزْ مَنِ اسْتَطَعْتَ مِنْهُم بِصَوْتِكَ وَأَجْلِبْ عَلَيْهِم
بِخَيْلِكَ وَرَجِلِكَ وَشَارِكْهُمْ فِي الْأَمْوَالِ وَالْأَوْلَادِ وَعِدْهُمْ ۚ
وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلَّا غُرُورًا
Wastafziz mani istataAAtaminhum bisawtika waajlib AAalayhim bikhaylika
warajlikawasharik-hum fee al-amwali wal-awladiwaAAidhum wama yaAAiduhumu
ashshaytanu illaghuroora
Swahili
Na wachochee uwawezao katika wao kwa sauti yako, na wakusanyie jeshi lako la
wapandao farasi na waendao kwa miguu. Na shirikiana nao katika mali na wana, na
waahidi. Na Shet'ani hawapi ahadi ila ya udanganyifu.
|
Ayah 17:65 الأية
إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ ۚ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ وَكِيلًا
Inna AAibadee laysa laka AAalayhimsultanun wakafa birabbika wakeela
Swahili
Hakika wewe huna mamlaka juu ya waja wangu. Na Mola wako Mlezi anatosha kuwa ni
wa kutegemewa.
|
Ayah 17:66 الأية
رَّبُّكُمُ الَّذِي يُزْجِي لَكُمُ الْفُلْكَ فِي الْبَحْرِ لِتَبْتَغُوا مِن
فَضْلِهِ ۚ إِنَّهُ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا
Rabbukumu allathee yuzjee lakumualfulka fee albahri litabtaghoo min fadlihi
innahukana bikum raheema
Swahili
Mola wenu Mlezi ndiye anaye kuendesheeni marikebu katika bahari ili mtafute
katika fadhila zake. Hakika Yeye ni Mwenye kukurehemuni nyinyi.
|
Ayah 17:67 الأية
وَإِذَا مَسَّكُمُ الضُّرُّ فِي الْبَحْرِ ضَلَّ مَن تَدْعُونَ إِلَّا إِيَّاهُ ۖ
فَلَمَّا نَجَّاكُمْ إِلَى الْبَرِّ أَعْرَضْتُمْ ۚ وَكَانَ الْإِنسَانُ كَفُورًا
Wa-itha massakumu addurrufee albahri dalla man tadAAoona illa iyyahufalamma
najjakum ila albarri aAAradtumwakana al-insanu kafoora
Swahili
Na inapo kufikieni taabu katika bahari, hao mnao waomba wanapotea, isipo kuwa
Yeye tu. Na anapo kuvueni mkafika nchi kavu, mnageuka. Ama mwanaadamu ni mwingi
wa kukanusha.
|
Ayah 17:68 الأية
أَفَأَمِنتُمْ أَن يَخْسِفَ بِكُمْ جَانِبَ الْبَرِّ أَوْ يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ
حَاصِبًا ثُمَّ لَا تَجِدُوا لَكُمْ وَكِيلًا
Afaamintum an yakhsifa bikum janibaalbarri aw yursila AAalaykum hasiban thumma
latajidoo lakum wakeela
Swahili
Je! Mmeaminisha ya kuwa hatakudidimizeni upande wowote katika nchi kavu, au
kwamba hatakuleteeni tufani la kokoto? Kisha msipate wa kumtegemea.
|
Ayah 17:69 الأية
أَمْ أَمِنتُمْ أَن يُعِيدَكُمْ فِيهِ تَارَةً أُخْرَىٰ فَيُرْسِلَ عَلَيْكُمْ
قَاصِفًا مِّنَ الرِّيحِ فَيُغْرِقَكُم بِمَا كَفَرْتُمْ ۙ ثُمَّ لَا تَجِدُوا
لَكُمْ عَلَيْنَا بِهِ تَبِيعًا
Am amintum an yuAAeedakum feehi taratanokhra fayursila AAalaykum qasifan mina
arreehifayughriqakum bima kafartum thumma la tajidoo lakumAAalayna bihi tabeeAAa
Swahili
Au mmeaminisha ya kuwa hatakurudisheni humo mara nyengine na kukupelekeeni
kimbunga cha upepo akakuzamisheni kwa mlivyo kufuru, na kisha msipate wa
kukunusuruni nasi.
|
Ayah 17:70 الأية
وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِي آدَمَ وَحَمَلْنَاهُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ
وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَىٰ كَثِيرٍ مِّمَّنْ
خَلَقْنَا تَفْضِيلًا
Walaqad karramna banee adamawahamalnahum fee albarri walbahriwarazaqnahum mina
attayyibati wafaddalnahumAAala katheerin mimman khalaqna tafdeela
Swahili
Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini,
na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko
wengi miongoni mwa tulio waumba.
|
Ayah 17:71 الأية
يَوْمَ نَدْعُو كُلَّ أُنَاسٍ بِإِمَامِهِمْ ۖ فَمَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ
بِيَمِينِهِ فَأُولَٰئِكَ يَقْرَءُونَ كِتَابَهُمْ وَلَا يُظْلَمُونَ فَتِيلًا
Yawma nadAAoo kulla onasin bi-imamihimfaman ootiya kitabahu biyameenihi
faola-ikayaqraoona kitabahum wala yuthlamoonafateela
Swahili
Siku tutapo waita kila kikundi cha watu kwa mujibu wa wakifuatacho - basi
atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, basi hao watasoma kitabu chao
wala hawatadhulumiwa hata chembe.
|
Ayah 17:72 الأية
وَمَن كَانَ فِي هَٰذِهِ أَعْمَىٰ فَهُوَ فِي الْآخِرَةِ أَعْمَىٰ وَأَضَلُّ
سَبِيلًا
Waman kana fee hathihi aAAmafahuwa fee al-akhirati aAAma waadallu sabeela
Swahili
Na aliye kuwa hapa kipofu, basi atakuwa kipofu Akhera, na atakuwa aliye ipotea
zaidi Njia.
|
Ayah 17:73 الأية
وَإِن كَادُوا لَيَفْتِنُونَكَ عَنِ الَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ لِتَفْتَرِيَ
عَلَيْنَا غَيْرَهُ ۖ وَإِذًا لَّاتَّخَذُوكَ خَلِيلًا
Wa-in kadoo layaftinoonaka AAani allatheeawhayna ilayka litaftariya AAalayna
ghayrahuwa-ithan lattakhathooka khaleela
Swahili
Na hakika walikaribia kukushawishi uache tuliyo kufunulia ili utuzulie
mengineyo. Na hapo ndio wangeli kufanya rafiki.
|
Ayah 17:74 الأية
وَلَوْلَا أَن ثَبَّتْنَاكَ لَقَدْ كِدتَّ تَرْكَنُ إِلَيْهِمْ شَيْئًا قَلِيلًا
Walawla an thabbatnaka laqadkidta tarkanu ilayhim shay-an qaleela
Swahili
Na lau kuwa hatukukuweka imara ungeli karibia kuwaelekea kidogo.
|
Ayah 17:75 الأية
إِذًا لَّأَذَقْنَاكَ ضِعْفَ الْحَيَاةِ وَضِعْفَ الْمَمَاتِ ثُمَّ لَا تَجِدُ لَكَ
عَلَيْنَا نَصِيرًا
Ithan laathaqnaka diAAfaalhayati wadiAAfa almamati thumma latajidu laka AAalayna
naseera
Swahili
Hapo basi bila ya shaka tungeli kuonjesha adhabu mardufu ya uhai, na adhabu
mardufu ya kifo. Kisha usinge pata mtu wa kukunusuru nasi.
|
Ayah 17:76 الأية
وَإِن كَادُوا لَيَسْتَفِزُّونَكَ مِنَ الْأَرْضِ لِيُخْرِجُوكَ مِنْهَا ۖ وَإِذًا
لَّا يَلْبَثُونَ خِلَافَكَ إِلَّا قَلِيلًا
Wa-in kadoo layastafizzoonaka minaal-ardi liyukhrijooka minha wa-ithan
layalbathoona khilafaka illa qaleela
Swahili
Na walitaka kukukera ili uitoke nchi. Na hapo wao wasingeli bakia humo ila kwa
muda mchache tu.
|
Ayah 17:77 الأية
سُنَّةَ مَن قَدْ أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ مِن رُّسُلِنَا ۖ وَلَا تَجِدُ لِسُنَّتِنَا
تَحْوِيلًا
Sunnata man qad arsalna qablaka minrusulina wala tajidu lisunnatina tahweela
Swahili
Huo ndio mwendo kwa Mitume tulio watuma kabla yako. Wala hupati mabadiliko
katika mwendo wetu.
|
Ayah 17:78 الأية
أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَىٰ غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ
الْفَجْرِ ۖ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا
Aqimi assalatalidulooki ashshamsi ila ghasaqi allayli waqur-anaalfajri inna
qur-ana alfajri kana mashhooda
Swahili
Shika Sala jua linapo pinduka mpaka giza la usiku, na Qur'ani ya al fajiri.
Hakika Qur'ani ya alfajiri inashuhudiwa daima.
|
Ayah 17:79 الأية
وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ
مَقَامًا مَّحْمُودًا
Wamina allayli fatahajjad bihi nafilatanlaka AAasa an yabAAathaka rabbuka
maqaman mahmooda
Swahili
Na amka usiku kwa ibada; ni ziada ya sunna khasa kwako wewe. Huenda Mola wako
Mlezi akakunyanyua cheo kinacho sifika.
|
Ayah 17:80 الأية
وَقُل رَّبِّ أَدْخِلْنِي مُدْخَلَ صِدْقٍ وَأَخْرِجْنِي مُخْرَجَ صِدْقٍ وَاجْعَل
لِّي مِن لَّدُنكَ سُلْطَانًا نَّصِيرًا
Waqul rabbi adkhilnee mudkhala sidqinwaakhrijnee mukhraja sidqin wajAAal lee
minladunka sultanan naseera
Swahili
Na sema: Mola wangu Mlezi! Niingize muingizo mwema, na unitoe kutoka kwema. Na
unipe nguvu zinazo toka kwako zinisaidie.
|
Ayah 17:81 الأية
وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ ۚ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا
Waqul jaa alhaqqu wazahaqa albatiluinna albatila kana zahooqa
Swahili
Na sema: Kweli imefika, na uwongo umetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke!
|
Ayah 17:82 الأية
وَنُنَزِّلُ مِنَ الْقُرْآنِ مَا هُوَ شِفَاءٌ وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ ۙ وَلَا
يَزِيدُ الظَّالِمِينَ إِلَّا خَسَارًا
Wanunazzilu mina alqur-ani mahuwa shifaon warahmatun lilmu/mineena walayazeedu
aththalimeena illakhasara
Swahili
Na tunateremsha katika Qur'ani yaliyo ni matibabu na rehema kwa Waumini. Wala
hayawazidishii madhaalimu ila khasara.
|
Ayah 17:83 الأية
وَإِذَا أَنْعَمْنَا عَلَى الْإِنسَانِ أَعْرَضَ وَنَأَىٰ بِجَانِبِهِ ۖ وَإِذَا
مَسَّهُ الشَّرُّ كَانَ يَئُوسًا
Wa-itha anAAamna AAalaal-insani aAArada wanaa bijanibihiwa-itha massahu
ashsharru kana yaoosa
Swahili
Na mwanaadamu tunapo mneemesha hugeuka na kujitenga kando. Na inapo mgusa shari
hukata tamaa.
|
Ayah 17:84 الأية
قُلْ كُلٌّ يَعْمَلُ عَلَىٰ شَاكِلَتِهِ فَرَبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَنْ هُوَ أَهْدَىٰ
سَبِيلًا
Qul kullun yaAAmalu AAala shakilatihifarabbukum aAAlamu biman huwa ahda sabeela
Swahili
Sema: Kila mmoja anafanya kwa namna yake. Na Mola wenu Mlezi anajua aliye ongoka
katika njia.
|
Ayah 17:85 الأية
وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الرُّوحِ ۖ قُلِ الرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّي وَمَا أُوتِيتُم
مِّنَ الْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا
Wayas-aloonaka AAani arroohiquli arroohu min amri rabbee wama ooteetummina
alAAilmi illa qaleela
Swahili
Na wanakuuliza khabari za Roho. Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi.
Nanyi hamkupewa katika ilimu ila kidogo tu.
|
Ayah 17:86 الأية
وَلَئِن شِئْنَا لَنَذْهَبَنَّ بِالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ ثُمَّ لَا تَجِدُ
لَكَ بِهِ عَلَيْنَا وَكِيلًا
Wala-in shi/na lanathhabannabillathee awhayna ilayka thumma latajidu laka bihi
AAalayna wakeela
Swahili
Na tungeli penda tungeli yaondoa tuliyo kufunulia. Kisha usingeli pata
mwakilishi wa kukupigania kwetu kwa haya.
|
Ayah 17:87 الأية
إِلَّا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ ۚ إِنَّ فَضْلَهُ كَانَ عَلَيْكَ كَبِيرًا
Illa rahmatan min rabbika innafadlahu kana AAalayka kabeera
Swahili
Isipo kuwa iwe rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika fadhila yake kwako ni
kubwa.
|
Ayah 17:88 الأية
قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَىٰ أَن يَأْتُوا بِمِثْلِ هَٰذَا
الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا
Qul la-ini ijtamaAAati al-insu waljinnuAAala an ya/too bimithli hatha alqur-ani
laya/toona bimithlihi walaw kana baAAduhum libaAAdinthaheera
Swahili
Sema: Wangeli kusanyika watu na majini ili walete mfano wa hii Qur'ani basi
hawaleti mfano wake, hata wakisaidiana wao kwa wao.
|
Ayah 17:89 الأية
وَلَقَدْ صَرَّفْنَا لِلنَّاسِ فِي هَٰذَا الْقُرْآنِ مِن كُلِّ مَثَلٍ فَأَبَىٰ
أَكْثَرُ النَّاسِ إِلَّا كُفُورًا
Walaqad sarrafna linnasifee hatha alqur-ani min kulli mathalin faabaaktharu
annasi illa kufoora
Swahili
Na hakika tumewaeleza watu katika hii Qur'ani kwa kila mfano. Lakini watu wengi
wanakataa isipo kuwa kukanusha tu.
|
Ayah 17:90 الأية
وَقَالُوا لَن نُّؤْمِنَ لَكَ حَتَّىٰ تَفْجُرَ لَنَا مِنَ الْأَرْضِ يَنبُوعًا
Waqaloo lan nu/mina laka hattatafjura lana mina al-ardi yanbooAAa
Swahili
Na walisema: Hatutakuamini mpaka ututimbulie chemchem katika ardhi hii.
|
Ayah 17:91 الأية
أَوْ تَكُونَ لَكَ جَنَّةٌ مِّن نَّخِيلٍ وَعِنَبٍ فَتُفَجِّرَ الْأَنْهَارَ
خِلَالَهَا تَفْجِيرًا
Aw takoona laka jannatun min nakheelinwaAAinabin fatufajjira al-anhara
khilalahatafjeera
Swahili
Au uwe na kitalu cha mitende na mizabibu, na utupitishie mito kati yake
ikimiminika.
|
Ayah 17:92 الأية
أَوْ تُسْقِطَ السَّمَاءَ كَمَا زَعَمْتَ عَلَيْنَا كِسَفًا أَوْ تَأْتِيَ
بِاللهِ وَالْمَلَائِكَةِ قَبِيلًا
Aw tusqita assamaa kamazaAAamta AAalayna kisafan aw ta/tiya billahiwalmala-ikati
qabeela
Swahili
Au utuangushie mbingu vipande vipande kama ulivyo dai; au utuletee Mwenyezi
Mungu na Malaika uso kwa uso.
|
Ayah 17:93 الأية
أَوْ يَكُونَ لَكَ بَيْتٌ مِّن زُخْرُفٍ أَوْ تَرْقَىٰ فِي السَّمَاءِ وَلَن
نُّؤْمِنَ لِرُقِيِّكَ حَتَّىٰ تُنَزِّلَ عَلَيْنَا كِتَابًا نَّقْرَؤُهُ ۗ قُلْ
سُبْحَانَ رَبِّي هَلْ كُنتُ إِلَّا بَشَرًا رَّسُولًا
Aw yakoona laka baytun min zukhrufin aw tarqafee assama-i walan nu/mina
liruqiyyika hattatunazzila AAalayna kitaban naqraohu qul subhanarabbee hal kuntu
illa basharan rasoola
Swahili
Au uwe na nyumba ya dhahabu, au upae mbinguni. Wala hatutaamini kupaa kwako
mpaka ututeremshie kitabu tukisome. Sema: Subhana Rabbi, Ametakasika Mola wangu
Mlezi! Kwani mimi ni nani isipo kuwa ni mwanaadamu na Mtume?
|
Ayah 17:94 الأية
وَمَا مَنَعَ النَّاسَ أَن يُؤْمِنُوا إِذْ جَاءَهُمُ الْهُدَىٰ إِلَّا أَن قَالُوا
أَبَعَثَ اللهُ بَشَرًا رَّسُولًا
Wama manaAAa annasa anyu/minoo ith jaahumu alhuda illa an qalooabaAAatha Allahu
basharan rasoola
Swahili
Na nini kilicho wazuilia watu kuamini ulipo wajia uwongofu isipo kuwa walisema:
Je! Mwenyezi Mungu humtuma mwanaadamu kuwa ni Mtume?
|
Ayah 17:95 الأية
قُل لَّوْ كَانَ فِي الْأَرْضِ مَلَائِكَةٌ يَمْشُونَ مُطْمَئِنِّينَ لَنَزَّلْنَا
عَلَيْهِم مِّنَ السَّمَاءِ مَلَكًا رَّسُولًا
Qul law kana fee al-ardi mala-ikatunyamshoona mutma-inneena lanazzalna AAalayhim
mina assama-imalakan rasoola
Swahili
Sema: Ingeli kuwa duniani wapo Malaika wanatembea kwa utulivu wao, basi bila ya
shaka tungeli wateremshia Malaika kuwa ni Mtume wao.
|
Ayah 17:96 الأية
قُلْ كَفَىٰ بِاللهِ شَهِيدًا بَيْنِي وَبَيْنَكُمْ ۚ إِنَّهُ كَانَ بِعِبَادِهِ
خَبِيرًا بَصِيرًا
Qul kafa billahishaheedan baynee wabaynakum innahu kana biAAibadihikhabeeran
baseera
Swahili
Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Shahidi baina yangu na nyinyi. Hakika Yeye
anawajua vyema waja wake na anawaona.
|
Ayah 17:97 الأية
وَمَن يَهْدِ اللهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِ ۖ وَمَن يُضْلِلْ فَلَن تَجِدَ لَهُمْ
أَوْلِيَاءَ مِن دُونِهِ ۖ وَنَحْشُرُهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ
عُمْيًا وَبُكْمًا وَصُمًّا ۖ مَّأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ كُلَّمَا خَبَتْ
زِدْنَاهُمْ سَعِيرًا
Waman yahdi Allahu fahuwa almuhtadiwaman yudlil falan tajida lahum awliyaa min
doonihiwanahshuruhum yawma alqiyamati AAalawujoohihim AAumyan wabukman wasumman
ma/wahumjahannamu kullama khabat zidnahum saAAeera
Swahili
Na anaye mhidi Mwenyezi Mungu basi huyo ndiye aliye hidika. Na anaye wapotoa
basi huto wapatia walinzi badala yake. Na tutawakusanya Siku ya Kiyama hali
wakikokotwa juu ya nyuso zao, nao ni vipofu na mabubu na viziwi. Na makaazi yao
ni Jahannamu. Kila moto ukifanya kusinzia tutazidi kuuchochea uwake kwa nguvu.
|
Ayah 17:98 الأية
ذَٰلِكَ جَزَاؤُهُم بِأَنَّهُمْ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا وَقَالُوا أَإِذَا كُنَّا
عِظَامًا وَرُفَاتًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ خَلْقًا جَدِيدًا
Thalika jazaohum bi-annahumkafaroo bi-ayatina waqaloo a-ithakunna AAithaman
warufatana-inna lamabAAoothoona khalqan jadeeda
Swahili
Hayo ni malipo yao kwa sababu walizikataa ishara zetu, na wakasema: Hivyo
tukisha kuwa mifupa na mapande yaliyo vurugika tutafufuliwa kwa umbo jipya?
|
Ayah 17:99 الأية
أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللهَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ قَادِرٌ
عَلَىٰ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُمْ وَجَعَلَ لَهُمْ أَجَلًا لَّا رَيْبَ فِيهِ فَأَبَى
الظَّالِمُونَ إِلَّا كُفُورًا
Awa lam yaraw anna Allaha allatheekhalaqa assamawati wal-ardaqadirun AAala an
yakhluqa mithlahum wajaAAala lahumajalan la rayba feehi faaba aththalimoonailla
kufoora
Swahili
Kwani hawakuona ya kwamba Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi ni Mwenye
kuweza kuumba mfano wao? Na Yeye amewawekea muda usio na shaka yoyote. Lakini
madhaalimu hawataki ila ukafiri.
|
Ayah 17:100 الأية
قُل لَّوْ أَنتُمْ تَمْلِكُونَ خَزَائِنَ رَحْمَةِ رَبِّي إِذًا لَّأَمْسَكْتُمْ
خَشْيَةَ الْإِنفَاقِ ۚ وَكَانَ الْإِنسَانُ قَتُورًا
Qul law antum tamlikoona khaza-inarahmati rabbee ithan laamsaktum khashyata
al-infaqiwakana al-insanu qatoora
Swahili
Sema: Lau kuwa nyinyi mnazimiliki khazina za rehema za Mola wangu Mlezi, basi
hapana shaka mngeli zuia kuzitumia kwa ajili ya kukhofu. Na mwanaadamu tangu
hapo tabia yake ni mchoyo!
|
Ayah 17:101 الأية
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَىٰ تِسْعَ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ ۖ فَاسْأَلْ بَنِي
إِسْرَائِيلَ إِذْ جَاءَهُمْ فَقَالَ لَهُ فِرْعَوْنُ إِنِّي لَأَظُنُّكَ يَا
مُوسَىٰ مَسْحُورًا
Walaqad atayna moosatisAAa ayatin bayyinatin fas-albanee isra-eela ith jaahum
faqalalahu firAAawnu innee laathunnuka ya moosamashoora
Swahili
Na kwa yakini tulimpa Musa ishara tisa zilizo wazi. Waulize Wana wa Israili
alipo wafikia, na Firauni akawaambia: Hakika mimi nakuona wewe Musa umerogwa!
|
Ayah 17:102 الأية
قَالَ لَقَدْ عَلِمْتَ مَا أَنزَلَ هَٰؤُلَاءِ إِلَّا رَبُّ السَّمَاوَاتِ
وَالْأَرْضِ بَصَائِرَ وَإِنِّي لَأَظُنُّكَ يَا فِرْعَوْنُ مَثْبُورًا
Qala laqad AAalimta ma anzalahaola-i illa rabbu assamawatiwal-ardi basa-ira
wa-innee laathunnukaya firAAawnu mathboora
Swahili
Musa akasema: Wewe unajua bila ya shaka kuwa haya hakuyateremsha ila Mola Mlezi
wa mbingu na ardhi ili kuwa ni ushahidi wa kuonekana. Na hakika mimi bila ya
shaka nakuona wewe, Firauni, kuwa umekwisha angamia.
|
Ayah 17:103 الأية
فَأَرَادَ أَن يَسْتَفِزَّهُم مِّنَ الْأَرْضِ فَأَغْرَقْنَاهُ وَمَن مَّعَهُ
جَمِيعًا
Faarada an yastafizzahum mina al-ardifaaghraqnahu waman maAAahu jameeAAa
Swahili
Basi Firauni akataka kuwafukuza katika nchi. Kwa hivyo tukamzamisha yeye na
walio kuwa pamoja naye wote.
|
Ayah 17:104 الأية
وَقُلْنَا مِن بَعْدِهِ لِبَنِي إِسْرَائِيلَ اسْكُنُوا الْأَرْضَ فَإِذَا جَاءَ
وَعْدُ الْآخِرَةِ جِئْنَا بِكُمْ لَفِيفًا
Waqulna min baAAdihi libanee isra-eelaoskunoo al-arda fa-itha jaa waAAdu
al-akhiratiji/na bikum lafeefa
Swahili
Na tukawaambia baada yake Wana wa Israili: Kaeni katika nchi. Itapo kuja ahadi
ya Akhera tutakuleteni nyote pamoja.
|
Ayah 17:105 الأية
وَبِالْحَقِّ أَنزَلْنَاهُ وَبِالْحَقِّ نَزَلَ ۗ وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا
مُبَشِّرًا وَنَذِيرًا
Wabilhaqqi anzalnahuwabilhaqqi nazala wama arsalnaka illamubashshiran wanatheera
Swahili
Na kwa Haki tumeiteremsha, na kwa Haki imeteremka. Na hatukukutuma ila uwe
mbashiri na mwonyaji.
|
Ayah 17:106 الأية
وَقُرْآنًا فَرَقْنَاهُ لِتَقْرَأَهُ عَلَى النَّاسِ عَلَىٰ مُكْثٍ وَنَزَّلْنَاهُ
تَنزِيلًا
Waqur-anan faraqnahulitaqraahu AAala annasi AAalamukthin wanazzalnahu tanzeela
Swahili
Na Qur'ani tumeigawanya sehemu mbali mbali ili uwasomee watu kwa kituo, na
tumeiteremsha kidogo kidogo.
|
Ayah 17:107 الأية
قُلْ آمِنُوا بِهِ أَوْ لَا تُؤْمِنُوا ۚ إِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ مِن
قَبْلِهِ إِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ يَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ سُجَّدًا
Qul aminoo bihi aw latu/minoo inna allatheena ootoo alAAilma min qablihi
ithayutla AAalayhim yakhirroona lil-athqanisujjada
Swahili
Sema: Iaminini au msiiamini. Hakika wale walio pewa ilimu kabla yake, wanapo
somewa hii, huanguka kifudifudi wanasujudu.
|
Ayah 17:108 الأية
وَيَقُولُونَ سُبْحَانَ رَبِّنَا إِن كَانَ وَعْدُ رَبِّنَا لَمَفْعُولًا
Wayaqooloona subhana rabbinain kana waAAdu rabbina lamafAAoola
Swahili
Na wanasema: Subhana Rabbina, Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika ahadi ya Mola
wetu Mlezi lazima itimizwe!
|
Ayah 17:109 الأية
وَيَخِرُّونَ لِلْأَذْقَانِ يَبْكُونَ وَيَزِيدُهُمْ خُشُوعًا ۩
Wayakhirroona lil-athqaniyabkoona wayazeeduhum khushooAAa
Swahili
Na huanguka kifudifudi na huku wanalia, na inawazidisha unyenyekevu.
|
Ayah 17:110 الأية
قُلِ ادْعُوا اللهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ
الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ وَلَا تَجْهَرْ بِصَلَاتِكَ وَلَا تُخَافِتْ بِهَا
وَابْتَغِ بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا
Quli odAAoo Allaha awi odAAoo arrahmanaayyan ma tadAAoo falahu al-asmao
alhusnawala tajhar bisalatika wala tukhafitbiha wabtaghi bayna thalika sabeela
Swahili
Sema: Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au mwombeni Rahman (Mwingi wa Rehema),
kwa jina lolote mnalo mwita. Kwani Yeye ana majina mazuri mazuri. Wala
usitangaze Sala yako kwa sauti kubwa, wala usiifiche kwa sauti ndogo, bali shika
njia ya kati na kati ya hizo.
|
Ayah 17:111 الأية
وَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي لَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ يَكُن لَّهُ
شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَلَمْ يَكُن لَّهُ وَلِيٌّ مِّنَ الذُّلِّ ۖ وَكَبِّرْهُ
تَكْبِيرًا
Waquli alhamdu lillahi allatheelam yattakhith waladan walam yakun lahu shareekun
feealmulki walam yakun lahu waliyyun mina aththulliwakabbirhu takbeera
Swahili
Na sema: Alhamdulillah, Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye hana mwana, wala
hana mshirika katika ufalme, wala hana rafiki wa kumsaidia kwa sababu ya udhaifu
wake. Na mtukuze kwa utukufu mkubwa.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|