1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
كهيعص
Kaf-ha-ya-AAayn-sad
Swahili
Kaf Ha Ya A'yn S'ad
|
Ayah 19:2 الأية
ذِكْرُ رَحْمَتِ رَبِّكَ عَبْدَهُ زَكَرِيَّا
Thikru rahmati rabbika AAabdahuzakariyya
Swahili
Huu ni Ukumbusho wa rehema ya Mola wako Mlezi kwa mja wake, Zakariya.
|
Ayah 19:3 الأية
إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ نِدَاءً خَفِيًّا
Ith nada rabbahu nidaankhafiyya
Swahili
Alipo mwita Mola wake Mlezi kwa siri.
|
Ayah 19:4 الأية
قَالَ رَبِّ إِنِّي وَهَنَ الْعَظْمُ مِنِّي وَاشْتَعَلَ الرَّأْسُ شَيْبًا وَلَمْ
أَكُن بِدُعَائِكَ رَبِّ شَقِيًّا
Qala rabbi innee wahana alAAathmuminnee washtaAAala arra/su shayban walam
akunbiduAAa-ika rabbi shaqiyya
Swahili
Akasema: Mola wangu Mlezi! Mafupa yangu yamedhoofika, na kichwa kinameremeta kwa
mvi; wala, Mola wangu Mlezi, sikuwa mwenye bahati mbaya kwa kukuomba Wewe.
|
Ayah 19:5 الأية
وَإِنِّي خِفْتُ الْمَوَالِيَ مِن وَرَائِي وَكَانَتِ امْرَأَتِي عَاقِرًا فَهَبْ
لِي مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا
Wa-innee khiftu almawaliya min wara-eewakanati imraatee AAaqiran fahab lee min
ladunkawaliyya
Swahili
Na hakika mimi nawakhofia jamaa zangu baada yangu. Na mke wangu ni tasa. Basi
nipe mrithi kutoka kwako.
|
Ayah 19:6 الأية
يَرِثُنِي وَيَرِثُ مِنْ آلِ يَعْقُوبَ ۖ وَاجْعَلْهُ رَبِّ رَضِيًّا
Yarithunee wayarithu min ali yaAAqoobawajAAalhu rabbi radiyya
Swahili
Atakaye nirithi mimi na awarithi ukoo wa Yaaqub. Ewe Mola wangu Mlezi! Na
umjaalie awe mwenye kuridhisha.
|
Ayah 19:7 الأية
يَا زَكَرِيَّا إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ اسْمُهُ يَحْيَىٰ لَمْ نَجْعَل لَّهُ
مِن قَبْلُ سَمِيًّا
Ya zakariyya innanubashshiruka bighulamin ismuhu yahya lamnajAAal lahu min qablu
samiyya
Swahili
(Akaambiwa): Ewe Zakariya! Hakika Sisi tunakubashiria mwana; jina lake ni Yahya.
Hatujapata kumpa jina hilo yeyote kabla yake.
|
Ayah 19:8 الأية
قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَكَانَتِ امْرَأَتِي عَاقِرًا وَقَدْ
بَلَغْتُ مِنَ الْكِبَرِ عِتِيًّا
Qala rabbi anna yakoonu leeghulamun wakanati imraatee AAaqiran waqadbalaghtu
mina alkibari AAitiyya
Swahili
Akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Vipi nitakuwa na mwana na hali mke wangu ni tasa,
na mimi nimesha fikia ukongwe katika uzee?
|
Ayah 19:9 الأية
قَالَ كَذَٰلِكَ قَالَ رَبُّكَ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ وَقَدْ خَلَقْتُكَ مِن قَبْلُ
وَلَمْ تَكُ شَيْئًا
Qala kathalika qalarabbuka huwa AAalayya hayyinun waqad khalaqtuka min qablu
walamtaku shay-a
Swahili
Akasema: Ndio hivyo hivyo amesema Mola wako Mlezi: Haya ni mepesi kwangu. Na
hakika Mimi nilikwisha kuumba wewe zamani na hali hukuwa kitu.
|
Ayah 19:10 الأية
قَالَ رَبِّ اجْعَل لِّي آيَةً ۚ قَالَ آيَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ النَّاسَ ثَلَاثَ
لَيَالٍ سَوِيًّا
Qala rabbi ijAAal lee ayatan qalaayatuka alla tukallima annasa thalathalayalin
sawiyya
Swahili
Akasema: Mola wangu Mlezi nijaalie Ishara. Akasema Ishara yako ni kuwa hutasema
na watu kwa masiku matatu, na hali ni mzima.
|
Ayah 19:11 الأية
فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِ مِنَ الْمِحْرَابِ فَأَوْحَىٰ إِلَيْهِمْ أَن سَبِّحُوا
بُكْرَةً وَعَشِيًّا
Fakharaja AAala qawmihi mina almihrabifaawha ilayhim an sabbihoo bukratan
waAAashiyya
Swahili
Basi akawatokea watu wake kutoka mihirabuni. Akawaashiria: Msabihini Mwenyezi
Mungu asubuhi na jioni.
|
Ayah 19:12 الأية
يَا يَحْيَىٰ خُذِ الْكِتَابَ بِقُوَّةٍ ۖ وَآتَيْنَاهُ الْحُكْمَ صَبِيًّا
Ya yahya khuthialkitaba biquwwatin waataynahu alhukmasabiyya
Swahili
Ewe Yahya! Kishike Kitabu kwa nguvu! Nasi tulimpa hikima angali mtoto.
|
Ayah 19:13 الأية
وَحَنَانًا مِّن لَّدُنَّا وَزَكَاةً ۖ وَكَانَ تَقِيًّا
Wahananan min ladunnawazakatan wakana taqiyya
Swahili
Na tukampa huruma itokayo kwetu, na utakaso, na akawa mchamungu.
|
Ayah 19:14 الأية
وَبَرًّا بِوَالِدَيْهِ وَلَمْ يَكُن جَبَّارًا عَصِيًّا
Wabarran biwalidayhi walam yakun jabbaranAAasiyya
Swahili
Na akawa mwema kwa wazazi wake, wala hakuwa jabari mua'si.
|
Ayah 19:15 الأية
وَسَلَامٌ عَلَيْهِ يَوْمَ وُلِدَ وَيَوْمَ يَمُوتُ وَيَوْمَ يُبْعَثُ حَيًّا
Wasalamun AAalayhi yawma wulidawayawma yamootu wayawma yubAAathu hayya
Swahili
Na amani iwe juu yake siku ya kuzaliwa, na siku ya kufa, na siku ya kufufuliwa.
|
Ayah 19:16 الأية
وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مَرْيَمَ إِذِ انتَبَذَتْ مِنْ أَهْلِهَا مَكَانًا
شَرْقِيًّا
Wathkur fee alkitabimaryama ithi intabathat min ahliha makanansharqiyya
Swahili
Na mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipo jitenga na jamaa zake mahali upande
wa mashariki;
|
Ayah 19:17 الأية
فَاتَّخَذَتْ مِن دُونِهِمْ حِجَابًا فَأَرْسَلْنَا إِلَيْهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ
لَهَا بَشَرًا سَوِيًّا
Fattakhathat min doonihim hijabanfaarsalna ilayha roohanafatamaththala laha
basharan sawiyya
Swahili
Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Roho wetu, akajifananisha kwake
sawa na mtu.
|
Ayah 19:18 الأية
قَالَتْ إِنِّي أَعُوذُ بِالرَّحْمَٰنِ مِنكَ إِن كُنتَ تَقِيًّا
Qalat innee aAAoothu birrahmaniminka in kunta taqiyya
Swahili
(Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe,
ukiwa ni mchamngu.
|
Ayah 19:19 الأية
قَالَ إِنَّمَا أَنَا رَسُولُ رَبِّكِ لِأَهَبَ لَكِ غُلَامًا زَكِيًّا
Qala innama ana rasoolurabbiki li-ahaba laki ghulaman zakiyya
Swahili
(Malaika) akasema: Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola wako Mlezi ili
nikubashirie tunu ya mwana aliye takasika.
|
Ayah 19:20 الأية
قَالَتْ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ وَلَمْ أَكُ
بَغِيًّا
Qalat anna yakoonu lee ghulamunwalam yamsasnee basharun walam aku baghiyya
Swahili
Akasema: Nitampataje mwana hali mwanaadamu yeyote hajanigusa, wala mimi si
kahaba?
|
Ayah 19:21 الأية
قَالَ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ ۖ وَلِنَجْعَلَهُ آيَةً
لِّلنَّاسِ وَرَحْمَةً مِّنَّا ۚ وَكَانَ أَمْرًا مَّقْضِيًّا
Qala kathaliki qalarabbuki huwa AAalayya hayyinun walinajAAalahu ayatan
linnasiwarahmatan minna wakana amran maqdiyya
Swahili
(Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi
kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na
hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa.
|
Ayah 19:22 الأية
فَحَمَلَتْهُ فَانتَبَذَتْ بِهِ مَكَانًا قَصِيًّا
Fahamalat-hu fantabathatbihi makanan qasiyya
Swahili
Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali.
|
Ayah 19:23 الأية
فَأَجَاءَهَا الْمَخَاضُ إِلَىٰ جِذْعِ النَّخْلَةِ قَالَتْ يَا لَيْتَنِي مِتُّ
قَبْلَ هَٰذَا وَكُنتُ نَسْيًا مَّنسِيًّا
Faajaaha almakhadu ilajithAAi annakhlati qalat ya laytaneemittu qabla hatha
wakuntu nasyan mansiyya
Swahili
Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningeli kufa
kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa!
|
Ayah 19:24 الأية
فَنَادَاهَا مِن تَحْتِهَا أَلَّا تَحْزَنِي قَدْ جَعَلَ رَبُّكِ تَحْتَكِ سَرِيًّا
Fanadaha min tahtihaalla tahzanee qad jaAAala rabbuki tahtakisariyya
Swahili
Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi amejaalia
chini yako kijito kidogo cha maji!
|
Ayah 19:25 الأية
وَهُزِّي إِلَيْكِ بِجِذْعِ النَّخْلَةِ تُسَاقِطْ عَلَيْكِ رُطَبًا جَنِيًّا
Wahuzzee ilayki bijithAAi annakhlatitusaqit AAalayki rutaban janiyya
Swahili
Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu.
|
Ayah 19:26 الأية
فَكُلِي وَاشْرَبِي وَقَرِّي عَيْنًا ۖ فَإِمَّا تَرَيِنَّ مِنَ الْبَشَرِ أَحَدًا
فَقُولِي إِنِّي نَذَرْتُ لِلرَّحْمَٰنِ صَوْمًا فَلَنْ أُكَلِّمَ الْيَوْمَ
إِنسِيًّا
Fakulee washrabee waqarree AAaynanfa-imma tarayinna mina albashari ahadan
faqooleeinnee nathartu lirrahmani sawmanfalan okallima alyawma insiyya
Swahili
Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote basi
sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo
sitasema na mtu.
|
Ayah 19:27 الأية
فَأَتَتْ بِهِ قَوْمَهَا تَحْمِلُهُ ۖ قَالُوا يَا مَرْيَمُ لَقَدْ جِئْتِ شَيْئًا
فَرِيًّا
Faatat bihi qawmaha tahmiluhuqaloo ya maryamu laqad ji/ti shay-an fariyya
Swahili
Akenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika
umeleta kitu cha ajabu!
|
Ayah 19:28 الأية
يَا أُخْتَ هَارُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ امْرَأَ سَوْءٍ وَمَا كَانَتْ أُمُّكِ
بَغِيًّا
Ya okhta haroona ma kanaabooki imraa saw-in wama kanat ommuki baghiyya
Swahili
Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba.
|
Ayah 19:29 الأية
فَأَشَارَتْ إِلَيْهِ ۖ قَالُوا كَيْفَ نُكَلِّمُ مَن كَانَ فِي الْمَهْدِ صَبِيًّا
Faasharat ilayhi qaloo kayfanukallimu man kana fee almahdi sabiyya
Swahili
Akawaashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeze aliye bado mdogo yumo katika
mlezi?
|
Ayah 19:30 الأية
قَالَ إِنِّي عَبْدُ اللهِ آتَانِيَ الْكِتَابَ وَجَعَلَنِي نَبِيًّا
Qala innee AAabdu Allahi ataniyaalkitaba wajaAAalanee nabiyya
Swahili
(Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na
amenifanya Nabii.
|
Ayah 19:31 الأية
وَجَعَلَنِي مُبَارَكًا أَيْنَ مَا كُنتُ وَأَوْصَانِي بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ
مَا دُمْتُ حَيًّا
WajaAAalanee mubarakan aynamakuntu waawsanee bissalati wazzakatima dumtu hayya
Swahili
Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na
Zaka maadamu ni hai,
|
Ayah 19:32 الأية
وَبَرًّا بِوَالِدَتِي وَلَمْ يَجْعَلْنِي جَبَّارًا شَقِيًّا
Wabarran biwalidatee walam yajAAalneejabbaran shaqiyya
Swahili
Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu.
|
Ayah 19:33 الأية
وَالسَّلَامُ عَلَيَّ يَوْمَ وُلِدتُّ وَيَوْمَ أَمُوتُ وَيَوْمَ أُبْعَثُ حَيًّا
Wassalamu AAalayya yawmawulidtu wayawma amootu wayawma obAAathu hayya
Swahili
Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku
nitakayo fufuliwa kuwa hai.
|
Ayah 19:34 الأية
ذَٰلِكَ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ ۚ قَوْلَ الْحَقِّ الَّذِي فِيهِ يَمْتَرُونَ
Thalika AAeesa ibnu maryamaqawla alhaqqi allathee feehi yamtaroon
Swahili
Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka.
|
Ayah 19:35 الأية
مَا كَانَ لِلَّهِ أَن يَتَّخِذَ مِن وَلَدٍ ۖ سُبْحَانَهُ ۚ إِذَا قَضَىٰ أَمْرًا
فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ
Ma kana lillahi anyattakhitha min waladin subhanahu itha qadaamran fa-innama
yaqoolu lahu kun fayakoon
Swahili
Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanahu, Yeye ametakasika! Anapo
lihukumia jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa.
|
Ayah 19:36 الأية
وَإِنَّ اللهَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ هَٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ
Wa-inna Allaha rabbee warabbukum faAAbudoohuhatha siratun mustaqeem
Swahili
Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, na Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni
Yeye. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka.
|
Ayah 19:37 الأية
فَاخْتَلَفَ الْأَحْزَابُ مِن بَيْنِهِمْ ۖ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا مِن
مَّشْهَدِ يَوْمٍ عَظِيمٍ
Fakhtalafa al-ahzabumin baynihim fawaylun lillatheena kafaroo min mashhadiyawmin
AAatheem
Swahili
Lakini makundi yakakhitalifiana wao kwa wao. Basi ole wao hao walio kufuru kwa
kuhudhuria Siku iliyo kuu!
|
Ayah 19:38 الأية
أَسْمِعْ بِهِمْ وَأَبْصِرْ يَوْمَ يَأْتُونَنَا ۖ لَٰكِنِ الظَّالِمُونَ الْيَوْمَ
فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ
AsmiAA bihim waabsir yawma ya/toonanalakini aththalimoona alyawmafee dalalin
mubeen
Swahili
Watasikia na wataona vizuri vilioje Siku watakayo tufikia! Lakini madhaalimu
sasa wamo katika upotofu ulio dhaahiri.
|
Ayah 19:39 الأية
وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ الْحَسْرَةِ إِذْ قُضِيَ الْأَمْرُ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ
وَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ
Waanthirhum yawma alhasrati ithqudiya al-amru wahum fee ghaflatin wahum
layu/minoon
Swahili
Na waonye siku ya majuto itapo katwa amri. Nao wamo katika ghafla, wala
hawaamini.
|
Ayah 19:40 الأية
إِنَّا نَحْنُ نَرِثُ الْأَرْضَ وَمَنْ عَلَيْهَا وَإِلَيْنَا يُرْجَعُونَ
Inna nahnu narithu al-ardawaman AAalayha wa-ilayna yurjaAAoon
Swahili
Hakika Sisi tutairithi ardhi na walio juu yake. Na kwetu watarejeshwa.
|
Ayah 19:41 الأية
وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِبْرَاهِيمَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صِدِّيقًا نَّبِيًّا
Wathkur fee alkitabiibraheema innahu kana siddeeqan nabiyya
Swahili
Na mtaje katika Kitabu Ibrahim. Hakika yeye alikuwa mkweli, Nabii.
|
Ayah 19:42 الأية
إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ لِمَ تَعْبُدُ مَا لَا يَسْمَعُ وَلَا يُبْصِرُ
وَلَا يُغْنِي عَنكَ شَيْئًا
Ith qala li-abeehi yaabati lima taAAbudu ma la yasmaAAu wala yubsiruwala yughnee
AAanka shay-a
Swahili
Alipo mwambia baba yake: Ewe baba yangu! Kwa nini unaabudu visivyo sikia, na
visivyo ona, na visivyo kufaa chochote?
|
Ayah 19:43 الأية
يَا أَبَتِ إِنِّي قَدْ جَاءَنِي مِنَ الْعِلْمِ مَا لَمْ يَأْتِكَ فَاتَّبِعْنِي
أَهْدِكَ صِرَاطًا سَوِيًّا
Ya abati innee qad jaanee minaalAAilmi ma lam ya/tika fattabiAAnee ahdika
siratansawiyya
Swahili
Ewe baba yangu! Kwa yakini imenifikia ilimu isiyo kufikia wewe. Basi nifuate
mimi, nami nitakuongoza Njia Iliyo Sawa.
|
Ayah 19:44 الأية
يَا أَبَتِ لَا تَعْبُدِ الشَّيْطَانَ ۖ إِنَّ الشَّيْطَانَ كَانَ لِلرَّحْمَٰنِ
عَصِيًّا
Ya abati la taAAbudi ashshaytanainna ashshaytana kana lirrahmaniAAasiyya
Swahili
Ewe baba yangu! Usimuabudu Shet'ani. Hakika Shet'ani ni mwenye kumuasi Mwingi wa
Rehema.
|
Ayah 19:45 الأية
يَا أَبَتِ إِنِّي أَخَافُ أَن يَمَسَّكَ عَذَابٌ مِّنَ الرَّحْمَٰنِ فَتَكُونَ
لِلشَّيْطَانِ وَلِيًّا
Ya abati innee akhafu anyamassaka AAathabun mina arrahmanifatakoona lishshyatani
waliyya
Swahili
Ewe baba yangu! Hakika mimi naogopa isikupate adhabu inayo toka kwa Mwingi wa
Rehema ukaja kuwa mwenziwe Shet'ani.
|
Ayah 19:46 الأية
قَالَ أَرَاغِبٌ أَنتَ عَنْ آلِهَتِي يَا إِبْرَاهِيمُ ۖ لَئِن لَّمْ تَنتَهِ
لَأَرْجُمَنَّكَ ۖ وَاهْجُرْنِي مَلِيًّا
Qala araghibun anta AAan alihateeya ibraheemu la-in lam tantahi laarjumannaka
wahjurneemaliyya
Swahili
(Baba) akasema: Unaichukia miungu yangu, ewe Ibrahim? Kama huachi, basi lazima
nitakupiga mawe. Na niondokelee mbali kwa muda!
|
Ayah 19:47 الأية
قَالَ سَلَامٌ عَلَيْكَ ۖ سَأَسْتَغْفِرُ لَكَ رَبِّي ۖ إِنَّهُ كَانَ بِي حَفِيًّا
Qala salamun AAalaykasaastaghfiru laka rabbee innahu kana bee hafiyya
Swahili
(Ibrahim) akasema: Salamun a'laika! Amani iwe juu yako! Mimi nitakuombea msamaha
kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ananihurumia sana.
|
Ayah 19:48 الأية
وَأَعْتَزِلُكُمْ وَمَا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللهِ وَأَدْعُو رَبِّي عَسَىٰ
أَلَّا أَكُونَ بِدُعَاءِ رَبِّي شَقِيًّا
WaaAAtazilukum wama tadAAoona mindooni Allahi waadAAoo rabbee AAasa allaakoona
biduAAa-i rabbee shaqiyya
Swahili
Nami najitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Na
ninamwomba Mola wangu Mlezi; asaa nisiwe mwenye kukosa bahati kwa kumwomba Mola
wangu Mlezi.
|
Ayah 19:49 الأية
فَلَمَّا اعْتَزَلَهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللهِ وَهَبْنَا لَهُ
إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۖ وَكُلًّا جَعَلْنَا نَبِيًّا
Falamma iAAtazalahum wamayaAAbudoona min dooni Allahi wahabna lahu
ishaqawayaAAqooba wakullan jaAAalna nabiyya
Swahili
Basi alipo jitenga nao na yale waliyo kuwa wakiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu,
tulimpa Is-haq na Yaaqub, na kila mmoja tukamfanya Nabii.
|
Ayah 19:50 الأية
وَوَهَبْنَا لَهُم مِّن رَّحْمَتِنَا وَجَعَلْنَا لَهُمْ لِسَانَ صِدْقٍ عَلِيًّا
Wawahabna lahum min rahmatinawajaAAalna lahum lisana sidqin AAaliyya
Swahili
Na tukawapa rehema zetu na tukawajaalia kupewa sifa za kweli tukufu.
|
Ayah 19:51 الأية
وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مُوسَىٰ ۚ إِنَّهُ كَانَ مُخْلَصًا وَكَانَ رَسُولًا
نَّبِيًّا
Wathkur fee alkitabimoosa innahu kana mukhlasan wakanarasoolan nabiyya
Swahili
Na mtaje Musa katika Kitabu. Hakika yeye alikuwa ni mwenye kuchaguliwa, na
alikuwa Mtume, Nabii.
|
Ayah 19:52 الأية
وَنَادَيْنَاهُ مِن جَانِبِ الطُّورِ الْأَيْمَنِ وَقَرَّبْنَاهُ نَجِيًّا
Wanadaynahu min janibiattoori al-aymani waqarrabnahu najiyya
Swahili
Na tulimwita upande wa kulia wa mlima na tukamsogeza kunong'ona naye.
|
Ayah 19:53 الأية
وَوَهَبْنَا لَهُ مِن رَّحْمَتِنَا أَخَاهُ هَارُونَ نَبِيًّا
Wawahabna lahu min rahmatinaakhahu haroona nabiyya
Swahili
Nasi kwa rehema zetu tukampa nduguye, Harun, awe Nabii.
|
Ayah 19:54 الأية
وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِسْمَاعِيلَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صَادِقَ الْوَعْدِ وَكَانَ
رَسُولًا نَّبِيًّا
Wathkur fee alkitabiismaAAeela innahu kana sadiqa alwaAAdi wakanarasoolan
nabiyya
Swahili
Na mtaje katika Kitabu Ismail. Bila ya shaka yeye alikuwa ni mkweli wa ahadi, na
alikuwa Mtume, Nabii.
|
Ayah 19:55 الأية
وَكَانَ يَأْمُرُ أَهْلَهُ بِالصَّلَاةِ وَالزَّكَاةِ وَكَانَ عِندَ رَبِّهِ
مَرْضِيًّا
Wakana ya/muru ahlahu bissalatiwazzakati wakana AAinda rabbihi mardiyya
Swahili
Na alikuwa akiwaamrisha watu wake Sala na Zaka, na alikuwa mbele ya Mola wake
Mlezi mwenye kuridhiwa.
|
Ayah 19:56 الأية
وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ إِدْرِيسَ ۚ إِنَّهُ كَانَ صِدِّيقًا نَّبِيًّا
Wathkur fee alkitabiidreesa innahu kana siddeeqan nabiyya
Swahili
Na mtaje katika Kitabu Idris. Hakika yeye alikuwa ni mkweli Nabii.
|
Ayah 19:57 الأية
وَرَفَعْنَاهُ مَكَانًا عَلِيًّا
WarafaAAnahu makanan AAaliyya
Swahili
Na tulimuinua daraja ya juu.
|
Ayah 19:58 الأية
أُولَٰئِكَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ مِن
ذُرِّيَّةِ آدَمَ وَمِمَّنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ وَمِن ذُرِّيَّةِ إِبْرَاهِيمَ
وَإِسْرَائِيلَ وَمِمَّنْ هَدَيْنَا وَاجْتَبَيْنَا ۚ إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ
آيَاتُ الرَّحْمَٰنِ خَرُّوا سُجَّدًا وَبُكِيًّا ۩
Ola-ika allatheena anAAama AllahuAAalayhim mina annabiyyeena min thurriyyati
adamawamimman hamalna maAAa noohin wamin thurriyyatiibraheema wa-isra-eela
wamimman hadayna wajtabaynaitha tutla AAalayhim ayatu arrahmanikharroo sujjadan
wabukiyya
Swahili
Hao ndio alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii katika uzao wa
Adam, na katika uzao wa wale tulio wapandisha pamoja na Nuhu, na katika uzao wa
Ibrahim na Israil, na katika wale tulio waongoa na tukawateuwa. Wanapo somewa
Aya za Mwingi wa Rehema huanguka kusujudu na kulia.
|
Ayah 19:59 الأية
فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ ۖ
فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا
Fakhalafa min baAAdihim khalfun adaAAooassalata wattabaAAoo ashshahawatifasawfa
yalqawna ghayya
Swahili
Lakini wakaja baada yao walio wabaya, wakaacha Sala, na wakafuata matamanio.
Basi watakuja kuta malipo ya ubaya.
|
Ayah 19:60 الأية
إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَأُولَٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ
وَلَا يُظْلَمُونَ شَيْئًا
Illa man taba waamanawaAAamila salihan faola-ika yadkhuloonaaljannata wala
yuthlamoona shay-a
Swahili
Isipo kuwa walio tubu, wakaamini, na wakatenda mema. Hao, basi, wataingia Peponi
wala hawatadhulumiwa chochote.
|
Ayah 19:61 الأية
جَنَّاتِ عَدْنٍ الَّتِي وَعَدَ الرَّحْمَٰنُ عِبَادَهُ بِالْغَيْبِ ۚ إِنَّهُ
كَانَ وَعْدُهُ مَأْتِيًّا
Jannati AAadnin allatee waAAada arrahmanuAAibadahu bighaybi innahu kana
waAAduhuma/tiyya
Swahili
Bustani za milele alizo waahidi Rahmani waja wake katika siri. Hakika ahadi yake
hapana shaka itafika.
|
Ayah 19:62 الأية
لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا إِلَّا سَلَامًا ۖ وَلَهُمْ رِزْقُهُمْ فِيهَا
بُكْرَةً وَعَشِيًّا
La yasmaAAoona feeha laghwanilla salaman walahum rizquhum feeha
bukratanwaAAashiyya
Swahili
Humo hawatasikia upuuzi, ila Salama tu. Na watapata humo riziki zao asubuhi na
jioni.
|
Ayah 19:63 الأية
تِلْكَ الْجَنَّةُ الَّتِي نُورِثُ مِنْ عِبَادِنَا مَن كَانَ تَقِيًّا
Tilka aljannatu allatee noorithu min AAibadinaman kana taqiyya
Swahili
Hiyo ndiyo Pepo tutayo warithisha katika waja wetu walio kuwa wachamngu.
|
Ayah 19:64 الأية
وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلَّا بِأَمْرِ رَبِّكَ ۖ لَهُ مَا بَيْنَ أَيْدِينَا وَمَا
خَلْفَنَا وَمَا بَيْنَ ذَٰلِكَ ۚ وَمَا كَانَ رَبُّكَ نَسِيًّا
Wama natanazzalu illa bi-amrirabbika lahu ma bayna aydeena wama khalfanawama
bayna thalika wama kana rabbukanasiyya
Swahili
(Nao watasema:) Wala hatuteremki ila kwa amri ya Mola wako Mlezi. Ni yake Yeye
yaliyoko mbele yetu na yaliyoko nyuma yetu, na yaliyomo katikati ya hayo. Na
Mola wako Mlezi si mwenye kusahau.
|
Ayah 19:65 الأية
رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ
لِعِبَادَتِهِ ۚ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا
Rabbu assamawati wal-ardiwama baynahuma faAAbudhu wastabirliAAibadatihi hal
taAAlamu lahu samiyya
Swahili
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake. Basi muabudu Yeye tu, na
udumu katika ibada yake. Je, mnamjua mwenye jina kama lake?
|
Ayah 19:66 الأية
وَيَقُولُ الْإِنسَانُ أَإِذَا مَا مِتُّ لَسَوْفَ أُخْرَجُ حَيًّا
Wayaqoolu al-insanu a-itha mamittu lasawfa okhraju hayya
Swahili
Na mwanaadamu husema: Hivyo, nitakapo kufa, ni kweli nitafufuliwa niwe hai tena?
|
Ayah 19:67 الأية
أَوَلَا يَذْكُرُ الْإِنسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِن قَبْلُ وَلَمْ يَكُ شَيْئًا
Awa la yathkuru al-insanuanna khalaqnahu min qablu walam yaku shay-a
Swahili
Je! Hakumbuki mwanaadamu ya kwamba tulimuumba kabla, na hali hakuwa chochote?
|
Ayah 19:68 الأية
فَوَرَبِّكَ لَنَحْشُرَنَّهُمْ وَالشَّيَاطِينَ ثُمَّ لَنُحْضِرَنَّهُمْ حَوْلَ
جَهَنَّمَ جِثِيًّا
Fawarabbika lanahshurannahum washshayateenathumma lanuhdirannahum hawla
jahannama jithiyya
Swahili
Basi naapa kwa Mola wako Mlezi! Kwa yakini tutawakusanya wao pamoja na
mashet'ani; kisha tutawahudhurisha kuizunguka Jahannamu, nao wamepiga magoti!
|
Ayah 19:69 الأية
ثُمَّ لَنَنزِعَنَّ مِن كُلِّ شِيعَةٍ أَيُّهُمْ أَشَدُّ عَلَى الرَّحْمَٰنِ
عِتِيًّا
Thumma lananziAAanna min kulli sheeAAatinayyuhum ashaddu AAala arrahmaniAAitiyya
Swahili
Kisha kwa yakini tutawatoa katika kila kundi wale miongoni mwao walio zidi
kumuasi Arrahmani, Mwingi wa Rahema..
|
Ayah 19:70 الأية
ثُمَّ لَنَحْنُ أَعْلَمُ بِالَّذِينَ هُمْ أَوْلَىٰ بِهَا صِلِيًّا
Thumma lanahnu aAAlamu billatheenahum awla biha siliyya
Swahili
Tena hakika Sisi tunawajua vyema zaidi wanao stahiki kuunguzwa humo.
|
Ayah 19:71 الأية
وَإِن مِّنكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا ۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتْمًا مَّقْضِيًّا
Wa-in minkum illa wariduhakana AAala rabbika hatman maqdiyya
Swahili
Wala hapana yeyote katika nyinyi ila ni mwenye kuifikia. Hiyo ni hukumu ya Mola
wako Mlezi ambayo lazima itimizwe.
|
Ayah 19:72 الأية
ثُمَّ نُنَجِّي الَّذِينَ اتَّقَوا وَّنَذَرُ الظَّالِمِينَ فِيهَا جِثِيًّا
Thumma nunajjee allatheena ittaqawwanatharu aththalimeena feehajithiyya
Swahili
Kisha tutawaokoa wale walio mchamngu; na tutawaacha madhaalimu humo wamepiga
magoti.
|
Ayah 19:73 الأية
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ قَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا
لِلَّذِينَ آمَنُوا أَيُّ الْفَرِيقَيْنِ خَيْرٌ مَّقَامًا وَأَحْسَنُ نَدِيًّا
Wa-itha tutla AAalayhim ayatunabayyinatin qala allatheena kafaroo
lillatheenaamanoo ayyu alfareeqayni khayrun maqaman waahsanunadiyya
Swahili
Na wanapo somewa Aya zetu zilizo wazi, walio kufuru huwaambia walio amini: Lipi
katika makundi mawili lenye cheo kizuri na lilio bora barazani?
|
Ayah 19:74 الأية
وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّن قَرْنٍ هُمْ أَحْسَنُ أَثَاثًا وَرِئْيًا
Wakam ahlakna qablahum min qarnin humahsanu athathan wari/ya
Swahili
Na kaumu ngapi tuliziangamiza zilizo kuwa na mapambo mazuri zaidi na wazuri
zaidi kwa kuwatazama!
|
Ayah 19:75 الأية
قُلْ مَن كَانَ فِي الضَّلَالَةِ فَلْيَمْدُدْ لَهُ الرَّحْمَٰنُ مَدًّا ۚ حَتَّىٰ
إِذَا رَأَوْا مَا يُوعَدُونَ إِمَّا الْعَذَابَ وَإِمَّا السَّاعَةَ
فَسَيَعْلَمُونَ مَنْ هُوَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضْعَفُ جُندًا
Qul man kana fee addalalatifalyamdud lahu arrahmanu maddan hattaitha raaw ma
yooAAadoona imma alAAathabawa-imma assaAAata fasayaAAlamoona man huwasharrun
makanan waadAAafu junda
Swahili
Sema: Walio katika upotofu basi Arrahmani Mwingi wa Rahema atawapururia muda
mpaka wayaone waliyo onywa - ama ni adhabu au ni Saa. Hapo ndipo watapo jua ni
nani mwenye makao mabaya na mwenye askari dhaifu.
|
Ayah 19:76 الأية
وَيَزِيدُ اللهُ الَّذِينَ اهْتَدَوْا هُدًى ۗ وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ
خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ مَّرَدًّا
Wayazeedu Allahu allatheenaihtadaw hudan walbaqiyatu assalihatukhayrun AAinda
rabbika thawaban wakhayrun maradda
Swahili
Na Mwenyezi Mungu huwazidishia uwongofu wenye kushika uwongofu. Na mema yenye
kudumu ni bora katika malipo mbele ya Mola wako Mlezi na yana mwisho mwema.
|
Ayah 19:77 الأية
أَفَرَأَيْتَ الَّذِي كَفَرَ بِآيَاتِنَا وَقَالَ لَأُوتَيَنَّ مَالًا وَوَلَدًا
Afaraayta allathee kafara bi-ayatinawaqala laootayanna malan wawalada
Swahili
Je, umemwona aliye zikanya Ishara zetu na akasema: Kwa hakika mimi nitapewa mali
na wana!
|
Ayah 19:78 الأية
أَطَّلَعَ الْغَيْبَ أَمِ اتَّخَذَ عِندَ الرَّحْمَٰنِ عَهْدًا
AttalaAAa alghayba ami ittakhathaAAinda arrahmani AAahda
Swahili
Kwani yeye amepata khabari za ghaibu, au amechukua ahadi kwa Arrahmani Mwingi wa
Rehema?
|
Ayah 19:79 الأية
كَلَّا ۚ سَنَكْتُبُ مَا يَقُولُ وَنَمُدُّ لَهُ مِنَ الْعَذَابِ مَدًّا
Kalla sanaktubu ma yaqooluwanamuddu lahu mina alAAathabi madda
Swahili
Hasha! Tutaandika anayo yasema, tutamkunjulia muda wa adhabu.
|
Ayah 19:80 الأية
وَنَرِثُهُ مَا يَقُولُ وَيَأْتِينَا فَرْدًا
Wanarithuhu ma yaqoolu waya/teenafarda
Swahili
Na tutamrithi hayo anayo yasema, na atatufikia mtupu peke yake!
|
Ayah 19:81 الأية
وَاتَّخَذُوا مِن دُونِ اللهِ آلِهَةً لِّيَكُونُوا لَهُمْ عِزًّا
Wattakhathoo min dooni Allahialihatan liyakoonoo lahum AAizza
Swahili
Na wamechukua miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati iwape nguvu.
|
Ayah 19:82 الأية
كَلَّا ۚ سَيَكْفُرُونَ بِعِبَادَتِهِمْ وَيَكُونُونَ عَلَيْهِمْ ضِدًّا
Kalla sayakfuroona biAAibadatihimwayakoonoona AAalayhim didda
Swahili
Sivyo kabisa! Wataikataa hiyo ibada yao, na watakuwa ndio dhidi yao.
|
Ayah 19:83 الأية
أَلَمْ تَرَ أَنَّا أَرْسَلْنَا الشَّيَاطِينَ عَلَى الْكَافِرِينَ تَؤُزُّهُمْ
أَزًّا
Alam tara anna arsalna ashshayateenaAAala alkafireena taozzuhum azza
Swahili
Kwani huoni ya kwamba tumewatuma mashet'ani kwa makafiri wawachochee kwa
uchochezi?
|
Ayah 19:84 الأية
فَلَا تَعْجَلْ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّمَا نَعُدُّ لَهُمْ عَدًّا
Fala taAAjal AAalayhim innamanaAAuddu lahum AAadda
Swahili
Basi usiwafanyie haraka. Sisi tunawahisabia idadi ya siku zao.
|
Ayah 19:85 الأية
يَوْمَ نَحْشُرُ الْمُتَّقِينَ إِلَى الرَّحْمَٰنِ وَفْدًا
Yawma nahshuru almuttaqeena ilaarrahmani wafda
Swahili
Siku tutayo wakusanya wachamngu kuwapeleka kwa Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa
ni wageni wake.
|
Ayah 19:86 الأية
وَنَسُوقُ الْمُجْرِمِينَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ وِرْدًا
Wanasooqu almujrimeena ila jahannamawirda
Swahili
Na tukawachunga wakhalifu kuwapeleka Jahannamu hali ya kuwa wana kiu.
|
Ayah 19:87 الأية
لَّا يَمْلِكُونَ الشَّفَاعَةَ إِلَّا مَنِ اتَّخَذَ عِندَ الرَّحْمَٰنِ عَهْدًا
La yamlikoona ashshafaAAatailla mani ittakhatha AAinda arrahmaniAAahda
Swahili
Hawatakuwa na mamlaka ya uombezi ila wale walio chukua ahadi kwa Arrahmani
Mwingi wa Rehema..
|
Ayah 19:88 الأية
وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَٰنُ وَلَدًا
Waqaloo ittakhatha arrahmanuwalada
Swahili
Na wao ati husema kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana!
|
Ayah 19:89 الأية
لَّقَدْ جِئْتُمْ شَيْئًا إِدًّا
Laqad ji/tum shay-an idda
Swahili
Hakika mmeleta jambo la kuchusha mno!
|
Ayah 19:90 الأية
تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنشَقُّ الْأَرْضُ وَتَخِرُّ
الْجِبَالُ هَدًّا
Takadu assamawatuyatafattarna minhu watanshaqqu al-ardu watakhirrualjibalu hadda
Swahili
Zinakaribia mbingu kutatuka kwa hilo, na ardhi kupasuka, na milima kuanguka
vipande vipande.
|
Ayah 19:91 الأية
أَن دَعَوْا لِلرَّحْمَٰنِ وَلَدًا
An daAAaw lirrahmaniwalada
Swahili
Kwa kudai kwao kuwa Arrahmani Mwingi wa Rehema ana mwana.
|
Ayah 19:92 الأية
وَمَا يَنبَغِي لِلرَّحْمَٰنِ أَن يَتَّخِذَ وَلَدًا
Wama yanbaghee lirrahmanian yattakhitha walada
Swahili
Wala hahitajii Arrahmani Mwingi wa Rehema kuwa na mwana.
|
Ayah 19:93 الأية
إِن كُلُّ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ إِلَّا آتِي الرَّحْمَٰنِ عَبْدًا
In kullu man fee assamawatiwal-ardi illa atee arrahmaniAAabda
Swahili
Hapana yeyote aliomo mbinguni na ardhini ila atafika kwa Arrahmani Mwingi wa
Rehema kuwa ni mtumwa wake.
|
Ayah 19:94 الأية
لَّقَدْ أَحْصَاهُمْ وَعَدَّهُمْ عَدًّا
Laqad ahsahum waAAaddahum AAadda
Swahili
Yeye hakika amewadhibiti na amewahisabu sawa sawa.
|
Ayah 19:95 الأية
وَكُلُّهُمْ آتِيهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَرْدًا
Wakulluhum ateehi yawma alqiyamatifarda
Swahili
Na kila mmoja katika wao atamfikia Siku ya Kiyama peke yake.
|
Ayah 19:96 الأية
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَيَجْعَلُ لَهُمُ الرَّحْمَٰنُ
وُدًّا
Inna allatheena amanoowaAAamiloo assalihati sayajAAalu lahumu arrahmanuwudda
Swahili
Hakika walio amini na wakatenda mema Arrahmani Mwingi wa Rehema atawajaalia
mapenzi.
|
Ayah 19:97 الأية
فَإِنَّمَا يَسَّرْنَاهُ بِلِسَانِكَ لِتُبَشِّرَ بِهِ الْمُتَّقِينَ وَتُنذِرَ
بِهِ قَوْمًا لُّدًّا
Fa-innama yassarnahu bilisanikalitubashshira bihi almuttaqeena watunthira bihi
qawmanludda
Swahili
Na hakika tumeifanya nyepesi (Qur'ani) kwa ulimi wako, ili uwabashirie kwayo
wachamngu, na uwaonye kwayo watu wabishi.
|
Ayah 19:98 الأية
وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّن قَرْنٍ هَلْ تُحِسُّ مِنْهُم مِّنْ أَحَدٍ أَوْ
تَسْمَعُ لَهُمْ رِكْزًا
Wakam ahlakna qablahum min qarnin haltuhissu minhum min ahadin aw tasmaAAu lahum
rikza
Swahili
Na kaumu ngapi tumezihiliki kabla yao. Je! Unawaona hata mmoja katika wao au
unasikia hata mchakato wao?
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|