First Ayah 1 الأية الأوليبِسْم ِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Ayah 20:2 الأية
مَا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْقُرْآنَ لِتَشْقَىٰ
Ma anzalna AAalayka alqur-analitashqa
Swahili
Hatukukuteremshia Qur'ani ili upate mashaka.
|
Ayah 20:3 الأية
إِلَّا تَذْكِرَةً لِّمَن يَخْشَىٰ
Illa tathkiratan liman yakhsha
Swahili
Bali ni mawaidha kwa wenye kunyenyekea.
|
Ayah 20:4 الأية
تَنزِيلًا مِّمَّنْ خَلَقَ الْأَرْضَ وَالسَّمَاوَاتِ الْعُلَى
Tanzeelan mimman khalaqa al-arda wassamawatialAAula
Swahili
Materemsho yatokayo kwa aliye umba ardhi na mbingu zilizo juu.
|
Ayah 20:5 الأية
الرَّحْمَٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
Arrahmanu AAalaalAAarshi istawa
Swahili
Arrahmani, Mwingi wa Rehema, aliye tawala juu ya Kiti cha Enzi.
|
Ayah 20:6 الأية
لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَمَا تَحْتَ
الثَّرَىٰ
Lahu ma fee assamawatiwama fee al-ardi wama baynahuma wamatahta aththara
Swahili
Ni vyake vyote viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, na viliomo baina yao,
na viliomo chini ya ardhi.
|
Ayah 20:7 الأية
وَإِن تَجْهَرْ بِالْقَوْلِ فَإِنَّهُ يَعْلَمُ السِّرَّ وَأَخْفَى
Wa-in tajhar bilqawli fa-innahuyaAAlamu assirra waakhfa
Swahili
Na ukinyanyua sauti kwa kusema...basi hakika Yeye anajua siri na duni kuliko
siri.
|
Ayah 20:8 الأية
اللَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ
Allahu la ilaha illahuwa lahu al-asmao alhusna
Swahili
Mwenyezi Mungu! Hapana mungu isipo kuwa Yeye. Yeye ana majina mazuri kabisa.
|
Ayah 20:9 الأية
وَهَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ مُوسَىٰ
Wahal ataka hadeethu moosa
Swahili
Na je! Imekufikia hadithi ya Musa?
|
Ayah 20:10 الأية
إِذْ رَأَىٰ نَارًا فَقَالَ لِأَهْلِهِ امْكُثُوا إِنِّي آنَسْتُ نَارًا لَّعَلِّي
آتِيكُم مِّنْهَا بِقَبَسٍ أَوْ أَجِدُ عَلَى النَّارِ هُدًى
Ith raa naran faqalali-ahlihi omkuthoo innee anastu naran laAAallee ateekumminha
biqabasin aw ajidu AAala annarihuda
Swahili
Alipo uona moto, akawaambia watu wake: Ngojeni! Mimi nimeuona moto, huenda
nikakuleteeni kijinga kutoka huo moto, au nikapata uongofu kwenye moto.
|
Ayah 20:11 الأية
فَلَمَّا أَتَاهَا نُودِيَ يَا مُوسَىٰ
Falamma ataha noodiya yamoosa
Swahili
Basi alipo ufikia akaitwa: Ewe Musa!
|
Ayah 20:12 الأية
إِنِّي أَنَا رَبُّكَ فَاخْلَعْ نَعْلَيْكَ ۖ إِنَّكَ بِالْوَادِ الْمُقَدَّسِ
طُوًى
Innee ana rabbuka fakhlaAAnaAAlayka innaka bilwadi almuqaddasi tuwa
Swahili
Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu vyako. Kwani upo katika bonde
takatifu la T'uwa.
|
Ayah 20:13 الأية
وَأَنَا اخْتَرْتُكَ فَاسْتَمِعْ لِمَا يُوحَىٰ
Waana ikhtartuka fastamiAAlima yooha
Swahili
Nami nimekuteua wewe; basi sikiliza unayo funuliwa.
|
Ayah 20:14 الأية
إِنَّنِي أَنَا اللَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدْنِي وَأَقِمِ الصَّلَاةَ
لِذِكْرِي
Innanee ana Allahu lailaha illa ana faAAbudnee waaqimi assalatalithikree
Swahili
Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana mungu ila Mimi tu. Basi niabudu Mimi,
na ushike Sala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi.
|
Ayah 20:15 الأية
إِنَّ السَّاعَةَ آتِيَةٌ أَكَادُ أُخْفِيهَا لِتُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا
تَسْعَىٰ
Inna assaAAata atiyatunakadu okhfeeha litujza kullu nafsin bimatasAAa
Swahili
Hakika Saa itakuja bila ya shaka. Nimekaribia kuificha, ili kila nafsi ilipwe
kwa iliyo yafanya.
|
Ayah 20:16 الأية
فَلَا يَصُدَّنَّكَ عَنْهَا مَن لَّا يُؤْمِنُ بِهَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ فَتَرْدَىٰ
Fala yasuddannaka AAanhaman la yu/minu biha wattabaAAa hawahufatarda
Swahili
Kwa hivyo asikukengeushe nayo yule ambaye haiamini na akafuata pumbao lake ukaja
kuhiliki.
|
Ayah 20:17 الأية
وَمَا تِلْكَ بِيَمِينِكَ يَا مُوسَىٰ
Wama tilka biyameenika ya moosa
Swahili
Na nini hicho kilichomo mkononi mwako wa kulia, ewe Musa?
|
Ayah 20:18 الأية
قَالَ هِيَ عَصَايَ أَتَوَكَّأُ عَلَيْهَا وَأَهُشُّ بِهَا عَلَىٰ غَنَمِي وَلِيَ
فِيهَا مَآرِبُ أُخْرَىٰ
Qala hiya AAasaya atawakkaoAAalayha waahushshu biha AAala ghanameewaliya feeha
maaribu okhra
Swahili
Akasema: Hii ni fimbo yangu; naiegemea na ninawaangushia majani kondoo na mbuzi
wangu. Tena inanifaa kwa matumizi mengine.
|
Ayah 20:19 الأية
قَالَ أَلْقِهَا يَا مُوسَىٰ
Qala alqiha ya moosa
Swahili
Akasema: Itupe, ewe Musa!
|
Ayah 20:20 الأية
فَأَلْقَاهَا فَإِذَا هِيَ حَيَّةٌ تَسْعَىٰ
Faalqaha fa-itha hiya hayyatuntasAAa
Swahili
Akaitupa. Mara ikawa nyoka anaye kwenda mbio.
|
Ayah 20:21 الأية
قَالَ خُذْهَا وَلَا تَخَفْ ۖ سَنُعِيدُهَا سِيرَتَهَا الْأُولَىٰ
Qala khuthha walatakhaf sanuAAeeduha seerataha al-oola
Swahili
Akasema: Ikamate, wala usiogope! Tutairudisha hali yake ya kwanza.
|
Ayah 20:22 الأية
وَاضْمُمْ يَدَكَ إِلَىٰ جَنَاحِكَ تَخْرُجْ بَيْضَاءَ مِنْ غَيْرِ سُوءٍ آيَةً
أُخْرَىٰ
Wadmum yadaka ila janahikatakhruj baydaa min ghayri soo-in ayatan okhra
Swahili
Na uambatishe mkono wako kwenye ubavu. Utatoka mweupe pasipo kuwa na madhara
yoyote. Hiyo ni ishara nyengine.
|
Ayah 20:23 الأية
لِنُرِيَكَ مِنْ آيَاتِنَا الْكُبْرَى
Linuriyaka min ayatinaalkubra
Swahili
Ili tukuonyeshe baadhi ya ishara zetu kubwa.
|
Ayah 20:24 الأية
اذْهَبْ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ
Ithhab ila firAAawna innahu tagha
Swahili
Nenda kwa Firauni; kwani hakika yeye amepindukia mipaka.
|
Ayah 20:25 الأية
قَالَ رَبِّ اشْرَحْ لِي صَدْرِي
Qala rabbi ishrah lee sadree
Swahili
(Musa) akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu,
|
Ayah 20:26 الأية
وَيَسِّرْ لِي أَمْرِي
Wayassir lee amree
Swahili
Na unifanyie nyepesi kazi yangu,
|
Ayah 20:27 الأية
وَاحْلُلْ عُقْدَةً مِّن لِّسَانِي
Wahlul AAuqdatan min lisanee
Swahili
Na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu,
|
Ayah 20:28 الأية
يَفْقَهُوا قَوْلِي
Yafqahoo qawlee
Swahili
Wapate kufahamu maneno yangu.
|
Ayah 20:29 الأية
وَاجْعَل لِّي وَزِيرًا مِّنْ أَهْلِي
WajAAal lee wazeeran min ahlee
Swahili
Na nipe waziri katika watu wangu,
|
Ayah 20:30 الأية
هَارُونَ أَخِي
Haroona akhee
Swahili
Harun, ndugu yangu.
|
Ayah 20:31 الأية
اشْدُدْ بِهِ أَزْرِي
Oshdud bihi azree
Swahili
Kwake yeye niongeze nguvu zangu.
|
Ayah 20:32 الأية
وَأَشْرِكْهُ فِي أَمْرِي
Waashrik-hu fee amree
Swahili
Na umshirikishe katika kazi yangu.
|
Ayah 20:33 الأية
كَيْ نُسَبِّحَكَ كَثِيرًا
Kay nusabbihaka katheera
Swahili
Ili tukutakase sana.
|
Ayah 20:34 الأية
وَنَذْكُرَكَ كَثِيرًا
Wanathkuraka katheera
Swahili
Na tukukumbuke sana.
|
Ayah 20:35 الأية
إِنَّكَ كُنتَ بِنَا بَصِيرًا
Innaka kunta bina baseera
Swahili
Hakika Wewe unatuona.
|
Ayah 20:36 الأية
قَالَ قَدْ أُوتِيتَ سُؤْلَكَ يَا مُوسَىٰ
Qala qad ooteeta su/laka yamoosa
Swahili
Akasema: Hakika Umepewa maombi yako, ewe Musa!
|
Ayah 20:37 الأية
وَلَقَدْ مَنَنَّا عَلَيْكَ مَرَّةً أُخْرَىٰ
Walaqad mananna AAalayka marratanokhra
Swahili
Na hakika tulikwisha kufanyia hisani mara nyengine...
|
Ayah 20:38 الأية
إِذْ أَوْحَيْنَا إِلَىٰ أُمِّكَ مَا يُوحَىٰ
Ith awhayna ilaommika ma yooha
Swahili
Pale tulipo mfunulia mama yako yaliyo funuliwa,
|
Ayah 20:39 الأية
أَنِ اقْذِفِيهِ فِي التَّابُوتِ فَاقْذِفِيهِ فِي الْيَمِّ فَلْيُلْقِهِ الْيَمُّ
بِالسَّاحِلِ يَأْخُذْهُ عَدُوٌّ لِّي وَعَدُوٌّ لَّهُ ۚ وَأَلْقَيْتُ عَلَيْكَ
مَحَبَّةً مِّنِّي وَلِتُصْنَعَ عَلَىٰ عَيْنِي
Ani iqthifeehi fee attabootifaqthifeehi fee alyammi falyulqihi alyammu
bissahiliya/khuthhu AAaduwwun lee waAAaduwwun lahu waalqaytuAAalayka mahabbatan
minnee walitusnaAAa AAalaAAaynee
Swahili
Ya kuwa mtie katika kisanduku, na kisha kitie mtoni, na mto utamfikisha
ufukweni. Atamchukua adui yangu naye ni adui yake. Na nimekutilia mapenzi yanayo
tokana kwangu, na ili ulelewe machoni mwangu.
|
Ayah 20:40 الأية
إِذْ تَمْشِي أُخْتُكَ فَتَقُولُ هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ مَن يَكْفُلُهُ ۖ
فَرَجَعْنَاكَ إِلَىٰ أُمِّكَ كَيْ تَقَرَّ عَيْنُهَا وَلَا تَحْزَنَ ۚ وَقَتَلْتَ
نَفْسًا فَنَجَّيْنَاكَ مِنَ الْغَمِّ وَفَتَنَّاكَ فُتُونًا ۚ فَلَبِثْتَ سِنِينَ
فِي أَهْلِ مَدْيَنَ ثُمَّ جِئْتَ عَلَىٰ قَدَرٍ يَا مُوسَىٰ
Ith tamshee okhtuka fataqoolu haladullukum AAala man yakfuluhu farajaAAnaka
ilaommika kay taqarra AAaynuha wala tahzanawaqatalta nafsan fanajjaynaka mina
alghammi wafatannakafutoonan falabithta sineena fee ahli madyana thumma ji/ta
AAalaqadarin ya moosa
Swahili
Dada yako alipo kwenda na akasema: Je! Nikujuulisheni mtu wa kuweza kumlea? Basi
tukakurejesha kwa mama yako ili macho yake yaburudike, wala asihuzunike. Na
ulimuuwa mtu, nasi tukakuokoa katika dhiki, na tukakujaribu kwa majaribio mengi.
Ukakaa miaka kwa watu wa Madyana. Kisha ukaja kama ilivyo kadiriwa, ewe Musa!
|
Ayah 20:41 الأية
وَاصْطَنَعْتُكَ لِنَفْسِي
WastanaAAtuka linafsee
Swahili
Na nimekuteuwa kwa ajili ya nafsi yangu.
|
Ayah 20:42 الأية
اذْهَبْ أَنتَ وَأَخُوكَ بِآيَاتِي وَلَا تَنِيَا فِي ذِكْرِي
Ithhab anta waakhooka bi-ayateewala taniya fee thikree
Swahili
Nenda, wewe na ndugu yako, pamoja na ishara zangu, wala msichoke kunikumbuka.
|
Ayah 20:43 الأية
اذْهَبَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ إِنَّهُ طَغَىٰ
Ithhaba ila firAAawnainnahu tagha
Swahili
Nendeni kwa Firauni. Hakika yeye amepindukia mipaka.
|
Ayah 20:44 الأية
فَقُولَا لَهُ قَوْلًا لَّيِّنًا لَّعَلَّهُ يَتَذَكَّرُ أَوْ يَخْشَىٰ
Faqoola lahu qawlan layyinanlaAAallahu yatathakkaru aw yakhsha
Swahili
Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa.
|
Ayah 20:45 الأية
قَالَا رَبَّنَا إِنَّنَا نَخَافُ أَن يَفْرُطَ عَلَيْنَا أَوْ أَن يَطْغَىٰ
Qala rabbana innananakhafu an yafruta AAalayna aw an yatgha
Swahili
Wakasema: Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tunaogopa asije akapindukia mipaka
juu yetu au kufanya jeuri.
|
Ayah 20:46 الأية
قَالَ لَا تَخَافَا ۖ إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَىٰ
Qala la takhafainnanee maAAakuma asmaAAu waara
Swahili
Akasema: Msiogope! Hakika Mimi ni pamoja nanyi. Nasikia na ninaona.
|
Ayah 20:47 الأية
فَأْتِيَاهُ فَقُولَا إِنَّا رَسُولَا رَبِّكَ فَأَرْسِلْ مَعَنَا بَنِي
إِسْرَائِيلَ وَلَا تُعَذِّبْهُمْ ۖ قَدْ جِئْنَاكَ بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكَ ۖ
وَالسَّلَامُ عَلَىٰ مَنِ اتَّبَعَ الْهُدَىٰ
Fa/tiyahu faqoola innarasoola rabbika faarsil maAAana banee isra-eelawala
tuAAaththibhum qad ji/naka bi-ayatinmin rabbika wassalamu AAala mani
ittabaAAaalhuda
Swahili
Basi mwendeeni, na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola wako Mlezi! Basi
waache Wana wa Israili watoke nasi, wala usiwaadhibu. Sisi tumekuletea ishara
itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na amani itakuwa juu ya aliye fuata uwongofu.
|
Ayah 20:48 الأية
إِنَّا قَدْ أُوحِيَ إِلَيْنَا أَنَّ الْعَذَابَ عَلَىٰ مَن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ
Inna qad oohiya ilaynaanna alAAathaba AAala man kaththaba watawalla
Swahili
Hakika tumefunuliwa sisi kwamba hapana shaka adhabu itamsibu anaye kadhibisha na
akapuuza.
|
Ayah 20:49 الأية
قَالَ فَمَن رَّبُّكُمَا يَا مُوسَىٰ
Qala faman rabbukuma yamoosa
Swahili
(Firauni) akasema: Basi Mola wenu Mlezi ni nani, ewe Musa?
|
Ayah 20:50 الأية
قَالَ رَبُّنَا الَّذِي أَعْطَىٰ كُلَّ شَيْءٍ خَلْقَهُ ثُمَّ هَدَىٰ
Qala rabbuna allatheeaAAta kulla shay-in khalqahu thumma hada
Swahili
Akasema: Mola wetu Mlezi ni yule aliye kipa kila kitu umbo lake, kisha
akakiongoa.
|
Ayah 20:51 الأية
قَالَ فَمَا بَالُ الْقُرُونِ الْأُولَىٰ
Qala fama balualqurooni al-oola
Swahili
Akasema: Nini hali ya karne za kwanza?
|
Ayah 20:52 الأية
قَالَ عِلْمُهَا عِندَ رَبِّي فِي كِتَابٍ ۖ لَّا يَضِلُّ رَبِّي وَلَا يَنسَى
Qala AAilmuha AAinda rabbeefee kitabin la yadillu rabbee walayansa
Swahili
Akasema: Ilimu yake iko kwa Mola wangu Mlezi katika Kitabu. Mola wangu Mlezi
hapotei wala hasahau.
|
Ayah 20:53 الأية
الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ مَهْدًا وَسَلَكَ لَكُمْ فِيهَا سُبُلًا وَأَنزَلَ
مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِّن نَّبَاتٍ شَتَّىٰ
Allathee jaAAala lakumu al-ardamahdan wasalaka lakum feeha subulan waanzala mina
assama-imaan faakhrajna bihi azwajan min nabatinshatta
Swahili
Ambaye amekufanyieni ardhi kuwa tandiko, na akakupitishieni humo njia, na
akakuteremshieni kutoka mbinguni maji. Na kwa hayo tukatoa namna mbali mbali za
mimema.
|
Ayah 20:54 الأية
كُلُوا وَارْعَوْا أَنْعَامَكُمْ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّأُولِي النُّهَىٰ
Kuloo warAAaw anAAamakum innafee thalika laayatin li-olee annuha
Swahili
Kuleni, na mchunge wanyama wenu. Hakika katika hayo zipo ishara kwa wenye akili.
|
Ayah 20:55 الأية
مِنْهَا خَلَقْنَاكُمْ وَفِيهَا نُعِيدُكُمْ وَمِنْهَا نُخْرِجُكُمْ تَارَةً
أُخْرَىٰ
Minha khalaqnakum wafeehanuAAeedukum waminha nukhrijukum taratan okhra
Swahili
Kutokana nayo (ardhi) tumekuumbeni, na humo tunakurudisheni, na kutoka humo
tutakutoeni mara nyengine.
|
Ayah 20:56 الأية
وَلَقَدْ أَرَيْنَاهُ آيَاتِنَا كُلَّهَا فَكَذَّبَ وَأَبَىٰ
Walaqad araynahu ayatinakullaha fakaththaba waaba
Swahili
Na hakika tulimwonyesha ishara zetu zote. Lakini alikadhibisha na akakataa.
|
Ayah 20:57 الأية
قَالَ أَجِئْتَنَا لِتُخْرِجَنَا مِنْ أَرْضِنَا بِسِحْرِكَ يَا مُوسَىٰ
Qala aji/tana litukhrijanamin ardina bisihrika ya moosa
Swahili
Akasema: Ewe Musa! Hivyo umetujia kututoa katika nchi yetu kwa uchawi wako?
|
Ayah 20:58 الأية
فَلَنَأْتِيَنَّكَ بِسِحْرٍ مِّثْلِهِ فَاجْعَلْ بَيْنَنَا وَبَيْنَكَ مَوْعِدًا
لَّا نُخْلِفُهُ نَحْنُ وَلَا أَنتَ مَكَانًا سُوًى
Falana/tiyannaka bisihrin mithlihi fajAAalbaynana wabaynaka mawAAidan la
nukhlifuhu nahnuwala anta makanan suwa
Swahili
Basi sisi hakika tutakueletea uchawi kama huo. Basi weka miadi baina yetu na
wewe, ambayo tusiivunje sisi wala wewe, mahali patapo kuwa sawa.
|
Ayah 20:59 الأية
قَالَ مَوْعِدُكُمْ يَوْمُ الزِّينَةِ وَأَن يُحْشَرَ النَّاسُ ضُحًى
Qala mawAAidukum yawmu azzeenatiwaan yuhshara annasu duha
Swahili
Akasema: Miadi yenu ni siku ya Sikukuu; na watu wakusanywe kabla ya adhuhuri.
|
Ayah 20:60 الأية
فَتَوَلَّىٰ فِرْعَوْنُ فَجَمَعَ كَيْدَهُ ثُمَّ أَتَىٰ
Fatawalla firAAawnu fajamaAAa kaydahuthumma ata
Swahili
Basi Firauni akarudi na akatengeneza hila yake, kisha akaja.
|
Ayah 20:61 الأية
قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ وَيْلَكُمْ لَا تَفْتَرُوا عَلَى اللَّهِ كَذِبًا
فَيُسْحِتَكُم بِعَذَابٍ ۖ وَقَدْ خَابَ مَنِ افْتَرَىٰ
Qala lahum moosa waylakum lataftaroo AAala Allahi kathiban
fayushitakumbiAAathabin waqad khaba mani iftara
Swahili
Musa akamwambia: Ole wenu! Msimzulie Mwenyezi Mungu uwongo, asije akakufutilieni
mbali kwa adhabu. Na mwenye kuzua lazima ashindwe!
|
Ayah 20:62 الأية
فَتَنَازَعُوا أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ وَأَسَرُّوا النَّجْوَىٰ
FatanazaAAoo amrahum baynahumwaasarroo annajwa
Swahili
Basi wakazozana kwa shauri yao wenyewe kwa wenyewe, na wakanong'ona kwa siri.
|
Ayah 20:63 الأية
قَالُوا إِنْ هَٰذَانِ لَسَاحِرَانِ يُرِيدَانِ أَن يُخْرِجَاكُم مِّنْ أَرْضِكُم
بِسِحْرِهِمَا وَيَذْهَبَا بِطَرِيقَتِكُمُ الْمُثْلَىٰ
Qaloo in hathani lasahiraniyureedani an yukhrijakum min ardikum
bisihrihimawayathhaba bitareeqatikumu almuthla
Swahili
Wakasema: Hakika hawa wawili ni wachawi, wanataka kukutoeni katika nchi yenu kwa
uchawi wao, na waondoe mila zenu zilizo bora kabisa.
|
Ayah 20:64 الأية
فَأَجْمِعُوا كَيْدَكُمْ ثُمَّ ائْتُوا صَفًّا ۚ وَقَدْ أَفْلَحَ الْيَوْمَ مَنِ
اسْتَعْلَىٰ
FaajmiAAoo kaydakum thumma i/too saffanwaqad aflaha alyawma mani istaAAla
Swahili
Kwa hivyo kusanyeni hila zenu zote, kisha mfike kwa kujipanga safu, na kwa
yakini atafuzu kweli kweli leo atakaye shinda.
|
Ayah 20:65 الأية
قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِمَّا أَن تُلْقِيَ وَإِمَّا أَن نَّكُونَ أَوَّلَ مَنْ
أَلْقَىٰ
Qaloo ya moosa immaan tulqiya wa-imma an nakoona awwala man alqa
Swahili
Wakasema: Ewe Musa! Je! Utatupa wewe, au tutakuwa sisi wa kwanza kutupa?
|
Ayah 20:66 الأية
قَالَ بَلْ أَلْقُوا ۖ فَإِذَا حِبَالُهُمْ وَعِصِيُّهُمْ يُخَيَّلُ إِلَيْهِ مِن
سِحْرِهِمْ أَنَّهَا تَسْعَىٰ
Qala bal alqoo fa-itha hibaluhumwaAAisiyyuhum yukhayyalu ilayhi min sihrihim
annahatasAAa
Swahili
Akasema: Bali tupeni nyinyi! Tahamaki kamba zao na fimbo zao zikaonekana mbele
yake, kwa uchawi wao, kuwa zinapiga mbio.
|
Ayah 20:67 الأية
فَأَوْجَسَ فِي نَفْسِهِ خِيفَةً مُّوسَىٰ
Faawjasa fee nafsihi kheefatan moosa
Swahili
Basi Musa akaingia khofu nafsi yake.
|
Ayah 20:68 الأية
قُلْنَا لَا تَخَفْ إِنَّكَ أَنتَ الْأَعْلَىٰ
Qulna la takhaf innaka antaal-aAAla
Swahili
Tukasema: Usikhofu! Hakika wewe ndiye utakaye shinda.
|
Ayah 20:69 الأية
وَأَلْقِ مَا فِي يَمِينِكَ تَلْقَفْ مَا صَنَعُوا ۖ إِنَّمَا صَنَعُوا كَيْدُ
سَاحِرٍ ۖ وَلَا يُفْلِحُ السَّاحِرُ حَيْثُ أَتَىٰ
Waalqi ma fee yameenika talqaf masanaAAoo innama sanaAAoo kaydu sahirinwala
yuflihu assahiru haythuata
Swahili
Na kitupe kilicho katika mkono wako wa kulia; kitavimeza walivyo viunda. Hakika
walivyo unda ni hila za mchawi tu, na mchawi hafanikiwi popote afikapo.
|
Ayah 20:70 الأية
فَأُلْقِيَ السَّحَرَةُ سُجَّدًا قَالُوا آمَنَّا بِرَبِّ هَارُونَ وَمُوسَىٰ
Faolqiya assaharatu sujjadanqaloo amanna birabbi haroona wamoosa
Swahili
Basi wachawi wakaangushwa wanasujudu. Wakasema: Tumemuamini Mola Mlezi wa Harun
na Musa!
|
Ayah 20:71 الأية
قَالَ آمَنتُمْ لَهُ قَبْلَ أَنْ آذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّهُ لَكَبِيرُكُمُ الَّذِي
عَلَّمَكُمُ السِّحْرَ ۖ فَلَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ
خِلَافٍ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ فِي جُذُوعِ النَّخْلِ وَلَتَعْلَمُنَّ أَيُّنَا
أَشَدُّ عَذَابًا وَأَبْقَىٰ
Qala amantum lahu qabla an athanalakum innahu lakabeerukumu allathee
AAallamakumu assihrafalaoqattiAAanna aydiyakum waarjulakum min
khilafinwalaosallibannakum fee juthooAAi annakhliwalataAAlamunna ayyuna ashaddu
AAathaban waabqa
Swahili
(Firauni) akasema: Oh! Mnamuamini kabla sijakupeni ruhusa? Hakika yeye ndiye
mkubwa wenu aliye kufundisheni uchawi. Basi kwa yakini nitakukateni mikono yenu
na miguu yenu kwa kutafautisha. Na nitakutundikeni misalabani katika vigogo vya
mitende, na hapo kwa yakini mtajua ni nani katika sisi aliye mkali wa kuadhibu
na kuiendeleza adhabu yake.
|
Ayah 20:72 الأية
قَالُوا لَن نُّؤْثِرَكَ عَلَىٰ مَا جَاءَنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالَّذِي
فَطَرَنَا ۖ فَاقْضِ مَا أَنتَ قَاضٍ ۖ إِنَّمَا تَقْضِي هَٰذِهِ الْحَيَاةَ
الدُّنْيَا
Qaloo lan nu/thiraka AAala majaana mina albayyinati wallatheefatarana faqdi ma
anta qadininnama taqdee hathihi alhayataaddunya
Swahili
Wakasema: Hatutokukhiari wewe kuliko ishara waziwazi zilizo tujia, na kuliko
yule aliye tuumba. Basi hukumu utavyo hukumu; kwani wewe unahukumu haya ya
maisha ya duniani tu.
|
Ayah 20:73 الأية
إِنَّا آمَنَّا بِرَبِّنَا لِيَغْفِرَ لَنَا خَطَايَانَا وَمَا أَكْرَهْتَنَا
عَلَيْهِ مِنَ السِّحْرِ ۗ وَاللَّهُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ
Inna amanna birabbinaliyaghfira lana khatayana wamaakrahtana AAalayhi mina
assihri wallahukhayrun waabqa
Swahili
Hakika sisi tumemuamini Mola wetu Mlezi ili atusamehe makosa yetu na uchawi ulio
tulazimisha kuufanya. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mbora na Mwenye kudumu zaidi.
|
Ayah 20:74 الأية
إِنَّهُ مَن يَأْتِ رَبَّهُ مُجْرِمًا فَإِنَّ لَهُ جَهَنَّمَ لَا يَمُوتُ فِيهَا
وَلَا يَحْيَىٰ
Innahu man ya/ti rabbahu mujriman fa-innalahu jahannama la yamootu feeha wala
yahya
Swahili
Hakika ataye mjia Mola wake Mlezi naye ni mkhalifu, basi kwa yakini, yake huyo
ni Jahannamu. Hafi humo wala haishi.
|
Ayah 20:75 الأية
وَمَن يَأْتِهِ مُؤْمِنًا قَدْ عَمِلَ الصَّالِحَاتِ فَأُولَٰئِكَ لَهُمُ
الدَّرَجَاتُ الْعُلَىٰ
Waman ya/tihi mu/minan qad AAamila assalihatifaola-ika lahumu addarajatu alAAula
Swahili
Na atakaye mjia naye ni Muumini aliye tenda mema, basi hao ndio wenye vyeo vya
juu.
|
Ayah 20:76 الأية
جَنَّاتُ عَدْنٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ
جَزَاءُ مَن تَزَكَّىٰ
Jannatu AAadnin tajree min tahtihaal-anharu khalideena feeha wathalikajazao man
tazakka
Swahili
Bustani za milele zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na hayo ni malipo ya
mwenye kujitakasa.
|
Ayah 20:77 الأية
وَلَقَدْ أَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنْ أَسْرِ بِعِبَادِي فَاضْرِبْ لَهُمْ
طَرِيقًا فِي الْبَحْرِ يَبَسًا لَّا تَخَافُ دَرَكًا وَلَا تَخْشَىٰ
Walaqad awhayna ilamoosa an asri biAAibadee fadriblahum tareeqan fee albahri
yabasan la takhafudarakan wala takhsha
Swahili
Na tulimfunulia Musa: Toka usiku na waja wangu, na uwapigie njia kavu baharini.
Usikhofu kukamatwa, wala usiogope.
|
Ayah 20:78 الأية
فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ بِجُنُودِهِ فَغَشِيَهُم مِّنَ الْيَمِّ مَا غَشِيَهُمْ
FaatbaAAahum firAAawnu bijunoodihifaghashiyahum mina alyammi ma ghashiyahum
Swahili
Firauni akawafuata pamoja na majeshi yake. Basi kiliwafudikiza humo baharini
kilicho wafudikiza.
|
Ayah 20:79 الأية
وَأَضَلَّ فِرْعَوْنُ قَوْمَهُ وَمَا هَدَىٰ
Waadalla firAAawnu qawmahu wamahada
Swahili
Na Firauni aliwapoteza watu wake wala hakuwaongoa.
|
Ayah 20:80 الأية
يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ قَدْ أَنجَيْنَاكُم مِّنْ عَدُوِّكُمْ وَوَاعَدْنَاكُمْ
جَانِبَ الطُّورِ الْأَيْمَنَ وَنَزَّلْنَا عَلَيْكُمُ الْمَنَّ وَالسَّلْوَىٰ
Ya banee isra-eela qad anjaynakummin AAaduwwikum wawaAAadnakum janiba
attoorial-aymana wanazzalna AAalaykumu almanna wassalwa
Swahili
Enyi Wana wa Israili! Hakika tulikuokoeni na adui yenu, na tukakuahidini upande
wa kulia wa mlima. Na tulikuteremshieni Manna na Salwa.
|
Ayah 20:81 الأية
كُلُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَلَا تَطْغَوْا فِيهِ فَيَحِلَّ
عَلَيْكُمْ غَضَبِي ۖ وَمَن يَحْلِلْ عَلَيْهِ غَضَبِي فَقَدْ هَوَىٰ
Kuloo min tayyibati marazaqnakum wala tatghaw feehi fayahillaAAalaykum ghadabee
waman yahlil AAalayhi ghadabeefaqad hawa
Swahili
Kuleni katika vitu vizuri hivyo tulivyo kuruzukuni, wala msiruke mipaka katika
hayo, isije ikakushukieni ghadhabu yangu. Na inaye mshukia ghadhabu yangu basi
huyo ameangamia.
|
Ayah 20:82 الأية
وَإِنِّي لَغَفَّارٌ لِّمَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا ثُمَّ اهْتَدَىٰ
Wa-innee laghaffarun liman tabawaamana waAAamila salihan thumma ihtada
Swahili
Na hakika Mimi ni Mwingi wa Kusamehe kwa anaye tubia, na akaamini, na akatenda
mema, tena akaongoka.
|
Ayah 20:83 الأية
وَمَا أَعْجَلَكَ عَن قَوْمِكَ يَا مُوسَىٰ
Wama aAAjalaka AAan qawmika yamoosa
Swahili
Na nini kilicho kutia haraka ukawaacha watu wako, ewe Musa?
|
Ayah 20:84 الأية
قَالَ هُمْ أُولَاءِ عَلَىٰ أَثَرِي وَعَجِلْتُ إِلَيْكَ رَبِّ لِتَرْضَىٰ
Qala hum ola-i AAalaatharee waAAajiltu ilayka rabbi litarda
Swahili
Akasema: Hao wapo nyuma yangu wananifuatia. Na nimefanya haraka kukujia, Mola
wangu Mlezi, ili uridhike.
|
Ayah 20:85 الأية
قَالَ فَإِنَّا قَدْ فَتَنَّا قَوْمَكَ مِن بَعْدِكَ وَأَضَلَّهُمُ السَّامِرِيُّ
Qala fa-inna qad fatannaqawmaka min baAAdika waadallahumu assamiriy
Swahili
(Mwenyezi Mungu) akasema: Sisi tumewatia mtihani watu wako baada yako, na
Msamaria amewapoteza.
|
Ayah 20:86 الأية
فَرَجَعَ مُوسَىٰ إِلَىٰ قَوْمِهِ غَضْبَانَ أَسِفًا ۚ قَالَ يَا قَوْمِ أَلَمْ
يَعِدْكُمْ رَبُّكُمْ وَعْدًا حَسَنًا ۚ أَفَطَالَ عَلَيْكُمُ الْعَهْدُ أَمْ
أَرَدتُّمْ أَن يَحِلَّ عَلَيْكُمْ غَضَبٌ مِّن رَّبِّكُمْ فَأَخْلَفْتُم
مَّوْعِدِي
FarajaAAa moosa ila qawmihighadbana asifan qala ya qawmi alamyaAAidkum rabbukum
waAAdan hasanan afatalaAAalaykumu alAAahdu am aradtum an yahilla AAalaykum
ghadabunmin rabbikum faakhlaftum mawAAidee
Swahili
Musa akarudi kwa watu wake kwa ghadhabu na kusikitika. Akasema: Enyi watu wangu!
Kwani Mola wenu Mlezi hakukuahidini ahadi nzuri? Je, umekuwa muda mrefu kwenu au
mmetaka ikushukieni ghadhabu ya Mola wenu Mlezi, ndio maana mkavunja miadi
yangu?
|
Ayah 20:87 الأية
قَالُوا مَا أَخْلَفْنَا مَوْعِدَكَ بِمَلْكِنَا وَلَٰكِنَّا حُمِّلْنَا أَوْزَارًا
مِّن زِينَةِ الْقَوْمِ فَقَذَفْنَاهَا فَكَذَٰلِكَ أَلْقَى السَّامِرِيُّ
Qaloo ma akhlafnamawAAidaka bimalkina walakinna hummilnaawzaran min zeenati
alqawmi faqathafnahafakathalika alqa assamiriy
Swahili
Wakasema: Sisi hatukuvunja miadi yako kwa khiari yetu, lakini tulibebeshwa
mizigo ya mapambo ya watu, basi tukaitupa. Na hivyo ndivyo alivyo toa shauri
Msamaria.
|
Ayah 20:88 الأية
فَأَخْرَجَ لَهُمْ عِجْلًا جَسَدًا لَّهُ خُوَارٌ فَقَالُوا هَٰذَا إِلَٰهُكُمْ
وَإِلَٰهُ مُوسَىٰ فَنَسِيَ
Faakhraja lahum AAijlan jasadan lahu khuwarunfaqaloo hatha ilahukum wa-ilahu
moosafanasiy
Swahili
Na akawaundia ndama, kiwiliwili chenye sauti. Na wakasema: Huyu ndiye mungu
wenu, na mungu wa Musa, lakini alisahau.
|
Ayah 20:89 الأية
أَفَلَا يَرَوْنَ أَلَّا يَرْجِعُ إِلَيْهِمْ قَوْلًا وَلَا يَمْلِكُ لَهُمْ ضَرًّا
وَلَا نَفْعًا
Afala yarawna alla yarjiAAuilayhim qawlan wala yamliku lahum darran walanafAAa
Swahili
Je! Hawakuona kuwa hakuwarudishia neno, wala hakuweza kuwadhuru wala kuwafaa?
|
Ayah 20:90 الأية
وَلَقَدْ قَالَ لَهُمْ هَارُونُ مِن قَبْلُ يَا قَوْمِ إِنَّمَا فُتِنتُم بِهِ ۖ
وَإِنَّ رَبَّكُمُ الرَّحْمَٰنُ فَاتَّبِعُونِي وَأَطِيعُوا أَمْرِي
Walaqad qala lahum haroonu minqablu ya qawmi innama futintum bihi
wa-innarabbakumu arrahmanu fattabiAAooneewaateeAAoo amree
Swahili
Na hakika Harun alikwisha waambia kabla yake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi
mmetiwa mtihanini tu kwa kitu hiki. Na kwa yakini Mola wenu Mlezi ni Arrahmani,
Mwingi wa Rehema. Basi nifuateni mimi, na t'iini amri yangu!
|
Ayah 20:91 الأية
قَالُوا لَن نَّبْرَحَ عَلَيْهِ عَاكِفِينَ حَتَّىٰ يَرْجِعَ إِلَيْنَا مُوسَىٰ
Qaloo lan nabraha AAalayhi AAakifeenahatta yarjiAAa ilayna moosa
Swahili
Wakasema: Hatutaacha kumuabudu mpaka Musa atapo rejea kwetu.
|
Ayah 20:92 الأية
قَالَ يَا هَارُونُ مَا مَنَعَكَ إِذْ رَأَيْتَهُمْ ضَلُّوا
Qala ya haroonu mamanaAAaka ith raaytahum dalloo
Swahili
(Musa) akasema: Ewe Harun! Ni nini kilicho kuzuia, ulipo waona wamepotea,
|
Ayah 20:93 الأية
أَلَّا تَتَّبِعَنِ ۖ أَفَعَصَيْتَ أَمْرِي
Alla tattabiAAani afaAAasaytaamree
Swahili
Hata usinifuate? Je, umeasi amri yangu?
|
Ayah 20:94 الأية
قَالَ يَا ابْنَ أُمَّ لَا تَأْخُذْ بِلِحْيَتِي وَلَا بِرَأْسِي ۖ إِنِّي خَشِيتُ
أَن تَقُولَ فَرَّقْتَ بَيْنَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلَمْ تَرْقُبْ قَوْلِي
Qala yabnaomma la ta/khuthbilihyatee wala bira/see innee khasheetu an
taqoolafarraqta bayna banee isra-eela walam tarqub qawlee
Swahili
Akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Usinishike ndevu zangu, wala kichwa changu.
Kwa hakika naliogopa usije sema: Umewafarikisha Wana wa Israil, na hukungojea
kauli yangu.
|
Ayah 20:95 الأية
قَالَ فَمَا خَطْبُكَ يَا سَامِرِيُّ
Qala fama khatbuka yasamiriy
Swahili
(Musa) akasema: Ewe Msamaria! Unataka nini ?
|
Ayah 20:96 الأية
قَالَ بَصُرْتُ بِمَا لَمْ يَبْصُرُوا بِهِ فَقَبَضْتُ قَبْضَةً مِّنْ أَثَرِ
الرَّسُولِ فَنَبَذْتُهَا وَكَذَٰلِكَ سَوَّلَتْ لِي نَفْسِي
Qala basurtu bima lamyabsuroo bihi faqabadtu qabdatan min athariarrasooli
fanabathtuha wakathalikasawwalat lee nafsee
Swahili
Akasema: Niliona wasiyo yaona wao, nikashika gao katika unyao wa Mtume. Kisha
nikalitupa. Na hivi ndivyo ilivyo nielekeza nafsi yangu.
|
Ayah 20:97 الأية
قَالَ فَاذْهَبْ فَإِنَّ لَكَ فِي الْحَيَاةِ أَن تَقُولَ لَا مِسَاسَ ۖ وَإِنَّ
لَكَ مَوْعِدًا لَّن تُخْلَفَهُ ۖ وَانظُرْ إِلَىٰ إِلَٰهِكَ الَّذِي ظَلْتَ
عَلَيْهِ عَاكِفًا ۖ لَّنُحَرِّقَنَّهُ ثُمَّ لَنَنسِفَنَّهُ فِي الْيَمِّ نَسْفًا
Qala fathhab fa-innalaka fee alhayati an taqoola la misasawa-inna laka mawAAidan
lan tukhlafahu wanthurila ilahika allathee thaltaAAalayhi AAakifan
lanuharriqannahu thummalanansifannahu fee alyammi nasfa
Swahili
(Musa) akasema: Basi ondoka! Na kwa yakini utakuwa katika maisha ukisema:
Usiniguse. Na hakika una ahadi kwako isiyo vunjwa. Na mtazame huyo mungu wako
uliye endelea kumuabudu - Sisi kwa hakika tutamchoma moto, kisha tutamtawanya
baharini atawanyike.
|
Ayah 20:98 الأية
إِنَّمَا إِلَٰهُكُمُ اللَّهُ الَّذِي لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ وَسِعَ كُلَّ
شَيْءٍ عِلْمًا
Innama ilahukumu Allahuallathee la ilaha illa huwa wasiAAakulla shay-in AAilma
Swahili
Hakika Mungu wenu ni Allah, Mwenyezi Mungu, tu. Hapana Mungu isipo kuwa Yeye.
Ujuzi wake umeenea kila kitu.
|
Ayah 20:99 الأية
كَذَٰلِكَ نَقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنبَاءِ مَا قَدْ سَبَقَ ۚ وَقَدْ آتَيْنَاكَ مِن
لَّدُنَّا ذِكْرًا
Kathalika naqussu AAalayka minanba-i ma qad sabaqa waqad ataynakamin ladunna
thikra
Swahili
Namna hivi tunakuhadithia katika khabari za yaliyo tangulia. Na hakika
tumekuletea kutoka kwetu mawaidha ya kukumbukwa.
|
Ayah 20:100 الأية
مَّنْ أَعْرَضَ عَنْهُ فَإِنَّهُ يَحْمِلُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وِزْرًا
Man aAArada AAanhu fa-innahu yahmiluyawma alqiyamati wizra
Swahili
Atakaye jitenga nayo, basi kwa yakini Siku ya Kiyama atabeba mzigo.
|
Ayah 20:101 الأية
خَالِدِينَ فِيهِ ۖ وَسَاءَ لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ حِمْلًا
Khalideena feehi wasaa lahumyawma alqiyamati himla
Swahili
Wadumu humo. Na ni mzigo muovu kwao kuubeba Siku ya Kiyama!
|
Ayah 20:102 الأية
يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ ۚ وَنَحْشُرُ الْمُجْرِمِينَ يَوْمَئِذٍ زُرْقًا
Yawma yunfakhu fee assooriwanahshuru almujrimeena yawma-ithin zurqa
Swahili
Siku litakapo pulizwa barugumu, na tukawakusanya wakhalifu Siku hiyo, hali macho
yao ya kibuluu.
|
Ayah 20:103 الأية
يَتَخَافَتُونَ بَيْنَهُمْ إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا عَشْرًا
Yatakhafatoona baynahum in labithtumilla AAashra
Swahili
Watanong'onezana wao kwa wao: Hamkukaa ila siku kumi tu.
|
Ayah 20:104 الأية
نَّحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَقُولُونَ إِذْ يَقُولُ أَمْثَلُهُمْ طَرِيقَةً إِن
لَّبِثْتُمْ إِلَّا يَوْمًا
Nahnu aAAlamu bima yaqooloonaith yaqoolu amthaluhum tareeqatan in labithtum
illayawma
Swahili
Sisi tunajua zaidi watakayo yasema, atakapo sema mbora wao katika mwendo: Nyinyi
hamkukaa ila siku moja tu.
|
Ayah 20:105 الأية
وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْجِبَالِ فَقُلْ يَنسِفُهَا رَبِّي نَسْفًا
Wayas-aloonaka AAani aljibali faqulyansifuha rabbee nasfa
Swahili
Na wanakuuliza khabari za milima. Waambie: Mola wangu Mlezi ataivuruga vuruga.
|
Ayah 20:106 الأية
فَيَذَرُهَا قَاعًا صَفْصَفًا
Fayatharuha qaAAan safsafa
Swahili
Na ataiacha tambarare, uwanda.
|
Ayah 20:107 الأية
لَّا تَرَىٰ فِيهَا عِوَجًا وَلَا أَمْتًا
La tara feeha AAiwajanwala amta
Swahili
Hutaona humo mdidimio wala muinuko.
|
Ayah 20:108 الأية
يَوْمَئِذٍ يَتَّبِعُونَ الدَّاعِيَ لَا عِوَجَ لَهُ ۖ وَخَشَعَتِ الْأَصْوَاتُ
لِلرَّحْمَٰنِ فَلَا تَسْمَعُ إِلَّا هَمْسًا
Yawma-ithin yattabiAAoona addaAAiyala AAiwaja lahu wakhashaAAati al-aswatu
lirrahmanifala tasmaAAu illa hamsa
Swahili
Siku hiyo watamfuata muitaji asiye na upotofu. Na sauti zote zitamnyenyekea
Arrahmani Mwingi wa Rahema. Basi husikii ila mchakato na mnong'ono.
|
Ayah 20:109 الأية
يَوْمَئِذٍ لَّا تَنفَعُ الشَّفَاعَةُ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ الرَّحْمَٰنُ
وَرَضِيَ لَهُ قَوْلًا
Yawma-ithin la tanfaAAu ashshafaAAatuilla man athina lahu arrahmanuwaradiya lahu
qawla
Swahili
Siku hiyo uombezi haufai kitu, ila wa aliye mruhusu Arrahmani Mwingi wa Rehema
na akamridhia kusema.
|
Ayah 20:110 الأية
يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا
YaAAlamu ma bayna aydeehim wamakhalfahum wala yuheetoona bihi AAilma
Swahili
Yeye anajua yaliyo mbele yao, na yaliyo nyuma yao. Wala wao hawawezi kumjua Yeye
vilivyo.
|
Ayah 20:111 الأية
وَعَنَتِ الْوُجُوهُ لِلْحَيِّ الْقَيُّومِ ۖ وَقَدْ خَابَ مَنْ حَمَلَ ظُلْمًا
WaAAanati alwujoohu lilhayyialqayyoomi waqad khaba man hamala thulma
Swahili
Na zitadhalilika nyuso mbele ya Aliye Hai Milele, Mwangalizi Mkuu. Na atakuwa
ameharibikiwa mwenye kubeba dhulma.
|
Ayah 20:112 الأية
وَمَن يَعْمَلْ مِنَ الصَّالِحَاتِ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَا يَخَافُ ظُلْمًا وَلَا
هَضْمًا
Waman yaAAmal mina assalihatiwahuwa mu/minun fala yakhafu thulmanwala hadma
Swahili
Na anaye tenda mema, naye ni Muumini, basi hatakhofu kudhulumiwa wala kupunjwa.
|
Ayah 20:113 الأية
وَكَذَٰلِكَ أَنزَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا وَصَرَّفْنَا فِيهِ مِنَ الْوَعِيدِ
لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ أَوْ يُحْدِثُ لَهُمْ ذِكْرًا
Wakathalika anzalnahu qur-ananAAarabiyyan wasarrafna feehi mina
alwaAAeedilaAAallahum yattaqoona aw yuhdithu lahum thikra
Swahili
Na namna hivi tumeiteremsha Qur'ani kwa Kiarabu, na tumekariri humo maonyo ili
wapate kuogopa na kujilinda na iwaletee makumbusho.
|
Ayah 20:114 الأية
فَتَعَالَى اللَّهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ ۗ وَلَا تَعْجَلْ بِالْقُرْآنِ مِن قَبْلِ
أَن يُقْضَىٰ إِلَيْكَ وَحْيُهُ ۖ وَقُل رَّبِّ زِدْنِي عِلْمًا
FataAAala Allahualmaliku alhaqqu wala taAAjal bilqur-animin qabli an yuqda
ilayka wahyuhu waqul rabbizidnee AAilma
Swahili
Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki. Wala usiifanyie haraka hii Qur'ani,
kabla haujamalizika ufunuo wake. Na sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie ilimu.
|
Ayah 20:115 الأية
وَلَقَدْ عَهِدْنَا إِلَىٰ آدَمَ مِن قَبْلُ فَنَسِيَ وَلَمْ نَجِدْ لَهُ عَزْمًا
Walaqad AAahidna ila adamamin qablu fanasiya walam najid lahu AAazma
Swahili
Na hapo zamani tuliagana na Adam, lakini alisahau, wala hatukuona kwake azma
kubwa.
|
Ayah 20:116 الأية
وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ
أَبَىٰ
Wa-ith qulna lilmala-ikatiosjudoo li-adama fasajadoo illa ibleesa aba
Swahili
Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam! Wakasujudu, isipo kuwa Iblisi,
alikataa.
|
|