1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
ص ۚ وَالْقُرْآنِ ذِي الذِّكْرِ
Sad walqur-ani theeaththikr
Swahili
S'ad, Naapa kwa Qur'ani yenye mawaidha.
|
Ayah 38:2 الأية
بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي عِزَّةٍ وَشِقَاقٍ
Bali allatheena kafaroo fee AAizzatinwashiqaq
Swahili
Lakini walio kufuru wamo katika majivuno na upinzani
|
Ayah 38:3 الأية
كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّن قَرْنٍ فَنَادَوا وَّلَاتَ حِينَ مَنَاصٍ
Kam ahlakna min qablihim min qarninfanadaw walata heena manas
Swahili
Mataifa mangapi tumeyaangamiza kabla yao, na wakapiga kelele, lakini wakati wa
kuokoka ulikwisha pita.
|
Ayah 38:4 الأية
وَعَجِبُوا أَن جَاءَهُم مُّنذِرٌ مِّنْهُمْ ۖ وَقَالَ الْكَافِرُونَ هَٰذَا
سَاحِرٌ كَذَّابٌ
WaAAajiboo an jaahum munthirunminhum waqala alkafiroona hatha sahirunkaththab
Swahili
Na walistaajabu kuwajia mwonyaji anaye tokana nao wenyewe, na makafiri wakasema:
Huyu ni mchawi, mwongo.
|
Ayah 38:5 الأية
أَجَعَلَ الْآلِهَةَ إِلَٰهًا وَاحِدًا ۖ إِنَّ هَٰذَا لَشَيْءٌ عُجَابٌ
AjaAAala al-alihata ilahan wahidaninna hatha lashay-on AAujab
Swahili
Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu.
|
Ayah 38:6 الأية
وَانطَلَقَ الْمَلَأُ مِنْهُمْ أَنِ امْشُوا وَاصْبِرُوا عَلَىٰ آلِهَتِكُمْ ۖ
إِنَّ هَٰذَا لَشَيْءٌ يُرَادُ
Wantalaqa almalao minhum aniimshoo wasbiroo AAala alihatikuminna hatha lashay-on
yurad
Swahili
Na wakaondoka wakubwa wao wakiwaambia: Nendeni zenu na dumuni na miungu yenu,
kwani hili ni jambo lililo pangwa.
|
Ayah 38:7 الأية
مَا سَمِعْنَا بِهَٰذَا فِي الْمِلَّةِ الْآخِرَةِ إِنْ هَٰذَا إِلَّا اخْتِلَاقٌ
Ma samiAAna bihatha feealmillati al-akhirati in hatha illa ikhtilaq
Swahili
Sisi hatukusikia haya katika mila hii ya mwisho. Haya si chochote ila ni uzushi
tu.
|
Ayah 38:8 الأية
أَأُنزِلَ عَلَيْهِ الذِّكْرُ مِن بَيْنِنَا ۚ بَلْ هُمْ فِي شَكٍّ مِّن ذِكْرِي ۖ
بَل لَّمَّا يَذُوقُوا عَذَابِ
Aonzila AAalayhi aththikru minbaynina bal hum fee shakkin min thikree bal
lammayathooqoo AAathab
Swahili
Ati yeye tu ndiye aliye teremshiwa mawaidha peke yake katika sisi? Lakini hao
wana shaka na mawaidha yangu, bali hawajaionja adhabu yangu.
|
Ayah 38:9 الأية
أَمْ عِندَهُمْ خَزَائِنُ رَحْمَةِ رَبِّكَ الْعَزِيزِ الْوَهَّابِ
Am AAindahum khaza-inu rahmatirabbika alAAazeezi alwahhab
Swahili
Au wanazo wao khazina za rehema za Mola wako Mlezi, Mwenye nguvu, Mpaji?
|
Ayah 38:10 الأية
أَمْ لَهُم مُّلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ فَلْيَرْتَقُوا
فِي الْأَسْبَابِ
Am lahum mulku assamawatiwal-ardi wama baynahuma falyartaqoofee al-asbab
Swahili
Au wao wana ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo kati yao? Basi nawazipande njia
za kwendea huko!
|
Ayah 38:11 الأية
جُندٌ مَّا هُنَالِكَ مَهْزُومٌ مِّنَ الْأَحْزَابِ
Jundun ma hunalika mahzoomunmina al-ahzab
Swahili
Hao ni askari watao shindwa miongoni mwa makundi yatayo shindwa.
|
Ayah 38:12 الأية
كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَعَادٌ وَفِرْعَوْنُ ذُو الْأَوْتَادِ
Kaththabat qablahum qawmu noohinwaAAadun wafirAAawnu thoo al-awtad
Swahili
Walikanusha kabla yao kaumu ya Nuhu, na kina A'adi na Firauni mwenye majengo.
|
Ayah 38:13 الأية
وَثَمُودُ وَقَوْمُ لُوطٍ وَأَصْحَابُ الْأَيْكَةِ ۚ أُولَٰئِكَ الْأَحْزَابُ
Wathamoodu waqawmu lootin waas-habual-aykati ola-ika al-ahzab
Swahili
Na Thamud na kaumu Lut'i na watu wa Machakani. Hayo ndiyo makundi.
|
Ayah 38:14 الأية
إِن كُلٌّ إِلَّا كَذَّبَ الرُّسُلَ فَحَقَّ عِقَابِ
In kullun illa kaththaba arrusulafahaqqa AAiqab
Swahili
Hao wote waliwakadhibisha Mitume; basi wakastahiki adhabu yangu.
|
Ayah 38:15 الأية
وَمَا يَنظُرُ هَٰؤُلَاءِ إِلَّا صَيْحَةً وَاحِدَةً مَّا لَهَا مِن فَوَاقٍ
Wama yanthuru haola-iilla sayhatan wahidatan ma lahamin fawaq
Swahili
Na hawa hawangojei ila ukelele mmoja tu usio na muda.
|
Ayah 38:16 الأية
وَقَالُوا رَبَّنَا عَجِّل لَّنَا قِطَّنَا قَبْلَ يَوْمِ الْحِسَابِ
Waqaloo rabbana AAajjil lanaqittana qabla yawmi alhisab
Swahili
Na wao husema: Mola wetu Mlezi! Tuletee upesi sehemu yetu ya adhabu kabla ya
Siku ya Hisabu.
|
Ayah 38:17 الأية
اصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَاذْكُرْ عَبْدَنَا دَاوُودَ ذَا الْأَيْدِ ۖ
إِنَّهُ أَوَّابٌ
Isbir AAala mayaqooloona wathkur AAabdana dawooda thaal-aydi innahu awwab
Swahili
Subiri kwa hayo wayasemayo, na umkumbuke mja wetu Daudi, mwenye nguvu. Hakika
yeye alikuwa mwingi wa kutubia.
|
Ayah 38:18 الأية
إِنَّا سَخَّرْنَا الْجِبَالَ مَعَهُ يُسَبِّحْنَ بِالْعَشِيِّ وَالْإِشْرَاقِ
Inna sakhkharna aljibalamaAAahu yusabbihna bilAAashiyyi wal-ishraq
Swahili
Hakika tuliidhalilisha milima pamoja naye ikisabihi jioni na asubuhi pamoja
naye.
|
Ayah 38:19 الأية
وَالطَّيْرَ مَحْشُورَةً ۖ كُلٌّ لَّهُ أَوَّابٌ
Wattayra mahshooratankullun lahu awwab
Swahili
Na pia ndege walio kusanywa makundi kwa makundi; wote walikuwa wanyenyekevu
kwake.
|
Ayah 38:20 الأية
وَشَدَدْنَا مُلْكَهُ وَآتَيْنَاهُ الْحِكْمَةَ وَفَصْلَ الْخِطَابِ
Washadadna mulkahu waataynahualhikmata wafasla alkhitab
Swahili
Na tukautia nguvu ufalme wake, na tukampa hikima, na kukata hukumu.
|
Ayah 38:21 الأية
وَهَلْ أَتَاكَ نَبَأُ الْخَصْمِ إِذْ تَسَوَّرُوا الْمِحْرَابَ
Wahal ataka nabao alkhasmi ithtasawwaroo almihrab
Swahili
Na je! Imekufikia khabari ya wagombanao walipo pindukia ukuta kuingia chumbani?
|
Ayah 38:22 الأية
إِذْ دَخَلُوا عَلَىٰ دَاوُودَ فَفَزِعَ مِنْهُمْ ۖ قَالُوا لَا تَخَفْ ۖ خَصْمَانِ
بَغَىٰ بَعْضُنَا عَلَىٰ بَعْضٍ فَاحْكُم بَيْنَنَا بِالْحَقِّ وَلَا تُشْطِطْ
وَاهْدِنَا إِلَىٰ سَوَاءِ الصِّرَاطِ
Ith dakhaloo AAala dawoodafafaziAAa minhum qaloo la takhaf khasmanibagha
baAAduna AAala baAAdinfahkum baynana bilhaqqi walatushtit wahdina ila
sawa-iassirat
Swahili
Walipo muingilia Daudi, naye akawaogopa. Wakasema: Usiogope! Sisi ni wagombanao
wawili, mmoja wetu amemdhulumu mwenziwe. Basi tuhukumu kwa haki, wala
usipendelee. Na utuongoe kwenye njia iliyo sawa.
|
Ayah 38:23 الأية
إِنَّ هَٰذَا أَخِي لَهُ تِسْعٌ وَتِسْعُونَ نَعْجَةً وَلِيَ نَعْجَةٌ وَاحِدَةٌ
فَقَالَ أَكْفِلْنِيهَا وَعَزَّنِي فِي الْخِطَابِ
Inna hatha akhee lahu tisAAunwatisAAoona naAAjatan waliya naAAjatun wahidatun
faqalaakfilneeha waAAazzanee fee alkhitab
Swahili
Hakika huyu ndugu yangu ana kondoo wa kike tisiini na tisa; na mimi ninaye
kondoo mke mmoja. Akasema: Nipe huyo nikufugie! Na amenishinda kwa maneno.
|
Ayah 38:24 الأية
قَالَ لَقَدْ ظَلَمَكَ بِسُؤَالِ نَعْجَتِكَ إِلَىٰ نِعَاجِهِ ۖ وَإِنَّ كَثِيرًا
مِّنَ الْخُلَطَاءِ لَيَبْغِي بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا
وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَقَلِيلٌ مَّا هُمْ ۗ وَظَنَّ دَاوُودُ أَنَّمَا
فَتَنَّاهُ فَاسْتَغْفَرَ رَبَّهُ وَخَرَّ رَاكِعًا وَأَنَابَ ۩
Qala laqad thalamakabisu-ali naAAjatika ila niAAajihi wa-innakatheeran mina
alkhulata-i layabghee baAAduhum AAalabaAAdin illa allatheena amanoowaAAamiloo
assalihati waqaleelun mahum wathanna dawoodu annama fatannahufastaghfara rabbahu
wakharra rakiAAan waanab
Swahili
Akasema: Kweli amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako mmoja kuongezea kwenye
kondoo wake. Na hakika washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao, isipo kuwa
walio amini na wakatenda mema. Na hao ni wachache. Na Daudi akajua kuwa
tumemfanyia mtihani. Basi akamwomba msamaha Mola wake Mlezi, na akaanguka
kusujudu na kutubia.
|
Ayah 38:25 الأية
فَغَفَرْنَا لَهُ ذَٰلِكَ ۖ وَإِنَّ لَهُ عِندَنَا لَزُلْفَىٰ وَحُسْنَ مَآبٍ
Faghafarna lahu thalikawa-inna lahu AAindana lazulfa wahusna maab
Swahili
Basi tukamsamehe kwa hayo. Naye kwa hakika anao mkaribisho mkubwa na marejeo
mazuri kwetu.
|
Ayah 38:26 الأية
يَا دَاوُودُ إِنَّا جَعَلْنَاكَ خَلِيفَةً فِي الْأَرْضِ فَاحْكُم بَيْنَ النَّاسِ
بِالْحَقِّ وَلَا تَتَّبِعِ الْهَوَىٰ فَيُضِلَّكَ عَن سَبِيلِ اللهِ ۚ إِنَّ
الَّذِينَ يَضِلُّونَ عَن سَبِيلِ اللهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا نَسُوا
يَوْمَ الْحِسَابِ
Ya dawoodu inna jaAAalnakakhaleefatan fee al-ardi fahkum bayna annasibilhaqqi
wala tattabiAAi alhawa fayudillakaAAan sabeeli Allahi inna allatheena
yadilloonaAAan sabeeli Allahi lahum AAathabun shadeedun bimanasoo yawma alhisab
Swahili
Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi. Basi wahukumu
watu kwa haki, wala usifuate matamanio yakakupoteza kwenye Njia ya Mwenyezi
Mungu. Hakika wanao ipotea Njia ya Mwenyezi Mungu wakaiacha, watapata adhabu
kali kwa sababu ya kusahau kwao Siku ya Hisabu.
|
Ayah 38:27 الأية
وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاءَ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا بَاطِلًا ۚ ذَٰلِكَ
ظَنُّ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا مِنَ النَّارِ
Wama khalaqna assamaawal-arda wama baynahuma batilanthalika thannu allatheena
kafaroofawaylun lillatheena kafaroo mina annar
Swahili
Na hatukuziumba mbingu na ardhi na viliomo ndani yao bure. Hiyo ni dhana ya
walio kufuru. Ole wao walio kufuru kwa Moto utao wapata.
|
Ayah 38:28 الأية
أَمْ نَجْعَلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ كَالْمُفْسِدِينَ فِي
الْأَرْضِ أَمْ نَجْعَلُ الْمُتَّقِينَ كَالْفُجَّارِ
Am najAAalu allatheena amanoowaAAamiloo assalihati kalmufsideenafee al-ardi am
najAAalu almuttaqeena kalfujjar
Swahili
Je! Tuwafanye walio amini na wakatenda mema kama wafanyao uharibifu katika nchi?
Au tuwafanye wachamngu kama waovu?
|
Ayah 38:29 الأية
كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ
أُولُو الْأَلْبَابِ
Kitabun anzalnahu ilayka mubarakunliyaddabbaroo ayatihi waliyatathakkara
olooal-albab
Swahili
Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake,
na wawaidhike wenye akili.
|
Ayah 38:30 الأية
وَوَهَبْنَا لِدَاوُودَ سُلَيْمَانَ ۚ نِعْمَ الْعَبْدُ ۖ إِنَّهُ أَوَّابٌ
Wawahabna lidawooda sulaymananiAAma alAAabdu innahu awwab
Swahili
Na Daudi tukamtunukia Suleiman. Alikuwa mja mwema. Na hakika alikuwa mwingi wa
kutubia.
|
Ayah 38:31 الأية
إِذْ عُرِضَ عَلَيْهِ بِالْعَشِيِّ الصَّافِنَاتُ الْجِيَادُ
Ith AAurida AAalayhi bilAAashiyyiassafinatu aljiyad
Swahili
Alipo pelekewa jioni farasi wasimamao kidete, tayari kutoka shoti;
|
Ayah 38:32 الأية
فَقَالَ إِنِّي أَحْبَبْتُ حُبَّ الْخَيْرِ عَن ذِكْرِ رَبِّي حَتَّىٰ تَوَارَتْ
بِالْحِجَابِ
Faqala innee ahbabtu hubbaalkhayri AAan thikri rabbee hatta tawaratbilhijab
Swahili
Basi akasema: Navipenda vitu vizuri kwa kumkumbuka Mola wangu Mlezi. Kisha
wakafichikana nyuma ya boma.
|
Ayah 38:33 الأية
رُدُّوهَا عَلَيَّ ۖ فَطَفِقَ مَسْحًا بِالسُّوقِ وَالْأَعْنَاقِ
Ruddooha AAalayya fatafiqa mashanbissooqi wal-aAAnaq
Swahili
(Akasema:) Nirudishieni! Akaanza kuwapapasa miguu na shingo.
|
Ayah 38:34 الأية
وَلَقَدْ فَتَنَّا سُلَيْمَانَ وَأَلْقَيْنَا عَلَىٰ كُرْسِيِّهِ جَسَدًا ثُمَّ
أَنَابَ
Walaqad fatanna sulaymanawaalqayna AAala kursiyyihi jasadan thumma anab
Swahili
Na tulimtia mtihanini Suleiman, na tukauweka mwili juu ya kiti chake, kisha
akarejea kwa kutubu.
|
Ayah 38:35 الأية
قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي وَهَبْ لِي مُلْكًا لَّا يَنبَغِي لِأَحَدٍ مِّن بَعْدِي ۖ
إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ
Qala rabbi ighfir lee wahab leemulkan la yanbaghee li-ahadin min baAAdee
innakaanta alwahhab
Swahili
Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usio mwelekea yeyote baada
yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji.
|
Ayah 38:36 الأية
فَسَخَّرْنَا لَهُ الرِّيحَ تَجْرِي بِأَمْرِهِ رُخَاءً حَيْثُ أَصَابَ
Fasakhkharna lahu arreehatajree bi-amrihi rukhaan haythu asab
Swahili
Basi tukaufanya upepo umtumikie, ukenda kwa amri yake, popote alipo taka kufika.
|
Ayah 38:37 الأية
وَالشَّيَاطِينَ كُلَّ بَنَّاءٍ وَغَوَّاصٍ
Washshayateena kulla banna-inwaghawwas
Swahili
Na tukayafanya mashet'ani yamtumikie, wote wajenzi na wapiga mbizi.
|
Ayah 38:38 الأية
وَآخَرِينَ مُقَرَّنِينَ فِي الْأَصْفَادِ
Waakhareena muqarraneena fee al-asfad
Swahili
Na wengine wafungwao kwa minyororo.
|
Ayah 38:39 الأية
هَٰذَا عَطَاؤُنَا فَامْنُنْ أَوْ أَمْسِكْ بِغَيْرِ حِسَابٍ
Hatha AAataona famnunaw amsik bighayri hisab
Swahili
Hichi ndicho kipawa chetu. Basi toa au zuia, bila ya hisabu.
|
Ayah 38:40 الأية
وَإِنَّ لَهُ عِندَنَا لَزُلْفَىٰ وَحُسْنَ مَآبٍ
Wa-inna lahu AAindana lazulfawahusna maab
Swahili
Na hakika yeye kwetu Sisi ana cheo cha kukaribishwa kwetu, na pahala pazuri pa
kurejea.
|
Ayah 38:41 الأية
وَاذْكُرْ عَبْدَنَا أَيُّوبَ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ أَنِّي مَسَّنِيَ الشَّيْطَانُ
بِنُصْبٍ وَعَذَابٍ
Wathkur AAabdanaayyooba ith nada rabbahu annee massaniya ashshaytanubinusbin
waAAathab
Swahili
Na mkumbuke mja wetu Ayubu alipo mwita Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika
Shet'ani amenifikishia udhia na adhabu.
|
Ayah 38:42 الأية
ارْكُضْ بِرِجْلِكَ ۖ هَٰذَا مُغْتَسَلٌ بَارِدٌ وَشَرَابٌ
Orkud birijlika hathamughtasalun baridun washarab
Swahili
(Akaambiwa:) Piga-piga ardhi kwa mguu wako! Basi haya maji baridi ya kuogea na
ya kunywa.
|
Ayah 38:43 الأية
وَوَهَبْنَا لَهُ أَهْلَهُ وَمِثْلَهُم مَّعَهُمْ رَحْمَةً مِّنَّا وَذِكْرَىٰ
لِأُولِي الْأَلْبَابِ
Wawahabna lahu ahlahu wamithlahummaAAahum rahmatan minna wathikrali-olee
al-albab
Swahili
Na tukampa ahali zake na wengine kama wao pamoja nao, kuwa ni rehema itokayo
kwetu, na iwe kumbusho kwa watu wenye akili.
|
Ayah 38:44 الأية
وَخُذْ بِيَدِكَ ضِغْثًا فَاضْرِب بِّهِ وَلَا تَحْنَثْ ۗ إِنَّا وَجَدْنَاهُ
صَابِرًا ۚ نِّعْمَ الْعَبْدُ ۖ إِنَّهُ أَوَّابٌ
Wakhuth biyadika dighthan fadribbihi wala tahnath inna wajadnahu sabiranniAAma
alAAabdu innahu awwab
Swahili
Na shika kicha cha vijiti tu mkononi mwako, kisha ndio upigie nacho, wala
usivunje kiapo. Hakika tulimkuta mwenye subira, mbora wa waja, kwa hakika
alikuwa mwingi wa kutubu.
|
Ayah 38:45 الأية
وَاذْكُرْ عِبَادَنَا إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ أُولِي الْأَيْدِي
وَالْأَبْصَارِ
Wathkur AAibadanaibraheema wa-ishaqa wayaAAqooba olee al-aydee wal-absar
Swahili
Na wakumbuke waja wetu, Ibrahim na Is-haqa na Yaa'qubu walio kuwa na nguvu na
busara.
|
Ayah 38:46 الأية
إِنَّا أَخْلَصْنَاهُم بِخَالِصَةٍ ذِكْرَى الدَّارِ
Inna akhlasnahum bikhalisatinthikra addar
Swahili
Sisi tumewakhusisha wao kwa sifa ya ukumbusho wa Akhera.
|
Ayah 38:47 الأية
وَإِنَّهُمْ عِندَنَا لَمِنَ الْمُصْطَفَيْنَ الْأَخْيَارِ
Wa-innahum AAindana lamina almustafaynaal-akhyar
Swahili
Na hakika wao kwetu sisi ni wateuliwa walio bora.
|
Ayah 38:48 الأية
وَاذْكُرْ إِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَذَا الْكِفْلِ ۖ وَكُلٌّ مِّنَ الْأَخْيَارِ
Wathkur ismaAAeelawa-ilyasaAAa watha alkifli wakullun mina al-akhyar
Swahili
Na mkumbuke Ismail na Alyasaa na Dhulkifli, na wote hao ni katika walio bora.
|
Ayah 38:49 الأية
هَٰذَا ذِكْرٌ ۚ وَإِنَّ لِلْمُتَّقِينَ لَحُسْنَ مَآبٍ
Hatha thikrun wa-innalilmuttaqeena lahusna maab
Swahili
Huu ni ukumbusho. Na hakika wachamngu wana marudio mazuri.
|
Ayah 38:50 الأية
جَنَّاتِ عَدْنٍ مُّفَتَّحَةً لَّهُمُ الْأَبْوَابُ
Jannati AAadnin mufattahatanlahumu al-abwab
Swahili
Bustani za milele zitazo funguliwa milango yao kwa ajili yao.
|
Ayah 38:51 الأية
مُتَّكِئِينَ فِيهَا يَدْعُونَ فِيهَا بِفَاكِهَةٍ كَثِيرَةٍ وَشَرَابٍ
Muttaki-eena feeha yadAAoona feehabifakihatin katheeratin washarab
Swahili
Humo wataegemea matakia, wawe wanaagiza humo matunda mengi na vinywaji.
|
Ayah 38:52 الأية
وَعِندَهُمْ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ أَتْرَابٌ
WaAAindahum qasiratu attarfiatrab
Swahili
Na pamoja nao wake zao wenye kutuliza macho, hirimu zao.
|
Ayah 38:53 الأية
هَٰذَا مَا تُوعَدُونَ لِيَوْمِ الْحِسَابِ
Hatha ma tooAAadoona liyawmialhisab
Swahili
Haya ndiyo mliyo ahidiwa kwa Siku ya Hisabu.
|
Ayah 38:54 الأية
إِنَّ هَٰذَا لَرِزْقُنَا مَا لَهُ مِن نَّفَادٍ
Inna hatha larizquna malahu min nafad
Swahili
Hakika hii ndiyo riziki yetu isiyo malizika.
|
Ayah 38:55 الأية
هَٰذَا ۚ وَإِنَّ لِلطَّاغِينَ لَشَرَّ مَآبٍ
Hatha wa-inna littagheenalasharra maab
Swahili
Ndio hivi! Na hakika wenye kuasi bila ya shaka watapata marudio maovu kabisa;
|
Ayah 38:56 الأية
جَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا فَبِئْسَ الْمِهَادُ
Jahannama yaslawnaha fabi/saalmihad
Swahili
Nayo ni Jahannamu! Wataingia humo. Nacho hicho ni kitanda kiovu mno cha kulalia.
|
Ayah 38:57 الأية
هَٰذَا فَلْيَذُوقُوهُ حَمِيمٌ وَغَسَّاقٌ
Hatha falyathooqoohu hameemunwaghassaq
Swahili
Ndio hivi! Basi na wayaonje maji ya moto na ya usaha!
|
Ayah 38:58 الأية
وَآخَرُ مِن شَكْلِهِ أَزْوَاجٌ
Waakharu min shaklihi azwaj
Swahili
Na adhabu nyenginezo za namna hii.
|
Ayah 38:59 الأية
هَٰذَا فَوْجٌ مُّقْتَحِمٌ مَّعَكُمْ ۖ لَا مَرْحَبًا بِهِمْ ۚ إِنَّهُمْ صَالُو
النَّارِ
Hatha fawjun muqtahimunmaAAakum la marhaban bihim innahum saloo annar
Swahili
Hili ndilo kundi litakalo ingia pamoja nanyi. Hapana makaribisho mema kwao.
Hakika hao wanaingia Motoni.
|
Ayah 38:60 الأية
قَالُوا بَلْ أَنتُمْ لَا مَرْحَبًا بِكُمْ ۖ أَنتُمْ قَدَّمْتُمُوهُ لَنَا ۖ
فَبِئْسَ الْقَرَارُ
Qaloo bal antum la marhabanbikum antum qaddamtumoohu lana fabi/sa alqarar
Swahili
Waseme: Lakini nyinyi! Hamna mapokezi mazuri! Nyinyi ndio mlio tusabibisha haya,
napo ni pahala paovu kabisa!
|
Ayah 38:61 الأية
قَالُوا رَبَّنَا مَن قَدَّمَ لَنَا هَٰذَا فَزِدْهُ عَذَابًا ضِعْفًا فِي النَّارِ
Qaloo rabbana man qaddama lanahatha fazidhu AAathaban diAAfan fee annar
Swahili
Waseme: Mola wetu Mlezi! Aliye tusabibisha haya mzidishie adhabu mara mbili
Motoni.
|
Ayah 38:62 الأية
وَقَالُوا مَا لَنَا لَا نَرَىٰ رِجَالًا كُنَّا نَعُدُّهُم مِّنَ الْأَشْرَارِ
Waqaloo ma lana lanara rijalan kunna naAAudduhum mina al-ashrar
Swahili
Watasema: Tuna nini hata hatuwaoni wale watu ambao tukiwahisabu ndio katika
waovu?
|
Ayah 38:63 الأية
أَتَّخَذْنَاهُمْ سِخْرِيًّا أَمْ زَاغَتْ عَنْهُمُ الْأَبْصَارُ
Attakhathnahum sikhriyyan am zaghatAAanhumu al-absar
Swahili
Tulikosea tulipo wafanyia maskhara, au macho yetu tu hayawaoni ?
|
Ayah 38:64 الأية
إِنَّ ذَٰلِكَ لَحَقٌّ تَخَاصُمُ أَهْلِ النَّارِ
Inna thalika lahaqqun takhasumuahli annar
Swahili
Hakika hayo bila ya shaka ndiyo makhasimiano ya watu wa Motoni.
|
Ayah 38:65 الأية
قُلْ إِنَّمَا أَنَا مُنذِرٌ ۖ وَمَا مِنْ إِلَٰهٍ إِلَّا اللهُ الْوَاحِدُ
الْقَهَّارُ
Qul innama ana munthirunwama min ilahin illa Allahu alwahidualqahhar
Swahili
Sema: Hakika mimi ni mwonyaji tu; na hapana mungu ila Mwenyezi Mungu Mmoja,
Mtenda nguvu,
|
Ayah 38:66 الأية
رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا الْعَزِيزُ الْغَفَّارُ
Rabbu assamawati wal-ardiwama baynahuma alAAazeezu alghaffar
Swahili
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na viliomo baina yake, Mwenye nguvu, Mwenye
kusamehe.
|
Ayah 38:67 الأية
قُلْ هُوَ نَبَأٌ عَظِيمٌ
Qul huwa nabaon AAatheem
Swahili
Sema: Hii ni khabari kubwa kabisa.
|
Ayah 38:68 الأية
أَنتُمْ عَنْهُ مُعْرِضُونَ
Antum AAanhu muAAridoon
Swahili
Ambayo nyinyi mnaipuuza.
|
Ayah 38:69 الأية
مَا كَانَ لِيَ مِنْ عِلْمٍ بِالْمَلَإِ الْأَعْلَىٰ إِذْ يَخْتَصِمُونَ
Ma kana liya min AAilmin bilmala-ial-aAAla ith yakhtasimoon
Swahili
Sikuwa na ilimu ya mambo ya viumbe wakuu watukufu walipo kuwa wakishindana.
|
Ayah 38:70 الأية
إِن يُوحَىٰ إِلَيَّ إِلَّا أَنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُّبِينٌ
In yooha ilayya illa annamaana natheerun mubeen
Swahili
Haikufunuliwa kwangu isipo kuwa ya kwamba hakika mimi ni mwonyaji dhaahiri.
|
Ayah 38:71 الأية
إِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِّن طِينٍ
Ith qala rabbuka lilmala-ikatiinnee khaliqun basharan min teen
Swahili
Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na
udongo.
|
Ayah 38:72 الأية
فَإِذَا سَوَّيْتُهُ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُوا لَهُ سَاجِدِينَ
Fa-itha sawwaytuhu wanafakhtu feehimin roohee faqaAAoo lahu sajideen
Swahili
Na nitakapo mkamilisha na kumpulizia roho inayo tokana nami, basi muangukieni
kwa kumt'ii.
|
Ayah 38:73 الأية
فَسَجَدَ الْمَلَائِكَةُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ
Fasajada almala-ikatu kulluhumajmaAAoon
Swahili
Basi Malaika wakat'ii wote pamoja.
|
Ayah 38:74 الأية
إِلَّا إِبْلِيسَ اسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِينَ
Illa ibleesa istakbara wakanamina alkafireen
Swahili
Isipo kuwa Iblisi; alijivuna na akawa katika makafiri.
|
Ayah 38:75 الأية
قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَيَّ ۖ
أَسْتَكْبَرْتَ أَمْ كُنتَ مِنَ الْعَالِينَ
Qala ya ibleesu mamanaAAaka an tasjuda lima khalaqtu biyadayya astakbarta
amkunta mina alAAaleen
Swahili
Mwenyezi Mungu akamwambia: Ewe Iblisi! Kipi kilicho kuzuia kumt'ii yule niliye
muumba kwa mikono yangu? Je! Umejiona mkubwa, au umekuwa katika wakuu kweli?
|
Ayah 38:76 الأية
قَالَ أَنَا خَيْرٌ مِّنْهُ ۖ خَلَقْتَنِي مِن نَّارٍ وَخَلَقْتَهُ مِن طِينٍ
Qala ana khayrun minhukhalaqtanee min narin wakhalaqtahu min teen
Swahili
Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa
udongo.
|
Ayah 38:77 الأية
قَالَ فَاخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ
Qala fakhruj minhafa-innaka rajeem
Swahili
Akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaanika.
|
Ayah 38:78 الأية
وَإِنَّ عَلَيْكَ لَعْنَتِي إِلَىٰ يَوْمِ الدِّينِ
Wa-inna AAalayka laAAnatee ila yawmiaddeen
Swahili
Na hakika laana yangu itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo.
|
Ayah 38:79 الأية
قَالَ رَبِّ فَأَنظِرْنِي إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ
Qala rabbi faanthirneeila yawmi yubAAathoon
Swahili
Akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watayo fufuliwa viumbe.
|
Ayah 38:80 الأية
قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ الْمُنظَرِينَ
Qala fa-innaka mina almunthareen
Swahili
Mwenyezi Mungu akasema: Basi umekwisha kuwa miongoni mwa walio pewa muhula,
|
Ayah 38:81 الأية
إِلَىٰ يَوْمِ الْوَقْتِ الْمَعْلُومِ
Ila yawmi alwaqti almaAAloom
Swahili
Mpaka siku ya wakati maalumu.
|
Ayah 38:82 الأية
قَالَ فَبِعِزَّتِكَ لَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ
Qala fabiAAizzatika laoghwiyannahumajmaAAeen
Swahili
Akasema (Iblisi): Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote,
|
Ayah 38:83 الأية
إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ الْمُخْلَصِينَ
Illa AAibadaka minhumualmukhlaseen
Swahili
Isipo kuwa wale waja wako miongoni mwao walio khitariwa.
|
Ayah 38:84 الأية
قَالَ فَالْحَقُّ وَالْحَقَّ أَقُولُ
Qala falhaqqu walhaqqaaqool
Swahili
Akasema: Haki! Na haki ninaisema.
|
Ayah 38:85 الأية
لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكَ وَمِمَّن تَبِعَكَ مِنْهُمْ أَجْمَعِينَ
Laamlaanna jahannama minka wamimmantabiAAaka minhum ajmaAAeen
Swahili
Bila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wewe na kwa hao wote wenye kukufuata
miongoni mwao.
|
Ayah 38:86 الأية
قُلْ مَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُتَكَلِّفِينَ
Qul ma as-alukum AAalayhi min ajrinwama ana mina almutakallifeen
Swahili
Sema (Ewe Mtume) : Sikuombeni ujira juu ya haya, wala mimi si katika
wadanganyifu.
|
Ayah 38:87 الأية
إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ
In huwa illa thikrun lilAAalameen
Swahili
Hayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu wote.
|
Ayah 38:88 الأية
وَلَتَعْلَمُنَّ نَبَأَهُ بَعْدَ حِينٍ
WalataAAlamunna nabaahu baAAda heen
Swahili
Na bila ya shaka mtajua khabari zake baada ya muda.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|