1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
حم
Ha-meem
Swahili
H'a Mim
|
Ayah 41:2 الأية
تَنزِيلٌ مِّنَ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Tanzeelun mina arrahmaniarraheem
Swahili
Uteremsho huu umetoka kwa Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.
|
Ayah 41:3 الأية
كِتَابٌ فُصِّلَتْ آيَاتُهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لِّقَوْمٍ يَعْلَمُونَ
Kitabun fussilat ayatuhuqur-anan AAarabiyyan liqawmin yaAAlamoon
Swahili
Hichi ni Kitabu kilicho pambanuliwa Aya zake, cha kusomwa kwa Kiarabu kwa watu
wanao jua.
|
Ayah 41:4 الأية
بَشِيرًا وَنَذِيرًا فَأَعْرَضَ أَكْثَرُهُمْ فَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ
Basheeran wanatheeran faaAAradaaktharuhum fahum la yasmaAAoon
Swahili
Kitoacho khabari njema, na chenye kuonya. Lakini wengi katika wao wamepuuza; kwa
hivyo hawasikii.
|
Ayah 41:5 الأية
وَقَالُوا قُلُوبُنَا فِي أَكِنَّةٍ مِّمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ وَفِي آذَانِنَا
وَقْرٌ وَمِن بَيْنِنَا وَبَيْنِكَ حِجَابٌ فَاعْمَلْ إِنَّنَا عَامِلُونَ
Waqaloo quloobuna fee akinnatinmimma tadAAoona ilayhi wafee athaninawaqrun wamin
baynina wabaynika hijabun faAAmalinnana AAamiloon
Swahili
Na wakasema: Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa hayo unayo tuitia, na masikio
yetu yana uziwi, na baina yetu na wewe lipo pazia. Basi wewe tenda, nasi
tunatenda.
|
Ayah 41:6 الأية
قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَٰهُكُمْ
إِلَٰهٌ وَاحِدٌ فَاسْتَقِيمُوا إِلَيْهِ وَاسْتَغْفِرُوهُ ۗ وَوَيْلٌ
لِّلْمُشْرِكِينَ
Qul innama ana basharunmithlukum yooha ilayya annama ilahukum ilahunwahidun
fastaqeemoo ilayhi wastaghfiroohuwawaylun lilmushrikeen
Swahili
Sema: Hakika mimi ni mtu kama nyinyi; inafunuliwa kwangu ya kwamba Mungu wenu ni
Mungu Mmoja tu. Basi nyookeni sawa kumwendea Yeye, na mumtake msamaha, na ole
wao wanao mshirikisha,
|
Ayah 41:7 الأية
الَّذِينَ لَا يُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ
Allatheena la yu/toona azzakatawahum bil-akhirati hum kafiroon
Swahili
Ambao hawatoi Zaka na wanaikataa Akhera.
|
Ayah 41:8 الأية
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ
Inna allatheena amanoowaAAamiloo assalihati lahum ajrun ghayrumamnoon
Swahili
Hakika wanao amini na wakatenda mema watakuwa na ujira usio na ukomo.
|
Ayah 41:9 الأية
قُلْ أَئِنَّكُمْ لَتَكْفُرُونَ بِالَّذِي خَلَقَ الْأَرْضَ فِي يَوْمَيْنِ
وَتَجْعَلُونَ لَهُ أَندَادًا ۚ ذَٰلِكَ رَبُّ الْعَالَمِينَ
Qul a-innakum latakfuroona billatheekhalaqa al-arda fee yawmayni watajAAaloona
lahu andadanthalika rabbu alAAalameen
Swahili
Sema: Hivyo nyinyi mnamkataa aliye umba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia
washirika? Huyu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote.
|
Ayah 41:10 الأية
وَجَعَلَ فِيهَا رَوَاسِيَ مِن فَوْقِهَا وَبَارَكَ فِيهَا وَقَدَّرَ فِيهَا
أَقْوَاتَهَا فِي أَرْبَعَةِ أَيَّامٍ سَوَاءً لِّلسَّائِلِينَ
WajaAAala feeha rawasiya minfawqiha wabaraka feeha waqaddara feehaaqwataha fee
arbaAAati ayyamin sawaanlissa-ileen
Swahili
Na akaweka humo milima juu yake, na akabarikia humo na akakadiria humo chakula
chake katika siku nne. Haya ni sawa kabisa kwa wanao uliza.
|
Ayah 41:11 الأية
ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ وَهِيَ دُخَانٌ فَقَالَ لَهَا وَلِلْأَرْضِ
ائْتِيَا طَوْعًا أَوْ كَرْهًا قَالَتَا أَتَيْنَا طَائِعِينَ
Thumma istawa ila assama-iwahiya dukhanun faqala laha walil-ardii/tiya tawAAan
aw karhan qalata ataynata-iAAeen
Swahili
Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni,
kwa khiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni wat'iifu.
|
Ayah 41:12 الأية
فَقَضَاهُنَّ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ فِي يَوْمَيْنِ وَأَوْحَىٰ فِي كُلِّ سَمَاءٍ
أَمْرَهَا ۚ وَزَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِمَصَابِيحَ وَحِفْظًا ۚ ذَٰلِكَ
تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ
Faqadahunna sabAAa samawatinfee yawmayni waawha fee kulli sama-in
amrahawazayyanna assamaa addunyabimasabeeha wahifthan thalikataqdeeru alAAazeezi
alAAaleem
Swahili
Basi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili, na akazipangia kila mbingu mambo
yake. Na tukaipamba mbingu ya chini kwa mataa na kwa ulinzi. Hichi ndicho kipimo
cha Mwenyezi Mungu Mwenye Kujua.
|
Ayah 41:13 الأية
فَإِنْ أَعْرَضُوا فَقُلْ أَنذَرْتُكُمْ صَاعِقَةً مِّثْلَ صَاعِقَةِ عَادٍ
وَثَمُودَ
Fa-in aAAradoo fuqul anthartukumsaAAiqatan mithla saAAiqati AAadin wathamood
Swahili
Basi wakipuuza wewe sema: Nakuhadharisheni adhabu mfano wa adhabu ya A'di na
Thamudi,
|
Ayah 41:14 الأية
إِذْ جَاءَتْهُمُ الرُّسُلُ مِن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا
تَعْبُدُوا إِلَّا اللهَ ۖ قَالُوا لَوْ شَاءَ رَبُّنَا لَأَنزَلَ مَلَائِكَةً
فَإِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ كَافِرُونَ
Ith jaat-humu arrusulumin bayni aydeehim wamin khalfihim alla taAAbudoo
illaAllaha qaloo law shaa rabbunalaanzala mala-ikatan fa-inna bima orsiltumbihi
kafiroon
Swahili
Walipo wajia Mitume mbele yao na nyuma yao wakawaambia: Msimuabudu ila Mwenyezi
Mungu! Wakasema: Angeli taka Mola wetu Mlezi bila ya shaka angeli wateremsha
Malaika. Basi sisi hakika tunayakataa hayo mliyo tumwa.
|
Ayah 41:15 الأية
فَأَمَّا عَادٌ فَاسْتَكْبَرُوا فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَقَالُوا مَنْ
أَشَدُّ مِنَّا قُوَّةً ۖ أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللهَ الَّذِي خَلَقَهُمْ هُوَ
أَشَدُّ مِنْهُمْ قُوَّةً ۖ وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يَجْحَدُونَ
Faamma AAadun fastakbaroofee al-ardi bighayri alhaqqi waqaloo manashaddu minna
quwwatan awa lam yaraw anna Allahaallathee khalaqahum huwa ashaddu minhum
quwwatan wakanoobi-ayatina yajhadoon
Swahili
Ama kina A'di walijivuna katika nchi bila ya haki, na wakasema: Nani aliye kuwa
na nguvu kushinda sisi? Kwani wao hawakuona kwamba Mwenyezi Mungu aliye waumba
ni Mwenye nguvu kushinda wao? Na wao wakawa wanazikataa Ishara zetu!
|
Ayah 41:16 الأية
فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا صَرْصَرًا فِي أَيَّامٍ نَّحِسَاتٍ لِّنُذِيقَهُمْ
عَذَابَ الْخِزْيِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَخْزَىٰ ۖ
وَهُمْ لَا يُنصَرُونَ
Faarsalna AAalayhim reehan sarsaranfee ayyamin nahisatin linutheeqahumAAathaba
alkhizyi fee alhayati addunyawalaAAathabu al-akhirati akhza wahum layunsaroon
Swahili
Basi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku za ukorofi, ili tuwaonjeshe
adhabu ya kuwahizi katika uhai wa duniani, na bila ya shaka adhabu ya Akhera ina
hizaya zaidi, na wala wao hawatanusuriwa.
|
Ayah 41:17 الأية
وَأَمَّا ثَمُودُ فَهَدَيْنَاهُمْ فَاسْتَحَبُّوا الْعَمَىٰ عَلَى الْهُدَىٰ
فَأَخَذَتْهُمْ صَاعِقَةُ الْعَذَابِ الْهُونِ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ
Waamma thamoodu fahadaynahumfastahabboo alAAama AAala alhudafaakhathat-hum
saAAiqatu alAAathabi alhoonibima kanoo yaksiboon
Swahili
Na ama Thamudi tuliwaongoza, lakini walipenda upofu kuliko uwongofu. Basi
uliwachukua moto wa adhabu ya kuwafedhehi kwa sababu ya yale waliyo kuwa
wakiyachuma.
|
Ayah 41:18 الأية
وَنَجَّيْنَا الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ
Wanajjayna allatheena amanoowakanoo yattaqoon
Swahili
Na tukawaokoa walio amini na wakawa wanamcha-mngu.
|
Ayah 41:19 الأية
وَيَوْمَ يُحْشَرُ أَعْدَاءُ اللهِ إِلَى النَّارِ فَهُمْ يُوزَعُونَ
Wayawma yuhsharu aAAdao Allahiila annari fahum yoozaAAoon
Swahili
Na siku watakapo kusanywa maadui wa Mwenyezi Mungu kwenye Moto, nao
wakikgawanywa kwa makundi.
|
Ayah 41:20 الأية
حَتَّىٰ إِذَا مَا جَاءُوهَا شَهِدَ عَلَيْهِمْ سَمْعُهُمْ وَأَبْصَارُهُمْ
وَجُلُودُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Hatta itha ma jaoohashahida AAalayhim samAAuhum waabsaruhum wajulooduhum
bimakanoo yaAAmaloon
Swahili
Hata watakapo ufikia Moto yatawashuhudia masikio yao, na macho yao na ngozi zao
kwa waliyo kuwa wakiyatenda.
|
Ayah 41:21 الأية
وَقَالُوا لِجُلُودِهِمْ لِمَ شَهِدتُّمْ عَلَيْنَا ۖ قَالُوا أَنطَقَنَا اللهُ
الَّذِي أَنطَقَ كُلَّ شَيْءٍ وَهُوَ خَلَقَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَإِلَيْهِ
تُرْجَعُونَ
Waqaloo lijuloodihim lima shahidtumAAalayna qaloo antaqana Allahuallathee antaqa
kulla shay-in wahuwa khalaqakumawwala marratin wa-ilayhi turjaAAoon
Swahili
Na wao wataziambia ngozi zao: Kwa nini mmetushuhudilia? Nazo zitasema:
Ametutamkisha Mwenyezi Mungu ambaye ametamkisha kila kitu! Na Yeye ndiye aliye
kuumbeni mara ya kwanza, na kwake Yeye tu mtarejeshwa.
|
Ayah 41:22 الأية
وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَن يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلَا
أَبْصَارُكُمْ وَلَا جُلُودُكُمْ وَلَٰكِن ظَنَنتُمْ أَنَّ اللهَ لَا يَعْلَمُ
كَثِيرًا مِّمَّا تَعْمَلُونَ
Wama kuntum tastatiroona an yashhadaAAalaykum samAAukum wala absarukum
walajuloodukum walakin thanantum anna Allahala yaAAlamu katheeran mimma
taAAmaloon
Swahili
Na hamkuwa wenye kujificha hata masikio yenu, na macho yenu, na ngozi zenu,
zisikushuhudilieni. Lakini mlidhani kwamba Mwenyezi Mungu hayajui mengi katika
mliyo kuwa mkiyatenda.
|
Ayah 41:23 الأية
وَذَٰلِكُمْ ظَنُّكُمُ الَّذِي ظَنَنتُم بِرَبِّكُمْ أَرْدَاكُمْ فَأَصْبَحْتُم
مِّنَ الْخَاسِرِينَ
Wathalikum thannukumuallathee thanantum birabbikum ardakumfaasbahtum mina
alkhasireen
Swahili
Basi hiyo dhana yenu mliyo kuwa mkimdhania Mola wenu Mlezi. Imekuangamizeni; na
mmekuwa miongoni mwa walio khasiri.
|
Ayah 41:24 الأية
فَإِن يَصْبِرُوا فَالنَّارُ مَثْوًى لَّهُمْ ۖ وَإِن يَسْتَعْتِبُوا فَمَا هُم
مِّنَ الْمُعْتَبِينَ
Fa-in yasbiroo fannarumathwan lahum wa-in yastaAAtiboo fama hum minaalmuAAtabeen
Swahili
Basi wakisubiri Moto ndio maskani yao. Na wakiomba radhi hawakubaliwi.
|
Ayah 41:25 الأية
وَقَيَّضْنَا لَهُمْ قُرَنَاءَ فَزَيَّنُوا لَهُم مَّا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا
خَلْفَهُمْ وَحَقَّ عَلَيْهِمُ الْقَوْلُ فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِم
مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا خَاسِرِينَ
Waqayyadna lahum quranaafazayyanoo lahum ma bayna aydeehim wama khalfahumwahaqqa
AAalayhimu alqawlu fee omamin qad khalat minqablihim mina aljinni wal-insi
innahum kanoo khasireen
Swahili
Na tukawawekea marafiki, na wakawapambia yaliyo mbele yao na nyuma yao. Basi
ikawathibitikia kauli wawe pamoja na mataifa yaliyo pita kabla yao, miongoni mwa
majini na watu. Hakika hao wamekuwa ni wenye kukhasirika.
|
Ayah 41:26 الأية
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَسْمَعُوا لِهَٰذَا الْقُرْآنِ وَالْغَوْا فِيهِ
لَعَلَّكُمْ تَغْلِبُونَ
Waqala allatheena kafaroo latasmaAAoo lihatha alqur-ani walghaw feehilaAAallakum
taghliboon
Swahili
Na walio kufuru walisema: Msiisikilize Qur'ani hii, na timueni zogo, huenda
mkashinda.
|
Ayah 41:27 الأية
فَلَنُذِيقَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا عَذَابًا شَدِيدًا وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَسْوَأَ
الَّذِي كَانُوا يَعْمَلُونَ
Falanutheeqanna allatheenakafaroo AAathaban shadeedan walanajziyannahum aswaa
allatheekanoo yaAAmaloon
Swahili
Basi hapana shaka tutawaonjesha hao walio kufuru adhabu kali, na hapana shaka
tutawalipa malipo mabaya ya yale waliyo kuwa wakiyafanya.
|
Ayah 41:28 الأية
ذَٰلِكَ جَزَاءُ أَعْدَاءِ اللهِ النَّارُ ۖ لَهُمْ فِيهَا دَارُ الْخُلْدِ ۖ
جَزَاءً بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَجْحَدُونَ
Thalika jazao aAAda-iAllahi annaru lahum feeha darualkhuldi jazaan bima kanoo
bi-ayatinayajhadoon
Swahili
Hayo ndiyo malipo ya Maadui wa Mwenyezi Mungu - Moto! Humo watakuwa na maskani
ya kudumu, ndiyo malipo yao kwa sababu walikuwa wakizikataa Ishara zetu.
|
Ayah 41:29 الأية
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا رَبَّنَا أَرِنَا اللَّذَيْنِ أَضَلَّانَا مِنَ
الْجِنِّ وَالْإِنسِ نَجْعَلْهُمَا تَحْتَ أَقْدَامِنَا لِيَكُونَا مِنَ
الْأَسْفَلِينَ
Waqala allatheena kafaroorabbana arina allathayni adallanamina aljinni wal-insi
najAAalhuma tahta aqdaminaliyakoona mina al-asfaleen
Swahili
Na walio kufuru watasema: Mola wetu Mlezi! Tuonyeshe walio tupoteza miongoni mwa
majini na watu ili tuwaweke chini ya miguu yetu, wapate kuwa miongoni wa walio
chini kabisa.
|
Ayah 41:30 الأية
إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ
عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا
بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ
Inna allatheena qaloo rabbunaAllahu thumma istaqamoo tatanazzalu
AAalayhimualmala-ikatu alla takhafoo wala tahzanoowaabshiroo biljannati allatee
kuntum tooAAadoon
Swahili
Hakika walio sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Kisha wakanyooka sawa, hao
huwateremkia Malaika wakawaambia: Msiogope, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa
Pepo mliyo kuwa mkiahidiwa.
|
Ayah 41:31 الأية
نَحْنُ أَوْلِيَاؤُكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَلَكُمْ
فِيهَا مَا تَشْتَهِي أَنفُسُكُمْ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ
Nahnu awliyaokum fee alhayatiaddunya wafee al-akhirati walakum feehama tashtahee
anfusukum walakum feeha mataddaAAoon
Swahili
Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na katika Akhera, na humo mtapata
kinacho tamaniwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyo vitaka.
|
Ayah 41:32 الأية
نُزُلًا مِّنْ غَفُورٍ رَّحِيمٍ
Nuzulan min ghafoorin raheem
Swahili
Ni takrima itokayo kwa Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
|
Ayah 41:33 الأية
وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِّمَّن دَعَا إِلَى اللهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ
إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ
Waman ahsanu qawlan mimman daAAaila Allahi waAAamila salihan waqalainnanee mina
almuslimeen
Swahili
Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na
akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu?
|
Ayah 41:34 الأية
وَلَا تَسْتَوِي الْحَسَنَةُ وَلَا السَّيِّئَةُ ۚ ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ
فَإِذَا الَّذِي بَيْنَكَ وَبَيْنَهُ عَدَاوَةٌ كَأَنَّهُ وَلِيٌّ حَمِيمٌ
Wala tastawee alhasanatu walaassayyi-atu idfaAA billatee hiya ahsanufa-itha
allathee baynaka wabaynahu AAadawatunkaannahu waliyyun hameem
Swahili
Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye
baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu.
|
Ayah 41:35 الأية
وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا ذُو حَظٍّ
عَظِيمٍ
Wama yulaqqaha illaallatheena sabaroo wama yulaqqahailla thoo haththin AAatheem
Swahili
Lakini hawapewi wema huu ila wanao subiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa.
|
Ayah 41:36 الأية
وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللهِ ۖ إِنَّهُ
هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ
Wa-imma yanzaghannaka mina ashshaytaninazghun fastaAAith billahi innahuhuwa
assameeAAu alAAaleem
Swahili
Na Shet'ani akikuchochea kwa uchochezi wewe jikinge kwa Mwenyezi Mungu. Hakika
Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
|
Ayah 41:37 الأية
وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا
لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ
إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ
Wamin ayatihi allaylu wannaharuwashshamsu walqamaru la tasjudoo lishshamsiwala
lilqamari wasjudoo lillahi alatheekhalaqahunna in kuntum iyyahu taAAbudoon
Swahili
Na katika Ishara zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Basi msilisujudie jua
wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliye viumba, ikiwa nyinyi mnamuabudu
Yeye tu.
|
Ayah 41:38 الأية
فَإِنِ اسْتَكْبَرُوا فَالَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ يُسَبِّحُونَ لَهُ بِاللَّيْلِ
وَالنَّهَارِ وَهُمْ لَا يَسْأَمُونَ ۩
Fa-ini istakbaroo fallatheenaAAinda rabbika yusabbihoona lahu billayli
wannahariwahum la yas-amoon
Swahili
Na ikiwa watajivuna, basi hao walioko kwa Mola wako Mlezi wanamtakasa Yeye usiku
na mchana, na wao hawachoki.
|
Ayah 41:39 الأية
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنَّكَ تَرَى الْأَرْضَ خَاشِعَةً فَإِذَا أَنزَلْنَا عَلَيْهَا
الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ ۚ إِنَّ الَّذِي أَحْيَاهَا لَمُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۚ
إِنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ
Wamin ayatihi annaka taraal-arda khashiAAatan fa-itha anzalnaAAalayha almaa
ihtazzat warabat inna allatheeahyaha lamuhyee almawta innahuAAala kulli shay-in
qadeer
Swahili
Na katika Ishara zake ni kwamba unaiona ardhi nyonge, lakini tunapo iteremshia
maji mara unaiona inataharaki na kuumuka. Bila ya shaka aliye ihuisha ardhi
ndiye atakaye huisha wafu. Hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu.
|
Ayah 41:40 الأية
إِنَّ الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي آيَاتِنَا لَا يَخْفَوْنَ عَلَيْنَا ۗ أَفَمَن
يُلْقَىٰ فِي النَّارِ خَيْرٌ أَم مَّن يَأْتِي آمِنًا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ
اعْمَلُوا مَا شِئْتُمْ ۖ إِنَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ
Inna allatheena yulhidoona feeayatina la yakhfawna AAalaynaafaman yulqa fee
annari khayrun ammanya/tee aminan yawma alqiyamati iAAmaloo mashi/tum innahu
bima taAAmaloona baseer
Swahili
Hakika wale wanao upotoa ukweli uliomo katika Ishara zetu hawatufichikii Sisi.
Je! Atakaye tupwa Motoni ni bora au atakaye kuja kwa amani Siku ya Kiyama?
Tendeni mpendavyo, kwa hakika Yeye anayaona mnayo yatenda.
|
Ayah 41:41 الأية
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِالذِّكْرِ لَمَّا جَاءَهُمْ ۖ وَإِنَّهُ لَكِتَابٌ
عَزِيزٌ
Inna allatheena kafaroo biththikrilamma jaahum wa-innahu lakitabun AAazeez
Swahili
Kwa hakika wanayo yakataa mawaidha haya yanapo wajia (wataangamia), na haya bila
ya shaka ni Kitabu chenye nguvu na utukufu.
|
Ayah 41:42 الأية
لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ ۖ تَنزِيلٌ
مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ
La ya/teehi albatilu min bayniyadayhi wala min khalfihi tanzeelun min hakeemin
hameed
Swahili
Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hikima,
Msifiwa.
|
Ayah 41:43 الأية
مَّا يُقَالُ لَكَ إِلَّا مَا قَدْ قِيلَ لِلرُّسُلِ مِن قَبْلِكَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ
لَذُو مَغْفِرَةٍ وَذُو عِقَابٍ أَلِيمٍ
Ma yuqalu laka illa maqad qeela lirrusuli min qablika inna rabbaka
lathoomaghfiratin wathoo AAiqabin aleem
Swahili
Huambiwi ila yale yale waliyo ambiwa Mitume wa kabla yako. Hakika Mola wako
Mlezi bila ya shaka ni Mwenye maghfira, na ni Mwenye adhabu chungu.
|
Ayah 41:44 الأية
وَلَوْ جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا أَعْجَمِيًّا لَّقَالُوا لَوْلَا فُصِّلَتْ آيَاتُهُ ۖ
أَأَعْجَمِيٌّ وَعَرَبِيٌّ ۗ قُلْ هُوَ لِلَّذِينَ آمَنُوا هُدًى وَشِفَاءٌ ۖ
وَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ فِي آذَانِهِمْ وَقْرٌ وَهُوَ عَلَيْهِمْ عَمًى ۚ
أُولَٰئِكَ يُنَادَوْنَ مِن مَّكَانٍ بَعِيدٍ
Walaw jaAAalnahu qur-ananaAAjamiyyan laqaloo lawla fussilat ayatuhuaaAAjamiyyun
waAAarabiyyun qul huwa lillatheena amanoohudan washifaon wallatheena
layu/minoona fee athanihim waqrun wahuwa AAalayhim AAaman ola-ikayunadawna min
makanin baAAeed
Swahili
Na lau tungeli ifanya Qur'ani kwa lugha ya kigeni wangeli sema: Kwanini Aya zake
haziku pambanuliwa? Yawaje lugha ya kigeni na Mtume Mwaarabu? Sema: Hii Qur'ani
ni uwongofu na poza kwa wenye kuamini. Na wasio amini umo uziwi katika masikio
yao, nayo kwao imezibwa hawaioni. Hao wanaitwa nao wako pahala mbali.
|
Ayah 41:45 الأية
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَاخْتُلِفَ فِيهِ ۗ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ
سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ
مُرِيبٍ
Walaqad atayna moosaalkitaba fakhtulifa feehi walawla kalimatunsabaqat min
rabbika laqudiya baynahum wa-innahum lafeeshakkin minhu mureeb
Swahili
Na hakika tulimpa Musa Kitabu, lakini pakatokea khitilafu kati yake. Na lau kuwa
halikwisha tangulia neno la Mola wako Mlezi wangeli hukumiwa. Na hakika wao wamo
katika shaka yenye kuwatia wasiwasi.
|
Ayah 41:46 الأية
مَّنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَنْ أَسَاءَ فَعَلَيْهَا ۗ وَمَا رَبُّكَ
بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ
Man AAamila salihanfalinafsihi waman asaa faAAalayha wamarabbuka bithallamin
lilAAabeed
Swahili
Anaye tenda mema basi anajitendea mwenyewe nafsi yake, na mwenye kutenda uovu
basi ni juu ya nafsi yake vile vile; wala Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu
waja.
|
Ayah 41:47 الأية
إِلَيْهِ يُرَدُّ عِلْمُ السَّاعَةِ ۚ وَمَا تَخْرُجُ مِن ثَمَرَاتٍ مِّنْ
أَكْمَامِهَا وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِ ۚ
وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ أَيْنَ شُرَكَائِي قَالُوا آذَنَّاكَ مَا مِنَّا مِن شَهِيدٍ
Ilayhi yuraddu AAilmu assaAAatiwama takhruju min thamaratin min akmamihawama
tahmilu min ontha wala tadaAAuilla biAAilmihi wayawma yunadeehim ayna
shuraka-eeqaloo athannaka ma minna minshaheed
Swahili
UJUZI wa kuijua Saa ya Kiyama unarudishwa kwake tu Mwenyezi Mungu. Na matunda
hayatoki katika mafumba yake, wala mwanamke hachukui mimba, wala hazai, ila kwa
kujua kwake. Na siku atakayo waita, akawaambia: Wako wapi washirika wangu? Hapo
watasema: Tunakiri kwako ya kwamba hapana miongoni mwetu anaye shuhudia hayo.
|
Ayah 41:48 الأية
وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَدْعُونَ مِن قَبْلُ ۖ وَظَنُّوا مَا لَهُم مِّن
مَّحِيصٍ
Wadalla AAanhum ma kanooyadAAoona min qablu wathannoo ma lahum minmahees
Swahili
Na wakawapotea wale walio kuwa wakiwaomba hapo kwanza, na wakawa na yakini kuwa
hawana pa kukimbilia.
|
Ayah 41:49 الأية
لَّا يَسْأَمُ الْإِنسَانُ مِن دُعَاءِ الْخَيْرِ وَإِن مَّسَّهُ الشَّرُّ
فَيَئُوسٌ قَنُوطٌ
La yas-amu al-insanu min duAAa-ialkhayri wa-in massahu ashsharru fayaoosun
qanoot
Swahili
Mwanaadamu hachoki kuomba dua za kheri, na inapo mpata shari, mara huvunjika
moyo akakata tamaa.
|
Ayah 41:50 الأية
وَلَئِنْ أَذَقْنَاهُ رَحْمَةً مِّنَّا مِن بَعْدِ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُ لَيَقُولَنَّ
هَٰذَا لِي وَمَا أَظُنُّ السَّاعَةَ قَائِمَةً وَلَئِن رُّجِعْتُ إِلَىٰ رَبِّي
إِنَّ لِي عِندَهُ لَلْحُسْنَىٰ ۚ فَلَنُنَبِّئَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِمَا
عَمِلُوا وَلَنُذِيقَنَّهُم مِّنْ عَذَابٍ غَلِيظٍ
Wala-in athaqnahu rahmatanminna min baAAdi darraa massat-hulayaqoolanna hatha
lee wama athunnu assaAAataqa-imatan wala-in rujiAAtu ila rabbee inna leeAAindahu
lalhusna falanunabbi-anna allatheenakafaroo bima AAamiloo walanutheeqannahum min
AAathabinghaleeth
Swahili
Na pindi tukimwonjesha rehema itokayo kwetu baada ya kumgusa dhara, bila ya
shaka husema: Haya nayastahiki mimi, wala sidhani kuwa Kiyama kitakuja. Na hata
nikirudishwa kwa Mola wangu Mlezi bila ya shaka nina mema yangu kwake! Basi kwa
yakini tutawaelezea walio kufuru hayo waliyo yatenda, na kwa yakini
tutawaonjesha adhabu ngumu.
|
Ayah 41:51 الأية
وَإِذَا أَنْعَمْنَا عَلَى الْإِنسَانِ أَعْرَضَ وَنَأَىٰ بِجَانِبِهِ وَإِذَا
مَسَّهُ الشَّرُّ فَذُو دُعَاءٍ عَرِيضٍ
Wa-itha anAAamna AAalaal-insani aAArada wanaa bijanibihiwa-itha massahu
ashsharru fathoo duAAa-inAAareed
Swahili
Na tukimneemesha mwanaadamu hugeuka na kujitenga upande, na inapo mgusa shari,
huwa na madua marefu marefu.
|
Ayah 41:52 الأية
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن كَانَ مِنْ عِندِ اللهِ ثُمَّ كَفَرْتُم بِهِ مَنْ أَضَلُّ
مِمَّنْ هُوَ فِي شِقَاقٍ بَعِيدٍ
Qul araaytum in kana min AAindi Allahithumma kafartum bihi man adallu mimman
huwa fee shiqaqinbaAAeed
Swahili
Sema: Mnaonaje! Ikiwa haya yanatoka kwa Mwenyezi Mungu, nanyi ikawa ndio
mmeyakataa, ni nani aliye potea zaidi kuliko aliye katika upinzani wa mbali?
|
Ayah 41:53 الأية
سَنُرِيهِمْ آيَاتِنَا فِي الْآفَاقِ وَفِي أَنفُسِهِمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَهُمْ
أَنَّهُ الْحَقُّ ۗ أَوَلَمْ يَكْفِ بِرَبِّكَ أَنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ
Sanureehim ayatina feeal-afaqi wafee anfusihim hattayatabayyana lahum annahu
alhaqqu awa lam yakfi birabbikaannahu AAala kulli shay-in shaheed
Swahili
Tutawaonyesha Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao wenyewe mpaka
iwabainikie kwamba haya ni kweli. Je! Haikutoshi kwamba Mola wako Mlezi kuwa
Yeye ni Shahidi wa kila kitu?
|
Ayah 41:54 الأية
أَلَا إِنَّهُمْ فِي مِرْيَةٍ مِّن لِّقَاءِ رَبِّهِمْ ۗ أَلَا إِنَّهُ بِكُلِّ
شَيْءٍ مُّحِيطٌ
Ala innahum fee miryatin min liqa-irabbihim ala innahu bikulli shay-in muheet
Swahili
Ama wao wamo katika shaka ya kukutana na Mola wao Mlezi! Ama hakika Yeye
amekizunguka kila kitu.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|