First Ayah 1 الأية الأوليبِسْم ِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
حم
Ha-meem
Swahili
H'a Mim
|
Ayah 42:2 الأية
عسق
AAayn-seen-qaf
Swahili
A'yn Sin Qaf
|
Ayah 42:3 الأية
كَذَٰلِكَ يُوحِي إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ اللَّهُ الْعَزِيزُ
الْحَكِيمُ
Kathalika yoohee ilayka wa-ilaallatheena min qablika Allahu alAAazeezu alhakeem
Swahili
Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu na Mwenye hikima anavyo kuletea Wahyi
wewe na walio kabla yako.
|
Ayah 42:4 الأية
لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ
Lahu ma fee assamawatiwama fee al-ardi wahuwa alAAaliyyu alAAatheem
Swahili
Ni vyake viliomo mbinguni, na viliomo katika ardhi. Na Yeye ndiye Mtukufu, Mkuu.
|
Ayah 42:5 الأية
تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِن فَوْقِهِنَّ ۚ وَالْمَلَائِكَةُ
يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِمَن فِي الْأَرْضِ ۗ أَلَا
إِنَّ اللَّهَ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ
Takadu assamawatuyatafattarna min fawqihinna walmala-ikatuyusabbihoona bihamdi
rabbihim wayastaghfiroonaliman fee al-ardi ala inna Allaha huwaalghafooru
arraheem
Swahili
Zinakaribia mbingu kupasuka juu huko, na Malaika wakimtakasa Mola wao Mlezi na
kumhimidi, na wakiwaombea maghfira waliomo kwenye ardhi. Ama hakika Mwenyezi
Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
|
Ayah 42:6 الأية
وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ اللَّهُ حَفِيظٌ عَلَيْهِمْ وَمَا
أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ
Wallatheena ittakhathoomin doonihi awliyaa Allahu hafeethunAAalayhim wama anta
AAalayhim biwakeel
Swahili
Na wale walio wafanya walinzi wengine badala yake Yeye, Mwenyezi Mungu ni
Mwangalizi juu yao. Wala wewe si wakili juu yao.
|
Ayah 42:7 الأية
وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لِّتُنذِرَ أُمَّ الْقُرَىٰ
وَمَنْ حَوْلَهَا وَتُنذِرَ يَوْمَ الْجَمْعِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۚ فَرِيقٌ فِي
الْجَنَّةِ وَفَرِيقٌ فِي السَّعِيرِ
Wakathalika awhaynailayka qur-anan AAarabiyyan litunthira omma alqurawaman
hawlaha watunthira yawma aljamAAi larayba feehi fareequn fee aljannati
wafareequn fee assaAAeer
Swahili
Na namna hivi tumekufunulia Qur'ani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Mama wa Miji
na walio pembezoni mwake. Na uhadharishe na Siku ya Mkutano, haina shaka hiyo.
Kundi moja litakuwa Peponi, na kundi jengine Motoni.
|
Ayah 42:8 الأية
وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ لَجَعَلَهُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَٰكِن يُدْخِلُ مَن
يَشَاءُ فِي رَحْمَتِهِ ۚ وَالظَّالِمُونَ مَا لَهُم مِّن وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ
Walaw shaa Allahu lajaAAalahumommatan wahidatan walakin yudkhilu man yashaofee
rahmatihi waththalimoonama lahum min waliyyin wala naseer
Swahili
Na Mwenyezi Mungu angeli penda ange wafanya wote umma mmoja, lakini anamwingiza
katika rehema yake amtakaye. Na wenye kudhulumu hawana mlinzi wala msaidizi.
|
Ayah 42:9 الأية
أَمِ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ ۖ فَاللَّهُ هُوَ الْوَلِيُّ وَهُوَ
يُحْيِي الْمَوْتَىٰ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ
Ami ittakhathoo min doonihi awliyaafallahu huwa alwaliyyu wahuwa yuhyee
almawtawahuwa AAala kulli shay-in qadeer
Swahili
Au wamechukua walinzi wengine badala yake! Lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi
khasa. Na Yeye ndiye anaye huisha wafu. Na Yeye ndiye Mweza wa kila kitu.
|
Ayah 42:10 الأية
وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّهِ ۚ ذَٰلِكُمُ
اللَّهُ رَبِّي عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ أُنِيبُ
Wama ikhtalaftum feehi min shay-in fahukmuhuila Allahi thalikumu Allahu
rabbeeAAalayhi tawakkaltu wa-ilayhi oneeb
Swahili
Na mkikhitalifiana katika jambo lolote, basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu.
Huyo Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi, ninaye mtegemea na kwake Yeye
narejea.
|
Ayah 42:11 الأية
فَاطِرُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ جَعَلَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا
وَمِنَ الْأَنْعَامِ أَزْوَاجًا ۖ يَذْرَؤُكُمْ فِيهِ ۚ لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ
وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
Fatiru assamawatiwal-ardi jaAAala lakum min anfusikum azwajanwamina al-anAAami
azwajan yathraokum feehilaysa kamithlihi shay-on wahuwa assameeAAu albaseer
Swahili
Yeye ndiye Muumba mbingu na ardhi, amekujaalieni mke na mume katika nafsi zenu,
na katika nyama hoa dume na jike, anakuzidishieni namna hii. Hapana kitu kama
mfano wake. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona.
|
Ayah 42:12 الأية
لَهُ مَقَالِيدُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ
وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ
Lahu maqaleedu assamawatiwal-ardi yabsutu arrizqa liman yashaowayaqdiru innahu
bikulli shay-in AAaleem
Swahili
Yeye ndiye Mwenye funguo za mbingu na ardhi. Humkunjulia riziki amtakaye, na
humpimia amtakaye. Hakika Yeye ni Mjuzi wa kila kitu.
|
Ayah 42:13 الأية
شَرَعَ لَكُم مِّنَ الدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا
إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰ ۖ أَنْ أَقِيمُوا
الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ ۚ كَبُرَ عَلَى الْمُشْرِكِينَ مَا تَدْعُوهُمْ
إِلَيْهِ ۚ اللَّهُ يَجْتَبِي إِلَيْهِ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي إِلَيْهِ مَن يُنِيبُ
SharaAAa lakum mina addeeni mawassa bihi noohan wallathee awhaynailayka wama
wassayna bihi ibraheemawamoosa waAAeesa an aqeemoo addeena walatatafarraqoo
feehi kabura AAala almushrikeena matadAAoohum ilayhi Allahu yajtabee ilayhi man
yashaowayahdee ilayhi man yuneeb
Swahili
Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na
tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane
kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayo waitia. Mwenyezi Mungu humteua kwake
amtakaye, na humwongoa kwake aelekeaye.
|
Ayah 42:14 الأية
وَمَا تَفَرَّقُوا إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۚ
وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى لَّقُضِيَ
بَيْنَهُمْ ۚ وَإِنَّ الَّذِينَ أُورِثُوا الْكِتَابَ مِن بَعْدِهِمْ لَفِي شَكٍّ
مِّنْهُ مُرِيبٍ
Wama tafarraqoo illa minbaAAdi ma jaahumu alAAilmu baghyan baynahum
walawlakalimatun sabaqat min rabbika ila ajalin musamman laqudiyabaynahum
wa-inna allatheena oorithoo alkitaba minbaAAdihim lafee shakkin minhu mureeb
Swahili
Na hawakufarikiana ila baada ya kuwajia ilimu kwa sababu ya husuda iliyo kuwa
baina yao. Na lau kuwa haikwisha tangulia kauli kutoka kwa Mola wako Mlezi ya
kuakhirisha mpaka muda maalumu, basi bila ya shaka palingeli hukumiwa baina yao.
Na hakika walio rithishwa Kitabu baada yao wanakitilia shaka inayo wahangaisha.
|
Ayah 42:15 الأية
فَلِذَٰلِكَ فَادْعُ ۖ وَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ ۖ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ
ۖ وَقُلْ آمَنتُ بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ مِن كِتَابٍ ۖ وَأُمِرْتُ لِأَعْدِلَ
بَيْنَكُمُ ۖ اللَّهُ رَبُّنَا وَرَبُّكُمْ ۖ لَنَا أَعْمَالُنَا وَلَكُمْ
أَعْمَالُكُمْ ۖ لَا حُجَّةَ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ ۖ اللَّهُ يَجْمَعُ بَيْنَنَا
ۖ وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ
Falithalika fadAAu wastaqimkama omirta wala tattabiAA ahwaahum waqul amantubima
anzala Allahu min kitabin waomirtuli-aAAdila baynakum Allahu rabbuna warabbukum
lanaaAAmaluna walakum aAAmalukum la hujjatabaynana wabaynakumu Allahu yajmaAAu
baynanawa-ilayhi almaseer
Swahili
Basi kwa haya waite! Nawe simama sawa sawa kama ulivyo amrishwa, wala usiyafuate
matamanio yao. Na sema: Naamini aliyo teremsha Mwenyezi Mungu katika Vitabu. Na
nimeamrishwa nifanye uadilifu baina yenu. Mwenyezi Mungu ni Mola wetu Mlezi, na
Mola wenu Mlezi. Sisi tuna jukumu kwa vitendo vyetu, na nyinyi mna jukumu kwa
vitendo vyenu. Hapana kuhojiana baina yetu na nyinyi. Na Mwenyezi Mungu
atatukusanya pamoja, na marejeo ni kwake.
|
Ayah 42:16 الأية
وَالَّذِينَ يُحَاجُّونَ فِي اللَّهِ مِن بَعْدِ مَا اسْتُجِيبَ لَهُ حُجَّتُهُمْ
دَاحِضَةٌ عِندَ رَبِّهِمْ وَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ
Wallatheena yuhajjoonafee Allahi min baAAdi ma istujeeba lahu
hujjatuhumdahidatun AAinda rabbihim waAAalayhim ghadabunwalahum AAathabun
shadeed
Swahili
Na wanao hojiana juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kukubaliwa, hoja za hawa ni
baat'ili mbele ya Mola wao Mlezi, na juu yao ipo ghadhabu, na itakuwa kwao
adhabu kali.
|
Ayah 42:17 الأية
اللَّهُ الَّذِي أَنزَلَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ وَالْمِيزَانَ ۗ وَمَا يُدْرِيكَ
لَعَلَّ السَّاعَةَ قَرِيبٌ
Allahu allathee anzala alkitababilhaqqi walmeezani wamayudreeka laAAalla
assaAAata qareeb
Swahili
Mwenyezi Mungu ndiye aliye teremsha Kitabu kwa Haki, na Mizani. Na nini
kitakacho kujuulisha ya kwamba pengine Saa ya Kiyama ipo karibu?
|
Ayah 42:18 الأية
يَسْتَعْجِلُ بِهَا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِهَا ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا
مُشْفِقُونَ مِنْهَا وَيَعْلَمُونَ أَنَّهَا الْحَقُّ ۗ أَلَا إِنَّ الَّذِينَ
يُمَارُونَ فِي السَّاعَةِ لَفِي ضَلَالٍ بَعِيدٍ
YastaAAjilu biha allatheena layu/minoona biha wallatheena amanoomushfiqoona
minha wayaAAlamoona annaha alhaqquala inna allatheena yumaroona fee
assaAAatilafee dalalin baAAeed
Swahili
Wasio amini huihimiza hiyo Saa ifike upesi; lakini wanao amini wanaiogopa, na
wanajua kwamba hakika hiyo ni kweli. Ama kwa hakika hao wanao bishana katika
khabari za hiyo Saa wamo katika upotofu wa mbali kabisa.
|
Ayah 42:19 الأية
اللَّهُ لَطِيفٌ بِعِبَادِهِ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ ۖ وَهُوَ الْقَوِيُّ الْعَزِيزُ
Allahu lateefun biAAibadihiyarzuqu man yashao wahuwa alqawiyyu alAAazeez
Swahili
Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja wake. Humruzuku ampendaye. Naye ni Mwenye
nguvu, Mtukufu.
|
Ayah 42:20 الأية
مَن كَانَ يُرِيدُ حَرْثَ الْآخِرَةِ نَزِدْ لَهُ فِي حَرْثِهِ ۖ وَمَن كَانَ
يُرِيدُ حَرْثَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَا لَهُ فِي الْآخِرَةِ مِن
نَّصِيبٍ
Man kana yureedu hartha al-akhiratinazid lahu fee harthihi waman kana yureedu
harthaaddunya nu/tihi minha wama lahu feeal-akhirati min naseeb
Swahili
Mwenye kutaka mavuno ya Akhera tutamzidishia katika mavuno yake, na mwenye
kutaka mavuno ya duniani tutampa katika hayo, lakini katika Akhera hana fungu.
|
Ayah 42:21 الأية
أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ
اللَّهُ ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةُ الْفَصْلِ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ ۗ وَإِنَّ
الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Am lahum shurakao sharaAAoo lahummina addeeni ma lam ya/than bihi Allahuwalawla
kalimatu alfasli laqudiya baynahumwa-inna aththalimeena lahum AAathabunaleem
Swahili
Au hao wana miungu ya kishirikina walio watungia dini asiyo itolea idhini
Mwenyezi Mungu? Na lau lisinge kuwako neno la kupambanua basi wangeli katiwa
hukumu baina yao. Na hakika wenye kudhulumu watapata adhabu chungu.
|
Ayah 42:22 الأية
تَرَى الظَّالِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا كَسَبُوا وَهُوَ وَاقِعٌ بِهِمْ ۗ
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فِي رَوْضَاتِ الْجَنَّاتِ ۖ لَهُم
مَّا يَشَاءُونَ عِندَ رَبِّهِمْ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَضْلُ الْكَبِيرُ
Tara aththalimeenamushfiqeena mimma kasaboo wahuwa waqiAAun bihim
wallatheenaamanoo waAAamiloo assalihati fee rawdatialjannati lahum ma yashaoona
AAinda rabbihimthalika huwa alfadlu alkabeer
Swahili
Utawaona hao madhaalimu wanavyo kuwa na khofu kwa sababu ya waliyo yachuma, nayo
yatawafika tu. Na walio amini na wakatenda mema watakuwamo katika mabustani ya
Peponi. Humo watapata wayatakayo kwa Mola wao Mlezi. Hiyo ndiyo fadhila kubwa.
|
Ayah 42:23 الأية
ذَٰلِكَ الَّذِي يُبَشِّرُ اللَّهُ عِبَادَهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا
الصَّالِحَاتِ ۗ قُل لَّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلَّا الْمَوَدَّةَ فِي
الْقُرْبَىٰ ۗ وَمَن يَقْتَرِفْ حَسَنَةً نَّزِدْ لَهُ فِيهَا حُسْنًا ۚ إِنَّ
اللَّهَ غَفُورٌ شَكُورٌ
Thalika allathee yubashshiruAllahu AAibadahu allatheena amanoowaAAamiloo
assalihati qul laas-alukum AAalayhi ajran illa almawaddata fee alqurbawaman
yaqtarif hasanatan nazid lahu feeha husnaninna Allaha ghafoorun shakoor
Swahili
Hayo ndiyo aliyo wabashiria Mwenyezi Mungu waja wake walio amini na wakatenda
mema. Sema: Sikuombeni malipo yoyote kwenu ila mapenzi katika kujikurubisha. Na
anaye fanya wema tutamzidishia wema. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu Mwenye
shukrani.
|
Ayah 42:24 الأية
أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّهِ كَذِبًا ۖ فَإِن يَشَإِ اللَّهُ يَخْتِمْ
عَلَىٰ قَلْبِكَ ۗ وَيَمْحُ اللَّهُ الْبَاطِلَ وَيُحِقُّ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ ۚ
إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ
Am yaqooloona iftara AAala Allahikathiban fa-in yasha-i Allahu yakhtim
AAalaqalbika wayamhu Allahu albatila wayuhiqqualhaqqa bikalimatihi innahu
AAaleemun bithatiassudoor
Swahili
Ati wanasema: Amemzulia Mwenyezi Mungu uwongo? Mwenyezi Mungu akipenda atapiga
muhuri juu ya moyo wako. Na Mwenyezi Mungu anaufuta upotofu na anaithibitisha
Haki kwa maneno yake. Hakika Yeye anayajua yaliomo vifuani.
|
Ayah 42:25 الأية
وَهُوَ الَّذِي يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَعْفُو عَنِ السَّيِّئَاتِ
وَيَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ
Wahuwa allathee yaqbalu attawbataAAan AAibadihi wayaAAfoo AAani
assayyi-atiwayaAAlamu ma tafAAaloon
Swahili
Naye ndiye anaye pokea toba kwa waja wake, na anasamehe makosa, na anayajua
mnayo yatenda.
|
Ayah 42:26 الأية
وَيَسْتَجِيبُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَيَزِيدُهُم مِّن
فَضْلِهِ ۚ وَالْكَافِرُونَ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ
Wayastajeebu allatheena amanoowaAAamiloo assalihati wayazeeduhum min
fadlihiwalkafiroona lahum AAathabun shadeed
Swahili
Na anawaitikia wanao amini na wakatenda mema, na anawazidishia fadhila zake. Na
makafiri watakuwa na adhabu chungu.
|
Ayah 42:27 الأية
وَلَوْ بَسَطَ اللَّهُ الرِّزْقَ لِعِبَادِهِ لَبَغَوْا فِي الْأَرْضِ وَلَٰكِن
يُنَزِّلُ بِقَدَرٍ مَّا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ بِعِبَادِهِ خَبِيرٌ بَصِيرٌ
Walaw basata Allahu arrizqaliAAibadihi labaghaw fee al-ardi walakinyunazzilu
biqadarin ma yashao innahu biAAibadihikhabeerun baseer
Swahili
Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli wakunjulia riziki waja wake, basi bila ya
shaka wangeli panda kiburi katika dunia. Lakini anaiteremsha kwa kipimo
akitakacho. Hakika Yeye anawajua vyema waja wake na anawaona.
|
Ayah 42:28 الأية
وَهُوَ الَّذِي يُنَزِّلُ الْغَيْثَ مِن بَعْدِ مَا قَنَطُوا وَيَنشُرُ رَحْمَتَهُ
ۚ وَهُوَ الْوَلِيُّ الْحَمِيدُ
Wahuwa allathee yunazzilu alghaythamin baAAdi ma qanatoo wayanshuru
rahmatahuwahuwa alwaliyyu alhameed
Swahili
Naye ndiye anaye iteremsha mvua baada ya wao kwisha kata tamaa, na hueneza
rehema yake. Naye ndiye Mlinzi Mwenye kuhimidiwa.
|
Ayah 42:29 الأية
وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَثَّ فِيهِمَا مِن
دَابَّةٍ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ جَمْعِهِمْ إِذَا يَشَاءُ قَدِيرٌ
Wamin ayatihi khalqu assamawatiwal-ardi wama baththa feehima min dabbatinwahuwa
AAala jamAAihim itha yashao qadeer
Swahili
Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na wanyama alio waeneza. Naye
ni Mwenye uweza wa kuwakusanya apendapo.
|
Ayah 42:30 الأية
وَمَا أَصَابَكُم مِّن مُّصِيبَةٍ فَبِمَا كَسَبَتْ أَيْدِيكُمْ وَيَعْفُو عَن
كَثِيرٍ
Wama asabakum min museebatinfabima kasabat aydeekum wayaAAfoo AAan katheer
Swahili
Na misiba inayo kusibuni ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu. Naye
anasamehe mengi.
|
Ayah 42:31 الأية
وَمَا أَنتُم بِمُعْجِزِينَ فِي الْأَرْضِ ۖ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّهِ مِن
وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ
Wama antum bimuAAjizeena fee al-ardiwama lakum min dooni Allahi min waliyyin
walanaseer
Swahili
Na nyinyi hamwezi kushinda katika ardhi. Na wala nyinyi hamna mlinzi wala
msaidizi badala ya Mwenyezi Mungu.
|
Ayah 42:32 الأية
وَمِنْ آيَاتِهِ الْجَوَارِ فِي الْبَحْرِ كَالْأَعْلَامِ
Wamin ayatihi aljawarifee albahri kal-aAAlam
Swahili
Na katika Ishara zake ni vyombo vinavyo kwenda na kurejea baharini kama vilima.
|
Ayah 42:33 الأية
إِن يَشَأْ يُسْكِنِ الرِّيحَ فَيَظْلَلْنَ رَوَاكِدَ عَلَىٰ ظَهْرِهِ ۚ إِنَّ فِي
ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ
In yasha/ yuskini arreehafayathlalna rawakida AAala thahrihiinna fee thalika
laayatin likulli sabbarinshakoor
Swahili
Akitaka, huutuliza upepo navyo hivyo vyombo husimama tutwe juu ya bahari. Hakika
katika hayo zipo Ishara kwa kila mwenye kusubiri akashukuru.
|
Ayah 42:34 الأية
أَوْ يُوبِقْهُنَّ بِمَا كَسَبُوا وَيَعْفُ عَن كَثِيرٍ
Aw yoobiqhunna bima kasaboo wayaAAfuAAan katheer
Swahili
Au huviangamiza hivyo vyombo kwa sababu ya waliyo yatenda hao watu. Naye
husamehe mengi.
|
Ayah 42:35 الأية
وَيَعْلَمَ الَّذِينَ يُجَادِلُونَ فِي آيَاتِنَا مَا لَهُم مِّن مَّحِيصٍ
WayaAAlama allatheena yujadiloonafee ayatina ma lahum min mahees
Swahili
Na ili wajue wanao jadiliana katika Ishara zetu kwamba hawana pahala pa
kukimbilia.
|
Ayah 42:36 الأية
فَمَا أُوتِيتُم مِّن شَيْءٍ فَمَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَمَا عِندَ
اللَّهِ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ لِلَّذِينَ آمَنُوا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ
Fama ooteetum min shay-in famataAAualhayati addunya wama AAindaAllahi khayrun
waabqa lillatheena amanoowaAAala rabbihim yatawakkaloon
Swahili
Basi vyote mlivyo pewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilichoko kwa
Mwenyezi Mungu ni bora, na cha kudumu kwa ajili ya walio amini, na wakawa
wanamtegemea Mola wao Mlezi,
|
Ayah 42:37 الأية
وَالَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ وَإِذَا مَا
غَضِبُوا هُمْ يَغْفِرُونَ
Wallatheena yajtaniboona kaba-iraal-ithmi walfawahisha wa-itha ma ghadiboohum
yaghfiroon
Swahili
Na wanayo yaepuka madhambi makubwa na mambo machafu, na wanapo kasirika wao
husamehe,
|
Ayah 42:38 الأية
وَالَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِرَبِّهِمْ وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَأَمْرُهُمْ شُورَىٰ
بَيْنَهُمْ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ
Wallatheena istajaboolirabbihim waaqamoo assalatawaamruhum shoora baynahum
wamimma razaqnahumyunfiqoon
Swahili
Na wanao mwitikia Mola wao Mlezi, na wakashika Sala, na mambo yao yakawa ni kwa
kushauriana baina yao, na kutokana na tulicho waruzuku wakawa wanatoa,
|
Ayah 42:39 الأية
وَالَّذِينَ إِذَا أَصَابَهُمُ الْبَغْيُ هُمْ يَنتَصِرُونَ
Wallatheena itha asabahumualbaghyu hum yantasiroon
Swahili
Na ambao wanapo fanyiwa jeuri hujitetea.
|
Ayah 42:40 الأية
وَجَزَاءُ سَيِّئَةٍ سَيِّئَةٌ مِّثْلُهَا ۖ فَمَنْ عَفَا وَأَصْلَحَ فَأَجْرُهُ
عَلَى اللَّهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ
Wajazao sayyi-atin sayyi-atun mithluhafaman AAafa waaslaha faajruhu AAalaAllahi
innahu la yuhibbu aththalimeen
Swahili
Na malipo ya uovu ni uovu mfano wa huo. Lakini mwenye kusamehe, na akasuluhisha,
basi huyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye hawapendi wenye
kudhulumu.
|
Ayah 42:41 الأية
وَلَمَنِ انتَصَرَ بَعْدَ ظُلْمِهِ فَأُولَٰئِكَ مَا عَلَيْهِم مِّن سَبِيلٍ
Walamani intasara baAAda thulmihifaola-ika ma AAalayhim min sabeel
Swahili
Na wanao jitetea baada ya kudhulumiwa, hao hapana njia ya kuwalaumu.
|
Ayah 42:42 الأية
إِنَّمَا السَّبِيلُ عَلَى الَّذِينَ يَظْلِمُونَ النَّاسَ وَيَبْغُونَ فِي
الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۚ أُولَٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Innama assabeelu AAalaallatheena yathlimoona annasawayabghoona fee al-ardi
bighayri alhaqqi ola-ikalahum AAathabun aleem
Swahili
Bali lawama ipo kwa wale wanao wadhulumu watu, na wanafanya jeuri katika nchi
bila ya haki. Hao watapata adhabu iliyo chungu.
|
Ayah 42:43 الأية
وَلَمَن صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ
Walaman sabara waghafara inna thalikalamin AAazmi al-omoor
Swahili
Na anaye subiri, na akasamehe, hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.
|
Ayah 42:44 الأية
وَمَن يُضْلِلِ اللَّهُ فَمَا لَهُ مِن وَلِيٍّ مِّن بَعْدِهِ ۗ وَتَرَى
الظَّالِمِينَ لَمَّا رَأَوُا الْعَذَابَ يَقُولُونَ هَلْ إِلَىٰ مَرَدٍّ مِّن
سَبِيلٍ
Waman yudlili Allahu famalahu min waliyyin min baAAdihi watara
aththalimeenalamma raawoo alAAathaba yaqooloona hal ilamaraddin min sabeel
Swahili
Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea, hana mlinzi baada yake. Na utawaona
wenye kudhulumu watakapo iona adhabu wanasema: Je! Ipo njia ya kurudi?
|
Ayah 42:45 الأية
وَتَرَاهُمْ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا خَاشِعِينَ مِنَ الذُّلِّ يَنظُرُونَ مِن طَرْفٍ
خَفِيٍّ ۗ وَقَالَ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ الْخَاسِرِينَ الَّذِينَ خَسِرُوا
أَنفُسَهُمْ وَأَهْلِيهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ أَلَا إِنَّ الظَّالِمِينَ فِي
عَذَابٍ مُّقِيمٍ
Watarahum yuAAradoona AAalayhakhashiAAeena mina aththulli yanthuroonamin tarfin
khafiyyin waqala allatheena amanooinna alkhasireena allatheena khasiroo
anfusahumwaahleehim yawma alqiyamati ala inna aththalimeenafee AAathabin muqeem
Swahili
Na utawaona wanapelekwa kwenye Moto, nao wamenyenyekea kwa unyonge, wanatazama
kwa mtazamo wa kificho. Na walio amini watasema: Hakika wapatao khasara ni hao
walio khasiri nafsi zao na ahali zao Siku ya Kiyama. Ama hakika wenye kudhulumu
watakuwa katika adhabu ya daima.
|
Ayah 42:46 الأية
وَمَا كَانَ لَهُم مِّنْ أَوْلِيَاءَ يَنصُرُونَهُم مِّن دُونِ اللَّهِ ۗ وَمَن
يُضْلِلِ اللَّهُ فَمَا لَهُ مِن سَبِيلٍ
Wama kana lahum min awliyaayansuroonahum min dooni Allahi waman yudliliAllahu
fama lahu min sabeel
Swahili
Wala hawatakuwa na walinzi wa kuwanusuru mbele ya Mwenyezi Mungu. Na ambaye
Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea, hana njia yoyote.
|
Ayah 42:47 الأية
اسْتَجِيبُوا لِرَبِّكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا مَرَدَّ لَهُ مِنَ
اللَّهِ ۚ مَا لَكُم مِّن مَّلْجَإٍ يَوْمَئِذٍ وَمَا لَكُم مِّن نَّكِيرٍ
Istajeeboo lirabbikum min qabli an ya/tiyayawmun la maradda lahu mina Allahi ma
lakummin malja-in yawma-ithin wama lakum min nakeer
Swahili
Muitikieni Mola wenu Mlezi kabla haijafika siku isiyo epukika itokayo kwa
Mwenyezi Mungu. Siku hiyo hamtakuwa pa kukimbilia wala hamtakuwa na cha
kukingia.
|
Ayah 42:48 الأية
فَإِنْ أَعْرَضُوا فَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ۖ إِنْ عَلَيْكَ إِلَّا
الْبَلَاغُ ۗ وَإِنَّا إِذَا أَذَقْنَا الْإِنسَانَ مِنَّا رَحْمَةً فَرِحَ بِهَا ۖ
وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ فَإِنَّ الْإِنسَانَ
كَفُورٌ
Fa-in aAAradoo fama arsalnakaAAalayhim hafeethan in AAalayka illaalbalaghu
wa-inna itha athaqnaal-insana minna rahmatan fariha bihawa-in tusibhum
sayyi-atun bima qaddamat aydeehimfa-inna al-insana kafoor
Swahili
Na wakipuuza, basi Sisi hatukukupeleka ili uwe mwangalizi wao. Si juu yako ila
kufikisha Ujumbe tu. Na hakika Sisi tukimwonjesha mtu rehema kutoka kwetu,
huifurahia. Na akisibiwa na ovu kwa sababu ya iliyo yatanguliza mikono yao, basi
hakika mtu huyu anakufuru.
|
Ayah 42:49 الأية
لِّلَّهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ يَهَبُ لِمَن
يَشَاءُ إِنَاثًا وَيَهَبُ لِمَن يَشَاءُ الذُّكُورَ
Lillahi mulku assamawatiwal-ardi yakhluqu ma yashao yahabuliman yashao inathan
wayahabu liman yashao aththukoor
Swahili
Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu; anaumba apendavyo, anamtunukia
amtakaye watoto wa kike, na anamtunukia amtakaye watoto wa kiume,
|
Ayah 42:50 الأية
أَوْ يُزَوِّجُهُمْ ذُكْرَانًا وَإِنَاثًا ۖ وَيَجْعَلُ مَن يَشَاءُ عَقِيمًا ۚ
إِنَّهُ عَلِيمٌ قَدِيرٌ
Aw yuzawwijuhum thukrananwa-inathan wayajAAalu man yashao AAaqeeman
innahuAAaleemun qadeer
Swahili
Au huwachanganya wanaume na wanawake, na akamfanya amtakaye tasa. Hakika Yeye ni
Mjuzi Mwenye uweza.
|
Ayah 42:51 الأية
وَمَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُكَلِّمَهُ اللَّهُ إِلَّا وَحْيًا أَوْ مِن وَرَاءِ
حِجَابٍ أَوْ يُرْسِلَ رَسُولًا فَيُوحِيَ بِإِذْنِهِ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ
عَلِيٌّ حَكِيمٌ
Wama kana libasharin anyukallimahu Allahu illa wahyan aw min wara-ihijabin aw
yursila rasoolan fayoohiya bi-ithnihima yashao innahu AAaliyyun hakeem
Swahili
Na haikuwa kwa mwanaadamu kwamba Mwenyezi Mungu amsemeze ila kwa Wahyi (Ufunuo),
au kwa nyuma ya pazia, au kumtuma Mjumbe. Naye humfunulia ayatakayo kwa idhini
yake. Hakika Yeye ni Mtukufu, Mwenye hikima.
|
Ayah 42:52 الأية
وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِّنْ أَمْرِنَا ۚ مَا كُنتَ تَدْرِي مَا
الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَٰكِن جَعَلْنَاهُ نُورًا نَّهْدِي بِهِ مَن
نَّشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا ۚ وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ
Wakathalika awhaynailayka roohan min amrina ma kunta tadree maalkitabu wala
al-eemanu walakinjaAAalnahu nooran nahdee bihi man nashao min AAibadinawa-innaka
latahdee ila siratin mustaqeem
Swahili
Na namna hivi tumekufunulia Qur'ani kwa amri yetu. Ulikuwa hujui Kitabu ni nini,
wala Imani. Lakini tumekifanya kuwa ni Nuru ambayo kwayo tunammwongoa tumtakaye
katika waja wetu. Na hakika wewe unaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka.
|
Ayah 42:53 الأية
صِرَاطِ اللَّهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ أَلَا
إِلَى اللَّهِ تَصِيرُ الْأُمُورُ
Sirati Allahi allatheelahu ma fee assamawati wamafee al-ardi ala ila Allahi
taseerual-omoor
Swahili
Njia ya Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake Yeye tu viliomo mbinguni na katika ardhi.
Jueni kuwa mambo yote yanarudi kwa Mwenyezi Mungu.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|