1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
حم
Ha-meem
Swahili
H'a Mim
|
Ayah 43:2 الأية
وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ
Walkitabi almubeen
Swahili
Naapa kwa Kitabu kinacho bainisha.
|
Ayah 43:3 الأية
إِنَّا جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ
Inna jaAAalnahu qur-ananAAarabiyyan laAAallakum taAAqiloona
Swahili
Hakika Sisi tumeifanya Qur'ani kwa Kiarabu ili mfahamu.
|
Ayah 43:4 الأية
وَإِنَّهُ فِي أُمِّ الْكِتَابِ لَدَيْنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ
Wa-innahu fee ommi alkitabi ladaynalaAAaliyyun hakeem
Swahili
Na hakika hiyo imo katika Asili ya Maandiko yalioko kwetu, ni tukufu na yenye
hikima.
|
Ayah 43:5 الأية
أَفَنَضْرِبُ عَنكُمُ الذِّكْرَ صَفْحًا أَن كُنتُمْ قَوْمًا مُّسْرِفِينَ
Afanadribu AAankumu aththikrasafhan an kuntum qawman musrifeen
Swahili
Je! Tuache kukukumbusheni kabisa kwa kuwa nyinyi ni watu mlio pita mipaka kwa
ukafiri?
|
Ayah 43:6 الأية
وَكَمْ أَرْسَلْنَا مِن نَّبِيٍّ فِي الْأَوَّلِينَ
Wakam arsalna min nabiyyin feeal-awwaleen
Swahili
Na Manabii wangapi tuliwatuma kwa watu wa zamani!
|
Ayah 43:7 الأية
وَمَا يَأْتِيهِم مِّن نَّبِيٍّ إِلَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ
Wama ya/teehim min nabiyyin illakanoo bihi yastahzi-oon
Swahili
Na hawajii Nabii yeyote ila walikuwa wakimkejeli.
|
Ayah 43:8 الأية
فَأَهْلَكْنَا أَشَدَّ مِنْهُم بَطْشًا وَمَضَىٰ مَثَلُ الْأَوَّلِينَ
Faahlakna ashadda minhum batshanwamada mathalu al-awwaleen
Swahili
Na tuliwaangamiza walio kuwa na nguvu kushinda wao. Na mfano wa watu wa zamani
umekwisha pita.
|
Ayah 43:9 الأية
وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ
خَلَقَهُنَّ الْعَزِيزُ الْعَلِيمُ
Wala-in saaltahum man khalaqa assamawatiwal-arda layaqoolunna khalaqahunna
alAAazeezualAAaleem
Swahili
Na ukiwauliza: Nani aliye ziumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka watasema:
Kaziumba Mwenye nguvu, Mjuzi,
|
Ayah 43:10 الأية
الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ مَهْدًا وَجَعَلَ لَكُمْ فِيهَا سُبُلًا
لَّعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ
Allathee jaAAala lakumu al-ardamahdan wajaAAala lakum feeha subulan laAAallakum
tahtadoon
Swahili
Ambaye amekufanyieni ardhi kama tandiko, na akakufanyieni ndani yake njia mpate
kuongoka.
|
Ayah 43:11 الأية
وَالَّذِي نَزَّلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً بِقَدَرٍ فَأَنشَرْنَا بِهِ بَلْدَةً
مَّيْتًا ۚ كَذَٰلِكَ تُخْرَجُونَ
Wallathee nazzala mina assama-imaan biqadarin faansharna bihi baldatan maytan
kathalikatukhrajoon
Swahili
Na ambaye ndiye aliye teremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi, na kwa hayo
tukaifufua nchi iliyo kufa. Na namna hivi ndivyo mtakavyo tolewa.
|
Ayah 43:12 الأية
وَالَّذِي خَلَقَ الْأَزْوَاجَ كُلَّهَا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ الْفُلْكِ
وَالْأَنْعَامِ مَا تَرْكَبُونَ
Wallathee khalaqa al-azwajakullaha wajaAAala lakum mina alfulki wal-anAAamima
tarkaboon
Swahili
Na ambaye ndiye aliye umba katika kila kitu jike na dume, na akakufanyieni
marikebu na wanyama mnao wapanda.
|
Ayah 43:13 الأية
لِتَسْتَوُوا عَلَىٰ ظُهُورِهِ ثُمَّ تَذْكُرُوا نِعْمَةَ رَبِّكُمْ إِذَا
اسْتَوَيْتُمْ عَلَيْهِ وَتَقُولُوا سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَٰذَا وَمَا
كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ
Litastawoo AAala thuhoorihithumma tathkuroo niAAmata rabbikum itha
istawaytumAAalayhi wataqooloo subhana allathee sakhkhara lanahatha wama kunna
lahu muqrineen
Swahili
Ili mkae vizuri migongoni mwao, kisha mkumbuke neema za Mola wenu Mlezi mnapokaa
sawa sawa juu yao na mseme: Ametakasika aliye mfanya huyu atutumikie, na
tusingeli weza kufanya haya wenyewe.
|
Ayah 43:14 الأية
وَإِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا لَمُنقَلِبُونَ
Wa-inna ila rabbinalamunqaliboon
Swahili
Na hakika sisi tutarudi kwa Mola wetu Mlezi.
|
Ayah 43:15 الأية
وَجَعَلُوا لَهُ مِنْ عِبَادِهِ جُزْءًا ۚ إِنَّ الْإِنسَانَ لَكَفُورٌ مُّبِينٌ
WajaAAaloo lahu min AAibadihi juz-aninna al-insana lakafoorun mubeen
Swahili
Na wanamfanyia katika waja wake fungu. Kwa hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila
aliye dhaahiri.
|
Ayah 43:16 الأية
أَمِ اتَّخَذَ مِمَّا يَخْلُقُ بَنَاتٍ وَأَصْفَاكُم بِالْبَنِينَ
Ami ittakhatha mimma yakhluqubanatin waasfakum bilbaneen
Swahili
Au amejichukulia watoto wanawake katika vile alivyo viumba, na akakuteulieni
nyinyi watoto wanaume?
|
Ayah 43:17 الأية
وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِمَا ضَرَبَ لِلرَّحْمَٰنِ مَثَلًا ظَلَّ وَجْهُهُ
مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ
Wa-itha bushshira ahaduhum bimadaraba lirrahmani mathalan thallawajhuhu
muswaddan wahuwa katheem
Swahili
Na anapo bashiriwa mmoja wao kwa yale aliyo mpigia mfano Mwenyezi Mungu, uso
wake husawijika na hujaa hasira.
|
Ayah 43:18 الأية
أَوَمَن يُنَشَّأُ فِي الْحِلْيَةِ وَهُوَ فِي الْخِصَامِ غَيْرُ مُبِينٍ
Awaman yunashshao fee alhilyatiwahuwa fee alkhisami ghayru mubeen
Swahili
Ati aliye lelewa katika mapambo, na katika mabishano hawezi kusema kwa
bayana...?
|
Ayah 43:19 الأية
وَجَعَلُوا الْمَلَائِكَةَ الَّذِينَ هُمْ عِبَادُ الرَّحْمَٰنِ إِنَاثًا ۚ
أَشَهِدُوا خَلْقَهُمْ ۚ سَتُكْتَبُ شَهَادَتُهُمْ وَيُسْأَلُونَ
WajaAAaloo almala-ikata allatheenahum AAibadu arrahmani inathanashahidoo
khalqahum satuktabu shahadatuhum wayus-aloon
Swahili
Na wakawafanya Malaika, ambao ni waja wa Mwingi wa Rehema, ni wanawake! Kwani
wameshuhudia kuumbwa kwao? Ushahidi wao utaandikwa na wao watahojiwa!
|
Ayah 43:20 الأية
وَقَالُوا لَوْ شَاءَ الرَّحْمَٰنُ مَا عَبَدْنَاهُم ۗ مَّا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنْ
عِلْمٍ ۖ إِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ
Waqaloo law shaa arrahmanuma AAabadnahum ma lahum bithalika minAAilmin in hum
illa yakhrusoon
Swahili
Nao husema: Angeli penda Mwingi wa Rehema tusingeli waabudu sisi. Hawana ujuzi
wowote wa hayo! Hawana ila kusema uwongo tu!
|
Ayah 43:21 الأية
أَمْ آتَيْنَاهُمْ كِتَابًا مِّن قَبْلِهِ فَهُم بِهِ مُسْتَمْسِكُونَ
Am ataynahum kitabanmin qablihi fahum bihi mustamsikoon
Swahili
Kwani tuliwapa Kitabu kabla ya hichi, na ikawa wao wanakishikilia hicho?
|
Ayah 43:22 الأية
بَلْ قَالُوا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم
مُّهْتَدُونَ
Bal qaloo inna wajadna abaanaAAala ommatin wa-inna AAala atharihimmuhtadoon
Swahili
Bali wanasema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi, basi na
sisi tunaongoza nyayo zao.
|
Ayah 43:23 الأية
وَكَذَٰلِكَ مَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّذِيرٍ إِلَّا قَالَ
مُتْرَفُوهَا إِنَّا وَجَدْنَا آبَاءَنَا عَلَىٰ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰ آثَارِهِم
مُّقْتَدُونَ
Wakathalika ma arsalnamin qablika fee qaryatin min natheerin illa qalamutrafooha
inna wajadna abaanaAAala ommatin wa-inna AAala atharihimmuqtadoon
Swahili
Na kadhaalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote ila watu wake walio deka
kwa starehe walisema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini makhsusi,
na sisi tunafuata nyayo zao.
|
Ayah 43:24 الأية
قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكُم بِأَهْدَىٰ مِمَّا وَجَدتُّمْ عَلَيْهِ آبَاءَكُمْ ۖ
قَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ كَافِرُونَ
Qala awa law ji/tukum bi-ahdamimma wajadtum AAalayhi abaakum qalooinna bima
orsiltum bihi kafiroon
Swahili
Akasema (Mwonyaji): Hata nikikuleteeni yenye uwongofu bora kuliko mlio wakuta
nao baba zenu? Wakasema: Sisi tunayakataa tu hayo mliyo tumwa.
|
Ayah 43:25 الأية
فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ
Fantaqamna minhum fanthurkayfa kana AAaqibatu almukaththibeen
Swahili
Basi tukawalipizia. Angalia ulikuwaje mwisho wa walio kadhibisha!
|
Ayah 43:26 الأية
وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِّمَّا
تَعْبُدُونَ
Wa-ith qala ibraheemuli-abeehi waqawmihi innanee baraon mimma taAAbudoon
Swahili
Na pale Ibrahim alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Hakika mimi ninajitenga
mbali na hayo mnayo yaabudu,
|
Ayah 43:27 الأية
إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ
Illa allathee fataraneefa-innahu sayahdeen
Swahili
Isipo kuwa yule aliye niumba, kwani Yeye ataniongoa.
|
Ayah 43:28 الأية
وَجَعَلَهَا كَلِمَةً بَاقِيَةً فِي عَقِبِهِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ
WajaAAalaha kalimatan baqiyatanfee AAaqibihi laAAallahum yarjiAAoon
Swahili
Na akalifanya hili liwe neno lenye kubaki katika vizazi vyake ili warejee.
|
Ayah 43:29 الأية
بَلْ مَتَّعْتُ هَٰؤُلَاءِ وَآبَاءَهُمْ حَتَّىٰ جَاءَهُمُ الْحَقُّ وَرَسُولٌ
مُّبِينٌ
Bal mattaAAtu haola-i waabaahumhatta jaahumu alhaqqu warasoolunmubeen
Swahili
Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka ikawafikia Haki na Mtume aliye
bainisha.
|
Ayah 43:30 الأية
وَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ قَالُوا هَٰذَا سِحْرٌ وَإِنَّا بِهِ كَافِرُونَ
Walamma jaahumu alhaqquqaloo hatha sihrun wa-inna bihi kafiroon
Swahili
Na ilipo wafikia Haki wakasema: Huu ni uchawi, na sisi hakika tunaukataa.
|
Ayah 43:31 الأية
وَقَالُوا لَوْلَا نُزِّلَ هَٰذَا الْقُرْآنُ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنَ الْقَرْيَتَيْنِ
عَظِيمٍ
Waqaloo lawla nuzzila hathaalqur-anu AAala rajulin mina alqaryatayni AAatheem
Swahili
Na walisema: Kwa nini Qur'ani hii haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji
miwili hii?
|
Ayah 43:32 الأية
أَهُمْ يَقْسِمُونَ رَحْمَتَ رَبِّكَ ۚ نَحْنُ قَسَمْنَا بَيْنَهُم مَّعِيشَتَهُمْ
فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَرَفَعْنَا بَعْضَهُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ
لِّيَتَّخِذَ بَعْضُهُم بَعْضًا سُخْرِيًّا ۗ وَرَحْمَتُ رَبِّكَ خَيْرٌ مِّمَّا
يَجْمَعُونَ
Ahum yaqsimoona rahmata rabbika nahnuqasamna baynahum maAAeeshatahum fee
alhayatiaddunya warafaAAna baAAdahum fawqabaAAdin darajatin liyattakhitha
baAAduhumbaAAdan sukhriyyan warahmatu rabbika khayrun mimmayajmaAAoon
Swahili
Kwani wao ndio wanao gawa rehema za Mola wako Mlezi? Sisi tumewagawanyia baina
yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawanyanyua baadhi yao juu ya
wengine kwa daraja nyingi; kwa hivyo baadhi yao wanawafanya wenginewe
wawatumikie. Na rehema za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya.
|
Ayah 43:33 الأية
وَلَوْلَا أَن يَكُونَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً لَّجَعَلْنَا لِمَن يَكْفُرُ
بِالرَّحْمَٰنِ لِبُيُوتِهِمْ سُقُفًا مِّن فِضَّةٍ وَمَعَارِجَ عَلَيْهَا
يَظْهَرُونَ
Walawla an yakoona annasuommatan wahidatan lajaAAalna liman yakfuru
birrahmanilibuyootihim suqufan min fiddatin wamaAAarijaAAalayha yathharoon
Swahili
Na lau isinge kuwa watu watakuwa kundi moja tungeli wajaalia wanao mkufuru
Rahmani wana nyumba zao zina dari ya fedha, na ngazi zao pia wanazo pandia,
|
Ayah 43:34 الأية
وَلِبُيُوتِهِمْ أَبْوَابًا وَسُرُرًا عَلَيْهَا يَتَّكِئُونَ
Walibuyootihim abwaban wasururanAAalayha yattaki-oon
Swahili
Na milango ya nyumba zao na vitanda wanavyo egemea juu yake,
|
Ayah 43:35 الأية
وَزُخْرُفًا ۚ وَإِن كُلُّ ذَٰلِكَ لَمَّا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ
وَالْآخِرَةُ عِندَ رَبِّكَ لِلْمُتَّقِينَ
Wazukhrufan wa-in kullu thalika lammamataAAu alhayati addunya wal-akhiratuAAinda
rabbika lilmuttaqeen
Swahili
Na mapambo. Lakini hayo si chochote ila ni starehe ya maisha ya dunia tu, na
Akhera iliyoko kwa Mola wako Mlezi ni ya wenye kumchamngu.
|
Ayah 43:36 الأية
وَمَن يَعْشُ عَن ذِكْرِ الرَّحْمَٰنِ نُقَيِّضْ لَهُ شَيْطَانًا فَهُوَ لَهُ
قَرِينٌ
Waman yaAAshu AAan thikri arrahmaninuqayyid lahu shaytanan fahuwa lahu qareen
Swahili
Anaye yafanyia upofu maneno ya Rahmani tunamwekea Shet'ani kuwa ndiye rafiki
yake.
|
Ayah 43:37 الأية
وَإِنَّهُمْ لَيَصُدُّونَهُمْ عَنِ السَّبِيلِ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُم مُّهْتَدُونَ
Wa-innahum layasuddoonahum AAani assabeeliwayahsaboona annahum muhtadoon
Swahili
Na hakika wao wanawazuilia Njia na wenyewe wanadhani kuwa wameongoka.
|
Ayah 43:38 الأية
حَتَّىٰ إِذَا جَاءَنَا قَالَ يَا لَيْتَ بَيْنِي وَبَيْنَكَ بُعْدَ
الْمَشْرِقَيْنِ فَبِئْسَ الْقَرِينُ
Hatta itha jaanaqala ya layta baynee wabaynaka buAAda almashriqaynifabi/sa
alqareen
Swahili
Hata atakapo tujia atasema: Laiti ungeli kuwako baina yangu na wewe kama umbali
baina ya mashariki na magharibi. Rafiki mwovu mno wewe!
|
Ayah 43:39 الأية
وَلَن يَنفَعَكُمُ الْيَوْمَ إِذ ظَّلَمْتُمْ أَنَّكُمْ فِي الْعَذَابِ
مُشْتَرِكُونَ
Walan yanfaAAakumu alyawma ith thalamtumannakum fee alAAathabi mushtarikoon
Swahili
Na kwa kuwa mlidhulumu, haitakufaeni kitu leo kwamba nyinyi mnashirikiana katika
adhabu.
|
Ayah 43:40 الأية
أَفَأَنتَ تُسْمِعُ الصُّمَّ أَوْ تَهْدِي الْعُمْيَ وَمَن كَانَ فِي ضَلَالٍ
مُّبِينٍ
Afaanta tusmiAAu assumma awtahdee alAAumya waman kana fee dalalinmubeen
Swahili
Je! Unaweza kuwasikilizisha viziwi, au unaweza kuwaongoa vipofu na waliomo
katika upotofu ulio wazi?
|
Ayah 43:41 الأية
فَإِمَّا نَذْهَبَنَّ بِكَ فَإِنَّا مِنْهُم مُّنتَقِمُونَ
Fa-imma nathhabanna bikafa-inna minhum muntaqimoon
Swahili
Na hata tukikuondoa, Sisi tutalipiza kisasi chetu kwao.
|
Ayah 43:42 الأية
أَوْ نُرِيَنَّكَ الَّذِي وَعَدْنَاهُمْ فَإِنَّا عَلَيْهِم مُّقْتَدِرُونَ
Aw nuriyannaka allathee waAAadnahumfa-inna AAalayhim muqtadiroon
Swahili
Au tutakuonyesha tulio waahidi. Nasi bila ya shaka tuna uweza juu yao.
|
Ayah 43:43 الأية
فَاسْتَمْسِكْ بِالَّذِي أُوحِيَ إِلَيْكَ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ
Fastamsik billatheeoohiya ilayka innaka AAala siratinmustaqeem
Swahili
Basi wewe yashike yaliyo funuliwa kwako. Hakika wewe uko kwenye Njia Iliyo
Nyooka.
|
Ayah 43:44 الأية
وَإِنَّهُ لَذِكْرٌ لَّكَ وَلِقَوْمِكَ ۖ وَسَوْفَ تُسْأَلُونَ
Wa-innahu lathikrun laka waliqawmikawasawfa tus-aloon
Swahili
Na hakika haya ni ukumbusho kwako na kwa kaumu yako. Na mtakuja ulizwa.
|
Ayah 43:45 الأية
وَاسْأَلْ مَنْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رُّسُلِنَا أَجَعَلْنَا مِن دُونِ
الرَّحْمَٰنِ آلِهَةً يُعْبَدُونَ
Was-al man arsalna minqablika min rusulina ajaAAalna min dooni arrahmanialihatan
yuAAbadoon
Swahili
Na waulize Mitume wetu tulio watuma kabla yako: Je! Tulifanya miungu mingine
iabudiwe badala ya Rah'mani?
|
Ayah 43:46 الأية
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَقَالَ
إِنِّي رَسُولُ رَبِّ الْعَالَمِينَ
Walaqad arsalna moosa bi-ayatinaila firAAawna wamala-ihi faqala innee rasoolu
rabbialAAalameen
Swahili
Na bila ya shaka tulimtuma Musa kwa Ishara zetu ende kwa Firauni na waheshimiwa
wake, na akasema: Hakika mimi ni Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote!
|
Ayah 43:47 الأية
فَلَمَّا جَاءَهُم بِآيَاتِنَا إِذَا هُم مِّنْهَا يَضْحَكُونَ
Falamma jaahum bi-ayatinaitha hum minha yadhakoon
Swahili
Lakini alipo wajia na Ishara zetu wakaingia kuzicheka.
|
Ayah 43:48 الأية
وَمَا نُرِيهِم مِّنْ آيَةٍ إِلَّا هِيَ أَكْبَرُ مِنْ أُخْتِهَا ۖ وَأَخَذْنَاهُم
بِالْعَذَابِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ
Wama nureehim min ayatin illahiya akbaru min okhtiha waakhathnahum
bilAAathabilaAAallahum yarjiAAoon
Swahili
Na hatukuwaonyesha Ishara yoyote ila hiyo ilikuwa kubwa zaidi kuliko nyenginewe.
Na tukawakamata kwa adhabu ili warejee.
|
Ayah 43:49 الأية
وَقَالُوا يَا أَيُّهَ السَّاحِرُ ادْعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَ
إِنَّنَا لَمُهْتَدُونَ
Waqaloo ya ayyuha asahiruodAAu lana rabbaka bima AAahida AAindaka
innanalamuhtadoon
Swahili
Na wakasema: Ewe mchawi! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa ile ahadi aliyo
kuahidi; hakika sisi tutakuwa wenye kuongoka.
|
Ayah 43:50 الأية
فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُمُ الْعَذَابَ إِذَا هُمْ يَنكُثُونَ
Falamma kashafna AAanhumualAAathaba itha hum yankuthoon
Swahili
Basi tulipo waondolea adhabu hiyo, mara wakaingia kuvunja ahadi.
|
Ayah 43:51 الأية
وَنَادَىٰ فِرْعَوْنُ فِي قَوْمِهِ قَالَ يَا قَوْمِ أَلَيْسَ لِي مُلْكُ مِصْرَ
وَهَٰذِهِ الْأَنْهَارُ تَجْرِي مِن تَحْتِي ۖ أَفَلَا تُبْصِرُونَ
Wanada firAAawnu fee qawmihi qalaya qawmi alaysa lee mulku misra
wahathihial-anharu tajree min tahtee afala tubsiroon
Swahili
Na Firauni alitangaza kwa watu wake, akisema: Enyi watu wangu! Kwani mimi sinao
huu ufalme wa Misri, na hii mito inapita chini yangu? Je! Hamwoni?
|
Ayah 43:52 الأية
أَمْ أَنَا خَيْرٌ مِّنْ هَٰذَا الَّذِي هُوَ مَهِينٌ وَلَا يَكَادُ يُبِينُ
Am ana khayrun min hatha allatheehuwa maheenun wala yakadu yubeen
Swahili
Au mimi si bora kuliko huyu aliye mnyonge, wala hawezi kusema waziwazi?
|
Ayah 43:53 الأية
فَلَوْلَا أُلْقِيَ عَلَيْهِ أَسْوِرَةٌ مِّن ذَهَبٍ أَوْ جَاءَ مَعَهُ
الْمَلَائِكَةُ مُقْتَرِنِينَ
Falawla olqiya AAalayhi aswiratun minthahabin aw jaa maAAahu
almala-ikatumuqtarineen
Swahili
Basi mbona hakuvikwa vikuku vya dhahabu, au hawakuja Malaika pamoja naye
wakamwandama?
|
Ayah 43:54 الأية
فَاسْتَخَفَّ قَوْمَهُ فَأَطَاعُوهُ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ
Fastakhaffa qawmahu faataAAoohuinnahum kanoo qawman fasiqeen
Swahili
Basi aliwachezea watu wake, na wakamt'ii. Kwa hakika hao walikuwa watu wapotovu.
|
Ayah 43:55 الأية
فَلَمَّا آسَفُونَا انتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَاهُمْ أَجْمَعِينَ
Falamma asafoonaintaqamna minhum faaghraqnahum ajmaAAeen
Swahili
Walipo tukasirisha tuliwapatiliza tukawazamisha wote!
|
Ayah 43:56 الأية
فَجَعَلْنَاهُمْ سَلَفًا وَمَثَلًا لِّلْآخِرِينَ
FajaAAalnahum salafan wamathalan lil-akhireen
Swahili
Kisha tukawafanya kuwa watangulizi na mfano kwa wa baadaye.
|
Ayah 43:57 الأية
وَلَمَّا ضُرِبَ ابْنُ مَرْيَمَ مَثَلًا إِذَا قَوْمُكَ مِنْهُ يَصِدُّونَ
Walamma duriba ibnu maryamamathalan itha qawmuka minhu yasiddoon
Swahili
Na alipo pigiwa mfano Mwana wa Mariamu, watu wako waliupiga ukelele.
|
Ayah 43:58 الأية
وَقَالُوا أَآلِهَتُنَا خَيْرٌ أَمْ هُوَ ۚ مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًا ۚ
بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ
Waqaloo aalihatunakhayrun am huwa ma daraboohu laka illajadalan bal hum qawmun
khasimoon
Swahili
Wakasema: Miungu yetu kwani si bora kuliko huyu? Hawakukupigia mfano huo ila kwa
ubishi tu. Bali hao ni watu wagomvi!
|
Ayah 43:59 الأية
إِنْ هُوَ إِلَّا عَبْدٌ أَنْعَمْنَا عَلَيْهِ وَجَعَلْنَاهُ مَثَلًا لِّبَنِي
إِسْرَائِيلَ
In huwa illa AAabdun anAAamnaAAalayhi wajaAAalnahu mathalan libanee isra-eel
Swahili
Hakuwa yeye (Isa) ila ni Mtumwa tuliye mneemesha na tukamfanya ni mfano kwa Wana
wa Israili.
|
Ayah 43:60 الأية
وَلَوْ نَشَاءُ لَجَعَلْنَا مِنكُم مَّلَائِكَةً فِي الْأَرْضِ يَخْلُفُونَ
Walaw nashao lajaAAalna minkummala-ikatan fee al-ardi yakhlufoon
Swahili
Na tungeli penda tungeli wafanyia miongoni mwenu Malaika katika ardhi
wakifuatana.
|
Ayah 43:61 الأية
وَإِنَّهُ لَعِلْمٌ لِّلسَّاعَةِ فَلَا تَمْتَرُنَّ بِهَا وَاتَّبِعُونِ ۚ هَٰذَا
صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ
Wa-innahu laAAilmun lissaAAatifala tamtarunna biha wattabiAAooni hathasiratun
mustaqeem
Swahili
Na kwa hakika yeye ni alama ya Saa ya Kiyama. Basi usiitilie shaka, na
nifuateni. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka.
|
Ayah 43:62 الأية
وَلَا يَصُدَّنَّكُمُ الشَّيْطَانُ ۖ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ
Wala yasuddannakumu ashshaytanuinnahu lakum AAaduwwun mubeen
Swahili
Wala asikuzuilieni Shet'ani. Hakika yeye ni adui yenu wa dhaahiri.
|
Ayah 43:63 الأية
وَلَمَّا جَاءَ عِيسَىٰ بِالْبَيِّنَاتِ قَالَ قَدْ جِئْتُكُم بِالْحِكْمَةِ
وَلِأُبَيِّنَ لَكُم بَعْضَ الَّذِي تَخْتَلِفُونَ فِيهِ ۖ فَاتَّقُوا اللهَ
وَأَطِيعُونِ
Walamma jaa AAeesa bilbayyinatiqala qad ji/tukum bilhikmati wali-obayyinalakum
baAAda allathee takhtalifoona feehi fattaqooAllaha waateeAAoon
Swahili
Na alipo kuja Isa na dalili zilizo wazi, alisema: Nimekujieni na hikima, na ili
nikuelezeni baadhi ya yale mliyo khitalifiana. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na
mnit'ii mimi.
|
Ayah 43:64 الأية
إِنَّ اللهَ هُوَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ هَٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ
Inna Allaha huwa rabbee warabbukum faAAbudoohuhatha siratun mustaqeem
Swahili
Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, na ni Mola wenu Mlezi. Basi
Muabuduni Yeye tu. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka.
|
Ayah 43:65 الأية
فَاخْتَلَفَ الْأَحْزَابُ مِن بَيْنِهِمْ ۖ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ ظَلَمُوا مِنْ
عَذَابِ يَوْمٍ أَلِيمٍ
Fakhtalafa al-ahzabumin baynihim fawaylun lillatheena thalamoomin AAathabi
yawmin aleem
Swahili
Lakini makundi kwa makundi yao yalikhitalifiana wao kwa wao. Ole wao walio
dhulumu kwa adhabu ya siku chungu.
|
Ayah 43:66 الأية
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَن تَأْتِيَهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا
يَشْعُرُونَ
Hal yanthuroona illa assaAAataan ta/tiyahum baghtatan wahum la yashAAuroon
Swahili
Je! Nini wanangojea ila Saa iwajie kwa ghafla na wala wao hawatambui?
|
Ayah 43:67 الأية
الْأَخِلَّاءُ يَوْمَئِذٍ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ إِلَّا الْمُتَّقِينَ
Al-akhillao yawma-ithin baAAduhumlibaAAdin AAaduwwun illa almuttaqeen
Swahili
Siku hiyo marafiki watakuwa ni maadui, wao kwa wao, isipo kuwa wachamngu.
|
Ayah 43:68 الأية
يَا عِبَادِ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمُ الْيَوْمَ وَلَا أَنتُمْ تَحْزَنُونَ
Ya AAibadi la khawfunAAalaykumu alyawma wala antum tahzanoon
Swahili
Enyi waja wangu! Hamtakuwa na khofu siku hiyo, wala hamtahuzunika.
|
Ayah 43:69 الأية
الَّذِينَ آمَنُوا بِآيَاتِنَا وَكَانُوا مُسْلِمِينَ
Allatheena amanoo bi-ayatinawakanoo muslimeen
Swahili
Ambao waliziamini Ishara zangu na walikuwa Waislamu.
|
Ayah 43:70 الأية
ادْخُلُوا الْجَنَّةَ أَنتُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ تُحْبَرُونَ
Odkhuloo aljannata antum waazwajukumtuhbaroon
Swahili
Ingieni Peponi, nyinyi na wake zenu; mtafurahishwa humo.
|
Ayah 43:71 الأية
يُطَافُ عَلَيْهِم بِصِحَافٍ مِّن ذَهَبٍ وَأَكْوَابٍ ۖ وَفِيهَا مَا تَشْتَهِيهِ
الْأَنفُسُ وَتَلَذُّ الْأَعْيُنُ ۖ وَأَنتُمْ فِيهَا خَالِدُونَ
Yutafu AAalayhim bisihafinmin thahabin waakwabin wafeeha matashtaheehi al-anfusu
watalaththu al-aAAyunu waantum feehakhalidoon
Swahili
Watakuwa wanapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe; na vitakuwamo ambavyo nafsi
zinavipenda na macho yanavifurahia, na nyinyi mtakaa humo milele.
|
Ayah 43:72 الأية
وَتِلْكَ الْجَنَّةُ الَّتِي أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Watilka aljannatu allatee oorithtumoohabima kuntum taAAmaloon
Swahili
Na hiyo ni Pepo mliyo rithishwa kwa hayo mliyo kuwa mkiyafanya.
|
Ayah 43:73 الأية
لَكُمْ فِيهَا فَاكِهَةٌ كَثِيرَةٌ مِّنْهَا تَأْكُلُونَ
Lakum feeha fakihatunkatheeratun minha ta/kuloon
Swahili
Mnayo humo matunda mengi mtakayo yala.
|
Ayah 43:74 الأية
إِنَّ الْمُجْرِمِينَ فِي عَذَابِ جَهَنَّمَ خَالِدُونَ
Inna almujrimeena fee AAathabijahannama khalidoon
Swahili
Kwa hakika wakosefu watakaa katika adhabu ya Jahannamu.
|
Ayah 43:75 الأية
لَا يُفَتَّرُ عَنْهُمْ وَهُمْ فِيهِ مُبْلِسُونَ
La yufattaru AAanhum wahum feehimublisoon
Swahili
Hawatapumzishwa nayo na humo watakata tamaa.
|
Ayah 43:76 الأية
وَمَا ظَلَمْنَاهُمْ وَلَٰكِن كَانُوا هُمُ الظَّالِمِينَ
Wama thalamnahumwalakin kanoo humu aththalimeen
Swahili
Wala Sisi hatukuwadhulumu, bali wao ndio walio kuwa madhaalimu.
|
Ayah 43:77 الأية
وَنَادَوْا يَا مَالِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ ۖ قَالَ إِنَّكُم مَّاكِثُونَ
Wanadaw ya maliku liyaqdiAAalayna rabbuka qala innakum makithoon
Swahili
Nao watapiga kelele waseme: Ewe Malik! Na atufishe Mola wako Mlezi! Naye aseme:
Hakika nyinyi mtakaa humo humo!
|
Ayah 43:78 الأية
لَقَدْ جِئْنَاكُم بِالْحَقِّ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَكُمْ لِلْحَقِّ كَارِهُونَ
Laqad ji/nakum bilhaqqiwalakinna aktharakum lilhaqqi karihoon
Swahili
Kwa yakini tulikuleteeni Haki, lakini wengi katika nyinyi mlikuwa mnaichukia
Haki.
|
Ayah 43:79 الأية
أَمْ أَبْرَمُوا أَمْرًا فَإِنَّا مُبْرِمُونَ
Am abramoo amran fa-inna mubrimoon
Swahili
Au waliweza kupitisha amri yao? Bali ni Sisi ndio tunao pitisha.
|
Ayah 43:80 الأية
أَمْ يَحْسَبُونَ أَنَّا لَا نَسْمَعُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَاهُم ۚ بَلَىٰ وَرُسُلُنَا
لَدَيْهِمْ يَكْتُبُونَ
Am yahsaboona anna lanasmaAAu sirrahum wanajwahum bala warusulunaladayhim
yaktuboon
Swahili
Au wanadhani kwamba hatusikii siri zao na minong'ono yao? Wapi! Na wajumbe wetu
wapo karibu nao, wanayaandika.
|
Ayah 43:81 الأية
قُلْ إِن كَانَ لِلرَّحْمَٰنِ وَلَدٌ فَأَنَا أَوَّلُ الْعَابِدِينَ
Qul in kana lirrahmaniwaladun faana awwalu alAAabideen
Swahili
Sema: Ingeli kuwa Rahmani ana mwana, basi mimi ningeli kuwa wa kwanza kumuabudu.
|
Ayah 43:82 الأية
سُبْحَانَ رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبِّ الْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ
Subhana rabbi assamawatiwal-ardi rabbi alAAarshi AAamma yasifoon
Swahili
Ametakasika Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, Mola Mlezi wa A'rshi, na hayo wanayo
msifia.
|
Ayah 43:83 الأية
فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي
يُوعَدُونَ
Fatharhum yakhoodoowayalAAaboo hatta yulaqoo yawmahumu allatheeyooAAadoon
Swahili
Basi waache wapige porojo wakicheza mpaka wakutwe na hiyo siku yao waliyo
ahidiwa.
|
Ayah 43:84 الأية
وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَٰهٌ وَفِي الْأَرْضِ إِلَٰهٌ ۚ وَهُوَ
الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ
Wahuwa allathee fee assama-iilahun wafee al-ardi ilahun wahuwa
alhakeemualAAaleem
Swahili
Na Yeye ndiye Mungu mbinguni, na ndiye Mungu katika ardhi. Naye ndiye Mwenye
hikima, Mwenye ujuzi.
|
Ayah 43:85 الأية
وَتَبَارَكَ الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا
وَعِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ
Watabaraka allathee lahu mulkuassamawati wal-ardi wamabaynahuma waAAindahu
AAilmu assaAAatiwa-ilayhi turjaAAoon
Swahili
Na ametukuka Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo ndani yake. Na uko
kwake ujuzi wa Saa ya Kiyama, na kwake Yeye mtarudishwa.
|
Ayah 43:86 الأية
وَلَا يَمْلِكُ الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ الشَّفَاعَةَ إِلَّا مَن شَهِدَ
بِالْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ
Wala yamliku allatheenayadAAoona min doonihi ashshafaAAata illaman shahida
bilhaqqi wahum yaAAlamoon
Swahili
Wala hao mnao waomba badala yake Yeye hawana uweza wa kumwombea mtu, isipo kuwa
anaye shuhudia kwa haki, na wao wanajua.
|
Ayah 43:87 الأية
وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَهُمْ لَيَقُولُنَّ اللهُ ۖ فَأَنَّىٰ
يُؤْفَكُونَ
Wala-in saaltahum man khalaqahumlayaqoolunna Allahu faanna yu/fakoon
Swahili
Na ukiwauliza ni nani aliye waumba? Bila ya shaka watasema: Mwenyezi Mungu! Basi
ni wapi wanako geuziwa?
|
Ayah 43:88 الأية
وَقِيلِهِ يَا رَبِّ إِنَّ هَٰؤُلَاءِ قَوْمٌ لَّا يُؤْمِنُونَ
Waqeelihi ya rabbi inna haola-iqawmun la yu/minoon
Swahili
Na usemi wake (Mtume) ni: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika hawa ni watu wasio amini.
|
Ayah 43:89 الأية
فَاصْفَحْ عَنْهُمْ وَقُلْ سَلَامٌ ۚ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ
Fasfah AAanhum waqulsalamun fasawfa yaAAlamoon
Swahili
Basi wasamehe, na uwambie maneno ya salama. Watakuja jua.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|