1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللهِ أَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ
Allatheena kafaroo wasaddooAAan sabeeli Allahi adalla aAAmalahum
Swahili
Walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, Yeye atavipotoa vitendo vyao.
|
Ayah 47:2 الأية
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَآمَنُوا بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ
مُحَمَّدٍ وَهُوَ الْحَقُّ مِن رَّبِّهِمْ ۙ كَفَّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ
وَأَصْلَحَ بَالَهُمْ
Wallatheena amanoowaAAamiloo assalihati waamanoo bimanuzzila AAala muhammadin
wahuwa alhaqqu minrabbihim kaffara AAanhum sayyi-atihim waaslahabalahum
Swahili
Na walio amini, na wakatenda mema, na wakaamini aliyo teremshiwa Muhammad - nayo
ni Haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi - atawafutia makosa yao na ataitengeneza
hali yao.
|
Ayah 47:3 الأية
ذَٰلِكَ بِأَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا اتَّبَعُوا الْبَاطِلَ وَأَنَّ الَّذِينَ
آمَنُوا اتَّبَعُوا الْحَقَّ مِن رَّبِّهِمْ ۚ كَذَٰلِكَ يَضْرِبُ اللهُ
لِلنَّاسِ أَمْثَالَهُمْ
Thalika bi-anna allatheenakafaroo ittabaAAoo albatila waanna allatheena
amanooittabaAAoo alhaqqa min rabbihim kathalika yadribuAllahu linnasi amthalahum
Swahili
Hayo ni kwa sababu walio kufuru wamefuata upotovu, na walio amini wamefuata Haki
iliyo toka kwa Mola wao Mlezi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo wapigia watu
mifano yao.
|
Ayah 47:4 الأية
فَإِذَا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا فَضَرْبَ الرِّقَابِ حَتَّىٰ إِذَا
أَثْخَنتُمُوهُمْ فَشُدُّوا الْوَثَاقَ فَإِمَّا مَنًّا بَعْدُ وَإِمَّا فِدَاءً
حَتَّىٰ تَضَعَ الْحَرْبُ أَوْزَارَهَا ۚ ذَٰلِكَ وَلَوْ يَشَاءُ اللهُ
لَانتَصَرَ مِنْهُمْ وَلَٰكِن لِّيَبْلُوَ بَعْضَكُم بِبَعْضٍ ۗ وَالَّذِينَ
قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللهِ فَلَن يُضِلَّ أَعْمَالَهُمْ
Fa-itha laqeetumu allatheenakafaroo fadarba arriqabi hattaitha athkhantumoohum
fashuddoo alwathaqa fa-immamannan baAAdu wa-imma fidaan hatta tadaAAaalharbu
awzaraha thalika walaw yashaoAllahu lantasara minhum walakinliyabluwa baAAdakum
bibaAAdin wallatheenaqutiloo fee sabeeli Allahi falan yudillaaAAmalahum
Swahili
Basi mnapo wakuta walio kufuru wapigeni shingoni mwao, mpaka mkiwadhoofisha
wafungeni pingu. Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe, mpaka vita vipoe.
Ndio hivyo. Na lau angeli taka Mwenyezi Mungu angeli washinda mwenyewe, lakini
haya ni kwa sababu akutieni mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na walio uliwa katika
njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza a'mali zao.
|
Ayah 47:5 الأية
سَيَهْدِيهِمْ وَيُصْلِحُ بَالَهُمْ
sayahdeehim wayuslihu balahum
Swahili
Atawaongoza na awatengezee hali yao.
|
Ayah 47:6 الأية
وَيُدْخِلُهُمُ الْجَنَّةَ عَرَّفَهَا لَهُمْ
Wayudkhiluhumu aljannata AAarrafahalahum
Swahili
Na atawaingiza katika Pepo aliyo wajuulisha.
|
Ayah 47:7 الأية
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ
أَقْدَامَكُمْ
Ya ayyuha allatheena amanooin tansuroo Allaha yansurkum wayuthabbit aqdamakum
Swahili
Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha
miguu yenu.
|
Ayah 47:8 الأية
وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْسًا لَّهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ
Wallatheena kafaroo fataAAsanlahum waadalla aAAmalahum
Swahili
Na walio kufuru, basi kwao ni maangamizo, na atavipoteza vitendo vyao.
|
Ayah 47:9 الأية
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنزَلَ اللهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ
Thalika bi-annahum karihoo maanzala Allahu faahbata aAAmalahum
Swahili
Hayo ni kwa sababu waliyachukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi
akaviangusha vitendo vyao.
|
Ayah 47:10 الأية
أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ
مِن قَبْلِهِمْ ۚ دَمَّرَ اللهُ عَلَيْهِمْ ۖ وَلِلْكَافِرِينَ أَمْثَالُهَا
Afalam yaseeroo fee al-ardi fayanthurookayfa kana AAaqibatu allatheena min
qablihimdammara Allahu AAalayhim walilkafireena amthaluha
Swahili
Kwani hawakutembea katika ardhi wakaona ulikuwaje mwisho wa walio kuwa kabla
yao? Mwenyezi Mungu aliwaangamiza, na kwa makafiri hawa itakuwa mfano wa hayo.
|
Ayah 47:11 الأية
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللهَ مَوْلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَأَنَّ الْكَافِرِينَ لَا
مَوْلَىٰ لَهُمْ
Thalika bi-anna Allaha mawlaallatheena amanoo waanna alkafireena lamawla lahum
Swahili
Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Na makafiri hawana
mlinzi.
|
Ayah 47:12 الأية
إِنَّ اللهَ يُدْخِلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ
تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا يَتَمَتَّعُونَ
وَيَأْكُلُونَ كَمَا تَأْكُلُ الْأَنْعَامُ وَالنَّارُ مَثْوًى لَّهُمْ
Inna Allaha yudkhilu allatheenaamanoo waAAamiloo assalihati jannatintajree min
tahtiha al-anharu wallatheenakafaroo yatamattaAAoona waya/kuloona kama ta/kulu
al-anAAamuwannaru mathwan lahum
Swahili
Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza walio amini na wakatenda mema katika Bustani
zipitiwazo na mito kati yake. Na walio kufuru hujifurahisha na hula kama walavyo
wanyama, na Moto ndio makaazi yao.
|
Ayah 47:13 الأية
وَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ هِيَ أَشَدُّ قُوَّةً مِّن قَرْيَتِكَ الَّتِي
أَخْرَجَتْكَ أَهْلَكْنَاهُمْ فَلَا نَاصِرَ لَهُمْ
Wakaayyin min qaryatin hiya ashaddu quwwatanmin qaryatika allatee akhrajatka
ahlaknahum fala nasiralahum
Swahili
Na miji mingapi iliyo kuwa na nguvu zaidi kuliko mji wako huu ulio kutoa; nao
tuliwateketeza na wala hawakuwa wa kuwanusuru.
|
Ayah 47:14 الأية
أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّهِ كَمَن زُيِّنَ لَهُ سُوءُ عَمَلِهِ
وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُم
Afaman kana AAala bayyinatinmin rabbihi kaman zuyyina lahu soo-o AAamalihi
wattabaAAooahwaahum
Swahili
Je! Mwenye kuwa na bayana kutoka kwa Mola wake Mlezi ni kama aliye pambiwa uovu
wa vitendo vyake, na wakafuata pumbao lao?
|
Ayah 47:15 الأية
مَّثَلُ الْجَنَّةِ الَّتِي وُعِدَ الْمُتَّقُونَ ۖ فِيهَا أَنْهَارٌ مِّن مَّاءٍ
غَيْرِ آسِنٍ وَأَنْهَارٌ مِّن لَّبَنٍ لَّمْ يَتَغَيَّرْ طَعْمُهُ وَأَنْهَارٌ
مِّنْ خَمْرٍ لَّذَّةٍ لِّلشَّارِبِينَ وَأَنْهَارٌ مِّنْ عَسَلٍ مُّصَفًّى ۖ
وَلَهُمْ فِيهَا مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَمَغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ ۖ كَمَنْ
هُوَ خَالِدٌ فِي النَّارِ وَسُقُوا مَاءً حَمِيمًا فَقَطَّعَ أَمْعَاءَهُمْ
Mathalu aljannati allatee wuAAidaalmuttaqoona feeha anharun min ma-in ghayri
asininwaanharun min labanin lam yataghayyar taAAmuhuwaanharun min khamrin
laththatin lishsharibeenawaanharun min AAasalin musaffan walahum feehamin kulli
aththamarati wamaghfiratun min rabbihimkaman huwa khalidun fee annari wasuqoo
maanhameeman faqattaAAa amAAaahum
Swahili
Mfano wa Pepo walio ahidiwa wachamngu ina mito ya maji yasiyo vunda, na mito ya
maziwa isiyo haribika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na
mito ya asali iliyo safishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda, na
maghfira kutoka kwa Mola wao Mlezi. Basi hao ni kama watakao dumu Motoni na
wakinyweshwa maji yanayo chemka ya kuwakata matumbo yao?
|
Ayah 47:16 الأية
وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ حَتَّىٰ إِذَا خَرَجُوا مِنْ عِندِكَ قَالُوا
لِلَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ مَاذَا قَالَ آنِفًا ۚ أُولَٰئِكَ الَّذِينَ طَبَعَ
اللهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُمْ
Waminhum man yastamiAAu ilayka hattaitha kharajoo min AAindika qaloo
lillatheenaootoo alAAilma matha qala anifan ola-ikaallatheena tabaAAa Allahu
AAalaquloobihim wattabaAAoo ahwaahum
Swahili
Na wapo miongoni mwao wanao kusikiliza, mpaka wakiondoka kwako huwauliza walio
pewa ilimu: Amesema nini sasa hivi? Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amepiga muhuri
juu ya nyoyo zao, na wakafuata pumbao lao.
|
Ayah 47:17 الأية
وَالَّذِينَ اهْتَدَوْا زَادَهُمْ هُدًى وَآتَاهُمْ تَقْوَاهُمْ
Wallatheena ihtadaw zadahumhudan waatahum taqwahum
Swahili
Na wale walio ongoka anawazidishia uongofu na anawapa uchamngu wao.
|
Ayah 47:18 الأية
فَهَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا السَّاعَةَ أَن تَأْتِيَهُم بَغْتَةً ۖ فَقَدْ جَاءَ
أَشْرَاطُهَا ۚ فَأَنَّىٰ لَهُمْ إِذَا جَاءَتْهُمْ ذِكْرَاهُمْ
Fahal yanthuroona illaassaAAata an ta/tiyahum baghtatan faqad jaaashratuha
faanna lahum itha jaat-humthikrahum
Swahili
Kwani wanangojea jengine isipo kuwa iwafikie Saa (ya Kiyama) kwa ghafla? Na
hakika alama zake zimekwisha kuja. Na itapo wajia kutawafaa wapi kukumbuka hapo?
|
Ayah 47:19 الأية
فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا اللهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ
وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ ۗ وَاللهُ يَعْلَمُ مُتَقَلَّبَكُمْ
وَمَثْوَاكُمْ
FaAAlam annahu la ilahailla Allahu wastaghfir lithanbikawalilmu/mineena
walmu/minati wallahuyaAAlamu mutaqallabakum wamathwakum
Swahili
Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi
zako na za Waumini wanaume na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua mahali
penu pa kwenda na kurudi, na mahali penu pa kukaa.
|
Ayah 47:20 الأية
وَيَقُولُ الَّذِينَ آمَنُوا لَوْلَا نُزِّلَتْ سُورَةٌ ۖ فَإِذَا أُنزِلَتْ
سُورَةٌ مُّحْكَمَةٌ وَذُكِرَ فِيهَا الْقِتَالُ ۙ رَأَيْتَ الَّذِينَ فِي
قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يَنظُرُونَ إِلَيْكَ نَظَرَ الْمَغْشِيِّ عَلَيْهِ مِنَ
الْمَوْتِ ۖ فَأَوْلَىٰ لَهُمْ
Wayaqoolu allatheena amanoolawla nuzzilat sooratun fa-itha onzilat sooratun
muhkamatunwathukira feeha alqitalu raayta allatheenafee quloobihim maradun
yanthuroona ilayka natharaalmaghshiyyi AAalayhi mina almawti faawla lahum
Swahili
Na Waumini wanasema: Kwa nini haiteremshwi Sura? Na inapo teremshwa Sura
madhubuti na ikatajwa ndani yake khabari ya vita, utawaona wenye maradhi katika
nyoyo zao wanakutazama mtazamo wa anaye zimia kwa mauti. Basi ni bora kwao
|
Ayah 47:21 الأية
طَاعَةٌ وَقَوْلٌ مَّعْرُوفٌ ۚ فَإِذَا عَزَمَ الْأَمْرُ فَلَوْ صَدَقُوا اللهَ
لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ
TaAAatun waqawlun maAAroofun fa-ithaAAazama al-amru falaw sadaqoo Allaha
lakanakhayran lahum
Swahili
Ut'iifu na kauli njema. Na jambo likisha azimiwa, basi wakiwa ni wakweli kwa
Mwenyezi Mungu, bila ya shaka itakuwa ni kheri kwao.
|
Ayah 47:22 الأية
فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِن تَوَلَّيْتُمْ أَن تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا
أَرْحَامَكُمْ
Fahal AAasaytum in tawallaytum an tufsidoofee al-ardi watuqattiAAoo arhamakum
Swahili
Basi yanayo tarajiwa kwenu mkitawala ndio mfisidi katika nchi na mwatupe jamaa
zenu?
|
Ayah 47:23 الأية
أُولَٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَىٰ أَبْصَارَهُمْ
Ola-ika allatheena laAAanahumuAllahu faasammahum waaAAma absarahum
Swahili
Hao ndio Mwenyezi Mungu alio walaani, na akawatia uziwi, na akawapofoa macho
yao.
|
Ayah 47:24 الأية
أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ أَمْ عَلَىٰ قُلُوبٍ أَقْفَالُهَا
Afala yatadabbaroona alqur-anaam AAala quloobin aqfaluha
Swahili
Je! Hawaizingatii hii Qur'ani? Au kwenye nyoyo (zao) zipo kufuli?
|
Ayah 47:25 الأية
إِنَّ الَّذِينَ ارْتَدُّوا عَلَىٰ أَدْبَارِهِم مِّن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ
الْهُدَى ۙ الشَّيْطَانُ سَوَّلَ لَهُمْ وَأَمْلَىٰ لَهُمْ
Inna allatheena irtaddoo AAalaadbarihim min baAAdi ma tabayyana lahumu
alhudaashshaytanu sawwala lahum waamla lahum
Swahili
Kwa hakika wanao rudi nyuma baada ya kwisha wabainikia uwongofu, Shetani huyo
amewashawishi na amewaghuri.
|
Ayah 47:26 الأية
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لِلَّذِينَ كَرِهُوا مَا نَزَّلَ اللهُ
سَنُطِيعُكُمْ فِي بَعْضِ الْأَمْرِ ۖ وَاللهُ يَعْلَمُ إِسْرَارَهُمْ
Thalika bi-annahum qaloo lillatheenakarihoo ma nazzala Allahu sanuteeAAukum
feebaAAdi al-amri wallahu yaAAlamu israrahum
Swahili
Hayo ni kwa sababu waliwaambia walio chukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu:
Tutakut'iini katika baadhi ya mambo. Na Mwenyezi Mungu anajua siri zao.
|
Ayah 47:27 الأية
فَكَيْفَ إِذَا تَوَفَّتْهُمُ الْمَلَائِكَةُ يَضْرِبُونَ وُجُوهَهُمْ
وَأَدْبَارَهُمْ
Fakayfa itha tawaffat-humu almala-ikatuyadriboona wujoohahum waadbarahum
Swahili
Basi itakuwaje Malaika watakapo wafisha wakawa wanawapiga nyuso zao na migongo
yao!
|
Ayah 47:28 الأية
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ اتَّبَعُوا مَا أَسْخَطَ اللهَ وَكَرِهُوا رِضْوَانَهُ
فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ
Thalika bi-annahumu ittabaAAoo maaskhata Allaha wakarihoo ridwanahufaahbata
aAAmalahum
Swahili
Hayo ni kwa sababu wao waliyafuata yaliyo mchukiza Mwenyezi Mungu na wakachukia
yanayo mridhisha, basi akaviangusha vitendo vyao.
|
Ayah 47:29 الأية
أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ أَن لَّن يُخْرِجَ اللهُ
أَضْغَانَهُمْ
Am hasiba allatheena feequloobihim maradun an lan yukhrija Allahu adghanahum
Swahili
Je! Wenye maradhi nyoyoni mwao wanadhani kwamba Mwenyezi Mungu hatazidhihirisha
chuki zao?
|
Ayah 47:30 الأية
وَلَوْ نَشَاءُ لَأَرَيْنَاكَهُمْ فَلَعَرَفْتَهُم بِسِيمَاهُمْ ۚ
وَلَتَعْرِفَنَّهُمْ فِي لَحْنِ الْقَوْلِ ۚ وَاللهُ يَعْلَمُ أَعْمَالَكُمْ
Walaw nashao laaraynakahumfalaAAaraftahum biseemahum walataAArifannahum fee
lahnialqawli wallahu yaAAlamu aAAmalakum
Swahili
Na tungeli penda tungeli kuonyesha hao na ungeli watambua kwa alama zao; lakini
bila ya shaka utawajua kwa namna ya msemo wao. Na Mwenyezi Mungu anavijua
vitendo vyenu.
|
Ayah 47:31 الأية
وَلَنَبْلُوَنَّكُمْ حَتَّىٰ نَعْلَمَ الْمُجَاهِدِينَ مِنكُمْ وَالصَّابِرِينَ
وَنَبْلُوَ أَخْبَارَكُمْ
Walanabluwannakum hattanaAAlama almujahideena minkum wassabireenawanabluwa
akhbarakum
Swahili
Na bila ya shaka tutakujaribuni mpaka tuwadhihirishe wapiganao Jihadi katika
nyinyi na wanao subiri. Nasi tutazifanyia mtihani khabari zenu.
|
Ayah 47:32 الأية
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللهِ وَشَاقُّوا الرَّسُولَ مِن
بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ الْهُدَىٰ لَن يَضُرُّوا اللهَ شَيْئًا وَسَيُحْبِطُ
أَعْمَالَهُمْ
Inna allatheena kafaroo wasaddooAAan sabeeli Allahi washaqqoo arrasoola
minbaAAdi ma tabayyana lahumu alhuda lan yadurooAllaha shay-an wasayuhbitu
aAAmalahum
Swahili
Kwa hakika walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu na wakapinzana na
Mtume baada ya kwisha wabainikia uwongofu, hao hawatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa
lolote. Naye ataviangusha vitendo vyao.
|
Ayah 47:33 الأية
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَلَا
تُبْطِلُوا أَعْمَالَكُمْ
Ya ayyuha allatheena amanooateeAAoo Allaha waateeAAoo arrasoolawala tubtiloo
aAAmalakum
Swahili
Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume, wala msiviharibu
vitendo vyenu.
|
Ayah 47:34 الأية
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللهِ ثُمَّ مَاتُوا وَهُمْ
كُفَّارٌ فَلَن يَغْفِرَ اللهُ لَهُمْ
Inna allatheena kafaroo wasaddooAAan sabeeli Allahi thumma matoo wahum
kuffarunfalan yaghfira Allahu lahum
Swahili
Hakika walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, kisha wakafa na hali
ni makafiri, Mwenyezi Mungu hatawasamehe makosa yao.
|
Ayah 47:35 الأية
فَلَا تَهِنُوا وَتَدْعُوا إِلَى السَّلْمِ وَأَنتُمُ الْأَعْلَوْنَ وَاللهُ
مَعَكُمْ وَلَن يَتِرَكُمْ أَعْمَالَكُمْ
Fala tahinoo watadAAoo ila assalmiwaantumu al-aAAlawna wallahu maAAakum
walanyatirakum aAAmalakum
Swahili
Basi msiregee na kutaka suluhu, maana nyinyi ndio mtakao shinda. Na Mwenyezi
Mungu yu pamoja nanyi, wala hatakunyimeni malipo ya vitendo vyenu.
|
Ayah 47:36 الأية
إِنَّمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا لَعِبٌ وَلَهْوٌ ۚ وَإِن تُؤْمِنُوا وَتَتَّقُوا
يُؤْتِكُمْ أُجُورَكُمْ وَلَا يَسْأَلْكُمْ أَمْوَالَكُمْ
Innama alhayatu addunyalaAAibun walahwun wa-in tu/minoo watattaqoo yu/tikum
ojoorakumwala yas-alkum amwalakum
Swahili
Hakika uhai wa duniani ni mchezo na pumbao. Na mkiamini na mkamchamngu Mwenyezi
Mungu atakupeni ujira wenu, wala hakutakeni mali yenu.
|
Ayah 47:37 الأية
إِن يَسْأَلْكُمُوهَا فَيُحْفِكُمْ تَبْخَلُوا وَيُخْرِجْ أَضْغَانَكُمْ
In yas-alkumooha fayuhfikumtabkhaloo wayukhrij adghanakum
Swahili
Na akikutakeni hayo na kukushikilieni mtafanya ubakhili, na atatoa undani wa
chuki zenu.
|
Ayah 47:38 الأية
هَا أَنتُمْ هَٰؤُلَاءِ تُدْعَوْنَ لِتُنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللهِ فَمِنكُم مَّن
يَبْخَلُ ۖ وَمَن يَبْخَلْ فَإِنَّمَا يَبْخَلُ عَن نَّفْسِهِ ۚ وَاللهُ
الْغَنِيُّ وَأَنتُمُ الْفُقَرَاءُ ۚ وَإِن تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْمًا
غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوا أَمْثَالَكُم
Ha antum haola-itudAAawna litunfiqoo fee sabeeli Allahi faminkum manyabkhalu
waman yabkhal fa-innama yabkhalu AAan nafsihi wallahualghaniyyu waantumu
alfuqarao wa-in tatawallaw yastabdilqawman ghayrakum thumma la yakoonoo
amthalakum
Swahili
Angalieni! Nyinyi mnaitwa mtumie katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wapo katika
nyinyi wanao fanya ubakhili. Na anaye fanya ubakhili basi anajifanyia ubakhili
mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu si mhitaji, na nyinyi ndio wahitaji. Na mkigeuka
atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|