1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
وَالنَّجْمِ إِذَا هَوَىٰ
Wannajmi itha hawa
Swahili
Naapa kwa nyota inapo tua,
|
Ayah 53:2 الأية
مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَىٰ
Ma dalla sahibukum wamaghawa
Swahili
Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea.
|
Ayah 53:3 الأية
وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ
Wama yantiqu AAani alhawa
Swahili
Wala hatamki kwa matamanio.
|
Ayah 53:4 الأية
إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ
In huwa illa wahyun yooha
Swahili
Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa;
|
Ayah 53:5 الأية
عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَىٰ
AAallamahu shadeedu alquwa
Swahili
Amemfundisha aliye mwingi wa nguvu,
|
Ayah 53:6 الأية
ذُو مِرَّةٍ فَاسْتَوَىٰ
Thoo mirratin fastawa
Swahili
Mwenye kutua, akatulia,
|
Ayah 53:7 الأية
وَهُوَ بِالْأُفُقِ الْأَعْلَىٰ
Wahuwa bil-ofuqi al-aAAla
Swahili
Naye yuko juu kabisa upeo wa macho.
|
Ayah 53:8 الأية
ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ
Thumma dana fatadalla
Swahili
Kisha akakaribia na akateremka.
|
Ayah 53:9 الأية
فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَىٰ
Fakana qaba qawsayni aw adna
Swahili
Akawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi.
|
Ayah 53:10 الأية
فَأَوْحَىٰ إِلَىٰ عَبْدِهِ مَا أَوْحَىٰ
Faawha ila AAabdihi maawha
Swahili
Akamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alicho mfunulia.
|
Ayah 53:11 الأية
مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَىٰ
Ma kathaba alfu-adu maraa
Swahili
Moyo haukusema uwongo uliyo yaona.
|
Ayah 53:12 الأية
أَفَتُمَارُونَهُ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ
Afatumaroonahu AAala mayara
Swahili
Je! Mnabishana naye kwa aliyo yaona?
|
Ayah 53:13 الأية
وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ
Walaqad raahu nazlatan okhra
Swahili
Na akamwona mara nyingine,
|
Ayah 53:14 الأية
عِندَ سِدْرَةِ الْمُنتَهَىٰ
AAinda sidrati almuntaha
Swahili
Penye Mkunazi wa mwisho.
|
Ayah 53:15 الأية
عِندَهَا جَنَّةُ الْمَأْوَىٰ
AAindaha jannatu alma/wa
Swahili
Karibu yake ndiyo ipo Bustani inayo kaliwa.
|
Ayah 53:16 الأية
إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَىٰ
Ith yaghsha assidratama yaghsha
Swahili
Kilipo ufunika huo Mkunazi hicho kilicho ufunuika.
|
Ayah 53:17 الأية
مَا زَاغَ الْبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ
Ma zagha albasaru wamatagha
Swahili
Jicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka.
|
Ayah 53:18 الأية
لَقَدْ رَأَىٰ مِنْ آيَاتِ رَبِّهِ الْكُبْرَىٰ
Laqad raa min ayatirabbihi alkubra
Swahili
Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi.
|
Ayah 53:19 الأية
أَفَرَأَيْتُمُ اللَّاتَ وَالْعُزَّىٰ
Afaraaytumu allata walAAuzza
Swahili
Je! Mmemuona Lata na Uzza?
|
Ayah 53:20 الأية
وَمَنَاةَ الثَّالِثَةَ الْأُخْرَىٰ
Wamanata aththalithataal-okhra
Swahili
Na Manaat, mwingine wa tatu?
|
Ayah 53:21 الأية
أَلَكُمُ الذَّكَرُ وَلَهُ الْأُنثَىٰ
Alakumu aththakaru walahual-ontha
Swahili
Je! Nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndio awe na wanawake?
|
Ayah 53:22 الأية
تِلْكَ إِذًا قِسْمَةٌ ضِيزَىٰ
Tilka ithan qismatun deeza
Swahili
Huo ni mgawanyo wa dhulma!
|
Ayah 53:23 الأية
إِنْ هِيَ إِلَّا أَسْمَاءٌ سَمَّيْتُمُوهَا أَنتُمْ وَآبَاؤُكُم مَّا أَنزَلَ
اللهُ بِهَا مِن سُلْطَانٍ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَمَا تَهْوَى
الْأَنفُسُ ۖ وَلَقَدْ جَاءَهُم مِّن رَّبِّهِمُ الْهُدَىٰ
In hiya illa asmaonsammaytumooha antum waabaokum maanzala Allahu biha min
sultanin inyattabiAAoona illa aththanna wamatahwa al-anfusu walaqad jaahum min
rabbihimu alhuda
Swahili
Hayo hayakuwa ila ni majina mliyo wapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu
hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati ila dhana tu na kipendacho
nafsi. Na kwa yakini uwongofu ulikwisha wafikia kutoka kwa Mola wao Mlezi.
|
Ayah 53:24 الأية
أَمْ لِلْإِنسَانِ مَا تَمَنَّىٰ
Am lil-insani ma tamanna
Swahili
Ati mtu anakipata kila anacho kitamani?
|
Ayah 53:25 الأية
فَلِلَّهِ الْآخِرَةُ وَالْأُولَىٰ
Falillahi al-akhiratu wal-oola
Swahili
Mwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye dunia na Akhera.
|
Ayah 53:26 الأية
وَكَم مِّن مَّلَكٍ فِي السَّمَاوَاتِ لَا تُغْنِي شَفَاعَتُهُمْ شَيْئًا إِلَّا
مِن بَعْدِ أَن يَأْذَنَ اللهُ لِمَن يَشَاءُ وَيَرْضَىٰ
Wakam min malakin fee assamawatila tughnee shafaAAatuhum shay-an illa minbaAAdi
an ya/thana Allahu liman yashao wayarda
Swahili
Na wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipo kuwa
baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia.
|
Ayah 53:27 الأية
إِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ لَيُسَمُّونَ الْمَلَائِكَةَ
تَسْمِيَةَ الْأُنثَىٰ
Inna allatheena la yu/minoonabil-akhirati layusammoona almala-ikatatasmiyata
al-ontha
Swahili
Hakika wasio amini Akhera bila ya shaka wao ndio wanawaita Malaika kwa majina ya
kike.
|
Ayah 53:28 الأية
وَمَا لَهُم بِهِ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ ۖ وَإِنَّ
الظَّنَّ لَا يُغْنِي مِنَ الْحَقِّ شَيْئًا
Wama lahum bihi min AAilmin inyattabiAAoona illa aththanna wa-innaaththanna la
yughnee mina alhaqqishay-a
Swahili
Nao hawana ujuzi wowote kwa hayo isipo kuwa wanafuata dhana tu. Na dhana
haisaidii chochote mbele ya haki.
|
Ayah 53:29 الأية
فَأَعْرِضْ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكْرِنَا وَلَمْ يُرِدْ إِلَّا الْحَيَاةَ
الدُّنْيَا
FaaAArid AAan man tawalla AAanthikrina walam yurid illa alhayataaddunya
Swahili
Basi mwachilie mbali anaye upa kisogo ukumbusho wetu, na wala hataki ila maisha
ya dunia.
|
Ayah 53:30 الأية
ذَٰلِكَ مَبْلَغُهُم مِّنَ الْعِلْمِ ۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ
عَن سَبِيلِهِ وَهُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اهْتَدَىٰ
Thalika mablaghuhum mina alAAilmiinna rabbaka huwa aAAlamu biman dalla AAan
sabeelihiwahuwa aAAlamu bimani ihtada
Swahili
Huo ndio mwisho wao wa ujuzi. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi
mwenye kuipotea njia yake, na Yeye ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuongoka.
|
Ayah 53:31 الأية
وَلِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ لِيَجْزِيَ الَّذِينَ
أَسَاءُوا بِمَا عَمِلُوا وَيَجْزِيَ الَّذِينَ أَحْسَنُوا بِالْحُسْنَى
Walillahi ma fee assamawatiwama fee al-ardi liyajziya allatheena asaoobima
AAamiloo wayajziya allatheena ahsanoobilhusna
Swahili
Ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, ili
awalipe walio tenda ubaya kwa waliyo yatenda, na walio tenda mema awalipe mema.
|
Ayah 53:32 الأية
الَّذِينَ يَجْتَنِبُونَ كَبَائِرَ الْإِثْمِ وَالْفَوَاحِشَ إِلَّا اللَّمَمَ ۚ
إِنَّ رَبَّكَ وَاسِعُ الْمَغْفِرَةِ ۚ هُوَ أَعْلَمُ بِكُمْ إِذْ أَنشَأَكُم مِّنَ
الْأَرْضِ وَإِذْ أَنتُمْ أَجِنَّةٌ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ ۖ فَلَا تُزَكُّوا
أَنفُسَكُمْ ۖ هُوَ أَعْلَمُ بِمَنِ اتَّقَىٰ
Allatheena yajtaniboona kaba-iraal-ithmi walfawahisha illa allamama innarabbaka
wasiAAu almaghfirati huwa aAAlamu bikum ithanshaakum mina al-ardi wa-ith antum
ajinnatun feebutooni ommahatikum fala tuzakkoo anfusakumhuwa aAAlamu bimani
ittaqa
Swahili
Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipo kuwa makosa
khafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana
tangu alipo kuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama
zenu. Basi msijisifu usafi. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga na maovu.
|
Ayah 53:33 الأية
أَفَرَأَيْتَ الَّذِي تَوَلَّىٰ
Afaraayta allathee tawalla
Swahili
Je! Umemwona yule aliye geuka?
|
Ayah 53:34 الأية
وَأَعْطَىٰ قَلِيلًا وَأَكْدَىٰ
WaaAAta qaleelan waakda
Swahili
Na akatoa kidogo, kisha akajizuia?
|
Ayah 53:35 الأية
أَعِندَهُ عِلْمُ الْغَيْبِ فَهُوَ يَرَىٰ
aAAindahu AAilmu alghaybi fahuwa yara
Swahili
Je! Anayo huyo ilimu ya ghaibu, basi ndio anaona?
|
Ayah 53:36 الأية
أَمْ لَمْ يُنَبَّأْ بِمَا فِي صُحُفِ مُوسَىٰ
Am lam yunabba/ bima fee suhufimoosa
Swahili
Au hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa?
|
Ayah 53:37 الأية
وَإِبْرَاهِيمَ الَّذِي وَفَّىٰ
Wa-ibraheema allathee waffa
Swahili
Na vya Ibrahimu aliye timiza ahadi?
|
Ayah 53:38 الأية
أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ
Alla taziru waziratun wizraokhra
Swahili
Ya kwamba hakika nafsi iliyo beba madhambi haibebi madhambi ya mwengine?
|
Ayah 53:39 الأية
وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ
Waan laysa lil-insani illa masaAAa
Swahili
Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe?
|
Ayah 53:40 الأية
وَأَنَّ سَعْيَهُ سَوْفَ يُرَىٰ
Waanna saAAyahu sawfa yura
Swahili
Na kwamba vitendo vyake vitaonekana?
|
Ayah 53:41 الأية
ثُمَّ يُجْزَاهُ الْجَزَاءَ الْأَوْفَىٰ
Thumma yujzahu aljazaa al-awfa
Swahili
Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu.
|
Ayah 53:42 الأية
وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الْمُنتَهَىٰ
Waanna ila rabbika almuntaha
Swahili
Na kwamba kwao Mola wako Mlezi ndio mwisho.
|
Ayah 53:43 الأية
وَأَنَّهُ هُوَ أَضْحَكَ وَأَبْكَىٰ
Waannahu huwa adhaka waabka
Swahili
Na kwamba Yeye ndiye anaye leta kicheko na kilio.
|
Ayah 53:44 الأية
وَأَنَّهُ هُوَ أَمَاتَ وَأَحْيَا
Waannahu huwa amata waahya
Swahili
Na kwamba Yeye ndiye anaye fisha na kuhuisha.
|
Ayah 53:45 الأية
وَأَنَّهُ خَلَقَ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ
Waannahu khalaqa azzawjayni aththakarawal-ontha
Swahili
Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike
|
Ayah 53:46 الأية
مِن نُّطْفَةٍ إِذَا تُمْنَىٰ
Min nutfatin itha tumna
Swahili
Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa.
|
Ayah 53:47 الأية
وَأَنَّ عَلَيْهِ النَّشْأَةَ الْأُخْرَىٰ
Waanna AAalayhi annash-ata al-okhra
Swahili
Na kwamba ni juu yake ufufuo mwengine.
|
Ayah 53:48 الأية
وَأَنَّهُ هُوَ أَغْنَىٰ وَأَقْنَىٰ
Waannahu huwa aghna waaqna
Swahili
Na kwamba ni Yeye ndiye anaye tosheleza na kukinaisha.
|
Ayah 53:49 الأية
وَأَنَّهُ هُوَ رَبُّ الشِّعْرَىٰ
Waannahu huwa rabbu ashshiAAra
Swahili
Na kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya Shii'ra.
|
Ayah 53:50 الأية
وَأَنَّهُ أَهْلَكَ عَادًا الْأُولَىٰ
Waannahu ahlaka AAadan al-oola
Swahili
Na kwamba Yeye ndiye aliye waangamiza A'di wa kwanza,
|
Ayah 53:51 الأية
وَثَمُودَ فَمَا أَبْقَىٰ
Wathamooda fama abqa
Swahili
Na Thamudi hakuwabakisha,
|
Ayah 53:52 الأية
وَقَوْمَ نُوحٍ مِّن قَبْلُ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا هُمْ أَظْلَمَ وَأَطْغَىٰ
Waqawma noohin min qablu innahum kanoohum athlama waatgha
Swahili
Na kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhaalimu zaidi, na waovu
zaidi;
|
Ayah 53:53 الأية
وَالْمُؤْتَفِكَةَ أَهْوَىٰ
Walmu/tafikata ahwa
Swahili
Na miji iliyo pinduliwa, ni Yeye aliye ipindua.
|
Ayah 53:54 الأية
فَغَشَّاهَا مَا غَشَّىٰ
Faghashshaha ma ghashsha
Swahili
Vikaifunika vilivyo funika.
|
Ayah 53:55 الأية
فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكَ تَتَمَارَىٰ
Fabi-ayyi ala-i rabbika tatamara
Swahili
Basi neema gani ya Mola wako Mlezi unayo ifanyia shaka?
|
Ayah 53:56 الأية
هَٰذَا نَذِيرٌ مِّنَ النُّذُرِ الْأُولَىٰ
Hatha natheerun mina annuthurial-oola
Swahili
Hili ni Onyo katika maonyo yale yale ya zamani.
|
Ayah 53:57 الأية
أَزِفَتِ الْآزِفَةُ
Azifati al-azifat
Swahili
Kiyama kimekaribia!
|
Ayah 53:58 الأية
لَيْسَ لَهَا مِن دُونِ اللهِ كَاشِفَةٌ
Laysa laha min dooni Allahi kashifat
Swahili
Hapana wa kukifichua isipo kuwa Mwenyezi Mungu.
|
Ayah 53:59 الأية
أَفَمِنْ هَٰذَا الْحَدِيثِ تَعْجَبُونَ
Afamin hatha alhadeethitaAAjaboon
Swahili
Je! Mnayastaajabia maneno haya?
|
Ayah 53:60 الأية
وَتَضْحَكُونَ وَلَا تَبْكُونَ
Watadhakoona wala tabkoon
Swahili
Na mnacheka, wala hamlii?
|
Ayah 53:61 الأية
وَأَنتُمْ سَامِدُونَ
Waantum samidoon
Swahili
Nanyi mmeghafilika?
|
Ayah 53:62 الأية
فَاسْجُدُوا لِلَّهِ وَاعْبُدُوا ۩
Fasjudoo lillahi waAAbudoo
Swahili
Basi msujudieni Mwenyezi Mungu, na mumuabudu.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|