First Ayah 1 الأية الأوليبِسْم ِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَجَعَلَ الظُّلُمَاتِ
وَالنُّورَ ۖ ثُمَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ
Alhamdu lillahi allatheekhalaqa assamawati wal-ardawajaAAala aththulumati
wannoorathumma allatheena kafaroo birabbihim yaAAdiloon
Swahili
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliye umba mbingu na ardhi, na akafanya
giza na mwangaza. Tena baada ya haya walio kufuru wanawafanya wengine sawa na
Mola wao Mlezi.
|
Ayah 6:2 الأية
هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن طِينٍ ثُمَّ قَضَىٰ أَجَلًا ۖ وَأَجَلٌ مُّسَمًّى
عِندَهُ ۖ ثُمَّ أَنتُمْ تَمْتَرُونَ
Huwa allathee khalaqakum min teeninthumma qada ajalan waajalun musamman AAindahu
thumma antumtamtaroon
Swahili
Yeye ndiye aliye kuumbeni kwa udongo, kisha akakuhukumieni ajali, na muda
maalumu uko kwake tu. Tena baada ya haya nyinyi mnatia shaka.
|
Ayah 6:3 الأية
وَهُوَ اللَّهُ فِي السَّمَاوَاتِ وَفِي الْأَرْضِ ۖ يَعْلَمُ سِرَّكُمْ
وَجَهْرَكُمْ وَيَعْلَمُ مَا تَكْسِبُونَ
Wahuwa Allahu fee assamawatiwafee al-ardi yaAAlamu sirrakum wajahrakum
wayaAAlamu mataksiboon
Swahili
Na Yeye ndiye Mwenyezi Mungu mbinguni na ardhini. Anajua ya ndani yenu na ya nje
yenu. Na anajua mnayo yachuma.
|
Ayah 6:4 الأية
وَمَا تَأْتِيهِم مِّنْ آيَةٍ مِّنْ آيَاتِ رَبِّهِمْ إِلَّا كَانُوا عَنْهَا
مُعْرِضِينَ
Wama ta/teehim min ayatin min ayatirabbihim illa kanoo AAanha muAArideen
Swahili
Na haiwafikii hata ishara moja katika ishara za Mola wao Mlezi ila wao huwa
wenye kuipa nyongo.
|
Ayah 6:5 الأية
فَقَدْ كَذَّبُوا بِالْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ ۖ فَسَوْفَ يَأْتِيهِمْ أَنبَاءُ مَا
كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ
Faqad kaththaboo bilhaqqilamma jaahum fasawfa ya/teehim anbao makanoo bihi
yastahzi-oon
Swahili
Wameikanusha Haki ilipo wajia. Basi zitawajia khabari za yale waliyo kuwa
wakiyakejeli.
|
Ayah 6:6 الأية
أَلَمْ يَرَوْا كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّن قَرْنٍ مَّكَّنَّاهُمْ فِي
الْأَرْضِ مَا لَمْ نُمَكِّن لَّكُمْ وَأَرْسَلْنَا السَّمَاءَ عَلَيْهِم
مِّدْرَارًا وَجَعَلْنَا الْأَنْهَارَ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمْ فَأَهْلَكْنَاهُم
بِذُنُوبِهِمْ وَأَنشَأْنَا مِن بَعْدِهِمْ قَرْنًا آخَرِينَ
Alam yaraw kam ahlakna min qablihimmin qarnin makkannahum fee al-ardi ma
lamnumakkin lakum waarsalna assamaa AAalayhimmidraran wajaAAalna al-anhara
tajree min tahtihimfaahlaknahum bithunoobihim waansha/na minbaAAdihim qarnan
akhareen
Swahili
Jee, hawaoni vizazi vingapi tulivyo viangamiza kabla yao? Tuliwaweka katika nchi
tusivyo kuwekeni nyinyi; tukawapelekea mvua nyingi na tukaifanya mito inapita
chini yao. Mwishoe tukawaangamiza kwa madhambi yao; na tukaanzisha baada yao
kizazi kingine.
|
Ayah 6:7 الأية
وَلَوْ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ كِتَابًا فِي قِرْطَاسٍ فَلَمَسُوهُ بِأَيْدِيهِمْ
لَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ
Walaw nazzalna AAalayka kitabanfee qirtasin falamasoohu bi-aydeehim laqala
allatheenakafaroo in hatha illa sihrun mubeen
Swahili
Na lau tungeli kuteremshia kitabu cha karatasi, wakakigusa kwa mikono yao,
wangeli sema walio kufuru: Haya si chochote ila ni uchawi dhaahiri.
|
Ayah 6:8 الأية
وَقَالُوا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ مَلَكٌ ۖ وَلَوْ أَنزَلْنَا مَلَكًا لَّقُضِيَ
الْأَمْرُ ثُمَّ لَا يُنظَرُونَ
Waqaloo lawla onzila AAalayhimalakun walaw anzalna malakan laqudiya
al-amruthumma la yuntharoon
Swahili
Na wao husema: Mbona hakuteremshiwa Malaika? Na kama tungeli teremsha Malaika,
basi bila ya shaka ingesha hukumiwa amri, tena hapo wasingeli pewa muhula.
|
Ayah 6:9 الأية
وَلَوْ جَعَلْنَاهُ مَلَكًا لَّجَعَلْنَاهُ رَجُلًا وَلَلَبَسْنَا عَلَيْهِم مَّا
يَلْبِسُونَ
Walaw jaAAalnahu malakan lajaAAalnahurajulan walalabasna AAalayhim ma yalbisoon
Swahili
Na kama tungeli mfanya Malaika bila ya shaka tungeli mfanya kama binaadamu, na
tungeli watilia matatizo yale wanayo yatatiza wao.
|
Ayah 6:10 الأية
وَلَقَدِ اسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِّن قَبْلِكَ فَحَاقَ بِالَّذِينَ سَخِرُوا مِنْهُم
مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ
Walaqadi istuhzi-a birusulin min qablika fahaqabillatheena sakhiroo minhum ma
kanoobihi yastahzi-oon
Swahili
Na hakika Mitume walio kabla yako walifanyiwa kejeli, lakini walio wafanyia
kejeli wakaja kuzungukwa na yale yale waliyo kuwa wao wanayafanyia kejeli.
|
Ayah 6:11 الأية
قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ ثُمَّ انظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكَذِّبِينَ
Qul seeroo fee al-ardi thumma onthurookayfa kana AAaqibatu almukaththibeen
Swahili
Sema: Tembeeni ulimwenguni, kisha mtazame ulikuwaje mwisho wa wanao kanusha.
|
Ayah 6:12 الأية
قُل لِّمَن مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ قُل لِّلَّهِ ۚ كَتَبَ عَلَىٰ
نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۚ لَيَجْمَعَنَّكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ
فِيهِ ۚ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ
Qul liman ma fee assamawatiwal-ardi qul lillahi kataba AAalanafsihi arrahmata
layajmaAAannakum ilayawmi alqiyamati la rayba feehi allatheenakhasiroo anfusahum
fahum la yu/minoon
Swahili
Sema: Ni vya nani viliomo katika mbingu na katika ardhi? Sema: Ni vya Mwenyezi
Mungu. Yeye amejilazimisha nafsi yake kurehemu. Hakika atakukusanyeni Siku ya
Kiyama isiyo kuwa na shaka. Walio jikhasiri wenyewe hawaamini.
|
Ayah 6:13 الأية
وَلَهُ مَا سَكَنَ فِي اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ ۚ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ
Walahu ma sakana fee allayli wannahariwahuwa assameeAAu alAAaleem
Swahili
Na ni vyake vilio tulia usiku na mchana. Naye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye
kujua.
|
Ayah 6:14 الأية
قُلْ أَغَيْرَ اللَّهِ أَتَّخِذُ وَلِيًّا فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ
وَهُوَ يُطْعِمُ وَلَا يُطْعَمُ ۗ قُلْ إِنِّي أُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ أَوَّلَ مَنْ
أَسْلَمَ ۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ
Qul aghayra Allahi attakhithuwaliyyan fatiri assamawati wal-ardiwahuwa yutAAimu
wala yutAAamu qul inneeomirtu an akoona awwala man aslama wala takoonanna
minaalmushrikeen
Swahili
Sema: Je, nimchukue rafiki mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba
mbingu na ardhi, naye ndiye anaye lisha wala halishwi? Sema: Mimi nimeamrishwa
niwe wa kwanza wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina.
|
Ayah 6:15 الأية
قُلْ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ
Qul innee akhafu in AAasayturabbee AAathaba yawmin AAatheem
Swahili
Sema: Mimi naogopa adhabu ya Siku kubwa hiyo ikiwa nitamuasi Mola wangu Mlezi.
|
Ayah 6:16 الأية
مَّن يُصْرَفْ عَنْهُ يَوْمَئِذٍ فَقَدْ رَحِمَهُ ۚ وَذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْمُبِينُ
Man yusraf AAanhu yawma-ithinfaqad rahimahu wathalika alfawzu almubeen
Swahili
Siku hiyo yule atakaye epushwa nayo adhabu hiyo atakuwa Mwenyezi Mungu
amemrehemu. Na huko ndiko kufuzu kulio wazi.
|
Ayah 6:17 الأية
وَإِن يَمْسَسْكَ اللَّهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن
يَمْسَسْكَ بِخَيْرٍ فَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ
Wa-in yamsaska Allahu bidurrinfala kashifa lahu illa huwa wa-in
yamsaskabikhayrin fahuwa AAala kulli shay-in qadeer
Swahili
Na ikiwa Mwenyezi Mungu akikugusisha madhara, basi hapana wa kukuondolea hayo
ila Yeye. Na ikiwa akikugusisha kheri, basi Yeye ndiye Mwenye uweza wa kila
kitu.
|
Ayah 6:18 الأية
وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ
Wahuwa alqahiru fawqa AAibadihiwahuwa alhakeemu alkhabeer
Swahili
Naye ndiye Mwenye nguvu juu ya waja wake, na ndiye Mwenye hikima na Mwenye
khabari zote.
|
Ayah 6:19 الأية
قُلْ أَيُّ شَيْءٍ أَكْبَرُ شَهَادَةً ۖ قُلِ اللَّهُ ۖ شَهِيدٌ بَيْنِي
وَبَيْنَكُمْ ۚ وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن
بَلَغَ ۚ أَئِنَّكُمْ لَتَشْهَدُونَ أَنَّ مَعَ اللَّهِ آلِهَةً أُخْرَىٰ ۚ قُل
لَّا أَشْهَدُ ۚ قُلْ إِنَّمَا هُوَ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ وَإِنَّنِي بَرِيءٌ مِّمَّا
تُشْرِكُونَ
Qul ayyu shay-in akbaru shahadatanquli Allahu shaheedun baynee wabaynakum
waoohiyailayya hatha alqur-anu li-onthirakum bihiwaman balagha a-innakum
latashhadoona anna maAAa Allahi alihatanokhra qul la ashhadu qul innama huwa
ilahunwahidun wa-innanee baree-on mimma tushrikoon
Swahili
Sema: Kitu gani ushahidi wake mkubwa kabisa? Sema: Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye
shahidi baina yangu na nyinyi. Na nimefunuliwa Qur'ani hii ili kwayo nikuonyeni
nyinyi na kila inayo mfikia. Ati kweli nyinyi mnashuhudia kuwa pamoja na
Mwenyezi Mungu wapo miungu wengine? Sema: Mimi sishuhudii hayo. Sema: Hakika
Yeye ni Mungu mmoja tu, nami ni mbali na mnao washirikisha.
|
Ayah 6:20 الأية
الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْرِفُونَهُ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَاءَهُمُ
ۘ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ
Allatheena ataynahumualkitaba yaAArifoonahu kama yaAArifoona abnaahumallatheena
khasiroo anfusahum fahum la yu/minoon
Swahili
Wale Tulio wapa Kitabu wanayajua haya kama wanavyo wajua watoto wao. Wale walio
zikhasiri nafsi zao hawaamini.
|
Ayah 6:21 الأية
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ
ۗ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ
Waman athlamu mimmani iftaraAAala Allahi kathiban aw kaththababi-ayatihi innahu
la yuflihu aththalimoon
Swahili
Na nani dhaalimu zaidi kuliko anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, na
akazikanusha Ishara zake? Hakika madhaalimu hawafanikiwi.
|
Ayah 6:22 الأية
وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا أَيْنَ
شُرَكَاؤُكُمُ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ
Wayawma nahshuruhum jameeAAan thummanaqoolu lillatheena ashrakoo ayna
shurakaokumu allatheenakuntum tazAAumoon
Swahili
Siku tutapo wakusanya wote pamoja, kisha tuwaambie walio shirikisha: Wako wapi
washirikishwa wenu mlio kuwa mnadai?
|
Ayah 6:23 الأية
ثُمَّ لَمْ تَكُن فِتْنَتُهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا وَاللَّهِ رَبِّنَا مَا كُنَّا
مُشْرِكِينَ
Thumma lam takun fitnatuhum illa an qaloowallahi rabbina ma kunnamushrikeen
Swahili
Kisha hautakuwa udhuru wao ila ni kusema: Wallahi! Mola wetu Mlezi! Hatukuwa
washirikina.
|
Ayah 6:24 الأية
انظُرْ كَيْفَ كَذَبُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ ۚ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا
يَفْتَرُونَ
Onthur kayfa kathabooAAala anfusihim wadalla AAanhum ma kanooyaftaroon
Swahili
Tazama jinsi wanavyo jisemea uwongo wenyewe. Na yamewapotea waliyo kuwa
wakiyazua.
|
Ayah 6:25 الأية
وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ ۖ وَجَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً
أَن يَفْقَهُوهُ وَفِي آذَانِهِمْ وَقْرًا ۚ وَإِن يَرَوْا كُلَّ آيَةٍ لَّا
يُؤْمِنُوا بِهَا ۚ حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوكَ يُجَادِلُونَكَ يَقُولُ الَّذِينَ
كَفَرُوا إِنْ هَٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ
Waminhum man yastamiAAu ilayka wajaAAalnaAAala quloobihim akinnatan an
yafqahoohu wafee athanihimwaqran wa-in yaraw kulla ayatin la yu/minoo bihahatta
itha jaooka yujadiloonakayaqoolu allatheena kafaroo in hatha illa
asateerual-awwaleen
Swahili
Na wapo miongoni mwao wanao kusikiliza; na tumezitia pazia nyoyo zao wasije
kuyafahamu. Na upo uziwi masikioni mwao, na wakiona kila Ishara hawaiamini. Hata
wakikujia kwa kujadiliana nawe, wanasema walio kufuru: Hizi si chochote ila
hadithi za watu wa kale.
|
Ayah 6:26 الأية
وَهُمْ يَنْهَوْنَ عَنْهُ وَيَنْأَوْنَ عَنْهُ ۖ وَإِن يُهْلِكُونَ إِلَّا
أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ
Wahum yanhawna AAanhu wayan-awna AAanhuwa-in yuhlikoona illa anfusahum wama
yashAAuroon
Swahili
Nao huwazuia watu, na wao wenyewe wanajitenga nayo. Nao hawaangamizi ila nafsi
zao tu, wala wao hawatambui.
|
Ayah 6:27 الأية
وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ وُقِفُوا عَلَى النَّارِ فَقَالُوا يَا لَيْتَنَا نُرَدُّ وَلَا
نُكَذِّبَ بِآيَاتِ رَبِّنَا وَنَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ
Walaw tara ith wuqifoo AAalaannari faqaloo ya laytananuraddu wala nukaththiba
bi-ayatirabbina wanakoona mina almu/mineen
Swahili
Na unge ona watakapo simamishwa kwenye Moto, wakawa wanasema: Laiti tungeli
rudishwa, wala hatutakanusha tena Ishara za Mola wetu Mlezi, na tutakuwa
miongoni wa Waumini.
|
Ayah 6:28 الأية
بَلْ بَدَا لَهُم مَّا كَانُوا يُخْفُونَ مِن قَبْلُ ۖ وَلَوْ رُدُّوا لَعَادُوا
لِمَا نُهُوا عَنْهُ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ
Bal bada lahum ma kanooyukhfoona min qablu walaw ruddoo laAAadoo limanuhoo
AAanhu wa-innahum lakathiboon
Swahili
Bali yamewadhihirikia waliyo kuwa wakiyaficha zamani. Na kama wangeli rudishwa
bila ya shaka wange yarejea yale yale waliyo katazwa. Na hakika hao ni waongo.
|
Ayah 6:29 الأية
وَقَالُوا إِنْ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ
Waqaloo in hiya illa hayatunaaddunya wama nahnu bimabAAootheen
Swahili
Na walisema: Hakuna mengine ila maisha yetu haya ya duniani, wala sisi
hatutafufuliwa.
|
Ayah 6:30 الأية
وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ وُقِفُوا عَلَىٰ رَبِّهِمْ ۚ قَالَ أَلَيْسَ هَٰذَا بِالْحَقِّ
ۚ قَالُوا بَلَىٰ وَرَبِّنَا ۚ قَالَ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ
تَكْفُرُونَ
Walaw tara ith wuqifoo AAalarabbihim qala alaysa hatha bilhaqqiqaloo bala
warabbina qala fathooqooalAAathaba bima kuntum takfuroon
Swahili
Na lau ungeli ona watavyo simamishwa mbele ya Mola wao Mlezi, akawaambia: Je, si
kweli haya? Na wao watasema: Kwani? Tunaapa kwa Mola Mlezi wetu ni kweli. Yeye
atasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya vile mlivyo kuwa mnakataa.
|
Ayah 6:31 الأية
قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِلِقَاءِ اللَّهِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَاءَتْهُمُ
السَّاعَةُ بَغْتَةً قَالُوا يَا حَسْرَتَنَا عَلَىٰ مَا فَرَّطْنَا فِيهَا وَهُمْ
يَحْمِلُونَ أَوْزَارَهُمْ عَلَىٰ ظُهُورِهِمْ ۚ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ
Qad khasira allatheena kaththaboobiliqa-i Allahi hatta itha jaat-humuassaAAatu
baghtatan qaloo ya hasratanaAAala ma farratna feeha wahumyahmiloona awzarahum
AAala thuhoorihimala saa ma yaziroon
Swahili
Hakika wamekhasirika walio kanusha kukutana na Mwenyezi Mungu, mpaka ilipo wajia
Saa kwa ghafla, wakasema: Ole wetu kwa tuliyo yapuuza! Nao watabeba mizigo yao
juu ya migongo yao. Ni maovu hayo wanayo yabeba.
|
Ayah 6:32 الأية
وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَعِبٌ وَلَهْوٌ ۖ وَلَلدَّارُ الْآخِرَةُ
خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ
Wama alhayatu addunyailla laAAibun walahwun waladdaru al-akhiratikhayrun
lillatheena yattaqoona afala taAAqiloon
Swahili
Na maisha ya dunia si chochte ila ni mchezo na pumbao tu. Na hakika nyumba ya
Akhera ni bora zaidi kwa wanao mcha Mungu. Basi, je, hamtii akilini?
|
Ayah 6:33 الأية
قَدْ نَعْلَمُ إِنَّهُ لَيَحْزُنُكَ الَّذِي يَقُولُونَ ۖ فَإِنَّهُمْ لَا
يُكَذِّبُونَكَ وَلَٰكِنَّ الظَّالِمِينَ بِآيَاتِ اللَّهِ يَجْحَدُونَ
Qad naAAlamu innahu layahzunuka allatheeyaqooloona fa-innahum la
yukaththiboonaka walakinnaaththalimeena bi-ayatiAllahi yajhadoon
Swahili
Tunajua ya kwamba yanakuhuzunisha wanayo yasema. Basi hakika wao hawakukanushi
wewe, lakini hao madhaalimu wanazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu.
|
Ayah 6:34 الأية
وَلَقَدْ كُذِّبَتْ رُسُلٌ مِّن قَبْلِكَ فَصَبَرُوا عَلَىٰ مَا كُذِّبُوا
وَأُوذُوا حَتَّىٰ أَتَاهُمْ نَصْرُنَا ۚ وَلَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِ اللَّهِ ۚ
وَلَقَدْ جَاءَكَ مِن نَّبَإِ الْمُرْسَلِينَ
Walaqad kuththibat rusulun minqablika fasabaroo AAala ma kuththiboowaoothoo
hatta atahum nasrunawala mubaddila likalimati Allahi walaqad jaakamin naba-i
almursaleen
Swahili
Na hakika walikanushwa Mitume wa kabla yako. Nao wakavumilia kule kukanushwa, na
kuudhiwa, mpaka ilipo wafikia nusura yetu. Na hapana wa kubadilisha maneno ya
Mwenyezi Mungu. Na bila ya shaka zimekujia baadhi ya khabari za Mitume hao.
|
Ayah 6:35 الأية
وَإِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكَ إِعْرَاضُهُمْ فَإِنِ اسْتَطَعْتَ أَن تَبْتَغِيَ
نَفَقًا فِي الْأَرْضِ أَوْ سُلَّمًا فِي السَّمَاءِ فَتَأْتِيَهُم بِآيَةٍ ۚ
وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ لَجَمَعَهُمْ عَلَى الْهُدَىٰ ۚ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ
الْجَاهِلِينَ
Wa-in kana kabura AAalayka iAAraduhumfa-ini istataAAta an tabtaghiya nafaqan fee
al-ardiaw sullaman fee assama-i fata/tiyahum bi-ayatinwalaw shaa Allahu
lajamaAAahum AAala alhudafala takoonanna mina aljahileen
Swahili
Na ikiwa ni makubwa kwako huku kukataa kwao, basi kama unaweza kutafuta njia ya
chini kwa chini ya ardhi, au ngazi kwendea mbinguni ili uwaletee Ishara -- Na
lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa angeli wakusanya kwenye uwongofu. Basi usiwe
miongoni mwa wasio jua.
|
Ayah 6:36 الأية
إِنَّمَا يَسْتَجِيبُ الَّذِينَ يَسْمَعُونَ ۘ وَالْمَوْتَىٰ يَبْعَثُهُمُ اللَّهُ
ثُمَّ إِلَيْهِ يُرْجَعُونَ
Innama yastajeebu allatheenayasmaAAoona walmawta yabAAathuhumu Allahuthumma
ilayhi yurjaAAoon
Swahili
Hakika wanao kubali ni wale wanao sikia. Na ama wafu Mwenyezi Mungu atawafufua,
na kisha kwake Yeye ndio watarejeshwa.
|
Ayah 6:37 الأية
وَقَالُوا لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِّن رَّبِّهِ ۚ قُلْ إِنَّ اللَّهَ
قَادِرٌ عَلَىٰ أَن يُنَزِّلَ آيَةً وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
Waqaloo lawla nuzzila AAalayhiayatun min rabbihi qul inna Allaha qadirunAAala an
yunazzila ayatan walakinnaaktharahum la yaAAlamoon
Swahili
Na wamesema: Kwa nini hakuteremshiwa muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema:
Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuteremsha muujiza. Lakini wengi wao hawajui.
|
Ayah 6:38 الأية
وَمَا مِن دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا طَائِرٍ يَطِيرُ بِجَنَاحَيْهِ إِلَّا
أُمَمٌ أَمْثَالُكُم ۚ مَّا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِن شَيْءٍ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ
رَبِّهِمْ يُحْشَرُونَ
Wama min dabbatin fee al-ardiwala ta-irin yateeru bijanahayhi illaomamun
amthalukum ma farratna feealkitabi min shay-in thumma ila rabbihim yuhsharoon
Swahili
Na hapana mnyama katika ardhi, wala ndege anaye ruka kwa mbawa zake mbili, ila
ni umma kama nyinyi. Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote. Kisha kwa Mola wao
Mlezi watakusanywa.
|
Ayah 6:39 الأية
وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا صُمٌّ وَبُكْمٌ فِي الظُّلُمَاتِ ۗ مَن يَشَإِ
اللَّهُ يُضْلِلْهُ وَمَن يَشَأْ يَجْعَلْهُ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ
Wallatheena kaththaboobi-ayatina summun wabukmun fee aththulumatiman yasha-i
Allahu yudlilhu waman yasha/ yajAAalhuAAala siratin mustaqeem
Swahili
Na walio kanusha Ishara zetu ni viziwi na mabubu waliomo gizani. Mwenyezi Mungu
humwachia kupotea amtakaye, na humweka katika Njia iliyo nyooka amtakaye.
|
Ayah 6:40 الأية
قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّهِ أَوْ أَتَتْكُمُ السَّاعَةُ
أَغَيْرَ اللَّهِ تَدْعُونَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ
Qul araaytakum in atakum AAathabuAllahi aw atatkumu assaAAatu aghayra
AllahitadAAoona in kuntum sadiqeen
Swahili
Sema: Mwaonaje ikikujieni adhabu ya Mwenyezi Mungu, au ikakufikieni hiyo Saa -
mtamwomba asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni wakweli?
|
Ayah 6:41 الأية
بَلْ إِيَّاهُ تَدْعُونَ فَيَكْشِفُ مَا تَدْعُونَ إِلَيْهِ إِن شَاءَ وَتَنسَوْنَ
مَا تُشْرِكُونَ
Bal iyyahu tadAAoona fayakshifu matadAAoona ilayhi in shaa watansawna ma
tushrikoon
Swahili
Bali Yeye ndiye mtakaye mwomba, naye atakuondoleeni mnacho mwombea akipenda. Na
mtasahau hao mnao wafanya washirika wake.
|
Ayah 6:42 الأية
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ أُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَأَخَذْنَاهُم بِالْبَأْسَاءِ
وَالضَّرَّاءِ لَعَلَّهُمْ يَتَضَرَّعُونَ
Walaqad arsalna ila omamin minqablika faakhathnahum bilba/sa-i
waddarra-ilaAAallahum yatadarraAAoon
Swahili
Na kwa yakini tulipeleka Mitume kwa kaumu zilizo kuwa kabla yako, kisha
tukazitia katika dhiki na mashaka ili zipate kunyenyekea.
|
Ayah 6:43 الأية
فَلَوْلَا إِذْ جَاءَهُم بَأْسُنَا تَضَرَّعُوا وَلَٰكِن قَسَتْ قُلُوبُهُمْ
وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Falawla ith jaahumba/suna tadarraAAoo walakin qasat quloobuhumwazayyana lahumu
ashshaytanu ma kanooyaAAmaloon
Swahili
Kwa nini wasinyenyekee ilipo wafika adhabu yetu? Lakini nyoyo zao zilikuwa
ngumu, na Shet'ani akawapambia waliyo kuwa wakiyafanya.
|
Ayah 6:44 الأية
فَلَمَّا نَسُوا مَا ذُكِّرُوا بِهِ فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ أَبْوَابَ كُلِّ شَيْءٍ
حَتَّىٰ إِذَا فَرِحُوا بِمَا أُوتُوا أَخَذْنَاهُم بَغْتَةً فَإِذَا هُم
مُّبْلِسُونَ
Falamma nasoo ma thukkiroobihi fatahna AAalayhim abwaba kulli shay-in hattaitha
farihoo bima ootoo akhathnahumbaghtatan fa-itha hum mublisoon
Swahili
Basi walipo sahau walio kumbushwa tuliwafungulia milango ya kila kitu. Mpaka
walipo furahia yale waliyo pewa tuliwashika kwa ghafla, na mara wakawa wenye
kukata tamaa.
|
Ayah 6:45 الأية
فَقُطِعَ دَابِرُ الْقَوْمِ الَّذِينَ ظَلَمُوا ۚ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ
الْعَالَمِينَ
FaqutiAAa dabiru alqawmi allatheenathalamoo walhamdu lillahirabbi alAAalameen
Swahili
Ikakatwa mizizi ya watu walio dhulumu - na wa kuhimidiwa ni Mwenyezi Mungu, Mola
Mlezi wa viumbe vyote.
|
Ayah 6:46 الأية
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَخَذَ اللَّهُ سَمْعَكُمْ وَأَبْصَارَكُمْ وَخَتَمَ عَلَىٰ
قُلُوبِكُم مَّنْ إِلَٰهٌ غَيْرُ اللَّهِ يَأْتِيكُم بِهِ ۗ انظُرْ كَيْفَ
نُصَرِّفُ الْآيَاتِ ثُمَّ هُمْ يَصْدِفُونَ
Qul araaytum in akhatha AllahusamAAakum waabsarakum wakhatama AAala
quloobikumman ilahun ghayru Allahi ya/teekum bihi onthurkayfa nusarrifu al-ayati
thumma hum yasdifoon
Swahili
Sema: Mwaonaje Mwenyezi Mungu akanyakua kusikia kwenu, na kuona kwenu, na
akaziziba nyoyo zenu, ni mungu gani asiye kuwa Mwenyezi Mungu ataye kuleteeni
hayo tena? Angalia vipi tunavyo zieleza Ishara, kisha wao wanapuuza.
|
Ayah 6:47 الأية
قُلْ أَرَأَيْتَكُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُ اللَّهِ بَغْتَةً أَوْ جَهْرَةً هَلْ
يُهْلَكُ إِلَّا الْقَوْمُ الظَّالِمُونَ
Qul araaytakum in atakum AAathabuAllahi baghtatan aw jahratan hal yuhlaku
illaalqawmu aththalimoon
Swahili
Sema: Mwaonaje, ikikufikieni adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa ghafla, au kwa
dhaahiri, jee wataangamizwa isipo kuwa walio dhulumu?
|
Ayah 6:48 الأية
وَمَا نُرْسِلُ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ ۖ فَمَنْ آمَنَ
وَأَصْلَحَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ
Wama nursilu almursaleena illamubashshireena wamunthireena faman amana
waaslahafala khawfun AAalayhim wala hum yahzanoon
Swahili
Na hatuwatumi Mitume ila huwa ni wabashiri na waonyaji. Na wenye kuamini na
wakatenda mema haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika.
|
Ayah 6:49 الأية
وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا يَمَسُّهُمُ الْعَذَابُ بِمَا كَانُوا
يَفْسُقُونَ
Wallatheena kaththaboobi-ayatina yamassuhumu alAAathabu bimakanoo yafsuqoon
Swahili
Na walio kanusha Ishara zetu itawagusa adhabu kwa walivyo kuwa wakipotoka.
|
Ayah 6:50 الأية
قُل لَّا أَقُولُ لَكُمْ عِندِي خَزَائِنُ اللَّهِ وَلَا أَعْلَمُ الْغَيْبَ وَلَا
أَقُولُ لَكُمْ إِنِّي مَلَكٌ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ ۚ قُلْ
هَلْ يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ ۚ أَفَلَا تَتَفَكَّرُونَ
Qul la aqoolu lakum AAindee khaza-inuAllahi wala aAAlamu alghayba wala
aqoolulakum innee malakun in attabiAAu illa ma yoohailayya qul hal yastawee
al-aAAma walbaseeruafala tatafakkaroon
Swahili
Sema: Mimi sikwambiini kuwa ninazo khazina za Mwenyezi Mungu. Wala sijui mambo
yaliyo fichikana. Wala sikwambiini kuwa mimi ni Malaika. Mimi sifuati ila yanayo
funuliwa kwangu. Sema: Je, wanakuwa sawa, kipofu na mwenye kuona. Basi
hamfikiri?
|
Ayah 6:51 الأية
وَأَنذِرْ بِهِ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحْشَرُوا إِلَىٰ رَبِّهِمْ ۙ لَيْسَ
لَهُم مِّن دُونِهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ
Waanthir bihi allatheena yakhafoonaan yuhsharoo ila rabbihim laysa lahum min
doonihiwaliyyun wala shafeeAAun laAAallahum yattaqoon
Swahili
Na waonye kwayo wanao ogopa kuwa watakusanywa kwa Mola wao Mlezi, hali kuwa
hawana mlinzi wala mwombezi isipo kuwa Yeye, ili wapate kuchamngu.
|
Ayah 6:52 الأية
وَلَا تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ
وَجْهَهُ ۖ مَا عَلَيْكَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَمَا مِنْ حِسَابِكَ
عَلَيْهِم مِّن شَيْءٍ فَتَطْرُدَهُمْ فَتَكُونَ مِنَ الظَّالِمِينَ
Wala tatrudi allatheenayadAAoona rabbahum bilghadati walAAashiyyiyureedoona
wajhahu ma AAalayka min hisabihimmin shay-in wama min hisabika AAalayhim
minshay-in fatatrudahum fatakoona mina aththalimeen
Swahili
Wala usiwafukuze wanao mwomba Mola Mlezi wao asubuhi na jioni kwa kutaka radhi
yake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, wala hisabu yako si juu yao hata
kidogo, hata uwafukuze na uwe miongoni mwa wenye kudhulumu.
|
Ayah 6:53 الأية
وَكَذَٰلِكَ فَتَنَّا بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لِّيَقُولُوا أَهَٰؤُلَاءِ مَنَّ اللَّهُ
عَلَيْهِم مِّن بَيْنِنَا ۗ أَلَيْسَ اللَّهُ بِأَعْلَمَ بِالشَّاكِرِينَ
Wakathalika fatanna baAAdahumbibaAAdin liyaqooloo ahaola-i manna AllahuAAalayhim
min baynina alaysa Allahu bi-aAAlama bishshakireen
Swahili
Na hivi ndivyo tunavyo wajaribu wao kwa wao, ili waseme: Ni hao ndio Mwenyezi
Mungu amewafadhilisha miongoni mwetu? Kwani Mwenyezi Mungu hawajui wanao
shukuru?
|
Ayah 6:54 الأية
وَإِذَا جَاءَكَ الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِنَا فَقُلْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ ۖ
كَتَبَ رَبُّكُمْ عَلَىٰ نَفْسِهِ الرَّحْمَةَ ۖ أَنَّهُ مَنْ عَمِلَ مِنكُمْ
سُوءًا بِجَهَالَةٍ ثُمَّ تَابَ مِن بَعْدِهِ وَأَصْلَحَ فَأَنَّهُ غَفُورٌ
رَّحِيمٌ
Wa-itha jaaka allatheenayu/minoona bi-ayatina faqul salamunAAalaykum kataba
rabbukum AAala nafsihi arrahmataannahu man AAamila minkum soo-an bijahalatin
thumma tabamin baAAdihi waaslaha faannahu ghafoorun raheem
Swahili
Na wanapo kujia wanao ziamini Ishara zetu waambie: Assalamu alaikum! Amani iwe
juu yenu! Mola wenu Mlezi amejilazimisha rehema, ya kwamba atakaye fanya uovu
miongoni mwenu kwa ujinga, kisha akatubu baada yake na akatengenea, basi hakika
Yeye ni Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu.
|
Ayah 6:55 الأية
وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ وَلِتَسْتَبِينَ سَبِيلُ الْمُجْرِمِينَ
Wakathalika nufassilu al-ayatiwalitastabeena sabeelu almujrimeen
Swahili
Na ndio hivi tunavyo zieleza Ishara ili ibainike njia ya wakosefu.
|
Ayah 6:56 الأية
قُلْ إِنِّي نُهِيتُ أَنْ أَعْبُدَ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّهِ ۚ قُل
لَّا أَتَّبِعُ أَهْوَاءَكُمْ ۙ قَدْ ضَلَلْتُ إِذًا وَمَا أَنَا مِنَ
الْمُهْتَدِينَ
Qul innee nuheetu an aAAbuda allatheenatadAAoona min dooni Allahi qul la
attabiAAu ahwaakumqad dalaltu ithan wama ana minaalmuhtadeen
Swahili
Sema: Mimi nimekatazwa kuwaabudu hao mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu. Sema:
mimi sifuati matamanio yenu. Hivyo nitakuwa nimepotea, na sitakuwa miongoni mwa
walio ongoka.
|
Ayah 6:57 الأية
قُلْ إِنِّي عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَكَذَّبْتُم بِهِ ۚ مَا عِندِي مَا
تَسْتَعْجِلُونَ بِهِ ۚ إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ ۖ يَقُصُّ الْحَقَّ ۖ وَهُوَ
خَيْرُ الْفَاصِلِينَ
Qul innee AAala bayyinatin min rabbeewakaththabtum bihi ma AAindee
matastaAAjiloona bihi ini alhukmu illa lillahiyaqussu alhaqqa wahuwa khayru
alfasileen
Swahili
Sema: Mimi nipo kwenye sharia iliyo wazi itokayo kwa Mola wangu Mlezi, nanyi
mnaikanusha. Mimi sinacho hicho mnacho kihimiza. Hapana hukumu ila ya Mwenyezi
Mungu. Yeye anasimulia yaliyo kweli; naye ni Mbora wa kuhukumu kuliko wote.
|
Ayah 6:58 الأية
قُل لَّوْ أَنَّ عِندِي مَا تَسْتَعْجِلُونَ بِهِ لَقُضِيَ الْأَمْرُ بَيْنِي
وَبَيْنَكُمْ ۗ وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِالظَّالِمِينَ
Qul law anna AAindee matastaAAjiloona bihi laqudiya al-amru baynee wabaynakum
wallahuaAAlamu biththalimeen
Swahili
Sema: Lau kuwa ninacho hicho mnacho kihimiza, ingeli kwisha katwa shauri baina
yangu na nyinyi. Na Mwenyezi Mungu anawashinda wote kuwajua madhaalimu.
|
Ayah 6:59 الأية
وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ وَيَعْلَمُ مَا فِي
الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۚ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا
حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ
مُّبِينٍ
WaAAindahu mafatihu alghaybi layaAAlamuha illa huwa wayaAAlamu ma feealbarri
walbahri wama tasqutu minwaraqatin illa yaAAlamuha wala habbatinfee thulumati
al-ardi wala ratbinwala yabisin illa fee kitabin mubeen
Swahili
Na ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua
kilioko nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje
katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinacho
bainisha.
|
Ayah 6:60 الأية
وَهُوَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُم بِاللَّيْلِ وَيَعْلَمُ مَا جَرَحْتُم بِالنَّهَارِ
ثُمَّ يَبْعَثُكُمْ فِيهِ لِيُقْضَىٰ أَجَلٌ مُّسَمًّى ۖ ثُمَّ إِلَيْهِ
مَرْجِعُكُمْ ثُمَّ يُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Wahuwa allathee yatawaffakumbillayli wayaAAlamu ma jarahtum binnaharithumma
yabAAathukum feehi liyuqda ajalun musamman thummailayhi marjiAAukum thumma
yunabbi-okum bima kuntumtaAAmaloon
Swahili
Naye ndiye anaye kufisheni usiku, na anakijua mlicho fanya mchana. Kisha Yeye
hukufufueni humo mchana ili muda ulio wekwa utimizwe. Kisha kwake Yeye ndiyo
marejeo yenu, na tena akwambieni mliyo kuwa mkiyafanya.
|
Ayah 6:61 الأية
وَهُوَ الْقَاهِرُ فَوْقَ عِبَادِهِ ۖ وَيُرْسِلُ عَلَيْكُمْ حَفَظَةً حَتَّىٰ
إِذَا جَاءَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ تَوَفَّتْهُ رُسُلُنَا وَهُمْ لَا يُفَرِّطُونَ
Wahuwa alqahiru fawqa AAibadihiwayursilu AAalaykum hafathatan hattaitha jaa
ahadakumu almawtu tawaffat-hurusuluna wahum la yufarritoon
Swahili
Naye ndiye Mwenye nguvu za kushinda, aliye juu ya waja wake. Na hukupelekeeni
waangalizi, mpaka mmoja wenu yakimjia mauti wajumbe wetu humfisha, nao hawafanyi
taksiri.
|
Ayah 6:62 الأية
ثُمَّ رُدُّوا إِلَى اللَّهِ مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ ۚ أَلَا لَهُ الْحُكْمُ وَهُوَ
أَسْرَعُ الْحَاسِبِينَ
Thumma ruddoo ila Allahi mawlahumualhaqqi ala lahu alhukmu wahuwa asraAAu
alhasibeen
Swahili
Kisha watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wao wa Haki. Hakika, hukumu ni yake.
Naye ni Mwepesi kuliko wote wanao hisabu.
|
Ayah 6:63 الأية
قُلْ مَن يُنَجِّيكُم مِّن ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ تَدْعُونَهُ تَضَرُّعًا
وَخُفْيَةً لَّئِنْ أَنجَانَا مِنْ هَٰذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ
Qul man yunajjeekum min thulumatialbarri walbahri tadAAoonahu
tadarruAAanwakhufyatan la-in anjana min hathihilanakoonanna mina ashshakireen
Swahili
Sema: Ni nani anaye kuokoeni katika giza la nchi kavu na baharini? Mnamwomba kwa
unyenyekevu na kwa siri, mkisema: Kama akituokoa na haya bila ya shaka tutakuwa
miongoni mwa wanao shukuru.
|
Ayah 6:64 الأية
قُلِ اللَّهُ يُنَجِّيكُم مِّنْهَا وَمِن كُلِّ كَرْبٍ ثُمَّ أَنتُمْ تُشْرِكُونَ
Quli Allahu yunajjeekum minhawamin kulli karbin thumma antum tushrikoon
Swahili
Sema: Mwenyezi Mungu hukuokoeni kutoka hayo, na kutoka kila mashaka, na kisha
nyinyi mnamshirikisha!
|
Ayah 6:65 الأية
قُلْ هُوَ الْقَادِرُ عَلَىٰ أَن يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عَذَابًا مِّن فَوْقِكُمْ
أَوْ مِن تَحْتِ أَرْجُلِكُمْ أَوْ يَلْبِسَكُمْ شِيَعًا وَيُذِيقَ بَعْضَكُم
بَأْسَ بَعْضٍ ۗ انظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ لَعَلَّهُمْ يَفْقَهُونَ
Qul huwa alqadiru AAala anyabAAatha AAalaykum AAathaban min fawqikum aw min
tahtiarjulikum aw yalbisakum shiyaAAan wayutheeqa baAAdakumba/sa baAAdin onthur
kayfa nusarrifual-ayati laAAallahum yafqahoon
Swahili
Sema: Yeye ndiye Muweza wa kukuleteeni adhabu kutoka juu yenu au kutoka chini ya
miguu yenu, au kukuleteeni fujo la mfarakano, na kuwaonjesha baadhi yenu jeuri
ya wenzao. Tazama vipi tunavyo zieleza Aya ili wapate kufahamu.
|
Ayah 6:66 الأية
وَكَذَّبَ بِهِ قَوْمُكَ وَهُوَ الْحَقُّ ۚ قُل لَّسْتُ عَلَيْكُم بِوَكِيلٍ
Wakaththaba bihi qawmuka wahuwa alhaqququl lastu AAalaykum biwakeel
Swahili
Na watu wako wameikanusha, nayo ni Haki. Sema: Mimi sikuwakilishwa juu yenu.
|
Ayah 6:67 الأية
لِّكُلِّ نَبَإٍ مُّسْتَقَرٌّ ۚ وَسَوْفَ تَعْلَمُونَ
Likulli naba-in mustaqarrun wasawfataAAlamoon
Swahili
Kila khabari ina kipindi chake. Nanyi mtakuja jua.
|
Ayah 6:68 الأية
وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ
يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا
تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ
Wa-itha raayta allatheenayakhoodoona fee ayatina faaAAridAAanhum hatta yakhoodoo
fee hadeethinghayrihi wa-imma yunsiyannaka ashshaytanufala taqAAud baAAda
aththikra maAAaalqawmi aththalimeen
Swahili
Na unapo waona wanao ziingilia Aya zetu, basi jitenge nao mpaka waingilie
mazungumzo mengine. Na kama Shet'ani akikusahaulisha, basi baada ya kutanabahi
usikae pamoja na watu madhaalimu.
|
Ayah 6:69 الأية
وَمَا عَلَى الَّذِينَ يَتَّقُونَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَلَٰكِن ذِكْرَىٰ
لَعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ
Wama AAala allatheenayattaqoona min hisabihim min shay-in walakinthikra
laAAallahum yattaqoon
Swahili
Wala wamchao Mungu hawana jukumu lolote kwao, lakini ni kukumbusha, asaa wapate
kujiepusha.
|
Ayah 6:70 الأية
وَذَرِ الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَهُمْ لَعِبًا وَلَهْوًا وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ
الدُّنْيَا ۚ وَذَكِّرْ بِهِ أَن تُبْسَلَ نَفْسٌ بِمَا كَسَبَتْ لَيْسَ لَهَا مِن
دُونِ اللَّهِ وَلِيٌّ وَلَا شَفِيعٌ وَإِن تَعْدِلْ كُلَّ عَدْلٍ لَّا يُؤْخَذْ
مِنْهَا ۗ أُولَٰئِكَ الَّذِينَ أُبْسِلُوا بِمَا كَسَبُوا ۖ لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ
حَمِيمٍ وَعَذَابٌ أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ
Wathari allatheena ittakhathoodeenahum laAAiban walahwan wagharrat-humu
alhayatuaddunya wathakkir bihi an tubsala nafsunbima kasabat laysa laha min
dooni Allahiwaliyyun wala shafeeAAun wa-in taAAdil kulla AAadlin layu/khath
minha ola-ika allatheenaobsiloo bima kasaboo lahum sharabun min
hameeminwaAAathabun aleemun bima kanoo yakfuroon
Swahili
Waachilie mbali walio ifanya dini yao ni mchezo na pumbao, na uhai wa dunia
ukawaghuri. Nawe kumbusha kwayo, isije nafsi ikaangamizwa kwa sababu ya iliyo
yachuma, nayo haina mlinzi wala mwombezi ila Mwenyezi Mungu. Na ingatoa kila
fidia haitokubaliwa. Hao ndio walio angamizwa kwa sababu ya yale waliyo yachuma.
Wao watapata kinywaji cha maji ya moto kabisa, na adhabu chungu.
|
Ayah 6:71 الأية
قُلْ أَنَدْعُو مِن دُونِ اللَّهِ مَا لَا يَنفَعُنَا وَلَا يَضُرُّنَا وَنُرَدُّ
عَلَىٰ أَعْقَابِنَا بَعْدَ إِذْ هَدَانَا اللَّهُ كَالَّذِي اسْتَهْوَتْهُ
الشَّيَاطِينُ فِي الْأَرْضِ حَيْرَانَ لَهُ أَصْحَابٌ يَدْعُونَهُ إِلَى الْهُدَى
ائْتِنَا ۗ قُلْ إِنَّ هُدَى اللَّهِ هُوَ الْهُدَىٰ ۖ وَأُمِرْنَا لِنُسْلِمَ
لِرَبِّ الْعَالَمِينَ
Qul anadAAoo min dooni Allahi mala yanfaAAuna wala yadurrunawanuraddu AAala
aAAqabina baAAda ithhadana Allahu kallathee istahwat-huashshayateenu fee al-ardi
hayranalahu as-habun yadAAoonahu ila alhudai/tina qul inna huda Allahi huwa
alhudawaomirna linuslima lirabbi alAAalameen
Swahili
Sema: Je, tumuombe asiye kuwa Mwenyezi Mungu ambae hatufai wala hatudhuru, na
turejee nyuma baada ya Mwenyezi Mungu kwisha tuhidi? Tuwe kama ambao mashet'ani
wamempumbaza katika ardhi, amebabaika? Anao marafiki wanao mwita ende kwenye
uwongofu, wakimwambia: Njoo kwetu! Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio
Uwongofu. Nasi tumeamrishwa tusilimu kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote,
|
Ayah 6:72 الأية
وَأَنْ أَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَاتَّقُوهُ ۚ وَهُوَ الَّذِي إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ
Waan aqeemoo assalatawattaqoohu wahuwa allathee ilayhi tuhsharoon
Swahili
Na mshike Sala, na mcheni Yeye, na kwake Yeye ndiko mtako kusanywa.
|
Ayah 6:73 الأية
وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۖ وَيَوْمَ يَقُولُ
كُن فَيَكُونُ ۚ قَوْلُهُ الْحَقُّ ۚ وَلَهُ الْمُلْكُ يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ
ۚ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْخَبِيرُ
Wahuwa allathee khalaqa assamawatiwal-arda bilhaqqi wayawma yaqoolukun fayakoonu
qawluhu alhaqqu walahu almulku yawmayunfakhu fee assoori AAalimu alghaybi
washshahadatiwahuwa alhakeemu alkhabeer
Swahili
Naye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi kwa Haki. Na anaposema: Kuwa! Basi huwa.
Kauli yake ni Haki. Na ufalme wote ni wake Siku litapo pulizwa barugumu, Mjuzi
wa yaliyo fichikana na yanayo onekana. Naye ndiye Mwenye hikima na Mwenye
khabari.
|
Ayah 6:74 الأية
وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ آزَرَ أَتَتَّخِذُ أَصْنَامًا آلِهَةً ۖ
إِنِّي أَرَاكَ وَقَوْمَكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ
Wa-ith qala ibraheemuli-abeehi azara atattakhithu asnaman alihataninnee araka
waqawmaka fee dalalin mubeen
Swahili
Na pale Ibrahim alipo mwambia baba yake, Azar: Unayafanya masanamu kuwa ni
miungu? Hakika mimi nakuona wewe na watu wako mmo katika opotofu ulio wazi.
|
Ayah 6:75 الأية
وَكَذَٰلِكَ نُرِي إِبْرَاهِيمَ مَلَكُوتَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلِيَكُونَ
مِنَ الْمُوقِنِينَ
Wakathalika nuree ibraheemamalakoota assamawati wal-ardiwaliyakoona mina
almooqineen
Swahili
Na kadhaalika tulimwonyesha Ibrahim ufalme wa mbingu na ardhi, na ili awe
miongoni mwa wenye yakini.
|
Ayah 6:76 الأية
فَلَمَّا جَنَّ عَلَيْهِ اللَّيْلُ رَأَىٰ كَوْكَبًا ۖ قَالَ هَٰذَا رَبِّي ۖ
فَلَمَّا أَفَلَ قَالَ لَا أُحِبُّ الْآفِلِينَ
Falamma janna AAalayhi allaylu raakawkaban qala hatha rabbee falamma afala
qalala ohibbu al-afileen
Swahili
Na ulipo muingilia usiku akiona nyota, akasema: Huyu ni Mola Mlezi wangu. Ilipo
tua akasema: Siwapendi wanao tua.
|
Ayah 6:77 الأية
فَلَمَّا رَأَى الْقَمَرَ بَازِغًا قَالَ هَٰذَا رَبِّي ۖ فَلَمَّا أَفَلَ قَالَ
لَئِن لَّمْ يَهْدِنِي رَبِّي لَأَكُونَنَّ مِنَ الْقَوْمِ الضَّالِّينَ
Falamma raa alqamara bazighanqala hatha rabbee falamma afala qalala-in lam
yahdinee rabbee laakoonanna mina alqawmi addalleen
Swahili
Alipo uona mwezi unachomoza alisema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu. Ulipotua
akasema: Kama Mola Mlezi wangu hakuniongoa, nitakuwa katika kaumu walio potea.
|
Ayah 6:78 الأية
فَلَمَّا رَأَى الشَّمْسَ بَازِغَةً قَالَ هَٰذَا رَبِّي هَٰذَا أَكْبَرُ ۖ
فَلَمَّا أَفَلَتْ قَالَ يَا قَوْمِ إِنِّي بَرِيءٌ مِّمَّا تُشْرِكُونَ
Falamma raa ashshamsabazighatan qala hatha rabbee hathaakbaru falamma afalat
qala ya qawmi inneebaree-on mimma tushrikoon
Swahili
Na alipo liona jua linachomoza akasema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu. Huyu mkubwa
kuliko wote. Lilipo tua, alisema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika hayo mnayo
fanyia ushirikina.
|
Ayah 6:79 الأية
إِنِّي وَجَّهْتُ وَجْهِيَ لِلَّذِي فَطَرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ حَنِيفًا ۖ
وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ
Innee wajjahtu wajhiya lillathee fataraassamawati wal-arda haneefanwama ana mina
almushrikeen
Swahili
Hakika mimi nimeuelekeza uso wangu sawa sawa kwa aliye ziumba mbingu na ardhi,
wala mimi si miongoni mwa washirikina.
|
Ayah 6:80 الأية
وَحَاجَّهُ قَوْمُهُ ۚ قَالَ أَتُحَاجُّونِّي فِي اللَّهِ وَقَدْ هَدَانِ ۚ وَلَا
أَخَافُ مَا تُشْرِكُونَ بِهِ إِلَّا أَن يَشَاءَ رَبِّي شَيْئًا ۗ وَسِعَ رَبِّي
كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا ۗ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ
Wahajjahu qawmuhu qala atuhajjoonneefee Allahi waqad hadani wala akhafu
matushrikoona bihi illa an yashaa rabbee shay-anwasiAAa rabbee kulla shay-in
AAilman afala tatathakkaroon
Swahili
Na watu wake wakamhoji. Akasema: Je, mnanihoji juu ya Mwenyezi Mungu, na hali
Yeye ameniongoa? Wala siogopi hao mnao washirikisha naye, ila Mola wangu Mlezi
akipenda kitu. Mola wangu Mlezi amekusanya ilimu ya kila kitu. Basi je,
hamkumbuki?
|
Ayah 6:81 الأية
وَكَيْفَ أَخَافُ مَا أَشْرَكْتُمْ وَلَا تَخَافُونَ أَنَّكُمْ أَشْرَكْتُم
بِاللَّهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ عَلَيْكُمْ سُلْطَانًا ۚ فَأَيُّ الْفَرِيقَيْنِ
أَحَقُّ بِالْأَمْنِ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ
Wakayfa akhafu ma ashraktumwala takhafoona annakum ashraktum billahima lam
yunazzil bihi AAalaykum sultanan faayyualfareeqayni ahaqqu bil-amni in kuntum
taAAlamoon
Swahili
Na vipi nivikhofu hivyo mnavyo vishirikisha, hali nyinyi hamkhofu kuwa nyinyi
mmemshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu ambacho hakukiteremshia uthibitisho. Basi
kundi gani katika mawili haya lina haki zaidi kupata amani, kama nyinyi mnajua?
|
Ayah 6:82 الأية
الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَٰئِكَ لَهُمُ
الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ
Allatheena amanoo walamyalbisoo eemanahum bithulmin ola-ikalahumu al-amnu wahum
muhtadoon
Swahili
Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma - hao ndio watakao
pata amani na wao ndio walio ongoka.
|
Ayah 6:83 الأية
وَتِلْكَ حُجَّتُنَا آتَيْنَاهَا إِبْرَاهِيمَ عَلَىٰ قَوْمِهِ ۚ نَرْفَعُ
دَرَجَاتٍ مَّن نَّشَاءُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ
Watilka hujjatuna ataynahaibraheema AAala qawmihi narfaAAu darajatinman nashao
inna rabbaka hakeemun AAaleem
Swahili
Na hizo ndizo hoja zetu tulizo mpa Ibrahim kuhojiana na watu wake. Tunamnyanyua
kwa vyeo tumtakaye. Hakika Mola Mlezi wako ni Mwenye hikima na Mwenye ujuzi.
|
Ayah 6:84 الأية
وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ ۚ كُلًّا هَدَيْنَا ۚ وَنُوحًا هَدَيْنَا
مِن قَبْلُ ۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِ دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ
وَمُوسَىٰ وَهَارُونَ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ
Wawahabna lahu ishaqawayaAAqooba kullan hadayna wanoohan hadaynamin qablu wamin
thurriyyatihi dawooda wasulaymanawaayyooba wayoosufa wamoosa waharoona
wakathalikanajzee almuhsineen
Swahili
Na tukamtunukia (Ibrahim) Is-haq na Yaakub. Kila mmoja wao tulimwongoa. Na Nuhu
tulimwongoa kabla. Na katika kizazi chake tulimwongoa Daud na Suleiman na Ayyub
na Yusuf na Musa na Harun. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wafanyao wema.
|
Ayah 6:85 الأية
وَزَكَرِيَّا وَيَحْيَىٰ وَعِيسَىٰ وَإِلْيَاسَ ۖ كُلٌّ مِّنَ الصَّالِحِينَ
Wazakariyya wayahyawaAAeesa walyasa kullun mina assaliheen
Swahili
Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyas. Wote walikuwa miongoni mwa watu wema.
|
Ayah 6:86 الأية
وَإِسْمَاعِيلَ وَالْيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطًا ۚ وَكُلًّا فَضَّلْنَا عَلَى
الْعَالَمِينَ
Wa-ismaAAeela walyasaAAawayoonusa walootan wakullan faddalna AAalaalAAalameen
Swahili
Na Ismail, na Al Yasaa, na Yunus, na Lut'. Na wote tuliwafadhilisha juu ya
walimwengu wote.
|
Ayah 6:87 الأية
وَمِنْ آبَائِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ وَإِخْوَانِهِمْ ۖ وَاجْتَبَيْنَاهُمْ
وَهَدَيْنَاهُمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ
Wamin aba-ihim wathurriyyatihimwa-ikhwanihim wajtabaynahum wahadaynahumila
siratin mustaqeem
Swahili
Na kutokana na baba zao, na vizazi vyao na ndugu zao. Na tukawateuwa na
tukawaongoa kwenye Njia iliyo nyooka.
|
Ayah 6:88 الأية
ذَٰلِكَ هُدَى اللَّهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚ وَلَوْ
أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Thalika huda Allahiyahdee bihi man yashao min AAibadihi walaw ashrakoolahabita
AAanhum ma kanoo yaAAmaloon
Swahili
Hiyo ni hidaya ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo humhidi amtakaye katika waja wake. Na
lau wangeli mshirikisha yangeli waharibikia waliyo kuwa wakiyatenda.
|
Ayah 6:89 الأية
أُولَٰئِكَ الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ۚ فَإِن
يَكْفُرْ بِهَا هَٰؤُلَاءِ فَقَدْ وَكَّلْنَا بِهَا قَوْمًا لَّيْسُوا بِهَا
بِكَافِرِينَ
Ola-ika allatheena ataynahumualkitaba walhukma wannubuwwatafa-in yakfur biha
haola-i faqad wakkalnabiha qawman laysoo biha bikafireen
Swahili
Hao ndio tulio wapa Vitabu na hukumu na Unabii. Ikiwa hawa watayakataa hayo,
basi tumekwisha yawakilisha kwa watu wasio yakataa.
|
Ayah 6:90 الأية
أُولَٰئِكَ الَّذِينَ هَدَى اللَّهُ ۖ فَبِهُدَاهُمُ اقْتَدِهْ ۗ قُل لَّا
أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا ۖ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْعَالَمِينَ
Ola-ika allatheena hadaAllahu fabihudahumu iqtadih qul la as-alukumAAalayhi
ajran in huwa illa thikra lilAAalameen
Swahili
Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewahidi. Basi fuata hidaya yao. Sema: Mimi
sikuombeni ujira. Haya hayakuwa ila ni mawaidha kwa walimwengu wote.
|
Ayah 6:91 الأية
وَمَا قَدَرُوا اللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِ إِذْ قَالُوا مَا أَنزَلَ اللَّهُ عَلَىٰ
بَشَرٍ مِّن شَيْءٍ ۗ قُلْ مَنْ أَنزَلَ الْكِتَابَ الَّذِي جَاءَ بِهِ مُوسَىٰ
نُورًا وَهُدًى لِّلنَّاسِ ۖ تَجْعَلُونَهُ قَرَاطِيسَ تُبْدُونَهَا وَتُخْفُونَ
كَثِيرًا ۖ وَعُلِّمْتُم مَّا لَمْ تَعْلَمُوا أَنتُمْ وَلَا آبَاؤُكُمْ ۖ قُلِ
اللَّهُ ۖ ثُمَّ ذَرْهُمْ فِي خَوْضِهِمْ يَلْعَبُونَ
Wama qadaroo Allaha haqqaqadrihi ith qaloo ma anzala AllahuAAala basharin min
shay-in qul man anzala alkitabaallathee jaa bihi moosa nooran wahudan
linnasitajAAaloonahu qarateesa tubdoonaha watukhfoonakatheeran waAAullimtum ma
lam taAAlamoo antum wala abaokumquli Allahu thumma tharhum fee
khawdihimyalAAaboon
Swahili
Na hawakumkadiria Mwenyezi Mungu kwa haki ya kadri yake, walipo sema: Mwenyezi
Mungu hakumteremshia mwanaadamu chochote. Sema: Nani aliyo teremsha Kitabu
alicho kuja nacho Musa, chenye nuru na uwongofu kwa watu, mlicho kifanya kurasa
kurasa mkizionyesha, na mengi mkiyaficha. Na mkafunzwa mlio kuwa hamyajui nyinyi
wala baba zenu? Sema: Mwenyezi Mungu. Kisha waache wacheze katika porojo lao.
|
Ayah 6:92 الأية
وَهَٰذَا كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ مُبَارَكٌ مُّصَدِّقُ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ
وَلِتُنذِرَ أُمَّ الْقُرَىٰ وَمَنْ حَوْلَهَا ۚ وَالَّذِينَ يُؤْمِنُونَ
بِالْآخِرَةِ يُؤْمِنُونَ بِهِ ۖ وَهُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ
Wahatha kitabun anzalnahumubarakun musaddiqu allathee bayna yadayhiwalitunthira
omma alqura waman hawlahawallatheena yu/minoona bil-akhiratiyu/minoona bihi
wahum AAala salatihim yuhafithoon
Swahili
Na hiki ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa, chenye kuhakikisha
yaliyo tangulia, na ili uuwonye Mama wa Miji na walio pembezoni mwake. Na wenye
kuamini Akhera wanakiamini hichi, nao wanazihifadhi Sala zao.
|
Ayah 6:93 الأية
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّهِ كَذِبًا أَوْ قَالَ أُوحِيَ
إِلَيَّ وَلَمْ يُوحَ إِلَيْهِ شَيْءٌ وَمَن قَالَ سَأُنزِلُ مِثْلَ مَا أَنزَلَ
اللَّهُ ۗ وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الظَّالِمُونَ فِي غَمَرَاتِ الْمَوْتِ
وَالْمَلَائِكَةُ بَاسِطُو أَيْدِيهِمْ أَخْرِجُوا أَنفُسَكُمُ ۖ الْيَوْمَ
تُجْزَوْنَ عَذَابَ الْهُونِ بِمَا كُنتُمْ تَقُولُونَ عَلَى اللَّهِ غَيْرَ
الْحَقِّ وَكُنتُمْ عَنْ آيَاتِهِ تَسْتَكْبِرُونَ
Waman athlamu mimmani iftaraAAala Allahi kathiban aw qala oohiyailayya walam
yooha ilayhi shay-on waman qalasaonzilu mithla ma anzala Allahu walaw taraithi
aththalimoona fee ghamaratialmawti walmala-ikatu basitooaydeehim akhrijoo
anfusakumu alyawma tujzawna AAathabaalhooni bima kuntum taqooloona AAala
Allahighayra alhaqqi wakuntum AAan ayatihitastakbiroon
Swahili
Nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzuliya uwongo Mwenyezi Mungu, au anaye
sema: Mimi nimeletewa wahyi; na hali hakuletewa wahyi wowote. Na yule anaye
sema: Nitateremsha kama alivyo teremsha Mwenyezi Mungu. Na lau ungeli waona
madhaalimu wanavyo kuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea
mikono wakiwambia: Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ya fedheha kwa sababu
ya mliyo kuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo ya haki, na mlivyo kuwa
mkizifanyia kiburi Ishara zake.
|
Ayah 6:94 الأية
وَلَقَدْ جِئْتُمُونَا فُرَادَىٰ كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَتَرَكْتُم
مَّا خَوَّلْنَاكُمْ وَرَاءَ ظُهُورِكُمْ ۖ وَمَا نَرَىٰ مَعَكُمْ شُفَعَاءَكُمُ
الَّذِينَ زَعَمْتُمْ أَنَّهُمْ فِيكُمْ شُرَكَاءُ ۚ لَقَد تَّقَطَّعَ بَيْنَكُمْ
وَضَلَّ عَنكُم مَّا كُنتُمْ تَزْعُمُونَ
Walaqad ji/tumoona furadakama khalaqnakum awwala marratin wataraktum
makhawwalnakum waraa thuhoorikum wamanara maAAakum shufaAAaakumu
allatheenazaAAamtum annahum feekum shurakao laqad taqattaAAabaynakum wadalla
AAankum ma kuntum tazAAumoon
Swahili
Nanyi mlitujia wapweke kama tulivyo kuumbeni mara ya kwanza. Na mkayaacha nyuma
yenu yote tuliyo kupeni, na wala hatuwaoni hao waombezi wenu, ambao mlidai kuwa
ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwenu. Yamekatika makhusiano baina yenu, na
yamekupoteeni mliyo kuwa mkidai.
|
Ayah 6:95 الأية
إِنَّ اللَّهَ فَالِقُ الْحَبِّ وَالنَّوَىٰ ۖ يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ
وَمُخْرِجُ الْمَيِّتِ مِنَ الْحَيِّ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّهُ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ
Inna Allaha faliqu alhabbiwannawa yukhriju alhayya mina almayyitiwamukhriju
almayyiti mina alhayyi thalikumu Allahufaanna tu/fakoon
Swahili
Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji mbegu na kokwa, zikachipua. Humtoa aliye
hai kutoka maiti, naye ni mtoaji maiti kutokana na aliye hai. Huyo ndiye
Mwenyezi Mungu. Basi vipi mnageuzwa?
|
Ayah 6:96 الأية
فَالِقُ الْإِصْبَاحِ وَجَعَلَ اللَّيْلَ سَكَنًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ
حُسْبَانًا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ
Faliqu al-isbahiwajaAAala allayla sakanan washshamsa walqamara husbananthalika
taqdeeru alAAazeezi alAAaleem
Swahili
Ndiye anaye pambazua mwangaza wa asubuhi; na ameufanya usiku kwa mapumziko na
utulivu, na jua na mwezi kwenda kwa hisabu. Hayo ndiyo makadirio ya Aliye tukuka
Mwenye nguvu, Mwenye ujuzi.
|
Ayah 6:97 الأية
وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ النُّجُومَ لِتَهْتَدُوا بِهَا فِي ظُلُمَاتِ
الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ
Wahuwa allathee jaAAala lakumu annujoomalitahtadoo biha fee thulumati
albarriwalbahri qad fassalna al-ayatiliqawmin yaAAlamoon
Swahili
Na Yeye ndiye aliye kuwekeeni nyota ili mwongoke kwazo katika kiza cha bara na
bahari. Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanao jua.
|
Ayah 6:98 الأية
وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ فَمُسْتَقَرٌّ وَمُسْتَوْدَعٌ ۗ
قَدْ فَصَّلْنَا الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَفْقَهُونَ
Wahuwa allathee anshaakum min nafsinwahidatin famustaqarrun wamustawdaAAun qad
fassalnaal-ayati liqawmin yafqahoon
Swahili
Na Yeye ndiye aliye kuzalisheni kutokana na nafsi moja. Pako pahali pa kutulia
na pa kupita njia. Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanao fahamu.
|
Ayah 6:99 الأية
وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجْنَا بِهِ نَبَاتَ كُلِّ
شَيْءٍ فَأَخْرَجْنَا مِنْهُ خَضِرًا نُّخْرِجُ مِنْهُ حَبًّا مُّتَرَاكِبًا وَمِنَ
النَّخْلِ مِن طَلْعِهَا قِنْوَانٌ دَانِيَةٌ وَجَنَّاتٍ مِّنْ أَعْنَابٍ
وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُشْتَبِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ ۗ انظُرُوا إِلَىٰ
ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَيَنْعِهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكُمْ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ
يُؤْمِنُونَ
Wahuwa allathee anzala mina assama-imaan faakhrajna bihi nabata kulli
shay-infaakhrajna minhu khadiran nukhriju minhu habbanmutarakiban wamina
annakhli min talAAihaqinwanun daniyatun wajannatin min aAAnabinwazzaytoona
warrummana mushtabihanwaghayra mutashabihin onthuroo ilathamarihi itha athmara
wayanAAihi inna fee thalikumlaayatin liqawmin yu/minoon
Swahili
Na Yeye ndiye anaye teremsha maji kutoka mbinguni; na kwayo tunatoa mimea ya
kila kitu. Kutokana na baadhi yao tukatoa mimea ya majani, tukatoa ndani yake
punje zilizo pandana; na kutokana na mitende yakatoka kwenye makole yake mashada
yaliyo inama; na bustani za mizabibu na mizaituni, na makomamanga, yaliyo fanana
na yasiyo fanana. Angalieni matunda yake yanapo zaa na yakawiva. Hakika katika
hayo pana Ishara kwa watu wanao amini.
|
Ayah 6:100 الأية
وَجَعَلُوا لِلَّهِ شُرَكَاءَ الْجِنَّ وَخَلَقَهُمْ ۖ وَخَرَقُوا لَهُ بَنِينَ
وَبَنَاتٍ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يَصِفُونَ
WajaAAaloo lillahi shurakaaaljinna wakhalaqahum wakharaqoo lahu baneena
wabanatinbighayri AAilmin subhanahu wataAAala AAammayasifoon
Swahili
Bado wamemfanyia Mwenyezi Mungu majini kuwa washirika wake, na hali Yeye ndiye
aliye waumba. Na wakamzulia, bila ya ujuzi wowote, kuwa ana wana wa kiume na wa
kike. Subhanahu, Ametakasika na ametukuka juu ya hayo wanayo mbandikiza nayo!
|
Ayah 6:101 الأية
بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ وَلَدٌ وَلَمْ تَكُن
لَّهُ صَاحِبَةٌ ۖ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ
BadeeAAu assamawatiwal-ardi anna yakoonu lahu waladun walamtakun lahu sahibatun
wakhalaqa kulla shay-in wahuwabikulli shay-in AAaleem
Swahili
Yeye ndiye Muumbaji wa mbingu na ardhi bila ya ruwaza. Itakuwaje awe na mwana
naye hakuwa na mke? Naye ndiye aliye umba kila kitu. Naye ni Mwenye kujua kila
kitu.
|
Ayah 6:102 الأية
ذَٰلِكُمُ اللَّهُ رَبُّكُمْ ۖ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ
فَاعْبُدُوهُ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ
Thalikumu Allahu rabbukum lailaha illa huwa khaliqu kulli shay-in
faAAbudoohuwahuwa AAala kulli shay-in wakeel
Swahili
Huyo ndiye Allah, Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, hapana mungu ila Yeye, Muumba
wa kila kitu. Basi muabuduni Yeye tu. Naye ni Mtegemewa wa kila kitu.
|
Ayah 6:103 الأية
لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ ۖ وَهُوَ اللَّطِيفُ
الْخَبِيرُ
La tudrikuhu al-absaru wahuwayudriku al-absara wahuwa allateefu alkhabeer
Swahili
Macho hayamfikilii bali Yeye anayafikilia macho. Naye ni Mjuzi, Mwenye khabari.
|
Ayah 6:104 الأية
قَدْ جَاءَكُم بَصَائِرُ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَنْ أَبْصَرَ فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَنْ
عَمِيَ فَعَلَيْهَا ۚ وَمَا أَنَا عَلَيْكُم بِحَفِيظٍ
Qad jaakum basa-iru minrabbikum faman absara falinafsihi waman AAamiya
faAAalayhawama ana AAalaykum bihafeeth
Swahili
Zimekwisha kukujieni hoja wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anaye ona ni kwa
faida yake mwenyewe, na anaye pofuka basi ni khasara yake. Nami si mtunzaji
wenu.
|
Ayah 6:105 الأية
وَكَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ وَلِيَقُولُوا دَرَسْتَ وَلِنُبَيِّنَهُ لِقَوْمٍ
يَعْلَمُونَ
Wakathalika nusarrifu al-ayatiwaliyaqooloo darasta walinubayyinahu liqawmin
yaAAlamoon
Swahili
Na namna hivyo tunazisarifu Aya, na wao wakwambie: Umesoma. Na ili tuyabainishe
kwa watu wanao jua.
|
Ayah 6:106 الأية
اتَّبِعْ مَا أُوحِيَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ
وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ
IttabiAA ma oohiya ilayka minrabbika la ilaha illa huwa waaAAridAAani
almushrikeen
Swahili
Fuata uliyo funuliwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Hapana mungu ila Yeye. Na
jitenge na washirikina.
|
Ayah 6:107 الأية
وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ مَا أَشْرَكُوا ۗ وَمَا جَعَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ۖ
وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ
Walaw shaa Allahu maashrakoo wama jaAAalnaka AAalayhim hafeethanwama anta
AAalayhim biwakeel
Swahili
Na lau Mwenyezi Mungu angeli penda, wasingeli shiriki. Na Sisi hatukukufanya
wewe uwe mtunzaji wao. Wala wewe si mlinzi juu yao.
|
Ayah 6:108 الأية
وَلَا تَسُبُّوا الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّهِ فَيَسُبُّوا اللَّهَ
عَدْوًا بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ كَذَٰلِكَ زَيَّنَّا لِكُلِّ أُمَّةٍ عَمَلَهُمْ ثُمَّ
إِلَىٰ رَبِّهِم مَّرْجِعُهُمْ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Wala tasubboo allatheenayadAAoona min dooni Allahi fayasubboo AllahaAAadwan
bighayri AAilmin kathalika zayyanna likulliommatin AAamalahum thumma ila
rabbihim marjiAAuhumfayunabbi-ohum bima kanoo yaAAmaloon
Swahili
Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao
wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua. Namna hivyo tumewapambia
kila umma vitendo vyao. Kisha marejeo yao yatakuwa kwa Mola wao Mlezi, naye
atawaambia waliyo kuwa wakiyatenda.
|
Ayah 6:109 الأية
وَأَقْسَمُوا بِاللَّهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ لَئِن جَاءَتْهُمْ آيَةٌ
لَّيُؤْمِنُنَّ بِهَا ۚ قُلْ إِنَّمَا الْآيَاتُ عِندَ اللَّهِ ۖ وَمَا
يُشْعِرُكُمْ أَنَّهَا إِذَا جَاءَتْ لَا يُؤْمِنُونَ
Waaqsamoo billahi jahda aymanihimla-in jaat-hum ayatun layu/minunna biha
qulinnama al-ayatu AAinda Allahi wamayushAAirukum annaha itha jaat layu/minoon
Swahili
Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu kwa ukomo wa viapo vyao, kuwa ikiwafikia Ishara
wataiamini. Sema: Ishara ziko kwa Mwenyezi Mungu. Na nyinyi hamjui kuwa zitapo
kuja hawato amini.
|
Ayah 6:110 الأية
وَنُقَلِّبُ أَفْئِدَتَهُمْ وَأَبْصَارَهُمْ كَمَا لَمْ يُؤْمِنُوا بِهِ أَوَّلَ
مَرَّةٍ وَنَذَرُهُمْ فِي طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ
Wanuqallibu af-idatahum waabsarahumkama lam yu/minoo bihi awwala marratin
wanatharuhumfee tughyanihim yaAAmahoon
Swahili
Nasi twazigeuza nyoyo zao na macho yao. Kama walivyo kuwa hawakuamini mara ya
kwanza, tunawaacha katika maasi yao wakitangatanga.
|
Ayah 6:111 الأية
وَلَوْ أَنَّنَا نَزَّلْنَا إِلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ الْمَوْتَىٰ
وَحَشَرْنَا عَلَيْهِمْ كُلَّ شَيْءٍ قُبُلًا مَّا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا إِلَّا أَن
يَشَاءَ اللَّهُ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ يَجْهَلُونَ
Walaw annana nazzalnailayhimu almala-ikata wakallamahumu almawta
wahasharnaAAalayhim kulla shay-in qubulan ma kanoo liyu/minooilla an yashaa
Allahu walakinnaaktharahum yajhaloon
Swahili
NA LAU kuwa tungeli wateremshia Malaika, na maiti wakazungumza nao, na
tukawakusanyia kila kitu mbele yao, bado wasingeli amini, ila Mwenyezi Mungu
atake. Lakini wengi wao wamo ujingani.
|
Ayah 6:112 الأية
وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا شَيَاطِينَ الْإِنسِ وَالْجِنِّ
يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ غُرُورًا ۚ وَلَوْ شَاءَ
رَبُّكَ مَا فَعَلُوهُ ۖ فَذَرْهُمْ وَمَا يَفْتَرُونَ
Wakathalika jaAAalna likullinabiyyin AAaduwwan shayateena al-insi waljinni
yooheebaAAduhum ila baAAdin zukhrufa alqawlighurooran walaw shaa rabbuka ma
faAAaloohu fatharhumwama yaftaroon
Swahili
Na kadhaalika tumemfanyia kila Nabii maadui mashet'ani wa kiwatu, na kijini,
wakifundishana wao kwa wao maneno ya kupamba-pamba, kwa udanganyifu. Na angeli
penda Mola wako Mlezi wasingeli fanya hayo. Basi waache na wanayo yazua.
|
Ayah 6:113 الأية
وَلِتَصْغَىٰ إِلَيْهِ أَفْئِدَةُ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ
وَلِيَرْضَوْهُ وَلِيَقْتَرِفُوا مَا هُم مُّقْتَرِفُونَ
Walitasgha ilayhi af-idatuallatheena la yu/minoona bil-akhiratiwaliyardawhu
waliyaqtarifoo ma hum muqtarifoon
Swahili
Na ili nyoyo za wasio amini Akhera zielekee hayo, nao wayaridhie na wayachume
wanayo yachuma.
|
Ayah 6:114 الأية
أَفَغَيْرَ اللَّهِ أَبْتَغِي حَكَمًا وَهُوَ الَّذِي أَنزَلَ إِلَيْكُمُ
الْكِتَابَ مُفَصَّلًا ۚ وَالَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَعْلَمُونَ أَنَّهُ
مُنَزَّلٌ مِّن رَّبِّكَ بِالْحَقِّ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ
Afaghayra Allahi abtaghee hakamanwahuwa allathee anzala ilaykumu alkitaba
mufassalanwallatheena ataynahumu alkitabayaAAlamoona annahu munazzalun min
rabbika bilhaqqifala takoonanna mina almumtareen
Swahili
Je, nimtafute hakimu ghairi ya Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliye kuteremshieni
Kitabu kilicho elezwa waziwazi? Na hao tulio wapa Kitabu wanajua ya kwamba
kimeteremshwa na Mola wako Mlezi kwa Haki. Basi usiwe katika wanao tia shaka.
|
Ayah 6:115 الأية
وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ صِدْقًا وَعَدْلًا ۚ لَّا مُبَدِّلَ لِكَلِمَاتِهِ ۚ
وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ
Watammat kalimatu rabbika sidqanwaAAadlan la mubaddila likalimatihi wahuwa
assameeAAualAAaleem
Swahili
Na yametimia maneno ya Mola Mlezi wako kwa kweli na uadilifu. Hapana awezaye
kuyabadilisha maneno yake. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua.
|
Ayah 6:116 الأية
وَإِن تُطِعْ أَكْثَرَ مَن فِي الْأَرْضِ يُضِلُّوكَ عَن سَبِيلِ اللَّهِ ۚ إِن
يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ
Wa-in tutiAA akthara man fee al-ardiyudillooka AAan sabeeli Allahi in
yattabiAAoona illaaththanna wa-in hum illa yakhrusoon
Swahili
Na ukiwat'ii wengi katika hawa waliomo duniani watakupoteza na Njia ya Mwenyezi
Mungu. Hawa hawafuati ila dhana tu, na hawakuwa ila ni wenye kusema uwongo tu.
|
|