إِنَّ رَبَّكَ يَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدْنَىٰ مِن ثُلُثَيِ اللَّيْلِ
وَنِصْفَهُ وَثُلُثَهُ وَطَائِفَةٌ مِّنَ الَّذِينَ مَعَكَ ۚ وَاللهُ يُقَدِّرُ
اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ ۚ عَلِمَ أَن لَّن تُحْصُوهُ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۖ
فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنَ الْقُرْآنِ ۚ عَلِمَ أَن سَيَكُونُ مِنكُم
مَّرْضَىٰ ۙ وَآخَرُونَ يَضْرِبُونَ فِي الْأَرْضِ يَبْتَغُونَ مِن فَضْلِ اللهِ
ۙ وَآخَرُونَ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللهِ ۖ فَاقْرَءُوا مَا تَيَسَّرَ مِنْهُ
ۚ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَأَقْرِضُوا اللهَ قَرْضًا حَسَنًا
ۚ وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللهِ هُوَ
خَيْرًا وَأَعْظَمَ أَجْرًا ۚ وَاسْتَغْفِرُوا اللهَ ۖ إِنَّ اللهَ غَفُورٌ
رَّحِيمٌ
Inna rabbaka yaAAlamu annaka taqoomu adnamin thuluthayi allayli wanisfahu
wathuluthahu wata-ifatunmina allatheena maAAaka wallahu yuqaddiruallayla
wannahara AAalima an lan tuhsoohufataba AAalaykum faqraoo ma tayassara
minaalqur-ani AAalima an sayakoonu minkum marda waakharoonayadriboona fee
al-ardi yabtaghoona min fadliAllahi waakharoona yuqatiloona fee sabeeliAllahi
faqraoo ma tayassara minhu waaqeemooassalata waatoo azzakatawaaqridoo Allaha
qardan hasanan wamatuqaddimoo li-anfusikum min khayrin tajidoohu AAinda
Allahihuwa khayran waaAAthama ajran wastaghfirooAllaha inna Allaha ghafoorun
raheem
Swahili
Hakika Mola wako Mlezi anajua ya kuwa hakika wewe unakesha karibu na thuluthi
mbili za usiku, na nusu yake, na thuluthi yake. Na baadhi ya watu walio pamoja
nawe kadhaalika. Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye ukadiria usiku na mchana. Anajua
kuwa hamwezi kuweka hisabu, basi amekusameheni. Basi someni kilicho chepesi
katika Qur'ani. Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine
wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu, na wengine
wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo,
na mshike Sala, na toeni Zaka, na mkopesheni Mwenyezi Mungu mkopo mwema. Na
kheri yoyote mnayo itanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Mwenyezi
Mungu, imekuwa bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana. Na mtakeni msamaha
Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.