Ya kuwa mtie katika kisanduku, na kisha kitie mtoni, na mto utamfikisha
ufukweni. Atamchukua adui yangu naye ni adui yake. Na nimekutilia mapenzi yanayo
tokana kwangu, na ili ulelewe machoni mwangu.
Dada yako alipo kwenda na akasema: Je! Nikujuulisheni mtu wa kuweza kumlea? Basi
tukakurejesha kwa mama yako ili macho yake yaburudike, wala asihuzunike. Na
ulimuuwa mtu, nasi tukakuokoa katika dhiki, na tukakujaribu kwa majaribio mengi.
Ukakaa miaka kwa watu wa Madyana. Kisha ukaja kama ilivyo kadiriwa, ewe Musa!
Basi mwendeeni, na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola wako Mlezi! Basi
waache Wana wa Israili watoke nasi, wala usiwaadhibu. Sisi tumekuletea ishara
itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na amani itakuwa juu ya aliye fuata uwongofu.
Ambaye amekufanyieni ardhi kuwa tandiko, na akakupitishieni humo njia, na
akakuteremshieni kutoka mbinguni maji. Na kwa hayo tukatoa namna mbali mbali za
mimema.
Na kitupe kilicho katika mkono wako wa kulia; kitavimeza walivyo viunda. Hakika
walivyo unda ni hila za mchawi tu, na mchawi hafanikiwi popote afikapo.
(Firauni) akasema: Oh! Mnamuamini kabla sijakupeni ruhusa? Hakika yeye ndiye
mkubwa wenu aliye kufundisheni uchawi. Basi kwa yakini nitakukateni mikono yenu
na miguu yenu kwa kutafautisha. Na nitakutundikeni misalabani katika vigogo vya
mitende, na hapo kwa yakini mtajua ni nani katika sisi aliye mkali wa kuadhibu
na kuiendeleza adhabu yake.
Wakasema: Hatutokukhiari wewe kuliko ishara waziwazi zilizo tujia, na kuliko
yule aliye tuumba. Basi hukumu utavyo hukumu; kwani wewe unahukumu haya ya
maisha ya duniani tu.
Hakika sisi tumemuamini Mola wetu Mlezi ili atusamehe makosa yetu na uchawi ulio
tulazimisha kuufanya. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mbora na Mwenye kudumu zaidi.
Kuleni katika vitu vizuri hivyo tulivyo kuruzukuni, wala msiruke mipaka katika
hayo, isije ikakushukieni ghadhabu yangu. Na inaye mshukia ghadhabu yangu basi
huyo ameangamia.
Musa akarudi kwa watu wake kwa ghadhabu na kusikitika. Akasema: Enyi watu wangu!
Kwani Mola wenu Mlezi hakukuahidini ahadi nzuri? Je, umekuwa muda mrefu kwenu au
mmetaka ikushukieni ghadhabu ya Mola wenu Mlezi, ndio maana mkavunja miadi
yangu?
Wakasema: Sisi hatukuvunja miadi yako kwa khiari yetu, lakini tulibebeshwa
mizigo ya mapambo ya watu, basi tukaitupa. Na hivyo ndivyo alivyo toa shauri
Msamaria.
Na hakika Harun alikwisha waambia kabla yake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi
mmetiwa mtihanini tu kwa kitu hiki. Na kwa yakini Mola wenu Mlezi ni Arrahmani,
Mwingi wa Rehema. Basi nifuateni mimi, na t'iini amri yangu!
Akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Usinishike ndevu zangu, wala kichwa changu.
Kwa hakika naliogopa usije sema: Umewafarikisha Wana wa Israil, na hukungojea
kauli yangu.
(Musa) akasema: Basi ondoka! Na kwa yakini utakuwa katika maisha ukisema:
Usiniguse. Na hakika una ahadi kwako isiyo vunjwa. Na mtazame huyo mungu wako
uliye endelea kumuabudu - Sisi kwa hakika tutamchoma moto, kisha tutamtawanya
baharini atawanyike.
Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki. Wala usiifanyie haraka hii Qur'ani,
kabla haujamalizika ufunuo wake. Na sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie ilimu.