Akasema: Mola wangu Mlezi! Mafupa yangu yamedhoofika, na kichwa kinameremeta kwa
mvi; wala, Mola wangu Mlezi, sikuwa mwenye bahati mbaya kwa kukuomba Wewe.
(Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi
kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na
hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa.
Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote basi
sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo
sitasema na mtu.
Nami najitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Na
ninamwomba Mola wangu Mlezi; asaa nisiwe mwenye kukosa bahati kwa kumwomba Mola
wangu Mlezi.
Hao ndio alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii katika uzao wa
Adam, na katika uzao wa wale tulio wapandisha pamoja na Nuhu, na katika uzao wa
Ibrahim na Israil, na katika wale tulio waongoa na tukawateuwa. Wanapo somewa
Aya za Mwingi wa Rehema huanguka kusujudu na kulia.
(Nao watasema:) Wala hatuteremki ila kwa amri ya Mola wako Mlezi. Ni yake Yeye
yaliyoko mbele yetu na yaliyoko nyuma yetu, na yaliyomo katikati ya hayo. Na
Mola wako Mlezi si mwenye kusahau.
Sema: Walio katika upotofu basi Arrahmani Mwingi wa Rahema atawapururia muda
mpaka wayaone waliyo onywa - ama ni adhabu au ni Saa. Hapo ndipo watapo jua ni
nani mwenye makao mabaya na mwenye askari dhaifu.
Na Mwenyezi Mungu huwazidishia uwongofu wenye kushika uwongofu. Na mema yenye
kudumu ni bora katika malipo mbele ya Mola wako Mlezi na yana mwisho mwema.