Zimeghafilika nyoyo zao. Na wale walio dhulumu hunong'onezana kwa siri: Ni nani
ati huyu isipo kuwa ni binaadamu tu kama nyinyi! Mnauwendea uchawi hali nanyi
mnaona?
Lakini wao walisema: Hizo ni ndoto za ovyo ovyo, bali amezizua tu, bali huyo ni
mtunga mashairi. Basi atuletee miujiza kama walivyo tumwa wale wa mwanzo.
Lau wangeli kuwamo humo miungu wengine isipo kuwa Mwenyezi Mungu basi bila ya
shaka hizo mbingu na ardhi zingeli fisidika. Subahana 'Llah Ametakasika Mwenyezi
Mungu, Bwana wa A'rshi (Kiti cha Enzi), na hayo wanayo yazua.
Au wanawaabudu miungu mingine badala yake? Sema: Leteni ushahidi wenu! Haya ni
ukumbusho wa hawa walio nami, na ukumbusho wa walio kabla yangu. Lakini wengi
wao hawaijui kweli, na kwa hivyo wanapuuza.
Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana,
kisha Sisi tukazibabandua? Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai? Basi je,
hawaamini?
Na wakikuona walio kufuru hawakufanyi wewe ila ni kitu cha maskhara tu,
(wakisema): Je! Ndiye huyu anaye itaja miungu yenu? Na hali wao wanakataa
kumkumbuka Arrahman, Mwingi wa Rehema!
Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka umri ukawa mrefu kwao. Je, hawaoni
ya kwamba Sisi tunaifikia ardhi tukiipunguza ncha zake? Basi je! Hao ni wenye
kushinda?
Nasi tutaweka mizani za uadilifu kwa Siku ya Kiyama. Basi nafsi haitadhulumiwa
kitu chochote. Hata ikiwa ni uzito wa chembe ya khardali tutaileta. Nasi
tunatosha kuwa washika hisabu.
Na Daud na Suleiman walipo kata hukumu katika kadhiya ya konde walipo lisha humo
mbuzi wa watu usiku. Na Sisi tulikuwa wenye kushuhudia hukumu yao hiyo.
Tukamfahamisha Suleiman. Na kila mmoja wao tulimpa hukumu na ilimu. Na
tuliifanya milima na ndege kuwa pamoja na Daud imnyenyekee na imtakase Mwenyezi
Mungu. Na Sisi ndio tulio fanya hayo.