Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la
nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama.
Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa
waumbaji.
Na hakika mnayo mazingatio makubwa katika nyama hoa - tunakunywesheni katika
vile viliomo matumboni mwao, na nyinyi mnapata katika hao manufaa mengi, na pia
mnawala.
Walisema wale wakuu walio kufuru katika watu wake: Huyu si chochote ila ni mtu
tu kama nyinyi. Anataka kujipa ubora juu yenu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu
amependa basi yakini angeli teremsha Malaika. Hatukusikia haya kwa baba zetu wa
zamani.
Tukampa wahyi: Unda jahazi mbele ya macho yetu na uwongozi wetu! Basi itapo fika
amri yetu na ikafurika tanuri, hapo waingize ndani yake wa kila namna dume na
jike, na ahali zako, isipo kuwa yule ambaye katika wao juu yake imekwisha
tangulia kauli. Wala usinitajie hao walio dhulumu. Kwani hao bila ya shaka
watazamishwa.
Basi utakapo tulia wewe na walio pamoja nawe humo marikebuni, sema:
Alhamdulillahi Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, aliye tuokoa na watu
madhaalimu!
Na wakubwa katika watu wake walio kufuru na wakakanusha mkutano wa Akhera, na
tukawadekeza kwa starehe katika maisha ya dunia, walisema: Huyu si chochote ila
ni binaadamu kama nyinyi; anakula mlacho, na anakunywa mnywacho.
Kisha tukawatuma Mitume wetu, mmoja baada ya mmoja. Kila umma alipo wafikia
Mtume wao walimkanusha. Tukawafuatanisha hawa baada ya hawa, na tukawafanya ni
hadithi za kusimuliwa. Wakapotelea mbali watu wasio amini.
Na lau kuwa Haki ingeli fuata matamanio yao, basi zingeli haribika mbingu na
ardhi na waliomo ndani. Bali tumewaletea ukumbusho wao, nao wanajitenga mbali na
ukumbusho wao.