First Ayah 1 الأية الأوليبِسْم ِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
طس ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْقُرْآنِ وَكِتَابٍ مُّبِينٍ
Swahili
T'aa Siin. (T'.S.), Hizi ni Aya za Qur'ani na Kitabu kinacho bainisha;
|
Ayah 27:2 الأية
هُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ
Swahili
Uwongofu na bishara kwa Waumini,
|
Ayah 27:3 الأية
الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ
يُوقِنُونَ
Swahili
Ambao wanashika Sala, na wanatoa Zaka, na Akhera wana yakini nayo.
|
Ayah 27:4 الأية
إِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ زَيَّنَّا لَهُمْ أَعْمَالَهُمْ
فَهُمْ يَعْمَهُونَ
Swahili
Kwa hakika wale wasio iamini Akhera tumewapambia vitendo vyao, kwa hivyo
wanatangatanga ovyo.
|
Ayah 27:5 الأية
أُولَٰئِكَ الَّذِينَ لَهُمْ سُوءُ الْعَذَابِ وَهُمْ فِي الْآخِرَةِ هُمُ
الْأَخْسَرُونَ
Swahili
Hao ndio watapata adhabu mbaya kabisa, na hao katika Akhera ndio watapata
khasara zaidi.
|
Ayah 27:6 الأية
وَإِنَّكَ لَتُلَقَّى الْقُرْآنَ مِن لَّدُنْ حَكِيمٍ عَلِيمٍ
Swahili
Na hakika wewe unafundishwa Qur'ani inayo tokana kwake Mwenye hikima Mwenye
kujua.
|
Ayah 27:7 الأية
إِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِأَهْلِهِ إِنِّي آنَسْتُ نَارًا سَآتِيكُم مِّنْهَا بِخَبَرٍ
أَوْ آتِيكُم بِشِهَابٍ قَبَسٍ لَّعَلَّكُمْ تَصْطَلُونَ
Swahili
(Kumbuka) Musa alipo waambia ahali zake: Hakika nimeona moto, nitakwenda
nikuleteeni khabari, au nitakuleteeni kijinga kinacho waka ili mpate kuota moto.
|
Ayah 27:8 الأية
فَلَمَّا جَاءَهَا نُودِيَ أَن بُورِكَ مَن فِي النَّارِ وَمَنْ حَوْلَهَا
وَسُبْحَانَ اللَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ
Swahili
Basi alipo fika ilinadiwa: Amebarikiwa aliomo katika moto huu na walioko
pembezoni mwake. Na ametakasika Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
|
Ayah 27:9 الأية
يَا مُوسَىٰ إِنَّهُ أَنَا اللَّهُ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ
Swahili
Ewe Musa! Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
|
Ayah 27:10 الأية
وَأَلْقِ عَصَاكَ ۚ فَلَمَّا رَآهَا تَهْتَزُّ كَأَنَّهَا جَانٌّ وَلَّىٰ مُدْبِرًا
وَلَمْ يُعَقِّبْ ۚ يَا مُوسَىٰ لَا تَخَفْ إِنِّي لَا يَخَافُ لَدَيَّ
الْمُرْسَلُونَ
Swahili
Na itupe fimbo yako! Alipo iona ikitikisika kama nyoka, aligeuka nyuma wala
hakungoja. Ewe Musa! Usikhofu! Hakika hawakhofu mbele yangu Mitume.
|
Ayah 27:11 الأية
إِلَّا مَن ظَلَمَ ثُمَّ بَدَّلَ حُسْنًا بَعْدَ سُوءٍ فَإِنِّي غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Swahili
Lakini aliye dhulumu, kisha akabadilisha wema baada ya ubaya, basi Mimi ni
Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
|
Ayah 27:12 الأية
وَأَدْخِلْ يَدَكَ فِي جَيْبِكَ تَخْرُجْ بَيْضَاءَ مِنْ غَيْرِ سُوءٍ ۖ فِي تِسْعِ
آيَاتٍ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَقَوْمِهِ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ
Swahili
Na ingiza mkono wako katika mfuko wako, utatoka mweupe bila ya maradhi. Ni
katika Ishara tisa za kumpelekea Firauni na kaumu yake. Hakika hao walikuwa watu
waovu.
|
Ayah 27:13 الأية
فَلَمَّا جَاءَتْهُمْ آيَاتُنَا مُبْصِرَةً قَالُوا هَٰذَا سِحْرٌ مُّبِينٌ
Swahili
Basi zilipo wafikia Ishara zetu hizo zenye kuonyesha, wakasema: Huu ni uchawi
dhaahiri.
|
Ayah 27:14 الأية
وَجَحَدُوا بِهَا وَاسْتَيْقَنَتْهَا أَنفُسُهُمْ ظُلْمًا وَعُلُوًّا ۚ فَانظُرْ
كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ
Swahili
Na wakazikataa kwa dhulma na kujivuna, na hali ya kuwa nafsi zao zina yakini
nazo. Basi angalia ulikuwaje mwisho wa mafisadi!
|
Ayah 27:15 الأية
وَلَقَدْ آتَيْنَا دَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ عِلْمًا ۖ وَقَالَا الْحَمْدُ لِلَّهِ
الَّذِي فَضَّلَنَا عَلَىٰ كَثِيرٍ مِّنْ عِبَادِهِ الْمُؤْمِنِينَ
Swahili
Na hakika tuliwapa Daudi na Sulaiman ilimu, na wakasema: Alhamdu Lillahi,
Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu aliye tufadhilisha kuliko wengi katika
waja wake Waumini.
|
Ayah 27:16 الأية
وَوَرِثَ سُلَيْمَانُ دَاوُودَ ۖ وَقَالَ يَا أَيُّهَا النَّاسُ عُلِّمْنَا مَنطِقَ
الطَّيْرِ وَأُوتِينَا مِن كُلِّ شَيْءٍ ۖ إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ الْفَضْلُ
الْمُبِينُ
Swahili
Na Sulaiman alimrithi Daudi, na akasema: Enyi watu! Tumefunzwa usemi wa ndege,
na tumepewa kila kitu. Hakika hii ni fadhila iliyo dhaahiri.
|
Ayah 27:17 الأية
وَحُشِرَ لِسُلَيْمَانَ جُنُودُهُ مِنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ وَالطَّيْرِ فَهُمْ
يُوزَعُونَ
Swahili
Na alikusanyiwa Sulaiman majeshi yake ya majini, na watu, na ndege; nayo
yakapangwa kwa nidhamu.
|
Ayah 27:18 الأية
حَتَّىٰ إِذَا أَتَوْا عَلَىٰ وَادِ النَّمْلِ قَالَتْ نَمْلَةٌ يَا أَيُّهَا
النَّمْلُ ادْخُلُوا مَسَاكِنَكُمْ لَا يَحْطِمَنَّكُمْ سُلَيْمَانُ وَجُنُودُهُ
وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ
Swahili
Mpaka walipo fika kwenye bonde la wadudu chungu, alisema mdudu chungu mmoja:
Enyi wadudu chungu! Ingieni majumbani mwenu, asikupondeni Sulaiman na majeshi
yake bila ya wao kutambua.
|
Ayah 27:19 الأية
فَتَبَسَّمَ ضَاحِكًا مِّن قَوْلِهَا وَقَالَ رَبِّ أَوْزِعْنِي أَنْ أَشْكُرَ
نِعْمَتَكَ الَّتِي أَنْعَمْتَ عَلَيَّ وَعَلَىٰ وَالِدَيَّ وَأَنْ أَعْمَلَ
صَالِحًا تَرْضَاهُ وَأَدْخِلْنِي بِرَحْمَتِكَ فِي عِبَادِكَ الصَّالِحِينَ
Swahili
Basi (Sulaiman) akatabasamu akacheka kwa neno hili, na akasema: Ee Mola wangu
Mlezi! Nizindue niishukuru neema yako uliyo nineemesha mimi na wazazi wangu, na
nipate kutenda mema uyapendayo, na uniingize kwa rehema yako katika waja wako
wema.
|
Ayah 27:20 الأية
وَتَفَقَّدَ الطَّيْرَ فَقَالَ مَا لِيَ لَا أَرَى الْهُدْهُدَ أَمْ كَانَ مِنَ
الْغَائِبِينَ
Swahili
Na akawakagua ndege, na akasema: Imekuwaje, mbona simwoni Hud-hud, au amekuwa
miongoni mwa walio ghibu?
|
Ayah 27:21 الأية
لَأُعَذِّبَنَّهُ عَذَابًا شَدِيدًا أَوْ لَأَذْبَحَنَّهُ أَوْ لَيَأْتِيَنِّي
بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ
Swahili
Kwa yakini nitamuadhibu kwa adhabu kali, au nitamchinja, au aniletee hoja ya
kutosha.
|
Ayah 27:22 الأية
فَمَكَثَ غَيْرَ بَعِيدٍ فَقَالَ أَحَطتُ بِمَا لَمْ تُحِطْ بِهِ وَجِئْتُكَ مِن
سَبَإٍ بِنَبَإٍ يَقِينٍ
Swahili
Basi (Hud-hud) akakaa si mbali na akasema: Nimegundua usilo gundua wewe, na
ninakujia hivi kutoka nchi ya Sabai, na nakuletea khabari za yakini.
|
Ayah 27:23 الأية
إِنِّي وَجَدتُّ امْرَأَةً تَمْلِكُهُمْ وَأُوتِيَتْ مِن كُلِّ شَيْءٍ وَلَهَا
عَرْشٌ عَظِيمٌ
Swahili
Hakika mimi nimemkuta mwanamke anawatawala, naye amepewa kila kitu, na anacho
kiti cha enzi kikubwa.
|
Ayah 27:24 الأية
وَجَدتُّهَا وَقَوْمَهَا يَسْجُدُونَ لِلشَّمْسِ مِن دُونِ اللَّهِ وَزَيَّنَ
لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ فَصَدَّهُمْ عَنِ السَّبِيلِ فَهُمْ لَا
يَهْتَدُونَ
Swahili
Nimemkuta yeye na watu wake wanalisujudia jua badala ya Mwenyezi Mungu; na
Shet'ani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia Njia. Kwa hivyo hawakuongoka,
|
Ayah 27:25 الأية
أَلَّا يَسْجُدُوا لِلَّهِ الَّذِي يُخْرِجُ الْخَبْءَ فِي السَّمَاوَاتِ
وَالْأَرْضِ وَيَعْلَمُ مَا تُخْفُونَ وَمَا تُعْلِنُونَ
Swahili
Na hawamsujudii Mwenyezi Mungu ambaye huyatoa yaliyo fichikana katika mbingu na
ardhi, na anayajua mnayo yaficha na mnayo yatangaza.
|
Ayah 27:26 الأية
اللَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ ۩
Swahili
Mwenyezi Mungu - hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa A'rshi tukufu..
|
Ayah 27:27 الأية
قَالَ سَنَنظُرُ أَصَدَقْتَ أَمْ كُنتَ مِنَ الْكَاذِبِينَ
Swahili
Akasema (Sulaiman): Tutatazama umesema kweli au wewe ni miongoni mwa waongo.
|
Ayah 27:28 الأية
اذْهَب بِّكِتَابِي هَٰذَا فَأَلْقِهْ إِلَيْهِمْ ثُمَّ تَوَلَّ عَنْهُمْ فَانظُرْ
مَاذَا يَرْجِعُونَ
Swahili
Nenda na barua yangu hii na uwafikishie, kisha waache na utazame watarejesha
nini.
|
Ayah 27:29 الأية
قَالَتْ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ إِنِّي أُلْقِيَ إِلَيَّ كِتَابٌ كَرِيمٌ
Swahili
(Malkia) akasema: Enyi wahishimiwa! Hakika nimeletewa barua tukufu.
|
Ayah 27:30 الأية
إِنَّهُ مِن سُلَيْمَانَ وَإِنَّهُ بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Swahili
Imetoka kwa Sulaiman nayo ni: Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema,
Mwenye kurehemu.
|
Ayah 27:31 الأية
أَلَّا تَعْلُوا عَلَيَّ وَأْتُونِي مُسْلِمِينَ
Swahili
Msinifanyie jeuri, na fikeni kwangu nanyi mmekwisha kuwa wenye kusalimu amri.
|
Ayah 27:32 الأية
قَالَتْ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ أَفْتُونِي فِي أَمْرِي مَا كُنتُ قَاطِعَةً
أَمْرًا حَتَّىٰ تَشْهَدُونِ
Swahili
Akasema: Enyi wahishimiwa! Nipeni shauri katika jambo langu hili, kwani mimi
sikati shauri yoyote mpaka mhudhurie.
|
Ayah 27:33 الأية
قَالُوا نَحْنُ أُولُو قُوَّةٍ وَأُولُو بَأْسٍ شَدِيدٍ وَالْأَمْرُ إِلَيْكِ
فَانظُرِي مَاذَا تَأْمُرِينَ
Swahili
Wakasema: Sisi ni wenye nguvu na wakali kwa vita; na amri iko kwako, basi tazama
ni nini unaamrisha.
|
Ayah 27:34 الأية
قَالَتْ إِنَّ الْمُلُوكَ إِذَا دَخَلُوا قَرْيَةً أَفْسَدُوهَا وَجَعَلُوا
أَعِزَّةَ أَهْلِهَا أَذِلَّةً ۖ وَكَذَٰلِكَ يَفْعَلُونَ
Swahili
Akasema: Hakika wafalme wanapo uingia mji wanauharibu, na wanawafanya wale
watukufu wake kuwa wanyonge. Na hivyo ndivyo watendavyo.
|
Ayah 27:35 الأية
وَإِنِّي مُرْسِلَةٌ إِلَيْهِم بِهَدِيَّةٍ فَنَاظِرَةٌ بِمَ يَرْجِعُ
الْمُرْسَلُونَ
Swahili
Lakini mimi nitawapelekea zawadi, nami nitangoja watakayo rudi nayo wajumbe.
|
Ayah 27:36 الأية
فَلَمَّا جَاءَ سُلَيْمَانَ قَالَ أَتُمِدُّونَنِ بِمَالٍ فَمَا آتَانِيَ اللَّهُ
خَيْرٌ مِّمَّا آتَاكُم بَلْ أَنتُم بِهَدِيَّتِكُمْ تَفْرَحُونَ
Swahili
Basi alipo fika (mjumbe) kwa Sulaiman, alisema (Sulaiman): Hivyo ndio nyinyi
mnanisaidia kwa mali? Aliyo nipa Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kuliko aliyo
kupeni nyinyi. Lakini nyinyi mnafurahia hii zawadi yenu.
|
Ayah 27:37 الأية
ارْجِعْ إِلَيْهِمْ فَلَنَأْتِيَنَّهُم بِجُنُودٍ لَّا قِبَلَ لَهُم بِهَا
وَلَنُخْرِجَنَّهُم مِّنْهَا أَذِلَّةً وَهُمْ صَاغِرُونَ
Swahili
Rejea kwao! Kwa yakini sisi tutawajia kwa majeshi wasio yaweza kuyakabili. Na
hakika tutawatoa humo na hali wao wamekuwa madhalili na wanyonge.
|
Ayah 27:38 الأية
قَالَ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ أَيُّكُمْ يَأْتِينِي بِعَرْشِهَا قَبْلَ أَن
يَأْتُونِي مُسْلِمِينَ
Swahili
Akasema: Enyi wahishimiwa! Ni nani kati yenu atakaye niletea kiti chake cha enzi
kabla hawajanijia nao wamekwisha salimu amri.
|
Ayah 27:39 الأية
قَالَ عِفْرِيتٌ مِّنَ الْجِنِّ أَنَا آتِيكَ بِهِ قَبْلَ أَن تَقُومَ مِن
مَّقَامِكَ ۖ وَإِنِّي عَلَيْهِ لَقَوِيٌّ أَمِينٌ
Swahili
Akasema: Afriti, katika majini: Mimi nitakuletea kabla hujainuka pahala pako
hapo. Na mimi kwa hakika nina nguvu na muaminifu.
|
Ayah 27:40 الأية
قَالَ الَّذِي عِندَهُ عِلْمٌ مِّنَ الْكِتَابِ أَنَا آتِيكَ بِهِ قَبْلَ أَن
يَرْتَدَّ إِلَيْكَ طَرْفُكَ ۚ فَلَمَّا رَآهُ مُسْتَقِرًّا عِندَهُ قَالَ هَٰذَا
مِن فَضْلِ رَبِّي لِيَبْلُوَنِي أَأَشْكُرُ أَمْ أَكْفُرُ ۖ وَمَن شَكَرَ
فَإِنَّمَا يَشْكُرُ لِنَفْسِهِ ۖ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ رَبِّي غَنِيٌّ كَرِيمٌ
Swahili
Akasema mwenye ilimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako.
Basi alipo kiona kimewekwa mbele yake, akasema: Haya ni katika fadhila zake Mola
wangu Mlezi, ili anijaribu nitashukuru au nitakufuru. Na mwenye kushukuru, kwa
hakika, anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake; na anaye kufuru, kwa hakika Mola
wangu Mlezi ni Mkwasi na Karimu.
|
Ayah 27:41 الأية
قَالَ نَكِّرُوا لَهَا عَرْشَهَا نَنظُرْ أَتَهْتَدِي أَمْ تَكُونُ مِنَ الَّذِينَ
لَا يَهْتَدُونَ
Swahili
Akasema: Mgeuzieni kiti chake cha enzi hiki, tuone ataongoka, au atakuwa
miongoni mwa wasio ongoka.
|
Ayah 27:42 الأية
فَلَمَّا جَاءَتْ قِيلَ أَهَٰكَذَا عَرْشُكِ ۖ قَالَتْ كَأَنَّهُ هُوَ ۚ
وَأُوتِينَا الْعِلْمَ مِن قَبْلِهَا وَكُنَّا مُسْلِمِينَ
Swahili
Basi (Malkia) alipo fika akaambiwa: Je! Kiti chako cha enzi ni kama hiki?
Akasema: Kama kwamba ndicho hichi. (Sulaiman na watu wake wakasema): Na sisi
tumepewa ilimu kabla yake (Malkia), na tukawa Waislamu.
|
Ayah 27:43 الأية
وَصَدَّهَا مَا كَانَت تَّعْبُدُ مِن دُونِ اللَّهِ ۖ إِنَّهَا كَانَتْ مِن قَوْمٍ
كَافِرِينَ
Swahili
Na yale aliyo kuwa akiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu yalimzuilia. Hakika yeye
(Malkia) alikuwa katika kaumu ya makafiri.
|
Ayah 27:44 الأية
قِيلَ لَهَا ادْخُلِي الصَّرْحَ ۖ فَلَمَّا رَأَتْهُ حَسِبَتْهُ لُجَّةً وَكَشَفَتْ
عَن سَاقَيْهَا ۚ قَالَ إِنَّهُ صَرْحٌ مُّمَرَّدٌ مِّن قَوَارِيرَ ۗ قَالَتْ رَبِّ
إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي وَأَسْلَمْتُ مَعَ سُلَيْمَانَ لِلَّهِ رَبِّ
الْعَالَمِينَ
Swahili
Akaambiwa: Liingie behewa la hili jumba. Alipo liona alidhani ni maji, na
akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake. (Sulaiman) akasema: Hakika hilo ni
behewa lilio sakafiwa kwa viyoo! Akasema (Malkia): Mola wangu Mlezi! Mimi
nimejidhulumu nafsi yangu, na sasa nanyenyekea pamoja na Sulaiman kwa Mwenyezi
Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
|
Ayah 27:45 الأية
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا إِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ
فَإِذَا هُمْ فَرِيقَانِ يَخْتَصِمُونَ
Swahili
Na kwa kina Thamud tulimtuma ndugu yao Saleh kuwaambia: Muabuduni Mwenyezi
Mungu. Basi wakawa makundi mawili yanayo gombana.
|
Ayah 27:46 الأية
قَالَ يَا قَوْمِ لِمَ تَسْتَعْجِلُونَ بِالسَّيِّئَةِ قَبْلَ الْحَسَنَةِ ۖ
لَوْلَا تَسْتَغْفِرُونَ اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ
Swahili
Akasema: Enyi watu wangu! Kwa nini mnauhimiza uwovu kabla ya wema? Kwa nini
hamuombi msamaha kwa Mwenyezi Mungu ili mrehemewe?
|
Ayah 27:47 الأية
قَالُوا اطَّيَّرْنَا بِكَ وَبِمَن مَّعَكَ ۚ قَالَ طَائِرُكُمْ عِندَ اللَّهِ ۖ
بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ تُفْتَنُونَ
Swahili
Wakasema: Tuna kisirani nawe na wale walio pamoja nawe. Yeye akasema: Uaguzi wa
ukorofi wenu uko kwa Mwenyezi Mungu; lakini nyinyi ni watu mnao jaribiwa.
|
Ayah 27:48 الأية
وَكَانَ فِي الْمَدِينَةِ تِسْعَةُ رَهْطٍ يُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ وَلَا
يُصْلِحُونَ
Swahili
Na walikuwamo mjini watu tisa wakifanya ufisadi katika nchi wala hawafanyi la
maslaha.
|
Ayah 27:49 الأية
قَالُوا تَقَاسَمُوا بِاللَّهِ لَنُبَيِّتَنَّهُ وَأَهْلَهُ ثُمَّ لَنَقُولَنَّ
لِوَلِيِّهِ مَا شَهِدْنَا مَهْلِكَ أَهْلِهِ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ
Swahili
Wakasema: Apishaneni kwa Mwenyezi Mungu tutamshambulia usiku yeye na ahali zake;
kisha tutamwambia mrithi wake: Sisi hatukuona maangamizo ya watu wake, na sisi
bila ya shaka tunasema kweli.
|
Ayah 27:50 الأية
وَمَكَرُوا مَكْرًا وَمَكَرْنَا مَكْرًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ
Swahili
Basi wakapanga mipango yao, na Sisi tukapanga mipango yetu, na wao hawatambui.
|
Ayah 27:51 الأية
فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ مَكْرِهِمْ أَنَّا دَمَّرْنَاهُمْ وَقَوْمَهُمْ
أَجْمَعِينَ
Swahili
Basi angalia ulivyo kuwa mwisho wa mipango yao, ya kwamba tuliwaangamiza wao
pamoja na watu wao wote.
|
Ayah 27:52 الأية
فَتِلْكَ بُيُوتُهُمْ خَاوِيَةً بِمَا ظَلَمُوا ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً
لِّقَوْمٍ يَعْلَمُونَ
Swahili
Basi hizo nyumba zao ni tupu kwa sababu ya walivyo dhulumu. Hakika bila ya shaka
katika hayo ipo Ishara kwa watu wanao jua.
|
Ayah 27:53 الأية
وَأَنجَيْنَا الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ
Swahili
Na tukawaokoa wale walio amini na walio kuwa wanamchamngu.
|
Ayah 27:54 الأية
وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ وَأَنتُمْ تُبْصِرُونَ
Swahili
Na Lut'i alipo waambia watu wake: Je! Mnafanya uchafu nanyi mnaona?
|
Ayah 27:55 الأية
أَئِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الرِّجَالَ شَهْوَةً مِّن دُونِ النِّسَاءِ ۚ بَلْ أَنتُمْ
قَوْمٌ تَجْهَلُونَ
Swahili
Hivyo nyinyi mnawaingilia wanaume kwa matamanio badala ya wanawake? Hakika
nyinyi ni watu mnao fanya ujinga kabisa!
|
Ayah 27:56 الأية
فَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلَّا أَن قَالُوا أَخْرِجُوا آلَ لُوطٍ مِّن
قَرْيَتِكُمْ ۖ إِنَّهُمْ أُنَاسٌ يَتَطَهَّرُونَ
Swahili
Basi haikuwa jawabu ya watu wake ila ni kusema: Wafukuzeni wafwasi wa Lut'i
katika mji wenu. Hao ni watu wanao jitia usafi.
|
Ayah 27:57 الأية
فَأَنجَيْنَاهُ وَأَهْلَهُ إِلَّا امْرَأَتَهُ قَدَّرْنَاهَا مِنَ الْغَابِرِينَ
Swahili
Basi tukamwokoa yeye na ahali zake, isipo kuwa mkewe; tukamkadiria katika walio
baki nyuma.
|
Ayah 27:58 الأية
وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا ۖ فَسَاءَ مَطَرُ الْمُنذَرِينَ
Swahili
Na tukawanyeshea mvua. Ni ovu kweli kweli hiyo mvua ya walio kwisha onywa.
|
Ayah 27:59 الأية
قُلِ الْحَمْدُ لِلَّهِ وَسَلَامٌ عَلَىٰ عِبَادِهِ الَّذِينَ اصْطَفَىٰ ۗ آللَّهُ
خَيْرٌ أَمَّا يُشْرِكُونَ
Swahili
Sema: Alhamdu Lillahi! Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu! Na amani ishuke juu ya
waja wake alio wateuwa. Je! Mwenyezi Mungu ni bora, au wale wanao washirikisha
naye?
|
Ayah 27:60 الأية
أَمَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ السَّمَاءِ مَاءً
فَأَنبَتْنَا بِهِ حَدَائِقَ ذَاتَ بَهْجَةٍ مَّا كَانَ لَكُمْ أَن تُنبِتُوا
شَجَرَهَا ۗ أَإِلَٰهٌ مَّعَ اللَّهِ ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ يَعْدِلُونَ
Swahili
AU NANI yule aliye ziumba mbingu na ardhi, na akakuteremshieni maji kutoka
mbinguni, na kwa hayo tukaziotesha bustani zenye kupendeza? Nyinyi hamna uwezo
wa kuiotesha miti yake. Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali hao ni
watu walio potoka.
|
Ayah 27:61 الأية
أَمَّن جَعَلَ الْأَرْضَ قَرَارًا وَجَعَلَ خِلَالَهَا أَنْهَارًا وَجَعَلَ لَهَا
رَوَاسِيَ وَجَعَلَ بَيْنَ الْبَحْرَيْنِ حَاجِزًا ۗ أَإِلَٰهٌ مَّعَ اللَّهِ ۚ
بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
Swahili
Au nani yule aliye ifanya ardhi mahali pa kutua, na akajaalia ndani yake mito,
na akaweka milima? Na akaweka baina ya bahari mbili kiziwizi? Je! Yupo mungu
pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali wengi wao hawajui.
|
Ayah 27:62 الأية
أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ وَيَجْعَلُكُمْ
خُلَفَاءَ الْأَرْضِ ۗ أَإِلَٰهٌ مَّعَ اللَّهِ ۚ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ
Swahili
Au nani yule anaye mjibu mwenye shida pale anapo mwomba, na akaiondoa dhiki, na
akakufanyeni warithi wa ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni
machache mnayo yazingatia.
|
Ayah 27:63 الأية
أَمَّن يَهْدِيكُمْ فِي ظُلُمَاتِ الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَمَن يُرْسِلُ الرِّيَاحَ
بُشْرًا بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ ۗ أَإِلَٰهٌ مَّعَ اللَّهِ ۚ تَعَالَى اللَّهُ
عَمَّا يُشْرِكُونَ
Swahili
Au nani yule anaye kuongoeni katika giza la bara na bahari, na akazipeleka pepo
kuleta bishara kabla ya rehema zake? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu?
Ametukuka Mwenyezi Mungu juu ya wanao washirikisha naye.
|
Ayah 27:64 الأية
أَمَّن يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَمَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ
وَالْأَرْضِ ۗ أَإِلَٰهٌ مَّعَ اللَّهِ ۚ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِن كُنتُمْ
صَادِقِينَ
Swahili
Au nani anaye uanzisha uumbaji, kisha akaurejesha? Na nani anaye kuruzukuni
kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema:
Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli.
|
Ayah 27:65 الأية
قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّهُ ۚ
وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ
Swahili
Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipo kuwa Mwenyezi Mungu.
Wala wao hawajui lini watafufuliwa.
|
Ayah 27:66 الأية
بَلِ ادَّارَكَ عِلْمُهُمْ فِي الْآخِرَةِ ۚ بَلْ هُمْ فِي شَكٍّ مِّنْهَا ۖ بَلْ
هُم مِّنْهَا عَمُونَ
Swahili
Kwani huo ujuzi wao umefikilia kuijua Akhera? Bali wao wamo katika shaka nayo
tu, bali wao ni vipofu nayo.
|
Ayah 27:67 الأية
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَإِذَا كُنَّا تُرَابًا وَآبَاؤُنَا أَئِنَّا
لَمُخْرَجُونَ
Swahili
Na wakasema walio kufuru: Tutapo kuwa mchanga, sisi na baba zetu, hivyo kweli
tutakuja tolewa?
|
Ayah 27:68 الأية
لَقَدْ وُعِدْنَا هَٰذَا نَحْنُ وَآبَاؤُنَا مِن قَبْلُ إِنْ هَٰذَا إِلَّا
أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ
Swahili
Haya haya tuliahidiwa sisi na baba zetu zamani. Hayakuwa haya ila ni hadithi za
uwongo za watu wa kale.
|
Ayah 27:69 الأية
قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُجْرِمِينَ
Swahili
Sema: Nendeni katika ardhi, na tazameni ulikuwaje mwisho wa wakosefu.
|
Ayah 27:70 الأية
وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَلَا تَكُن فِي ضَيْقٍ مِّمَّا يَمْكُرُونَ
Swahili
Wala usiwahuzunukie wala usiwe katika dhiki kwa sababu ya hila zao wanazo
zifanya.
|
Ayah 27:71 الأية
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ
Swahili
Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa mnasema kweli?
|
Ayah 27:72 الأية
قُلْ عَسَىٰ أَن يَكُونَ رَدِفَ لَكُم بَعْضُ الَّذِي تَسْتَعْجِلُونَ
Swahili
Sema: Asaa ni karibu kukufikieni sehemu ya yale mnayo yahimiza.
|
Ayah 27:73 الأية
وَإِنَّ رَبَّكَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا
يَشْكُرُونَ
Swahili
Na hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye fadhila kwa watu, lakini wengi wao
hawashukuru.
|
Ayah 27:74 الأية
وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَعْلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمْ وَمَا يُعْلِنُونَ
Swahili
Na hakika Mola wako Mlezi anayajua yanayo ficha vifua vyao na wanayo yatangaza.
|
Ayah 27:75 الأية
وَمَا مِنْ غَائِبَةٍ فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ
Swahili
Na hakuna siri katika mbingu na ardhi ila imo katika Kitabu kinacho bainisha.
|
Ayah 27:76 الأية
إِنَّ هَٰذَا الْقُرْآنَ يَقُصُّ عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَكْثَرَ الَّذِي هُمْ
فِيهِ يَخْتَلِفُونَ
Swahili
Hakika Qur'ani hii inawasimulia Wana wa Israili mengi wanayo khitalifiana nayo.
|
Ayah 27:77 الأية
وَإِنَّهُ لَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ
Swahili
Nayo hakika ni Uwongofu na Rehema kwa Waumini.
|
Ayah 27:78 الأية
إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُم بِحُكْمِهِ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْعَلِيمُ
Swahili
Hakika Mola wako Mlezi atawahukumu kwa hukumu yake, naye ni Mwenye nguvu Mjuzi.
|
Ayah 27:79 الأية
فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ ۖ إِنَّكَ عَلَى الْحَقِّ الْمُبِينِ
Swahili
Basi mtegemee Mweneyezi Mungu; hakika wewe uko juu ya Haki iliyo wazi.
|
Ayah 27:80 الأية
إِنَّكَ لَا تُسْمِعُ الْمَوْتَىٰ وَلَا تُسْمِعُ الصُّمَّ الدُّعَاءَ إِذَا
وَلَّوْا مُدْبِرِينَ
Swahili
Kwa hakika wewe huwezi kuwafanya maiti wasikie, wala kuwafanya viziwi wasikie
wito, wanapo kwisha geuka kwenda zao.
|
Ayah 27:81 الأية
وَمَا أَنتَ بِهَادِي الْعُمْيِ عَن ضَلَالَتِهِمْ ۖ إِن تُسْمِعُ إِلَّا مَن
يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا فَهُم مُّسْلِمُونَ
Swahili
Wala huwezi kuwaongoa vipofu waache upotovu wao. Huwezi kuwafanya wasikie isipo
kuwa wenye kuziamini Ishara zetu; na hao ndio wat'iifu.
|
Ayah 27:82 الأية
وَإِذَا وَقَعَ الْقَوْلُ عَلَيْهِمْ أَخْرَجْنَا لَهُمْ دَابَّةً مِّنَ الْأَرْضِ
تُكَلِّمُهُمْ أَنَّ النَّاسَ كَانُوا بِآيَاتِنَا لَا يُوقِنُونَ
Swahili
Na itapo waangukia kauli juu yao, tutawatolea mnyama katika ardhi atakaye
wasemeza, ya kuwa watu walikuwa hawana na yakini na Ishara zetu.
|
Ayah 27:83 الأية
وَيَوْمَ نَحْشُرُ مِن كُلِّ أُمَّةٍ فَوْجًا مِّمَّن يُكَذِّبُ بِآيَاتِنَا فَهُمْ
يُوزَعُونَ
Swahili
Na Siku tutapo kusanya kutoka kila umma kundi katika wanao kadhibisha Ishara
zetu, nao watagawanywa mafungu mafungu.
|
Ayah 27:84 الأية
حَتَّىٰ إِذَا جَاءُوا قَالَ أَكَذَّبْتُم بِآيَاتِي وَلَمْ تُحِيطُوا بِهَا
عِلْمًا أَمَّاذَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Swahili
Hata watakapo fika, atasema (Mwenyezi Mungu): Je! Nyinyi si mlizikanusha Ishara
zangu pasipo kuzijua vyema? Au mlikuwa mkifanya nini?
|
Ayah 27:85 الأية
وَوَقَعَ الْقَوْلُ عَلَيْهِم بِمَا ظَلَمُوا فَهُمْ لَا يَنطِقُونَ
Swahili
Na kauli itawaangukia juu yao kwa vile walivyo dhulumu. Basi hao hawatasema
lolote.
|
Ayah 27:86 الأية
أَلَمْ يَرَوْا أَنَّا جَعَلْنَا اللَّيْلَ لِيَسْكُنُوا فِيهِ وَالنَّهَارَ
مُبْصِرًا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ
Swahili
Je! Hawaoni kwamba sisi tumeufanya usiku ili watulie, na mchana wa kuangaza.
Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanao amini.
|
Ayah 27:87 الأية
وَيَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَفَزِعَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ
إِلَّا مَن شَاءَ اللَّهُ ۚ وَكُلٌّ أَتَوْهُ دَاخِرِينَ
Swahili
Na Siku litapo pulizwa baragumu, watahangaika waliomo mbinguni na katika ardhi,
ila amtakaye Mwenyezi Mungu. Na wote watamfikia nao ni wanyonge.
|
Ayah 27:88 الأية
وَتَرَى الْجِبَالَ تَحْسَبُهَا جَامِدَةً وَهِيَ تَمُرُّ مَرَّ السَّحَابِ ۚ
صُنْعَ اللَّهِ الَّذِي أَتْقَنَ كُلَّ شَيْءٍ ۚ إِنَّهُ خَبِيرٌ بِمَا تَفْعَلُونَ
Swahili
Na unaiona milima unaidhunia imetulia; nayo inakwenda kama mwendo wa mawingu.
Huo ndio ufundi wa Mwenyezi Mungu aliye tengeneza vilivyo kila kitu. Hakika Yeye
anazo khabari za yote myatendayo.
|
Ayah 27:89 الأية
مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ خَيْرٌ مِّنْهَا وَهُم مِّن فَزَعٍ يَوْمَئِذٍ
آمِنُونَ
Swahili
Watakao kuja na mema, watapata bora kuliko hayo. Nao watasalimika na mahangaiko
ya Siku hiyo.
|
Ayah 27:90 الأية
وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَكُبَّتْ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ هَلْ تُجْزَوْنَ
إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Swahili
Na watakao kuja na uovu, basi zitasunukishwa nyuso zao Motoni. Je! Kwani
mnalipwa isipo kuwa mliyo kuwa mkiyatenda?
|
Ayah 27:91 الأية
إِنَّمَا أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ رَبَّ هَٰذِهِ الْبَلْدَةِ الَّذِي حَرَّمَهَا
وَلَهُ كُلُّ شَيْءٍ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُسْلِمِينَ
Swahili
Ama mimi nimeamrishwa nimuabudu Mola Mlezi wa mji huu aliye ufanya ni mtakatifu;
na ni vyake Yeye tu vitu vyote. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu,
wenye kunyenyekea.
|
Ayah 27:92 الأية
وَأَنْ أَتْلُوَ الْقُرْآنَ ۖ فَمَنِ اهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِي لِنَفْسِهِ ۖ
وَمَن ضَلَّ فَقُلْ إِنَّمَا أَنَا مِنَ الْمُنذِرِينَ
Swahili
Na niisome Qur'ani. Na mwenye kuongoka, basi ameongoka kwa faida ya nafsi yake;
na aliye potea - basi sema: Hakika mimi ni miongoni mwa waonyaji.
|
Ayah 27:93 الأية
وَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّهِ سَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ فَتَعْرِفُونَهَا ۚ وَمَا رَبُّكَ
بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ
Swahili
Na sema: Alhamdu Lillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu. Yeye
atakuonyesheni Ishara zake, na mtazijua. Na Mola wako Mlezi si mwenye
kughafilika na myatendayo.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|