Na walio amini, na wakatenda mema, na wakaamini aliyo teremshiwa Muhammad - nayo
ni Haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi - atawafutia makosa yao na ataitengeneza
hali yao.
Hayo ni kwa sababu walio kufuru wamefuata upotovu, na walio amini wamefuata Haki
iliyo toka kwa Mola wao Mlezi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo wapigia watu
mifano yao.
Basi mnapo wakuta walio kufuru wapigeni shingoni mwao, mpaka mkiwadhoofisha
wafungeni pingu. Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe, mpaka vita vipoe.
Ndio hivyo. Na lau angeli taka Mwenyezi Mungu angeli washinda mwenyewe, lakini
haya ni kwa sababu akutieni mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na walio uliwa katika
njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza a'mali zao.
Kwani hawakutembea katika ardhi wakaona ulikuwaje mwisho wa walio kuwa kabla
yao? Mwenyezi Mungu aliwaangamiza, na kwa makafiri hawa itakuwa mfano wa hayo.
Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza walio amini na wakatenda mema katika Bustani
zipitiwazo na mito kati yake. Na walio kufuru hujifurahisha na hula kama walavyo
wanyama, na Moto ndio makaazi yao.
Mfano wa Pepo walio ahidiwa wachamngu ina mito ya maji yasiyo vunda, na mito ya
maziwa isiyo haribika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na
mito ya asali iliyo safishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda, na
maghfira kutoka kwa Mola wao Mlezi. Basi hao ni kama watakao dumu Motoni na
wakinyweshwa maji yanayo chemka ya kuwakata matumbo yao?
Na wapo miongoni mwao wanao kusikiliza, mpaka wakiondoka kwako huwauliza walio
pewa ilimu: Amesema nini sasa hivi? Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amepiga muhuri
juu ya nyoyo zao, na wakafuata pumbao lao.
Kwani wanangojea jengine isipo kuwa iwafikie Saa (ya Kiyama) kwa ghafla? Na
hakika alama zake zimekwisha kuja. Na itapo wajia kutawafaa wapi kukumbuka hapo?
Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi
zako na za Waumini wanaume na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua mahali
penu pa kwenda na kurudi, na mahali penu pa kukaa.
Na Waumini wanasema: Kwa nini haiteremshwi Sura? Na inapo teremshwa Sura
madhubuti na ikatajwa ndani yake khabari ya vita, utawaona wenye maradhi katika
nyoyo zao wanakutazama mtazamo wa anaye zimia kwa mauti. Basi ni bora kwao
Na tungeli penda tungeli kuonyesha hao na ungeli watambua kwa alama zao; lakini
bila ya shaka utawajua kwa namna ya msemo wao. Na Mwenyezi Mungu anavijua
vitendo vyenu.
Kwa hakika walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu na wakapinzana na
Mtume baada ya kwisha wabainikia uwongofu, hao hawatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa
lolote. Naye ataviangusha vitendo vyao.
Angalieni! Nyinyi mnaitwa mtumie katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wapo katika
nyinyi wanao fanya ubakhili. Na anaye fanya ubakhili basi anajifanyia ubakhili
mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu si mhitaji, na nyinyi ndio wahitaji. Na mkigeuka
atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.