First Ayah 1 الأية الأوليبِسْم ِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
ق ۚ وَالْقُرْآنِ الْمَجِيدِ
Swahili
Qaaf. Naapa kwa Qur'ani tukufu!
|
Ayah 50:2 الأية
بَلْ عَجِبُوا أَن جَاءَهُم مُّنذِرٌ مِّنْهُمْ فَقَالَ الْكَافِرُونَ هَٰذَا
شَيْءٌ عَجِيبٌ
Swahili
Bali wanastaajabu kwamba amewafikia mwonyaji kutoka miongoni mwao, na wakasema
makafiri: Hili ni jambo la ajabu!
|
Ayah 50:3 الأية
أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا ۖ ذَٰلِكَ رَجْعٌ بَعِيدٌ
Swahili
Ati tukifa na tukawa udongo...? Kurejea huko kuko mbali!
|
Ayah 50:4 الأية
قَدْ عَلِمْنَا مَا تَنقُصُ الْأَرْضُ مِنْهُمْ ۖ وَعِندَنَا كِتَابٌ حَفِيظٌ
Swahili
Hakika Sisi tunajua kiasi cha kila kinacho punguzwa na ardhi kutokana nao. Na
kwetu kipo Kitabu kinacho hifadhi yote.
|
Ayah 50:5 الأية
بَلْ كَذَّبُوا بِالْحَقِّ لَمَّا جَاءَهُمْ فَهُمْ فِي أَمْرٍ مَّرِيجٍ
Swahili
Lakini waliikanusha Haki ilipo wajia; kwa hivyo wamo katika mambo ya mkorogo.
|
Ayah 50:6 الأية
أَفَلَمْ يَنظُرُوا إِلَى السَّمَاءِ فَوْقَهُمْ كَيْفَ بَنَيْنَاهَا
وَزَيَّنَّاهَا وَمَا لَهَا مِن فُرُوجٍ
Swahili
Je! Hawaangalii mbingu zilizo juu yao! Vipi tulivyo zijenga, na tukazipamba.
Wala hazina nyufa.
|
Ayah 50:7 الأية
وَالْأَرْضَ مَدَدْنَاهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنبَتْنَا فِيهَا مِن
كُلِّ زَوْجٍ بَهِيجٍ
Swahili
Na ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea mizuri ya kila
namna.
|
Ayah 50:8 الأية
تَبْصِرَةً وَذِكْرَىٰ لِكُلِّ عَبْدٍ مُّنِيبٍ
Swahili
Yawe haya ni kifumbua macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kuelekea.
|
Ayah 50:9 الأية
وَنَزَّلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً مُّبَارَكًا فَأَنبَتْنَا بِهِ جَنَّاتٍ
وَحَبَّ الْحَصِيدِ
Swahili
Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji yaliyo barikiwa, na kwa hayo tukaotesha
mabustani na nafaka za kuvunwa.
|
Ayah 50:10 الأية
وَالنَّخْلَ بَاسِقَاتٍ لَّهَا طَلْعٌ نَّضِيدٌ
Swahili
Na mitende mirefu yenye makole yaliyo zaa kwa wingi,
|
Ayah 50:11 الأية
رِّزْقًا لِّلْعِبَادِ ۖ وَأَحْيَيْنَا بِهِ بَلْدَةً مَّيْتًا ۚ كَذَٰلِكَ
الْخُرُوجُ
Swahili
Ili iwe ni riziki kwa waja wangu. Na tukaifufua kwa maji nchi iliyo kuwa
imekufa. Kama hivyo ndivyo utakavyo kuwa ufufuaji.
|
Ayah 50:12 الأية
كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَأَصْحَابُ الرَّسِّ وَثَمُودُ
Swahili
Kabla yao walikadhibisha kaumu ya Nuhu na wakaazi wa Rassi na Thamudi.
|
Ayah 50:13 الأية
وَعَادٌ وَفِرْعَوْنُ وَإِخْوَانُ لُوطٍ
Swahili
Na A'di na Firauni na kaumu ya Lut'i.
|
Ayah 50:14 الأية
وَأَصْحَابُ الْأَيْكَةِ وَقَوْمُ تُبَّعٍ ۚ كُلٌّ كَذَّبَ الرُّسُلَ فَحَقَّ
وَعِيدِ
Swahili
Na wakaazi wa Machakani, na watu wa Tubbaa'. Wote hao waliwakanusha Mitume, kwa
hivyo onyo likathibitika juu yao.
|
Ayah 50:15 الأية
أَفَعَيِينَا بِالْخَلْقِ الْأَوَّلِ ۚ بَلْ هُمْ فِي لَبْسٍ مِّنْ خَلْقٍ جَدِيدٍ
Swahili
Kwani tulichoka kwa kuumba mara ya kwanza. Bali wao wamo katika shaka tu juu ya
umbo jipya.
|
Ayah 50:16 الأية
وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ وَنَعْلَمُ مَا تُوَسْوِسُ بِهِ نَفْسُهُ ۖ
وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنْ حَبْلِ الْوَرِيدِ
Swahili
Na hakika tumemuumba mtu, nasi tunayajua yanayo mpitikia katika nafsi yake. Na
Sisi tuko karibu naye kuliko mshipa wa shingoni mwake.
|
Ayah 50:17 الأية
إِذْ يَتَلَقَّى الْمُتَلَقِّيَانِ عَنِ الْيَمِينِ وَعَنِ الشِّمَالِ قَعِيدٌ
Swahili
Wanapo pokea wapokeaji wawili, wanao kaa kuliani na kushotoni.
|
Ayah 50:18 الأية
مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ
Swahili
Hatamki neno ila karibu yake yupo mwangalizi tayari.
|
Ayah 50:19 الأية
وَجَاءَتْ سَكْرَةُ الْمَوْتِ بِالْحَقِّ ۖ ذَٰلِكَ مَا كُنتَ مِنْهُ تَحِيدُ
Swahili
Na uchungu wa kutoka roho utamjia kwa haki. Hayo ndiyo uliyo kuwa ukiyakimbia.
|
Ayah 50:20 الأية
وَنُفِخَ فِي الصُّورِ ۚ ذَٰلِكَ يَوْمُ الْوَعِيدِ
Swahili
Na litapulizwa baragumu. Hiyo ndiyo Siku ya Miadi.
|
Ayah 50:21 الأية
وَجَاءَتْ كُلُّ نَفْسٍ مَّعَهَا سَائِقٌ وَشَهِيدٌ
Swahili
Na kila nafsi itakuja na pamoja nayo mchungaji na shahidi.
|
Ayah 50:22 الأية
لَّقَدْ كُنتَ فِي غَفْلَةٍ مِّنْ هَٰذَا فَكَشَفْنَا عَنكَ غِطَاءَكَ فَبَصَرُكَ
الْيَوْمَ حَدِيدٌ
Swahili
(Aambiwe): Kwa hakika ulikuwa umeghafilika na haya; basi leo tumekuondolea pazia
lako, na kwa hivyo kuona kwako leo ni kukali.
|
Ayah 50:23 الأية
وَقَالَ قَرِينُهُ هَٰذَا مَا لَدَيَّ عَتِيدٌ
Swahili
Na mwenzake atasema: Huyu niliye naye mimi kesha tayarishwa.
|
Ayah 50:24 الأية
أَلْقِيَا فِي جَهَنَّمَ كُلَّ كَفَّارٍ عَنِيدٍ
Swahili
Mtupeni katika Jahannamu kila kafiri mwenye inda,
|
Ayah 50:25 الأية
مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ مُّرِيبٍ
Swahili
Akatazaye kheri, arukaye mipaka, mwenye kutia shaka,
|
Ayah 50:26 الأية
الَّذِي جَعَلَ مَعَ اللَّهِ إِلَٰهًا آخَرَ فَأَلْقِيَاهُ فِي الْعَذَابِ
الشَّدِيدِ
Swahili
Aliye weka mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi mtupeni katika adhabu
kali.
|
Ayah 50:27 الأية
قَالَ قَرِينُهُ رَبَّنَا مَا أَطْغَيْتُهُ وَلَٰكِن كَانَ فِي ضَلَالٍ بَعِيدٍ
Swahili
Mwenzake aseme: Ee Mola wetu Mlezi! Sikumpoteza mimi, bali yeye mwenyewe alikuwa
katika upotovu wa mbali.
|
Ayah 50:28 الأية
قَالَ لَا تَخْتَصِمُوا لَدَيَّ وَقَدْ قَدَّمْتُ إِلَيْكُم بِالْوَعِيدِ
Swahili
(Mwenyezi Mungu) aseme: Msigombane mbele yangu. Nilikuleteeni mbele onyo langu.
|
Ayah 50:29 الأية
مَا يُبَدَّلُ الْقَوْلُ لَدَيَّ وَمَا أَنَا بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ
Swahili
Mbele yangu haibadilishwi kauli, wala Mimi siwadhulumu waja wangu.
|
Ayah 50:30 الأية
يَوْمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ امْتَلَأْتِ وَتَقُولُ هَلْ مِن مَّزِيدٍ
Swahili
Siku tutapo iambia Jahannamu: Je! Umejaa? Nayo itasema: Je! Kuna ziada?
|
Ayah 50:31 الأية
وَأُزْلِفَتِ الْجَنَّةُ لِلْمُتَّقِينَ غَيْرَ بَعِيدٍ
Swahili
Na Pepo italetwa karibu kwa ajili ya wachamngu, haitakuwa mbali.
|
Ayah 50:32 الأية
هَٰذَا مَا تُوعَدُونَ لِكُلِّ أَوَّابٍ حَفِيظٍ
Swahili
Haya ndiyo mnayo ahidiwa kwa kila mwenye kurejea kwa Mwenyezi Mungu na
akajilinda.
|
Ayah 50:33 الأية
مَّنْ خَشِيَ الرَّحْمَٰنَ بِالْغَيْبِ وَجَاءَ بِقَلْبٍ مُّنِيبٍ
Swahili
Mwenye kumwogopa Mwingi wa Rehema hali kuwa hamwoni, na akaja kwa moyo ulio
elekea-
|
Ayah 50:34 الأية
ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ ۖ ذَٰلِكَ يَوْمُ الْخُلُودِ
Swahili
(Ataambiwa) ingieni kwa salama. Hiyo ndiyo siku ya daima dawamu.
|
Ayah 50:35 الأية
لَهُم مَّا يَشَاءُونَ فِيهَا وَلَدَيْنَا مَزِيدٌ
Swahili
Humo watapata wakitakacho, na kwetu yako ya ziada.
|
Ayah 50:36 الأية
وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّن قَرْنٍ هُمْ أَشَدُّ مِنْهُم بَطْشًا
فَنَقَّبُوا فِي الْبِلَادِ هَلْ مِن مَّحِيصٍ
Swahili
Na kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao walio kuwa na nguvu zaidi kuliko hawa!
Nao walitanga tanga katika nchi nyingi. Je! Walipata pa kukimbilia?
|
Ayah 50:37 الأية
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَذِكْرَىٰ لِمَن كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ
وَهُوَ شَهِيدٌ
Swahili
Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo
anashuhudia.
|
Ayah 50:38 الأية
وَلَقَدْ خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ
أَيَّامٍ وَمَا مَسَّنَا مِن لُّغُوبٍ
Swahili
Na bila ya shaka Sisi tumeziumba mbingu na ardhi na vilio baina yao mnamo siku
sita; na wala hayakutugusa machofu.
|
Ayah 50:39 الأية
فَاصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ قَبْلَ طُلُوعِ
الشَّمْسِ وَقَبْلَ الْغُرُوبِ
Swahili
Basi vumilia kwa hayo wasemayo, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi kabla ya
kuchomoza jua na kabla ya kuchwa.
|
Ayah 50:40 الأية
وَمِنَ اللَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَأَدْبَارَ السُّجُودِ
Swahili
Na katika usiku pia mtakase, na baada ya kusujudu.
|
Ayah 50:41 الأية
وَاسْتَمِعْ يَوْمَ يُنَادِ الْمُنَادِ مِن مَّكَانٍ قَرِيبٍ
Swahili
Na sikiliza siku atapo nadi mwenye kunadi kutoka pahala karibu.
|
Ayah 50:42 الأية
يَوْمَ يَسْمَعُونَ الصَّيْحَةَ بِالْحَقِّ ۚ ذَٰلِكَ يَوْمُ الْخُرُوجِ
Swahili
Siku watakapo sikia ukelele wa haki. Hiyo ndiyo siku ya kufufuka.
|
Ayah 50:43 الأية
إِنَّا نَحْنُ نُحْيِي وَنُمِيتُ وَإِلَيْنَا الْمَصِيرُ
Swahili
Hakika Sisi tunahuisha na tunafisha, na kwetu Sisi ndio marejeo.
|
Ayah 50:44 الأية
يَوْمَ تَشَقَّقُ الْأَرْضُ عَنْهُمْ سِرَاعًا ۚ ذَٰلِكَ حَشْرٌ عَلَيْنَا يَسِيرٌ
Swahili
Siku itapo wapasukia ardhi mbio mbio! Mkusanyo huo kwetu ni mwepesi.
|
Ayah 50:45 الأية
نَّحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَقُولُونَ ۖ وَمَا أَنتَ عَلَيْهِم بِجَبَّارٍ ۖ فَذَكِّرْ
بِالْقُرْآنِ مَن يَخَافُ وَعِيدِ
Swahili
Sisi tunajua kabisa wayasemayo. Wala wewe si mwenye kuwatawalia kwa ujabari.
Basi mkumbushe kwa Qur'ani anaye liogopa onyo.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|