First Ayah 1 الأية الأوليبِسْم ِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
تَبَارَكَ الَّذِي بِيَدِهِ الْمُلْكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ
Swahili
AMETUKUKA ambaye mkononi mwake umo Ufalme wote; na Yeye ni Mwenye uweza juu ya
kila kitu.
|
Ayah 67:2 الأية
الَّذِي خَلَقَ الْمَوْتَ وَالْحَيَاةَ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا
ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْغَفُورُ
Swahili
Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye
vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha.
|
Ayah 67:3 الأية
الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا ۖ مَّا تَرَىٰ فِي خَلْقِ الرَّحْمَٰنِ
مِن تَفَاوُتٍ ۖ فَارْجِعِ الْبَصَرَ هَلْ تَرَىٰ مِن فُطُورٍ
Swahili
Aliye umba mbingu saba kwa matabaka. Huoni tafauti yoyote katika uumbaji wa
Mwingi wa Rehema. Hebu rudisha nadhari! Unaona kosa lolote?
|
Ayah 67:4 الأية
ثُمَّ ارْجِعِ الْبَصَرَ كَرَّتَيْنِ يَنقَلِبْ إِلَيْكَ الْبَصَرُ خَاسِئًا وَهُوَ
حَسِيرٌ
Swahili
Tena rudisha nadhari mara mbili, nadhari yako itakurejea mwenyewe hali ya kuwa
imehizika nayo imechoka.
|
Ayah 67:5 الأية
وَلَقَدْ زَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِمَصَابِيحَ وَجَعَلْنَاهَا رُجُومًا
لِّلشَّيَاطِينِ ۖ وَأَعْتَدْنَا لَهُمْ عَذَابَ السَّعِيرِ
Swahili
Na kwa hakika tumeipamba mbingu ya karibu kwa mataa, na tumeyafanya ili
kuwapigia mashetani, na tumewaandalia adhabu ya Moto uwakao kwa nguvu.
|
Ayah 67:6 الأية
وَلِلَّذِينَ كَفَرُوا بِرَبِّهِمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ
Swahili
Na kwa walio mkufuru Mola wao Mlezi ipo adhabu ya Jahannamu. Na ni marejeo maovu
yalioje hayo!
|
Ayah 67:7 الأية
إِذَا أُلْقُوا فِيهَا سَمِعُوا لَهَا شَهِيقًا وَهِيَ تَفُورُ
Swahili
Watakapo tupwa humo watausikia mngurumo wake na huku inafoka.
|
Ayah 67:8 الأية
تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ الْغَيْظِ ۖ كُلَّمَا أُلْقِيَ فِيهَا فَوْجٌ سَأَلَهُمْ
خَزَنَتُهَا أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَذِيرٌ
Swahili
Inakaribia kupasuka kwa hasira. Kila mara likitupwa kundi humo walinzi wake
huwauliza: Kwani hakukujieni mwonyaji?
|
Ayah 67:9 الأية
قَالُوا بَلَىٰ قَدْ جَاءَنَا نَذِيرٌ فَكَذَّبْنَا وَقُلْنَا مَا نَزَّلَ اللَّهُ
مِن شَيْءٍ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا فِي ضَلَالٍ كَبِيرٍ
Swahili
Watasema: Kwani! Ametujia mwonyaji, lakini tulimkadhibisha, na tukasema:
Mwenyezi Mungu hakuteremsha chochote. Nyinyi hamumo ila katika upotovu mkubwa!
|
Ayah 67:10 الأية
وَقَالُوا لَوْ كُنَّا نَسْمَعُ أَوْ نَعْقِلُ مَا كُنَّا فِي أَصْحَابِ السَّعِيرِ
Swahili
Na watasema: Lau kuwa tungeli sikia, au tungeli kuwa na akili, tusingeli kuwa
katika watu wa Motoni!
|
Ayah 67:11 الأية
فَاعْتَرَفُوا بِذَنبِهِمْ فَسُحْقًا لِّأَصْحَابِ السَّعِيرِ
Swahili
Wakakiri dhambi zao. Basi kuangamia ni kwa watu wa Motoni!
|
Ayah 67:12 الأية
إِنَّ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِالْغَيْبِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ
كَبِيرٌ
Swahili
Hakika wanao mwogopa Mola wao Mlezi kwa ghaibu, watapata maghfira na ujira
mkubwa.
|
Ayah 67:13 الأية
وَأَسِرُّوا قَوْلَكُمْ أَوِ اجْهَرُوا بِهِ ۖ إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ
Swahili
Na ficheni kauli zenu, au zitangazeni; hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani.
|
Ayah 67:14 الأية
أَلَا يَعْلَمُ مَنْ خَلَقَ وَهُوَ اللَّطِيفُ الْخَبِيرُ
Swahili
Asijue aliye umba, naye ndiye Mjua siri, Mwenye khabari?
|
Ayah 67:15 الأية
هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ ذَلُولًا فَامْشُوا فِي مَنَاكِبِهَا
وَكُلُوا مِن رِّزْقِهِ ۖ وَإِلَيْهِ النُّشُورُ
Swahili
Yeye ndiye aliye idhalilisha ardhi kwa faida yenu, basi tembeeni katika pande
zake, na kuleni katika riziki zake. Na kwake Yeye ndio kufufuliwa.
|
Ayah 67:16 الأية
أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ
تَمُورُ
Swahili
Mnadhani mko salama kwa alioko juu kuwa hatakudidimizeni kwenye ardhi, na
tahamaki hiyo inatikisika!
|
Ayah 67:17 الأية
أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ
فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ
Swahili
Au mnadhani mko salama kwa alioko juu ya kuwa Yeye hakupelekeeni kimbunga chenye
changarawe? Mtajua vipi maonyo yangu?
|
Ayah 67:18 الأية
وَلَقَدْ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ
Swahili
Na bila ya shaka walikwisha kanusha walio kuwa kabla yao; basi kulikuwaje
kukasirika kwangu?
|
Ayah 67:19 الأية
أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَى الطَّيْرِ فَوْقَهُمْ صَافَّاتٍ وَيَقْبِضْنَ ۚ مَا
يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا الرَّحْمَٰنُ ۚ إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ بَصِيرٌ
Swahili
Kwani hawawaoni ndege walioko juu yao namna wanavyo zikunjua mbawa zao, na
kuzikunja? Hawawashikilii ila Mwingi wa rehema. Hakika Yeye ni Mwenye kuona kila
kitu.
|
Ayah 67:20 الأية
أَمَّنْ هَٰذَا الَّذِي هُوَ جُندٌ لَّكُمْ يَنصُرُكُم مِّن دُونِ الرَّحْمَٰنِ ۚ
إِنِ الْكَافِرُونَ إِلَّا فِي غُرُورٍ
Swahili
Au ni lipi hilo jeshi lenu la kukunusuruni badala ya Mwingi wa Rehema? Hakika
makafiri hawamo ila katika udanganyifu.
|
Ayah 67:21 الأية
أَمَّنْ هَٰذَا الَّذِي يَرْزُقُكُمْ إِنْ أَمْسَكَ رِزْقَهُ ۚ بَل لَّجُّوا فِي
عُتُوٍّ وَنُفُورٍ
Swahili
Au ni nani huyo ambaye atakupeni riziki kama Yeye akizuia riziki yake? Bali wao
wanakakamia tu katika jeuri na chuki.
|
Ayah 67:22 الأية
أَفَمَن يَمْشِي مُكِبًّا عَلَىٰ وَجْهِهِ أَهْدَىٰ أَمَّن يَمْشِي سَوِيًّا عَلَىٰ
صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ
Swahili
Je! Anaye kwenda akisinukia juu ya uso wake ni mwongofu zaidi, au yule anaye
kwenda sawasawa katika Njia Iliyo Nyooka?
|
Ayah 67:23 الأية
قُلْ هُوَ الَّذِي أَنشَأَكُمْ وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ
وَالْأَفْئِدَةَ ۖ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ
Swahili
Sema: Yeye ndiye aliye kuumbeni tangu mwanzo, na akakupeni masikio na macho, na
nyoyo. Ni kidogo kabisa shukrani zenu.
|
Ayah 67:24 الأية
قُلْ هُوَ الَّذِي ذَرَأَكُمْ فِي الْأَرْضِ وَإِلَيْهِ تُحْشَرُونَ
Swahili
Sema: Yeye ndiye aliye kutawanyeni katika ardhi, na kwake mtakusanywa.
|
Ayah 67:25 الأية
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ
Swahili
Na wanasema: Lini ahadi hii, ikiwa mnasema kweli?
|
Ayah 67:26 الأية
قُلْ إِنَّمَا الْعِلْمُ عِندَ اللَّهِ وَإِنَّمَا أَنَا نَذِيرٌ مُّبِينٌ
Swahili
Sema: Hakika ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu; na hakika mimi ni mwonyaji tu
mwenye kubainisha.
|
Ayah 67:27 الأية
فَلَمَّا رَأَوْهُ زُلْفَةً سِيئَتْ وُجُوهُ الَّذِينَ كَفَرُوا وَقِيلَ هَٰذَا
الَّذِي كُنتُم بِهِ تَدَّعُونَ
Swahili
Lakini watakapo iona karibu, nyuso za walio kufuru zitahuzunishwa, na itasemwa:
Hayo ndiyo mliyo kuwa mkiyaomba.
|
Ayah 67:28 الأية
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَهْلَكَنِيَ اللَّهُ وَمَن مَّعِيَ أَوْ رَحِمَنَا فَمَن
يُجِيرُ الْكَافِرِينَ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ
Swahili
Sema: Mwaonaje, ikiwa Mwenyezi Mungu atanihiliki mimi na walio pamoja nami, au
akiturehemu, ni nani atakaye walinda makafiri na adhabu chungu?
|
Ayah 67:29 الأية
قُلْ هُوَ الرَّحْمَٰنُ آمَنَّا بِهِ وَعَلَيْهِ تَوَكَّلْنَا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ
مَنْ هُوَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ
Swahili
Sema: Yeye ndiye Mwingi wa Rehema; tunamuamini Yeye, na juu yake tunategemea.
Mtakuja jua ni nani aliye katika upotovu ulio dhaahiri.
|
Ayah 67:30 الأية
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَصْبَحَ مَاؤُكُمْ غَوْرًا فَمَن يَأْتِيكُم بِمَاءٍ
مَّعِينٍ
Swahili
Sema: Mwaonaje, yakiwa maji yenu yamedidimia chini, nani atakueleteeni maji
yanayo miminika?
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|