First Ayah 1 الأية الأوليبِسْم ِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
ن ۚ وَالْقَلَمِ وَمَا يَسْطُرُونَ
Swahili
Nuun. Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo,
|
Ayah 68:2 الأية
مَا أَنتَ بِنِعْمَةِ رَبِّكَ بِمَجْنُونٍ
Swahili
Kwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu.
|
Ayah 68:3 الأية
وَإِنَّ لَكَ لَأَجْرًا غَيْرَ مَمْنُونٍ
Swahili
Na kwa hakika wewe una malipo yasiyo katika.
|
Ayah 68:4 الأية
وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٍ
Swahili
Na hakika wewe una tabia tukufu.
|
Ayah 68:5 الأية
فَسَتُبْصِرُ وَيُبْصِرُونَ
Swahili
Karibu utaona, na wao wataona,
|
Ayah 68:6 الأية
بِأَييِّكُمُ الْمَفْتُونُ
Swahili
Ni nani kati yenu aliye pandwa na wazimu.
|
Ayah 68:7 الأية
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِ وَهُوَ أَعْلَمُ
بِالْمُهْتَدِينَ
Swahili
Hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye ajuaye zaidi nani aliye ipotea Njia yake, na
Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka.
|
Ayah 68:8 الأية
فَلَا تُطِعِ الْمُكَذِّبِينَ
Swahili
Basi usiwat'ii wanao kadhibisha.
|
Ayah 68:9 الأية
وَدُّوا لَوْ تُدْهِنُ فَيُدْهِنُونَ
Swahili
Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie.
|
Ayah 68:10 الأية
وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَّهِينٍ
Swahili
Wala usimt'ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa,
|
Ayah 68:11 الأية
هَمَّازٍ مَّشَّاءٍ بِنَمِيمٍ
Swahili
Mtapitapi, apitaye akifitini,
|
Ayah 68:12 الأية
مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ
Swahili
Mwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi,
|
Ayah 68:13 الأية
عُتُلٍّ بَعْدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ
Swahili
Mkavu, na juu ya hayo, mshari, amejipachika tu.
|
Ayah 68:14 الأية
أَن كَانَ ذَا مَالٍ وَبَنِينَ
Swahili
Ati kwa kuwa ana mali na watoto!
|
Ayah 68:15 الأية
إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ
Swahili
Anapo somewa Aya zetu, husema: Hizi ni simulizi za uwongo za watu wa zamani!
|
Ayah 68:16 الأية
سَنَسِمُهُ عَلَى الْخُرْطُومِ
Swahili
Tutamtia kovu juu ya pua yake.
|
Ayah 68:17 الأية
إِنَّا بَلَوْنَاهُمْ كَمَا بَلَوْنَا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ إِذْ أَقْسَمُوا
لَيَصْرِمُنَّهَا مُصْبِحِينَ
Swahili
Hakika tumewajaribu hawa kama tulivyo wajaribu wale wenye shamba, walipo apa
kwamba watayavuna mazao yake itakapo kuwa asubuhi.
|
Ayah 68:18 الأية
وَلَا يَسْتَثْنُونَ
Swahili
Wala hawakusema: Mungu akipenda!
|
Ayah 68:19 الأية
فَطَافَ عَلَيْهَا طَائِفٌ مِّن رَّبِّكَ وَهُمْ نَائِمُونَ
Swahili
Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako Mlezi, nao wamelala!
|
Ayah 68:20 الأية
فَأَصْبَحَتْ كَالصَّرِيمِ
Swahili
Likawa kama usiku wa giza.
|
Ayah 68:21 الأية
فَتَنَادَوْا مُصْبِحِينَ
Swahili
Asubuhi wakaitana.
|
Ayah 68:22 الأية
أَنِ اغْدُوا عَلَىٰ حَرْثِكُمْ إِن كُنتُمْ صَارِمِينَ
Swahili
Ya kwamba nendeni kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna.
|
Ayah 68:23 الأية
فَانطَلَقُوا وَهُمْ يَتَخَافَتُونَ
Swahili
Basi walikwenda na huku wakinong'onezana,
|
Ayah 68:24 الأية
أَن لَّا يَدْخُلَنَّهَا الْيَوْمَ عَلَيْكُم مِّسْكِينٌ
Swahili
Ya kuwa leo hata masikini mmoja asikuingilieni.
|
Ayah 68:25 الأية
وَغَدَوْا عَلَىٰ حَرْدٍ قَادِرِينَ
Swahili
Na walikwenda asubuhi, nao wameshikilia azimio hilo.
|
Ayah 68:26 الأية
فَلَمَّا رَأَوْهَا قَالُوا إِنَّا لَضَالُّونَ
Swahili
Basi walipo liona, wakasema: Hakika tumepotea!
|
Ayah 68:27 الأية
بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ
Swahili
Bali tumenyimwa!
|
Ayah 68:28 الأية
قَالَ أَوْسَطُهُمْ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ لَوْلَا تُسَبِّحُونَ
Swahili
Mbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Mwenyezi Mungu?
|
Ayah 68:29 الأية
قَالُوا سُبْحَانَ رَبِّنَا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ
Swahili
Wakasema: Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tulikuwa wenye kudhulumu.
|
Ayah 68:30 الأية
فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَلَاوَمُونَ
Swahili
Basi wakakabiliana kulaumiana wao kwa wao.
|
Ayah 68:31 الأية
قَالُوا يَا وَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا طَاغِينَ
Swahili
Wakasema: Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka!
|
Ayah 68:32 الأية
عَسَىٰ رَبُّنَا أَن يُبْدِلَنَا خَيْرًا مِّنْهَا إِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا
رَاغِبُونَ
Swahili
Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni
wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi.
|
Ayah 68:33 الأية
كَذَٰلِكَ الْعَذَابُ ۖ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا
يَعْلَمُونَ
Swahili
Namna hivi yanakuwa mateso, na bila ya shaka mateso ya Akhera ni makubwa zaidi,
laiti wangeli jua!
|
Ayah 68:34 الأية
إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتِ النَّعِيمِ
Swahili
Hakika wachamngu watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao Mlezi.
|
Ayah 68:35 الأية
أَفَنَجْعَلُ الْمُسْلِمِينَ كَالْمُجْرِمِينَ
Swahili
Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu?
|
Ayah 68:36 الأية
مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ
Swahili
Mna nini? Mnahukumu vipi?
|
Ayah 68:37 الأية
أَمْ لَكُمْ كِتَابٌ فِيهِ تَدْرُسُونَ
Swahili
Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma?
|
Ayah 68:38 الأية
إِنَّ لَكُمْ فِيهِ لَمَا تَخَيَّرُونَ
Swahili
Kuwa mtapata humo mnayo yapenda?
|
Ayah 68:39 الأية
أَمْ لَكُمْ أَيْمَانٌ عَلَيْنَا بَالِغَةٌ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۙ إِنَّ
لَكُمْ لَمَا تَحْكُمُونَ
Swahili
Au mnazo ahadi za viapo juu yetu za kufika Siku ya Kiyama ya kuwa hakika mtapata
kila mnayo jihukumia?
|
Ayah 68:40 الأية
سَلْهُمْ أَيُّهُم بِذَٰلِكَ زَعِيمٌ
Swahili
Waulize: Ni nani miongoni mwao dhamini wa haya?
|
Ayah 68:41 الأية
أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ فَلْيَأْتُوا بِشُرَكَائِهِمْ إِن كَانُوا صَادِقِينَ
Swahili
Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wanasema kweli.
|
Ayah 68:42 الأية
يَوْمَ يُكْشَفُ عَن سَاقٍ وَيُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ
Swahili
Siku utakapo wekwa wazi mundi, na wataitwa kusujudu, lakini hawataweza,
|
Ayah 68:43 الأية
خَاشِعَةً أَبْصَارُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۖ وَقَدْ كَانُوا يُدْعَوْنَ إِلَى
السُّجُودِ وَهُمْ سَالِمُونَ
Swahili
Macho yao yatainama chini, fedheha itawafunika. Na hakika walikuwa wakiitwa
wasujudu walipo kuwa wazima -
|
Ayah 68:44 الأية
فَذَرْنِي وَمَن يُكَذِّبُ بِهَٰذَا الْحَدِيثِ ۖ سَنَسْتَدْرِجُهُم مِّنْ حَيْثُ
لَا يَعْلَمُونَ
Swahili
Basi niache na wanao kadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kwa
mahali wasipo pajua.
|
Ayah 68:45 الأية
وَأُمْلِي لَهُمْ ۚ إِنَّ كَيْدِي مَتِينٌ
Swahili
Na ninawapururia muhula; hakika hila zangu ni imara.
|
Ayah 68:46 الأية
أَمْ تَسْأَلُهُمْ أَجْرًا فَهُم مِّن مَّغْرَمٍ مُّثْقَلُونَ
Swahili
Au unawaomba ujira, na wao wanaemewa na gharama hiyo?
|
Ayah 68:47 الأية
أَمْ عِندَهُمُ الْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ
Swahili
Au iko kwao siri, basi wao wanaiandika?
|
Ayah 68:48 الأية
فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ الْحُوتِ إِذْ نَادَىٰ وَهُوَ
مَكْظُومٌ
Swahili
Basi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi, wala usiwe kama mmezwa na samaki, alipo
nadi naye kazongwa.
|
Ayah 68:49 الأية
لَّوْلَا أَن تَدَارَكَهُ نِعْمَةٌ مِّن رَّبِّهِ لَنُبِذَ بِالْعَرَاءِ وَهُوَ
مَذْمُومٌ
Swahili
Kama isingeli mfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angeli
tupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa.
|
Ayah 68:50 الأية
فَاجْتَبَاهُ رَبُّهُ فَجَعَلَهُ مِنَ الصَّالِحِينَ
Swahili
Lakini Mola wake Mlezi alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema.
|
Ayah 68:51 الأية
وَإِن يَكَادُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَيُزْلِقُونَكَ بِأَبْصَارِهِمْ لَمَّا سَمِعُوا
الذِّكْرَ وَيَقُولُونَ إِنَّهُ لَمَجْنُونٌ
Swahili
Na walio kufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanapo sikia mawaidha, na
wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu.
|
Ayah 68:52 الأية
وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ
Swahili
Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|