First Ayah 1 الأية الأوليبِسْم ِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَنفَالِ ۖ قُلِ الْأَنفَالُ لِلَّهِ وَالرَّسُولِ ۖ
فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَصْلِحُوا ذَاتَ بَيْنِكُمْ ۖ وَأَطِيعُوا اللَّهَ
وَرَسُولَهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ
Swahili
Wanakuuliza juu ya Ngawira. Sema: Ngawira ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume. Basi
mcheni Mwenyezi Mungu na suluhisheni mambo baina yenu, na mt'iini Mwenyezi Mungu
na Mtume wake ikiwa nyinyi ni Waumini.
|
Ayah 8:2 الأية
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللَّهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ
وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ
يَتَوَكَّلُونَ
Swahili
Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa khofu,
na wanapo somewa Aya zake huwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi.
|
Ayah 8:3 الأية
الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ
Swahili
Hao ambao wanashika Sala na wanatoa katika yale tunayo waruzuku.
|
Ayah 8:4 الأية
أُولَٰئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا ۚ لَّهُمْ دَرَجَاتٌ عِندَ رَبِّهِمْ
وَمَغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ
Swahili
Hao kweli ndio Waumini. Wao wana vyeo, na maghfira, na riziki bora, kwa Mola wao
Mlezi.
|
Ayah 8:5 الأية
كَمَا أَخْرَجَكَ رَبُّكَ مِن بَيْتِكَ بِالْحَقِّ وَإِنَّ فَرِيقًا مِّنَ
الْمُؤْمِنِينَ لَكَارِهُونَ
Swahili
Kama Mola wako Mlezi alivyo kutoa nyumbani kwako kwa Haki, na hakika kundi moja
la Waumini linachukia.
|
Ayah 8:6 الأية
يُجَادِلُونَكَ فِي الْحَقِّ بَعْدَمَا تَبَيَّنَ كَأَنَّمَا يُسَاقُونَ إِلَى
الْمَوْتِ وَهُمْ يَنظُرُونَ
Swahili
Wanajadiliana nawe kwa jambo la Haki baada ya kwisha bainika, kama kwamba
wanasukumwa kwenye mauti nao wanaona.
|
Ayah 8:7 الأية
وَإِذْ يَعِدُكُمُ اللَّهُ إِحْدَى الطَّائِفَتَيْنِ أَنَّهَا لَكُمْ وَتَوَدُّونَ
أَنَّ غَيْرَ ذَاتِ الشَّوْكَةِ تَكُونُ لَكُمْ وَيُرِيدُ اللَّهُ أَن يُحِقَّ
الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ وَيَقْطَعَ دَابِرَ الْكَافِرِينَ
Swahili
Na Mwenyezi Mungu alipo kuahidini kuwa moja katika makundi mawili ni lenu. Nanyi
mkapenda lisilo na nguvu ndio liwe lenu; na Mwenyezi Mungu anapenda ahakikishe
Haki kwa maneno yake, na aikate mizizi ya makafiri.
|
Ayah 8:8 الأية
لِيُحِقَّ الْحَقَّ وَيُبْطِلَ الْبَاطِلَ وَلَوْ كَرِهَ الْمُجْرِمُونَ
Swahili
Ili ahakikishe Haki na auvunje upotovu na wangachukia wakosefu.
|
Ayah 8:9 الأية
إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَاسْتَجَابَ لَكُمْ أَنِّي مُمِدُّكُم بِأَلْفٍ
مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُرْدِفِينَ
Swahili
Mlipo kuwa mkimuomba msaada Mola wenu Mlezi, naye akakujibuni kuwa: Kwa yakini
Mimi nitakusaidieni kwa Malaika elfu wanao fuatana mfululizo.
|
Ayah 8:10 الأية
وَمَا جَعَلَهُ اللَّهُ إِلَّا بُشْرَىٰ وَلِتَطْمَئِنَّ بِهِ قُلُوبُكُمْ ۚ وَمَا
النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِندِ اللَّهِ ۚ إِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ
Swahili
Na Mwenyezi Mungu hakufanya haya ila kuwa ni bishara na ili nyoyo zenu zituwe.
Na haupatikani ushindi ila kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni
Mwenye nguvu, na Mwenye hikima.
|
Ayah 8:11 الأية
إِذْ يُغَشِّيكُمُ النُّعَاسَ أَمَنَةً مِّنْهُ وَيُنَزِّلُ عَلَيْكُم مِّنَ
السَّمَاءِ مَاءً لِّيُطَهِّرَكُم بِهِ وَيُذْهِبَ عَنكُمْ رِجْزَ الشَّيْطَانِ
وَلِيَرْبِطَ عَلَىٰ قُلُوبِكُمْ وَيُثَبِّتَ بِهِ الْأَقْدَامَ
Swahili
Alipo kufunikeni kwa usingizi uwe ni uaminisho kutoka kwake, na akakuteremshieni
maji kutoka mbinguni ili kukusafisheni kwayo na kukuondoleeni uchafu wa
Shet'ani, na kuzipa nguvu nyoyo zenu, na kuitia imara miguu yenu.
|
Ayah 8:12 الأية
إِذْ يُوحِي رَبُّكَ إِلَى الْمَلَائِكَةِ أَنِّي مَعَكُمْ فَثَبِّتُوا الَّذِينَ
آمَنُوا ۚ سَأُلْقِي فِي قُلُوبِ الَّذِينَ كَفَرُوا الرُّعْبَ فَاضْرِبُوا فَوْقَ
الْأَعْنَاقِ وَاضْرِبُوا مِنْهُمْ كُلَّ بَنَانٍ
Swahili
Mola wako Mlezi alipo wafunulia Malaika: Hakika Mimi ni pamoja nanyi, basi
watieni nguvu walio amini. Nitatia woga katika nyoyo za walio kufuru. Basi
wapigeni juu ya shingo na wapigeni kwenye kila ncha za vidole.
|
Ayah 8:13 الأية
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ شَاقُّوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ ۚ وَمَن يُشَاقِقِ اللَّهَ
وَرَسُولَهُ فَإِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ
Swahili
Hayo ni kwa sababu wamemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mwenye kumuasi
Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
|
Ayah 8:14 الأية
ذَٰلِكُمْ فَذُوقُوهُ وَأَنَّ لِلْكَافِرِينَ عَذَابَ النَّارِ
Swahili
Ndio hivyo! Basi ionjeni! Na bila ya shaka makafiri wana adhabu ya Moto.
|
Ayah 8:15 الأية
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا زَحْفًا فَلَا
تُوَلُّوهُمُ الْأَدْبَارَ
Swahili
Enyi Mlio amini! Mkikutana na walio kufuru vitani msiwageuzie mgongo.
|
Ayah 8:16 الأية
وَمَن يُوَلِّهِمْ يَوْمَئِذٍ دُبُرَهُ إِلَّا مُتَحَرِّفًا لِّقِتَالٍ أَوْ
مُتَحَيِّزًا إِلَىٰ فِئَةٍ فَقَدْ بَاءَ بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّهِ وَمَأْوَاهُ
جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ
Swahili
Na atakaye wageuzia mgongo wake siku hiyo - isipo kuwa kwa mbinu za vita au
kuungana na kikosi - basi atakuwa amestahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na
pahala pake ni Jahannamu, na huo ni mwisho muovu.
|
Ayah 8:17 الأية
فَلَمْ تَقْتُلُوهُمْ وَلَٰكِنَّ اللَّهَ قَتَلَهُمْ ۚ وَمَا رَمَيْتَ إِذْ
رَمَيْتَ وَلَٰكِنَّ اللَّهَ رَمَىٰ ۚ وَلِيُبْلِيَ الْمُؤْمِنِينَ مِنْهُ بَلَاءً
حَسَنًا ۚ إِنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
Swahili
Hamkuwauwa nyinyi lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye wauwa. Na wewe hukutupa,
walakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye tupa, ili awajaribu Waumini majaribio mema
yatokayo kwake. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Msikizi na Mjuzi.
|
Ayah 8:18 الأية
ذَٰلِكُمْ وَأَنَّ اللَّهَ مُوهِنُ كَيْدِ الْكَافِرِينَ
Swahili
Ndio hivyo! Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kudhoofisha vitimbi vya makafiri.
|
Ayah 8:19 الأية
إِن تَسْتَفْتِحُوا فَقَدْ جَاءَكُمُ الْفَتْحُ ۖ وَإِن تَنتَهُوا فَهُوَ خَيْرٌ
لَّكُمْ ۖ وَإِن تَعُودُوا نَعُدْ وَلَن تُغْنِيَ عَنكُمْ فِئَتُكُمْ شَيْئًا
وَلَوْ كَثُرَتْ وَأَنَّ اللَّهَ مَعَ الْمُؤْمِنِينَ
Swahili
Kama mnataka hukumu basi hukumu imekwisha kujieni. Na mkiacha itakuwa ndio kheri
kwenu. Na mkirejea Sisi pia tutarejea. Na jeshi lenu halitakufaeni kitu, japo
likiwa kubwa. Kwani hakika Mwenyezi yu pamoja na Waumini.
|
Ayah 8:20 الأية
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَا تَوَلَّوْا
عَنْهُ وَأَنتُمْ تَسْمَعُونَ
Swahili
Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msijiepushe naye,
nanyi mnasikia.
|
Ayah 8:21 الأية
وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ قَالُوا سَمِعْنَا وَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ
Swahili
Wala msiwe kama wale wanao sema: Tumesikia, na kumbe hawasikii.
|
Ayah 8:22 الأية
إِنَّ شَرَّ الدَّوَابِّ عِندَ اللَّهِ الصُّمُّ الْبُكْمُ الَّذِينَ لَا
يَعْقِلُونَ
Swahili
Hakika vinyama viovu mbele ya Mwenyezi Mungu ni vile viziwi na bubu visio tumia
akili zao.
|
Ayah 8:23 الأية
وَلَوْ عَلِمَ اللَّهُ فِيهِمْ خَيْرًا لَّأَسْمَعَهُمْ ۖ وَلَوْ أَسْمَعَهُمْ
لَتَوَلَّوا وَّهُم مُّعْرِضُونَ
Swahili
Na Mwenyezi Mungu angeli jua wema wowote kwao ange wasikilizisha, na lau ange
wasikilizisha wangeli geuka wakapuuza.
|
Ayah 8:24 الأية
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا
دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ ۖ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ
وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ
Swahili
Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la
kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na
moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.
|
Ayah 8:25 الأية
وَاتَّقُوا فِتْنَةً لَّا تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنكُمْ خَاصَّةً ۖ
وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ
Swahili
Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na
jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
|
Ayah 8:26 الأية
وَاذْكُرُوا إِذْ أَنتُمْ قَلِيلٌ مُّسْتَضْعَفُونَ فِي الْأَرْضِ تَخَافُونَ أَن
يَتَخَطَّفَكُمُ النَّاسُ فَآوَاكُمْ وَأَيَّدَكُم بِنَصْرِهِ وَرَزَقَكُم مِّنَ
الطَّيِّبَاتِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ
Swahili
Na kumbukeni mlipo kuwa wachache, mkionekana wanyonge katika nchi, mnaogopa watu
wasikunyakueni, naye akakupeni pahala pazuri pa kukaa, na akakutieni nguvu kwa
nusura yake, na akakupeni riziki nzuri ili mpate kushukuru.
|
Ayah 8:27 الأية
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَخُونُوا اللَّهَ وَالرَّسُولَ وَتَخُونُوا
أَمَانَاتِكُمْ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ
Swahili
Enyi mlio amini! Msimfanyie khiana Mwenyezi Mungu na Mtume, wala msikhini amana
zenu, nanyi mnajua.
|
Ayah 8:28 الأية
وَاعْلَمُوا أَنَّمَا أَمْوَالُكُمْ وَأَوْلَادُكُمْ فِتْنَةٌ وَأَنَّ اللَّهَ
عِندَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ
Swahili
Na jueni ya kwamba mali zenu na wana wenu ni Fitna (mtihani), na kwamba kwa
Mwenyezi Mungu upo ujira mkubwa.
|
Ayah 8:29 الأية
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَتَّقُوا اللَّهَ يَجْعَل لَّكُمْ فُرْقَانًا
وَيُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۗ وَاللَّهُ ذُو الْفَضْلِ
الْعَظِيمِ
Swahili
Enyi mlio amini! Mkimcha Mwenyezi Mungu atakupeni kipambanuo, na atakufutieni
makosa, na atakusameheni, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.
|
Ayah 8:30 الأية
وَإِذْ يَمْكُرُ بِكَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِيُثْبِتُوكَ أَوْ يَقْتُلُوكَ أَوْ
يُخْرِجُوكَ ۚ وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللَّهُ ۖ وَاللَّهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ
Swahili
Na walipo kupangia mpango walio kufuru wakufunge, au wakuuwe, au wakutoe.
Wakapanga mipango yao, na Mwenyezi Mungu akapanga yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye
mbora wa mipango.
|
Ayah 8:31 الأية
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا قَالُوا قَدْ سَمِعْنَا لَوْ نَشَاءُ
لَقُلْنَا مِثْلَ هَٰذَا ۙ إِنْ هَٰذَا إِلَّا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ
Swahili
Na wanapo somewa Aya zetu, wao husema: Tumesikia. Na lau tungeli penda tunge
sema kama haya. Haya si chochote ila hadithi za watu wa kale tu.
|
Ayah 8:32 الأية
وَإِذْ قَالُوا اللَّهُمَّ إِن كَانَ هَٰذَا هُوَ الْحَقَّ مِنْ عِندِكَ فَأَمْطِرْ
عَلَيْنَا حِجَارَةً مِّنَ السَّمَاءِ أَوِ ائْتِنَا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ
Swahili
Na walipo sema: Ee Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ni kweli itokayo kwako basi
tunyeshee mawe kutoka mbinguni, au tuletee adhabu yoyote iliyo chungu.
|
Ayah 8:33 الأية
وَمَا كَانَ اللَّهُ لِيُعَذِّبَهُمْ وَأَنتَ فِيهِمْ ۚ وَمَا كَانَ اللَّهُ
مُعَذِّبَهُمْ وَهُمْ يَسْتَغْفِرُونَ
Swahili
Na Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu nawe umo pamoja nao, wala Mwenyezi Mungu
si wa kuwaadhibu na hali ya kuwa wanaomba msamaha.
|
Ayah 8:34 الأية
وَمَا لَهُمْ أَلَّا يُعَذِّبَهُمُ اللَّهُ وَهُمْ يَصُدُّونَ عَنِ الْمَسْجِدِ
الْحَرَامِ وَمَا كَانُوا أَوْلِيَاءَهُ ۚ إِنْ أَوْلِيَاؤُهُ إِلَّا الْمُتَّقُونَ
وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
Swahili
Lakini wana jambo gani hata Mwenyezi Mungu asiwaadhibu, na hali ya kuwa
wanawazuilia watu Msikiti Mtakatifu? Wala wao hawakuwa ndio walinzi wake, bali
walinzi wake hawakuwa ila wacha-Mngu tu. Lakini wengi katika wao hawajui.
|
Ayah 8:35 الأية
وَمَا كَانَ صَلَاتُهُمْ عِندَ الْبَيْتِ إِلَّا مُكَاءً وَتَصْدِيَةً ۚ فَذُوقُوا
الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ
Swahili
Na haikuwa ibada yao kwenye hiyo Nyumba (Al Kaaba) ila ni kupiga miunzi na
makofi. Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyo kuwa mkikufuru.
|
Ayah 8:36 الأية
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّوا عَن سَبِيلِ
اللَّهِ ۚ فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ
ۗ وَالَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ
Swahili
Hakika wale walio kufuru hutoa mali yao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu.
Basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto, na kisha watashindwa. Na wale
walio kufuru watakusanywa kwenye Jahannam.
|
Ayah 8:37 الأية
لِيَمِيزَ اللَّهُ الْخَبِيثَ مِنَ الطَّيِّبِ وَيَجْعَلَ الْخَبِيثَ بَعْضَهُ
عَلَىٰ بَعْضٍ فَيَرْكُمَهُ جَمِيعًا فَيَجْعَلَهُ فِي جَهَنَّمَ ۚ أُولَٰئِكَ هُمُ
الْخَاسِرُونَ
Swahili
Ili Mwenyezi Mungu apate kuwa pambanua walio waovu na walio wema, na kuwaweka
waovu juu ya waovu wengine, na kuwarundika wote pamoja, na kuwatupa katika
Jahannam. Hao ndio walio khasirika.
|
Ayah 8:38 الأية
قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا إِن يَنتَهُوا يُغْفَرْ لَهُم مَّا قَدْ سَلَفَ وَإِن
يَعُودُوا فَقَدْ مَضَتْ سُنَّتُ الْأَوَّلِينَ
Swahili
Waambie wale walio kufuru: Wakikoma watasamehewa yaliyo kwisha pita. Na
wakiyarudia basi imekwisha pita mifano ya wa zamani.
|
Ayah 8:39 الأية
وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّهِ ۚ
فَإِنِ انتَهَوْا فَإِنَّ اللَّهَ بِمَا يَعْمَلُونَ بَصِيرٌ
Swahili
Na piganeni nao mpaka isiwepo fitna na mateso, na Dini yote iwe kwa ajili ya
Mwenyezi Mungu. Lakini wakiacha, basi hakika Mwenyezi Mungu anayaona wanayo
yatenda.
|
Ayah 8:40 الأية
وَإِن تَوَلَّوْا فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ مَوْلَاكُمْ ۚ نِعْمَ الْمَوْلَىٰ
وَنِعْمَ النَّصِيرُ
Swahili
Na kama wakigeuka basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mola wenu, ni Mola
Mwema na Msaidizi Mwema.
|
Ayah 8:41 الأية
وَاعْلَمُوا أَنَّمَا غَنِمْتُم مِّن شَيْءٍ فَأَنَّ لِلَّهِ خُمُسَهُ
وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ
السَّبِيلِ إِن كُنتُمْ آمَنتُم بِاللَّهِ وَمَا أَنزَلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا
يَوْمَ الْفُرْقَانِ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ ۗ وَاللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ
قَدِيرٌ
Swahili
NA JUENI ya kwamba ngawira mnayo ipata, basi khums (sehemu moja katika tano) ni
kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na
wasafiri, ikiwa nyinyi mmemuamini Mwenyezi Mungu na tuliyo yateremsha kwa mja
wetu siku ya kipambanuo, siku yalipo kutana majeshi mawili. Na Mwenyezi Mungu ni
Muweza wa kila kitu.
|
Ayah 8:42 الأية
إِذْ أَنتُم بِالْعُدْوَةِ الدُّنْيَا وَهُم بِالْعُدْوَةِ الْقُصْوَىٰ وَالرَّكْبُ
أَسْفَلَ مِنكُمْ ۚ وَلَوْ تَوَاعَدتُّمْ لَاخْتَلَفْتُمْ فِي الْمِيعَادِ ۙ
وَلَٰكِن لِّيَقْضِيَ اللَّهُ أَمْرًا كَانَ مَفْعُولًا لِّيَهْلِكَ مَنْ هَلَكَ
عَن بَيِّنَةٍ وَيَحْيَىٰ مَنْ حَيَّ عَن بَيِّنَةٍ ۗ وَإِنَّ اللَّهَ لَسَمِيعٌ
عَلِيمٌ
Swahili
Kumbukeni pale mlipo kuwa nyinyi kwenye ng'ambo ya karibu ya bonde, na wao
wakawa ng'ambo ya mbali, na msafara ulipo kuwa chini yenu. Na ingeli kuwa
mmeagana mngeli khitalifiana katika miadi. Lakini (mkakutana) ili Mwenyezi Mungu
atimize jambo lilio kuwa lazima litendeke, kwa sababu aangamie wa kuangamia kwa
dalili zilizo dhaahiri, na asalimike wa kusalimika kwa dalili zilizo dhaahiri.
Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.
|
Ayah 8:43 الأية
إِذْ يُرِيكَهُمُ اللَّهُ فِي مَنَامِكَ قَلِيلًا ۖ وَلَوْ أَرَاكَهُمْ كَثِيرًا
لَّفَشِلْتُمْ وَلَتَنَازَعْتُمْ فِي الْأَمْرِ وَلَٰكِنَّ اللَّهَ سَلَّمَ ۗ
إِنَّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ
Swahili
Kumbuka alipo kuonyesha usingizini mwako kwamba wao ni wachache - na lau angeli
kuonyesha kuwa ni wengi, mngeli ingiwa na woga, na mngeli zozana katika jambo
hilo. Lakini Mwenyezi Mungu kakuvueni. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua yalio
vifuani.
|
Ayah 8:44 الأية
وَإِذْ يُرِيكُمُوهُمْ إِذِ الْتَقَيْتُمْ فِي أَعْيُنِكُمْ قَلِيلًا
وَيُقَلِّلُكُمْ فِي أَعْيُنِهِمْ لِيَقْضِيَ اللَّهُ أَمْرًا كَانَ مَفْعُولًا ۗ
وَإِلَى اللَّهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ
Swahili
Na mlipo kutana akakuonyesheni machoni mwenu kuwa wao ni wachache, na
akakufanyeni nyinyi ni wachache machoni mwao, ili Mwenyezi Mungu atimize jambo
lilio kuwa liwe. Na mambo yote hurejezwa kwa Mwenyezi Mungu.
|
Ayah 8:45 الأية
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا لَقِيتُمْ فِئَةً فَاثْبُتُوا وَاذْكُرُوا
اللَّهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
Swahili
Enyi mlio amini! Mkikutana na jeshi, basi kueni imara, na mkumbukeni Mwenyezi
Mungu sana ili mpate kufanikiwa.
|
Ayah 8:46 الأية
وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَا تَنَازَعُوا فَتَفْشَلُوا وَتَذْهَبَ
رِيحُكُمْ ۖ وَاصْبِرُوا ۚ إِنَّ اللَّهَ مَعَ الصَّابِرِينَ
Swahili
Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na
zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao
subiri.
|
Ayah 8:47 الأية
وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ خَرَجُوا مِن دِيَارِهِم بَطَرًا وَرِئَاءَ النَّاسِ
وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّهِ ۚ وَاللَّهُ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ
Swahili
Wala msiwe kama wale walio toka majumbani mwao kwa fakhari na kujionyesha kwa
watu, na wakawazuilia watu Njia ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu
ameyazunguka yote wanayo yafanya.
|
Ayah 8:48 الأية
وَإِذْ زَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ وَقَالَ لَا غَالِبَ لَكُمُ
الْيَوْمَ مِنَ النَّاسِ وَإِنِّي جَارٌ لَّكُمْ ۖ فَلَمَّا تَرَاءَتِ الْفِئَتَانِ
نَكَصَ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ وَقَالَ إِنِّي بَرِيءٌ مِّنكُمْ إِنِّي أَرَىٰ مَا لَا
تَرَوْنَ إِنِّي أَخَافُ اللَّهَ ۚ وَاللَّهُ شَدِيدُ الْعِقَابِ
Swahili
Na pale Shet'ani alipo wapambia vitendo vyao, na akawaambia: Hapana watu wa
kukushindeni hii leo, na hali mimi ni mlinzi wenu. Yalipo onana majeshi mawili,
akarudi nyuma, na akasema: Mimi si pamoja nanyi. Mimi naona msiyo yaona. Mimi
namwogopa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.
|
Ayah 8:49 الأية
إِذْ يَقُولُ الْمُنَافِقُونَ وَالَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ غَرَّ هَٰؤُلَاءِ
دِينُهُمْ ۗ وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَإِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ
Swahili
Na walipo sema wanaafiki, na wale wenye ugonjwa nyoyoni mwao: Watu hawa dini yao
imewadanganya. Na Mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni
Mwenye nguvu Ametukuka, na Mwenye hikima.
|
Ayah 8:50 الأية
وَلَوْ تَرَىٰ إِذْ يَتَوَفَّى الَّذِينَ كَفَرُوا ۙ الْمَلَائِكَةُ يَضْرِبُونَ
وُجُوهَهُمْ وَأَدْبَارَهُمْ وَذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ
Swahili
Na laiti ungeli ona Malaika wanapo wafisha wale walio kufuru wakiwapiga nyuso
zao na migongo yao, na kuwaambia: Ionjeni adhabu ya Moto!
|
Ayah 8:51 الأية
ذَٰلِكَ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيكُمْ وَأَنَّ اللَّهَ لَيْسَ بِظَلَّامٍ
لِّلْعَبِيدِ
Swahili
Hayo ni kwa sababu ya yale yaliyo kwisha tangulizwa na mikono yenu, na hakika
Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja.
|
Ayah 8:52 الأية
كَدَأْبِ آلِ فِرْعَوْنَ ۙ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّهِ
فَأَخَذَهُمُ اللَّهُ بِذُنُوبِهِمْ ۗ إِنَّ اللَّهَ قَوِيٌّ شَدِيدُ الْعِقَابِ
Swahili
Kama ada ya watu wa Firauni na walio kuwa kabla yao - walizikataa Ishara za
Mwenyezi Mungu. Basi Mwenyezi Mungu aliwashika kwa sababu ya madhambi yao. Na
hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na mkali wa kuadhibu.
|
Ayah 8:53 الأية
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّهَ لَمْ يَكُ مُغَيِّرًا نِّعْمَةً أَنْعَمَهَا عَلَىٰ قَوْمٍ
حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ ۙ وَأَنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
Swahili
Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu habadilishi kabisa neema alizo waneemesha
watu, mpaka wao wabadilishe yaliyomo ndani ya nafsi zao. Na hakika Mwwnyezi
Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
|
Ayah 8:54 الأية
كَدَأْبِ آلِ فِرْعَوْنَ ۙ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَذَّبُوا بِآيَاتِ
رَبِّهِمْ فَأَهْلَكْنَاهُم بِذُنُوبِهِمْ وَأَغْرَقْنَا آلَ فِرْعَوْنَ ۚ وَكُلٌّ
كَانُوا ظَالِمِينَ
Swahili
Ni kama ada ya watu wa Firauni na walio kabla yao - walizikanusha Ishara za Mola
wao Mlezi, basi tukawateketeza kwa madhambi yao. Na tukawazamisha watu wa
Firauni. Na wote walikuwa wenye kudhulumu.
|
Ayah 8:55 الأية
إِنَّ شَرَّ الدَّوَابِّ عِندَ اللَّهِ الَّذِينَ كَفَرُوا فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ
Swahili
Hakika vinyama vilio viovu kabisa mbele ya Mwenyezi Mungu ni wale wanao kufuru,
basi hao hawaamini;
|
Ayah 8:56 الأية
الَّذِينَ عَاهَدتَّ مِنْهُمْ ثُمَّ يَنقُضُونَ عَهْدَهُمْ فِي كُلِّ مَرَّةٍ
وَهُمْ لَا يَتَّقُونَ
Swahili
Wale ambao miongoni mwao umepatana nao ahadi, kisha wanavunja ahadi yao kila
mara, wala hawamchi Mungu.
|
Ayah 8:57 الأية
فَإِمَّا تَثْقَفَنَّهُمْ فِي الْحَرْبِ فَشَرِّدْ بِهِم مَّنْ خَلْفَهُمْ
لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ
Swahili
Basi ukiwakuta vitani wakimbize walio nyuma yao ili wapate kukumbuka.
|
Ayah 8:58 الأية
وَإِمَّا تَخَافَنَّ مِن قَوْمٍ خِيَانَةً فَانبِذْ إِلَيْهِمْ عَلَىٰ سَوَاءٍ ۚ
إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْخَائِنِينَ
Swahili
Na ukichelea khiana kwa watu fulani basi watupilie ahadi yao kwa usawa. Hakika
Mwenyezi Mungu hawapendi makhaini.
|
Ayah 8:59 الأية
وَلَا يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا سَبَقُوا ۚ إِنَّهُمْ لَا يُعْجِزُونَ
Swahili
Wala wasidhanie wale walio kufuru kwamba wao wametangulia mbele. La, wao
hawatashinda.
|
Ayah 8:60 الأية
وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ وَمِن رِّبَاطِ الْخَيْلِ
تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ وَآخَرِينَ مِن دُونِهِمْ لَا
تَعْلَمُونَهُمُ اللَّهُ يَعْلَمُهُمْ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِن شَيْءٍ فِي سَبِيلِ
اللَّهِ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ
Swahili
Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari,
ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao
hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na mkitoa chochote katika Njia ya
Mwenyezi Mungu mtarudishiwa, na wala nyinyi hamtadhulumiwa.
|
Ayah 8:61 الأية
وَإِن جَنَحُوا لِلسَّلْمِ فَاجْنَحْ لَهَا وَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ ۚ إِنَّهُ
هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ
Swahili
Na wakielekea amani nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye
ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua.
|
Ayah 8:62 الأية
وَإِن يُرِيدُوا أَن يَخْدَعُوكَ فَإِنَّ حَسْبَكَ اللَّهُ ۚ هُوَ الَّذِي
أَيَّدَكَ بِنَصْرِهِ وَبِالْمُؤْمِنِينَ
Swahili
Na wakitaka kukukhadaa basi Mwenyezi Mungu atakutosheleza. Kwani Yeye ndiye
aliye kuunga mkono kwa nusura yake na kwa Waumini.
|
Ayah 8:63 الأية
وَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ ۚ لَوْ أَنفَقْتَ مَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا مَّا
أَلَّفْتَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ وَلَٰكِنَّ اللَّهَ أَلَّفَ بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّهُ
عَزِيزٌ حَكِيمٌ
Swahili
Na akaziunga nyoyo zao. Na lau wewe ungeli toa vyote viliomo duniani usingeli
weza kuziunga nyoyo zao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye waunganisha. Hakika
Yeye ndiye Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
|
Ayah 8:64 الأية
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ حَسْبُكَ اللَّهُ وَمَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ
Swahili
Ewe Nabii! Mwenyezi Mungu anakutoshelezea wewe na Waumini walio kufuata.
|
Ayah 8:65 الأية
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ حَرِّضِ الْمُؤْمِنِينَ عَلَى الْقِتَالِ ۚ إِن يَكُن
مِّنكُمْ عِشْرُونَ صَابِرُونَ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ ۚ وَإِن يَكُن مِّنكُم
مِّائَةٌ يَغْلِبُوا أَلْفًا مِّنَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا
يَفْقَهُونَ
Swahili
Ewe Nabii! Wahimize Waumini wende vitani. Wakiwapo kati yenu ishirini wanao
subiri watawashinda mia mbili. Na wakiwapo kati yenu mia watawashinda elfu moja
katika walio kufuru. Kwa sababu wao ni watu wasio fahamu.
|
Ayah 8:66 الأية
الْآنَ خَفَّفَ اللَّهُ عَنكُمْ وَعَلِمَ أَنَّ فِيكُمْ ضَعْفًا ۚ فَإِن يَكُن
مِّنكُم مِّائَةٌ صَابِرَةٌ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ ۚ وَإِن يَكُن مِّنكُمْ أَلْفٌ
يَغْلِبُوا أَلْفَيْنِ بِإِذْنِ اللَّهِ ۗ وَاللَّهُ مَعَ الصَّابِرِينَ
Swahili
Sasa Mwenyezi Mungu amekupunguzieni, na anajua kuwa upo udhaifu kwenu. Kwa hivyo
wakiwa wapo watu mia moja kati yenu wenye kusubiri watawashinda mia mbili. Na
wakiwapo elfu moja watawashinda elfu mbili, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na
Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.
|
Ayah 8:67 الأية
مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَكُونَ لَهُ أَسْرَىٰ حَتَّىٰ يُثْخِنَ فِي الْأَرْضِ ۚ
تُرِيدُونَ عَرَضَ الدُّنْيَا وَاللَّهُ يُرِيدُ الْآخِرَةَ ۗ وَاللَّهُ عَزِيزٌ
حَكِيمٌ
Swahili
Haimfalii Nabii yeyote kuwa na mateka mpaka awe ameshinda baraabara katika nchi.
Mnataka vitu vya dunia, na Mwenyezi Mungu anataka Akhera. Na Mwenyezi Mungu ni
Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye hikima.
|
Ayah 8:68 الأية
لَّوْلَا كِتَابٌ مِّنَ اللَّهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمْ فِيمَا أَخَذْتُمْ عَذَابٌ
عَظِيمٌ
Swahili
Lau isingeli kuwa hukumu iliyo kwisha tangulia kutoka kwa Mwenyezi Mungu ingeli
kupateni adhabu kubwa kwa vile mlivyo chukua.
|
Ayah 8:69 الأية
فَكُلُوا مِمَّا غَنِمْتُمْ حَلَالًا طَيِّبًا ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۚ إِنَّ
اللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Swahili
Basi kuleni katika mlivyo teka, ni halali na vizuri, na mcheni Mwenyezi Mungu.
Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.
|
Ayah 8:70 الأية
يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّمَن فِي أَيْدِيكُم مِّنَ الْأَسْرَىٰ إِن يَعْلَمِ
اللَّهُ فِي قُلُوبِكُمْ خَيْرًا يُؤْتِكُمْ خَيْرًا مِّمَّا أُخِذَ مِنكُمْ
وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۗ وَاللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Swahili
Ewe Nabii! Waambie mateka waliomo mikononi mwenu: Kama Mwenyezi akiona kheri
yoyote nyoyoni mwenu atakupeni bora kuliko vilivyo chukuliwa kwenu, na
atakusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
|
Ayah 8:71 الأية
وَإِن يُرِيدُوا خِيَانَتَكَ فَقَدْ خَانُوا اللَّهَ مِن قَبْلُ فَأَمْكَنَ
مِنْهُمْ ۗ وَاللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ
Swahili
Ikiwa wanataka kukufanyia khiana, wao walikwisha mfanyia khiana Mwenyezi Mungu
kabla yake, na Yeye akakuwezesha kuwashinda. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua
Mwenye hikima.
|
Ayah 8:72 الأية
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ
فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالَّذِينَ آوَوا وَّنَصَرُوا أُولَٰئِكَ بَعْضُهُمْ
أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يُهَاجِرُوا مَا لَكُم مِّن
وَلَايَتِهِم مِّن شَيْءٍ حَتَّىٰ يُهَاجِرُوا ۚ وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي
الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ إِلَّا عَلَىٰ قَوْمٍ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم
مِّيثَاقٌ ۗ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ
Swahili
Hakika wale walio amini na wakahama na wakapigania Njia ya Mwenyezi Mungu kwa
mali yao na nafsi zao, na wale walio toa mahala pa kukaa, na wakanusuru, hao ni
marafiki na walinzi wao kwa wao. Na wale walio amini lakini hawakuhama, nyinyi
hamna waajibu wa ulinzi kwao hata kidogo mpaka wahame. Lakini wakiomba msaada
kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia, isipo kuwa juu ya watu ambao
yapo mapatano baina yenu na wao. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda.
|
Ayah 8:73 الأية
وَالَّذِينَ كَفَرُوا بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ إِلَّا تَفْعَلُوهُ تَكُن
فِتْنَةٌ فِي الْأَرْضِ وَفَسَادٌ كَبِيرٌ
Swahili
Na wale walio kufuru ni marafiki wenyewe kwa wenyewe. Msipo fanya hivi itakuwako
fitna katika nchi na fisadi kubwa.
|
Ayah 8:74 الأية
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالَّذِينَ
آوَوا وَّنَصَرُوا أُولَٰئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا ۚ لَّهُم مَّغْفِرَةٌ
وَرِزْقٌ كَرِيمٌ
Swahili
Na walio amini wakahama na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na
walio toa mahala pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Watapata
msamaha wa Mwenyezi Mungu na kuruzukiwa kwema.
|
Ayah 8:75 الأية
وَالَّذِينَ آمَنُوا مِن بَعْدُ وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا مَعَكُمْ فَأُولَٰئِكَ
مِنكُمْ ۚ وَأُولُو الْأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَىٰ بِبَعْضٍ فِي كِتَابِ اللَّهِ
ۗ إِنَّ اللَّهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ
Swahili
Na watakao amini baadaye na wakahajiri, na wakapigana Jihadi pamoja nanyi, basi
hao ni katika nyinyi. Na jamaa wa nasaba wanastahikiana wenyewe kwa wenyewe
zaidi katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua
kila kitu.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|