1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
الم
Alif-lam-meem
Swahili
Alif Lam Mim (A.L.M.)
|
Ayah 30:2 الأية
غُلِبَتِ الرُّومُ
Ghulibati arroom
Swahili
Warumi wameshindwa,
|
Ayah 30:3 الأية
فِي أَدْنَى الْأَرْضِ وَهُم مِّن بَعْدِ غَلَبِهِمْ سَيَغْلِبُونَ
Fee adna al-ardi wahum minbaAAdi ghalabihim sayaghliboon
Swahili
Katika nchi iliyo karibu. Nao baada ya kushindwa kwao watashinda
|
Ayah 30:4 الأية
فِي بِضْعِ سِنِينَ ۗ لِلَّهِ الْأَمْرُ مِن قَبْلُ وَمِن بَعْدُ ۚ وَيَوْمَئِذٍ
يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ
Fee bidAAi sineena lillahial-amru min qablu wamin baAAdu wayawma-ithin
yafrahualmu/minoon
Swahili
Katika miaka michache. Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na
siku hiyo Waumini watafurahi.
|
Ayah 30:5 الأية
بِنَصْرِ اللهِ ۚ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ
Binasri Allahi yansuruman yashao wahuwa alAAazeezu arraheem
Swahili
Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye
kurehemu.
|
Ayah 30:6 الأية
وَعْدَ اللهِ ۖ لَا يُخْلِفُ اللهُ وَعْدَهُ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا
يَعْلَمُونَ
WaAAda Allahi la yukhlifu AllahuwaAAdahu walakinna akthara annasi layaAAlamoon
Swahili
Ni ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake. Lakini watu wengi
hawajui.
|
Ayah 30:7 الأية
يَعْلَمُونَ ظَاهِرًا مِّنَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ عَنِ الْآخِرَةِ هُمْ
غَافِلُونَ
YaAAlamoona thahiranmina alhayati addunya wahum AAanial-akhirati hum ghafiloon
Swahili
Wanajua hali ya dhaahiri ya maisha ya dunia, na wameghafilika na Akhera.
|
Ayah 30:8 الأية
أَوَلَمْ يَتَفَكَّرُوا فِي أَنفُسِهِم ۗ مَّا خَلَقَ اللهُ السَّمَاوَاتِ
وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَأَجَلٍ مُّسَمًّى ۗ وَإِنَّ
كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ لَكَافِرُونَ
Awa lam yatafakkaroo fee anfusihim makhalaqa Allahu assamawati wal-ardawama
baynahuma illa bilhaqqiwaajalin musamman wa-inna katheeran mina annasibiliqa-i
rabbihim lakafiroon
Swahili
Je! Hawajifikirii nafsi zao? Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na viliomo
ndani yake ila kwa Haki na kwa muda maalumu. Na hakika watu wengi bila ya shaka
ni wenye kukataa kuwa watakutana na Mola wao Mlezi.
|
Ayah 30:9 الأية
أَوَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ
مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَانُوا أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَأَثَارُوا الْأَرْضَ
وَعَمَرُوهَا أَكْثَرَ مِمَّا عَمَرُوهَا وَجَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ
ۖ فَمَا كَانَ اللهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ
Awa lam yaseeroo fee al-ardi fayanthurookayfa kana AAaqibatu allatheena min
qablihimkanoo ashadda minhum quwwatan waatharoo al-ardawaAAamarooha akthara
mimma AAamarooha wajaat-humrusuluhum bilbayyinati fama kana Allahuliyathlimahum
walakin kanoo anfusahumyathlimoon
Swahili
Je! Hawatembei katika ardhi wakaona ulivyo kuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao?
Nao walikuwa na nguvu zaidi kuliko wao, na wakaitimbua ardhi na wakaistawisha
zaidi kuliko walivyo istawisha wao. Na Mitume wao wakawajia na dalili zilizo
wazi. Basi hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa
wakijidhulumu nafsi zao.
|
Ayah 30:10 الأية
ثُمَّ كَانَ عَاقِبَةَ الَّذِينَ أَسَاءُوا السُّوأَىٰ أَن كَذَّبُوا بِآيَاتِ
اللهِ وَكَانُوا بِهَا يَسْتَهْزِئُونَ
Thumma kana AAaqibata allatheenaasaoo assoo-a an kaththaboo bi-ayatiAllahi
wakanoo biha yastahzi-oon
Swahili
Kisha ulikuwa mwisho wa walio fanya ubaya ni kuzikanusha Ishara za Mwenyezi
Mungu, na wakawa wanazifanyia maskhara.
|
Ayah 30:11 الأية
اللهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ
Allahu yabdao alkhalqa thummayuAAeeduhu thumma ilayhi turjaAAoon
Swahili
Mwenyezi Mungu huanzisha uumbaji, tena akaurudisha mara ya pili, na kisha
mtarejeshwa kwake.
|
Ayah 30:12 الأية
وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يُبْلِسُ الْمُجْرِمُونَ
Wayawma taqoomu assaAAatuyublisu almujrimoon
Swahili
Na itapo simama Saa wakosefu watakata tamaa.
|
Ayah 30:13 الأية
وَلَمْ يَكُن لَّهُم مِّن شُرَكَائِهِمْ شُفَعَاءُ وَكَانُوا بِشُرَكَائِهِمْ
كَافِرِينَ
Walam yakun lahum min shuraka-ihimshufaAAao wakanoo bishuraka-ihim kafireen
Swahili
Wala hawatakuwa na waombezi miongoni mwa walio kuwa wakiwashirikisha na Mungu;
na wao wenyewe watawakataa hao washirikishwa wao.
|
Ayah 30:14 الأية
وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يَوْمَئِذٍ يَتَفَرَّقُونَ
Wayawma taqoomu assaAAatuyawma-ithin yatafarraqoon
Swahili
Na siku itapo simama Saa, siku hiyo watagawanyika.
|
Ayah 30:15 الأية
فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَهُمْ فِي رَوْضَةٍ
يُحْبَرُونَ
Faamma allatheena amanoowaAAamiloo assalihati fahum fee rawdatinyuhbaroon
Swahili
Ama walio amini na wakatenda mema watafurahishwa katika Bustani.
|
Ayah 30:16 الأية
وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَلِقَاءِ الْآخِرَةِ
فَأُولَٰئِكَ فِي الْعَذَابِ مُحْضَرُونَ
Waamma allatheena kafaroo wakaththaboobi-ayatina waliqa-i al-akhiratifaola-ika
fee alAAathabi muhdaroon
Swahili
Na ama walio kufuru na wakazikanusha Ishara zetu na mkutano wa Akhera, hao basi
watahudhurishwa katika adhabu.
|
Ayah 30:17 الأية
فَسُبْحَانَ اللهِ حِينَ تُمْسُونَ وَحِينَ تُصْبِحُونَ
Fasubhana Allahi heenatumsoona waheena tusbihoon
Swahili
Basi Subhanallah! Mtakaseni Mwenyezi Mungu jioni na asubuhi,
|
Ayah 30:18 الأية
وَلَهُ الْحَمْدُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَعَشِيًّا وَحِينَ تُظْهِرُونَ
Walahu alhamdu fee assamawatiwal-ardi waAAashiyyan waheena tuthhiroon
Swahili
Na sifa zote njema ni zake katika mbingu na ardhi, na alasiri na adhuhuri.
|
Ayah 30:19 الأية
يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَيُحْيِي
الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ وَكَذَٰلِكَ تُخْرَجُونَ
Yukhriju alhayya mina almayyitiwayukhriju almayyita mina alhayyi wayuhyee
al-ardabaAAda mawtiha wakathalika tukhrajoon
Swahili
Hukitoa kilicho hai kutokana na kilicho kufa, na hukitoa kilicho kufa kutokana
na kilicho hai. Na huihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Na kama hivyo ndivyo
mtavyo fufuliwa.
|
Ayah 30:20 الأية
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ إِذَا أَنتُم بَشَرٌ
تَنتَشِرُونَ
Wamin ayatihi an khalaqakummin turabin thumma itha antum basharun tantashiroon
Swahili
Na katika Ishara zake ni kuwa kakuumbeni kwa udongo. Kisha mmekuwa watu mlio
tawanyika kote kote.
|
Ayah 30:21 الأية
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا
إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ
لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ
Wamin ayatihi an khalaqa lakummin anfusikum azwajan litaskunoo ilayha
wajaAAalabaynakum mawaddatan warahmatan inna fee thalika laayatinliqawmin
yatafakkaroon
Swahili
Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili
mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika
haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.
|
Ayah 30:22 الأية
وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافُ أَلْسِنَتِكُمْ
وَأَلْوَانِكُمْ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّلْعَالِمِينَ
Wamin ayatihi khalqu assamawatiwal-ardi wakhtilafu alsinatikumwaalwanikum inna
fee thalika laayatinlilAAalimeen
Swahili
Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutafautiana ndimi zenu na
rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wajuzi.
|
Ayah 30:23 الأية
وَمِنْ آيَاتِهِ مَنَامُكُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَابْتِغَاؤُكُم مِّن
فَضْلِهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ
Wamin ayatihi manamukumbillayli wannahari wabtighaokummin fadlihi inna fee
thalika laayatinliqawmin yasmaAAoon
Swahili
Na katika Ishara zake ni kulala kwenu usiku na mchana, na kutafuta kwenu fadhila
zake. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao sikia.
|
Ayah 30:24 الأية
وَمِنْ آيَاتِهِ يُرِيكُمُ الْبَرْقَ خَوْفًا وَطَمَعًا وَيُنَزِّلُ مِنَ
السَّمَاءِ مَاءً فَيُحْيِي بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ
لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ
Wamin ayatihi yureekumualbarqa khawfan watamaAAan wayunazzilu mina assama-imaan
fayuhyee bihi al-arda baAAda mawtihainna fee thalika laayatin liqawminyaAAqiloon
Swahili
Na katika Ishara zake hukuonyesheni umeme kwa kukutieni khofu na tamaa. Na
hukuteremshieni maji kutoka mbinguni, na kwa hayo huifufua ardhi baada ya kufa
kwake. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanao zingatia.
|
Ayah 30:25 الأية
وَمِنْ آيَاتِهِ أَن تَقُومَ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ بِأَمْرِهِ ۚ ثُمَّ إِذَا
دَعَاكُمْ دَعْوَةً مِّنَ الْأَرْضِ إِذَا أَنتُمْ تَخْرُجُونَ
Wamin ayatihi an taqooma assamaowal-ardu bi-amrihi thumma itha daAAakumdaAAwatan
mina al-ardi itha antum takhrujoon
Swahili
Na katika Ishara zake ni kuwa mbingu na ardhi zimesimama kwa amri yake. Kisha
atakapo kuiteni mwito mmoja tu, hapo mtatoka kwenye ardhi.
|
Ayah 30:26 الأية
وَلَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ
Walahu man fee assamawatiwal-ardi kullun lahu qanitoon
Swahili
Na vyake Yeye vilivyo mbinguni na katika ardhi. Vyote vinamt'ii Yeye.
|
Ayah 30:27 الأية
وَهُوَ الَّذِي يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ ۚ
وَلَهُ الْمَثَلُ الْأَعْلَىٰ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ
الْحَكِيمُ
Wahuwa allathee yabdao alkhalqathumma yuAAeeduhu wahuwa ahwanu AAalayhi walahu
almathalu al-aAAlafee assamawati wal-ardiwahuwa alAAazeezu alhakeem
Swahili
Na Yeye ndiye anaye anzisha uumbaji, kisha ataurudisha mara nyengine. Na jambo
hili ni jepesi zaidi kwake. Naye ndiye mwenye mfano bora katika mbingu na ardhi.
Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
|
Ayah 30:28 الأية
ضَرَبَ لَكُم مَّثَلًا مِّنْ أَنفُسِكُمْ ۖ هَل لَّكُم مِّن مَّا مَلَكَتْ
أَيْمَانُكُم مِّن شُرَكَاءَ فِي مَا رَزَقْنَاكُمْ فَأَنتُمْ فِيهِ سَوَاءٌ
تَخَافُونَهُمْ كَخِيفَتِكُمْ أَنفُسَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ
لِقَوْمٍ يَعْقِلُونَ
Daraba lakum mathalan min anfusikumhal lakum mimma malakat aymanukum min
shurakaafee ma razaqnakum faantum feehi sawaon takhafoonahumkakheefatikum
anfusakum kathalika nufassilu al-ayatiliqawmin yaAAqiloon
Swahili
Amekupigieni mfano kutokana na nafsi zenu. Je! Katika hao iliyo wamiliki mikono
yenu ya kulia mnao washirika katika hivyo tulivyo kuruzukuni, mkawa nyinyi
katika hivyo ni sawasawa, mnawaogopa kama mnavyo ogopana wenyewe kwa wenyewe?
Namna hivi tunazipambanua Aya zetu kwa watu wenye akili.
|
Ayah 30:29 الأية
بَلِ اتَّبَعَ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَهْوَاءَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۖ فَمَن يَهْدِي
مَنْ أَضَلَّ اللهُ ۖ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ
Bali ittabaAAa allatheena thalamooahwaahum bighayri AAilmin faman yahdee man
adallaAllahu wama lahum min nasireen
Swahili
Bali walio dhulumu wamefuata mapendo ya nafsi zao pasina kujua. Basi nani
atamwongoa ambaye Mwenyezi Mungu amemuacha apotee? Wala hao hawatakuwa na wa
kuwanusuru.
|
Ayah 30:30 الأية
فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا ۚ فِطْرَتَ اللهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ
عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللهِ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ
وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ
Faaqim wajhaka liddeeni haneefanfitrata Allahi allatee fatara annasaAAalayha la
tabdeela likhalqi Allahi thalikaaddeenu alqayyimu walakinna akthara annasila
yaAAlamoon
Swahili
Basi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini - ndilo umbile la Mwenyezi Mungu
alilo waumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo
ndiyo Dini iliyo nyooka sawa. Lakini watu wengi hawajui.
|
Ayah 30:31 الأية
مُنِيبِينَ إِلَيْهِ وَاتَّقُوهُ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَلَا تَكُونُوا مِنَ
الْمُشْرِكِينَ
Muneebeena ilayhi wattaqoohuwaaqeemoo assalata wala takoonoomina almushrikeen
Swahili
Muwe wenye kutubia kwake, na mcheni Yeye, na shikeni Sala, na wala msiwe katika
washirikina.
|
Ayah 30:32 الأية
مِنَ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا ۖ كُلُّ حِزْبٍ بِمَا
لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ
Mina allatheena farraqoo deenahum wakanooshiyaAAan kullu hizbin bima ladayhim
farihoon
Swahili
Katika wale ambao kwamba wameigawanya dini yao, na wakawa makundi makundi, kila
kikundi kinafurahia kilicho nacho.
|
Ayah 30:33 الأية
وَإِذَا مَسَّ النَّاسَ ضُرٌّ دَعَوْا رَبَّهُم مُّنِيبِينَ إِلَيْهِ ثُمَّ إِذَا
أَذَاقَهُم مِّنْهُ رَحْمَةً إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُم بِرَبِّهِمْ يُشْرِكُونَ
Wa-itha massa annasa durrundaAAaw rabbahum muneebeena ilayhi thumma itha
athaqahumminhu rahmatan itha fareequn minhum birabbihimyushrikoon
Swahili
Yakiwapata watu madhara humwomba Mola wao Mlezi nao wametubu kwake. Kisha
akiwaonjesha rehema itokayo kwake, mara kikundi miongoni mwao humshirikisha Mola
wao Mlezi,
|
Ayah 30:34 الأية
لِيَكْفُرُوا بِمَا آتَيْنَاهُمْ ۚ فَتَمَتَّعُوا فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ
Liyakfuroo bima ataynahumfatamattaAAoo fasawfa taAAlamoon
Swahili
Kwa kuyakataa tuliyo wapa. Basi stareheni. Mtakuja jua!
|
Ayah 30:35 الأية
أَمْ أَنزَلْنَا عَلَيْهِمْ سُلْطَانًا فَهُوَ يَتَكَلَّمُ بِمَا كَانُوا بِهِ
يُشْرِكُونَ
Am anzalna AAalayhim sultananfahuwa yatakallamu bima kanoo bihi yushrikoon
Swahili
Au tumewateremshia hoja ambayo kwayo ndio wanafanya ushirikina?
|
Ayah 30:36 الأية
وَإِذَا أَذَقْنَا النَّاسَ رَحْمَةً فَرِحُوا بِهَا ۖ وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ
بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ إِذَا هُمْ يَقْنَطُونَ
Watha athaqna annasarahmatan farihoo biha wa-in tusibhumsayyi-atun bima qaddamat
aydeehim itha hum yaqnatoon
Swahili
Na watu tunapo waonjesha rehema huifurahia, na ukiwasibu uovu kwa iliyo
yatanguliza mikono yao wenyewe, mara wanakata tamaa.
|
Ayah 30:37 الأية
أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللهَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ ۚ
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ
Awa lam yaraw anna Allaha yabsutuarrizqa liman yashao wayaqdiru inna fee
thalikalaayatin liqawmin yu/minoon
Swahili
Kwani hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na humdhikisha
amtakaye? Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanao amini.
|
Ayah 30:38 الأية
فَآتِ ذَا الْقُرْبَىٰ حَقَّهُ وَالْمِسْكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ
لِّلَّذِينَ يُرِيدُونَ وَجْهَ اللهِ ۖ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ
Faati tha alqurba haqqahuwalmiskeena wabna assabeeli thalikakhayrun lillatheena
yureedoona wajha Allahi waola-ikahumu almuflihoon
Swahili
Basi mpe jamaa haki yake, na masikini, na msafiri. Hayo ni kheri kwa watakao
radhi ya Mwenyezi Mungu. Na hao ndio wenye kufanikiwa.
|
Ayah 30:39 الأية
وَمَا آتَيْتُم مِّن رِّبًا لِّيَرْبُوَ فِي أَمْوَالِ النَّاسِ فَلَا يَرْبُو
عِندَ اللهِ ۖ وَمَا آتَيْتُم مِّن زَكَاةٍ تُرِيدُونَ وَجْهَ اللهِ
فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُضْعِفُونَ
Wama ataytum min ribanliyarbuwa fee amwali annasi falayarboo AAinda Allahi wama
ataytum min zakatintureedoona wajha Allahi faola-ika humu almudAAifoon
Swahili
Na mnacho kitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki
mbele ya Mwenyezi Mungu. Lakini mnacho kitoa kwa Zaka kwa kutaka radhi ya
Mwenyezi Mungu, basi hao ndio watao zidishiwa.
|
Ayah 30:40 الأية
اللهُ الَّذِي خَلَقَكُمْ ثُمَّ رَزَقَكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ
ۖ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَفْعَلُ مِن ذَٰلِكُم مِّن شَيْءٍ ۚ سُبْحَانَهُ
وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ
Allahu allathee khalaqakumthumma razaqakum thumma yumeetukum thumma yuhyeekum
halmin shuraka-ikum man yafAAalu min thalikum minshay-in subhanahu wataAAala
AAammayushrikoon
Swahili
Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni, kisha akakuruzukuni, kisha anakufisheni, na
kisha anakufufueni. Je! Yupo yeyote katika hao mnao washirikisha na Mwenyezi
Mungu afanyae lolote katika hayo? Yeye ametakasika, na ametukuka na hayo mnayo
mshirikisha naye.
|
Ayah 30:41 الأية
ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ
لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ
Thahara alfasadu feealbarri walbahri bima kasabat aydee annasiliyutheeqahum
baAAda allathee AAamiloolaAAallahum yarjiAAoon
Swahili
Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili
Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu.
|
Ayah 30:42 الأية
قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن
قَبْلُ ۚ كَانَ أَكْثَرُهُم مُّشْرِكِينَ
Qul seeroo fee al-ardi fanthurookayfa kana AAaqibatu allatheena min qablu
kanaaktharuhum mushrikeen
Swahili
Sema: Safirini duniani muangalie ulikuwaje mwisho wa walio tangulia. Wengi wao
walikuwa washirikina.
|
Ayah 30:43 الأية
فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ الْقَيِّمِ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا
مَرَدَّ لَهُ مِنَ اللهِ ۖ يَوْمَئِذٍ يَصَّدَّعُونَ
Faaqim wajhaka liddeeni alqayyimimin qabli an ya/tiya yawmun la maradda lahu
mina Allahiyawma-ithin yassaddaAAoon
Swahili
Basi uelekeze uso wako kwenye Dini Iliyo Nyooka kabla ya kufika Siku hiyo isiyo
zuilika, inayo toka kwa Mwenyezi Mungu. Siku hiyo watu watatengana.
|
Ayah 30:44 الأية
مَن كَفَرَ فَعَلَيْهِ كُفْرُهُ ۖ وَمَنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِأَنفُسِهِمْ
يَمْهَدُونَ
Man kafara faAAalayhi kufruhu waman AAamila salihanfali-anfusihim yamhadoon
Swahili
Anaye kufuru basi ukafiri wake utakuwa juu yake mwenyewe, na anaye tenda mema,
basi wanazitengezea nafsi zao.
|
Ayah 30:45 الأية
لِيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِن فَضْلِهِ ۚ إِنَّهُ لَا
يُحِبُّ الْكَافِرِينَ
Liyajziya allatheena amanoowaAAamiloo assalihati min fadlihiinnahu la yuhibbu
alkafireen
Swahili
Ili awalipe walio amini na wakatenda mema kutokana na fadhila yake. Hakika Yeye
hawapendi makafiri.
|
Ayah 30:46 الأية
وَمِنْ آيَاتِهِ أَن يُرْسِلَ الرِّيَاحَ مُبَشِّرَاتٍ وَلِيُذِيقَكُم مِّن
رَّحْمَتِهِ وَلِتَجْرِيَ الْفُلْكُ بِأَمْرِهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ
وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ
Wamin ayatihi an yursila arriyahamubashshiratin waliyutheeqakum min
rahmatihiwalitajriya alfulku bi-amrihi walitabtaghoo min fadlihiwalaAAallakum
tashkuroon
Swahili
Na katika Ishara zake ni kuzituma pepo ziletazo bishara njema, na ili
kukuonjesheni baadhi ya rehema zake, na ili majahazi yende kwa amri yake; na
mtafute kutokana na fadhila yake, na ili mumshukuru.
|
Ayah 30:47 الأية
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ رُسُلًا إِلَىٰ قَوْمِهِمْ فَجَاءُوهُم
بِالْبَيِّنَاتِ فَانتَقَمْنَا مِنَ الَّذِينَ أَجْرَمُوا ۖ وَكَانَ حَقًّا
عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ
Walaqad arsalna min qablika rusulanila qawmihim fajaoohum bilbayyinatifantaqamna
mina allatheena ajramoo wakanahaqqan AAalayna nasru almu/mineen
Swahili
Na hakika tulikwisha watuma Mitume kwa kaumu zao, na wakawajia kwa hoja zilizo
wazi. Tukawaadhibu wale walio fanya ukosefu. Na ilikuwa ni haki juu yetu
kuwanusuru Waumini.
|
Ayah 30:48 الأية
اللهُ الَّذِي يُرْسِلُ الرِّيَاحَ فَتُثِيرُ سَحَابًا فَيَبْسُطُهُ فِي
السَّمَاءِ كَيْفَ يَشَاءُ وَيَجْعَلُهُ كِسَفًا فَتَرَى الْوَدْقَ يَخْرُجُ مِنْ
خِلَالِهِ ۖ فَإِذَا أَصَابَ بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ إِذَا هُمْ
يَسْتَبْشِرُونَ
Allahu allathee yursilu arriyahafatutheeru sahaban fayabsutuhu fee assama-ikayfa
yashao wayajAAaluhu kisafan fatara alwadqayakhruju min khilalihi fa-itha asaba
bihiman yashao min AAibadihi itha humyastabshiroon
Swahili
Mwenyezi Mungu ndiye anaye zituma pepo zikayatimua mawingu, kisha akayatandaza
mbinguni kama apendavyo. Na akayafanya mapande mapande, basi ukaiona mvua
inatoka ndani yake. Anapo wafikishia awatakao katika waja wake, mara hao huwa na
furaha.
|
Ayah 30:49 الأية
وَإِن كَانُوا مِن قَبْلِ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْهِم مِّن قَبْلِهِ لَمُبْلِسِينَ
Wa-in kanoo min qabli an yunazzalaAAalayhim min qablihi lamubliseen
Swahili
Na ingawa kabla ya kuteremshiwa walikuwa wenye kukata tamaa.
|
Ayah 30:50 الأية
فَانظُرْ إِلَىٰ آثَارِ رَحْمَتِ اللهِ كَيْفَ يُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ
مَوْتِهَا ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ
قَدِيرٌ
Fanthur ila atharirahmati Allahi kayfa yuhyee al-ardabaAAda mawtiha inna thalika
lamuhyee almawtawahuwa AAala kulli shay-in qadeer
Swahili
Basi ziangalie athari za rehema ya Mwenyezi Mungu, jinsi anavyo ihuisha ardhi
baada ya kufa kwake. Basi hakika huyo ndiye bila ya shaka Mwenye kuhuisha wafu.
Na Yeye ni Muweza wa kila kitu.
|
Ayah 30:51 الأية
وَلَئِنْ أَرْسَلْنَا رِيحًا فَرَأَوْهُ مُصْفَرًّا لَّظَلُّوا مِن بَعْدِهِ
يَكْفُرُونَ
Wala-in arsalna reehanfaraawhu musfarran lathalloo min baAAdihiyakfuroon
Swahili
Na tunge utuma upepo na wakauona umekuwa rangi ya manjano, juu ya hayo wange
endelea kukufuru.
|
Ayah 30:52 الأية
فَإِنَّكَ لَا تُسْمِعُ الْمَوْتَىٰ وَلَا تُسْمِعُ الصُّمَّ الدُّعَاءَ إِذَا
وَلَّوْا مُدْبِرِينَ
Fa-innaka la tusmiAAu almawtawala tusmiAAu assumma adduAAaaitha wallaw mudbireen
Swahili
Kwani wewe hakika huwafanyi maiti wakasikia, wala viziwi wakasikia wito wakisha
geuka kukupa mgongo.
|
Ayah 30:53 الأية
وَمَا أَنتَ بِهَادِ الْعُمْيِ عَن ضَلَالَتِهِمْ ۖ إِن تُسْمِعُ إِلَّا مَن
يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا فَهُم مُّسْلِمُونَ
Wama anta bihadi alAAumyi AAandalalatihim in tusmiAAu illa man yu/minu
bi-ayatinafahum muslimoon
Swahili
Wala wewe huwaongoi vipofu na upotovu wao. Huwasikilizishi ila wanao ziamini Aya
zetu. Hao ndio Waislamu, walio nyenyekea.
|
Ayah 30:54 الأية
اللهُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن ضَعْفٍ ثُمَّ جَعَلَ مِن بَعْدِ ضَعْفٍ قُوَّةً
ثُمَّ جَعَلَ مِن بَعْدِ قُوَّةٍ ضَعْفًا وَشَيْبَةً ۚ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۖ
وَهُوَ الْعَلِيمُ الْقَدِيرُ
Allahu allathee khalaqakum mindaAAfin thumma jaAAala min baAAdi daAAfin
quwwatanthumma jaAAala min baAAdi quwwatin daAAfan washaybatanyakhluqu ma yashao
wahuwa alAAaleemu alqadeer
Swahili
Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni kutokana na udhaifu kisha akajaalia nguvu
baada ya unyonge, kisha akajaalia baada ya nguvu unyonge tena na ukongwe.
Anaumba atakavyo. Naye ndiye Mjuzi, Mwenye uweza.
|
Ayah 30:55 الأية
وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يُقْسِمُ الْمُجْرِمُونَ مَا لَبِثُوا غَيْرَ سَاعَةٍ
ۚ كَذَٰلِكَ كَانُوا يُؤْفَكُونَ
Wayawma taqoomu assaAAatuyuqsimu almujrimoona ma labithoo ghayra saAAatin
kathalikakanoo yu/fakoon
Swahili
Na siku itapo simama Saa wakosefu wataapa kwamba hawakukaa duniani ila saa moja
tu. Hivyo ndivyo walivyo kuwa wakipotozwa.
|
Ayah 30:56 الأية
وَقَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ وَالْإِيمَانَ لَقَدْ لَبِثْتُمْ فِي كِتَابِ
اللهِ إِلَىٰ يَوْمِ الْبَعْثِ ۖ فَهَٰذَا يَوْمُ الْبَعْثِ وَلَٰكِنَّكُمْ
كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ
Waqala allatheena ootooalAAilma wal-eemana laqad labithtum fee kitabiAllahi ila
yawmi albaAAthi fahatha yawmualbaAAthi walakinnakum kuntum la taAAlamoon
Swahili
Na walio pewa ilimu na Imani watasema: Hakika nyinyi mlikwisha kaa katika hukumu
ya Mwenyezi Mungu mpaka Siku ya kufufuliwa. Basi hii ndiyo Siku ya kufufuliwa!
Lakini nyinyi mlikuwa hamuijui.
|
Ayah 30:57 الأية
فَيَوْمَئِذٍ لَّا يَنفَعُ الَّذِينَ ظَلَمُوا مَعْذِرَتُهُمْ وَلَا هُمْ
يُسْتَعْتَبُونَ
Fayawma-ithin la yanfaAAu allatheenathalamoo maAAthiratuhum wala
humyustaAAtaboon
Swahili
Basi Siku hiyo hautawafaa walio dhulumu udhuru wao, wala haitotakiwa toba yao.
|
Ayah 30:58 الأية
وَلَقَدْ ضَرَبْنَا لِلنَّاسِ فِي هَٰذَا الْقُرْآنِ مِن كُلِّ مَثَلٍ ۚ وَلَئِن
جِئْتَهُم بِآيَةٍ لَّيَقُولَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ أَنتُمْ إِلَّا
مُبْطِلُونَ
Walaqad darabna linnasifee hatha alqur-ani min kulli mathalin wala-inji/tahum
bi-ayatin layaqoolanna allatheena kafarooin antum illa mubtiloon
Swahili
Na hakika tulikwisha wapigia watu kila mfano katika hii Qur'ani. Na ukiwaletea
Ishara yoyote hapana shaka walio kufuru watasema: Nyinyi si chochote ila ni
waongo.
|
Ayah 30:59 الأية
كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ اللهُ عَلَىٰ قُلُوبِ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ
Kathalika yatbaAAu AllahuAAala quloobi allatheena la yaAAlamoon
Swahili
Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo piga muhuri kwenye nyoyo za wasio jua.
|
Ayah 30:60 الأية
فَاصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ اللهِ حَقٌّ ۖ وَلَا يَسْتَخِفَّنَّكَ الَّذِينَ لَا
يُوقِنُونَ
Fasbir inna waAAda Allahihaqqun wala yastakhiffannaka allatheena layooqinoon
Swahili
Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki. Wala wasikupaparishe hao
wasio kuwa na yakini.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|