Hawana akaunti bado? Unaweza kujenga mmoja. Kama Mtumiaji aliyesajiliwa unaweza kuwa na baadhi ya faida kama meneja wa mandhari, comments Configuration na maoni post kwa jina yako.
Makatazo Ya Kishari’ah Kwa Wanawake – 6
Katazo La
Kujipiga piga Na Kuchana Nguo Wakati Wa Msiba
Katazo la Kuingia katika Hammamaat [sehemu za
kuogea zilizojengewa kama vile mahodhi mabwawa na kadhalika na kuruhusiwa
kutumiwa na kila mtu].
Jamii nyingi huweka sehemu ambazo huwa zinaruhusiwa
kutumiwa na kila mtu kwa malengo tofauti kama vile mabustani, maduni na
kadhalika; pia hutenga sehemu nyingine ili zitumike kwa malengo maalumu; kama
vile sehemu za kuogea au kuogolea, au sehemu za kuumika, au sehemu za kukandwa,
au sehemu za kutengenezwa nyuso au nywele, au sehemu za kupambwa, au sehemu za
kubadilisha mavazi au kujilinga, au sehemu za kupumzika, au sehemu za kufua nguo
na kadhalika.
Sehemu hizi katika baadhi ya jamii huwa ziko
zilizotengwa maalumu kwa wanawake na kutenganishwa na za wanaume, na katika
jamii nyingine huwa hakuna mtengano katika sehemu kama hizo; hivyo utaona baadhi
ya jamii hata katika hospitali zao huwa wanawaweka wagonjwa wa kike na wa kiume
katika chumba kimoja na chenye kuwatenganisha huwa ni pazia tu, na wako wenye
kudai kutaka kuweko choo cha wote [wake kwa waume] bila ya mtengano.
((Hakika Waislamu
wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na watiifu
wanaume na watiifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wasemao kweli wanawake,
na wanaosubiri wanaume na wanaosubiri wanawake, na wanyenyekevu wanaume na
wanyenyekevu wanawake, na watoao sadaka wanaume na watoao sadaka wanawake, na
wanaofunga wanaume na wanaofunga wanawake, na wanaojihifadhi tupu zao wanaume na
wanawake na wanaomdhukuru Allah kwa wingi wanaume na wanawake, Allah
Amewaandalia msamaha na ujira mkubwa)) [Al-Ahzaab:35]
Kama tunavyoona katika Aayah hiyo tukufu kwamba kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa
Ta'ala) kwa wingi ni sifa ya kumi na ya mwisho; mja atakapoweza kuzichuma sifa
zote hizo kumi basi malipo yake yatakuwa ni kusamehwa madhambi yao na kulipwa
thawabu nyingi kabisa.
Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa
“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”
Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - MIFANO
YA WANAWAKE WATUKUFU
(Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)
Kilichochapishwa Na Daarul Arqam,
Chapa Ya Pili,
MIFANO YA WANAWAKE WATUKUFU
UMMUL MU’MININA ‘AISHAH BINT ABUBAKR AS-SIDDIQ:
Alizaliwa mwaka wa 4 Baada ya Utume (614 BI). Babake alikuwa ni ‘AbdAllaah bin
‘Uthman bin ‘Aamir at-Taymi au Abu Bakr as-Siddiq bin Abi Quhafah. Mamake
alikuwa Umm Ruman bint ‘Aamir bin ‘Uwaymir al-Kananiyah. ‘Aishah (Radhiya
Allaahu ‘anha) alikuwa ni msomi, mwenye akili, uoni wa hali ya juu na uwezo wa
kutatua mambo nyeti na mazito ya Dini. Alikuwa msitari wa mbele katika upokeaji
wa Hadithi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), nambari sita
miongoni mwa Masahaba wote (Radhiya Allaahu ‘anhum).
Amepokea Hadithi 2,220, miongoni mwa hizo 174 zikiwa ni Muttafaqun ‘alayhi, 54
katika al-Bukhari, 67 katika Muslim, na 2,017 katika vitabu vyengine vya Hadithi.
Alikuwa mjuzi sana katika elimu za Qur’ani, Hadithi, Fikihi, Mashairi, Historia
na Nasaba. Anahesabiwa miongoni mwa Mujtahid na jina lake linatajwabila ya shaka
pamoja na yale ya Abu bakr, ‘Umar, ‘Athman, ‘Ali, Ibn Mas‘ud, Ibn ‘Abbas na Ibn
‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhum). Alikuwa akitoa fatwa wakati wa Abu Bakr, ‘Umar
na ‘Athman.
‘Aishah (Radhiya Allaahu ‘anha) alikuwa na fadhila kubwa kuliko wanawake wote.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Ubora wa ‘Aishah
kulinganisha na wanawake wengine ni kama ubora wa tharid kwa aina nyengine ya
vyakula”.
Msamaha Na Ujira Mkubwa Tutakaopata Baada Ya Kuzichuma Sifa Kumi Njema
Baada kukumbushana maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika Aayah tukufu
iliyotaja sifa kumi njema, tumeona kwamba mwisho kabisa Allaah (Subhaanahu wa
Ta'ala) Anasema:
((أَعَدَّ اللَّهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا))
((Allah Amewaandalia msamaha na ujira mkubwa)) [Al-Hazab:35]
Vile vile Anasema katika Aayah nyingine:
((وَعَدَ اللّهُ الَّذِينَ آمَنُواْ وَعَمِلُواْ الصَّالِحَاتِ
لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌ))
((Allah Amewaahidi waliomuamini na wakatenda mema kwamba watapata maghfira na
malipo makubwa)) [Al-Maaidah]
Maana kwamba;
Tutasamehewa Madhambi yetu ambayo hakuna aliyeepukana nayo, lakini Mola wetu ni
Mkarimu Mwingi Wa Kurehemu na Mwingi wa Msamaha Hukubali toba zetu wakati wowote
kama Anavyotuahidi katika Qur-aan na pia katika Hadiyth za Mtume (Swalla Allahu
'alayhi wa aalihi wa sallam):
Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa
“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”
Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - HAJA
YETU YA MWANAMKE MUISLAMU MWENYE MUAMKO
Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)
Kilichochapishwa Na Daarul Arqam,
Chapa Ya Pili,
HAJA YETU YA MWANAMKE MUISLAMU MWENYE MUAMKO
Bila ya shaka, Ummah wa Kiislamu unahitaji wanawake wasomi wenye kufanya kazi
ambao watasimama katikakujenga watoto watakaoshiriki katika muelekeo
uliobarikiwa na muamko na kuelewa majukumu yao.
Hamu yao ni kuzitakasa nafsi zao na za waume wao, watoto wao na kila
kitakachorudisha katika Ummah wa Kiislamu nguvu na utukufu.
Jambo hili ni wajibu
liwe katika akili yake anapolala na kuamka na wala asiwe ni mwenye
kushughulishwa na mambo mengi ya Maisha ambayo yamewasahaulisha kuhusu ndugu zao
Waislamu na dini yao.
Ni vizuri sana muamko wao uzinduliwe katika kutekeleza na kuwasaidia Waislamu
wenziwao na Uislamu kwa nia mzuri, ikhlasi na kutaka ridhaa ya Allaah (Subhaanahu
Wa Ta’ala).
Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa
“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”
Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - DURU
YA WANAWAKE WA MWANZO KATIKA KUSOMA NA KUENEZA ELIMU
(Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)
Kilichochapishwa Na Daarul Arqam,
Chapa Ya Pili,
DURU YA WANAWAKE WA MWANZO KATIKA KUSOMA NA KUENEZA ELIMU
Hakika duru ya mwanamke Muislamu katika historia ya Uislamu, historia ya Da‘wah
na historia ya mataifa na watu imesajili upeo wa ubora, utukufu na utakaso
katika nyaraka. Sote tunajua na kuelewa yale aliyoyafanya Mama wa Waumini Bibi
‘Aishah bint Abubakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) katika kuhifadhi Hadithi nyingi
pamoja na kuzisomesha. Huyu bibi mtukufu alikuwa anaulizwa maswali mengi na
wakubwa miongoni mwa Masahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) katika mambo mengi ya
dini.
Historia ya Kiislamu imesajili kwa herufi za nuru na dhahabu majina ya Sahabiyat
watukufu (Radhiya Allaahu ‘anhum) mfano wa Asmaa bint Abubakr, Umm ‘Atiyyah al-Ansariyah,
Umm Kabshah Qadha‘iyah, Asmaa bint ‘Umays, Umm Sulaym bint Milhan, Umm Dardaa na
fatimah bint Qays (Radhiya Allaahu ‘anha), wote walikuwa wapokezi na waalimu wa
Hadithi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa
“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”
Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - ELIMU
ANAZOPASWA KUSOMA MWANAMKE
(Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)
Kilichochapishwa Na Daarul Arqam,
Chapa Ya Pili,
ELIMU ANAZOPASWA KUSOMA MWANAMKE1 KUSAHIHISHA UFAHAMU MBAYA:
Huenda wakaona baadhi ya watu kuwa mwanamke wa Kiislamu hana uwezo wa kusoma na
kusomesha. Na kuwa kuna vikwazo vya kisheria ya dini ya Kiislamu vinavyozuia
harakati zake katika jambo hili. Muono huu ni wa makosa unaotokana na ufahamu
mbaya wa Uislamu, kwani Uislamu ni nidhamu kamili ya Maisha. Yule anayeangalia
kwa kina hali ya mwanamke na harakati zake katika chimbuko la Uislamu na duru
yake katika historia kuanzia hasa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa
aalihi wa sallam) na Makhalifa Waongofu (Radhiya Allaahu ‘anhum) ataona hayo.
Kinachotakikana leo kutoka kwa mwanamke Muislamu ni kujinyanyua kwa kila njia
ili atekeleze majukumu yake ya kihistoria na kuutengeneza Ummah.
2 MASHARUTI YA MUAMKO:
Uislamu umempatia mwanamke na mwanamume amana ya Dini ambayo ni amana muhimu
katika Maisha, bali ndio nguzo na msingi. Uislamu ulimjaalia kila mmoja ni
mchungaji hasa katika kusahihisha na kuweka sawa ‘Aqiydah yake, ibadah zake,
maadili yake na amali zake. Yule ambaye hatasoma hukumu za ‘ibadah na
mafungamano na mahusiano na Allaah na mfumo wa utamaduni … na yule asiyesoma
Misingi ya ‘aqiydah na asiye dhamini falsafa ya kweli na muelekeo wa jamii na
ubora wa maadili na malengo ya maisha na misingi ya adabu, asiyesoma au
kufundishwa haya na yote ni katika milango ya elimu na yenye kuondosha mateso ya
ujinga na giza la hisia na maaddah ameingia katika dhambi la kupunguza. Na hapo
ameitia nafsi yake katika kazi ya kubaki myuma katika ulimwengu na Akhera.
Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa
“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”
Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - MSIMAMO
WA UISLAMU KATIKA KUSOMESHA WANAWAKE
(Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)
Kilichochapishwa Na Daarul Arqam,
Chapa Ya Pili,
MSIMAMO WA UISLAMU KATIKA KUSOMESHA WANAWAKE
1 WAJIBU WA KUSOMESHWA WANAWAKE:
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kutafuta elimu ni
faradhi (lazima) kwa kila Muislamu”. Tunaona kuwa mwanamke yumo ndani katika
ujumla wa Hadithi kwani Muislamu anakuwa mume au mke na wote ni sawa. Yeyote
atakaye ingia katika hukumu za kisheria ataona kuwa kwa hakika wanawake ni ndugu
za wanaume wala hawana hukumu hasa kwao wao ila baadhi ya hukumu
zinazotofautisha baina ya maumbile ya wanaume na wanawake.
Asili ni kuunganisha sheria na ujumla wa maneno wala haijathubutu utofauti ila
kwa dalili. Mwanamke ni sawa na mwanamume katika majukumu ya ibadah za kinafsi (Dhikri,
Swalah, Swaumu, Zakah, Hajj, n.k.) na katika maadili na mahusiano (ukweli,
uadilifu, wema, taqwa na adabu) na Maisha kwa ujumla (subira, hijrah, kinyume
cha ukafiri, twaa, kuwa pamoja na kikundi cha Waumini, urafiki na usaidizi).
Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa
“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”
Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - ELIMU
ANAZOPASWA KUSOMA MWANAMKE
(Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)
Kilichochapishwa Na Daarul Arqam,
Chapa Ya Pili,
ELIMU ANAZOPASWA KUSOMA MWANAMKE
1 SEHEMU YA ELIMU:
Elimu katika Uislamu ina sehemu na daraja ambayo haijapatiwa na dini nyengine
yeyote. Hii tunaiona wazi katika aya tukufu inayosema, “Soma kwa jina la Mola
wako Aliyeumba”. Kama alivyosema tena Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala),
“Sema: ‘Je, wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?”
Dini ambayo maagizo yake ya kwanza ni kusoma na elimu ni dini ambayo inataka
wafuasi wake wawe msitari wa mbele katika kusambaza elimu. Huu kwa hakika ni
mfumo wa Mola, Ambaye ameifanya elimu kuwa faradhi (lazima) kama ilivyokuja
katika Hadithi. Imepokewa na Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, “Kutafuta elimu ni
faradhi kwa kila Muislamu”. Lafdhi ya Muslim (Muislamu) ina makusudio ya wanaume
na wanawake kwani imewachang’anya wote bila kubagua.
Shaykh 'Abdullaah 'Adhamiy
Imefasiriwa na Iliyaasa
Muenzi Mke Wako
Kwa kuoa huchukui tu mke, Bali unachukua ulimwengu wako mzima. Kuanzia hapo
mpaka maisha yako yote mke wako atakuwa mwenzio, mwandani wako, na rafiki yako
mpenzi.
Atashiriki katika nyakati zako nzuri, siku zako, na miaka yako. Atakuwa pamoja
nawe katika furaha na shida, katika mafanikio na tabu, katika ndoto zako na
katika wakati wa hofu. Ukiumwa, atakupa huduma bora kabisa. Wakati unapohitaji
msaada atafanya vyovyote awezavyo kwa ajili yako. Wakati una siri, ataitunza
siri yako, wakati unahitaji ushauri, atakupa ushauri mzuri kabisa.
Atakuwa na wewe utakapoamka asubuhi kitu cha kwanza ambacho macho yako yataona
ni macho yake.
Wakati wa mchana, atakuwa na wewe, kama kuna wakati mchache
hatokuwa na wewe kwa kimwili, atakuwa anakufikiria wewe, anakuombea dua kwa moyo
wake wote, akili yake yote, na roho yake nyote. Ukienda kulala usiku, kitu cha
mwisho macho yako kuona itakuwa ni yeye, na ukilala bado utakuwa unamuona katika
ndoto zako. Kwa kifupi atakuwa ni ulimwengu wako mzima na wewe utakuwa ulimwengu
wake mzima.
Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa
Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - UTANGULIZI
“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”
(Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)
Kilichochapishwa Na Daarul Arqam, Chapa Ya Pili,
1.0 UTANGULIZI
Sifa zote njema anastahiki Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala), ambaye Ameumba
wanadamu, Akawaongoza na Kuwafundisha kwa kutumia kalamu. Akawaongoza pia kwa
yale wasio yajua. Swalah na salamu zimshukie yule Aliyetumwa kuwa rehema kwa
walimwengu Nabii wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na
juu ya ahli zake na swahaba zake na waliomfuata miongoni mwa watu.
Shaykh Muhammad 'Abdul-Haliym Haamid
Imetarjumiwa na Ummu Ummu Ayman..
Ili kusaidia familia za Kiislam na kueneza mafundisho ya Uislam katika kujenga
familia, MSA (Muslim Students Association) katika Chuo Kikuu cha Alberta,
Canada, kimetayarisha ufupisho wa tafsiri ya vitabu viwili. Vitabu katika lugha
ya kiarabu vilivyotungwa na Shaykh Muhammad 'Abdul-Haliym Haamid. Mwanachuoni wa
Kimisri, ambaye amemaliza masomo yake katika chuo cha Islamic University cha
Madiyna An-Nabiwiyyah huko Saudi Arabia. Vitabu vyenyewe ni :
1. Namna ya kumfurahisha Mkeo
2. Namna ya kumfurahisha Mumeo
Hivi ni vitabu vizuri kabisa vya Kiarabu ambavyo tumeviona katika
somo hili. Vimekwenda mbali katika kuelezea, kuanzia haki
na wajibu mpaka adaab (tabia njema) na kwenda mbali katika
kutekeleza haki hizi katika maisha ya kila siku. Ufupisho ufuatao unamulika
zaidi katika majukumu ya nini kinaweza au kinachotakiwa kifanywe. Kila jambo
lililotajwa na muandishi limeegemezwa katika ushahidi wa Qur-aan, Sunnah au
matendo ya Maswahaba, bali ushahidi haukuwekwa katika tafsiri hii. Ifuatayo ni
tafsiri ya kitabu cha kwanza.
Imefasiriwa na Ummu 'Abdil-Wahhaab
Vidokezo Muhimu Kwa Wazazi Wenye Wasichana Na Wavulana
((ALHIDAAYA imerekebisha baadhi ya majina na usemi ili makala ifahamike vizuri
na Jamii yetu))
NINI WAZAZI WAFANYE ILI VIJANA WAO WAWE NI WAISLAMU WENYE KUTEKELEZA UISLAMU KWA
VITENDO?
1. Yatilie Bidii Malezi Kuliko Hata Kazi Yako Ya Kutwa NzimaHii ina maana kwamba wazazi wote wawili ni lazima waelewe kuwa watoto wao ni wa kweli kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), na baba atakuja kuulizwa vipi kawalea watoto wake. Ikiwa watoto wao hawatokulia katika kuutekeleza Uislamu kwa sababu ya mapuuza ya wazazi wao, halitokuwa ni jambo la kukubalika kwa maisha ya hapa duniani na hata ya baadae.
2. Punguza Au Badilisha Masaa Ya Kazi Kwa Ajili Ya Kupata Muda Wa Kuwa Pamoja Na Familia YakoNi bora kuwa na kazi moja yenye muda wa kudumu, anasa chache katika nyumba (yaani sio magari mengi, nguo za gharama nyingi, nyumba kubwa ya fakhari, televisheni kila pahali), na muda zaidi wa kuwa pamoja na familia, kuliko kuwa na mambo mengi ya anasa na kukakosekana malezi. Haya yote yanawahusu mababa na mamama. Wazazi hawawezi kuwafunza watoto wao bila ya wao kuwepo nao kikawaida. Acha kazi za ziada kwenye siku za mwisho wa wiki au kazi za jioni na badala yake nenda na watoto msikitini kwa ajili ya Halaqah (darsa za dini) na shughuli nyenginezo. Au tilia maanani kugeuza nyakati za kazi ili uwe nyumbani wakati ambao watoto wapo.
Umoja wa Kiislamu wa Elimu Uchumi na Maendeleo Zanzibar
Hikma
Ya Ruhusa Ya Ukewenza: Umoja wa Kiislamu wa Elimu Uchumi na Maendeleo Zanzibar
Kuna sababu nyingi za kibinafsi, kimaadili, kiuchumi na kijamii zinazoonesha kuwa wakati mwengine kuoa mke zaidi ya mmoja ni jambo lisilobudi.
Kabla ya kulieleza jambo hili ni vyema tukaelewa nini maana hasa ya ndoa (Nikaah) katika Uislam. Ndoa ni mkataba ('Aqd) wa hiari kati ya mume na mke wa kuishi pamoja kwa wema na upendo kufuatana na masharti na taratibu zilizowekwa na sheria ya Kiislam.
Kwani umuhimu wa ndoa kwa mtazamo wa Uislam ni jambo lililokokotezwa sana kutokana na umuhimu wake katika kujenga na kuendeleza jamii. Kama Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Alivyosema katika kitabu Chake kitukufu cha Qur-aan Suratun-Nuur, Aayah ya 32:
Fadhila Za Hijaab: Hijaab ni ‘Iffah (Stara), Hijaab ni Twahara (Utakaso), Hijaab Ni Ngao, Hijaab ni Taqwah (Ucha Mungu), Hijaab Ni Iymaan, Hijaab ni Hayaa, Hijaab ni (Ghiyrah) Ghera
Hijaab ni tendo tiifu kwa Allaah na kwa Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) kasema katika Qur-aan;
{{Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Allaah na Mtume Wake wanapokata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Allaah na Mtume Wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.}} Al-Ahzaab: 36
Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) pia kasema;
{{Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unaodhihirika. Na waangushe shungi zao (juyuubihinna) juu ya vifua vyao}} An-Nuur: 31
Mama…Kisha Mama…Kisha Mama: Ni Mama Yako Ewe Mja Wa Allaah - Waja Wema Na Kuamiliana Kwao Na Mama
Tutakuwa pamoja nanyi tukizungumzia moyo wenye huruma, moyo wenye ulaini, moyo ulio umbiwa huruma. Tutakuwa tukizungumzia moyo ambao umeumbwa siku ulipoumbwa, ukapandikizwa huruma, tutakuwa na moyo wenye kuhurumia hata kama unafanyiwa ukali. Je, mmeufahamu moyo huo? Hakika si mwingine bali moyo huo ni mama.
Tunamzungumzia mama ambaye maadui wa Allaah wamemuwekea siku moja tu na wakaiita "siku ya mama" na hili si katika Uislamu kwa chochote. Uislamu umeamrisha kumfanyia wema mama (kila siku) mwaka mzima.
Huyo ndiye mama enyi waja wa Allaah. Kiumbe ambaye ameendelea kuwa mbele na mshindi daima.
Eda ni kipindi anachokaa mwanamke aliyeachika au aliyefiwa na mumewe, na baada ya kipindi hicho ndoa yake huwa halali. Na imeitwa eda kwa jina hili kutokana na jina la kiarabu ‘iddah’ kwa kukusanya kwake (idadi) ya miezi au ‘quruu’ [1] au hedhi au vipindi vya tohara ya hedhi.
HEKIMA YA KUHALALISHWA EDA Hapa tunaona baadhi ya mawazo ya wanachuoni ambao wameona hizi ndizo hekima au sababu za kuwekewa eda shari'ah, ingawa hekima ya mwanzo na ya mwisho ni hiyo ya mwisho hapo chini ya fungu hili: •Kutambua kama mwanamke ni mjamzito au la. •Kuweza kubainika nasaba au kizazi ili kuepusha utata wa kutokujulikana nani ndiye baba.
Amri kuu aliyopatiwa mwanamke wa Kiislamu inayomtofautisha na ndugu yake wa kiume ni ile inayosema: "Ee Mtume! Waambie wake zako, na binti zako, na wanawake wa Kiislamu wajiteremshie uzuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapelekea upesi wajulikane wasiudhiwe." (Suratul-Ahzaab: 59)
Vipi kuvaa nguo leo hii imekuwa viroja kwa Waislam? Kwani wamesahau mavazi yao, leo imekuwa watafuta kila mavazi kisha tunasema yetu, kisa tumejisahau lipi lililotulazimu kwetu na lililo muhimu kwetu na kwa Mola wetu?
Imefasiriwa Na: Ummu Ahmad MANUFAA KATIKA NDOA 1. Kupata kizazi ambacho kwanza kitasaidia katika ujengaji wa jamii, pili kueneza jinsia ya watu wa kila kabila au mataifa mbali mbali, na kubwa zaidi ni kuongeza idadi ya kizazi cha jamii ya kiislamu. 2. Kumridhisha Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa kueneza idadi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika hadithi sahihi: “Oeni wake wema muwapendao na wataowapatia kizazi chema, kwani siku ya Qiyaamah nitajivunia ukubwa wa umati wangu.” [Ahmad] 3. Kupata baraka za mtoto mwema ambaye atakayemsomea dua mzee wake (atakapofariki). Maneno haya yamethibitishwa na Hadiyth maarufu inayosema kuwa: “Binaadamu anapokufa, basi ‘amali zake nzuri hukatika au humalizika, isipokuwa mambo matatu makuu nayo ni: Sadaka yenye kuendelea, Elimu yenye kunufaisha na Mtoto mwema atakayemuombea du’aa mzee/wazee wake.” [Riyadhus-Swaalihiyn] Faida nyenginezo zipatikanazo katika ndoa ni:
رسالة إلى المرأة: Ujumbe Kwa Mwanamke 'Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Mfasiri: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
Bismi Allaahi Ar-Rahmaani Ar-Rahiym. Alhamdu Allaahi Rabil 'Aalamiyn. Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad (swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na ahli zake na Maswahaba wake kwa jumla (radhiya Allaahu ´anhum). Tumesikia kwenye hizi khutbah mbili zenye baraka khayr nyingi kutoka kwa Khatwiyb wetu - Allaah Ampe mafanikio. Kazungumzia masuala ya khatari, nayo ni masuala ya mwanamke. Mwanamke enyi ndugu! Allaah Kamuumba kwa lengo kubwa katika maisha haya, kama Alivyomuumba mwanaume. Na kila mmoja ana umuhimu [kazi] Yake. Mwanaume ana kazi yake na mwanamke ana kazi yake. Kila mmoja akishikamana na kazi yake na kuitimiza, jamii itafikia khayr kubwa. Na ikiwa nidhamu itayumbishwa, ndiyo kunatokea kasoro nyingi. Kama mlivyosikia jukumu la mwanamke wakati wa Ujaahiliyyah (kabla ya kuja Uislamu), na jukumu lake leo kwenye miji ya kikafiri na kwa Waislamu wenye misimamo.
Muftiy al-´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aal ash-Shaykh Mfasiri: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
Himidi zote zi Zake Allaah. Tunamhimidi na kumtaka msaada na tunamuomba msamaha na tunatubia Kwake. Na tunajikinga Kwake na shari za nafsi zetu na matendo yetu maovu. Hakika yule Aliyemuongoza Allaah hakuna wa kumpoteza. Na Aliyempoteza hakuna wa kumuongoza. Nashuhudia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allaah wa pekee Asiyekuwa na mshirika. Na ninashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake swalah za salaam zimuendee na ahli zake na Maswahaba wake mpaka siku ya mwisho. Amma ba´ad:
Kwanza kabisa, ijulikane wazi kwamba kusudio la makala hii si kutoa fatwa wala hukumu. Lengo ni kuweka wazi manufaa na madhara ya Facebook ili mtu binafsi atoe hukumu yake mwenyewe. Je, ni Facebook au Fitnabook? Hili ni suali ambalo watu wengi wameanza kujiuliza baada ya kujionea vitimbi na kashfa kadhaa katika huu mtandao ambao unazidi kujipatia umaarufu kila pembe ya dunia. Naam, kuna vitimbi kadhaa vinafanyika kwa jina la Facebook. Na ndio kuna vijana wengi ambao wametumbikia katika janga la fitna katika Facebook lakini nini suluhisho la hili? Kabla hatujatazama hebu kwanza tuangalie manufaa na madhara ya Facebook.
Shaykh ´Abu ´Abdul-Haliym ´Abdul-Haadiy Mfasiri: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
Waja wa Allaah! Ninawausia baada ya kuiusia nafsi yangu kumcha Allaah, ndiyo zawadi yetu ya kukutana na Allaah.Anasema Allaah (Ta´ala): وَتَزَوَّدُواْ فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَى وَاتَّقُونِ يَا أُوْلِي الأَلْبَابِ “Na jitengezeeni zawadi. Na hakika bora yazawadi ni ucha Mungu. Na nicheni Mimi, enyi wenye akili!” (02:197) Na anasema Mtume ( :( صلى لله عليه وسلم "Muogope Allaah popote ulipo, na lifutishe ovu [baya] kwa jema, na tangamana na watu kwa tabia zilizo njema."
Katazo La Kujipiga piga Na Kuchana Nguo Wakati Wa Msiba
Msiba ni katika Sunnah na mitihani ya uhai, Allaah Anasema:
“Na bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao. Na wabashirie wenye kusubiri.” [Al-Baqarah 2: 155].
Pia Allaah Anasema: “Kila nafsi itaonja mauti. Na hakika mtalipwa kikamilifu ujira wenu Siku ya Qiyaamah. Basi atakayewekwa mbali na Moto na akaingizwa Jannah kwa yakini amefuzu. Na maisha ya dunia si lolote ila ni starehe ya udanganyifu.” [Aal-‘Imraan 3: 185].
((Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na watiifu wanaume na watiifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wasemao kweli, wanaosubiri wanaume na wanaosubiri wanawake ….)) [Ahzaab:35]
Katazo la Kuingia katika Hammamaat [sehemu za kuogea zilizojengewa kama vile mahodhi mabwawa na kadhalika na kuruhusiwa kutumiwa na kila mtu].
Jamii nyingi huweka sehemu ambazo huwa zinaruhusiwa kutumiwa na kila mtu kwa malengo tofauti kama vile mabustani, maduni na kadhalika; pia hutenga sehemu nyingine ili zitumike kwa malengo maalumu; kama vile sehemu za kuogea au kuogolea, au sehemu za kuumika, au sehemu za kukandwa, au sehemu za kutengenezwa nyuso au nywele, au sehemu za kupambwa, au sehemu za kubadilisha mavazi au kujilinga, au sehemu za kupumzika, au sehemu za kufua nguo na kadhalika.
Kipimo chake ni maneno ya kiusuli yasemayo: •Kila sehemu pana mazungumzo husika•Na kila mazungumzo yana kipimo husika•Katika kipindi cha nyuma kidogo na mpaka sasa baadhi ya mitandao ya simu imekuwa ikitoa ofa ya kuongea muda mrefu kwa gharama ndogo, na mtu bila kujali kuwa huu ni wakati wa kazi au usiku watu wamelala na kadhalika, anarefusha mazungumzo kisa na mkasa ni kwamba leo ana ofa ya kuongea bure masaa 24 au 12 kwa thamani ndogo ya vocha alizoingiza katika simu yake.
Simu katika lugha ya kiarabu inaitwa “HAATWIF” au “AL-JAWWAAL” au “TILFUUN” vyovyote iwavyo simu ni chombo kitumikacho kwa ajili ya kuwasiliana.
Uislamu upo pamoja na wakati (Yaani haujapitwa na wakati kama wanavyodhani wasioujua Uislamu au maadui wa Uislamu kadhalika. Wakati upo na Uislamu.) Tazama watu wakisema nani wa kwanza kufika mbinguni? (si kwenye sayari kama tunavyosikia na kuona katika vitabu). Basi jawabu si mwengine bali ni Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Vile vile wakisema ni nani wa kwanza kufanyiwa upasuwaji? Basi jibu si mwengine bali ni Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam); bali kafanyiwa upasuaji mara mbili.
((Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na watiifu wanaume na watiifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wasemao kweli wanawake, na wanaosubiri wanaume na wanaosubiri wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanyenyekevu wanawake, na watoao sadaka wanaume na watoao sadaka wanawake, na wanaofunga wanaume na wanaofunga wanawake…)) [Al-Ahzaab:35]