Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   
 
Hijaab - Kuwajibika Kwake
 
Mkuu - teknolojia na taaluma Imefasiriwa Na Ummu ‘Aliy
Nataka kulenga shabaha kwenye mojawapo ya vifaa vya stara. Kitu muhimu katika maisha ya mwanamke ni Hijaab. Nitaanza na Hijaab ya wanawake.Ingelikuwa kaka zetu na dada zetu wa kiislamu wana haya, basi jamii yetu ingeongoka katika njia ya haki. Lengo langu sio kushambulia au kuhukumu wanawake. Namuomba Allaah سبحانه وتعالى Awape thawabu kwa kuchukua wakati kusoma maneno haya. Nitaanza na mojawapo ya rangi za stara, nayo ni stara ya mwanamke.

Kwanini naanza na mwanamke? Nataka kumshambulia au kumhukumu? Labda sitaki kuwaudhi wanaume? La hasha! Allaah سبحانه وتعالى  Asijaaliye. Lakini mwanamke akiongoka na akihifadhi stara yake, basi jamii yote pia itaongoka na itahifadhi stara yake.

Hivyo basi , maadui wa waislamu wanapotaka kuangamiza kitu, kitu cha kwanza wanacho athiri ni mwanamke! Kwasababu mwanamke akipoteza stara yake, ni rahisi kwa vijana pia kupotea, hivyo basi ni rahisi kwa jamii nzima kupoteza stara yao. Kwahivyo tukisema stara kwa mwanamume ni wajib, basi kwa mwanamke pia ni wajib, na ni mujibu. Kwa ajili ya tabia ya mwanamke ya kuwa na haya, ni rahisi kwake kuwa karibu na stara. Na kitu muhimu kabisa kwa mwanamke ni nini?
Ni kujihifadhi na kujifunika mwili wake. Kitu kikubwa anachomiliki mwanamke, ni Hijaab yake. Kwa kaka na dada wanaosoma haya, someni na muwafahamishe dada zenu na jamaa zenu. Na dada yangu katika Uislamu, ikiwa unasoma haya, ilihali wewe ni muhajjaba (mwenye kuvaa Hijaab), basi eneza risala hii kwa dada zako wa kiislamu, na ikiwa wewe sio muhajjaba, basi jaribu upate faida kutokana na haya.
 
Kitu kilichotukuka kabisa ambacho mwanamke anamiliki, ni stara. Na kitu cha thamani katika stara ni Hijaab. Nikikuuliza kitu gani cha thamani unachomiliki, itakuwa ni nini? Ukiwa na kitu cha thamani, utakitunza na kukihifadhi? Utakificha au la? Ukiwa na lulu au johari, je, utaihifadhi mahali pazuri au la? Kila thamani yake ikizidi, basi utazidi kutaka kuihifadhi. Hivyo basi, utaificha watu wasiione. Au utaionyesha na kuiweka wazi mbele ya kila mtu aione na achukue atakacho kutokana nayo?
Hakika utaihifadhi! Vile vile, mwanamke ni kiumbe mwenye thamani kubwa kwa hivyo inampasa ajihifadhi.
Ndugu na dada, je, unajua kama lulu inahifadhiwa na kaka (ganda) lake? Kweli au si kweli. Kwa hivyo huwezi kuwa bila ya Hijaab kwani Hijaab inakuhifadhi na fitna nyingi.
Mwanamke ni lazima ajistiri kwa kuvaa Hijaab kwasababu ni rahisi sana mwanamume kumtongoza yeye kwa uzuri wake.
Kabla ya Uislamu kutujia, mataifa mengi yaliamini kuwa uzuri wenye thamani unapatikana katika mwili wa mwanamke peke yake. Uislamu ulipokuja ulibadili fikra hizo kwa kufundisha watu kuwa uzuri wa mwanamke sio wa mwili peke yake, bali ni wa tabia, fikra na mengineyo mengi.
Haijaandikwa kabisa sheria ya kuwa mwanamke lazima ajioneshe uzuri wake. Hakuna apasae kuuona wala kuufaidi uzuri wake ispokuwa mumewe. Watu aina gani wanampa mwanamke heshima anayostahiki? Watu ambao wanamfanya mwanake ajioneshe uzuri wake, au wenye kumfundisha ajistiri uzuri wake ila kwa wale wanaostahiki kumuona uzuri wake? Wengine wanadai kuwa Hijaab sio wajibu. Tuangalie Qur-aan inasema nini kuhusu Hijaab.
{Ewe Mtume ) صلى الله عليه وسلم ) waambie wake zako, na binti zako, na wanawake  wa Kiislamu wajiteremshe uzuri nguo zao.  Kufanya hivyo kutapeleka upesi wajulikane (kuwa ni watu wa heshima) wasiudhiwe.  Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe (na) Mwingi wa kurehemu} Al-Ahzaab 33: 59

Tuzingatie kuwa Allaah anapozungumzia kuhusu Hijaab kuwa wajibu, Amejumuisha wanawake wenye kuamini pia, sio wake za Mtume صلى الله عليه وسلم    peke yake, kwa hivyo ni wazi kuwa aya hii haikuteremshwa kwa jamii ya Mtume صلى الله عليه وسلم pekee, imeteremshwa kwa ajili ya kuhifadhi wanawake wote. Kwa hivyo wanawake wote wenye kuamini ni lazima wavae Hijaab ili waheshimiwe na wajulikane kuwa ni wenye haya. Hakuna atakaemdhuru kwa ajili ya heshima aliyojiwekea juu ya mavazi yake.
 
Hijaab ni lazima! Sio Sunna tu, Allaah سبحانه وتعالى pia Anasema:
{Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa} An-Nuur 24: 31
Wataalamu wengi wanasema kuwa ni lazima wanawake wajifunike  mwili wote ispokuwa viganja vya mkono na uso.
Allaah سبحانه وتعالى Aliposema wanawake wavae Khimaar, Hakumaanisha kuwa wavae leso kubwa tu, bali ni kuwa mwanamke akivaa hiyo Khimaar, itamfunika mapambo yake muhimu, nayo ni masikio, shingo na kifua. Kwa hivyo, mwanamke akivaa kitambaa kidogo ambacho hakimsitiri mapambo yake hayo tuloyataja, basi hiyo sio Hijaab
Baada ya kuona katika Qur-aan kuwa Hijaab ni wajibu, inampasa mume kumhimiza mkewe na kumshawishi avae Hijaab ili aheshimiwe na athaminiwe kuwa ni mcha Mungu. Katika aya nyengine Allaah سبحانه وتعالى   anawahutubia wanawake wa Kiislamu wasioneshe mapambo yao kama walivyokuwa wakifanya wanawake wakati wa jahilia (kabla Uislamu). Wanawake wa jahilia walikuwa wakivaa nguo ndefu lakini mapambo yao yote yalikuwa yakionekana, kama vile shingo, masikio, nywele na kadhalika.
Aayah ya Hijaab ilipoteremka tu, wanawake wote walitoka huku wamevaa Hijaab. Wanaume waliposikia aya hiyo waliwaeleza wanawake maana yake, basi wanawake walikuwa tayari Kufuata sharia ya Allaah سبحانه وتعالى kama alivyoieleza katika Qur-aan. Madhali walikuwa hawana uwezo wa kununua nguo mpya, walinyanyua nguo zao kwa sehemu mbili ili watumie kama Hijaab.
Hiyo ni kinyume na vile wanawake wakisasa walivyo. Wao hutoa visingizio kwa kutovaa Hijaab inayotakikana. Mtume صلى الله عليه وسلم alisema: 
 
“Kikundi cha wanawake  hawataingia peponi.  Hao ni miongoni mwa wale wanaovaa nguo za kubana, za kuonyesha mwili na hawafuati amri ya Allaah سبحانه وتعالى ya kuvaa Hijaab. Hawataingia tu peponi bali hata hawatasikia harufu ya pepo ambayo  harufu yake husikilizana masafa ya mwendo wa miaka 500.” Hadiyth imesimuliwa na Muslim    
Kutilia mkazo umuhimu wa kujifunika, Ilimbidi Mtume صلى الله عليه وسلم  alipige vita kabila moja la Kiyahudi ambalo lilimchezea shere mwanamke wa Kiislamu sokoni. Walimfanyia hila huyo mwanamke kwa kuifunga nguo yake ili akitembea aanguke na nguo yake ipasuke kisha awe uchi. Basi mwanamume mmoja aliyeshuhudia hayo, alipigana na kumuuwa yule Yahudi aliyefanya mambo hayo. Mtume صلى الله عليه وسلم    aliamrisha jeshi lake liwa*****uze kabila hilo la Kiyahudi nje ya Madinah.

Ni Ipi Sababu Yako Ya Kutovaa Hijaab?  
1.      Sijasadikika Na Hijaab.
Sasa nitakuuliza wewe ni nani? Utajibu wewe ni Muislamu. Uislamu unaamanisha nini? Uislamu ni kumtii Allaah سبحانه وتعالى  kabisa kwa mambo yote aliyotuamrisha. Na kuvaa Hijaab ni mojawapo ya maamrisho ya Allaah سبحانه وتعالى. Mwanamke ambae hataki kuvaa Hijaab basi hajamtii Allaah سبحانه وتعالى.
2. Sababu Ya Pili.
Mwanamke ambae anadai kuwa kitu muhimu ni nia yake, na kuwa dhamira yake sio mbaya na kuwa yeye ni mtu mzuri, na kuwa Hijaab ni ya moyo. Mwanamke huyo huyo anadai kuwa anaswali swala tano, sunna na swala za usiku na anatoa sadaka. Kweli anafanya yote hayo, lakini kisha anasema ibada hizo zinatosha. Subhana Allaah!   Kasema Allaah سبحانه وتعالى:
{Je! Mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakataa baadhi yake? Basi hana malipo mwenye kutenda hayo miongoni mwenu ila hizaya katika maisha ya duniani, na Siku ya Kiyama watapelekwa kwenye adhabu kali kabisa. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale mnayo yatenda}.  Al-Baqarah 2: 85 
Kwa hivyo tufanye hisabu, unasema unafanya mengi mema, kuwa nia yako ni nzuri na moyo wako ni msafi. Sawa, lakini kila siku unapotoka, wanaume wangapi wanakuangalia nywele zako, na uzuri wako wote, je unakusanya madhambi tele au la? Hakika unakusanya madhambi kwasababu hukufuata amri ya Allaah سبحانه وتعالى. Na huyu mwanamke atashindana kuwa sio makosa yake wanaume wakimuangalia kwasababu nia yake sio mbaya, bali atasema kuwa wanaume ndio watakao pata madhambi. La hasha! Wewe ndio chanzo cha hao wanaume kukuangalia kwasababu hujavaa Hijaab na unavutia. 

Mwanamke ambae havai Hijaab bila shaka anakusanya madahmbi mengi, kwasababu, wanaume wana nyoyo zenye matamanio na macho yenye kutaka. Hebu fikiria madhambi kiasi gani anayakusanya mwanamke huyu. Je, yale mema yote yanamtosha yakilinganishwa na madhambi yake? Fikiria akitoka, ndani ya mabasi, ndani ya treni, kazini, barabarani, na kila pahali, madhambi mangapi atapata kwa kila mwanamume anaemuangalia uzuri wake akamtamani?
Allaah سبحانه وتعالى Hakukuamrisha uvae Hijaab? Nakuogopea kuwa mema yako yana anguka kutoka kwenye m*****o uliopasuka. Yale mema yanaingia kwa juu na kutoka kwa chini.
3. Hijaab Na Joto.
Mwanamke anaweza akalalamika kuwa nywele zake zinadondoka akivaa Hijaab kwa ajili ya joto, na akakuuliza, “unataka niwe kipara sasa?” Ewe dada, Allaah سبحانه وتعالى    anasema kuwa moto wa jahannam ni mkali kuliko moto wa duniani.
Mtume صلى الله عليه وسلم  amesema:
“Moto umezungukwa na matamanio yetu, na pepo imezungukwa na juhudi zetu.”
Bado unaona tabu kuvaa Hijaab, unaona tabu kufuata maamrisho ya Allaah سبحانه وتعالى . 
4. Sio Hoja Kuvaa Hijaab Kuwa Ndio Heshima.
Wengine husema kuwa wanajua wanawake ambao wanavaa Hijaab lakini wana tabia mbaya kabisa. Kwa hivyo hawataki kuvaa Hijaab wakaonekana kama hao.Sasa basi kwa yule mwanamke anaedai  hayo:  Tunajua watu tele wanaoswali lakini wanafanya maaswia, hiyo   inamaanisha sisi pia tusiswali? Wengine ni muhujjaj na wanafanya mambo yasiokuwa, inamaana tusende hajj? Kwa hivyo dada yangu Hijaab sio mbaya, bali mwenye kuivaa na kuiharibia sifa zake ndio mbaya.
 
5. Allaah سبحانه وتعالى Hajaniongoza Bado.
Nitavaa Hijaab baadae lakini sio sasa kwasababu Allaah سبحانه وتعالى hajaniongoza  bado.Kwa hivyo nikifika miaka hamsini baada ya   kufaidi ujana wangu, ndio nitavaa Hijaab. La, dada yangu! Hiyo  ni makosa kabisa. Allaah سبحانه وتعالى  anasema kuwa Habadili hali ya   watu mpaka wale watu     wabidili yaliyomo mwao. Huwezi kuvaa  Hijaab mpaka ujitahidi. Haikubaliki kusema kuwa Allaah سبحانه وتعالى hajakuongoza, la, Allaah سبحانه وتعالى amekuongoza kiasi ya kuwa  unasoma makala haya. Sibabu ya wewe kusoma haya ni kuwa Allaah سبحانه وتعالى anakufungulia njia ya kuongoka, Nae Hamuachi mja Wake ispokuwa Anamuonesha uongofu, sasa ni   uu ya yule mja kufuata au kukanusha.

6. Nikiolewa Nitavaa Hijaab.
Wanaume wengi wanapotaka kuoa, hutafuta wanawake wacha Mngu walio na heshima wanaovaa Hijaab. Munapotaka kuolewa, oleweni na     wanaume ambao watakupendeni kwa ajili ya dini yenu na watakao waheshimu. Kwa hivyo Allaah سبحانه وتعالى Atakupeni waume  walioshika dini.
Yuko mtu alikwenda kwa ulamaa akamuuliza,” nikitaka kumuozesha   dada yangu, nimuozeshe mtu aina gani?” ‘Aalim akamjibu, “Muozeshe mwanamume ambae ni rafiki wa Uislamu, hivyo basi,   akimpenda, atamheshimu, na akimchukia hatomfanyia ubaya.
Kwa hivyo dada zangu, oleweni na wanaume ambao watakao wakinga na kuwaheshimu na kufurahikia kuwa nyinyi ni Muhjaba.

7. Mimi Bado Kijana.
Unajua lini utaiaga hii dunia dada yangu? Vifo vya vijana vimeenea! Nitawapa mfano. Kisa  hichi kilitendeka kikweli huko Misri(Egypt, Alexandria) wakati wa  Ramadhani
Yuko mtu na mkewe ambae ni muhajaba na majirani zao ambao    ndani   yake yumo msichana ambae sio muhajaba. Huyo msichana   kama wasichana wengi wakiislamu alikuwa na moyo mzuri, lakini  hakufahamu maana ya Hijaab katika Uislamu. Huyo mwanamke muhajaba alikuwa na uhusiano mzuri na yule msichana. Hakumpuuza  kwa ajili havai Hijaab, la, alikuwa rafiki yake. Siku moja yule msichana alimuomba yule mwanamke ampeleke madukani akanunue  ya patashika ( jeans). Yule mwanamke  muhajaba alikuwa na hikma na alijua kuwa ni lazima ampe yule  msichana mawaidha, basi  akakubali kumpeleka lakini kwa shuruti moja. Akamwambia amfuate kwenye muhadhara. Basi yule   msichana akakubali.
Walipokwenda kwenye muhadhara, mada ilikuwa kuhusu kutubia  kwa Allaah سبحانه وتعالى  Basi yule msichana aliingiwa na imani nyingi kwa yale yaliyokuwa yakisemwa, mpaka akaanza kulia na huku akirudia  maneno haya,”nimetubu Mola wangu, nifunikeni”. Wale waliohudhuria wakamwambia watampeleka nyumbani ili akavae   Hijaab, lakini yule msichana alikataa, alitaka avae Hijaab pale pale,   kasema hawezi kutoka hapo bila ya kuvaa Hijaab. Basi akatafutiwa  Hijaab akavishwa, akitoka tu na kutaka kudakia barabara, gari    likamgonga, hapo hapo akafariki. MashaAllaah! Msichana huyo alikufa baada tu ya kutubia, Subhana Allaah! Kwa hivyo wasichana, musitoe  sibabu ya kuwa bado nyinyi ni wadogo, hakuna anaejua ataondoka  duniani saa ngapi.

8. Nataka Kufuata Fesheni, Nikivaa Hijaab Nitaachwa Nyuma.
Mola wako mlezi sio bora kuliko fesheni? Nakuhakikishia, ukivaa   Hijaab utakuwa  una nuruitokayo kwako.

9.  Nataka Kuiga Watu Wa Magharibi (Westerners).
Nani anaemheshimu mwanamke zaidi? Uislamu au wale ambao hawawezi kuuza kitu bila ya kuweka picha ya mwanamke aliye kuwa tupu? Wao ndio wamempa mwanamke heshima au wamemdhulumu? Au Uislamu uliomheshimu mwanamke na kumpa daraja za juu na   kumstiri kutokana na kudhulumiwa?
10. Sitaki Kuvaa Hijaab Kwa Sababu Naogopa Nitaivua.
Subhaana Allaah! Dada, kwanini huvai Hijaab na nia madhubuti huku unamuomba   Allaah سبحانه وتعالى Akuhifadhi na kuitoa. Kuitoa Hijaab ni madhambi makubwa, usifanye hivyo, utakuwa unatoa mfano gani?
 
Vaa Hijaab kisha ufanye mambo haya ili uhakikishe kuwa hutoitoa   Hijaab yako. 
1.     Kuwa na marafiki wema walioshika dini.
2.     Hudhuria na sikiliza mawaidha ya Kiislamu.
3.     Omba dua kwa Allaah سبحانه وتعالى Akuzidishie Imani ya dini yako na Akupe guvu ili uvae Hijaab yako kila siku.
11. Naona Hayaa:
Naona haya na aibu kutokana na yale watakayoyasema marafiki zangu nikivaa Hijaab. Dada, hutaona haya mbele ya Allaah سبحانه وتعالى siku ya kiama? Hutotahayuri mbele ya Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم? Hakuna kutahayuri wala kuona haya mbele ya waja ikiwa unamuasi Mola wako.
 
Siku ya kiama utakuwa na kiu cha ajabu, na Mtume صلى الله عليه وسلم atakuwa anawapa watu maji. Utamkimbilia Mtume صلى الله عليه وسلم ili na wewe upate maji, lakini Malaika wawili watakuzuia ili usimfikie Mtume صلى الله عليه وسلم. Nae Mtume صلى الله عليه وسلم atawaambia wale Malaika wakuache kwasababu wewe ni katika umma wake. Wale Malaika watamwambia Mtume صلى الله عليه وسلم kuwa huyu ni katika wale ambao hawakufuata maamrisho ya Allaah سبحانه وتعالى. Basi Mtume صلى الله عليه وسلم ataondoka na kwenda mbali nawe huku anasema hataki uhusiano wowote na wewe kwa ajili hukufuata maamrisho ya Allaah سبحانه وتعالى.
Nani atatahayuri wakati huo? Yule ambae anaonesha mapambo yake kwa kila mtu au yule anaejistiri na kujiheshimu?
Mtume صلى الله عليه وسلم amesema: “Ukamateni Uislamu na mikono yenu na meno yenu”.
Nawasisitiza dada zangu katika Uislamu, mukitaka kuvaa Hijaab, vaeni sasa musisubiri     baadae, kwani hamujui kama mutafika wakati huo munaoutarajia. Ukivaa Hijaab sasa, Mshukuru Allaah سبحانه وتعالى, swali kwa saa zake, tafuta marafiki wema na soma Qur-aan kila siku hata kama ni kidogo.
Mukifanya mambo hayo, basi inshaAllaah Hijaab yako itakwenda sambamba na kuabudu kwako, tabia yako njema, na pia utakuwa mfano mzuri kwa wanawake Waislamu na wasiokuwa Waislamu. 

Ukiwa umeamua kuwa muhajaba, basi usifikirie kuwa kuvaa Hijaab ndio kumekamilisha ibada zako na utaingia peponi, la, kuvaa Hijaab ndio miongoni mwa njia za kuelekea kwa Allaah سبحانه وتعالى.      
Kumbuka kuwa wewe ni mfano kwa wanawake Waislamu na wasiokuwa Waislamu, kwa tabia yako njema, kuabudu kwako, mavazi yako, na kadhalika. Bila shaka utamuathiri kila anaekuona hata bila ya kusema chochote. Utakuwa umeisafisha jamii, na matendo yako mema yako katika daraja ya juu mbele ya Allaah سبحانه وتعالى. Utawaongoza dada zako katika Uislamu kwasababu wewe ndio mfano na waziri wa Waislamu. 

Yafuatayo ni machache tu kuhusu namna gani kuvaa Hijaab. Ikiwa hufuati haya, basi ina maana kuwa huvai Hijaab sawa sawa.

1- Sio-lazima uvae Khimaar au ‘Abaayah. Unaweza ukavaa chochote, alimradi iwe ndefu na sio ya kushika mwili, na ifunike mwili wote. Ukivaa chochote ambacho kinaonesha umbile la miguu, kiuno, mabega, kifua, na kadhalika, basi hujavaa Hijaab sawa sawa.
2- Kutovaa nguo nyembamba zinazoonyesha mwili.
3- Kujifunika mwili mzima.
4- Kutovaa nguo zinazofanana na nguo za kiume.
5- Kutotia manukato unapotoka nje. 
Ukifuata hoja hizi wakati wote, basi umekamilisha Hijaab na umekuwa Muhajjabah Insha Allaah.


 Posted By Posted juu ya Thursday, May 10 @ 20:35:57 PDT na MediaSwahiliTeam
 

Comments 💬 التعليقات
 

For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora
Vizuri Sana
Mema
Kawaidar
Mbaya


Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa RafikiMada zinazohusiana

Mkuu - teknolojia na taaluma

 

EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And IslamAfrica.Com