Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   
 


Hijrah: Chanzo Cha Mageuzi
 
bakom domstolens rättspraxis ya Kii
Khutbah Ya Ijumaa 

Allaah Amejaalia njia ya haki kuwa na ishara za wazi. Na Akajaalia kufikiwa katika lengo linalohitajika kwa juhudi na kujitolea. Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:



“Hakika Allaah Amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Allaah - wanaua na wanauawa. Hii ni ahadi aliyojilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur-aan. Na nani atimizae ahadi kuliko Allaah? Basi furahini kwa biashara yenu mliyofanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa” (9: 111)

 
Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alibeba bendera ya ushujaa mpaka ikawa ni yenye kunyanyuka katika kila sehemu ya pembe ya ulimwengu. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikaa miaka 13 Makkah baada ya kupewa utume akiilingania kaumu yake katika Uislamu. Hakika alibughudhiwa, kuudhiwa na kukadhibishwa Da‘awah yake. Mbali na hayo walikuwa wanajua ukweli na uaminifu wake mpaka wakawa wanamuita As-Swaadiqul Amiyn (Mkweli Muaminifu).

 
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake walivumilia maudhi yao yote, adhabu na mateso. Katika mwezi wa Muharram Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliashiria kwa Maswahaba zake kuhamia Madinah. Wakatoka wote isipokuwa wale waliokuwa na haja zao katika mji wa Makkah au walioshikwa na kufungwa kwa nguvu na makafiri.

 
Sababu ya Hijrah, ni pale Ma-Quraysh waliposhindwa kumkinaisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuacha Da‘awah yake na kuendelea kwake kumuabudu Allaah tu. Hivyo, walifikiria ima kumfunga au kumuua au kumtoa katika mji lakini uamuzi uliochukuliwa ulikuwa ni kumuua kabisa. Walichagua vijana wenye nguvu kutoka kila ukoo ili kutekeleza mkakati wao huo. Vitimbi vyao hivyo vilifichuliwa na Mwenye habari na Mjuzi, naye alitoka mbele ya vijana bila kuonekana na hao vijana waliokuwa wamekaa nje ya nyumba yake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

“Na walipokupangia mpango waliokufuru wakufunge, au wakuuwe, au wakutoe. Wakapanga mipango yao, na Allaah Akapanga yake. Na Allaah ndiye Mbora wa mipango” (8: 30).

 
Walifika kwenye pango na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akawalinda na maadui hao ambao walikuja mpaka kwenye mdomo wa pango la Thawr. Abubakar (Radhiya Allaahu 'anhu) alipowaona makafiri wakiwa nje ya pango alisema: “Lau mmoja wao ataangalia chini ya miguu yake basi atatuona”. Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa utulivu na bila wasiwasi alimwambia: “Ee Abu Bakr! Dhana yako ni ipi kwa wawili ambao watatu wao ni Allaah” (al-Bukhaariy na Muslim). Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Analizungumzia tukio hilo kwa kusema:

 
“Ikiwa nyinyi hamtamnusuru Mtume, basi Allaah Alikwishamnusuru walipomtoa waliokufuru, naye ni wa pili katika wawili walipokuwa katika pango, naye akamwambia sahibu yake: Usihuzunike. Hakika Allaah Yu pamoja nasi. Allaah Akamteremshia utulivu wake, na Akamuunga mkono kwa majeshi msiyoyaona, na Akalifanya neno la waliokufuru kuwa chini, na Neno la Allaah kuwa ndilo juu. Na Allaah Ndiye Mwenye nguvu Mwenye hekima” (9: 40).

 
Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aliwaokoa wao wawili na vitimbi vya mushrikina. Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ataendelea Kuwahami na Kuwalinda walinganiaji wa haki mpaka Siku ya Kiyama.

 
Na hapo makafiri wakatoa zawadi ya ngamia mia moja (100) kwa atakaye wapata hai au maiti. Na hii hii ndiyo mbinu ambayo inatumiwa na makafiri wa sasa wanavyofanya wakati wanawatafuta watu. Na ndio wanazuoni wetu wakasema: “Ukafiri mila yao ni moja”.

 
‘Umar ibn al-Khattwaab (Radhiya Allaahu 'anhu) baada ya kushauriana na Maswahaba waliokuwa hai wakati wa Ukhalifa wake waliamua kuanza tarehe ya Kiislamu kwa tukio hilo, kwani ndio ilokuwa chanzo cha ushindi na kubadilisha historia yote. Hapo wakawa Waislamu Mashariki ya ardhi na Magharibi yake wanafahamu kabisa kwa uhakika kuwa ni Hijrah ndiyo iliyoharakisha mapambano na kujitolea mhanga. Lakini ni masikitiko kuwa hatufahamu umuhimu wa tukio hilo isipokuwa ni msimu wa kidini ambapo tunakariri matukio ya kimada ya Hijrah na jinsi alivyohama Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake na walivyopokewa kwa ukarimu Madinah na kula pilau kumaliza kabisa shughuli yenyewe 

 
Ama mazingatio, maana matukufu makuu huwa mara nyingi hatuyataji sana na tukiyataja basi hayafiki kooni. Hakika, Hijrah ina mambo mawili: Zingatio la kimada na la kiroho.

1.  Zingatio la kimada: Hii inaanza wakati alipotoka Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Makkah na kurudi kwake akiwa mshindi, huku akinyanyua bendera ya Tawhiyd na kuvunja masanamu. Na faida hii tunaiona mpaka wakati wetu huu wa sasa ambapo watu wanaingia katika Uislamu bila hesabu.

2.  Zingatio la kiroho: Hii ni matokeo ya mapinduzi makubwa katika nafsi ya Muislamu na Ummah kwa ujumla wake kwa kufanya Da‘awah, na kutoka katika giza la ujinga na shirki kuelekea katika nuru ya elimu na Imani. Hijra inatufundisha kuacha maovu na riyaa na kujitwika tabia ya ukweli na uwazi na kupeana nasaha na kuifanya ndio msingi wa mahusiano yetu na watu wote – viongozi na raia bila kuogopa. Aliingia wakati mmoja ‘Amr ibn ‘Ubaydah kwa Khaliyfah wa Bani ‘Abbaas, al-Mansuur na akamsomea aya ifuatayo:

“Hakika Mola wako yupo kwenye mavizio anawavizia” (89: 14).

Khaliyfah akasema: “Onyo hili ni kwa nani, ewe Abu ‘Ubaydah? 

 
Akamjibu bila khofu: “Hakika ni kwa wale wanaofanya mfano unayofanya wewe. Mche Allaah, ewe Amiri wa Waumini! Hakika katika mlango wako upo moto unaowaka, haufuati Kitabu cha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  wala Sunnah ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) nawe una jukumu na utaulizwa kwa unayoyafanya na wala sio wanayoyafanya. Hivyo, usitengeneze dunia yao kwa kuiharibu Akhera yako. Ama WAllaahi lau wafanyakazi wako wangejua kuwa huridhiki ila uadilifu wangekuja karibu nawe. Ewe Amiri wa Waumini! Hakika watu wamekuchukua kama ngazi, wewe ndiye mshikaji pembe na wengine ndio wenye kukama maziwa. Hawa hawatakunufaisha chochote kwa Allaah. nami nakunasihi ewe Amiri wa Waumini, hakika wamelaaniwa Bani Israili kwa ulimi wa Dawuud na ‘Iysa kwani wao walikuwa:

 
“Walikuwa hawakatazani maovu waliyokuwa wakiyafanya. Hakika ni maovu yalioje mambo waliyokuwa wakiyafanya!” (5: 79).

 
Hijrah inatakiwa ibadilishe maadili yetu – ya mtu na jamaa, na inatakiwa itutoe katika usingizi na iwe nukta ya kuanzia, hapo ndio tutaanza ili kutengeneza jamii nzuri zaidi na yenye ufanisi wa nyumba zote mbili (duniani na Akhera). Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa anahama aliomba kwa kusema: “Ee Mola wangu! Hakika Wewe Unajua kuwa wao (yaani makafiri) wamenitoa katika mji ninaoupenda zaidi, hivyo nipatie maskani katika mji Unaopendwa zaidi na Wewe”

Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atubariki, Aturehemu na Atupatie fanaka katika mwaka huu wa Hijri. Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atupatie hima ya kurudi katika misimamo ya sawa na njia ya sawa inayompendeza Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) pamoja na kufuata mwenendo wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). In shaa Allaah sote tuwe na azma ya kikweli kweli ya kubadilika na tutie bidii katika hilo na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atatusaidia katika hilo. Kwani Amesema:

 
“Hakika Allaah habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao” (13: 11).


 Posted By Posted juu ya Thursday, May 10 @ 20:40:29 PDT na MediaSwahiliTeam
 

Comments 💬 التعليقات
 

For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا

Kuhusiana Viungo

· zaidi bakom domstolens rättspraxis ya Kii
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu bakom domstolens rättspraxis ya Kii:
Simulizi (Kisa) Ya Hijaab Ya Khawla: Maoni ya Hijaab


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora
Vizuri Sana
Mema
Kawaidar
Mbaya


Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa Rafiki





Mada zinazohusiana

bakom domstolens rättspraxis ya Kii

 

Ẹsin Islam الدين الإسلامي Religion of Islam Addinin Musulunci Agama Islam Religión del Islam 伊斯兰教 Dini ya Kiislamu Религия Ислам Religião do Islã イスラム教 Esin Islam 이슬람의 종교 Portal African Muslim Website - Arabic English African Islamic Website For World News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Articles, Radio, Audio, Video, Quran, Hadith, TV Channels, Fatwas, Muslim News, Newspapers, Magazines Headlines, Forums, College, Schools, Universities, Mosques, Quranic, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Ramadan, Vidoes, Books, Fasting, PDFs On EsinIslam.Com And IslamAfrica.Com