Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   
 
Fataawa Za Wanachuoni Kuhusu Mavazi Ya Mwanamke ‘Arusini Na Wanapokuwa Na Wanawa
 
Mkuu - teknolojia na taaluma
Fataawa Za Wanachuoni Kuhusu Mavazi Ya Mwanamke ‘Arusini Na Wanapokuwa Na Wanawake Wenzao

Swali:

Nini shari'ah ya kiislamu kwa wanawake kuvaa nguo za wazi kabisa wanapohudhuria harusi, Kama kanzu fupi zinazoonyesha miguu au mikono yote kuwa wazi au kuvaa bega na moja liko wazi, baadhi ya au kifua kuwa wazi, au kanzu kumbana (tight) hadi mwili wote viungo vyake vinaonekana, au mgongo kuwa wazi n.k.. Je inaruhusiwa kwa vile wako mbele ya wanawake wenzao? ipi mipaka ya mavazi baina Yao?


1) Ni kweli kwamba 'awrah ya wanawake mbele ya wanawake wengine ni kutoka kitovu cha magoti?


Tumesikia kwamba 'awrah (uchi) wa mwanamke mbele ya wanawake wengine ni kutoka kitovu na magoti. Je hili ni sahihi?
Haswa katika makumbi ya sherehe tunaona wanawake wanaokuja –Tunamuomba Allaah Atulinde na Atupe afya– wanakuja huku wamevaa nguo fupi au mtu anaona vuliomo ndani ya nguo, au mavazi na miundo ya kukatwa ambazo inaonyesha ndama zao, au wao wanavaa nguo za kuonyesha mwili ndani kabisa, au vazi linaloonyesha sehemu ya kifua au sehemu ya nyuma wazi... Hivyo wanawake Waislamu wanatoka nje na wanaonekana kama wachezaji sinema katika nchi za kikafiri au mavazi mabaya kwenye sinema na televisheni. Na tunawaambia kutofanya hivyo, wanasema, Hakuna ubaya wowote kwa hilo, kwa kuwa 'awrah ya wanawake ni kutoka kitovu hadi magoti. Hayaa imetoweka kabisa na wanawake wamekuwa wanawaiga makafiri, na tatizo hili limefikia kiwango kikubwa mno. Tafadhali tunaomba ushauri wenu, Allaah Awalipe.

Jibu:

AlhamduliLlaah,

Mwanamke yeye wote (mwili wake wote) ni 'awrah mbele ya wanaume ambao si Mahram zake (anayeweza kumuoa), na haijuzu kwake kuonekana mbele ya wanaume hata kama atakuwa ni mwenye kujisitiri, kwa kuhofia fitnah kwa kumuangalia na kuona jinsi ni alivyo na jinsi anavyotembea. Kuhusiana na lililosemwa kuhusu 'awrah ya mwanamke mbele ya wanawake wenziwe kuwa ni kutoka kitovu hadi magoti, hii inatumika tu wakati atakuwa kwenye nyumba yake miongoni mwa dada zake na wanawake ambao anaishi nao.
Kanuni za msingi bado zinasisitiza asitiri mwili wake wote ili achukuliwe kama kiigizo bora na haya mazoea maovu yameenea miongoni mwa wanawake. Vile vile, anapaswa kusitiri uzuri wake mbele ya mahram wake na wanawake wageni ili baadhi ya mahram wake wavutiwe (waathirike) nae kitabia na adabu, au ili baadhi ya wanawake wasije kwenda kumuelezea yeye wasifu wake kwa wengine (wanaume). Imeripotiwa katika Hadiyth kuwa Mtume (Swala Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema:

"Haitakiwi mwanamke kumuelezea mwanamke mwengine kwa mume wake, hivyo ni kama (mumewe) anamuona yeye" Kinachomaanishwa ni kuwa uzuri wake, kama vile kifua chake, mabega yake, tumbo lake, nyuma, mikono yake, shingo yake na ndama yake inakuwa wazi, kila mtu anaona kwamba ni jambo lisiloweza kuepukwa, mtu kuwa na hisia yake.
Na ni kawaida wanawake huelezea juu wa waliyoyaona kwa familia zao, sawa wanamume na wanawake. Hivyo mwanamke anaweza kutaja hayo mbele ya watu ambao si Mahram wake, kwa namna ambayo inaweza kuwafanya wao kuvutiwa kwake [huyo mwanamke], au ambayo inaweza kusababisha watu wabaya kutafuta njia kuanzisha uhusiano naye.
Kwa sababu hii, wanawake wanatakiwa kufunika 'awrah [sehemu zisizotokiwa kuonekana katika miili] yao - kama vile vifua vyao, migongo, mikono, ndama, n.k, - vile vile hata mbele ya mahram wake na wanawake wengine.

Kujisitiri huku kunakuwa muhimu zaidi katika sehemu za makundi, maeneo ya sherehe, hospitali, na mashule, hata kama kutakuwepo wanawake tu, kwa sababu baadhi ya wanaume ambao si Mahram na hata vijana wanaweza kuwaona au kuwachukua picha hali ya kuwa hawana stara zao kamili, na hiyo  itakuwa ni sababu ya fitnah kwa wale wanaowaona.

Onyo kali imetolewa kwa wale [wanawake] ambao wanajionyesha na wavaao nguo za kuonyesha au za kubana, wakati Mtume (Swala Allaahu 'alayhi wa sallam) aliposema:

Aina mbili za watu wa motoni siwaoni... Wanawake ambao wamevaa lakini wako uchi, wanawashawishi wanaume wawatongoze, na wanaelekea kwao (kwa kuwa warahisi). Vichwa vyao kama nundu za ngamia zinazoyumba (aina ya msuko wa nywele wanaosuka wanawake). Hawataingia Peponi wala hawatasikia harufu yake ingawa harufu yake inaweza kunuswa kutoka masafa kadhaa na kadhaa” [Muslim]

Kinachomaanishwa ni kwamba wamevaa nguo za kuonyesha au nguo za kubana ambazo zinaonyesha maumbile yao, au kunapokuwepo fursa ya ajira kwenye kampuni ambayo [mavazi yao] huonyesha vifua vyao, matiti yao na sehemu zingine zisizofaa kabisa kuonekana. Hili limeenea katika makundi na katika mikusanyiko ya ujumla yote.  Na Allaah Anajua zaidi.

Kutoka Fataawa za Shaykh 'Abdullaah bin 'Abdir-Rahmaan al-Jibriyn

Swali:

2) Nini ambacho mwanamke anaruhusiwa kudhihirisha mbele ya wanawake wengine na mahram wake?

Yapi maoni yako kwa wayafanyayo wanawake wengi siku hizi, ambapo wao huvaa nguo fupi sana wakati wako pamoja na wanawake wengine na kunakuwa hakuna wanaume wengine? Baadhi ya nguo hizo huonyesha sehemu kubwa ya nyuma na tumbo, au wanavaa nguo hizo fupi mbele ya watoto wao nyumbani?

Jibu:

AlhamduliLlaah,

Kamati ya Kudumu (al-Lajnah al-Daa'imah) ya Utafiti wa Elimu na mas-ala ya Fatwa wana maelezo yafuatayo juu ya suala hili, ambayo inasomeka kama ifuatavyo:

Shukrani zote zinamstahiki Allaah, Mola wa walimwengu wote, na swalah na salaam ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad, na juu ya familia yake yote na Swahaba zake.

Waumini wanawake mwanzo wa Uislamu walikuwa safi sana, wenye hayaa na wenye aibu, jambo ambalo ilikuwa ni baraka ya imani kutoka kwa Allaah na Mtume Wake, na walikuwa wakifuata Qur-aan na Sunnah. Wanawake katika kipindi hicho walikuwa na ada ya kuvaa nguo za kujisitiri, na haikujulikana kwamba walikuwa wakijifunua wanapokutana na mmoja au wanapokutana na mahram zao. Wanawake wa ummah huu wanatakiwa wafuate tabia hii nzuri - AlhamduliLlaah - kizazi baada ya kizazi mpaka hivi karibuni.
Lakini wakati uharibifu na fitnah zilipoingia kwa wanawake, njia ya mavazi yao na wanavyojiweka kwa sababu nyingi (inasikitisha sana kabisa), jambo ambalo hatuna nafasi ya kulijadili hapa.

Kwa sababu ya idadi kubwa ya maswali ambayo yametumwa kwenye Kamati ya Kudumu ya Utafiti wa Elimu na Fatwa kuhusu wanawake kuangalia wanawake wenzao, na nini anachopaswa mwanamke kuvaa, Kamati inawaambia wanawake wote wa Kiislamu kwamba wanawake ni wajibu kwao kuwa na tabia ya kuwa na hayaa, jambo ambalo Mtume (Swala Allaahu 'alayhi wa sallam) alielezea kuwa ni sehemu ya imani na moja ya matawi ya imani.
Suala la hayaa ambalo ni amri iliyotolewa na Uislamu na kwa desturi ni kuwa wanawake wanapaswa wajisitiri, kuwa na hayaa, tabia na maadili ambayo yatawaweka mbali na kuanguka katika fitnah (majaribio) na hali ya utata.

Qur-aan inaonyesha wazi kuwa mwanamke hapaswi kuonyesha wanawake wengine chochote zaidi ya wanawake ambao ni Mahram wake, hali ambayo ni ya kawaida yeye kujifunua katika nyumba yake ni wakati wa kufanya kazi za nyumbani, kama jinsi Allaah Anavyosema:

 “…wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unaodhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao,” [An-Nuur 24:31]

Ikiwa haya ndiyo maandiko ya Qur-aan na ndiyo latambulikana katika Sunnah, basi hili ndilo ambalo wake wa Mtume (Swala Allaahu 'alayhi wa sallam) na wanawake wa Maswahaba walivyokuwa wakifanya, na wanawake wa Ummah ambao waliwafuata kwa wema mpaka siku ya leo.
Jambo la kawaida la wanawake kujifunua ni wakati wao wako nyumbani na wakati wanafanya kazi za nyumbani, hali ambayo ni vigumu kujizuia, kama vile kujifunua kichwa, mikono, shingo na miguu.

Tukenda upande wa kuvuka mipaka katika kujifunua, hakuna dalili katika Qur-aan na Sunnah kwamba inajuzu. Hii pia ni njia inayoongoza kwa mwanamke kumjaribu au kujaribiwa kwa wanawake wengine, ambayo hufanyika kati yao. Pia inakuwa ni mfano mbaya kwa wanawake wengine, kama vile kuwaiga wanawake wa Kikafiri, makahaba na wanawake waovu jinsi wanavyovaa.
Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swala Allaahu 'alayhi wa sallam) amesema:
“Yeyote atakayeiga (jinafananisha) na watu basi atakuwa miongoni mwao.”
Imepokelewa na Imaam Ahmad na Abu Daawuud. Katika Swahiyh Muslim (2077)

Imesimuliwa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr kuwa Mtume (Swala Allaahu 'alayhi wa sallam) alimuona amevaa nguo mbili za hariri, akasema:
“Haya ni katika mavazi ya makafiri, usiyavae.”
Pia imepokelewa katika Swahiyh Muslim (2128) Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allahu 'anhu): Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Aina mbili za watu wa motoni siwaoni; Watu ambao wana fimbo (mijeledi) kama mkia wa ng'ombe dume ambazo wanawapigia watu, na wanawake ambao wamevaa lakini wako uchi, wanawashawishi wanaume wawatongoze, na wanaelekea kwao (kwa kuwa warahisi). Vichwa vyao kama nundu za ngamia zinazoyumba (kwa mtindo wa nywele wanaosuka). Hawataingia Peponi wala hawatasikia harufu yake ingawa harufu yake inaweza kunuswa kutoka masafa kadhaa na kadhaa.”

Maana ya kauli hii “wamevaa lakini wako uchi” ni kwamba mwanamke amevaa nguo ambayo haijamsitiri, kwa hiyo amevaa, lakini kwa staili ambayo bado yuko uchi, kama vile wakati anavaa nguo nyembamba ambayo inaonyesha rangi ya ngozi yake, au vazi ambayo inaonyesha hali ya mwili wake, au vazi fupi ambalo haisitiri sehemu za viungo vyake.

Kwa hiyo, jambo ambalo wanawake wa Kiislamu wanapaswa kufanya ni kushikamana na uongofu waliokuwa wakifuata mama wa Waumini (wake wa Mtume) na wanawake wa Maswahaba (Radhi za Allaah ziwashukie), na wanawake wa ummah huu ambao wanawafuata hao kwa wema, na wajitahidi kujisitiri na kuwa na hayaa. Hili litawafanya kuwa mbali kuwasababishia fitnah na litawalinda na mambo yanayosababisha uchochezi wa tamaa na kuanguka katika zinaa.

Waislamu wanawake wanapaswa kujihadhari kuanguka katika mambo ambayo Allaah na Mtume wamekataza, kama kuwaiga wanawake wa kikafiri na makahaba.
Wanatakiwa kumtii Allaah na Mtume Wake, na kwa kutumai kupata malipo kwa Allaah, na kuwa na hofu ya adhabu Yake.

Kila Muislamu pia (mwanaume) anapaswa kumuogopa Allaah kuhusiana na wanawake ambao wako chini ya ulinzi wake, na kutowaacha wakavaa mavazi ambayo Allaah na Mtume Wake wameharamisha, kama vile nguo za kuvutia, au mavazi ambayo ni ya kudhihirisha maumbile na uchi, au yale ya majaribio (fitnah) ya kuwashawishi watu. Anapaswa kukumbuka (mwanaume) kuwa yeye ni mchungaji na ataulizwa kwa alichokichunga siku ya Qiyaamah.

Tunaomba Allaah Ayaweke mambo ya Waislamu yawe sawa, na Atuongoze sote kwenye njia iliyonyooka, kwa kuwa Yeye ni Mwenye kusikia, Aliye Karibu na Mwenye Kujibu du’aa. Allaah Azitume swalah na salaam juu ya Mtume wetu Muhammad na juu ya familia yake Swahaba zake.

Fataawa al-Lajnah al-Daa'imah, 17/290


Pia imesemwa kwenye Fataawa al-Lajnah al-Daa'imah (17/297):

Nini ambacho mwanamke anaruhusiwa kudhihirisha mbele ya watoto wake ni yale mambo ambayo kidesturi huwa wazi, kama vile uso, mikono, miguu, na kadhalika.

Na Allaah Anajua zaidi

Swali:

Kipi kiasi kinachochukuliwa kuwa ni 'awrah kwa mwanamke awapo na wajomba zake kwa upande wa mama, wajomba zake upande wa baba na ndugu zake, nyumbani?

Jibu:
Anaruhusiwa kuonyesha kwa Mahram wake: uso, kichwa, shingo, mikono, miguu, chini ya muundi, na anapaswa kusitiri kila kitu mbali na hivyo tulivyotaja.

Shaykh Muhammad bin Swaalih al-‘Uthaymiyn Hijaab Mar-ah wa ziynatuha, ukurasa wa 43.


 Posted By Posted juu ya Thursday, May 10 @ 20:47:25 PDT na MediaSwahiliTeam
 

Comments 💬 التعليقات
 

For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 5
Kura: 2


Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora
Vizuri Sana
Mema
Kawaidar
Mbaya


Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa RafikiMada zinazohusiana

Mkuu - teknolojia na taaluma

 

EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And IslamAfrica.Com