Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   
 
Haki Hii Haki Gani Mbele Ya Allaah?
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis
Haki Hii Haki Gani Mbele Ya Allaah?

Bint Ahmadah
Mwenyezi Mungu Anatusimulia moja ya visa vilivyomo katika Qur-aan Tukufu:

"Na Maryam mtoto wa 'Imraan aliyejihifadhi nafsi yake na Tukampulizia humo roho Yetu (inayotokana na Sisi), na akayasadikisha maneno ya Mola wake, na Vitabu Vyake; na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevu (wakubwa)." (Suratu at-Tahrym: 12)"Na Maryam mtoto wa 'Imraan aliyejihifadhi nafsi yake na Tukampulizia humo roho Yetu (inayotokana na Sisi), na akayasadikisha maneno ya Mola wake, na Vitabu Vyake; na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevu (wakubwa)." (Suratu at-Tahrym: 12)

Je kusimama mbele ya vyombo vya habari, au kwenye mikutano ya hadhara, kwa msichana na kudai haki zinazoitwa za binaadamu kwa lengo la kutembea utupu au kujifananisha na mwanaume ndio haki aliyoipigania Bibi Mariamu?

Dada yangu, haki hiyo waitaka hali ya kuwa ni kichwa kitupu kisichomuelewa Mola Mlezi utaipata wapi? Ikiwa aya za Mungu wazigeuza unavyozitaka wewe, salama utaipata wapi? Elewa ya kwamba, hao waliotaka haki ya kweli basi walijitoa kiroho, kiimani, kisubra na kinguvu kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Pitia kurasa za Bibi Fatwimah, Mama 'Aaishah na Bibi Summayyah (Radhiya Allaahu ‘Anhunna) muone namna walivyokuwa na msimamo madhubuti wa iymaan ya Uislamu. Hawakupigania haki hizo kwa ajili ya matamanio yao binafsi na msukumo wa watu fulani (makafiri na wanafiki).

Waislamu hawatakiwi kushirikiana na makafiri kwenye masuala ya kuzipinda kanuni za Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) kama hayo ya haki za binaadamu. Wao ndio wafanyao njama mbali mbali za kuwapotosha Waislamu katika kila upande kama hili suala la kudai haki za wanawake ambalo wao wamelivalia njuga.

Lengo lao kuu si jengine ila kuwaelekeza njia nyengine Waislam wauone Uislam ni mgumu usiokwenda na wakati kabisa. Wanatufanyia hila kwa nia ya kwamba Uislam uonekane unawakandamiza wanawake kudai haki yao ya kupanda majukwaani kwenye mambo ya anasa. Anasa zinazohusu utembeaji utupu na uimbaji. Hali ya kuwa Uislam umekataza sauti ya mwanamke kusikikana nje ya mipaka, na imefanananishwa sauti hiyo mfano wa sauti ya punda.

Je wanawake tupo tayari kuwa sawa na mapunda kwa kufananishwa na kitendo hicho ambacho Mwenyezi Mungu Amekikataza? Tukiona makafiri wa kike wakisimama juu ya majukwaa na wakifanya wao wana haki ya kusema kila kitu hata kama sivyo, na wewe dada yangu Muislam unataka kuwaiga wao wanachokifanya. Si vyema kufanya kila ulionalo, pambanua mambo, na awali ya yote 'tafakari kabla ya athari'.

Tambuwa ya kwamba hayo si ya kuiga kwa Muislam wa kweli wa kiimani na kivitendo. Haitokuwa na maana utakaposimama mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na Uislam wa kuchovya jina tu wakati vitendo huna kitu. Haki hizi zipaniwazo sio haki tunazozitaka, bali ni mabalaa ndio tunayoyaomba yatufike kutokana na maasi hayo. Kisha tunakaa vikao na kusugua vichwa kujadiliana matatizo ya dunia. Matatizo haya yanatokana na nini kama kiumbe kuacha kutafakari ukubwa wa Aliyetuumba? Hatutafakari tumemkosa nini Mungu?

Waliopita nyuma kama Qawm 'Aad waliangamizwa kwa upepo tu kutokana na maasi waliyotenda. Mioyo yao ilifanana na hao wanawake wanaodai haki zao zisizoeleweka mbele ya Mola Mlezi. Hawakujali ujumbe wa Nabii Huud (‘Alayhi swalaatu was-salaam). Qur-aan inatueleza ya kwamba Qawm Huud waliangamizwa kwa upepo mkali, upepo uliowangoa watu hao mfano wa mti unavyongolewa mzima mzima kutoka ardhini:

"Hakika Tuliwapelekea upepo mkali katika siku ya nuhsi iendeleayo (kwao mpaka leo).

Ukiwang'oa watu (katika ardhi kisha unawabwata chini, wamelala, wamekufa) kana kwamba ni magogo ya mitende iliyong'olewa.

Basi ilikuwaje adhabu Yangu na maonyo Yangu!" (Suratul-Qamar: 19-21)

Je na sisi hatuyaoni majanga yote yanayotupata? Juzi Indonesia, jana India, kesho kutwa Tanzania. Tunawaiga Qawm Huud iliyolinganiwa miaka nenda miaka rudi lakini bado hawakuelewa kitu. Leo tuna miaka 1400 ya kushushwa Qur-aan, tunaipa kisogo huku tukijifunza kuimba nyimbo na kutingisha miili mbele ya majukwaa. Tupambanue athari za matendo yetu, tusije kufikwa na mitihani kama hiyo mikubwa mikubwa.

Hatutafika pahala kwa kusimama majukwaani tukidai kuwa ndio tunatetea haki zetu wanawake. Na kwa hakika, Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Habadilishi nyoyo za watu hadi wao wenyewe wawe tayari kubadilishika.

Kama Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anavyosema:

“Allaah Habadilishi hali za watu mpaka wafanye juhudi kubadilisha yaliyo nafsini mwao” (Suratu ar-Ra'ad: 11).

Huo ndio uhuru na demokrasia Aliotuwekea Mola wetu. Tupo huru kumuasi asubuhi na mchana, lakini tuelewe khatima yetu itakuwa mbaya mno:

"Na Mwenyezi Mungu Anapowatakia watu adhabu hakuna cha kuzuia wala hawana mlinzi yoyote badala Yake (Mwenyezi Mungu)." (Suratu ar-Ra'ad: 11).

Tujitahidi kurejea kwa Mola wetu kikweli na tulete toba iliyo ya kweli na tuache yale yote Mola Aliyoyakataza.

 Posted By Posted juu ya Thursday, May 10 @ 23:04:08 PDT na MediaSwahiliTeam
 

Comments 💬 التعليقات
 

For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا

Kuhusiana Viungo

· zaidi Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis:
Jinsi Ya Kumfurahisha Mkeo


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora
Vizuri Sana
Mema
Kawaidar
Mbaya


Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa RafikiMada zinazohusiana

Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

 

EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And IslamAfrica.Com