Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   
 
Yaliyokuwa Sunnah Na Bid'ah Katika Sherehe Za 'Iyd
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis Imefasiriwa na Ummu 'Abdil-Wahhaab
Yaliyokuwa Sunnah Na Bid'ah Katika Sherehe Za 'Iyd


BismiLLaahi wa AlhamduliLLaah wa swalaatu wa salaam 'alaa RasuliLLaah Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa aswahaabihi wa sallam.

“Kwa kila jamii ya watu kuna sikukuu, na hii ‘Iyd ndiyo sikukuu yetu” alisema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumwambia Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu). [Al-Bukhaariy na Muslim].“Sikukuu yetu” ina maana kubwa kwa Waislaam, kwa sababu inatujulisha kwamba hii ni yetu na asili yake imetokea kwenye sharia zetu tu peke yake.  Kwa kuwa sherehe hizi zimeegemea kwenye taratibu za kidini, ni muhimu sana kuzifafanua ili ziwe na furaha kubwa na mikusanyiko yenye kuleta hisia ya kuwa hizi sikukuu ni zetu (sisi Waislaam), na ni tofauti na zile sikukuu za Mushrikiyna. Haturuhusiwi kusherehekea Christmas, Hanuka, au sikukuu za Kipagani, na shukrani zetu zote tuzielekeze kwa Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) peke yake.


Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuamrisha katika hutuba zake nyingi kuwa tujitofautishe na Mushrikiyn (Wapagani), na hizi ‘Iyd mbili ni miongoni mwa sikukuu zile ambazo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametutaka tuchukue tahadhari kubwa ya kujitofautisha sana nao (Mushrikiyn).  Ndiyo sababu akasema, baada ya kuona watu wa Madinah walipokuwa na sherehe mbili wakizisherehekea kabla ya kuja Uislaam, “Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala)) ameshakupeni nyinyi kilicho bora kuliko vyote (sikukuu):  ‘Iydul-Adhw-haa (ya kuchinja) na ‘Iydul-Fitwr”. [Ahmad, Abu Dawuud na An Nasaaiy].


‘Iydul-Adhw-haa huja baada ya kumalizika ibada ya Hijja na ‘Iydul-Fitwr huja baada ya kumalizika Swawm ya mwezi wa Ramadhaan. Kwa hivyo haishangazi hiyo, ni lazima tuzionyeshe na tuzifafanue ‘Iyd zetu. Kutokana na bayana hizi zilizo wazi, Wanavyuoni wa Kiislaam ni lazima watilie mkazo sana juu ya kuzitofautisha sherehe zetu kutokana na zile za Mushrikiyn.


Hii ni kwa sababu sherehe zina taathira kubwa katika akili na tabia ya mwanaadam. Kuwa tofauti katika Sherehe vile vile ina maana kwamba ni lazima tusijishirikishe (tusihudhurie) kabisa katika sherehe za Mushrikiyn. ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema: “Msijifundishe lugha ya Mushrikiyn – bila ya kuwa kuna umuhimu ndani yake – wala Msiingie makanisani wakati wa sherehe zao kwa sababu Hasira za Allaah huteremka juu yao.” [Al-Bayhaqiy].


Sisi, Waislaam, huenda hata tufunge (Swawm) katika siku za sikukuu za Mushrikiyn. Ummu Salamah (Radhiya Allaahu ‘anha) amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na kawaida ya kufunga siku za Jumamosi na Jumapili, na alipoulizwa Alisema: Kuna siku mbili katika siku za sherehe za Mushrikiyn kwa hivyo napenda kwenda kinyume na wao katika sherehe zao”. [Ahmad na An-Nasaaiy].    


Kulikadiria wazo hili la kuwa tofauti na Mushrikiyn, ni muhimu sana kusema kwamba: Ili tuwe tofauti kwenye sherehe zetu na katika mwenendo ambao Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametutaka tuwe nao, ni lazima tufuate mwenendo wake (Sunnah) kikamilifu. Kwa kufanya hivyo kutatupatia malipo mema (thawabu) ya kuwa wafuasi wa kweli wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Kwa hivyo tukitaka kuwa wafuasi wake ni lazima tuelewe ni yepi Bid’ah (uzushi) katika sherehe zetu. Bid’ah inakuja pale Sunnah hutumika mahali pasipo pake! Ibn Taymiyyah amesema: “Hakuna nafasi katika moyo wa binaadam kwa yote mawili; Sunnah na Bid’ah.” [Al-Iqtidhwaa]. Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Amesema:


{Sema – Ewe Muhammad – Ikiwa kweli mnampenda Allaah basi nifuateni mimi, Allaah Atakupendeni}. [Aali-Imraan, 3:31]


Ndugu wapenzi, tunawasilisha kwenu baadhi ya matendo ya Sunnah katika sikukuu ili muweze kujaribu kuyatekeleza. Vile vile yanawasilishwa baadhi ya yaliyokuwa Bid’ah ili katika sikukuu muweze kuyaepuka. Kuna umuhimu mkubwa sana katika kufuata mwenendo wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wa ‘Iyd ili kikweli kweli tuweze kusema kwamba sikukuu zetu ni tofauti na zile sikukuu za Mushrikiyn.
YALIYOKUWA SUNNAH KATIKA 'IYD 

KUVAA MAVAZI MAZURI
Siku ya ‘Iyd ni Sunnah kuvaa mavazi mazuri kabisa tuliyo nayo. Imehadithiwa kwamba Ibn ‘Umar alikuwa akifanya hivyo pamoja na Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). [Fat-hul-Baariy


KUSWALI SWALAH YA 'IYD
Ni lazima (Waajib) kusali Swalah ya ‘Iydul-Fitwr. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake hawakuacha kabisa kufanya hivyo, na vile vile walikuwa wakiwakusanya watu kuitekeleza Swalah hiyo wakiwemo wanawake wenye  hedhi (hawaingii kwenye kuswali lakini wanashuhudia kheri na du’aa kwa Waislamu), watoto na vikongwe. [Al-Bukhaariy na Muslim]. 

KULA TENDE KABLA YA KWENDA KUSWALI (KATIKA 'IYDUL-FITWR)
Ni Sunnah kula tende kabla ya kuondoka kuelekea kusali Swalah ya ‘Iyd ili kuonyesha kwamba hatujafunga. “Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa hatoki kwenda kuswali Swalah ya ‘Iyd ila baada ya kula tende.” [Al-Bukhaariy na Ahmad]. Ama katika 'Iydul-Adhwhaa ni Sunnah kutokula kabla ya kwenda msikitini, na anaposhuka baada ya Swalah ni bora kitu cha kwanza kula ni ile nyama ya Udhw-hiyah ikiwa itapatikana. 

KULETA TAKBIRA KWA SAUTI
Ni Sunnah kuleta Takbira kwa sauti tunapotoka majumbani mwetu kuelekeya kwenye Swalah ya ‘Iyd. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akileta Takbira mpaka anamaliza Swalah. [Silsilat Al-Ahadiyth As-Swahiyhah - Shaykh Al-Albaaniy]
Hakuna Hadiyth inayohusiana na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba nini kisemwe wakati wa kuleta Takbira tunapoelekeya kusali, lakini Ibn Mas’uud alikuwa akisema yafuatayo:
Allaahu Akbar (mara mbili) (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa)


Laa Ilaha Illa Allaah (Hapana Mola Ila Mwenyezi Mungu)


Allaahu Akbar (mara mbili) (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa)


Wa Lillaahil Hamdu (Na Shukrani Zote ni za Mwenyezi Mungu) [Imesimuliwa na Ibn Abi Shaybah]. 

KUBADILISHA NJIA WAKATI WA KWENDA KUSWALI NA WAKATI WA KURUDI
Jaabir (Radhiya Allaahu ‘anhu) amehadithia: “Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akirudi kutoka kwenye Swalah ya ‘Iydul-Fitwr kupitia njia tofauti na ile aliyoendea.” [Al-Bukhaariy]. 

KUSWALI KWENYE MUSWALLAA
Ni Sunnah kwa wenye kuswali Swalah ya ‘Iyd kuswali kwenye Muswallaa (katika uwanja ulio wazi) na sio Misikitini. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwahi kuswali Swalah ya ‘Iyd Msikitini. Abu Sa’iyd (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesimulia: “Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akienda kuswali ‘Iydul-Fitwr na ‘Iydul-Adhw-haa kwenye Muswallaa, na kitu cha awali alichokuwa akikifanya ni kuswali.” [Al-Bukhaariy na Muslim] 

SWALAH YA 'IYD HAINA ADHAANA WALA IQAAMAH
Jaabir ibn Samurah (Radhiya Allaahu 'anhu) kasema: "Niliswali zaidi ya mara moja na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na haikuweko Adhana wala Iqaamah" [Muslim]  

HAKUNA SWALAH YA SUNNAH KABLA AU BAADA YA SWALAH YA 'IYD


 Ibn ‘Abbaas amesimulia: “Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Aliswali rakaa mbili kwa ajili ya ‘Iyd na hakuswali tena baada yake au kabla yake.” [Al-Bukhaariy] 

RUHUSA KUSIKILIZA NASHIYD
Siku ya Sikukuu inaruhusiwa kusikiliza Nashiyd bila ya kutiwa ala za muziki hususan kwa watoto. 
YALIYOKUWA BID'AH KATIKA 'IYD (UZUSHI KATIKA DINI)
Ni Bid’ah (uzushi katika dini):


KUNYOA NDEVU
Kunyoa ndevu hasa kwa makusudi ya kukusudia ‘Iyd. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametukataza kunyoa ndevu zetu; ni aibu kufanya hivyo katika siku kubwa ambayo ni ya kufafanua na kudhihirisha tofauti ya sherehe zetu na zile za Mushrikiyn, Muislaam hunyoa ndevu akajisafisha kabisa na kuonekana kuwa hana tofauti (hufanana) na Mushrikiyn

KUWAIGA MAKAFIRI KATIKA MAAMKIZI YAO   
Kuwaiga Mushrikiyn katika mienendo yao na mavazi yao, na kupeana mikono na Wanawake. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Ni bora kwa mwanamme kupigwa sindano katika kichwa chake kuliko kuushika mkono wa mwanamke ambaye si halali yake.” [Silsilat Al-Ahadiyth As-Swahiyhah - Shaykh Al-Albaaniy]  

KUSHERHEKEA KWA TAFRIJA (PARTY) ZA MAASI
Kukusanyika na kuchanganyika wanawake na wanaume kwa karamu, kusikiliza muziki, ngoma, kuvaaa mavazi yasiyo katika sheria na kuweko vinywajii vya haramu.   Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kutakuja watu katika ummah wangu watakaozini, wanaume watakaovaa hariri, wengine watakunywa ulevi, na muziki utahalalishwa.” [Al-Bukhaariy, Abu Dawuud na Al Bayhaqiy]. 

WANAWAKE KUTOTIMIZA HIJAAB
Wanawake kutokuvaa vazi la stara (hijaab), kujipamba, kunyoa nyusi, na kuonyesha mapambo yao wazi kama kutokufunika nywele, kujiremba na kujitokeza mbele ya wasio Mahram wao. (ambao hawawezi kuwaoa kama baba, kaka n.k.)  Kufanya hivyo kunadhaniwa kwamba ni kusherehekea ‘Iyd na ilhali kunatendwa dhambi kubwa. 

KUZURU MAKABURI
Kuzuru makaburini hususan siku ya ‘Iyd. Inaruhusiwa kuzuru makaburini siku yoyote katika mwaka lakini isiwekwe kuwa siku ya ‘Iyd ni maalumu kufanya hivyo.


KUFANYA ISRAFU
Kuharibu pesa na kufanya israfu ya chakula badala ya kuwapa  maskini (na mafakiri).


Tunamuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala)) Atusaidie tuepukane na Bid’ah, na Atuelekeze kwenye kuzifuata Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 Posted By Posted juu ya Friday, June 29 @ 17:37:57 PDT na MediaSwahiliTeam
 

Comments 💬 التعليقات
 

For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا

Kuhusiana Viungo

· zaidi Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis:
Jinsi Ya Kumfurahisha Mkeo


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora
Vizuri Sana
Mema
Kawaidar
Mbaya


Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa RafikiMada zinazohusiana

Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

 

EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And IslamAfrica.Com