Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   
 
Matayarisho Ya Ramadhaan: Jitathmini Kabla Ya Ramadhaan
 
Maamuzi Ya Kufunga Ramadhan Na Kuabudu Imetayarishwa na: Abu Faatwimah
Matayarisho Ya Ramadhaan: Jitathmini Kabla Ya Ramadhaan

1 - Nitapenda kuikaribisha Ramadhaan kwa:
A.     Kuomba Du'aa kufikishwa kukutana na Ramadhaan nikiwa katika hali ya siha nzuri na usalama na kuwafikishwa kuweza kuifunga na kufanya ibadah zangu kama zitakiwavo kwa kufuata Sunnah na kwa hamu, uchangamfu na wepesi.B.     Kujitayarisha kwa kujiwekea maazimio nitayopenda kuwafikishwa kuyafikia na kuwa tayari kwa kila aina ya matayarisho yatayoweza kunifikisha kuwa na fursa nzuri ya kuchuma mema.
C.    Kuomba Tawbatun-Nasuuha na kuwaomba msamaha wale niliowakosea. 
D.    Kujikumbusha Fiqh ya Swawm.
E.     Kujitathmini na kufungua ukurasa mpya katika maisha yangu.
2 - Cha mwanzo ninachofikiria kuhusu Ramadhaan ni:
A.     Maakulaati na vinywaji vya aina mbali mbali, futari, daku.
B.     Njaa, kiu, taabu.
C.    Kufunga na kujiepusha na yote yaliyokatazwa.
D.    Kusoma Qur-aan kwa wingi na kuswali Taarawiyh.
E.     Kucheza karata, ludo, keram , mpira kwa wingi na kadhalika.
F.     Kutazama sana filamu na vipindi mbalimbali kwenye TV kuvuta wakati.
3 - Lengo kubwa nitalopenda kuwafikishwa kulifikia katika Ramadhaan hii ni:
A.     Kuongeza daraja ya ucha Mungu wangu.
B.     Kujenga na kurekebisha tabia zangu.
C.    Kuiga hali za wema waliotangulia.
D.    Kufunga kwa Iymaan na Ihtisaab ili kuyapata yaliyoandaliwa kwa wenye kufunga huku wakiwa na hali hivyo.
4 – Kuhusu Swalaah, nitapenda kufikia yafuatayo:
A.     Kuwa na khushuu’ na utulivu katika Swalaah zote nitazoswali.
B.     Kuswali Taarawiyh katika siku za mwanzo na katika kumi la mwisho.
C.    Kuswali Swalaah zote kwa Jamaa’ah Msikitini.
D.    Kujihimu kuswali Swalaah ya Taarawiyh Jamaa’ah kwani kila mtu hupenda kuiswali.
E.     Kuhakikisha  kuwa kila siku nahitimisha rakaa za Tarawiyh na Imaam nipate thawabu za Qiyaamul-Layl.
F.     Kushikama na Swalaah za Sunnah ziwe za Muakkadah (zilizosisitizwa) na zisizo Muakkadah (zisizosisitizwa) na Swalaah ya Dhuhaa.  
5- Uhusianao wangu na Qur-aan, nitapenda kuwafikishwa kufikia:
A.     Kuhitimisha Qur-aan angalau mara moja.
B.     Kuwashawishi ndugu, jamaa na marafiki zangu kusoma Qur-aan sana.
C.    Kusoma Qur-aan kwa pamoja na familia yangu.
D.    Kuhitimisha Qur-aan baada ya siku kumi (mara tatu kwa mwezi).
E.     Kuhitimisha Qur-aan kila baada ya wiki (mara nne kwa mwezi).
F.     Kuhitimisha Qur-aan kila baada sita (mara tano kwa mwezi).
G.    Kusoma tafsiri ya Qur-aan hasa Suurah au Aayah nitazozisoma japo kwa ufupi.
6 - Kuhusu milango ya kheri, nitapenda niwafikishwe katika yafuatayo:
A.     Kumfutarisha japo mtu mmoja katika waliofunga katika watu wema na sio  kila mtu tu.
B.     Kuhakikisha kuwa kila siku nafanya/natekeleza japo  jema moja.
C.    Kutoa Swadaqah kwa wingi.
D.    Kujitahidi kuleta Adhkaar na kumkumbuka Allaah kila wakati na kujihakikishia kuwa naleta na kushikamana na Adhkaar zilizothibiti baada ya kila Swalaah.
E.     Kuwa na Niyyah ya kumtembelea mgonjwa/wagonjwa japo mara moja kwa wiki.
F.     Kuwa na Niyyah ya kuhudhuria mazishi ya Muislamu yatayotokea katika Ramadhaan.
G.    Kuwa na Niyyah ya kulisha masikini na kufutarisha jamaa zangu nyumbani.
H.    Kumpelekea kitu nikipikacho jirani yangu japo mmoja kila siku au kila siku mbili au tatu.
7 - Kuhusu elimu na maarifa, nitapenda kuwafikishwa katika yafuatayo:
A.     Kusoma kitabu japo kimoja katika fani ya ’Aqiydah/Tawhiyd  na Siyrah.
B.     Kuhudhuria darsa na mihadhara ya Dini.
C.    Kuongeza maarifa yangu katika Fiqh ya Swawm.
D.    Kutembelea website za Kiislam zenye mafunzo sahihi.

E.     Kuangalia na kusikiliza CDs za Wahadhiri wenye kushikamana na ‘Aqiydah sahihi na Sunnah.
F.     Kusoma kitabu au mlango katika kitabu cha Swahiyh Al-Bukhaariy au Swahiyh Muslim kwa lugha ninayoielewa. Na vitabu mbalimbali vinavyopatikana bure kwenye mtandao kama hapa http://www.alhidaaya.com/sw/vitabu
8 - Kuhusu Munkar (maovu) nitapenda kuwafikishwa katika yafuatayo:
A.     Kuachana na kuwa mbali na kusema uongo.
B.     Kuachana na kusengenya.
C.    kuwa mbali na kufitinisha watu.
D.    Kuweka nia ya kuwa mbali na mihadhara au shughuli za watu wanaopinga  Sunnah na kulingania au kushajiisha kila uzushi.
E.     Kuwa mbali istihzai (mzaha) au mchezo au kukejeli Sunnah yoyote ile katika Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na watu wake hata kama mimi siitekelezi.
F.     Kujitenga, kujiepusha na kuwa mbali na watu, baraza na mikusanyiko yenye kukejeli Dini na kukejeli kila lenye kuambatana na Dini na watu wanaotekeleza au wanaoisimamia Dini.
G.    Kujiepusha au kuachana na kuwatumia watu ujumbe au maelezo yasiyokuwa sahihi kuhusu Dini na kuachana mara moja kutuma ujumbe kila siku ya Ijumaa kwa kusema Jumaa Mubaarak au Jumaa Kariim.
9 - Kuhusu Da’wah, nitapenda niwafikishwe katika yafuatayo:
A.     Kuamrisha japo jema moja na kukataza japo baya moja katika jamii yangu.
B.     Kugawa na kutawanya CD’s au makala za Dini zenye mafunzo sahihi.
C.    Kuwatumia wenzangu ujumbe ‘messages’ wa Dini kama vile Hadiyth sahihi au Aayah katika email (barua pepe) zao au simu zao angalau kila wiki.
D.    Kushiriki kikamilifu katika mipango yoyote ile yenye lengo la kuwakusanya Waislamu ili wasikie chochote kile kilicho sawa na sahihi kuhusu Dini yao.
E.     Kumsemesha asiyenisemesha; kuwapatanisha waliogombana na kuhasimiana, kumsamehe aliyenikosea.
F.     Kumsaidia mwenye haja na kumuwepesishia mwenye uzito na shida.
G.    Kuwakumbuka kwa du’aa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki katika masiku yote ya Ramadhaan hasa walionitangulia mbele ya Haki.
10 - Kuhusu wakati,  nitapenda  niwafikishwe kama ifuatavyo:
A.     Baada ya Swalaah ya Alfajiri mpaka kuchomoza kwa Jua; kumkumbuka Allaah na kuswali raka'ah mbili litapokuwa Jua limenyanyuka kadiri ya mshale  na kutarajia fadhila za wenye kufanya hivyo.
B.     Kabla ya Jua kuzama (Magharibi); kujishughulisha na Adhkaar, kumsabihi Allaah na kuomba du’aa.
C.    Wakati wa Suhuur (wakati wa kula daku kabla ya Alfajiri); kujishughulisha na moja tu, nalo ni kuomba maghfira (Istighfaar).
11 - Kuhusu adabu za Swawm nitapenda kushikamana na:
A.     Kuchelewesha kula daku.
B.     Kuharakisha kufutari mara tu ikithibiti kuzama kwa Jua.
C.    Kuanza kufungua kinywa kwa tende au maji.
12 - Kuhusu Swawm nitapenda niwafikishwe na kujitahidi kujichunga na kuwa mbali na:
A.     Kula au kunywa kwa makusudi.
B.     Kuingiliana au kuchezeana kwa kukumbatiana kubusiana na mke/mume wangu


C.    Kujitapisha kwa makusudi.


D.    Kujichua (kuyatoa manii) kwa makusudi.


E.     Kuazimia (kutia Niyyah ya) kula.
13 - Kuhusu Swawm yangu; sitokuwa na wasiwasi na yafuatayo kwa kuwa hayatoiharibu:
A.     Kula au kunywa kwa kusahau, kimakosa au kulazimishwa.
B.     Kuingia maji ndani ya matundu ya mwili bila kukusudia, kwa mfano wakati wa kuoga.
C.    Kudungwa sindano mwilini kama vile chanjo za safari
D.    Kutumia dawa katika macho.


E.     Kuoga na kujimwagia maji mwilini.


F.     Kuonja chakula.


G.    Kuamka na janaba au kuota mchana wa Ramadhaan na kutokwa na manii.
H.    Kupiga mswaki wakati wowote ule nikiwa katika Swawm.
I.     Kutumia dawa ya Asthma ya kuvuta hewa mwilini .


 Posted By Posted juu ya Friday, June 29 @ 17:41:43 PDT na MediaSwahiliTeam
 

Comments 💬 التعليقات
 

For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا

Kuhusiana Viungo

· zaidi Maamuzi Ya Kufunga Ramadhan Na Kuabudu
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu Maamuzi Ya Kufunga Ramadhan Na Kuabudu:
Sha'abaan: Fadhila Zake Na Uzushi Wa Nisfu Sha'abaan - Nasiha Za Minas


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora
Vizuri Sana
Mema
Kawaidar
Mbaya


Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa RafikiMada zinazohusiana

Maamuzi Ya Kufunga Ramadhan Na Kuabudu

 

EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And IslamAfrica.Com