Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   
 
Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Kumi (Ya Mwisho) Wanaume Na Wanawake Wanaomdhu
 
Habari Idadi ya habari na hadithi Makala Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Kumi (Ya Mwisho) Wanaume Na Wanawake Wanaomdhukuru sana Allaah

Anasema Allaah سبحانه وتعالى:
إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِينَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِينَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ وَالصَّائِمِينَ وَالصَّائِمَاتِ وَالْحَافِظِينَ فُرُوجَهُمْ وَالْحَافِظَاتِ وَالذَّاكِرِينَ اللَّهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا ﴿35﴾
((Hakika
Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na watiifu wanaume na watiifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wasemao kweli wanawake, na wanaosubiri wanaume na wanaosubiri wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanyenyekevu wanawake, na watoao sadaka wanaume na watoao sadaka wanawake, na wanaofunga wanaume na wanaofunga wanawake, na wanaojihifadhi tupu zao wanaume na wanawake na wanaomdhukuru Allah kwa wingi wanaume na wanawake, Allah Amewaandalia msamaha na ujira mkubwa)) [Al-Ahzaab:35]

Kama tunavyoona katika Aayah hiyo tukufu kwamba kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa wingi ni sifa ya kumi na ya mwisho; mja atakapoweza kuzichuma sifa zote hizo kumi basi malipo yake yatakuwa ni kusamehwa madhambi yao na kulipwa thawabu nyingi kabisa.
قَالَ اِبْن أَبِي حَاتِم عَنْ أَبِي سَعِيد الْخُدْرِيّ رَضِيَ اللَّه عَنْهُ قَالَ : إِنَّ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((إِذَا أَيْقَظَ الرَّجُل اِمْرَأَته مِنْ اللَّيْل فَصَلَّيَا رَكْعَتَيْنِ كَانَا تِلْكَ اللَّيْلَة مِنْ الذَّاكِرِينَ اللَّه كَثِيرًا وَالذَّاكِرَات)) أبو داود ،
Ibn Abi Haatim amesesma kutoka kwa Abi Sa'iydil-Khudriy (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (Mume akimuamsha mkewe usiku wakaswali Rakaa mbili watakuwa usiku huo ni miongoni mwa wale wanaume na wanawake wanaomdhukuru Allah sana)) [Abu Daawud]

عَنْ أَبِي هُرَيْرَة رَضِيَ اللَّه عَنْهُ قَالَ : كَانَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَسِير فِي طَرِيق مَكَّة فَأَتَى عَلَى جُمْدَان فَقَالَ ((هَذَا جُمْدَان سِيرُوا فَقَدْ سَبَقَ الْمُفَرِّدُونَ)) قَالُوا وَمَا الْمُفَرِّدُونَ ؟ قَالَ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((الذَّاكِرُونَ اللَّه كَثِيرًا وَالذَّاكِرَات)) ثُمَّ قَالَ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((اللَّهُمَّ اِغْفِرْ لِلْمُحَلِّقِينَ)) قَالُوا وَالْمُقَصِّرِينَ قَالَ ((اللَّهُمَّ اِغْفِرْ لِلْمُحَلِّقِينَ)) قَالُوا وَالْمُقَصِّرِينَ قَالَ ((وَالْمُقَصِّرِينَ)) إمام أحمد تفرد به من هذا الوجه، ورواه مسلم دون آخره

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba: Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitembea katika njia ya Makkah na alipofika mlima wa Jumdaan akasema: ((Huu ni (mlima wa) Jumdaan, endeleeni kwani Mufarriduun wametangulia mbele)). Wakasema: Ni nani Mufarraduun? Akasema: ((Wanaomdhukuru Allah sana wanaume na wanawake)). Kisha akasema: ((Ewe Allah, Waghufurie walionyoa nywele zao)). Wakasema: "Na waliopunguza". Akasema: ((Ewe Allah Waghufurie walionyoa nywele zao)). Wakasema: "Na waliopunguza". Akasema: ((Na waliopunguza)). [Imaam Ahmad kaipokea kwa masimulizi hayo, na Muslim bila ya maelezo ya mwisho]

Kumkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ni amri pia kutoka Kwake kama Anavyosema:

(( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا اللَّهَ ذِكْراً كَثِيراً))

((Enyi mlioamini mtajeni Allah sana)) [Suratul-Ahzaab: 41]

Na fadhila za kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ni nyingi sana, tutazitaja chache tu hapa:

Ukimkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Naye Atakukumbuka:

Amesema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)

((فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُواْ لِي وَلاَ تَكْفُرُونِ ))

((Nitajeni Nami Nitawataja, na Nishukuruni na wala msinikufuru)) [Suratul Baqarah:152]

Ni ibada bora kabisa yenye daraja ya juu:

قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((أَلَا أُخْبِركُمْ بِخَيْرِ أَعْمَالكُمْ وَأَزْكَاهَا عِنْد مَلِيككُمْ وَأَرْفَعهَا فِي دَرَجَاتكُمْ وَخَيْر لَكُمْ مِنْ تَعَاطِي الذَّهَب وَالْفِضَّة وَمِنْ أَنْ تَلْقَوْا عَدُوّكُمْ غَدًا فَتَضْرِبُوا أَعْنَاقهمْ وَيَضْرِبُوا أَعْنَاقكُمْ ؟ قَالُوا بَلَى يَا رَسُول اللَّه قَالَ ذِكْر اللَّه عَزَّ وَجَلَّ)) أحمد
((Hivi niwaambieni khabari ya matendo yenu bora, na ambayo ni masafi mno mbele ya Mola wenu, na ambayo ni ya juu mno katika daraja zenu, na ambayo ni bora kwenu kuliko kutoa dhahabu na fedha, na ambayo ni bora kuliko kukutana na adui zenu, mkawapiga shingo zao)) Wakasema masahaba: Ndio . Akasema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Ni kumtaja Allah)) [Ahmad]

Mwenye kumkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) huwa karibu Naye:

وقال صلى الله عليه وسلم ((يقول الله تعالى : أنا عند ظن عبدي بي ، وأنا معه إذا ذكرني ، فإن ذكرني في نفسه ذكرتهُ في نفسي ، وإن ذكرني في ملأ ذكرته في ملأ خير منهم ،وإن تقرب إلى شبراً تقربت إليه ذراعاً ،وإن تقرب إلي ذراعاً تقربت إليه باعاً ، وإن أتاني يمشي أتيتهُ هرولة)) البخاري و مسلم

Amesema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Allah Anasema: Mimi Niko mbele ya dhana ya mja Wangu Kwangu, akinitaja moyoni Nami Ninamtaja moyoni na akinitaja katika kundi, Nami Namtaja katika kundi bora zaidi ya hilo lake, na akijikurubisha Kwangu paa moja, basi Mimi Najikurubisha kwake kiasi cha dhiraa, na akijikurubisha Kwangu kiasi cha dhiraa, basi Mimi Nitajikurubisha kwake kiasi cha kunyoosha mkono hadi kati ya kifua, na akinijia kwa mwendo mdogo basi Nami Nitamjia kwa mwendo wa kasi)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Asiyemkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ni kama mtu aliyekufa:

قال صلى الله عليه وسلم ((مثل الذي يذكر ربه والذي لا يذكر ربه مثل الحي والميت)) البخاري

((Mfano wa anayemtaja Mola wake na asiyemtaja ni mfano wa alie hai na maiti)) [Al-Bukhaariy]

Kumkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) ni ibada nyepesi inayowezwa kudumishwa

عن عبد الله بن بسرٍ رضي الله عنهُ أن رجلاً قال : يا رسول الله إن شرائع الإسلام قد كثرت علي فأخبرني بشيءٍ أتشبث به. قال : (( لا يزال لسانك رطباً من ذكر الله )) ألترمذي, إبن ماجه وصححه شيخ الألباني

Imepokelewa kutoka kwa Abdullah Bin Busr (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba mtu mmoja alisema: Ewe Mjumbe wa Allah, ibada za dini zimekuwa nyingi kwangu, basi nieleze kitu ambacho nitaweza kudumu nacho. Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: ((Ulimi wako utaendelea kuwa rutuba (yaani sio ukavu) kwa kumtaja Allah)) [At-Tirmidhiy na Ibn Maajah na Sahiyh Shaykh Al-Albaaniy kataja kuwa ni sahihi]
‘Abdulllah Ibn ‘Amru Ibn Al-‘Aasw - Swahaba aliyekuwa akimdhukuru sana Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)

Ni Swahaba ambaye aliingia katika Uislamu kabla ya baba yake tokea siku aliyochukua kiapo cha bay’aa (kiapo cha utiifu). Alikuwa mwenye moyo uliojaa nuru ya twaa ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)

Alitumia wakati wote katika kusoma na kuifahamu Qur-aan ili utakapofika wakati wa kumalizika wahyi wote awe ameshaihifadhi yote. Na hakuisoma tu kwa ajili ya uwezo wa kuihifadhi, bali aliisoma na kufuata amri zake kama Maswahaba wengineo.

‘Abdullah ibn ‘Amru ibn Al-‘Aasw alikuwa Mcha Mungu sana, hakuna lolote ambalo lilimzuia au kumshughulisha na ibada. Katika vita na maadui wa Kiislamu alionekana katika mstari wa mbele kabisa akitamani kufa kama shahidi. Kisha msikitini daima akionekana, akiwa anafunga mchana, akiswali usiku na ulimi wake haukujua la kuzungumza ya kidunia ila tu kumtaja Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Alikuwa akikhitimisha Qur-aan kila siku moja. Hali yake hii ya ibada kutwa kucha ilimfanya Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amuingilie katika ibada yake kwa kumnasihi apunguze ili afuate Sunnah zake na akipe kila kitu haki yake. Hadiyth yake ni ndefu mashuhuri iliyokusanywa na Maimam sita mashuhuri wa hadiyth. Na hapa chini ni masimulizi kutoka kwa Imam Muslim:
"كنت أصوم الدهر ، وأقرأ القرآن كل ليلة ، قال: فإما ذكرت لرسـول الله -صلى الله عليه وسلم- ، وإما أرسل لي ، فأتيته ، فقال : "ألم أُخبر أنك تصوم الدهر وتقرأ القرآن كل لـيـلـة ؟" فقلت: بلى يا نبي الله؛ ولم أرد إلا الخـيـر، قال:" فـإن بحـسـبك أن تصوم من كل شهر ثلاثة أيام... ، ثم قال : "واقرأ القرآن في كل شهر" ، قال: قلت: يا نبي الله: إني أطيق أفضل من ذلك ، قال :"فاقرأه في سـبـع، ولا تـزد عـلــى ذلك ، فإن لزوجك عليك حقاً ، ولزورك عليك حقاً ، ولجسدك عليك حقاً"، قال : فشددت ؛ فشدد علي ، قال: وقال لي النبي-صلى الله عليه وسلم- :"لعلك يطول بك العـمــر" ، فصرتُ إلى الذي قال لي النبي-صلى الله عليه وسلم- ، فلما كبرت وددت أني قبلت رخصة النبي-صلى الله عليه وسلم-.

Nilikuwa nikifunga mwaka mzima, na nikisoma Qur-aan kila usiku". Akasema: Alipojulishwa Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaniita kwake nikaenda. Akasema: ((Nimesikia kwamba unafunga mwaka mzima na unasoma (unakhitimisha) Qur-aan kila usiku?)) Nikasema: Ndio ewe Mtume wa Allah. Wala sitaki lolote ila kheri tu. Akasema: ((Inakutosheleza ukifunga katika kila mwezi siku tatu…)) Kisha akasema: ((Na usome Qur-aan (ukhitimishe) kila mwezi)). Akasema: Nikasema: Ewe Mtume wa Allah, mimi hakika naweza kufanya vizuri zaidi ya hivyo. Akasema: ((Basi soma katika siku saba na usizidishe juu ya hivyo, kwani mke wako ana haki na wewe, na wageni wako wana haki kwako, na mwili wako una haki kwako)). Akasema: Kila nikimkazania (nizidishe ibada) alikuwa akinikazania (nipunguze ibada). Akasema: Akaniambia Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): ((Huenda umri ukawa mrefu kwako)) Nikaendeleza (ibada) kama alivyoniambia Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Nilipokuwa mkubwa kiumri nilipendelea kufuata rukhsa aliyonipa Nabii (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)


 Posted By Posted juu ya Monday, December 03 @ 22:39:28 PST na MediaSwahiliTeam
 

Comments 💬 التعليقات
 

For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا

Kuhusiana Viungo

· zaidi Habari Idadi ya habari na hadithi Makala
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu Habari Idadi ya habari na hadithi Makala:
Vidokezo Muhimu Kwa Wazazi Wenye Wasichana Na Wavulana


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora
Vizuri Sana
Mema
Kawaidar
Mbaya


Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa RafikiMada zinazohusiana

Habari Idadi ya habari na hadithi Makala

 

EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And IslamAfrica.Com