Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   
 
Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Saba - Wanaume Na Wanawake Watoao Sadaka
 
Maamuzi Ya Kufunga Ramadhan Na Kuabudu Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Saba - Wanaume Na Wanawake Watoao Sadaka

Anasema Allaah سبحانه وتعالى:
((إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِينَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِينَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ …))
((Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na watiifu wanaume na watiifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wasemao kweli wanawake, na wanao subiri wanaume na wanaosubiri wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanyenyekevu wanawake, na watoao sadaka wanaume na watoao sadaka wanawake…)) [Al-Ahzaab:35]Nini maana ya sadaka?

Sadaka ni kufanya wema kwa watu wenye kuhitaji na ambao ni dhaifu, wasiokuwa na uwezo wa kifedha za kuwatoshelezea mahitaji yao, au kuwasaidia wasiokuwa na watu wa kuwapa msaada wa fedha. Hivyo huwapa kutoka katika mali zao zinazozidi kwa mapenzi na kutaka kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa kutekeleza Aliyoyaamrisha katika Qur-aan kama anavyosema:

((وَمَا تُنفِقُواْ مِنْ خَيْرٍ فَلأنفُسِكُمْ وَمَا تُنفِقُونَ إِلاَّ ابْتِغَاء وَجْهِ اللّهِ وَمَا تُنفِقُواْ مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لاَ تُظْلَمُونَ))

((Na kheri yoyote mnayotoa ni kwa nafsi zenu. Wala msitoe ila kwa kutafuta wajihi wa Allah. Na kheri yoyote mtakayotoa mtalipwa kwa ukamilifu, wala hamtadhulumiwa)) [Al-Baqarah:272]

Al-Hasan Al-Basri amesema: "Kila Muumini anapotumia (sadaka) pamoja na matumizi yake mwenyewe hutafuta radhi za Allah [Ibn Haatim 3:1115].
Abubakar (Radhiya Allahu 'anhu) alijulikana kuwa na sifa hiyo ya ukarimu wa kutoa sadaka na ndio maana zilipoteremka Aayah:

وَسَيُجَنَّبُهَا الْأَتْقَى ﴿17﴾ الَّذِي يُؤْتِي مَالَهُ يَتَزَكَّى ﴿18﴾ وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُ مِن نِّعْمَةٍ تُجْزَى ﴿19﴾ إِلَّا ابْتِغَاء وَجْهِ رَبِّهِ الْأَعْلَى ﴿20﴾ وَلَسَوْفَ يَرْضَى ﴿21﴾


17. Na mcha Mungu ataepushwa nao

18. Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa

19. Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliyemfanyia hisani ndio anamlipa.

20. Ila ni kutaka wajihi wa Mola wake Mlezi aliye juu kabisa

21. Naye atakuja ridhika
[Al-Layl:17-21]

Wafasiri wengi wa Qur-aan wametaja kuwa Aayah hizo zinamhusu Abu Bakar As-Swiddiyq (Radhiya Allahu 'anhu). Hata baadhi yao wametaja kuwa kuna makubaliano baina ya wafasiri wa Qur-aan kuhusu Aayah hizo. Hakuna shaka kuwa ni yeye aliyekusudiwa katika Aayah hizo kwa vile yeye ni mwenye kustahiki katika Ummah huu kupewa sifa hizo pamoja na sifa nyingine nyingi njema. Hakika yeye ni mkweli, mcha Mungu, mkarimu mwenye kutoa daima mali yake kwa wanaohitajia na alimsaidia sana Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kutoa mali yake Fiy Sabili-Llah.

Muislam anapotoa sadaka kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), thawabu zake zitakuweko kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) bila ya shaka. Hatoulizwa ikiwa sadaka imemfikia mtu mwema au muovu (bila ya kukusudia) au mwenye kustahiki kupata sadaka au asiyestahiki kupokea sadaka. Atalipwa thawabu zake kutokana na Niya yake. Hadiyth ifuatayo inayopatikana katika Swahiyhayn (Al-Bukhaariy na Muslim) inatupa mafundisho hayo:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَة رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رَسُول اللَّه - صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ (( قَالَ رَجُل "لَأَتَصَدَّقَنَّ اللَّيْلَة بِصَدَقَةٍ" فَخَرَجَ بِصَدَقَتِهِ فَوَضَعَهَا فِي يَد زَانِيَةٍ فَأَصْبَحَ النَّاس يَتَحَدَّثُونَ "تُصُدِّقَ عَلَى زَانِيَة" فَقَالَ : "اللَّهُمَّ لَك الْحَمْد عَلَى زَانِيَة لَأَتَصَدَّقَنَّ اللَّيْلَة بِصَدَقَةٍ" فَوَضَعَهَا فِي يَد غَنِيّ فَأَصْبَحُوا يَتَحَدَّثُونَ "تُصُدِّقَ اللَّيْلَة عَلَى غَنِيّ" قَالَ : "اللَّهُمَّ لَك الْحَمْد عَلَى غَنِيّ لَأَتَصَدَّقَنَّ اللَّيْلَة بِصَدَقَةٍ" فَخَرَجَ فَوَضَعَهَا فِي يَد سَارِق فَأَصْبَحُوا يَتَحَدَّثُونَ "تُصُدِّقَ اللَّيْلَة عَلَى سَارِق" فَقَالَ : "اللَّهُمَّ لَك الْحَمْد عَلَى زَانِيَة وَعَلَى غَنِيّ وَعَلَى سَارِق" فَأُتِيَ فَقِيلَ لَهُ "أَمَّا صَدَقَتك فَقَدْ قُبِلَتْ وَأَمَّا الزَّانِيَة فَلَعَلَّهَا أَنْ تَسْتَعِفَّ بِهَا عَنْ زِنًا وَلَعَلَّ الْغَنِيّ يَعْتَبِر فَيُنْفِق مِمَّا أَعْطَاهُ اللَّه وَلَعَلَّ السَّارِق أَنْ يَسْتَعِفَّ بِهَا عَنْ سَرِقَته")). البخاري و مسلم

Imetoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Mtu mmoja alisema: "Leo nitatoa sadaka". Akatoka na sadaka yake na (bila ya kujua) akampa mzinifu. Asubuhi ya pili watu wakasema: "Sadaka imetolewa kwa mzinifu". Yule mtu akasema: "Yaa Allah! Sifa njema zote ni Zako (Nimetoa sadaka yangu) kwa mzinifu. Usiku wa leo nitatoa sadaka tena". Akatoka na sadaka yake na (bila ya kujua) akampa tajiri. Siku ya pili (watu) wakasema: "Usiku wa jana tajiri kapewa sadaka". Akasema: "Yaa Allah! Sifa njema zote ni Zako. (Nimetoka sadaka) kwa tajiri. Usiku wa leo nitatoa sadaka tena". Akatoka na sadaka yake na (bila ya kujua) akampa mwizi. Asubuhi ya pili (watu) wakasema: "Usiku wa jana mwizi alipewa sadaka". Akasema: "Yaa Allah! Sifa njema zote ni Zako (nimetoa sadaka) kwa mzinifu, tajiri na mwizi" Akaja mtu na kumwambia: "Sadaka uliyoitoa imekubaliwa. Kwani mzinifu, huenda sadaka ikamzuia kufanya uzinifu. Ama tajiri, huenda ikampa fundisho naye atoe (sadaka) mali yake aliyopewa na Allah. Ama mwizi, huenda ikamzuia kuiba")) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Aayah nyingi na Hadiyth zimetaja kuhusu fadhila za kutoa sadaka. Na Muislamu anapotoa sadaka Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Humlipa duniani marudufu na Akhera pia hupata ujira wake. Na jambo la kutia moyo katika kutoa sadaka ni kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ametuhakikishia kuwa tunapotoa basi ni kama mkopo tunaomkopesha Yeye:

((مَن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ وَلَهُ أَجْرٌ كَرِيمٌ))

((Ni nani atakayemkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema, ili Amrudishie maradufu, na apate malipo ya ukarimu)) [Al-Hadiyd:11]
Na Muislamu asidharau kutoa japo kitu kidogo kama kipande cha tende :

وعَن عَدِيِّ بنِ حاتم رضي اللَّه عنه أَن رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : (( اتَّقُوا النَّارَ وَلَوْ بِشِقِّ تَمَرةٍ )) متفقٌ عليه

Imetoka kwa 'Adiyyi bin Haatim (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Jikingeni na moto hata kwa kipande cha tende)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

VISA VYA WALIOKUWA WAKITOA SADAKA KUTOKA KATIKA BUSTANI ZAO

Tunatoa visa viwili vyenye mafunzo muhimu vinavyohusu watu waliokuwa na bustani zao zenye mazao na matunda wakawa wanatoa sadaka humo. Kisa kimoja kutoka katika Hadiyth na kimoja kutoka katika Qur-aan:

Kisa kutoka katika Hadiyth:

عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال ((بيْنَما رَجُلٌ يَمشِي بِفَلاةٍ مِن الأَرض ، فَسَمِعَ صَوتاً في سَحَابَةٍ : اسقِ حَدِيقَةَ فُلانٍ ، فَتَنَحَّى ذلكَ السَّحَابُ فَأَفْرَغَ مَاءَهُ في حَرَّةٍ ، فإِذا شرجة من تِلْكَ الشِّراجِ قَدِ اسْتَوعَبَتْ ذلِكَ الماءَ كُلَّهُ فَتَتَبَّعَ الماءَ ، فإِذا رَجُلٌ قَائِمٌ في حَدِيقَتِهِ يُحَوِّلُ المَاءَ بمِسحَاتِهِ ، فقال له : يا عَبْدَ اللَّهِ ما اسْمُكَ قال : فُلانٌ، للاسْمِ الَّذِي سَمِعَ في السَّحَابَةِ ، فقال له : يَا عَبْدَ اللَّهِ لِمَ تَسْأَلُنِي عَنِ اسْمِي ؟ فَقَال : إني سَمِعْتُ صَوتاً في السَّحَابِ الذي هذَا مَاؤُهُ يقُولُ : اسقِ حَدِيقَةَ فُلانٍ لإسمِكَ ، فما تَصْنَعُ فِيها ؟ فقال : أَما إِذْ قُلْتَ هَذَا ، فَإني أَنْظُرُ إِلى ما يَخْرُجُ مِنها ، فَأَتَّصَدَّقُ بثُلُثِه ، وآكُلُ أَنا وعِيالي ثُلُثاً ، وأَردُّ فِيها ثُلثَهُ)) . رواه مسلم

Imetoka kwa Abu Hurayra (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Wakati mtu mmoja alikuwa anatembea njiani katika ardhi ya ukame ambayo haina alama ya maji, alisikia sauti inatoka kutoka katika mawingu ikisema: "Mwagia maji bustani ya fulani". Mawingu yakaelekea upande fulani na kuanza kumwaga maji juu ya miamba tambarare. Mchiriziko ukatiririka katika mfereji mkubwa. Mtu huyo akaufuata mfereji huo hadi ukafika katika bustani na akamuona mwenye kumiliki bustani amesimama katikati yake akiyatandaza maji kwa sepeto (huku anabadilisha njia ya maji yaelekee katika sehemu nyingine ya bustani). Akamuuliza: "Ewe mja wa Allah! Jina lako nani?". Akamwambia jina lake ambalo ni lile lile alilolisikia kutoka katika mawingu. Mwenye bustani akamuuliza: "Ewe Mja wa Allah! Kwa nini umeniuliza jina langu?" Akamjibu: "Nimesikia sauti kutoka katika mawingu yaliyomwaga maji ikisema: "Mwagia maji bustani ya fulani". Nataka kujua huwa unaifanyia jambo gani?". Akasema: "Kwa vile umeniuliza nitakuambia: Hupima mapato ya bustani na kugawa thuluthi moja katika sadaka, na thuluthi moja natumia mwenyewe na familia yangu, na thuluthi moja nairudisha katika (kuizalisha) bustani")) [Muslim]

Kisa kutoka katika Qur-aan:

Alikuweko mtu mmoja ambaye alikuwa ana bustani ambayo ikitoa mazao na matunda mbali mbali, na kila anapochuma mazao alikuwa akigawa sehemu tatu; sehemu moja akiirudisha katika kuzalisha tena mazao, sehemu ya pili akila yeye pamoja na watoto wake, na inayozidi alikuwa akitoa sadaka. Alipofariki na watoto wake waliporithi hiyo bustani, hawakutaka kufanya kama alivyokuwa akifanya baba yao. Walisema: "Hakika baba yetu alikuwa mpumbavu kutoa mazao ya bustani kuwapa masikini. Tukizuia sisi tusiwape, basi tutakuwa na mazao mengi yetu wenyewe". Usiku mmoja wakapanga mpango na wakaapa kuwa wakiamka asubuhi yake watakwenda kuchuma mazao yote ili masikini watakapokuja kuomba hawatotambua wamefanya hivyo. Na wala hawakusema "Allah Akipenda". Lakini Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Alitaka kuvunja kiapo chao na Akawapa mtihani kwa kuwaangamizia bustani yao usiku huo. Akaifanya bustani ikauke kabisa na ipige weusi kama vile imeungua au kama mfano iliyokwishavunwa kisha ikawa kavu kabisa.

Walipoamka asubuhi, wakaitana ili waende katika bustani kuchuma kama walivyopanga na kuapa. Wakaondoka huku wakinongo'nezana ili mtu yeyote asiwasikie. Wakaenda lakini walipofika walidhani kuwa wamepotea maana hawakuitambua bustani yao kabisa. Hapo tena ndio wakatambua kuwa hakika ni hiyo hiyo bustani yao ila tu imeangamia na wamekosa kila kitu. Wakaanza kulaumiana wenyewe kwa wenyewe na majuto yakawa makubwa! Kisha tena wakakiri makosa yao na kujirudi nafsi zao wakaomba kwa Mola wao Awaghufurie na mwishowe wakawa watu wema.
Baadhi ya Salaf wamesema kuwa watu hao walikuwa ni watu kutoka Yemen. Sa'iyd bin Jubayr amesema kuwa: "Ni watu kutoka katika kijiji kilichoitwa Darawaan ambacho kilikuwa ni maili sita kutoka San'aa". Imesemekena vile vile kuwa ni miongoni mwa Ahlul-Kitaab kutoka Ethiopia. Na Allah Anajua zaidi [Tafsiyr ya Ibn Kathiyr]

Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ameelezea kisha hichi katika Suratul-Qalam kama ifuatavyo.

إِنَّا بَلَوْنَاهُمْ كَمَا بَلَوْنَا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ إِذْ أَقْسَمُوا لَيَصْرِمُنَّهَا مُصْبِحِينَ ﴿17﴾ وَلَا يَسْتَثْنُونَ ﴿18﴾ فَطَافَ عَلَيْهَا طَائِفٌ مِّن رَّبِّكَ وَهُمْ نَائِمُونَ ﴿19﴾ فَأَصْبَحَتْ كَالصَّرِيمِ ﴿20﴾ فَتَنَادَوا مُصْبِحِينَ ﴿21﴾ أَنِ اغْدُوا عَلَى حَرْثِكُمْ إِن كُنتُمْ صَارِمِينَ ﴿22﴾ فَانطَلَقُوا وَهُمْ يَتَخَافَتُونَ ﴿23﴾ أَن لَّا يَدْخُلَنَّهَا الْيَوْمَ عَلَيْكُم مِّسْكِينٌ ﴿24﴾ وَغَدَوْا عَلَى حَرْدٍ قَادِرِينَ ﴿25﴾ فَلَمَّا رَأَوْهَا قَالُوا إِنَّا لَضَالُّونَ ﴿26﴾ بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ ﴿27﴾ قَالَ أَوْسَطُهُمْ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ لَوْلَا تُسَبِّحُونَ ﴿28﴾ قَالُوا سُبْحَانَ رَبِّنَا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ ﴿29﴾ فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَى بَعْضٍ يَتَلَاوَمُونَ ﴿30﴾ قَالُوا يَا وَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا طَاغِينَ ﴿31﴾ عَسَى رَبُّنَا أَن يُبْدِلَنَا خَيْرًا مِّنْهَا إِنَّا إِلَى رَبِّنَا رَاغِبُونَ ﴿32﴾ كَذَلِكَ الْعَذَابُ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿33
17. Hakika Tutawatia mtihani (Makureshi) kama Tulivyowatia mtihani wenye shamba, walipoapa kwamba watayavuna (mazao yake) itakapokuwa asubhuhi (ili wasionekane na maskini wakaombwa).

18. Wala hawakugawa katika kiapo chao. (Wafasiri wengine wamesema: Kwa kusema Insha-Allah, na wengine wamesema kuwa waliapa kutosaidia maskini yeyote)

19. Basi ulilifikia (shamba hilo) msiba mkubwa utokao kwa Mola wako, na hali wao walikuwa wamelala.

20. Ikawa kama lililoungua.

21. Asubuhi wakaitana.

22. Ya Kwamba: "Nendeni mapema kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna (bila kuonekana na maskini)".

23. Basi walikwenda na huku wakinong'onezana.

24. Ya kuwa: "Leo maskini asiingie humo mwenu"

25. Na wakaenda asubuhi hali wanadhani kuwa wanao uwezo wa kuzuia (masikini).

26. Basi walipoliona, (limeungua vile walidhani kuwa silo) wakasema: "Bila shaka tumepotea!" (Siko huku; silo shamba letu hili, tumepotea)".

27. (Walipotazama zaidi wakayakinisha kuwa ndilo walisema) "Bali tumenyimwa!" (mavuno yake)

28. M-bora wao akasema: "Je, sikukuambieni (msitie niya mbaya ya kuwazuilia haki yao maskini? Sasa) rejeeni kwa Mola wenu mtubie Kwake".

29. Wakasema: "Utukufu ni wa Mola wetu! Hakika tulikuwa madhalimu. (Basi tusamehe Mola wetu)

30. Basi wakakabiliana kulaumiana.

31. Wakasema: "Hasara yetu! Hakika tulikuwa tumeruka mipaka (Ya Allah)"

32. 'Asaa Mola wetu Atatubadilishia (shamba) lililo bora kuliko hili, hakika sisi tunajipendekeza (sasa) kwa Mola wetu".

33. Namna hivi inakuwa adhabu (ya Mola Wako duniani). Na adhabu ya Akhera ni kubwa zaidi, laiti wangalijua!

[Al-Qalam: 17-33]

Tunatumai visa hivyo vitakuwa ni mafunzo kwetu ambayo yatatukinaisha na kutuzidishia iymaan zetu tupende kutoa sadaka kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kuwapa masikini, wenye kuhitaji, mayatima, ndugu zetu, Fiy Sabiyli-Llah, tukitarajia Radhi za Mola Mtukufu na tukitaraji Atulipe kheri za dunia na Akhera.


 Posted By Posted juu ya Monday, December 03 @ 22:53:47 PST na MediaSwahiliTeam
 

Comments 💬 التعليقات
 

For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا

Kuhusiana Viungo

· zaidi Maamuzi Ya Kufunga Ramadhan Na Kuabudu
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu Maamuzi Ya Kufunga Ramadhan Na Kuabudu:
Sha'abaan: Fadhila Zake Na Uzushi Wa Nisfu Sha'abaan - Nasiha Za Minas


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora
Vizuri Sana
Mema
Kawaidar
Mbaya


Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa RafikiMada zinazohusiana

Maamuzi Ya Kufunga Ramadhan Na Kuabudu

 

EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And IslamAfrica.Com