Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   
 
Hajj: Hatua Kwa Hatua: Tazama Televisheni Ya Saudi Arabia kujua wanayofanya Mahu
 
Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis
1 – 7 Dhul-Hijjah – Makkah au Madiynah

Kuzuru Msikiti wa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  au kuweko Makkah kufanya 'Umrah (kwa Wanaofanya Hajjut-tamattu'u) na kuendelea kuswali hapo Masjidul-Haraam.Madiynah
Kuswali Masjidun-Nabawy na wanaume kuzuru    kaburi la Mtume صلى الله عليه وآله وسلم.

Makkah

Kufanya Twawwaaf  Kuzunguka Ka'abah mara 7
Kuswali Raka'ah mbili Maqaam Ibraahiym

Sa'yi  -  Swafaa  Na Marwah
Kuanza Kilima cha Swafaa kwenda kilima cha Marwah mara saba.

Wakimaliza 'Umrah watabakia Makkah na kuswali katika Masjidul-Haraam kupata fadhila zake

8 Dhul-Hijjah – Mina

Asubuhi Wanaondoka Makkah kuelekea Mina.

9  Dhul-Hijjah – Siku ya 'Arafah

Wanaondoka kutoka Mina asubuhi kuelekea 'Arafah na kubaki hadi jua litakapozama. 

Ni siku ya kutekeleza fardhi kubwa miongoni mwa taratibu za Hajj. Siku ya kuomba Du'aa sana. Na ndiyo siku iliyokamilika dini yetu tukufu aliposimama Mtume صلى الله عليه وآله وسلم katika mlima wa 'Arafah na kutoa khutbah yake ya mwisho. Na ni siku ambayo wengi wetu wataachiwa huru na moto.

Hapa wataswali Swalah ya Adhuhuri na Alasiri 'jam'an wa Qaswran' (kujumuisha na kufupisha Rakaah mbili mbili). Watasikiliza khutbah (watakaojaaliwa kuweko karibu na Masjidun-Namirah).  Wasiokuwepo huko siku hiyo watafunga Swawm ya 'Arafah ambayo Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kasema inafuta madhambi ya mwaka uliopita na ujao.

Jua likizama, wataelekea Muzdalifah.

10  Dhul-Hijjah – Muzdalifah – Mina - Makkah

Watafika Muzdalifah usiku na wataswali Magharibi na 'Ishaa  'jam'an wa Qaswran' (kujumuisha na kufupisha Rakaah mbili mbili)

Watabakia Muzdalifah usiku mzima kwa kumkumbuka Allaah سبحانه وتعالى sana na kuokota vijiwe vya kurusha katika Jamaraat.

Asubuhi – Yawmun-Nahr (siku ya kuchinja) kwa Mahujaji, na kwa wasiokuwepo huko ni siku ya 'Iyd. Wataelekea kutekeleza vitendo vifuatavyo vya fardhi za Hajj:

1) Kurusha vijiwe katika Jamaraat

2) Kutufu Twaaful-Ifaadhwah

3) Kunyoa nywele  

4) Kuchinja

(vyovyote watakavyotanguliza  katika vitendo hivi inajuzu)

Kurusha mawe katika Jamaraat 

11 – 12 Dhul-Hijjah – Ayyaamut-Tashriyq

(Siku ya kwanza na ya pili ya Tashriyq)

Watarudi Mina na kwa ajili ya kurusha mawe katika Jamaraat.

Ni siku za kula na kunywa na kumkumbuka sana Allaah سبحانه وتعالى  

13 Dhul-Hijjah  (Siku ya mwisho ya Tashriyq)

Wanaopenda kubakia Mina watabakia kisha watarudi Makkah na ikiwa safari imewadia watafanya Twawwaaful-Wida'a (Twawwaaf ya kuaga)

AL HIDAAYA inawaombea ndugu zetu Waislamu wote ulimwenguni waliokwenda kutekeleza nguzo hiyo ya tano ya Dini, Hajju-m-Mabruur, Wa Dhambu-m-Maghfuur na warudi salama kwa watu wao.

Na inawaombea wasiojaaliwa kutekeleza nguzo hii Allaah سبحانه وتعالى Awajaalie mwakani wawe miongoni mwa Mahujaji InshaAllaah. Aamiyn.


 Posted By Posted juu ya Tuesday, October 05 @ 21:24:16 PDT na MediaSwahiliTeam
 

Comments 💬 التعليقات
 

For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا

Kuhusiana Viungo

· zaidi Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis
· Habari na MediaSwahiliTeam


Kweli kusoma hadithi kuhusu Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis:
Jinsi Ya Kumfurahisha Mkeo


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora
Vizuri Sana
Mema
Kawaidar
Mbaya


Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa RafikiMada zinazohusiana

Ulimwengu wa Kiislamu na masuala ya Kiis

 

EsinIslam The Muslim World Portal For Islamics, News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Quranic Islamic Articles, Radio, Audio Quran, TV Channels, Fatwa Rulings, Muslim News Newspapers Magazines Headlines Articles Forums Schools, Universities, Colleges, Mosques, Qur'an, Hadith, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Fasting Ramadan, Vidoes, Books On EsinIslam.Com And IslamAfrica.Com