Saa hii, kuna hatua ya baraza na wewe mwenyewe 2 Mgeni (wageni) na 3 mwanachama (s) ambayo juu ya Hatua.
Mwanachama (wanachama) pamoja na wanachama wa Awqaf. kuona ni nyingine mbunge (s) online na wewe click Kubonyeza Hapa
Tafuta
Lugha
Mabadiliko ya lugha mbalimbali::
Categories Menu
Hakuna bidhaa sasa hivi kwa ajili ya kuzuia hili.
Sanduku Kuingia
Hawana akaunti bado? Unaweza kujenga mmoja. Kama Mtumiaji aliyesajiliwa unaweza kuwa na baadhi ya faida kama meneja wa mandhari, comments Configuration na maoni post kwa jina yako.
Kwanza kabisa, ijulikane wazi kwamba kusudio la makala hii si kutoa fatwa wala hukumu. Lengo ni kuweka wazi manufaa na madhara ya Facebook ili mtu binafsi atoe hukumu yake mwenyewe. Je, ni Facebook au Fitnabook? Hili ni suali ambalo watu wengi wameanza kujiuliza baada ya kujionea vitimbi na kashfa kadhaa katika huu mtandao ambao unazidi kujipatia umaarufu kila pembe ya dunia. Naam, kuna vitimbi kadhaa vinafanyika kwa jina la Facebook. Na ndio kuna vijana wengi ambao wametumbikia katika janga la fitna katika Facebook lakini nini suluhisho la hili? Kabla hatujatazama hebu kwanza tuangalie manufaa na madhara ya Facebook.
Manufaa Kama ilivyo kawaida ya vitu vingi, Facebook ina faida yake. Lakini je, hizo faida ni nyingi kuliko madhara? Katika sehemu hii tutaja manufaa ambayo yako wazi kutokana na utumiaji wa Facebook. Manufaa hayo ni kama yafuatayo: 1. Kufanya da’wah ( kuwalingania watu kwenye Uislam) Madaa’iyah kadhaa pamoja na baadhi ya Mashaykh hutumia Facebook kwa kazi za da’wah. Huwekwa na kutumwa vitu mbalimbali vya kufikisha mafunzo mbalimbali ya Dini kama: video za mawaidha, makala za Kislamu na njia mbalimbali za kunufaisha wasomaji.
2. Kuwasiliana na jamaa na marafiki wa mbali Mara nyingi watu hutumia Facebook kwa kuwasiliana na jamaa zao ambao wanaishi nje ya nchi kwa hoja ya kwamba ni njia rahisi na ya nyepesi ukilinganisha na njia nyinginezo.
3. Kutangaza shughuli na harakati za Kiislam Ijtimai na mikusanyiko mingi ya Kiislamu na mambo yanayowahusu Waislamu mara nyingi huwa yanatangaziwa kwa kutumia Facebook. Njia hii pia inaruhusu waandaaji kujua watu wangapi watahudhuria au kupatikana katika shughuli au harakati zao.
Madhara Ijapokuwa kuna manufaa kadhaa juu ya utumiaji wa Facebook, kuna balaa na fitnah nyingi hupatikana humo, kadhalika watu wengi wanaitumia kwa njia mbaya. Katika madhara ya Facebook ni haya:
1. Kupoteza muda kwa mambo ya upuuzi Watu wengi hasa vijana hupoteza masaa juu ya Facebook wakati wangeliutumia muda ule kwa kufanya kitu cha muhimu.
2. Mchanganyiko wa wanaume na wanawake Ada kuu iliyoshamiri na kuenea kati ya watumiaji ya Facebook ni kutazama na kuongea na watu wasio Mahram zao.
3. Kutokewepo kwa hayaa na heshima Uislamu umekuja kulinda heshima ya binaadam lakini cha ajabu vijana wengi wa Kiislamu hutokwa na hayaa na huvuruga heshima zao kupitia Facebook. Wasichana wangapi wameweka picha zao bila ya hijaab kwenye Facebook kwa kutaka kujionyesha? Wanawake wangapi wameharibu heshima zao na za familia zao kwa kutuma maasi yao kwenye Facebook?
4. Kukashifiwa Mtume na Uislam Kubwa zaidi na baya zaidi na la hatari zaidi, ni hili lililotokea majuzi la kukashiwa kwa Mtume kwenye Facebook, jambo ambalo limewasikitisha wengi wetu na tuna kila haki ya kuhuzunika juu ya hilo. Picha mbalimbali za kashfa na za kumlinganisha Mtume wetu mtukufu Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mambo maovu na machafu, zimewekwa huko kwa kuchorwa vikatuni vinavyodaiwa kuwa ni yeye. Na yamejitokeza makundi tofauti yaliyoungana huko kwenye Facebook ili kuukashifu Uislamu na Waislamu na kumdhalilisha Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Haya yote ni matunda ya hiyo Facebook.
Suluhisho Baada ya kujionea na kutafakari juu ya madhara na manufaa yaliyomo kwenye Facebook, lilobakia ni kujiamulia mwenyewe. Ikiwa utaona kwamba Facebook madhara yake ni makubwa kuliko faida, basi ni juu yako kujihadhari juu ya kuitumia na bora zaidi kujiepusha nayo. Ikiwa utaona kwamba manufaa yamezidi basi ni pia juu yako kujichunga na madhara yaliyomo huko. Inawezekana kitu ukakiona kina manufaa kadhaa lakini madhara yake ni mengi zaidi. Allaah Anasema kuhusu ulevi na kamari يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ قُلْ فِيهِمَا إِثْمٌ كَبِيرٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَإِثْمُهُمَآ أَكْبَرُ مِن نَّفْعِهِمَا “Wanakuuliza kuhusu ulevi na kamari, sema ndani yake yamo madhara mengi na manufaa kwa watu, lakini madhara ni makubwa kuliko manufaa.” [Al-Baqarah 2: 219] Isitoshe, pahala ambapo anatukanwa Allaah au Mtume Wake, au Qur-aan au Sunnah au jambo lolote la Dini, basi sehemu hiyo inapaswa kuhamwa au kutengwa hadi itakapojirudi au kuomba radhi na kubadili mwelekeo wako. Na ikiwa Facebook imeomba radhi kwa matendo yake ya kumtusi na kumdhalilisha Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), hapo tena Muislamu ana khiyari ya kutumia ukumbi huo kwa manufaa yaliyotajwa au kuuacha na kuutenga kwa madhara yaliyoelezwa. Na bia shaka madhara na uadui waliouonyesha kwa Uislamu na Waislamu, unamtosha Muislamu kuwa mbali na ukumbi kama huo au mwengine wowote unaofanana na huo. Kadhalika hivi sasa Waislamu wamefungua kumbi kama hizo za kuweka mambo yanayowahusu Waislamu na yasiyokuwa na fitnah ndani yake wala utata. Kwahiyo, tujihadhari, hasa katika mambo ambayo yana utata ili tuweze kulinda Dini yetu na heshima yetu.
Posted By
Posted juu ya Monday, December 03 @ 23:09:49 PST na MediaSwahiliTeam