Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - HAJA YETU YA MWANAMKE MUISLAMU M
 
Makala hii inakuja kutoka
EsinIslam Media Swahili :: http://esinislam.com/MediaSwahili
 
The URL kwa ajili ya hadithi hii ni:
http://esinislam.com/MediaSwahili/modules.php?name=News&file=article&sid=78

 
Mfumo Na Muelekeo Wa Nyaraka Hizi Umechukuliwa Kutoka Kwa Kijitabu Kinachoitwa 

“Al-Mar’at Al-Muslimah Fiy Twalabil ‘Ilm”  

Elimu Ni Wajibu Kwa Mwanamke Wa Kiislamu - HAJA YETU YA MWANAMKE MUISLAMU MWENYE MUAMKO 

Mwanamke Muislamu Katika Kutafuta Elimu)

Kilichochapishwa Na Daarul Arqam,  Chapa Ya Pili, 

HAJA YETU YA MWANAMKE MUISLAMU MWENYE MUAMKO 

Bila ya shaka, Ummah wa Kiislamu unahitaji wanawake wasomi wenye kufanya kazi ambao watasimama katikakujenga watoto watakaoshiriki katika muelekeo uliobarikiwa na muamko na kuelewa majukumu yao. Hamu yao ni kuzitakasa nafsi zao na za waume wao, watoto wao na kila kitakachorudisha katika Ummah wa Kiislamu nguvu na utukufu. 

Jambo hili ni wajibu liwe katika akili yake anapolala na kuamka na wala asiwe ni mwenye kushughulishwa na mambo mengi ya Maisha ambayo yamewasahaulisha kuhusu ndugu zao Waislamu na dini yao. Ni vizuri sana muamko wao uzinduliwe katika kutekeleza na kuwasaidia Waislamu wenziwao na Uislamu kwa nia mzuri, ikhlasi na kutaka ridhaa ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala).

DHARURA YA MUAMKO:

Kwa hivyo, hapana budi kumpatia ujuzi Muislamu mwanamke ambaye anaipendelea mazuri jamii kwa kuyabeba majukumu pamoja na mwanamume. Muamko unamfungulia msichana njia ya utekelezaji mwingi ambao atafahamu katika hicho kipindi ukweli wa Maisha bila kuyakuza au kuyafanya madogo. Muamko unafungua mlango wa mbele kwa msichana kuweza kuwa na uoni wa mbali na kuona njia za matendo, kazi na changa moto. Kwa njia hii atakuwa na uwezo zaidi wa kuwa na msimamo wa imara katika nyanja ya mapambano.
Muamko, kabla ya yote hayo inamjaalia msichana awe na ufahamu wa Imani na ukweli wa Uislamu. Hivyo anayafunga matendo yake kwa kutafuta radhi za Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala). Maadili yake yanaimarika kwa uwongofu wa sheria na mapendeleo yake yanakuwa na hofu ili asije akaipenda fitna na ufisadi. Muamko ni kipimo muhimu ambacho mwanamke na mwanamume wako sawa. Lakini sisi tutafuata njia itakayo saidia hilo.

Kipimi kinakua kwa kuongezeka Imani na kujikita ndani ya nafsi ya mwanamke na mwanamume. Itazidi kuongezeka kwa kuamsha hisia ambazo ni za kufuatilia maamrisho ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) na atabaki kuangalia Siku yahesabu na kudumu ku*****iria Akhera. Hivyo hivyo, hiyo inapanuka kwa kupanuka maarifa na majaribio. Maarifa ya uhakika ya jamii ambayo imetuzunguka na ufahamu wa majaribio ambayo yameelezwa na wanavyuoni na wale walio wakweli kabla yetu na pia mitihani yaliyotukia.

Pindi atakapoweza mwanamke kutizama mambo kwa macho ya ukamilifu na kwa njia inayowafikiana na uoni wa Kiislamu wa Maisha, atazidi kuwa na muamko kwa Maisha haya na ufahamu wa mambo. Na atakapoweza kujua majukumu yake ya hakika katika kujenga jamii ya Kiislamu na kuyapanga mambo yanayotakiwa kupawa kipao mbele na yaliyo muhimu katika Maisha yake, bila shaka muamko utavama ndani na uoni wake utafunguka.

Muamko unapatikana kwa kuwa mbali na ujinga, ufahamu mdogo, uoni wa sehemu na kujikalifisha kwa mambo ya nje.

NJIA YA KUPATA MUAMKO:

Maadamu muamko umekusanya yote hayo, hatokuwa tayari mwanamke Muislamu kwa uharaka unaohitajika na hakuna budi kwa malezi ya pole pole na kuazima mfumo wa masomo ya yaliyopita na ya sasa ili juhudi hizi kuzaa matunda na kutoa natija mzuri kwa kufungua masikio na kuuwekea umuhimu.

Hapana budi kabla ya hayo kurudisha mazingatio katika urithi wetu wa zamani wa Uislamu na ufahamu wetu ambao tumeupata kutoka hapa na pale. Kurudi katika Kitabu cha Allaah, Aliyetukuka (yaani Qur’ani) mwanzo kabisa kwa kuisoma kikweli na kwa ikhlasi. Hivyo kuhakikisha kuwa mmoja amepata darasa ya kina na ufahamu wa uoni na mazingatio, inafungua njia kubwa kwa kuweka wazi muamko katika nafsi. Pindi nafsi itakapokuwa wazi kwa kupata maana ya Qur’ani Tukufu ina fanana na ardhi yenye rutuba inayongoja kupandwa mbegu na miche ili yatoe miti yaliyo imara na matunda yaliyo mazuri kabisa. 

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa ni Qur’ani inayotembea katika ardhi na aliwatayarisha Masahaba - wanaume kwa wanawake wawe katika hali hiyo. Maamrisho yote yaliyomo ndani ya Qur-aan yalikuwa yanatekelezwa barabara bila herufi moja kuanguka.

ATHARI YA MUAMKO KATIKA SHAKHSITA YA MWANAMKE:

Muamko utakapopatikana kwa mwanamke Muislamu ataweza kuutoa na kuzalisha matokeo mazuri.

· Wakati huo atafahamu Uislamu wake kwa njia iliyo wazi na kamili, bila kuichukua kuwa ni sehemu ndogo wala kuchukua Pembe moja na kuacha nyengine.
· Atafahamu Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), atafanya juhudi kupata maarifa hayo na kuyafanyia kazi katika aina zote za adabu na rangi tofauti za maisha.
· Atafahamu kuwa na istiqaamah (kuwa na msimamo) katika dini na hasa katika zama hizi za sasa. Japokuwa hali zimekuwa ngumu lakini ataishi kwa kumtegemea na kumuamini Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala). Hivyo anapata utulivu kwa kuridhiwa Naye (Subhaanahu Wa Ta’ala) hata balaa na shida ikizidi namna gani.
· Anaweza kuondoa shaka na kuitoa katika nafsi yake. Pia anamaliza unyonge na kuogopa na anajua kuwa atafuzu mbele ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) maadamu anashikilia hii dini. Kwa hivyo hatamuogopa yeyote isipokuwa Allaah pekee.
· Atahakikisha na kupata katika nafsi yake aina ya ulinzi wa kibinafsi katika uso na umbele wa mashambulizi. Utamaduni wa kisasa ambao umenyanyua bendera ya kijinsi na kuchukua njia ya kueneza ufisadi wa kizazi na kupiga vita maadili na kutoa hukumu juu ya ‘aqeedah.
· Muamko huu unamlinda na kumfanya afuate Maisha ya Kiislamu yaliyotakasika. Hivyo atajitokeza mbele ya wasichana wa jinsi yake kwa sura iliyo ya juu na mzuri, hapigi vita maumbile ya kibinadamu alioumbiwa nayo na Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) wala haumii na dhiki za moyo ambazo zimeanzishwa na utamaduni wa mijini.
· Naye anafanya kazi ya jamii kwa njia yenye kuleta natija mzuri, anaita kwa maadili na matendo yake na kuwa yeye ni kiigizo na mfano mzuri wa wakati huo. Ataweza kulingania kwa njia mzuri kila mtu na kwa usawa na kuweka wazi ukweli wa Maisha kama laivyosoma katika Qur’ani na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
· Naye atatoka katika duara ya taqleed (kufuata kama kipofu) mbovu ambayo imezuliwa na mashetani wa sasa kwa kupotosha katika jina la kukaa uchi na kubadilisha mambo kwa kufuata mambo ya kisasa yanayokwenda kinyume na Dini. Yeye anamiliki uhuru wake wa uhakika kuweza kuishi kama mwanamke anayetukuzwa mbali na macho ya kumdhalilisha na kumtweza na misimamo ya kumkandamiza.
· Hivyo hivyo ameleta athari njema katika jamii kwa njia ya adabu na fikra na kutekeleza amali na mawaidha mazuri na yaliyo wazi.

Miongoni mwa muamko wa mwanamke Muislamu ni kuyachukulia umuhimu yanayotendeka katika Maisha ya Ummah na yanayo wafikia Waislamu katika mambo maovu ambayo anatakikana ayakataze. Pia katika mambo ya upotevu na kutoka katika mipaka ya Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: 

“Mfano wa Waumini katika kupendana kwao na kurehemeana kwao na kuoneana huruma kwao ni kama mfano wa mwili. Pindi kinaposhtakia kiungo ndani yake, mwili wote unakosa usingizi na kuwa na homa”. Dkt. Abdul-Kareem Zaydan amesema yafuatayo alipokuwa akiielezea Hadithi hiyo juu katika kitabu chake, “Ama kuchukulia umuhimu wa mambo ya Waislamu kwa ujumla ni katika haki yake (mwanamke) bali ni wajibu wake. 

Miongoni mwa mambo ya Waislamu ni haja zao kwa ujumla ambazo wanazirekebisha au kulalamika. Katika umuhimu wa nje ni kufikiria haja zao na kueneza ufahamu wa Uislamu ambao utamleta mwanamke karibu na mumewe, watoto wake, jamaa na majirani. Yeye ana haki ya kutoa rai yake katika mambo ya kawaida na ya jumla na kutoa nasiha kwa njia anayoweza na kufuatana na maumbile yake kama kuandika vitabu, kuandaa mikutano ya wanawake na kuwafundisha na kueneza maadili na adabu tukufu ndani yao na kuwahimiza katika kutekeleza wajibu wao na mfano wa hayo na kuwaepusha maovu na uchafu”.

Na katika jambo hili amesema al-Bahi al-Khouli, “Hivyo ni kuwa mwanamke Muislamu wa mwanzo hakudang’anya nyanja kwa upofu au kupoteza au kujiachilia bali alijifunika kwa matayarisho na mipango ya wazi. Jamii ilikuwa inamuita kwake ili achukue sehemu yake katika safu iliyo imara, kusaidiana juu ya kipimo na maslahi na muelekeo wate wenye kupimika na wa kiroho. 

Hakutoa mkono wake wala hakuwa peke yake … Na kwa mipango hii na maandalizi hakutoweka kwa fikra zake na kuwepo kwake katika kuona umuhimu kwa mambo ya jamii. Huenda akawa mwanamke wa pekee katika historia ya dunia ambaye kwamba umuhimu alioweka katika mambo kwa jumla hayapungui wala hayazidi ukilinganisha na umuhimu wa mambo yake hasa”.

Hakuna ajabu kwa hayo kwani sheria ya Kiislamu imempatia wizani na uhuru katika nyanja zote za maisha hata akawa anashiriki mashauri ya jamii na kutoa nasaha zake. Haya yalionekana katika kisa cha shura baada ya kuuliwa kwa ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) na kushiriki wanawake. Amesema Ibn Katheer katika Al-Bidayah wan-Nihayah, “Kisha akaanza ‘Abdur-Rahman bin ‘Auf (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuchukua rai za watu kuhusu wao (yaani ‘Athman bin ‘Affan na ‘Ali bin Abi Talib). 

Akajumlisha rai za Waislamu kwa rai za viongozi wa watu kwa pamoja na mmoja mmoja, wawili wawili na walio peke yao, aliojumuika kwa siri na Dhahiri mpaka akamalizia kwa wanawake waliokuwa wamekaa nyumbani”. 

Mwanamke katika sheria amepatiwa uwezo wa kumiliki na kutumia mali na kufanya biashara. Qaylah bint Umm Bani Atmar amesema, “Mimi ni mawanamke ninaye uza na kununua”.

Kwa haya tunamalizia kuwa mwanamke Muislamu mwenye muamko na uoni na mwenye kushindana na kuwa na juhudi anahitajika. Jamii leo ina haja kubwa sana ya wao kwani kujenga jamii ya Kiislamu inahitaji wenye silaha ya imani na muamko na kujua malengo na kuyaendea kwa kujiamini na uoni.



 

Mada: Waislamu Wanawake - maisha yao na Famili


Comments 💬 التعليقات