Saa hii, kuna hatua ya baraza na wewe mwenyewe 2 Mgeni (wageni) na 3 mwanachama (s) ambayo juu ya Hatua.
Mwanachama (wanachama) pamoja na wanachama wa Awqaf. kuona ni nyingine mbunge (s) online na wewe click Kubonyeza Hapa
Tafuta
Lugha
Mabadiliko ya lugha mbalimbali::
Categories Menu
Hakuna bidhaa sasa hivi kwa ajili ya kuzuia hili.
Sanduku Kuingia
Hawana akaunti bado? Unaweza kujenga mmoja. Kama Mtumiaji aliyesajiliwa unaweza kuwa na baadhi ya faida kama meneja wa mandhari, comments Configuration na maoni post kwa jina yako.
Imefasiriwa na Ummu 'Abdil-Wahhaab
Vidokezo Muhimu Kwa Wazazi Wenye Wasichana Na Wavulana
((ALHIDAAYA imerekebisha baadhi ya majina na usemi ili makala ifahamike vizuri
na Jamii yetu))
NINI WAZAZI WAFANYE ILI VIJANA WAO WAWE NI WAISLAMU WENYE KUTEKELEZA UISLAMU KWA
VITENDO?
1. Yatilie Bidii Malezi Kuliko Hata Kazi Yako Ya Kutwa NzimaHii ina maana kwamba wazazi wote wawili ni lazima waelewe kuwa watoto wao ni wa kweli kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), na baba atakuja kuulizwa vipi kawalea watoto wake. Ikiwa watoto wao hawatokulia katika kuutekeleza Uislamu kwa sababu ya mapuuza ya wazazi wao, halitokuwa ni jambo la kukubalika kwa maisha ya hapa duniani na hata ya baadae.
2. Punguza Au Badilisha Masaa Ya Kazi Kwa Ajili Ya Kupata Muda Wa Kuwa Pamoja Na Familia YakoNi bora kuwa na kazi moja yenye muda wa kudumu, anasa chache katika nyumba (yaani sio magari mengi, nguo za gharama nyingi, nyumba kubwa ya fakhari, televisheni kila pahali), na muda zaidi wa kuwa pamoja na familia, kuliko kuwa na mambo mengi ya anasa na kukakosekana malezi. Haya yote yanawahusu mababa na mamama. Wazazi hawawezi kuwafunza watoto wao bila ya wao kuwepo nao kikawaida. Acha kazi za ziada kwenye siku za mwisho wa wiki au kazi za jioni na badala yake nenda na watoto msikitini kwa ajili ya Halaqah (darsa za dini) na shughuli nyenginezo. Au tilia maanani kugeuza nyakati za kazi ili uwe nyumbani wakati ambao watoto wapo.
Amri kuu aliyopatiwa mwanamke wa Kiislamu inayomtofautisha na ndugu yake wa kiume ni ile inayosema: "Ee Mtume! Waambie wake zako, na binti zako, na wanawake wa Kiislamu wajiteremshie uzuri nguo zao. Kufanya hivyo kutapelekea upesi wajulikane wasiudhiwe." (Suratul-Ahzaab: 59)
Vipi kuvaa nguo leo hii imekuwa viroja kwa Waislam? Kwani wamesahau mavazi yao, leo imekuwa watafuta kila mavazi kisha tunasema yetu, kisa tumejisahau lipi lililotulazimu kwetu na lililo muhimu kwetu na kwa Mola wetu?
Namshukuru Allaah ambaye Ameniwezesha kuandaa makala hii muhimu ambayo itagusia sana umuhimu wa Muislamu kuchunga muda wake na kutokuuangamiza kwa kufanya mambo ya kipuuzi ambayo hayatomsaidia si duniani wala Akhera. Waislamu wengi tunashinda siku kutwa na kujishughulisha na mambo ya kipuuzi ambayo mengi katika hayo hayamridhishi Allaah.
Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Kumi (Ya Mwisho) Wanaume Na Wanawake Wanaomdhukuru sana Allaah
Anasema Allaah سبحانه وتعالى: إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِينَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِينَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ وَالصَّائِمِينَ وَالصَّائِمَاتِ وَالْحَافِظِينَ فُرُوجَهُمْ وَالْحَافِظَاتِ وَالذَّاكِرِينَ اللَّهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا ﴿35﴾ ((Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na watiifu wanaume na watiifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wasemao kweli wanawake, na wanaosubiri wanaume na wanaosubiri wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanyenyekevu wanawake, na watoao sadaka wanaume na watoao sadaka wanawake, na wanaofunga wanaume na wanaofunga wanawake, na wanaojihifadhi tupu zao wanaume na wanawake na wanaomdhukuru Allah kwa wingi wanaume na wanawake, Allah Amewaandalia msamaha na ujira mkubwa)) [Al-Ahzaab:35]
Mtume (Swalla Llaahu ‘Alayhi Wa Sallam) Akiwa Madiynah
Anasema Shaykh Abu Bakr Al-Jazairiy:
"Hakika ya miaka yote kumi na tatu aliloishi Mtume (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) pale Makkah tokea alipopewa utume mpaka siku ile aliyohama kwenda Madiynah, yote ilikuwa ni maumivu na machozi na huzuni. Hakupata kufurahi hata kwa muda wa saa moja au kustarehe angalau kwa siku moja.
Kila sifa njema anastahiki Allah na rehma na amani zimfikiye Mtume Muhamad na ahli zake na sahabaze na wenye kufuwata wayo kwa ihsani mpaka siku ya mwisho,
Mwito Kutoka Masjidul-Haraam Kwa Wanawake Wote Waislamu Ulimwenguni!
Sifa zote ni za Allah, Mwingi Wa Rehma Mwenye Kurehemu. Rehma na amani zimshukie Mtume Muhammad صلى الله عليه وسلم.
Dada zangu waislamu, hamutaweza kufikia ukamilifu munaotaka, hamutaweza kurudisha taadhima ya kale, wala kufikia daraja ya juu kabisa, isipokuwa mukifuata mafundisho ya Kiislamu na musipite mipaka ya sheria. Hii itawafanya nyoyo zenu zipende na kuthamini mitindo mizuri na kuepukana na mitindo mibaya.
Mwezi huu mtukufu umejaa fursa ya kujichumia mengi ya kheri ambayo thawabu zake huanzia tokea kumi hadi zaidi ya mia saba pamoja na malipo maalum yatokayo kwa Allaah kwa Mfungaji, kama alivyosema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم