1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
هَلْ أَتَىٰ عَلَى الْإِنسَانِ حِينٌ مِّنَ الدَّهْرِ لَمْ يَكُن شَيْئًا
مَّذْكُورًا
Hal ata AAala al-insani heenunmina addahri lam yakun shay-an mathkoora
Swahili
Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba hakuwa kitu
kinacho tajwa.
|
Ayah 76:2 الأية
إِنَّا خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن نُّطْفَةٍ أَمْشَاجٍ نَّبْتَلِيهِ فَجَعَلْنَاهُ
سَمِيعًا بَصِيرًا
Inna khalaqna al-insanamin nutfatin amshajin nabtaleehi fajaAAalnahusameeAAan
baseera
Swahili
Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika,
tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona.
|
Ayah 76:3 الأية
إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا
Inna hadaynahu assabeelaimma shakiran wa-imma kafoora
Swahili
Hakika Sisi tumembainishia Njia. Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru.
|
Ayah 76:4 الأية
إِنَّا أَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ سَلَاسِلَ وَأَغْلَالًا وَسَعِيرًا
Inna aAAtadna lilkafireenasalasila waaghlalan wasaAAeera
Swahili
Hakika Sisi tumewaandalia makafiri minyororo na pingu na Moto mkali.
|
Ayah 76:5 الأية
إِنَّ الْأَبْرَارَ يَشْرَبُونَ مِن كَأْسٍ كَانَ مِزَاجُهَا كَافُورًا
Inna al-abrara yashraboona min ka/sinkana mizajuha kafoora
Swahili
Hakika watu wema watakunywa katika vinywaji vilivyo changanyika na kafuri,
|
Ayah 76:6 الأية
عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا عِبَادُ اللهِ يُفَجِّرُونَهَا تَفْجِيرًا
AAaynan yashrabu biha AAibaduAllahi yufajjiroonaha tafjeera
Swahili
Ni chemchem watakao inywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakiifanya imiminike kwa
wingi.
|
Ayah 76:7 الأية
يُوفُونَ بِالنَّذْرِ وَيَخَافُونَ يَوْمًا كَانَ شَرُّهُ مُسْتَطِيرًا
Yoofoona binnathri wayakhafoonayawman kana sharruhu mustateera
Swahili
Wanatimiza ahadi, na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana,
|
Ayah 76:8 الأية
وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا
WayutAAimona attaAAamaAAala hubbihi miskeenan wayateeman waaseera
Swahili
Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa.
|
Ayah 76:9 الأية
إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمْ جَزَاءً وَلَا
شُكُورًا
Innama nutAAimukum liwajhi Allahila nureedu minkum jazaan wala shukoora
Swahili
Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo
wala shukrani.
|
Ayah 76:10 الأية
إِنَّا نَخَافُ مِن رَّبِّنَا يَوْمًا عَبُوسًا قَمْطَرِيرًا
Inna nakhafu min rabbinayawman AAaboosan qamtareera
Swahili
Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida na taabu.
|
Ayah 76:11 الأية
فَوَقَاهُمُ اللهُ شَرَّ ذَٰلِكَ الْيَوْمِ وَلَقَّاهُمْ نَضْرَةً وَسُرُورًا
Fawaqahumu Allahu sharra thalikaalyawmi walaqqahum nadratan wasuroora
Swahili
Basi Mwenyezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na raha
na furaha.
|
Ayah 76:12 الأية
وَجَزَاهُم بِمَا صَبَرُوا جَنَّةً وَحَرِيرًا
Wajazahum bima sabaroojannatan wahareera
Swahili
Na atawajazi Bustani za Peponi na maguo ya hariri kwa vile walivyo subiri.
|
Ayah 76:13 الأية
مُّتَّكِئِينَ فِيهَا عَلَى الْأَرَائِكِ ۖ لَا يَرَوْنَ فِيهَا شَمْسًا وَلَا
زَمْهَرِيرًا
Muttaki-eena feeha AAala al-ara-ikila yarawna feeha shamsan wala zamhareera
Swahili
Humo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona humo jua kali wala baridi kali.
|
Ayah 76:14 الأية
وَدَانِيَةً عَلَيْهِمْ ظِلَالُهَا وَذُلِّلَتْ قُطُوفُهَا تَذْلِيلًا
Wadaniyatan AAalayhim thilaluhawathullilat qutoofuha tathleela
Swahili
Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yataning'inia mpaka
chini.
|
Ayah 76:15 الأية
وَيُطَافُ عَلَيْهِم بِآنِيَةٍ مِّن فِضَّةٍ وَأَكْوَابٍ كَانَتْ قَوَارِيرَا
Wayutafu AAalayhim bi-aniyatinmin fiddatin waakwabin kanat qawareera
Swahili
Na watapitishiwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae,
|
Ayah 76:16 الأية
قَوَارِيرَ مِن فِضَّةٍ قَدَّرُوهَا تَقْدِيرًا
Qawareera min fiddatinqaddarooha taqdeera
Swahili
Vya fedha safi kama kiyoo, wamevipima kwa vipimo.
|
Ayah 76:17 الأية
وَيُسْقَوْنَ فِيهَا كَأْسًا كَانَ مِزَاجُهَا زَنجَبِيلًا
Wayusqawna feeha ka/san kanamizajuha zanjabeela
Swahili
Na humo watanyweshwa kinywaji kilicho changanyika na tangawizi.
|
Ayah 76:18 الأية
عَيْنًا فِيهَا تُسَمَّىٰ سَلْسَبِيلًا
AAaynan feeha tusammasalsabeela
Swahili
Hiyo ni chemchem iliyo humo inaitwa Salsabil.
|
Ayah 76:19 الأية
وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَانٌ مُّخَلَّدُونَ إِذَا رَأَيْتَهُمْ حَسِبْتَهُمْ
لُؤْلُؤًا مَّنثُورًا
Wayatoofu AAalayhim wildanunmukhalladoona itha raaytahum hasibtahum
lu/lu-anmanthoora
Swahili
Na watawazungukia kuwatumikia wavulana wasio pevuka, ukiwaona utawafikiri ni
lulu zilizo tawanywa.
|
Ayah 76:20 الأية
وَإِذَا رَأَيْتَ ثَمَّ رَأَيْتَ نَعِيمًا وَمُلْكًا كَبِيرًا
Wa-itha raayta thamma raaytanaAAeeman wamulkan kabeera
Swahili
Na utakapo yaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa.
|
Ayah 76:21 الأية
عَالِيَهُمْ ثِيَابُ سُندُسٍ خُضْرٌ وَإِسْتَبْرَقٌ ۖ وَحُلُّوا أَسَاوِرَ مِن
فِضَّةٍ وَسَقَاهُمْ رَبُّهُمْ شَرَابًا طَهُورًا
AAaliyahum thiyabu sundusinkhudrun wa-istabraqun wahulloo asawira minfiddatin
wasaqahum rabbuhum sharaban tahoora
Swahili
Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya
at'ilasi. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji
safi kabisa.
|
Ayah 76:22 الأية
إِنَّ هَٰذَا كَانَ لَكُمْ جَزَاءً وَكَانَ سَعْيُكُم مَّشْكُورًا
Inna hatha kana lakum jazaanwakana saAAyukum mashkoora
Swahili
Hakika haya ni malipo yenu; na juhudi zenu zimekubaliwa.
|
Ayah 76:23 الأية
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْقُرْآنَ تَنزِيلًا
Inna nahnu nazzalnaAAalayka alqur-ana tanzeela
Swahili
Hakika Sisi tumekuteremshia Qur'ani kidogo kidogo.
|
Ayah 76:24 الأية
فَاصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تُطِعْ مِنْهُمْ آثِمًا أَوْ كَفُورًا
Fasbir lihukmi rabbikawala tutiAA minhum athiman aw kafoora
Swahili
Basi ngojea hukumu ya Mola wako Mlezi wala usimt'ii miongoni mwao mwenye dhambi
au mwenye kufuru.
|
Ayah 76:25 الأية
وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ بُكْرَةً وَأَصِيلًا
Wathkuri isma rabbikabukratan waaseela
Swahili
Na likumbuke jina la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni;
|
Ayah 76:26 الأية
وَمِنَ اللَّيْلِ فَاسْجُدْ لَهُ وَسَبِّحْهُ لَيْلًا طَوِيلًا
Wamina allayli fasjud lahu wasabbihhulaylan taweela
Swahili
Na usiku msujudie Yeye, na umtakase usiku, wakati mrefu.
|
Ayah 76:27 الأية
إِنَّ هَٰؤُلَاءِ يُحِبُّونَ الْعَاجِلَةَ وَيَذَرُونَ وَرَاءَهُمْ يَوْمًا
ثَقِيلًا
Inna haola-i yuhibboonaalAAajilata wayatharoona waraahum yawmanthaqeela
Swahili
Kwa hakika watu hawa wanapenda maisha ya kidunia, na wanaiacha nyuma yao siku
nzito.
|
Ayah 76:28 الأية
نَّحْنُ خَلَقْنَاهُمْ وَشَدَدْنَا أَسْرَهُمْ ۖ وَإِذَا شِئْنَا بَدَّلْنَا
أَمْثَالَهُمْ تَبْدِيلًا
Nahnu khalaqnahum washadadnaasrahum wa-itha shi/na baddalna amthalahumtabdeela
Swahili
Sisi tumewaumba, na tukavitia nguvu viungo vyao. Na tukitaka tutawabadilisha
mfano wao wawe badala yao.
|
Ayah 76:29 الأية
إِنَّ هَٰذِهِ تَذْكِرَةٌ ۖ فَمَن شَاءَ اتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِ سَبِيلًا
Inna hathihi tathkiratun famanshaa ittakhatha ila rabbihi sabeela
Swahili
Hakika haya ni mawaidha; basi anaye taka atashika Njia ya kwenda kwa Mola wake
Mlezi.
|
Ayah 76:30 الأية
وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللهُ ۚ إِنَّ اللهَ كَانَ عَلِيمًا
حَكِيمًا
Wama tashaoona illa anyashaa Allahu inna Allaha kanaAAaleeman hakeema
Swahili
Wala hamwezi kutaka ila atakapo Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye
ilimu, Mwenye hikima.
|
Ayah 76:31 الأية
يُدْخِلُ مَن يَشَاءُ فِي رَحْمَتِهِ ۚ وَالظَّالِمِينَ أَعَدَّ لَهُمْ عَذَابًا
أَلِيمًا
Yudkhilu man yashao fee rahmatihiwaththalimeena aAAadda lahum AAathabanaleema
Swahili
Humuingiza amtakaye katika rehema yake. Na wenye kudhulumu amewawekea adhabu
iliyo chungu.
|
|