First Ayah 1 الأية الأوليبِسْم ِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Ayah 45:2 الأية
تَنزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ
Swahili
Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
|
Ayah 45:3 الأية
إِنَّ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّلْمُؤْمِنِينَ
Swahili
Hakika katika mbingu na ardhi ziko Ishara kwa Waumini.
|
Ayah 45:4 الأية
وَفِي خَلْقِكُمْ وَمَا يَبُثُّ مِن دَابَّةٍ آيَاتٌ لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ
Swahili
Na katika umbo lenu na katika wanyama alio watawanya zimo Ishara kwa watu wenye
yakini.
|
Ayah 45:5 الأية
وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَمَا أَنزَلَ اللَّهُ مِنَ السَّمَاءِ مِن
رِّزْقٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ آيَاتٌ
لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ
Swahili
Na kupishana usiku na mchana, na riziki anayo iteremsha Mwenyezi Mungu kutoka
mbinguni, na kwayo akaifufua ardhi baada ya kufa kwake, na mabadiliko ya upepo,
ni Ishara kwa watu wenye akili.
|
Ayah 45:6 الأية
تِلْكَ آيَاتُ اللَّهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ ۖ فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَ
اللَّهِ وَآيَاتِهِ يُؤْمِنُونَ
Swahili
Hizi Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki; basi hadithi gani watakayo
iamini baada ya Mwenyezi Mungu na Aya zake?
|
Ayah 45:7 الأية
وَيْلٌ لِّكُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ
Swahili
Ole wake kila mzushi mwenye dhambi!
|
Ayah 45:8 الأية
يَسْمَعُ آيَاتِ اللَّهِ تُتْلَىٰ عَلَيْهِ ثُمَّ يُصِرُّ مُسْتَكْبِرًا كَأَن
لَّمْ يَسْمَعْهَا ۖ فَبَشِّرْهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ
Swahili
Anaye sikia Aya za Mwenyezi Mungu akisomewa, kisha anashikilia yale yale aliyo
katazwa, na anajivuna, kama kwamba hakuzisikia. Basi mbashirie adhabu chungu!
|
Ayah 45:9 الأية
وَإِذَا عَلِمَ مِنْ آيَاتِنَا شَيْئًا اتَّخَذَهَا هُزُوًا ۚ أُولَٰئِكَ لَهُمْ
عَذَابٌ مُّهِينٌ
Swahili
Na anapo kijua kitu kidogo katika Aya zetu hukifanyia mzaha. Watu hao ndio
watakao kuwa na adhabu ya kufedhehesha.
|
Ayah 45:10 الأية
مِّن وَرَائِهِمْ جَهَنَّمُ ۖ وَلَا يُغْنِي عَنْهُم مَّا كَسَبُوا شَيْئًا وَلَا
مَا اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّهِ أَوْلِيَاءَ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ
Swahili
Na nyuma yao ipo Jahannamu. Na walio yachuma hayatawafaa hata kidogo, wala
walinzi walio washika badala ya Mwenyezi Mungu. Na watapata adhabu kubwa.
|
Ayah 45:11 الأية
هَٰذَا هُدًى ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ لَهُمْ عَذَابٌ مِّن
رِّجْزٍ أَلِيمٌ
Swahili
Huu ni uwongofu. Na wale wale walio zikataa Ishara za Mola wao Mlezi watapata
adhabu inayo tokana na ghadhabu iliyo chungu.
|
Ayah 45:12 الأية
اللَّهُ الَّذِي سَخَّرَ لَكُمُ الْبَحْرَ لِتَجْرِيَ الْفُلْكُ فِيهِ بِأَمْرِهِ
وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ
Swahili
Mwenyezi Mungu ndiye aliye ifanya bahari ikutumikieni, ili humo zipite marikebu
kwa amri yake, na ili mtafute fadhila yake, na mpate kushukuru.
|
Ayah 45:13 الأية
وَسَخَّرَ لَكُم مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا مِّنْهُ ۚ
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ
Swahili
Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote
vimetoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanao fikiri.
|
Ayah 45:14 الأية
قُل لِّلَّذِينَ آمَنُوا يَغْفِرُوا لِلَّذِينَ لَا يَرْجُونَ أَيَّامَ اللَّهِ
لِيَجْزِيَ قَوْمًا بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ
Swahili
Waambie walio amini wawasamehe wale wasio zitaraji siku za Mwenyezi Mungu, ili
awalipe kwa waliyo kuwa wakiyachuma.
|
Ayah 45:15 الأية
مَنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَنْ أَسَاءَ فَعَلَيْهَا ۖ ثُمَّ إِلَىٰ
رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ
Swahili
Mwenye kutenda mema basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na mwenye kutenda uovu ni
juu yake mwenyewe. Kisha mtarudishwa kwa Mola wenu Mlezi.
|
Ayah 45:16 الأية
وَلَقَدْ آتَيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ
وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ
Swahili
Na hakika tuliwapa Wana wa Israili Kitabu na hukumu na Unabii, na tukawaruzuku
vitu vizuri vizuri, na tukawafadhilisha kuliko walimwengu wote.
|
Ayah 45:17 الأية
وَآتَيْنَاهُم بَيِّنَاتٍ مِّنَ الْأَمْرِ ۖ فَمَا اخْتَلَفُوا إِلَّا مِن بَعْدِ
مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُمْ
يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ
Swahili
Na tukawapa maelezo wazi ya amri. Basi hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia
ujuzi, kwa ajili ya uhasidi uliyo kuwa baina yao. Hakika Mola wako Mlezi
atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika mambo waliyo kuwa wakikhitalifiana.
|
Ayah 45:18 الأية
ثُمَّ جَعَلْنَاكَ عَلَىٰ شَرِيعَةٍ مِّنَ الْأَمْرِ فَاتَّبِعْهَا وَلَا تَتَّبِعْ
أَهْوَاءَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ
Swahili
Kisha tukakuweka wewe juu ya Njia ya haya mambo, basi ifuate, wala usifuate
matamanio ya wasio jua kitu.
|
Ayah 45:19 الأية
إِنَّهُمْ لَن يُغْنُوا عَنكَ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا ۚ وَإِنَّ الظَّالِمِينَ
بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۖ وَاللَّهُ وَلِيُّ الْمُتَّقِينَ
Swahili
Kwa hakika hao hawatakufaa kitu mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hakika wenye
kudhulumu ni marafiki wao kwa wao. Na Mwenyezi Mungu ni rafiki wa wamchao.
|
Ayah 45:20 الأية
هَٰذَا بَصَائِرُ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ
Swahili
Hizi ni dalili zilizo wazi kwa watu wote, na ni uwongofu, na rehema kwa watu
wanao yakinisha.
|
Ayah 45:21 الأية
أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ اجْتَرَحُوا السَّيِّئَاتِ أَن نَّجْعَلَهُمْ كَالَّذِينَ
آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ سَوَاءً مَّحْيَاهُمْ وَمَمَاتُهُمْ ۚ سَاءَ مَا
يَحْكُمُونَ
Swahili
Je! Wanadhani wanao tenda maovu kuwa tutawafanya kama walio amini, na wakatenda
mema, sawa sawa uhai wao na kufa kwao? Ni hukumu mbaya wanayo ihukumu!
|
Ayah 45:22 الأية
وَخَلَقَ اللَّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ وَلِتُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ
بِمَا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ
Swahili
Na Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa haki, na ili kila nafsi ilipwe
yale iliyo yachuma. Nao hawatadhulumiwa.
|
Ayah 45:23 الأية
أَفَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَٰهَهُ هَوَاهُ وَأَضَلَّهُ اللَّهُ عَلَىٰ عِلْمٍ
وَخَتَمَ عَلَىٰ سَمْعِهِ وَقَلْبِهِ وَجَعَلَ عَلَىٰ بَصَرِهِ غِشَاوَةً فَمَن
يَهْدِيهِ مِن بَعْدِ اللَّهِ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Swahili
Je! Umemwona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu
akamwacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi, na akapiga muhuri juu ya masikio
yake, na moyo wake, na akambandika vitanga machoni mwake? Basi nani atamwongoa
huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Hamkumbuki?
|
Ayah 45:24 الأية
وَقَالُوا مَا هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا
يُهْلِكُنَا إِلَّا الدَّهْرُ ۚ وَمَا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنْ عِلْمٍ ۖ إِنْ هُمْ
إِلَّا يَظُنُّونَ
Swahili
Na walisema: Hapana ila huu uhai wetu wa duniani - twafa na twaishi, na hapana
kinacho tuhiliki isipo kuwa dahari. Lakini wao hawana ilimu ya hayo, ila wao
wanadhani tu.
|
Ayah 45:25 الأية
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ مَّا كَانَ حُجَّتَهُمْ إِلَّا
أَن قَالُوا ائْتُوا بِآبَائِنَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ
Swahili
Na wakisomewa Aya zetu zilizo wazi hawana hoja ila kusema: Waleteni baba zetu,
ikiwa nyinyi ni wasemao kweli.
|
Ayah 45:26 الأية
قُلِ اللَّهُ يُحْيِيكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يَجْمَعُكُمْ إِلَىٰ يَوْمِ
الْقِيَامَةِ لَا رَيْبَ فِيهِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ
Swahili
Sema: Mwenyezi Mungu anakuhuisheni, kisha anakufisheni, kisha anakukusanyeni
Siku ya Kiyama isiyo na shaka. Lakini watu wengi hawajui.
|
Ayah 45:27 الأية
وَلِلَّهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ
يَوْمَئِذٍ يَخْسَرُ الْمُبْطِلُونَ
Swahili
Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Na siku itapo simama
Saa ya Kiyama, siku hiyo wataangamia wenye kushikamana na upotovu.
|
Ayah 45:28 الأية
وَتَرَىٰ كُلَّ أُمَّةٍ جَاثِيَةً ۚ كُلُّ أُمَّةٍ تُدْعَىٰ إِلَىٰ كِتَابِهَا
الْيَوْمَ تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Swahili
Na utauona kila umma umepiga magoti, na kila umma utaitwa kwenda soma kitabu
chake: Leo mtalipwa mliyo kuwa mkiyatenda.
|
Ayah 45:29 الأية
هَٰذَا كِتَابُنَا يَنطِقُ عَلَيْكُم بِالْحَقِّ ۚ إِنَّا كُنَّا نَسْتَنسِخُ مَا
كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Swahili
Hichi kitabu chetu kinasema juu yenu kwa haki. Hakika Sisi tulikuwa tukiyaandika
mliyo kuwa mkiyatenda.
|
Ayah 45:30 الأية
فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُدْخِلُهُمْ رَبُّهُمْ فِي
رَحْمَتِهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْمُبِينُ
Swahili
Ama walio amini na wakatenda mema, Mola wao Mlezi atawatia katika rehema yake.
Huko ndiko kufuzu kulio wazi.
|
Ayah 45:31 الأية
وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا أَفَلَمْ تَكُنْ آيَاتِي تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ
فَاسْتَكْبَرْتُمْ وَكُنتُمْ قَوْمًا مُّجْرِمِينَ
Swahili
Na ama walio kufuru, wataambiwa: Kwani hamkuwa mkisomewa Aya zangu nanyi
mkapanda kichwa, na mkawa watu wakosefu?
|
Ayah 45:32 الأية
وَإِذَا قِيلَ إِنَّ وَعْدَ اللَّهِ حَقٌّ وَالسَّاعَةُ لَا رَيْبَ فِيهَا قُلْتُم
مَّا نَدْرِي مَا السَّاعَةُ إِن نَّظُنُّ إِلَّا ظَنًّا وَمَا نَحْنُ
بِمُسْتَيْقِنِينَ
Swahili
Na ikisemwa: Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli, na Saa haina shaka, nyinyi
mkisema: Hatuijui hiyo Saa, tunadhania dhana tu, wala hatuna yakini.
|
Ayah 45:33 الأية
وَبَدَا لَهُمْ سَيِّئَاتُ مَا عَمِلُوا وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ
يَسْتَهْزِئُونَ
Swahili
Basi ubaya wa waliyo yatenda utawadhihirikia, na yatawazunguka waliyo yafanyia
maskhara.
|
Ayah 45:34 الأية
وَقِيلَ الْيَوْمَ نَنسَاكُمْ كَمَا نَسِيتُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَٰذَا
وَمَأْوَاكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن نَّاصِرِينَ
Swahili
Na itasemwa: Leo tunakusahauni kama nyinyi mlivyo sahau mkutano wa siku yenu
hii; na mahali penu ni Motoni, wala hamna wa kukunusuruni.
|
Ayah 45:35 الأية
ذَٰلِكُم بِأَنَّكُمُ اتَّخَذْتُمْ آيَاتِ اللَّهِ هُزُوًا وَغَرَّتْكُمُ
الْحَيَاةُ الدُّنْيَا ۚ فَالْيَوْمَ لَا يُخْرَجُونَ مِنْهَا وَلَا هُمْ
يُسْتَعْتَبُونَ
Swahili
Hayo ni kwa sababu nyinyi mlizifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu; na maisha ya
dunia yakakudanganyeni. Basi leo hawatatolewa humo wala hao hawatakubaliwa
udhuru wao.
|
Ayah 45:36 الأية
فَلِلَّهِ الْحَمْدُ رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَرَبِّ الْأَرْضِ رَبِّ الْعَالَمِينَ
Swahili
Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa mbingu, na Mola Mlezi
wa ardhi, na Mola Mlezi wa walimwengu wote.
|
Ayah 45:37 الأية
وَلَهُ الْكِبْرِيَاءُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ
الْحَكِيمُ
Swahili
Na ukubwa ni wake Yeye tu, mbinguni na katika ardhi, naye ni Mwenye nguvu,
Mwenye hikima.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|