First Ayah 1 الأية الأوليبِسْم ِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ وَقُرْآنٍ مُّبِينٍ
Swahili
Alif Lam Ra. (A.L.R). Hizi ni Aya za Kitabu na Qur'ani inayo bainisha.
|
Ayah 15:2 الأية
رُّبَمَا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ كَانُوا مُسْلِمِينَ
Swahili
HUENDA ikawa walio kufuru wakatamani wange kuwa Waislamu.
|
Ayah 15:3 الأية
ذَرْهُمْ يَأْكُلُوا وَيَتَمَتَّعُوا وَيُلْهِهِمُ الْأَمَلُ ۖ فَسَوْفَ
يَعْلَمُونَ
Swahili
Waache wale, na wastarehe, na iwazuge tamaa. Watakuja jua.
|
Ayah 15:4 الأية
وَمَا أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ إِلَّا وَلَهَا كِتَابٌ مَّعْلُومٌ
Swahili
Na hatukuuangamiza mji wowote ule ila ulikuwa na muda wake maalumu.
|
Ayah 15:5 الأية
مَّا تَسْبِقُ مِنْ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسْتَأْخِرُونَ
Swahili
Hawawezi watu wowote kuitangulia ajali yao, wala kuchelewa.
|
Ayah 15:6 الأية
وَقَالُوا يَا أَيُّهَا الَّذِي نُزِّلَ عَلَيْهِ الذِّكْرُ إِنَّكَ لَمَجْنُونٌ
Swahili
Na walisema: Ewe uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe ni mwendawazimu.
|
Ayah 15:7 الأية
لَّوْ مَا تَأْتِينَا بِالْمَلَائِكَةِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ
Swahili
Mbona hutuletei Malaika ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli?
|
Ayah 15:8 الأية
مَا نُنَزِّلُ الْمَلَائِكَةَ إِلَّا بِالْحَقِّ وَمَا كَانُوا إِذًا مُّنظَرِينَ
Swahili
Sisi hatuwateremshi Malaika ila kwa sababu ya haki, na hapo hawatapewa muhula.
|
Ayah 15:9 الأية
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ
Swahili
Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.
|
Ayah 15:10 الأية
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِي شِيَعِ الْأَوَّلِينَ
Swahili
Na hakika tulikwisha watumia Mitume mataifa ya mwanzo.
|
Ayah 15:11 الأية
وَمَا يَأْتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ
Swahili
Na hakuwafikia Mtume ila walimkejeli.
|
Ayah 15:12 الأية
كَذَٰلِكَ نَسْلُكُهُ فِي قُلُوبِ الْمُجْرِمِينَ
Swahili
Na kama hivi ndivyo tunavyo ingiza katika nyoyo za wakosefu.
|
Ayah 15:13 الأية
لَا يُؤْمِنُونَ بِهِ ۖ وَقَدْ خَلَتْ سُنَّةُ الْأَوَّلِينَ
Swahili
Hawayaamini haya, na hali ya kuwa umekwisha wapitia mfano wa watu wa kale.
|
Ayah 15:14 الأية
وَلَوْ فَتَحْنَا عَلَيْهِم بَابًا مِّنَ السَّمَاءِ فَظَلُّوا فِيهِ يَعْرُجُونَ
Swahili
Na lau tungeli wafungulia mlango wa mbingu, wakawa wanapanda,
|
Ayah 15:15 الأية
لَقَالُوا إِنَّمَا سُكِّرَتْ أَبْصَارُنَا بَلْ نَحْنُ قَوْمٌ مَّسْحُورُونَ
Swahili
Basi wangeli sema: Macho yetu yamelevywa, bali sisi wenyewe tumerogwa.
|
Ayah 15:16 الأية
وَلَقَدْ جَعَلْنَا فِي السَّمَاءِ بُرُوجًا وَزَيَّنَّاهَا لِلنَّاظِرِينَ
Swahili
Na hakika tumeweka katika mbingu vituo vya sayari, na tumezipamba kwa wenye
kuangalia.
|
Ayah 15:17 الأية
وَحَفِظْنَاهَا مِن كُلِّ شَيْطَانٍ رَّجِيمٍ
Swahili
Na tumezilinda na kila shetani afukuzwaye.
|
Ayah 15:18 الأية
إِلَّا مَنِ اسْتَرَقَ السَّمْعَ فَأَتْبَعَهُ شِهَابٌ مُّبِينٌ
Swahili
Isipo kuwa mwenye kusikiliza kwa kuibia, naye hufuatwa na kijinga cha moto
kinacho onekana.
|
Ayah 15:19 الأية
وَالْأَرْضَ مَدَدْنَاهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنبَتْنَا فِيهَا مِن
كُلِّ شَيْءٍ مَّوْزُونٍ
Swahili
Na ardhi tumeitandaza na humo tumeweka milima, na tumeotesha kila kitu kwa kiasi
chake.
|
Ayah 15:20 الأية
وَجَعَلْنَا لَكُمْ فِيهَا مَعَايِشَ وَمَن لَّسْتُمْ لَهُ بِرَازِقِينَ
Swahili
Na tumekujaalieni humo vitu vya maisha yenu, na ya hao ambao nyinyi sio wenye
kuwaruzuku.
|
Ayah 15:21 الأية
وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلَّا عِندَنَا خَزَائِنُهُ وَمَا نُنَزِّلُهُ إِلَّا بِقَدَرٍ
مَّعْلُومٍ
Swahili
Na hakuna chochote ila asili yake inatokana na Sisi; wala hatukiteremshi ila kwa
kipimo maalumu.
|
Ayah 15:22 الأية
وَأَرْسَلْنَا الرِّيَاحَ لَوَاقِحَ فَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً
فَأَسْقَيْنَاكُمُوهُ وَمَا أَنتُمْ لَهُ بِخَازِنِينَ
Swahili
Na tunazipeleka pepo za kupandishia, na tunateremsha kutoka mbinguni maji, kisha
tukakunywesheni maji hayo. Wala si nyinyi mnayo yaweka.
|
Ayah 15:23 الأية
وَإِنَّا لَنَحْنُ نُحْيِي وَنُمِيتُ وَنَحْنُ الْوَارِثُونَ
Swahili
Na Sisi ndio tunao huisha na tunao fisha. Na Sisi ndio Warithi.
|
Ayah 15:24 الأية
وَلَقَدْ عَلِمْنَا الْمُسْتَقْدِمِينَ مِنكُمْ وَلَقَدْ عَلِمْنَا
الْمُسْتَأْخِرِينَ
Swahili
Na tunawajua walio tangulia katika nyinyi, na tunawajua walio taakhari.
|
Ayah 15:25 الأية
وَإِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَحْشُرُهُمْ ۚ إِنَّهُ حَكِيمٌ عَلِيمٌ
Swahili
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye atakaye wakusanya. Hakika Yeye ni Mwenye hikima
na Mjuzi.
|
Ayah 15:26 الأية
وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ
Swahili
Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa
sura.
|
Ayah 15:27 الأية
وَالْجَانَّ خَلَقْنَاهُ مِن قَبْلُ مِن نَّارِ السَّمُومِ
Swahili
Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto.
|
Ayah 15:28 الأية
وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِّن صَلْصَالٍ مِّنْ
حَمَإٍ مَّسْنُونٍ
Swahili
Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo
unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.
|
Ayah 15:29 الأية
فَإِذَا سَوَّيْتُهُ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِي فَقَعُوا لَهُ سَاجِدِينَ
Swahili
Basi nitakapo mkamilisha na nikampulizia roho yangu, basi mumwangukie
kumsujudia.
|
Ayah 15:30 الأية
فَسَجَدَ الْمَلَائِكَةُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ
Swahili
Basi Malaika wote pamoja walimsujudia,
|
Ayah 15:31 الأية
إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ أَن يَكُونَ مَعَ السَّاجِدِينَ
Swahili
Isipo kuwa Iblisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na walio sujudu.
|
Ayah 15:32 الأية
قَالَ يَا إِبْلِيسُ مَا لَكَ أَلَّا تَكُونَ مَعَ السَّاجِدِينَ
Swahili
(Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Iblisi! Una nini hata hukuwa pamoja na walio
sujudu?
|
Ayah 15:33 الأية
قَالَ لَمْ أَكُن لِّأَسْجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقْتَهُ مِن صَلْصَالٍ مِّنْ حَمَإٍ
مَّسْنُونٍ
Swahili
Akasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliye muumba kwa udongo unao toa sauti, unao
tokana na matope yenye sura.
|
Ayah 15:34 الأية
قَالَ فَاخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ
Swahili
(Mwenyezi Mungu) akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe ni maluuni!
|
Ayah 15:35 الأية
وَإِنَّ عَلَيْكَ اللَّعْنَةَ إِلَىٰ يَوْمِ الدِّينِ
Swahili
Na hakika juu yako ipo laana mpaka Siku ya Malipo.
|
Ayah 15:36 الأية
قَالَ رَبِّ فَأَنظِرْنِي إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ
Swahili
Akasema (Iblisi): Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watapo fufuliwa.
|
Ayah 15:37 الأية
قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ الْمُنظَرِينَ
Swahili
(Mwenyezi Mungu) akasema: Hakika wewe ni katika walio pewa muhula
|
Ayah 15:38 الأية
إِلَىٰ يَوْمِ الْوَقْتِ الْمَعْلُومِ
Swahili
Mpaka siku ya wakati maalumu.
|
Ayah 15:39 الأية
قَالَ رَبِّ بِمَا أَغْوَيْتَنِي لَأُزَيِّنَنَّ لَهُمْ فِي الْأَرْضِ
وَلَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ
Swahili
Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyo kuwa umenitia makosani, basi nahakikisha
nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote,
|
Ayah 15:40 الأية
إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ الْمُخْلَصِينَ
Swahili
Ila waja wako walio safika.
|
Ayah 15:41 الأية
قَالَ هَٰذَا صِرَاطٌ عَلَيَّ مُسْتَقِيمٌ
Swahili
Akasema: Hii Njia ya kujia kwangu Iliyo Nyooka.
|
Ayah 15:42 الأية
إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ إِلَّا مَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ
الْغَاوِينَ
Swahili
Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipo kuwa wale wapotofu
walio kufuata.
|
Ayah 15:43 الأية
وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوْعِدُهُمْ أَجْمَعِينَ
Swahili
Na bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipo ahidiwa wote.
|
Ayah 15:44 الأية
لَهَا سَبْعَةُ أَبْوَابٍ لِّكُلِّ بَابٍ مِّنْهُمْ جُزْءٌ مَّقْسُومٌ
Swahili
Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu walio tengewa.
|
Ayah 15:45 الأية
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ
Swahili
Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem.
|
Ayah 15:46 الأية
ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ آمِنِينَ
Swahili
(Wataambiwa:) Ingieni kwa salama na amani.
|
Ayah 15:47 الأية
وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ إِخْوَانًا عَلَىٰ سُرُرٍ
مُّتَقَابِلِينَ
Swahili
Na tutaondoa chuki iliyo kuwamo vifuani mwao, wawe ndugu juu ya viti vya enzi
wameelekeana.
|
Ayah 15:48 الأية
لَا يَمَسُّهُمْ فِيهَا نَصَبٌ وَمَا هُم مِّنْهَا بِمُخْرَجِينَ
Swahili
Humo hayatawagusa machofu, wala hawatatolewa humo.
|
Ayah 15:49 الأية
نَبِّئْ عِبَادِي أَنِّي أَنَا الْغَفُورُ الرَّحِيمُ
Swahili
Waambie waja wangu ya kwamba Mimi ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
|
Ayah 15:50 الأية
وَأَنَّ عَذَابِي هُوَ الْعَذَابُ الْأَلِيمُ
Swahili
Na kwamba adhabu yangu ndio adhabu iliyo chungu!
|
Ayah 15:51 الأية
وَنَبِّئْهُمْ عَن ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ
Swahili
Na uwape khabari za wageni wa Ibrahim.
|
Ayah 15:52 الأية
إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا قَالَ إِنَّا مِنكُمْ وَجِلُونَ
Swahili
Walipo ingia kwake na wakasema: Salama! Yeye akasema: Hakika sisi tunakuogopeni.
|
Ayah 15:53 الأية
قَالُوا لَا تَوْجَلْ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ
Swahili
Wakasema: Usiogope. Sisi tunakubashiria kijana mwenye ujuzi.
|
Ayah 15:54 الأية
قَالَ أَبَشَّرْتُمُونِي عَلَىٰ أَن مَّسَّنِيَ الْكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ
Swahili
Akasema: Mnanibashiria nami uzee umenishika! Basi kwa njia gani mnanibashiria?
|
Ayah 15:55 الأية
قَالُوا بَشَّرْنَاكَ بِالْحَقِّ فَلَا تَكُن مِّنَ الْقَانِطِينَ
Swahili
Wakasema: Tunakubashiria kwa haki; basi usiwe miongoni mwa wanao kata tamaa.
|
Ayah 15:56 الأية
قَالَ وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِ إِلَّا الضَّالُّونَ
Swahili
Akasema: Na nani anaye kata tamaa na rehema ya Mola wake Mlezi ila wale walio
potea?
|
Ayah 15:57 الأية
قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ
Swahili
Akasema: Hebu nini amri yenu, enyi wajumbe?
|
Ayah 15:58 الأية
قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ
Swahili
Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya wakosefu!
|
Ayah 15:59 الأية
إِلَّا آلَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمْ أَجْمَعِينَ
Swahili
Isipo kuwa walio mfuata Luut'i. Bila ya shaka sisi tutawaokoa hao wote.
|
Ayah 15:60 الأية
إِلَّا امْرَأَتَهُ قَدَّرْنَا ۙ إِنَّهَا لَمِنَ الْغَابِرِينَ
Swahili
Ila mkewe. Tunakadiria huyo atakuwa miongoni watao bakia nyuma.
|
Ayah 15:61 الأية
فَلَمَّا جَاءَ آلَ لُوطٍ الْمُرْسَلُونَ
Swahili
Basi wale wajumbe walipo fika kwa Luut'i,
|
Ayah 15:62 الأية
قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ
Swahili
Alisema (Luut'i): Hakika nyinyi ni watu msio juulikana.
|
Ayah 15:63 الأية
قَالُوا بَلْ جِئْنَاكَ بِمَا كَانُوا فِيهِ يَمْتَرُونَ
Swahili
Wakasema: Bali sisi tumekuletea yale waliyo kuwa wakiyafanyia shaka.
|
Ayah 15:64 الأية
وَأَتَيْنَاكَ بِالْحَقِّ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ
Swahili
Na tumefika kwako kwa Haki, na hakika sisi tunasema kweli.
|
Ayah 15:65 الأية
فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِّنَ اللَّيْلِ وَاتَّبِعْ أَدْبَارَهُمْ وَلَا
يَلْتَفِتْ مِنكُمْ أَحَدٌ وَامْضُوا حَيْثُ تُؤْمَرُونَ
Swahili
Basi ondoka na ahli zako usiku ungalipo, nawe ufuate nyuma yao, wala yeyote kati
yenu asigeuke nyuma. Na mwende mnapo amrishwa.
|
Ayah 15:66 الأية
وَقَضَيْنَا إِلَيْهِ ذَٰلِكَ الْأَمْرَ أَنَّ دَابِرَ هَٰؤُلَاءِ مَقْطُوعٌ
مُّصْبِحِينَ
Swahili
Na tukamfunulia hukumu hiyo, ya kwamba hata wa mwisho wao hao ikifika asubuhi
atakuwa kesha katiliwa mbali.
|
Ayah 15:67 الأية
وَجَاءَ أَهْلُ الْمَدِينَةِ يَسْتَبْشِرُونَ
Swahili
Na wakaja watu wa mji ule nao furahani.
|
Ayah 15:68 الأية
قَالَ إِنَّ هَٰؤُلَاءِ ضَيْفِي فَلَا تَفْضَحُونِ
Swahili
Akasema: Hakika hawa wageni wangu, basi msinifedheheshe.
|
Ayah 15:69 الأية
وَاتَّقُوا اللَّهَ وَلَا تُخْزُونِ
Swahili
Na mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi.
|
Ayah 15:70 الأية
قَالُوا أَوَلَمْ نَنْهَكَ عَنِ الْعَالَمِينَ
Swahili
Wakasema: Sisi hatukukukataza usimkaribishe yeyote?
|
Ayah 15:71 الأية
قَالَ هَٰؤُلَاءِ بَنَاتِي إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ
Swahili
Akasema: Hawa binti zangu, ikiwa nyinyi ni watendaji.
|
Ayah 15:72 الأية
لَعَمْرُكَ إِنَّهُمْ لَفِي سَكْرَتِهِمْ يَعْمَهُونَ
Swahili
Naapa kwa umri wako! Hakika hao walikuwa katika ulevi wao, wakihangaika ovyo.
|
Ayah 15:73 الأية
فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ مُشْرِقِينَ
Swahili
Ukelele ukawatwaa wakipambaukiwa.
|
Ayah 15:74 الأية
فَجَعَلْنَا عَالِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِّن
سِجِّيلٍ
Swahili
Na tukaigeuza nchi juu chini, na tukawanyeshea mvua ya mawe ya udongo wa Motoni.
|
Ayah 15:75 الأية
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّلْمُتَوَسِّمِينَ
Swahili
Hakika katika hayo zipo ishara kwa waaguzi.
|
Ayah 15:76 الأية
وَإِنَّهَا لَبِسَبِيلٍ مُّقِيمٍ
Swahili
Na miji hii ipo kwenye njia inayo pitiwa.
|
Ayah 15:77 الأية
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لِّلْمُؤْمِنِينَ
Swahili
Hakika katika hayo ipo ishara kwa Waumini.
|
Ayah 15:78 الأية
وَإِن كَانَ أَصْحَابُ الْأَيْكَةِ لَظَالِمِينَ
Swahili
Na hakika watu wa Kichakani walikuwa wenye kudhulumu.
|
Ayah 15:79 الأية
فَانتَقَمْنَا مِنْهُمْ وَإِنَّهُمَا لَبِإِمَامٍ مُّبِينٍ
Swahili
Kwa hivyo tukawaadhibu. Na nchi mbili hizi ziko kwenye njia ilio wazi.
|
Ayah 15:80 الأية
وَلَقَدْ كَذَّبَ أَصْحَابُ الْحِجْرِ الْمُرْسَلِينَ
Swahili
Na bila ya shaka wakaazi wa Hijr waliwakanusha Mitume.
|
Ayah 15:81 الأية
وَآتَيْنَاهُمْ آيَاتِنَا فَكَانُوا عَنْهَا مُعْرِضِينَ
Swahili
Na tuliwapa ishara zetu, nao wakazipuuza.
|
Ayah 15:82 الأية
وَكَانُوا يَنْحِتُونَ مِنَ الْجِبَالِ بُيُوتًا آمِنِينَ
Swahili
Nao walikuwa wakichonga majumba katika milima kwa amani.
|
Ayah 15:83 الأية
فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ مُصْبِحِينَ
Swahili
Basi ukelele ukawatwaa asubuhi.
|
Ayah 15:84 الأية
فَمَا أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ
Swahili
Hayakuwafaa waliyo kuwa wakiyachuma.
|
Ayah 15:85 الأية
وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ ۗ
وَإِنَّ السَّاعَةَ لَآتِيَةٌ ۖ فَاصْفَحِ الصَّفْحَ الْجَمِيلَ
Swahili
Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ila kwa ajili ya Haki.
Na hakika Kiyama kitafika. Basi samehe msamaha mzuri.
|
Ayah 15:86 الأية
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ الْخَلَّاقُ الْعَلِيمُ
Swahili
Hakika Mola wako Mlezi ndiye Muumbaji Mjuzi.
|
Ayah 15:87 الأية
وَلَقَدْ آتَيْنَاكَ سَبْعًا مِّنَ الْمَثَانِي وَالْقُرْآنَ الْعَظِيمَ
Swahili
Na tumekupa Aya saba zinazo somwa mara kwa mara, na Qur'ani Tukufu.
|
Ayah 15:88 الأية
لَا تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِّنْهُمْ وَلَا
تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِلْمُؤْمِنِينَ
Swahili
Usivitumbulie macho yako vitu tulivyo waneemesha makundi fulani kati yao, wala
usiwahuzunikie. Na wainamishie bawa lako (la huruma) Waumini.
|
Ayah 15:89 الأية
وَقُلْ إِنِّي أَنَا النَّذِيرُ الْمُبِينُ
Swahili
Na sema: Hakika mimi ni mwonyaji mwenye kubainisha.
|
Ayah 15:90 الأية
كَمَا أَنزَلْنَا عَلَى الْمُقْتَسِمِينَ
Swahili
Kama hivyo tuliwateremshia walio gawa,
|
Ayah 15:91 الأية
الَّذِينَ جَعَلُوا الْقُرْآنَ عِضِينَ
Swahili
Ambao wakaifanya Qur'ani vipande vipande.
|
Ayah 15:92 الأية
فَوَرَبِّكَ لَنَسْأَلَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ
Swahili
Basi Naapa kwa Mola wako Mlezi! Tutawahoji wote,
|
Ayah 15:93 الأية
عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Swahili
Kwa waliyo kuwa wakiyatenda.
|
Ayah 15:94 الأية
فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ
Swahili
Basi wewe yatangaze uliyo amrishwa, na jitenge na washirikina.
|
Ayah 15:95 الأية
إِنَّا كَفَيْنَاكَ الْمُسْتَهْزِئِينَ
Swahili
Hakika Sisi tunatosha kukukinga na wanao kejeli.
|
Ayah 15:96 الأية
الَّذِينَ يَجْعَلُونَ مَعَ اللَّهِ إِلَٰهًا آخَرَ ۚ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ
Swahili
Hao wanao fanya kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu yupo mungu mwingine. Basi,
watakuja jua!
|
Ayah 15:97 الأية
وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّكَ يَضِيقُ صَدْرُكَ بِمَا يَقُولُونَ
Swahili
Na Sisi tunajua kwa hakika kuwa wewe kifua chako kinaona dhiki kwa hayo
wayasemayo.
|
Ayah 15:98 الأية
فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَكُن مِّنَ السَّاجِدِينَ
Swahili
Basi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi, na uwe miongoni wanao msujudia.
|
Ayah 15:99 الأية
وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ
Swahili
Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|