First Ayah 1 الأية الأوليبِسْم ِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Ayah 40:2 الأية
تَنزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّهِ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ
Swahili
Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mwenye kujua.
|
Ayah 40:3 الأية
غَافِرِ الذَّنبِ وَقَابِلِ التَّوْبِ شَدِيدِ الْعِقَابِ ذِي الطَّوْلِ ۖ لَا
إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ إِلَيْهِ الْمَصِيرُ
Swahili
Anaye samehe dhambi na anaye pokea toba, Mkali wa kuadhibu, Mwenye ukarimu,
hakuna mungu ila Yeye; marejeo ni kwake.
|
Ayah 40:4 الأية
مَا يُجَادِلُ فِي آيَاتِ اللَّهِ إِلَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَلَا يَغْرُرْكَ
تَقَلُّبُهُمْ فِي الْبِلَادِ
Swahili
Hawazibishi Ishara za Mwenyezi Mungu ila walio kufuru; basi kusikughuri wewe
kutanga tanga kwao katika nchi.
|
Ayah 40:5 الأية
كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَالْأَحْزَابُ مِن بَعْدِهِمْ ۖ وَهَمَّتْ
كُلُّ أُمَّةٍ بِرَسُولِهِمْ لِيَأْخُذُوهُ ۖ وَجَادَلُوا بِالْبَاطِلِ
لِيُدْحِضُوا بِهِ الْحَقَّ فَأَخَذْتُهُمْ ۖ فَكَيْفَ كَانَ عِقَابِ
Swahili
Kabla yao walikadhibisha kaumu ya Nuhu na makundi mengine baada yao. Na kila
taifa lilikuwa na hamu juu ya Mtume wao wamkamate. Na walibishana kwa upotovu
ili kuipindua haki. Kwa hivyo niliwakamata. Basi ilikuwaje adhabu yangu!
|
Ayah 40:6 الأية
وَكَذَٰلِكَ حَقَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّهُمْ
أَصْحَابُ النَّارِ
Swahili
Namna hivi limewathibitikia makafiri neno la Mola wako Mlezi ya kwamba wao ni
watu wa Motoni.
|
Ayah 40:7 الأية
الَّذِينَ يَحْمِلُونَ الْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ
وَيُؤْمِنُونَ بِهِ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ
شَيْءٍ رَّحْمَةً وَعِلْمًا فَاغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا وَاتَّبَعُوا سَبِيلَكَ
وَقِهِمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ
Swahili
Wale wanao beba A'rshi, na wanao izunguka, wanamsabihi na kumhimidi Mola wao
Mlezi, na wanamuamini, na wanawaombea msamaha walio amini kwa kusema: Mola wetu
Mlezi! Umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi. Basi wasamehe walio tubu na
wakaifuata Njia yako, na waepushe na adhabu ya Jahannamu.
|
Ayah 40:8 الأية
رَبَّنَا وَأَدْخِلْهُمْ جَنَّاتِ عَدْنٍ الَّتِي وَعَدتَّهُمْ وَمَن صَلَحَ مِنْ
آبَائِهِمْ وَأَزْوَاجِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ
الْحَكِيمُ
Swahili
Mola wetu Mlezi! Na waingize katika Bustani za Milele ulizo waahidi. Na uwape
haya pia wale walio fanya mema miongoni mwa wazee wao na wake zao na dhuriya
zao. Hakika Wewe ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
|
Ayah 40:9 الأية
وَقِهِمُ السَّيِّئَاتِ ۚ وَمَن تَقِ السَّيِّئَاتِ يَوْمَئِذٍ فَقَدْ رَحِمْتَهُ ۚ
وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ
Swahili
Na waepushe na maovu; kwani umwepushaye maovu siku hiyo, hakika umemrehemu; na
huko ndiko kufuzu kukubwa.
|
Ayah 40:10 الأية
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنَادَوْنَ لَمَقْتُ اللَّهِ أَكْبَرُ مِن مَّقْتِكُمْ
أَنفُسَكُمْ إِذْ تُدْعَوْنَ إِلَى الْإِيمَانِ فَتَكْفُرُونَ
Swahili
Kwa hakika wale walio kufuru watanadiwa: Bila ya shaka kukuchukieni Mwenyezi
Mungu ni kukubwa kuliko kujichukia nyinyi nafsi zenu, mlipo kuwa mnaitwa kwenye
Imani nanyi mkakataa.
|
Ayah 40:11 الأية
قَالُوا رَبَّنَا أَمَتَّنَا اثْنَتَيْنِ وَأَحْيَيْتَنَا اثْنَتَيْنِ
فَاعْتَرَفْنَا بِذُنُوبِنَا فَهَلْ إِلَىٰ خُرُوجٍ مِّن سَبِيلٍ
Swahili
Watasema: Mola wetu Mlezi! Umetufisha mara mbili, na umetuhuisha mara mbili!
Basi tunakiri madhambi yetu. Basi je, ipo njia ya kutoka?
|
Ayah 40:12 الأية
ذَٰلِكُم بِأَنَّهُ إِذَا دُعِيَ اللَّهُ وَحْدَهُ كَفَرْتُمْ ۖ وَإِن يُشْرَكْ
بِهِ تُؤْمِنُوا ۚ فَالْحُكْمُ لِلَّهِ الْعَلِيِّ الْكَبِيرِ
Swahili
Hayo ni hivyo kwa sababu mlikuwa akiombwa Mwenyezi Mungu peke yake mnakataa. Na
akishirikishwa mnaamini. Basi hukumu ni ya Mwenyezi Mungu Mtukufu Mkuu.
|
Ayah 40:13 الأية
هُوَ الَّذِي يُرِيكُمْ آيَاتِهِ وَيُنَزِّلُ لَكُم مِّنَ السَّمَاءِ رِزْقًا ۚ
وَمَا يَتَذَكَّرُ إِلَّا مَن يُنِيبُ
Swahili
Yeye ndiye anaye kuonyesheni Ishara zake, na anakuteremshieni kutoka mbinguni
riziki. Na hapana anaye kumbuka ila anaye rejea.
|
Ayah 40:14 الأية
فَادْعُوا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ
Swahili
Basi mwombeni Mwenyezi Mungu mkimsafia Dini Yeye tu, na wangachukia makafiri.
|
Ayah 40:15 الأية
رَفِيعُ الدَّرَجَاتِ ذُو الْعَرْشِ يُلْقِي الرُّوحَ مِنْ أَمْرِهِ عَلَىٰ مَن
يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ لِيُنذِرَ يَوْمَ التَّلَاقِ
Swahili
Yeye ndiye Mwenye vyeo vya juu, Mwenye A'rshi. Hupeleka Roho kwa amri yake juu
ya amtakaye katika waja wake, ili kuonya kwa Siku ya Mkutano.
|
Ayah 40:16 الأية
يَوْمَ هُم بَارِزُونَ ۖ لَا يَخْفَىٰ عَلَى اللَّهِ مِنْهُمْ شَيْءٌ ۚ لِّمَنِ
الْمُلْكُ الْيَوْمَ ۖ لِلَّهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّارِ
Swahili
Siku watakayo dhihiri wao. Hapana kitacho fichikana chochote chao kwa Mwenyezi
Mungu. Ufalme ni wa nani leo? Ni wa Mwenyezi Mungu Mmoja Mtenda nguvu.
|
Ayah 40:17 الأية
الْيَوْمَ تُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ ۚ لَا ظُلْمَ الْيَوْمَ ۚ إِنَّ
اللَّهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ
Swahili
Leo kila nafsi italipwa kwa iliyo chuma. Hapana dhulma leo. Hakika Mwenyezi
Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu.
|
Ayah 40:18 الأية
وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ الْآزِفَةِ إِذِ الْقُلُوبُ لَدَى الْحَنَاجِرِ كَاظِمِينَ ۚ
مَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلَا شَفِيعٍ يُطَاعُ
Swahili
Na waonye siku inayo kurubia, wakati nyoyo zitakapo fika kooni, nao wamejaa
huzuni. Madhaalimu hawatakuwa na rafiki, wala mwombezi wa kuitikiwa.
|
Ayah 40:19 الأية
يَعْلَمُ خَائِنَةَ الْأَعْيُنِ وَمَا تُخْفِي الصُّدُورُ
Swahili
(Mwenyezi Mungu) anajua khiyana ya macho na yanayo ficha vifua.
|
Ayah 40:20 الأية
وَاللَّهُ يَقْضِي بِالْحَقِّ ۖ وَالَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ لَا يَقْضُونَ
بِشَيْءٍ ۗ إِنَّ اللَّهَ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
Swahili
Na Mwenyezi Mungu huhukumu kwa haki; lakini hao wanao waomba badala yake
hawahukumu chochote. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia Mwenye kuona.
|
Ayah 40:21 الأية
أَوَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ
كَانُوا مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَانُوا هُمْ أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَآثَارًا فِي
الْأَرْضِ فَأَخَذَهُمُ اللَّهُ بِذُنُوبِهِمْ وَمَا كَانَ لَهُم مِّنَ اللَّهِ مِن
وَاقٍ
Swahili
Kwani hawatembei katika ardhi wakaona jinsi ulivyo kuwa mwisho wa walio kuwa
kabla yao? Hao walikuwa wamewazidi hawa kwa nguvu na athari katika nchi. Na
Mwenyezi Mungu aliwatia mkononi kwa sababu ya madhambi yao. Na wala hapakuwa wa
kuwalinda na Mwenyezi Mungu.
|
Ayah 40:22 الأية
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانَت تَّأْتِيهِمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَكَفَرُوا
فَأَخَذَهُمُ اللَّهُ ۚ إِنَّهُ قَوِيٌّ شَدِيدُ الْعِقَابِ
Swahili
Hayo ni kwa sababu walikuwa wanawajia Mitume wao kwa hoja zilizo wazi, lakini
wakawakataa, ndipo Mwenyezi Mungu akawakamata. Bila ya shaka Yeye ni Mwenye
nguvu, Mkali wa kuadhibu.
|
Ayah 40:23 الأية
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍ مُّبِينٍ
Swahili
Na kwa yakini tulimtuma Musa pamoja na Ishara zetu na uthibitisho ulio wazi,
|
Ayah 40:24 الأية
إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَقَارُونَ فَقَالُوا سَاحِرٌ كَذَّابٌ
Swahili
Kumwendea Firauni na Hamana na Qaruni, wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo mkubwa.
|
Ayah 40:25 الأية
فَلَمَّا جَاءَهُم بِالْحَقِّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا اقْتُلُوا أَبْنَاءَ الَّذِينَ
آمَنُوا مَعَهُ وَاسْتَحْيُوا نِسَاءَهُمْ ۚ وَمَا كَيْدُ الْكَافِرِينَ إِلَّا فِي
ضَلَالٍ
Swahili
Basi alipo waletea Haki inayo toka kwetu, walisema: Waueni watoto wanaume wa
wale walio muamini na wawacheni hai wanawake wao. Na haviwi vitimbi vya makafiri
ila katika upotovu.
|
Ayah 40:26 الأية
وَقَالَ فِرْعَوْنُ ذَرُونِي أَقْتُلْ مُوسَىٰ وَلْيَدْعُ رَبَّهُ ۖ إِنِّي أَخَافُ
أَن يُبَدِّلَ دِينَكُمْ أَوْ أَن يُظْهِرَ فِي الْأَرْضِ الْفَسَادَ
Swahili
Na Firauni akasema: Niachieni nimuuwe Musa, naye amwite Mola wake Mlezi! Mimi
nachelea asije kubadilishieni dini yenu, au akatangaza uharibifu katika nchi.
|
Ayah 40:27 الأية
وَقَالَ مُوسَىٰ إِنِّي عُذْتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُم مِّن كُلِّ مُتَكَبِّرٍ لَّا
يُؤْمِنُ بِيَوْمِ الْحِسَابِ
Swahili
Na Musa akasema: Mimi najikinga kwa Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi anilinde
na kila mwenye jeuri asiye iamini Siku ya Hisabu.
|
Ayah 40:28 الأية
وَقَالَ رَجُلٌ مُّؤْمِنٌ مِّنْ آلِ فِرْعَوْنَ يَكْتُمُ إِيمَانَهُ أَتَقْتُلُونَ
رَجُلًا أَن يَقُولَ رَبِّيَ اللَّهُ وَقَدْ جَاءَكُم بِالْبَيِّنَاتِ مِن
رَّبِّكُمْ ۖ وَإِن يَكُ كَاذِبًا فَعَلَيْهِ كَذِبُهُ ۖ وَإِن يَكُ صَادِقًا
يُصِبْكُم بَعْضُ الَّذِي يَعِدُكُمْ ۖ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ
مُسْرِفٌ كَذَّابٌ
Swahili
Na akasema mtu mmoja Muumini, aliye kuwa mmoja katika watu wa Firauni aliye
ficha Imani yake: Mtamuuwa mtu kwa sababu anasema Mola wangu Mlezi ni Mwenyezi
Mungu? Na hali naye amekujieni na hoja zilizo wazi? Na akiwa yeye mwongo basi
uwongo wake ni juu yake mwenyewe, na akiwa mkweli yatakufikieni baadhi ya hayo
anayo kuahidini. Hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi apindukiaye mipaka, mwongo
mkubwa.
|
Ayah 40:29 الأية
يَا قَوْمِ لَكُمُ الْمُلْكُ الْيَوْمَ ظَاهِرِينَ فِي الْأَرْضِ فَمَن يَنصُرُنَا
مِن بَأْسِ اللَّهِ إِن جَاءَنَا ۚ قَالَ فِرْعَوْنُ مَا أُرِيكُمْ إِلَّا مَا
أَرَىٰ وَمَا أَهْدِيكُمْ إِلَّا سَبِيلَ الرَّشَادِ
Swahili
Enyi watu wangu! Leo mna ufalme, mmeshinda katika nchi; basi ni nani atakaye
nisaidia kutuokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu kama ikitufikia? Firauni akasema:
Sikupeni shauri ila ile niliyo iona, wala sikuongozeni ila kwenye njia ya
uwongofu.
|
Ayah 40:30 الأية
وَقَالَ الَّذِي آمَنَ يَا قَوْمِ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُم مِّثْلَ يَوْمِ
الْأَحْزَابِ
Swahili
Na akasema yule aliye amini: Enyi watu wangu! Hakika mimi nakukhofieni mfano wa
siku za makundi,
|
Ayah 40:31 الأية
مِثْلَ دَأْبِ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ وَالَّذِينَ مِن بَعْدِهِمْ ۚ وَمَا
اللَّهُ يُرِيدُ ظُلْمًا لِّلْعِبَادِ
Swahili
Mfano wa hali ya watu wa Nuhu na A'di na Thamudi na wale wa baada yao. Na
Mwenyezi Mungu hataki kuwadhulumu waja.
|
Ayah 40:32 الأية
وَيَا قَوْمِ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ يَوْمَ التَّنَادِ
Swahili
Na enyi watu wangu! Hakika mimi nakukhofieni Siku ya mayowe.
|
Ayah 40:33 الأية
يَوْمَ تُوَلُّونَ مُدْبِرِينَ مَا لَكُم مِّنَ اللَّهِ مِنْ عَاصِمٍ ۗ وَمَن
يُضْلِلِ اللَّهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ
Swahili
Siku mtakapo geuka kurudi nyuma. Hamtakuwa na wa kukulindeni kwa Mwenyezi Mungu.
Na mwenye kuhukumiwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi huyo hana wa kumwongoa.
|
Ayah 40:34 الأية
وَلَقَدْ جَاءَكُمْ يُوسُفُ مِن قَبْلُ بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا زِلْتُمْ فِي شَكٍّ
مِّمَّا جَاءَكُم بِهِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا هَلَكَ قُلْتُمْ لَن يَبْعَثَ اللَّهُ مِن
بَعْدِهِ رَسُولًا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّهُ مَنْ هُوَ مُسْرِفٌ مُّرْتَابٌ
Swahili
Na alikwisha wajieni Yusuf zamani kwa dalili zilizo wazi, lakini nyinyi
mliendelea katika shaka kwa yale aliyo kuleteeni; mpaka alipo kufa mkasema:
Mwenyezi Mungu hataleta kabisa Mtume baada yake. Kama hivyo Mwenyezi Mungu
humwacha kupotea anaye pindukia mipaka katika maasi anaye jitia shaka.
|
Ayah 40:35 الأية
الَّذِينَ يُجَادِلُونَ فِي آيَاتِ اللَّهِ بِغَيْرِ سُلْطَانٍ أَتَاهُمْ ۖ كَبُرَ
مَقْتًا عِندَ اللَّهِ وَعِندَ الَّذِينَ آمَنُوا ۚ كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ اللَّهُ
عَلَىٰ كُلِّ قَلْبِ مُتَكَبِّرٍ جَبَّارٍ
Swahili
Hao ambao wanajadiliana katika Ishara za Mwenyezi Mungu pasipo ushahidi wowote
ulio wafikia, ni chukizo kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya walio amini.
Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu apigavyo muhuri juu ya kila moyo wa jeuri anaye
jivuna.
|
Ayah 40:36 الأية
وَقَالَ فِرْعَوْنُ يَا هَامَانُ ابْنِ لِي صَرْحًا لَّعَلِّي أَبْلُغُ
الْأَسْبَابَ
Swahili
Na Firauni akasema: Ewe Hamana! Nijengee mnara ili nipate kuzifikia njia,
|
Ayah 40:37 الأية
أَسْبَابَ السَّمَاوَاتِ فَأَطَّلِعَ إِلَىٰ إِلَٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُ
كَاذِبًا ۚ وَكَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِفِرْعَوْنَ سُوءُ عَمَلِهِ وَصُدَّ عَنِ
السَّبِيلِ ۚ وَمَا كَيْدُ فِرْعَوْنَ إِلَّا فِي تَبَابٍ
Swahili
Njia za mbinguni ili nikamwone Mungu wa Musa. Na kwa hakika mimi bila ya shaka
namjua kuwa ni mwongo tu. Na hivi ndivyo Firauni alivyo pambiwa ubaya wa vitendo
vyake, na akazuiliwa Njia. Na vitimbi vya Firauni havikuwa ila katika kuangamia
tu.
|
Ayah 40:38 الأية
وَقَالَ الَّذِي آمَنَ يَا قَوْمِ اتَّبِعُونِ أَهْدِكُمْ سَبِيلَ الرَّشَادِ
Swahili
Na yule aliye amini alisema: Enyi watu wangu! Nifuateni mimi, nitakuongozeni
njia ya uwongozi mwema.
|
Ayah 40:39 الأية
يَا قَوْمِ إِنَّمَا هَٰذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا مَتَاعٌ وَإِنَّ الْآخِرَةَ
هِيَ دَارُ الْقَرَارِ
Swahili
Enyi watu wangu! Hakika haya maisha ya dunia ni starehe ipitayo tu, na hakika
Akhera ndiyo nyumba ya daima.
|
Ayah 40:40 الأية
مَنْ عَمِلَ سَيِّئَةً فَلَا يُجْزَىٰ إِلَّا مِثْلَهَا ۖ وَمَنْ عَمِلَ صَالِحًا
مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ
يُرْزَقُونَ فِيهَا بِغَيْرِ حِسَابٍ
Swahili
Mwenye kutenda uovu hatalipwa ila sawa na huo uwovu wake, na anaye tenda wema,
akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini, basi hao wataingia Peponi,
waruzukiwe humo bila ya hisabu.
|
Ayah 40:41 الأية
وَيَا قَوْمِ مَا لِي أَدْعُوكُمْ إِلَى النَّجَاةِ وَتَدْعُونَنِي إِلَى النَّارِ
Swahili
Na enyi watu wangu! Kwa nini mimi nakuiteni kwenye uwokofu, nanyi mnaniita
kwenye Moto?
|
Ayah 40:42 الأية
تَدْعُونَنِي لِأَكْفُرَ بِاللَّهِ وَأُشْرِكَ بِهِ مَا لَيْسَ لِي بِهِ عِلْمٌ
وَأَنَا أَدْعُوكُمْ إِلَى الْعَزِيزِ الْغَفَّارِ
Swahili
Mnaniita nimkufuru Mwenyezi Mungu na nimshirikishe na yule ambaye simjui, nami
nakuiteni kwa Mwenye nguvu Mwenye kusamehe?
|
Ayah 40:43 الأية
لَا جَرَمَ أَنَّمَا تَدْعُونَنِي إِلَيْهِ لَيْسَ لَهُ دَعْوَةٌ فِي الدُّنْيَا
وَلَا فِي الْآخِرَةِ وَأَنَّ مَرَدَّنَا إِلَى اللَّهِ وَأَنَّ الْمُسْرِفِينَ
هُمْ أَصْحَابُ النَّارِ
Swahili
Bila ya shaka mnaye niitia kumuabudu hastahiki wito duniani wala Akhera. Na
hakika marejeo yetu ni kwa Mwenyezi Mungu. Na wanao pindukia mipaka ndio watu wa
Motoni!
|
Ayah 40:44 الأية
فَسَتَذْكُرُونَ مَا أَقُولُ لَكُمْ ۚ وَأُفَوِّضُ أَمْرِي إِلَى اللَّهِ ۚ إِنَّ
اللَّهَ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ
Swahili
Basi mtayakumbuka ninayo kuambieni. Nami namkabidhi Mwenyezi Mungu mambo yangu.
Hakika Mwenyezi Mungu anawaona waja wake.
|
Ayah 40:45 الأية
فَوَقَاهُ اللَّهُ سَيِّئَاتِ مَا مَكَرُوا ۖ وَحَاقَ بِآلِ فِرْعَوْنَ سُوءُ
الْعَذَابِ
Swahili
Basi Mwenyezi Mungu akamlinda na ubaya wa hila walizo zifanya. Na adhabu mbaya
itawazunguka watu wa Firauni.
|
Ayah 40:46 الأية
النَّارُ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا غُدُوًّا وَعَشِيًّا ۖ وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ
أَدْخِلُوا آلَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ الْعَذَابِ
Swahili
Wanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni. Na itapo fika Saa ya Kiyama patasemwa:
Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!
|
Ayah 40:47 الأية
وَإِذْ يَتَحَاجُّونَ فِي النَّارِ فَيَقُولُ الضُّعَفَاءُ لِلَّذِينَ
اسْتَكْبَرُوا إِنَّا كُنَّا لَكُمْ تَبَعًا فَهَلْ أَنتُم مُّغْنُونَ عَنَّا
نَصِيبًا مِّنَ النَّارِ
Swahili
Na watapo hojiana huko Motoni, wanyonge watawaambia walio jitukuza: Hakika sisi
tulikuwa wafuasi wenu, basi je, hamtuondolei sehemu ya huu Moto?
|
Ayah 40:48 الأية
قَالَ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا كُلٌّ فِيهَا إِنَّ اللَّهَ قَدْ حَكَمَ
بَيْنَ الْعِبَادِ
Swahili
Watasema walio jitukuza: Hakika sote sisi tumo humo humo! Kwani Mwenyezi Mungu
kesha hukumu baina ya waja!
|
Ayah 40:49 الأية
وَقَالَ الَّذِينَ فِي النَّارِ لِخَزَنَةِ جَهَنَّمَ ادْعُوا رَبَّكُمْ يُخَفِّفْ
عَنَّا يَوْمًا مِّنَ الْعَذَابِ
Swahili
Na walio Motoni watawaambia walinzi wa Jahannamu: Mwombeni Mola wenu Mlezi
atupunguzie walau siku moja ya adhabu.
|
Ayah 40:50 الأية
قَالُوا أَوَلَمْ تَكُ تَأْتِيكُمْ رُسُلُكُم بِالْبَيِّنَاتِ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۚ
قَالُوا فَادْعُوا ۗ وَمَا دُعَاءُ الْكَافِرِينَ إِلَّا فِي ضَلَالٍ
Swahili
Nao watasema: Je! Hawakuwa wakikufikieni Mitume wenu kwa hoja zilio wazi?
Watasema: Kwani? Watasema: Basi ombeni! Na maombi ya makafiri hayawi ila ni
kupotea bure.
|
Ayah 40:51 الأية
إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا
وَيَوْمَ يَقُومُ الْأَشْهَادُ
Swahili
Hakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na walio amini katika uhai wa
duniani na siku watapo simama Mashahidi,
|
Ayah 40:52 الأية
يَوْمَ لَا يَنفَعُ الظَّالِمِينَ مَعْذِرَتُهُمْ ۖ وَلَهُمُ اللَّعْنَةُ وَلَهُمْ
سُوءُ الدَّارِ
Swahili
Siku ambayo hautawafaa madhaalimu udhuru wao, nao watapata laana, na watapata
makaazi mabaya kabisa.
|
Ayah 40:53 الأية
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْهُدَىٰ وَأَوْرَثْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ الْكِتَابَ
Swahili
Na kwa hakika tulimpa Musa uwongofu, na tukawarithisha Wana wa Israili Kitabu,
|
Ayah 40:54 الأية
هُدًى وَذِكْرَىٰ لِأُولِي الْأَلْبَابِ
Swahili
Ambacho ni Uwongofu na Ukumbusho kwa wenye akili.
|
Ayah 40:55 الأية
فَاصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ اللَّهِ حَقٌّ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ
رَبِّكَ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَارِ
Swahili
Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli. Na omba msamaha kwa dhambi
zako, na umtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi jioni na asubuhi.
|
Ayah 40:56 الأية
إِنَّ الَّذِينَ يُجَادِلُونَ فِي آيَاتِ اللَّهِ بِغَيْرِ سُلْطَانٍ أَتَاهُمْ ۙ
إِن فِي صُدُورِهِمْ إِلَّا كِبْرٌ مَّا هُم بِبَالِغِيهِ ۚ فَاسْتَعِذْ بِاللَّهِ
ۖ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ
Swahili
Hakika hao wanao bishana katika Ishara za Mwenyezi Mungu bila ya uthibitisho
wowote uliyo wajia, hawana vifuani mwao ila kutaka ukubwa tu, na wala huo
hawaufikilii. Basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia,
Mwenye kuona.
|
Ayah 40:57 الأية
لَخَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَكْبَرُ مِنْ خَلْقِ النَّاسِ وَلَٰكِنَّ
أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ
Swahili
Bila ya shaka kuumba mbingu na ardhi ni kukubwa zaidi kuliko kuwaumba watu.
Lakini watu wengi hawajui.
|
Ayah 40:58 الأية
وَمَا يَسْتَوِي الْأَعْمَىٰ وَالْبَصِيرُ وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا
الصَّالِحَاتِ وَلَا الْمُسِيءُ ۚ قَلِيلًا مَّا تَتَذَكَّرُونَ
Swahili
Na kipofu na mwenye kuona hawalingani; na walio amini na watendao mema
hawalingani na muovu. Ni machache mnayo yakumbuka.
|
Ayah 40:59 الأية
إِنَّ السَّاعَةَ لَآتِيَةٌ لَّا رَيْبَ فِيهَا وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا
يُؤْمِنُونَ
Swahili
Hakika Saa (ya Kiyama) itafika, nayo haina shaka. Lakini watu wengi hawaamini.
|
Ayah 40:60 الأية
وَقَالَ رَبُّكُمُ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ
عَنْ عِبَادَتِي سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ
Swahili
Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao
wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike.
|
Ayah 40:61 الأية
اللَّهُ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَالنَّهَارَ
مُبْصِرًا ۚ إِنَّ اللَّهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ
النَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ
Swahili
Mwenyezi Mungu aliye kufanyieni usiku ili mpate kutulia humo, na mchana wa
kuonea. Hakika Mwenyezi Mungu bila ya shaka ni Mwenye fadhila juu ya watu,
lakini watu wengi hawashukuru.
|
Ayah 40:62 الأية
ذَٰلِكُمُ اللَّهُ رَبُّكُمْ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ لَّا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ
فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ
Swahili
Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi, Muumba wa kila kitu. Hapana mungu ila
Yeye; basi mnageuzwa wapi?
|
Ayah 40:63 الأية
كَذَٰلِكَ يُؤْفَكُ الَّذِينَ كَانُوا بِآيَاتِ اللَّهِ يَجْحَدُونَ
Swahili
Namna hivi ndivyo walivyo geuzwa walio kuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi
Mungu.
|
Ayah 40:64 الأية
اللَّهُ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ قَرَارًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً
وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ وَرَزَقَكُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ ۚ ذَٰلِكُمُ
اللَّهُ رَبُّكُمْ ۖ فَتَبَارَكَ اللَّهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ
Swahili
Ni Mwenyezi Mungu aliye kufanyieni ardhi kuwa ni pahala pa kukaa, na mbingu kuwa
dari. Na akakutieni sura, na akazifanya nzuri sura zenu, na akakuruzukuni vitu
vizuri. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu
Mola Mlezi wa walimwengu wote.
|
Ayah 40:65 الأية
هُوَ الْحَيُّ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ فَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ ۗ
الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ
Swahili
Yeye ndiye aliye Hai - hapana mungu isipo kuwa Yeye. Basi muabuduni Yeye
mkimsafishia Dini Yeye. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa
walimwengu wote.
|
Ayah 40:66 الأية
قُلْ إِنِّي نُهِيتُ أَنْ أَعْبُدَ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّهِ لَمَّا
جَاءَنِيَ الْبَيِّنَاتُ مِن رَّبِّي وَأُمِرْتُ أَنْ أُسْلِمَ لِرَبِّ
الْعَالَمِينَ
Swahili
Sema: Mimi nimekatazwa kuwaabudu hao mnao waomba badala ya Mwenyezi Mungu,
zilipo nijia hoja zilizo dhaahiri kutokana na Mola wangu Mlezi. Na nimeamrishwa
nisilimu kwa Mola wa walimwengu wote.
|
Ayah 40:67 الأية
هُوَ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ مِنْ عَلَقَةٍ
ثُمَّ يُخْرِجُكُمْ طِفْلًا ثُمَّ لِتَبْلُغُوا أَشُدَّكُمْ ثُمَّ لِتَكُونُوا
شُيُوخًا ۚ وَمِنكُم مَّن يُتَوَفَّىٰ مِن قَبْلُ ۖ وَلِتَبْلُغُوا أَجَلًا
مُّسَمًّى وَلَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ
Swahili
Yeye ndiye aliye kuumbeni kwa udongo, kisha kwa tone la manii, kisha kwa pande
la damu, kisha akakutoeni katika hali ya mtoto mchanga, kisha mpate kufikilia
utu uzima, kisha mpate kuwa wazee. Na kati yenu wapo wanao kufa kabla, na ili
mfikie muda ulio kwisha wekwa, na ili mpate kufahamu.
|
Ayah 40:68 الأية
هُوَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ فَإِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ
كُن فَيَكُونُ
Swahili
Yeye ndiye anaye huisha na anaye fisha. Akihukumu jambo liwe, basi huliambia:
Kuwa! Likawa.
|
Ayah 40:69 الأية
أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يُجَادِلُونَ فِي آيَاتِ اللَّهِ أَنَّىٰ يُصْرَفُونَ
Swahili
Je! Huwaoni wale wanao bishana katika Ishara za Mwenyezi Mungu? Wanageuziwa
wapi?
|
Ayah 40:70 الأية
الَّذِينَ كَذَّبُوا بِالْكِتَابِ وَبِمَا أَرْسَلْنَا بِهِ رُسُلَنَا ۖ فَسَوْفَ
يَعْلَمُونَ
Swahili
Ambao wamekanusha Kitabu na yale tuliyo watuma Mitume wetu. Basi watakuja jua.
|
Ayah 40:71 الأية
إِذِ الْأَغْلَالُ فِي أَعْنَاقِهِمْ وَالسَّلَاسِلُ يُسْحَبُونَ
Swahili
Zitakapo kuwa pingu shingoni mwao na minyororo, huku wanabururwa
|
Ayah 40:72 الأية
فِي الْحَمِيمِ ثُمَّ فِي النَّارِ يُسْجَرُونَ
Swahili
Katika maji ya moto, kisha wanaunguzwa Motoni,
|
Ayah 40:73 الأية
ثُمَّ قِيلَ لَهُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ تُشْرِكُونَ
Swahili
Tena wataambiwa: Wako wapi mlio kuwa mkiwashirikisha
|
Ayah 40:74 الأية
مِن دُونِ اللَّهِ ۖ قَالُوا ضَلُّوا عَنَّا بَل لَّمْ نَكُن نَّدْعُو مِن قَبْلُ
شَيْئًا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّهُ الْكَافِرِينَ
Swahili
Badala ya Mwenyezi Mungu? Watasema: Wametupotea, bali tangu zamani hatukuwa
tukiomba kitu! Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anawaachia makafiri wapotelee mbali.
|
Ayah 40:75 الأية
ذَٰلِكُم بِمَا كُنتُمْ تَفْرَحُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَبِمَا
كُنتُمْ تَمْرَحُونَ
Swahili
Haya ni kwa sababu mlikuwa mkijitapa katika ardhi pasipo haki, na kwa sababu
mlikuwa mkijishaua.
|
Ayah 40:76 الأية
ادْخُلُوا أَبْوَابَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۖ فَبِئْسَ مَثْوَى
الْمُتَكَبِّرِينَ
Swahili
Ingieni kwenye milango ya Jahannamu, mdumu humo milele. Basi ni maovu yaliyoje
makaazi ya wanao takabari!
|
Ayah 40:77 الأية
فَاصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ اللَّهِ حَقٌّ ۚ فَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ الَّذِي
نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيْنَا يُرْجَعُونَ
Swahili
Basi subiri, hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Na ama tukikuonyesha
baadhi ya yale tuliyo waahidi au tukikufisha, lakini wao watarudishwa kwetu tu.
|
Ayah 40:78 الأية
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ مِنْهُم مَّن قَصَصْنَا عَلَيْكَ
وَمِنْهُم مَّن لَّمْ نَقْصُصْ عَلَيْكَ ۗ وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَن يَأْتِيَ
بِآيَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّهِ ۚ فَإِذَا جَاءَ أَمْرُ اللَّهِ قُضِيَ بِالْحَقِّ
وَخَسِرَ هُنَالِكَ الْمُبْطِلُونَ
Swahili
Na bila ya shaka tuliwatuma Mitume kabla yako. Wengine katika hao tumekusimulia
khabari zao, na wengine hatukukusimulia. Na haiwi Mtume alete Ishara yoyote ila
kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Basi ikija amri ya Mwenyezi Mungu huhukumiwa kwa
Haki, na hapo wapotofu watakhasiri.
|
Ayah 40:79 الأية
اللَّهُ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَنْعَامَ لِتَرْكَبُوا مِنْهَا وَمِنْهَا
تَأْكُلُونَ
Swahili
Mwenyezi Mungu aliye kujaalieni nyama hoa, mifugo, ili muwapande baadhi yao, na
muwale baadhi yao.
|
Ayah 40:80 الأية
وَلَكُمْ فِيهَا مَنَافِعُ وَلِتَبْلُغُوا عَلَيْهَا حَاجَةً فِي صُدُورِكُمْ
وَعَلَيْهَا وَعَلَى الْفُلْكِ تُحْمَلُونَ
Swahili
Na katika hao mnayo manufaa kadhaa wa kadhaa, na mnapata kwao haja ziliomo
vifuani mwenu; na mnachukuliwa juu yao, na juu ya marikebu.
|
Ayah 40:81 الأية
وَيُرِيكُمْ آيَاتِهِ فَأَيَّ آيَاتِ اللَّهِ تُنكِرُونَ
Swahili
Naye anakuonyesheni Ishara zake. Basi Ishara gani za Mwenyezi Mungu mnazo
zikataa?
|
Ayah 40:82 الأية
أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ
مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَانُوا أَكْثَرَ مِنْهُمْ وَأَشَدَّ قُوَّةً وَآثَارًا فِي
الْأَرْضِ فَمَا أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ
Swahili
Kwani hawatembei katika ardhi wakaona ulikuwaje mwisho wa walio kuwa kabla yao?
Wao walikuwa wengi kuliko hawa, na wamewashinda kwa nguvu na athari katika nchi.
Wala hayakuwafaa hayo waliyo kuwa wakiyachuma.
|
Ayah 40:83 الأية
فَلَمَّا جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَرِحُوا بِمَا عِندَهُم مِّنَ
الْعِلْمِ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ
Swahili
Walipo wajia Mitume wao kwa dalili zilizo wazi walijitapa kwa ilimu waliyo kuwa
nayo. Basi yakawazunguka waliyo kuwa wakiyafanyia maskhara.
|
Ayah 40:84 الأية
فَلَمَّا رَأَوْا بَأْسَنَا قَالُوا آمَنَّا بِاللَّهِ وَحْدَهُ وَكَفَرْنَا بِمَا
كُنَّا بِهِ مُشْرِكِينَ
Swahili
Walipo iona adhabu yetu walisema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni wa pekee,
na tunaikataa miungu tuliyo kuwa tukiishirikisha naye.
|
Ayah 40:85 الأية
فَلَمْ يَكُ يَنفَعُهُمْ إِيمَانُهُمْ لَمَّا رَأَوْا بَأْسَنَا ۖ سُنَّتَ اللَّهِ
الَّتِي قَدْ خَلَتْ فِي عِبَادِهِ ۖ وَخَسِرَ هُنَالِكَ الْكَافِرُونَ
Swahili
Lakini imani yao haikuwa yenye kuwafaa kitu wakati ambao wamekwisha iona adhabu
yetu. Huu ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu ulio kuwa kwa waja wake. Na hapo walio
kufuru walikhasiri.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|