First Ayah 1 الأية الأوليبِسْم ِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ
Swahili
Ewe uliye jigubika!
|
Ayah 74:2 الأية
قُمْ فَأَنذِرْ
Swahili
Simama uonye!
|
Ayah 74:3 الأية
وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ
Swahili
Na Mola wako Mlezi mtukuze!
|
Ayah 74:4 الأية
وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ
Swahili
Na nguo zako, zisafishe.
|
Ayah 74:5 الأية
وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ
Swahili
Na yaliyo machafu yahame!
|
Ayah 74:6 الأية
وَلَا تَمْنُن تَسْتَكْثِرُ
Swahili
Wala usitoe kwa kutaraji kuzidishiwa.
|
Ayah 74:7 الأية
وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ
Swahili
Na kwa ajili ya Mola wako Mlezi, subiri!
|
Ayah 74:8 الأية
فَإِذَا نُقِرَ فِي النَّاقُورِ
Swahili
Basi litapo pulizwa barugumu,
|
Ayah 74:9 الأية
فَذَٰلِكَ يَوْمَئِذٍ يَوْمٌ عَسِيرٌ
Swahili
Siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu.
|
Ayah 74:10 الأية
عَلَى الْكَافِرِينَ غَيْرُ يَسِيرٍ
Swahili
Kwa makafiri haitakuwa nyepesi.
|
Ayah 74:11 الأية
ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا
Swahili
Niache peke yangu na niliye muumba;
|
Ayah 74:12 الأية
وَجَعَلْتُ لَهُ مَالًا مَّمْدُودًا
Swahili
Na nikamjaalia awe na mali mengi,
|
Ayah 74:13 الأية
وَبَنِينَ شُهُودًا
Swahili
Na wana wanao onekana,
|
Ayah 74:14 الأية
وَمَهَّدتُّ لَهُ تَمْهِيدًا
Swahili
Na nikamtgenezea mambo vizuri kabisa.
|
Ayah 74:15 الأية
ثُمَّ يَطْمَعُ أَنْ أَزِيدَ
Swahili
Kisha anatumai nimzidishie!
|
Ayah 74:16 الأية
كَلَّا ۖ إِنَّهُ كَانَ لِآيَاتِنَا عَنِيدًا
Swahili
Hasha! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu!
|
Ayah 74:17 الأية
سَأُرْهِقُهُ صَعُودًا
Swahili
Nitamtesa kwa mateso yasio wezekana.
|
Ayah 74:18 الأية
إِنَّهُ فَكَّرَ وَقَدَّرَ
Swahili
Kwani hakika yeye alifikiri na akapima.
|
Ayah 74:19 الأية
فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ
Swahili
Basi ameangamia! Vipi alivyo pima!
|
Ayah 74:20 الأية
ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ
Swahili
Tena ameangamia! Vipi alivyo pima!
|
Ayah 74:21 الأية
ثُمَّ نَظَرَ
Swahili
Kisha akatazama,
|
Ayah 74:22 الأية
ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ
Swahili
Kisha akakunja kipaji, na akanuna.
|
Ayah 74:23 الأية
ثُمَّ أَدْبَرَ وَاسْتَكْبَرَ
Swahili
Kisha akaipa kisogo haki, na akatakabari.
|
Ayah 74:24 الأية
فَقَالَ إِنْ هَٰذَا إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ
Swahili
Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulio nukuliwa.
|
Ayah 74:25 الأية
إِنْ هَٰذَا إِلَّا قَوْلُ الْبَشَرِ
Swahili
Haya si chochote ila kauli ya binaadamu.
|
Ayah 74:26 الأية
سَأُصْلِيهِ سَقَرَ
Swahili
Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar.
|
Ayah 74:27 الأية
وَمَا أَدْرَاكَ مَا سَقَرُ
Swahili
Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar?
|
Ayah 74:28 الأية
لَا تُبْقِي وَلَا تَذَرُ
Swahili
Haubakishi wala hausazi.
|
Ayah 74:29 الأية
لَوَّاحَةٌ لِّلْبَشَرِ
Swahili
Unababua ngozi iwe nyeusi.
|
Ayah 74:30 الأية
عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ
Swahili
Juu yake wapo kumi na tisa.
|
Ayah 74:31 الأية
وَمَا جَعَلْنَا أَصْحَابَ النَّارِ إِلَّا مَلَائِكَةً ۙ وَمَا جَعَلْنَا
عِدَّتَهُمْ إِلَّا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا لِيَسْتَيْقِنَ الَّذِينَ
أُوتُوا الْكِتَابَ وَيَزْدَادَ الَّذِينَ آمَنُوا إِيمَانًا ۙ وَلَا يَرْتَابَ
الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْمُؤْمِنُونَ ۙ وَلِيَقُولَ الَّذِينَ فِي
قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَالْكَافِرُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّهُ بِهَٰذَا مَثَلًا ۚ
كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّهُ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَمَا يَعْلَمُ
جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَ ۚ وَمَا هِيَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْبَشَرِ
Swahili
Na hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni Malaika, wala hatukuifanya idadi yao
hiyo ila kuwatatanisha walio kufuru, wapate kuwa na yakini walio pewa Kitabu, na
wazidi Imani wale walio amini, wala wasiwe na shaka walio pewa Kitabu na
Waumini, na wapate kusema wenye maradhi katika nyoyo zao na makafiri: Mwenyezi
Mungu amekusudia nini kwa mfano huu? Ndio kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha
apotee amtakaye, na humwongoa amtakaye. Na hapana yeyote anaye jua majeshi ya
Mola wako Mlezi ila Yeye tu. Na haya si chochote ila ni ukumbusho kwa binaadamu.
|
Ayah 74:32 الأية
كَلَّا وَالْقَمَرِ
Swahili
Hasha! Naapa kwa mwezi!
|
Ayah 74:33 الأية
وَاللَّيْلِ إِذْ أَدْبَرَ
Swahili
Na kwa usiku unapo kucha!
|
Ayah 74:34 الأية
وَالصُّبْحِ إِذَا أَسْفَرَ
Swahili
Na kwa asubuhi inapo pambazuka!
|
Ayah 74:35 الأية
إِنَّهَا لَإِحْدَى الْكُبَرِ
Swahili
Hakika huo Moto ni katika mambo yaliyo makubwa kabisa!
|
Ayah 74:36 الأية
نَذِيرًا لِّلْبَشَرِ
Swahili
Ni onyo kwa binaadamu,
|
Ayah 74:37 الأية
لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَتَقَدَّمَ أَوْ يَتَأَخَّرَ
Swahili
Kwa anaye taka miongoni mwenu kutangulia au kuchelewa.
|
Ayah 74:38 الأية
كُلُّ نَفْسٍ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَةٌ
Swahili
Kila nafsi imo rahanini kwa mabaya iliyo yachuma.
|
Ayah 74:39 الأية
إِلَّا أَصْحَابَ الْيَمِينِ
Swahili
Isipo kuwa watu wa kuliani.
|
Ayah 74:40 الأية
فِي جَنَّاتٍ يَتَسَاءَلُونَ
Swahili
Hao watakuwa katika Mabustani, wawe wanaulizana
|
Ayah 74:41 الأية
عَنِ الْمُجْرِمِينَ
Swahili
Khabari za wakosefu:
|
Ayah 74:42 الأية
مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ
Swahili
Ni nini kilicho kupelekeni Motoni?
|
Ayah 74:43 الأية
قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ
Swahili
Waseme: Hatukuwa miongoni walio kuwa wakisali.
|
Ayah 74:44 الأية
وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ الْمِسْكِينَ
Swahili
Wala hatukuwa tukiwalisha masikini.
|
Ayah 74:45 الأية
وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ الْخَائِضِينَ
Swahili
Na tulikuwa tukizama pamoja na walio zama katika maovu.
|
Ayah 74:46 الأية
وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ الدِّينِ
Swahili
Na tulikuwa tukiikanusha siku ya malipo.
|
Ayah 74:47 الأية
حَتَّىٰ أَتَانَا الْيَقِينُ
Swahili
Mpaka yakini ilipo tufikia.
|
Ayah 74:48 الأية
فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ
Swahili
Basi hautawafaa kitu uombezi wa waombezi.
|
Ayah 74:49 الأية
فَمَا لَهُمْ عَنِ التَّذْكِرَةِ مُعْرِضِينَ
Swahili
Basi wana nini hata wanapuuza onyo hili?
|
Ayah 74:50 الأية
كَأَنَّهُمْ حُمُرٌ مُّسْتَنفِرَةٌ
Swahili
Kama kwamba wao ni mapunda walio timuliwa,
|
Ayah 74:51 الأية
فَرَّتْ مِن قَسْوَرَةٍ
Swahili
Wanao mkimbia simba!
|
Ayah 74:52 الأية
بَلْ يُرِيدُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُؤْتَىٰ صُحُفًا مُّنَشَّرَةً
Swahili
Ati kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizo funuliwa.
|
Ayah 74:53 الأية
كَلَّا ۖ بَل لَّا يَخَافُونَ الْآخِرَةَ
Swahili
Hasha! Kwani wao hawaiogopi Akhera?
|
Ayah 74:54 الأية
كَلَّا إِنَّهُ تَذْكِرَةٌ
Swahili
Hasha! Kwa hakika huu ni ukumbusho!
|
Ayah 74:55 الأية
فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ
Swahili
Basi anaye taka atakumbuka.
|
Ayah 74:56 الأية
وَمَا يَذْكُرُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّهُ ۚ هُوَ أَهْلُ التَّقْوَىٰ وَأَهْلُ
الْمَغْفِرَةِ
Swahili
Na hawatakumbuka isipo kuwa Mwenyezi Mungu atake. Uchamngu ni kwake Yeye, na
msamaha ni wake Yeye.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|